Nenda kwa yaliyomo

Ghadiiriyya

Kutoka wikishia

Ghadiiriyya (Kiarabu: الغديرية): ni mashairi yanayozingatia tukio la Ghadiir Khum. Yasemekana kwamba; mashairi ya mwanzo kabisa kabisa kuhuisana na Ghadir Khum yalitungwa na Hassan bin Thabit. Kiuhalisia, mashairi ya Ghadiiriyya hayazungumzii tu tukio la Ghadiir na hadhi ya Imamu Ali (a.s) katika kushika nafasi ya ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), bali pia yanachambua masuala mengine mbali mbali muhimu ndani yake kama vile; Hadithi ya Udugu (Hadithul Ukhuwwah), Hadithi ya Manzilat, pamoja na kisa cha Leilat al-Mabit.

Allama Amini (aliyefariki mwaka 1390 Hijria), alikusanya wasifu na zaidi ya kazi za mia moja za washairi wa Kiarabu, waliotunga mashairi ya Ghadiiriya katika kitabu chake maarufu kiitwacho Al-Ghadiir. Aidha kuna mashairi kadhaa ya Ghadiiriya kwa lugha ya Kifarsi kutoka karne ya nne hadi karne ya kumi na nne Hijria, ambayo yamerikodiwa katika kitabu kiitwacho Ghadiiriyehaye Farsi.

Utambulisho wa Ghadiiriya

Ghadiiriya ni mashairi yanayozungumzia tukio la Ghadiir pamoja na sifa za Imamu Ali (a.s) na uongozi wake. Mashairi haya kikawaida huwa yanataja rasmi jina la Ghadir Khum ndani yake. [1] Mashairi haya kwa kawaida huwa yanasomwa kwa mtindo wa qasida. [2] Kuna baadhi ya wataalamu wa fasihi wanaoamini kwamba; kasida halisi za Ghadiiriya ni lazima zizingatie kwa kina tukio la Ghadiir pamoja na uteuzi wa Imam Ali (a.s.). Mashairi yanayozungumzia fadhila na sifa za Imamu, huku yakirejelea tukio la Ghadiir kwa namna ya mpito tu, hayawezi kwa ujumla kuitwa Ghadiiriya kwa maana kamili. [3]

Kwa mujibu wa maelezo ya Jawad Muḥaddithī, ambaye ni mwanazuoni, mshairi na mwandishi maarufu wa Kishia, ni kwamba; msingi wa kitabu al-Ghadiir, kilichoandikwa na Allama Amini, umejengwa juu ya mashairi ya Ghadiiriyya. Mashairi ambayo yameandikwa na washairi mbalimbali tangu enzi za bwana Mtume (s.a.w.w) hadi zama za mwandishi wa kitabu hicho. [4]

Aidha, baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba; mashairi ya Ghadiiriyya hayabebi tu kumbukumbu ya tukio moja la kihistoria, bali pia yanaakisi ukweli na maarifa ya hali ya juu, ambayo ndiyo chemchemi msingi ya elimu nyingine zote, huku yakijenga msingi wa utamaduni wa kudumu na wa asili kwa vizazi vijavyo. [5]

Washairi wa Kiarabu wa Mashairi ya Ghadiiriyya

Hassan bin Thabit katika Wasifu wa Tukio la Ghadir
ینادیهم یوم الغدیر نبیهم * بخم و أسمع بالرسول منادیا
فقال فمن مولاکم و ولیکم * فقالوا و لم یبدوا هناک التعادیا


إلهک مولانا و أنت ولینا * و لم‌تر منا فی المقالة عاصیا
فقال له قم یا علی فإننی * رضیتک من بعدی إماما و هادیا


فمن کنت مولاه فهذا ولیه * فکونوا له أنصار صدق موالیا
هناک دعا اللهم وال ولیه * و کن للذی عادی علیا معادیا


Tafsiri: Nabii wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) aliwaita wao siku ya Ghadir, wito uliokuwa na thamani kubwa mno. Alisema akiwambia: "Enyi watu kiogozi wenu ni nani?" Wakajibu bila mashaka wakisema: "Mola wako, ndiye kiongozi wetu, na wewe ndiye mtawala wetu na kiongozi wetu (kwa niaba yake). Katu sisi hatutajaribu kwenda kinyume na amri zako." Hapo Ndipo Nabii (s.a.w.w) alipowambia Ali: "Simama kani mimi nimekuteua wewe uwe ndiye mrithi wa nafasi yangu baada yangu." Kisha akaongeza akisema: "Kila yule ambaye (anakiri kuwa) mimi ndiye kiongozi wake, basi huyu (Ali) ndiye kiongozi wake." Hivyo basi nyote, mfwateni yeye kwa nia moja bila ya kuachana naye. Ee Mungu, mpende yule ampendaye yeye na umchukie yule anayemchukia.



