Dua ya Nadi Ali

Kutoka wikishia

Dua ya Nadi Ali ni anuani ya dua mbili zinazotoa wasifu wa Imam Ali (as) na ambayo inaanza na ibara isemayo: نادِ عَلِياً مَظهَرَ [أو مُظهِرَ] العَجائِب" (muite Ali! Mwenye kudhihirisha maajabu. Inaelezwa kuwa, ilikuwa ni katika vita vya Uhud wakati, Mtume (saww) aliponong'onezwa dua hii katika masikio yake na ulimwengu wa ghaibu. Dua ya Nadi Ali Swaghir ni fupi na inaelezwa kuwa, inaondoa kila huzuni na ghamu kwa baraka za Utume wa Mtume Muhammad (sawww) na Wilaya (uongozi) wa Imama Ali (as), Allama Majlisi amenukuu na kuileta dua hii katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar, hata hivyo hakuashiria chanzo chake. Hata hivyo Yadullah Duzduzani, fakihi wa Kishia, amesema kuwa, Dua ya Nadi Ali Swaghir haina nyaraka za kuaminika ili kuifanya iwe na itibari. Pamoja na hayo, kumeandikwa vitabu vya kutoa ufafanuzi na maelezo kuhusiana na dua hii. Dua ya Nadi Ali Kabir nayo ina madhumuni na maana inayoshabihiana na Dua ya Nadi Ali Swaghir; hata hivyo ukubwa wake ni mara kadhaa ya Dua ya Nadi Ali Swaghir.

Dua ya Nadi Ali Swaghir

Kwa mujibu wa kile kilichokuja katika ufafanuzi wa diwani ya mashairi inayonasibishwa na Imam Ali (as) iliyoandikwa na Maybudi Yazdi, alimu na msomi wa Kishafii wa karne ya 10 Hijria ni kwamba, Mtume (saww) alisikia hivi katika vita vya Uhud kutoka kwa ulimwengu wa Ghaibu:

[1] «نَادِ عَلِيّاً مَظْهَرَ الْعَجَائِبِ، تَجِدْهُ عَوْناً لَكَ فِي النَّوَائِبِ، كُلُّ هَمٍّ وَ غَمٍّ سَيَنْجَلِي، بِوَلايَتِكَ يَا عَلِيُّ»

Maneno haya yana nyongeza katika kitabu cha Farhang Ghadir kilichoandikwa na Jawad Muhaddithi:

«نَادِ عَلِيّاً مَظْهَرَ الْعَجَائِبِ، تَجِدْهُ عَوْناً لَكَ فِي النَّوَائِبِ، كُلُّ هَمٍّ وَ غَمٍّ سَيَنْجَلِي، بِنُبُوَّتِکَ یا مُحَمَّد، بِوَلايَتِكَ يَا عَلِيُّ»

Maneno ambayo tarjumi yake ni:

Muite Ali, mwenye kudhihirisha maajabu, utampata ni mwenye kukusaidia katika mazonge/matatiizo yako; kila huzuni na ghamu inaondoka kwa baraka za Utume wako Ewe Muhammad, na kwa Wilaya (uongozi) wa Ali! [2]

Allama Majlisi katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar na Mirza Muhammad Taqi Sepehr katika kitabu chake cha Nasikh al-Tawarikh wameashiria hadithi na riwaya ya Maybudi Yazdi. [3] Hata hivyo katiika kitabu cha Bihar al-Awnar hakujaashiriwa chanzo cha dua hii. [4] Yadullah Duzduzani, mmoja wa mafakihi wa Kishia wa karne ya 15 Hijria, licha ya kuwa ametanbua kuwa, kusoma dhikri na dua hii kwa ajiili ya matarajio ya thawabu hakuna tatizo, lakini ameeleza kwamba, hakuna nyaraka na hoja yenye itibari kuhusu hili. [5] Taqi al-Din Ibrahim al-Kaf’ami, mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 15 Hijria anasema katika kitabu chake cha Misbah kwamba aliona kipengee tajwa kikiwa na hati ya al-Shahid al-Awwal na anaongeza kusema kwamba, kilikuwa kikisomwa na kukaririwa ili kupata kitu kilichopotea na mtumwa aliyekimbia. [6] Muhaddith Nuri amenukuu katika kitabu chake cha Mustadrak al-Wasail nukta hii hii. [7] Alllama Seyyid Muhammad Hussein Husseini Tehrani amenukuu kutoka kwa marejemu Seyyid Hashim Haddad ya kwamba, kila ambaye atasoma dua hii kila siku mara 110 na akadumisha usomaji huu kwa muda wa siku tatu mfululizo, basi Mwenyezi Mungu atamjibu kila haja atakayomuomba. [8]

«نادِ علیًّا مَظهَرَ العجائبَ، تَجِدْهُ عَونًا لکَ فی النَّوائب، کُلُّ همٍّ و غمٍّ سَیَنجَلی، بعَظَمَتِکَ یا اللَهُ، بِنُبوَّتِکَ یا محمّد، بولایتکَ یا علیُّ یا علیُّ یا علیّ»

