Aya ya Sa’ala Saailun
Jina la Aya | Aya ya Sa’ala Saailun |
---|---|
Sura Husika | Surat al-Maarij |
Namba ya Aya | 1 na 2 |
Juzuu | 29 |
Sababu ya Kushuka | Adhabu ya Nu'man bin Harith al-Fihri, Ambaye Alipinga Ukhalifa wa Imamu Ali (a.s) Pale Ghadir Khum. |
Mahali pa Kushuka | Makka |
Aya ya Sa’ala Saailun (Kiarabu: آية سأل سائل) au Aya ya Adhabun waaqiun ( عذاب واقع): ni jina maarufu za Aya mbili za mwanzoni mwa za Surat al-Ma’arij. Kiuhalisia Aya hizi zinahusiana na ombi la kushuka kwa adhabu kutoka kwa Mungu lililo ombwa na mtu mmoja ambaye asiye amini Mungu. Kulingana na maelezo ya wafasiri; Baada ya mtu huyu kuomba ombi hilo, Mwenye Mungu alimshushia jiwe juu ya kichwa kutoka mbinguni na kumuua papo hapo.
Wafasiri wa madhehebu ya Shia, wanaamini kwamba; sababu ya kushuka kwa Aya hii ni malalamiko ya Nu’uman bin Harith Fahri juu ya tangazo la urithi wa Imam Ali (a.s) la kushika nafasi ya Ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), tangazo ambalo lilitangazwa na bwana Mtume (s.a.w.w) katika bonde la Ghadir. Ibn Taimiyyah, kiongozi wa Salafi, ameonyesha shaka kuhusu sababu ya kushuka kwa Aya hii katika tukio la Ghadir. Madai ya kuwa Surat al-Maarj ni Sura iliyoteremshwa Makka na kutokuwa maarufu kwa tukio lililotajwa hapo juu ni baadhi ya sababu zilizo tegemewa na Ibnu Taimiyyah.
Allama Tabatabai, akijibu shaka ya Ibn Taimiyyah, amesema: Ingawa muktadha wa Aya zilizotajwa katika Sura hii unalingana na Sura za Makka, lakini Aya nyingine za Sura hii zinazohusiana na wanafiki na kuwajibishwa kwa amali ya kutoa zaka, Aya ambazo kiuhalisia zinaendana na Aya za Sura za Madinan; kwa sababu hiyo basi, hata Aya ya Sa’al Sa’ilun. Allama Amini, katika kitabu cha Al-Ghadir, akirejelea kauli za watu thalathini mashuhuri kutoka upande wa madhehebu ya Ahlu-Sunna, amethibitisha kwamba ni maarufu mbele ya wanazuoni kuwa Aya hizi ni Aya za Madinan.
Matini Asili ya Aya Pamoja na Tafsiri Yake
﴾ (۲)سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ(۱) لِلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ﴿
Mtu anayeuliza kuhusu adhabu itakayotokea, ambayo ni maalum kwa makafiri na hakuna wa kuizuia.