Rejea: (Sayyid Radhi, Khawas al-A’imma, 1406 Q, Uk. 42)


Ḥassān bin Thābit ndiye mshairi wa kwanza wa Ghadiiriya, aliyepata idhini ya bwana Mtume (s.a.w.w) kuandika mashairi kuhusiana na tukio la Ghadiir katika siku tukio hilo. [6]

Mashairi yake ndiyo yaliyofungua njia kwa washairi wengine kuonyesha mapenzi yao kwa Imamu Ali (a.s), wakitukuza tukio hili adhimu. Miongoni mwa washairi maarufu waliotunga mashairi ya aina hii ni: Kumayt bin Zayd Asadi (alifariki mwaka 126 Hijria), Sayyid Isma'il al-Himyari (alifariki mwaka 173 Hijria), al-‘Abdī, Abu Tammam Habib bin Aws al-Ta'i (alifariki mwaka 231 Hijria), Di'ibil bin Ali Khuzā'ī (alifariki mwaka 246 Hijria). Allama Amini, katika kitabu chake maarufu al-Ghadiir, amekusanya taarifa za zaidi ya washairi mia moja walioandika mashairi ya Ghadiiriya, kuanzia karne ya kwanza hadi ya kumi na moja. Majina na wasifu wao yameainishwa katika juzuu ya pili, ya saba na ya kumi na moja ndani ya kazi hii maarufu ya Allama Amini. [7]

Mashairi ya Ghadiriyya Yaliyonukuliwa Kutoka kwa Imamu Ali (a.s) Yenye Madhumuni Kama Ifwatavyo:
مُحَمَّدٌ النَّبِی أَخِی وَ صِنْوِی * وَ حَمْزَةُ سَیدُ الشُّهَدَاءِ عَمِّی
و جعفرٌ الّذی یُضحی و یُمسی * یطیرُ مع الملائکة ابنُ اُمّی


وَ بِنْتُ مُحَمَّدٍ سَکَنِی وَ عِرْسِی * مَنوطٌ لَحْمُهَا بِدَمِی وَ لَحْمِی
و سبطا أحمد وَلَدای منها * فَأیّکمُ له سَهْمٌ کسهمی


وَ أَوْجَبَ لِی وَلَایتَهُ عَلَیکُمْ * رَسُولُ اللَّهِ یوْمَ غَدِیرِ خُمٍ
فَوَیلٌ ثُمَّ وَیلٌ ثُمَّ وَیلٌ‌ * لِمَنْ یلْقَی الْإِلَهَ غَداً بِظُلْمِی‌


Tafsiri: Muhammad ni Nabii wangu, ndugu yangu, na jamaa yangu; Hamza ni bwana wa mashahidi naye pia ni mjomba wangu; na Ja'far, anayepaa pamoja na malaika asubuhi na jioni, ni ndugu yangu. Binti wa Nabii, (Fatima (a.s)), ni faraja yangu na mke wangu, ambaye nyama yake imeunganishwa na damu yangu. Hassan na Hussein, wajukuu wa Nabii, ni watoto wangu kutoka kwa Fatima. Basi ni nani kati yenu mwenye sifa kama zangu, hali ya kwamba mimi nimekukiukeni nyote kwa sifa njema? Nabii alitoa hukumu ya wajibu wa uongozi wangu juu yenu siku ya Ghadir. Basi, ole wake yule ambaye siku ya Kiyama atakutana na Mwenye Ezi Mungu akiwa amenidhulumu haki yangu!



Rejea: (Tabarsi, Al-Ihtijaj 'ala Ahli al-Lajaaj, Juz. 1, Uk. 180)


Katika kitabu hiki, pia kuna majina ya baadhi ya maadui wa Imam Ali (a.s) yaliyo rodheshwa kama ni miongoni mwa watunzi wa Ghadiriyya. Kwa mfano, Amru bin As (aliyefariki: 43 Hijiria) anaye julikana kwa kasida yake maarufu ya Jaljuliyyah inayohusiana na mada hii, ni mongoni walio orodheshwa ndani ya oradha hii. [Maelezo 1]

Zuhra Fat-hullah Nouri, mtafiti wa Kishia, amewachunguza waandishi wanane mashuhuri wa Ghadiriyyakutoka karne ya 14 na 15, akiwemo Paul Salam, Said Aql, George Shakur, na Victor El-Kik. Baada ya uchunguzi wake anasema kwamba; kinachovutia hisia za watu katika Ghadiriyya za Kiarabu ni uwepo wa Ghadiriyya za «Joseph Aoun» na «George Zaki al-Hajj», ambao ni washairi wa kisasa wa Kikristo kutoka Lebanon, waliandika mashairi yao kwa lahaja za Kiarabu cha Kilebanon. [8]

Miktadha ya Kasida za Ghadiriyya

Kubra Salehi, katika tasnifu yake jina la: «Negahi Sabkeshenaasaane be Ghadiriyyehaye Asre Awwal Abbasi» (Mtazamo wa Kiuchunguzi juu ya Ghadiriyya za Nyakati za Kwanza za Abbasiyya), anasisitiza kwamba; Ghadiriyya zinajumuisha miktadha ifuatayo ndani yake: [9]

Waandishi wa Ghadiriyya za Kifarsi

Makala Kuu: Faharasa ya Watunzi wa Kasida za Ghadiriyya kwa Kifarsi
Kitabu Ghadiriyehaye Farsi (kutoka karne ya 4 hadi 14), kilichoandikwa na Muhammad Sehti Sardroudi, kilichochapishwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu.

Katika makala yake, “Ghadiriyyehaye Farsi az Qarne Chaharom ta Qarne Chahardahom” (Orodha ya Waandishi wa Ghadiriyya za Kifarsi), Muhammad Sihhati Sardwardi, mwanafunzi wa kidini wa Kishia, amekusanya waandishi 179 wa kasida za Ghadiriyya za Kifarsi kutoka karne ya nne hadi karne ya kumi na nne Hijiria. Orodha hii imekusanywa kutoka kitabu cha Al-Ghadir, na kuandikwa kwa ule ule uliotumika ndani ya kitabu hicho. [10]

Baadhi ya kasida za Ghadiriyya za Kifarsi zinazohusiana na karne ya saba na nane ya Hijiria ni kama ifuatavyo:

افضل چو ز علم و فضل آگاه علی است * درمسند عرفان ازل، شاه علی است
ز بعد نبی امام خلق دو جهان * باالله علی است، ثُم باالله علی است


Ali ndiye bora kwa elimu na fadhila, na katika kiti cha maarifa ya milele, Ali ndiye mfalme. Baada ya Mtume, yeye ndiye Imamu wa duniani na Akhera, wallahi ni Ali, tena wallah ni Ali.



Kasida ya Baabaa Afdhal Kashani [11]


ازین سبب پیغمبر با اجتهاد * نام خودوآن علی مولا نهاد
گفت: هرکو را منم مولا و دوست * ابن عم من، علی، مولای اوست


Ali ndiye bora kwa elimu na fadhila,   na katika kiti cha maarifa ya milele, Ali ndiye mfalme. Baada ya Mtume, yeye ndiye Imamu wa duniani na Akhera, wallahi ni Ali, tena wallah ni Ali.



Kasida ya Jalalu Al-Din Balkhi (Maulawi) [12]


سرو بستان امامت، دُرّ دریای هدیٰ * شمع ایوان ولایت، نور چشم اولیا
قلعه‌گیر کشور دین، حیدر درنده حی * دسته‌بند لالهٔ عصمت، وصی مصطفی
ره به منزل برد، هر کو مذهب حیدر گرفت * آب حیوان یافت، آن کو خضر را رهبر گرفت


Msonobari wa bustani ya Uimamu, lulu ya bahari ya uongofu, Taa ya ukumbi wa Uongozi, nuru ya macho ya wapenzi wa Mwenye Ezi Mungu. Ngome ya nchi ya dini, Haidar simba wa Mwenye Ezi Mungu, taji la utoharifu, wasii wa Mustafa. Yeyote aliyeshika njia ya Haidar, atafika kwenye nyumba ya mani, na yeyote atakaye shikamana na madhehebu ya Haidar (Imamu Ali), huyo atakuwa ameyafikia maji ya uhai, na bila shake yeye huyo atakuwa amemfanya Khidhri kuwa ndiye kiongozi wake.



