Nenda kwa yaliyomo

Hadithi ya Qasim al-Naar wa al-Jannah

Kutoka wikishia

Hadithi ya Qasim al-Naar wa al-Jannah (Kiarabu: حديث قسيم النار والجنة) ni riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo inaeleza fadhila za Imam Ali bin Abi Talib (a.s), na inamtambulisha yeye kwamba, ni mgawaji wa Pepo na Jahanamu. Hadithi hii imenukuliwa katika vyanzo vya Kishia na Kisuni kwa ibara tofauti.

Katika hadithi na maneno ya Maulamaa wa Kiislamu, kuna maana mbili kuhusiana ambazo zimefahamiwa katika hadithi hii: Mosi ni kuwa, kipenzi cha Ali (a.s) atakuwa peponi na adui wake atakuwa katika moto wa jahanamu.

Pili, katika Siku ya Kiyama, Imam Ali (a.s) atawaainisha watu wa peponi na watu wa motoni.

Baadhi ya Maulamaa wa Kishia na Kisuni wameitambua hadithi hii kwamba, ni mutawatir (iliyokithiri mapokezi yake); ingawa baadhi ya Ahlul-Sunna wakitaja sanadi maalumu (mlolongo wa mapokezi) wameitaja hadithi hii kwamba, ni dhaifu. Hadithi ya “Ali mgawaji wa moto na pepo” imetumiwa na washairi katika mashairi ya Kiarabu na Kifarsi.

Andiko la hadithi

Hadithi ya «قسیم النار و الجنة» ni riwaya iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Imam Ali (a.s) ambayo imenukuliwa kwa ibara mbalimbali:

  • «یا عَلِی إِنَّکَ قَسِیمُ الْجَنَّةِ وَ النَّارِ»; “Ewe Ali! hakika wewe ni mgawaji wa pepo na moto. [1] Katika sahifa ya Imam Ridha (a.s), neno moto (jahanamu) limekuja kabla ya pepo: «یا عَلِی إِنَّکَ قَسِیمُ النَّارِ وَ الْجَنَّةِ» ; “Ewe Ali! Hakika wewe ni mgawaji wa moto na pepo.” [2] Imekuja katika baadhi ya vyanzo ya kwamba: «تُدخِلُ مُحِبِّیکَ الْجَنَّةَ وَ مُبْغِضِیکَ النَّارَ» ; “Unamuingiza peponi akupandaye, na unamuingiza motoni akuchukiaye.” [3]
  • «یا عَلِی أَنْتَ قَسِیمُ الْجَنَّةِ یوْمَ الْقِیامَةِ تَقُولُ لِلنَّارِ هَذَا لِی وَ هَذَا لَکِ» ; “Ewe Ali! wewe ni mgawaji wa pepo siku ya Kiyama, utauambia moto, huyu ni wa kwako na huyu ni wa kwangu”. [4]
  • «یا علی إنَّکَ قَسیمُ النّارِ وَ إِنَّکَ تَقْرَعُ بَابَ الْجَنَّةِ فَتَدْخُلُهَا بِلَا حِسَاب» ; “Ewe Ali, wewe ni mgawaji wa pepo, unagonga mlango wa pepo na unaingia bila hesabu.[5]

Imam Ali (a.s) pia alijitambulisha kwa ibara tofauti kwamba yeye ni mgawaji wa pepo na moto. [6] Miongoni mwazo ni: «أنَا الفارُوقُ الّذِی أَفرُقُ بَینَ الحَقِّ و البَاطِلِ، ‌أنَا أُدْخِلُ أَوْلِیائی الجَنَّةَ و أَعْدائی النَّارَ» ; Mimi ni mtenganishaji ambaye ninatenganisha baina ya haki na batili, ninawaingiza peponi marafiki zangu na maadui zangu ninawaingiza motoni. [7]

«قسیم الجنة والنار» linahesabiwa kuwa miongoni mwa lakabu za Imam Ali (a.s). [8] Katika Ziyara za Imam Ali (a.s) pia hadithi hii imeashiriwa. [9]