Suratu al-Ma’arij(70:1-2)
Kulingana na Allama Tabatabai, Aya ya Sa’ilun inaambatana na aina ya shinikizo kejeli katika jibu lake, na inasimulia tukio la ombi la adhabu (adhabu ambayo ni mahsusi kwa makafiri ambayo hakuna kinachoweza kuiepusha), aombi ambalo lilitolewa na baadhi ya makafiri. [1] Na neno “swali” lilikoko kwenye ibara ya Aya hizi limefasiriwa kwa maana ya kuomba. [2]
Sababu ya Kushuka Kwake
Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya wafasiri wa Shia, Aya za kwanza za Sura Al-Ma’arij zinamhusu Nu’uman bin Harith Fahri au pia yawezekana pia kuwa inahusiana na mtu mwingine, [3] ambaye alipinga tangazo la urithi wa Imam Ali (a.s) - wa kurithi nafasi ya Mtume (s.a.w.w) - katika tukio la Ghadir. [4] Kwa maoni ya wafasiri hao ni kwamba; pale yeye aliposikia tangazo la bwana Mtume (s.a.w.w) juu ya urithi wa Imamu Ali (a.s) wa kushiaka nafasi ya Mtume (s.a.w.w) baada ya kifo chake, alimtamkia bwana Mtume (s.a.w.w) maneno ya jeuri, akimwambia: «Ulituomba tushuhudie umoja wa Mungu na unabii wako, nasi tukafanya ulivyo tuambia, kisha ukatuamuru kupigana jihadi, kuhiji, kufunga, kusali na kutoa zaka, nasi tulikubali; lakini bado hukuridhika mpaka ukaamua kumteua huyu kijana (Ali (a.s)) kuwa ndiye mrithi wako». [5] Je, uamuzi huu ni wako au ni wa Mungu? Mtume (s.a.w.w) akamjibu kwa kula kiapo ya kwamba maneno hayo yanatokana na Mwenye Ezi Mungu. Hapo basi Nu’man akasema, «Ee Mwenye Ezi Mungu, ikiwa maneno haya ni ya kweli, na kwamba yanatoka kwako, basi tuletee jiwe kutoka mbinguni lianguke juu yetu». [6] Kulingana na hadithi, baada ya ombi lake, jiwe lilimwangukia kutoka mbinguni na akauawa. Kisha aya hii iliteremshwa. [7]
Baadhi ya wafasiri wamehusisha chanzo na sababu ya kushuka kwa Aya hizi na Nadhru bin Harith. [8] Yeye, katika Masjid al-Haram, kwa dhihaka kabisa alitamka na alimwambia Mtume (s.a.w.w) akisema: «Ewe Mungu, ikiwa Muhammad yuko sahihi na kile anachosema, na kwamba kweli kile akisemacho kinatoka kwako, basi tuletee mvua ya mawe au tutumbukiza katika adhabu kali iumizayo». [9] Baada tu ya kumaliza maneno yake, Mwenye Ezi Mungu akamshushia Mtume Muhammad (s.a.w.w) Aya hiyo. [10] Hata hivyo. Ingawaje kundi la wafasiri hawa liliegeiegemeza Aya hizi kwa Nadhru bin Harith, ila pia chini ya Aya hizi wameashiria kisa na riwaya ya Nu’man bin Harith. [11] Pia, imesemekana kwamba; Aya hizi zilimshikia Abu Jahli, na hata Aya iseamayo: «فَأَسْقِطْ عَلَيْنا كِسَفاً مِنَ السَّماءِ إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ» “Basi tuangushe kipande cha mbingu ikiwa wewe ni mkweli” ni Aya inayo nukuu maneno yake yeye. [12] Kulingana na mtazamo wa Nassir Makarim Shirazi ni kwamba; Kuna khitilafu baina ya wanazuoni kuhusiana na jina hasa la mtu huyu. Hivyo basi, hakuna uhakika kwamba je alikuwa ni Nu’man bin Harith Fahri, au Harith bin Nu’man, au Jabir bin Nadhr. Ila jambo hili halina athari kwenye msingi wa kisa cha kushuka kwa Aya hii. [13] Baadhi ya waandishi akiwemo Makarem Shirazi, wanamtambulisha Nu’man kama ni mtu mnafiki, [14] na wakati wengine wanamuelezea na kumtambulisha kama Myahudi. [15]
Uhusiano Wake na Tukio la Ghadiri