Kasida ya Khajawi Kirmani [13]


Kulingana na baadhi ya maoni, ukandamizaji wa watawala wa Kisunni dhidi ya itikadi za Kishia, ulisababisha kuwepo totauti kubwa katika wingi na viwango vya mashairi ya Ghadiriya, kabla na baada ya enzi za utawala wa Safawiyya (Safawid). Kwa mfano, Ferdusi alifukuzwa katika baraza ya mfalme Ghaznawiy (Ghaznavid), na Amir Mu'izzi, licha ya hadhi yake kubwa mbele ya mfalme Malik Shah na Sultan Sanjar, alilazimika kuomba msamaha mara moja pale alipokuwa akisoma mashairi yake na kutamka neno «Wasii» katika mashairi hayo. Yeye alijihadhari sana na neno hili, ambalo lilitumika na Mashia kumrejelea Imamu Ali (a.s). Kwa hiyo kila alipolitamka neno hili, ilimbidi kuomba radhi ili kuepukana na hasira ya Sultan na wanazuoni wa Kisunni. [14]

Bibliografia

  • Al-Ghadir, kilichoandikwa na Allama Amini na kutafsiriwa na Muhammad Baqir Behbudi, na kuchapishwa na Taasisis ya Kitabkhone Bozorge Islami.
  • Ghadir katika Mashairi ya Kiajemi (Ghadir dar Shi’iri Farsi), kilichoandikwa na Mostafa Mousawi Garmarudi na kuchapishwa na Taasisi ya Dalil.
  • Ghadiriya za Kiajemi “Ghadiriyyehaye Farsi” (Kuanzia karne ya nne hadi ya kumi na nne), kilichoandikwa na Muhammad Sehhati Sardrudi, na kuchachapishwa na Wizara ya Utamaduni na Uongozi wa Kiislamu “Wizarate Farhangi wa Irshad Islami”.
  • Saauti ya Ghadir “Golbang Ghadir”, kilichandikwa na Mohammad Mahdi Behdarvand, na kuchapishwa na Taasisi ya Peyam Azadi Tehran.
  • Ufukweni mwa Ghadir “Dar Saahile Ghadir”, kilichoandikwa na Ahmad Ahmadi-Birjandi, na kuchapishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Haram ya Imam Reza (a.s) mjini Mash’had.
  • Kuwasaika na Ghadir “Khalwate baa Ghadir” kilichoandikwa na Mohammad Mahdi Behdarvand, kuchapishwa na Taasisi ya Har mjini Tehran.

Maelezo

  1. Ghadiriyya ya ‘Amr bin ‘As inajulikana hasa kwa jina la kasida ya Juljuliyyah (جُلجُلیه), lenye maana ya Kengele. Kutungwa kwa shairi hili kumesimuliwa kwa njia isemayo kwamba: Katika zama fulani Muawiyah alimhukumu ‘Amr bin ‘As, ambaye alikuwa ni mtawala wa Misri, kwa sababu kukataa kwake kutuma kodi. Katika kujibu hukumu hiyo, ‘Amr bin ‘As aliandiaka barua yenye mistari beti 66 iliyojulikana kwa jina la kasida ya Juljuliyyah, ambayo inatoa uthibitisho wa baadhi ya ukweli wa kihistoria wa wakati huo. Kasida hii inaanza na beti ifuatayo: (معـاويـة الفضل لا تنس لي * وعـن نهـج الحـق لا تعـدل ; Ewe Muawiya, usisahau fadhila zangu, na wala usikae kando na njia ya haki), na shairi hili limepewa jina la Juljuliyyah kwa kuwa shairi hili lina ubeti usemao: (فـإن كـنت فيـها بلغت المنى * فـفي عـنقي عـلق الجُلجُل ; Na ikiwa umefikia (umefahamu) lengo langu, basi tundika kengele shingoni mwangu). Rejea: (Amini, Al-Ghadir, 1368 SH, Juz. 3, ukurasa 213).

Rejea

Vyanzo