Dua ya Nadi Ali imeandikwa ikiwa na mabadiliko kidogo katika sentensi ya mwisho katika msikiti mkuu wa Bijapur (Vijayapur) kusini mwa India. [9] Sehemu iliyotajwa yenye tofauti ni:

[10] ، بِنُبوَّتِکَ یا محمّد، بولایتکَ یا علیُّ یا علیُّ یا علیّ» Ibara hii imendikwa pia katika ngome ya Ahmadnagar India na inaonekana kwa umbo la simba. [11]

Mashairi ya Kifarsi

Washairi na malenga kadhaa wa Kifarsi wameashiria katika athari zao dua ya Nadi Ali Swaghir; miongoni mwao ni Mirza Muhammad Taqi mashuhuri kwa jina la Tabrizi. [12] Mshairi mwingine aliyeashiria hili ambaye jina lake halifahamiki alisema hivi katika baadhi ya beti zake za mashairi: [13]

Katika madhehebu yetu maneno ya haki ni Nadi Ali Twaa na ibada ilipokubaliwa na Mungu ilikuwa Nadi Ali

Nadi Ali Kabir

Tuliashiria mwanzoni mwa makala hii kwamba, Nadi Ali ni anuani ya dua mbili ambazo ni Nadi Ali Swaghir na Nadi Ali Kabir. Nadi Ali Swaghir kama tulivyoashiria na ambayo ndio mashuhuri zaidi yenyewe ni fupi. Lakini kuna Nadi Ali Kabiri ambayo ni ndefu. Allama Majlisi amenukuu na kuleta maandiko ya dua kamili ya Nadi Ali Kabir katika kitabu chake cha Zad al-Ma’ad. [14]

Dua kamili ya Nadi Ali Kabir ni:
بِسمِ اللهِ الرَّحمن الرَّحیم

نَادِ عَلِيّاً مَظْهَرَ الْعَجَائِبِ تَجِدْهُ عَوْناً لَكَ فِي النَّوَائِبِ لِي إِلَى اللهِ حَاجَتِي وَعَلَيْهِ مُعَوَّلِي كُلَّمَا رَمْيَتُهُ وَرَمَيْتَ مُقْتَضَی كُلِّ هَمٍّ وَغَمٍّ سَيَنْجَلِي بِعَظَمَتِكَ يَا اللهُ وَبِنُبُوَّتِكَ يَا مُحَمَّدُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ وَ سَلَّمَ وَبِوَلَايَتِكَ يَا عَلِيُّ يَا عَلِيُّ يَا عَلِيُّ أَدْرِكْنِي بِحَقِّ لُطْفِكَ الْخَفِيِّ، اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ أَنَا مِنْ شَرِّ أَعْدَائِكَ بَرِي‌ءٌ بَرِي‌ءٌ بَرِي‌ءٌ اللهُ صَمَدِي بِحَقِّ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ يَا أَبَا الْغَيْثِ أَغِثْنِي يَا عَلِيُّ أَدْرِكْنِي يَا قَاهِرَ الْعَدُوِّ وَيَا وَالِيَ الْوَلِيِّ يَا مَظْهَرَ الْعَجَائِبِ يَا مُرْتَضَى عَلِيُّ يَا قَهَّارُ تَقَهَّرْتَ بِالْقَهْرِ وَالْقَهْرُ فِي قَهْرِ قَهْرِكَ يَا قَهَّارُ يَا ذَا الْبَطْشِ الشَّدِيدِ أَنْتَ الْقَاهِرُ الْجَبَّارُ الْمُهْلِكُ الْمُنْتَقِمُ الْقَوِيُّ وَ الَّذِي لَا يُطَاقُ انْتِقَامُهُ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللهِ إِنَّ اللهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ حَسْبِيَ اللهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ نِعْمَ الْمَوْلَى وَنِعْمَ النَّصِيرُ يَا غِيَاثَ الْمُسْتَغِيثِينَ أَغِثْنِي يَا رَاحِمَ الْمَسَاكِينِ ارْحَمْنِي يَا عَلِيُّ وَأَدْرِكْنِي يَا عَلِيُّ أَدْرِكْنِي يَا عَلِيُّ أَدْرِكْنِي بِرَحْمَتِكَ يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ [15].

Athari zinazohusiana

Kumeandika makala na vitabu mbalimbali kuhusiana na dua ya Nadi Ali ambavyo vinabainisha sifa maalumu za dua hii’. Mmiongoni mwa athari hizo ni kitabu cha Kifarsi chenye anuani ya “Nadi Aliyan Madh’har al-Ajaaib…” ambacho kinapatikana katika makataba ya Mar’ashi Najafi katika mji wa Qom, Iran. [16] Kadhalika Ali Sadrai Khui, ameashiria katika kitabu chake nakala za hati ya mkono za hadithi na elimu ya hadithi orodha ya vitabu vilivyotoa ufafanuzi wa dua ya “Nadi Aliyann Madh’har al-Ajaaib”. [17]