Kinachofahamika katika hadithi

Kuna tafsiri mbili kuu kwa mujibu wa kile kilichofahamiwa na Maulamaa wa Kiislamu katika tafsiri mbili kuu za ibara ya “mgawaji wa jahanamu na pepo”:

  • Wapenzi wa Ali (a.s) wameongoka na hivyo wataingia peponi, na maadui zake wamepotea na kwa msingi huo wataingia jahanamu. [10] Ahmad bin Hambal mmoja wa mafakihi wa Ahlu-Sunna (aliaga dunia 241 Hijria) akimjibu mtu anayekana hadithi ya “mimi ni mgawaji wa moto” akitumia hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Imam Ali (a.s) isemayo: “Ewe Ali! Hakupendi isipokuwa muumini na hakuchukii isipokuwa mnafiki” na kubainisha nafasi na daraja ya waumini peponi na nafasi ya mnafiki katika moto wa jahanami, anatoa natija hii kwamba, “Ali ni mgawaji wa jahanamu.” [11]
  • Nyingine ni kuwa, kwa hakika Siku ya Kiyama, Imam Ali (a.s) mgawaji wa pepo na moto na atawapeleka watu peponi au motoni. [12]

Madhumuni ya maana hizi mbili yamekuja katika baadhi ya hadithi pia. [13] Baadhi wamesema pia kwamba, kwa kuwa Imam Ali (a.s) ana cheo cha Uimamu, kauli na matendo yake ni hoja. Kwa msingi huo, wafuasi wake ni watu wa peponi na wengine wasiokuwa wao ni watu wa motoni. [14]

Itibari na sanadi

Hadithi ya “Mgawaji wa moto na pepo” kwa mtazamo wa Allama Majlisi [15] na baadhi ya Maulamaa wa Ahlu-Sunna ni mutawatir. [16] Jabir bin Abdallah, [17] Abdallah bin Abbas, [18] Abdallah bin Omar, [19] Abdallah bin Mas’oud, [20] Abu al-Tufayl, [21] na Aba al-Salt Hirawi [22] ni miongoni mwa wapokezi wa hadithi hii. Pamoja na hayo, kundi miongoni mwa Maulamaa wa Kisunni, wamenukuu hadithi hii kupitia kwa Mussa bin Turayf na Abaya bin Rib’i na kuwahesabu wapokezi hawa kuwa ni dhaifu. [23]

Katika mashairi

Hadithi ya “Ali mgawaji wa moto na pepo” imetumiwa na washairi katika mashairi ya Kiarabu [24] na Kifarsi. [25] Kwa mafno beti za mashairi zifuatazo zinanasibishwa na Muhammad bin Idris Shafii (aliaga dunia 204 Hijiria), ambaye ni kiongoni wa madhehebu ya Shafi:

علیٌّ حُبُّه جُنَّة ***قسیمُ النَّار و الجَنّة

کَیفَ أَسْتَسْقی لِطِفْلی فَاَبَوْا أَن یرْحَمُونی *** إمام الإنس و الجِنَّة

وصیّ المصطفی حقا *** و سَقَوهُ سَهْمَ بَغْی عِوَضَ الماءِ المَعینِ



Kumpenda Ali ni kinga, Mgawaji wa moto na pepo, Wasii wa haki wa Mtume, Imam wa watu na majini [26]

Kadhalika kuna beti za mashairi zenye maudhui kama hii ambazo zinanasibishwa kwa Qutb al-Din al-Rawandi (aliaga dunia 573Hijria) ambaye ni mpokezi wa hadithi wa Kishia.