Ibn Timiyyah na Alusi, ambao ni wanazuoni na wafasiri wa madhehebu ya Sunni, wanaamini kwamba; Aya hii haina uhusiano na tukio la Ghadir. Hii ni kwa sababu ya kwamba Surat al-Ma’arij iliteremshwa huko Makka kabla ya Hijra ya bwana Mtume (s.a.w.w) ya kutoka Makkka kwenda Madina, wakati tukio la Ghadir lilitokea katika mwaka wa kumi Hijria, baada ya bwana Mtume (s.a.w.w) kurejea kutoka Hija Al-wadaa (Hija ya mwisho kabla ya kufariki kwake). [17] Kinyume chake, Allama Tabatabai amesema kwamba; Ingawa muktadha wa Aya za mwanzo za sura hii ni sawa na muktadha wa Sura zilizoteremshwa Makka, ambazo zinahusiana na adhabu ya makafiri Siku ya Kiyama, lakini katika Sura hii pia, kuna Aya zinazoonyesha kwamba, hata Aya za mwanzo za Sura hii ni za Madina; ikiwemo Aya ya 24 ambayo inazungumzia zaka, na ni jambo la wazi kwamba zaka ilifaradhiswa Madina. [18] Kulingana na mawazo yake yeye (Allama Tabatabai), Aya zilizotajwa hapo zinahusu wanafiki, na hii inaendana zaidi na kuwa ni Aya hizo ni za Madina; kwa sababu unafiki ulianza katika mji wa Madina. [19]
Ibnu Timiyyah pia anaamini kwamba; Ikiwa tutakubaliana juu ya kisa cha Nu’man bin Harith [Maelezo 1: Ila, Ibn Taymiyyah alitaja jina la mtu huyu kama ni Harith bin Nu’man (Ibn Taymiyyah, Minhaju al-Sunnah al-Nabawiyyah, 1406H, Juzuu ya 7, Ukurasa 44] na kuamini kuwa ni sahihi, pia bado kutakuwa na utata kati ya yaliyomo katika Aya ya 33 ya Surat Al-Anfal, kwa sababu yaonesha kwamba, Nu’man alishukiwa na adhabu katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w), bali tukio hilo lilitokea mbele ya Mtume (s.a.w.w). [20] Kimantiki jambo hii haliwezekani, kwa sababu yeye alikuwa na muuminini. Hii ni kwa sababu; Aya ya 33 ya Surat Al-Anfal, inasema kwamba; Mungu hawadhibu watu wakati ambao Mtume (s.a.w.w) yupo miongoni kwenye umma wake. [21] Katika kujibu madai ya hoja hii, imeelezwa kwamba; Aya ya 33 ya Surat Al-Anfal inahusiana na adhabu ya umma kamili kiujumla jamala, na haihusishi adhabu za binafsi;[22] kama ilivyoandikwa katika historia ya Uislamu ya kwamba; Abu Zama’a, Malik bin Talalah na Hakim bin Abi Al-Aas, ni miongoni mwa watu walioadhibiwa na Mungu wakati wa Mtume (s.a.w.w). [23] Pia, kupinga kwa Nu’man amri ya Mungu ni ukafiri mkubwa mno, na kwa namna fulani inahesabika kuwa ni miongoni mwa matendo ya kuritadi (kutoka nje ya Uislamu), jambao ambalo linastahiki adhabu. [24]
Kutokutajwa kwa jina la Nu’man katika baadhi ya vyanzo vya historia ya Masahaba, kama vile Al-Isti’abu, na kutokuwa maarufu kwa kisa chake kama kilivyo kuwa maaruu kisa cha As’hab al-Fiil, ni mojawapo ya pingamizi za Ibn Taymiyyah alizotumia kuthibitisha madai yake. [25] Waliojibu tanzu na tata zake wamesema kwamba; Katika vyanzo vya historia ya Masahaba, hakukutajwa majina ya Masahaba wote wa bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa mfano, katika kitabu cha “Usudu al-Ghaba” kilicho andikwa kuhusiana na maisha ya Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), ni majina ya watu 7,504 tu yalio tajwa na kurikodiwa ndani yake, hali ya kwamba wakati katika Hijatu al-Wadaa, kulikuwa na idadi watu 100,000 au zaidi walioandamana na bwana Mtume (s.a.w.w) katika hija hiyo. Pia, imeelezwa kwamba; tukio la Nu’man bin Harith ndio sababu maarufu ya kushuka kwa Aya hizo, Pia Allama Amini na katika kitabu cha Al-Ghadir, amelinukuu tukio hili kutoka kwa wanazuoni thalathini maarufu wa madhehebu Ahlu-Sunna, jambo ambalo linatilia mkazo tukio hilo. [27]
Maudhui Zinazo Fungamana
Rejea
Vyanzo