Madhumuni ya beti hizo za mashairi ni:

Ali ni mgawaji wa moto, mtu mwenye kheri, Ni uzuri ulioje kesho (Kiyama) tutaokoka na moto wa jahanamu, Muhammad katika dini ni mithili ya jua, Na baada yake ni Ali anayeng’ara kama mwezi.[27]

Rejea

Vyanzo

  • Albānī, Muḥammad Nāṣir al-Dīn. Sīlsīlat al-aḥādīth al-ḍaʿīfa wa al-mawḍūʿa wa atharuhā al-sayyiʾ fī al-ʾumma. Riyadh: Dār al-Maʿārif, 1412 AH/1992.
  • Dārqutnī, ʿAlī b. ʿUmar al-. Al-ʿIlal al-wāridah fī al-aḥādīth al-nabawī. Riyadh: Dār al-Ṭayyiba, 1405 AH.
  • Dāwūdī, Yūsuf b. Jawda. Manhaj al-imām al-dārqutnī fī naqd al-ḥadīth fī kitāb al-ʿilal. Cairo: Dār al-Muḥadithīn, 1432 AH/2011.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Mīzān al-iʿtidāl. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Maʿrifa li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1382 AH.
  • Furāt al-Kūfī, Abu l-Qāsim Furāt b. Ibrāhīm. Tafsīr furāt al-kūfī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ḥamūyī al-Juwaynī, Ibrāhīm b. Muḥammad al-. Frāʾid al-samaṭayn. Edited by Muḥammad Bāqīr Muḥamūdī. Beirut: Muʾassisat al-Muḥamūdī, 1400 AH.
  • Ḥusaynī Tihrānī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Imām shināsī. Mashhad: Allāma Ṭabāṭabāʾī, 1426 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balāgha. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Qom: Maktabat Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1404 AH.
  • Ibn Abī Yaʿlī, Muḥammad b. Muḥammad. Ṭabaqāt al-ḥanābila. Edited by Muḥammad Ḥāmid al-Faqī. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. Ḥasan. Tārīkh-i damishq. Edited by ʿAmr-i b. Gharāma al-ʿAmrawī. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH/ 1995.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Lisān al-mīzān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1390 AH/ 1971.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407AH-1986.
  • Ibn Maghāzīlī, ʿAlī b. Muḥammad. Manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1424 AH.
  • Ibn Mardawayh Iṣfahānī. Manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib wa mā nazal min al-Qurān fī ʿAlī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1424 AH.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
  • Ibn ʿUqda Kūfī, Aḥmad b. Muḥammad. Faḍāʾīl Amīr al-Muʾminīn(a). Edited by ʿAbd al- Razzāq Muḥammad Ḥusayn Ḥirz al-Dīn, Qom: Dalīl-i Mā, 1424 AH.
  • Khazzāz Rāzī,ʿAlī b. Muḥammad. Kifāyat al-athar fī al-naṣṣ ʿalā aʾima al-ithnā ʿashar. Edited by ʿAbd al-Laṭīf Ḥusaynī kūhkamarī. Qom: Bīdār, 1401 AH.
  • Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Al-Manāqib. Edited by Mālik Mahmūdī. Qom: 1414 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Māzandarānī, Muḥammad Sāliḥ b. Ahmad. Sharḥ uṣūl kāfī. Edited by Abdu l-Ḥassan Shaʿrānī. Tehran: Maktaba al-Islāmīyya, 1382 AH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Mustadrak al-wasāʾil wa musṭanbit al-wasā'il. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1408 AH.
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm. Yanābīʿ al-mawadat li-dhi l-qurbā. Edited by Alī Jamāl Ashraf Husaynī. Qom: Dār al-ʾUswa, 1416 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Tehran: Intishārāt-i Dāwarī, 1385 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Maʿānī al-akhbār. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1403 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣāʾir al-darajāt fī faḍāʾil-i Āl-i Muḥammad. Edited by Muḥsin Kūchabāghī. Qom: Kitābkhāna-yi Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Saḥīfa al-Imām al-Riḍā(a). Edited by Muḥammad Mahdī Najaf. Mashhad: Kungira-yi Jahānī-yi Imām al-Riḍā(a), First edition, 1406 AH.
  • Ṭabarī Āmulī, ʿImād al-Dīn al-. Bishārat al-Muṣṭafā li Shīʿat al-Murtaḍā. 2nd edition. Najaf: al-Maktaba al-Ḥaydarīyya, 1383 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH