Mwislamu wa Kwanza

Kutoka wikishia

Mwislamu wa kwanza (Kiarabu: أول المسلمين) ni yule mtu wa kwanza kumwamini Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kule kuwa ni Muislamu wa kwanza, huhisabiwa kuwa na hadhi maalumu mbele ya Waislamu. Mashia wanamchukulia Imam Ali (a.s) kuwa ndiye mwanamume wa kwanza kuwa Mwislamu na bibi Khadijah ni mwanamke wa kwanza kuwa Mwislamu. Jambo hili pia limetajwa katika vyanzo vya kihistoria vya Sunni.

Kwa mujibu wa ripoti zitokazo katika baadhi ya vyanzo vya Sunni, Abu Bakar ametambulishwa kuwa ndiye mtu wa kwanza kusilimu. Rasul Jafarian, mwanahistoria wa Kishia, ameyachukulia madai hayo ya baadhi ya Masunni kuwa ni matokeo ya migogoro ya kimadhehebu baina ya Waislamu ambayo haina mashiko ya kihistoria.

Hadhi na nafasi yake

Mwislamu wa kwanza ni yule mtu wa kwanza aliyemwamini Mtume wa Uislamu (s.a.w.w). Suala la kuwa Muislamu wa kwanza kunazingatiwa kuwa ni heshima na hadhi maalumu kwa mtu huyo. [1] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, kule Imamu Ali (a.s) kuwa ndiye Mwislamu wa kwanza, Mtume (s.a.w.w) alilizingatia suala hilo kuwa ni suala linalompa yeye nafasi na hadhi maalumu katika jamii. [3]

Khadija (a.s) ni mwanamke wa kwanza wa kusilimu

Wanahistoria hawapingani kuhusiana na suala la bibi Khadija kuwa ndiye mwanamke wa kwanza kusilamu [4] Baadhi yao wamemtaja kuwa ndiye Muislamu wa kwanza kutoka pande zote mbili ( wanawake na wanaume). [5] Ibnu Athir, ambaye ni mwanahistoria wa Kisunni, amedai kuwepo makubaliano baina ya Waislamu juu ya suala la kwamba yeye alikuwa ndiye muumini wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w). [6]

Kwa mujibu wa kauli ya Ahmad bin Abi Yaqub, mwanahistoria wa karne ya tatu; Bibi Khadijah ndiye mwanamke wa kwanza na Ali (a.s) ndiye mwanamume wa kwanza kumwamini Mtume (s.a.w.w). [7]

Ali (a.s) mwanamume wa kwanza kusilimu

Kwa mujibu wa hadithi, Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) alimtambulisha Imam Ali (a.s) kuwa ni Mwislamu wa kwanza, Muumini wa kwanza [8] na mtu wa kwanza kumkubali Mtume Muhammad (s.a.w.w). [9] Sheikh Tusi alisimulia hadithi kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kwamba; Imam Ali (a.s) ametambulishwa kama ndiye muumini wa kwanza wa Mtume wa Uislamu. [10] Inasemekana kwamba Shia wana maafikiano juu ya kwamba Imam Ali (a.s) alikuwa Muislamu wa kwanza. [11] pia Imam Ali (a.s) katika maneneo yake mbali mbali, ametaja wazikuwa yeye ndiye mtu wa kwanza katika Uislamu.[12]

Allameh Majlisi [13] na Hussein bin Hamdan Khasiibiy [14], mwandishi wa Shia wa karne ya nne, wamemtambua Imam Ali (a.s) kuwa ni Mwislamu wa kwanza. Pia, Muhammad bin Jarir Tabari, [15] Shamsuddin Dhahabi [16] na wengine [17] kutoka kwa wanahistoria wa Kisunni wamesimulia hadithi kadhaa kuhusu Imam Ali (a.s) kuwa ni Mwislamu wa kwanza.


Ripoti nyingine kadhaa

Baadhi ya Masunni wamezitaja riwaya ambazo zinasema kwa Abu Bakar [18] au Zaid bin Harith walikuwa ndiwo Waislamu wa kwanza [19] Mwanahistoria wa Kisunni Maqriziy katika kitabu chake "Imtina'u al-Asma'i" alimchukulia Abu Bakar kuwa ndiye Muislamu wa kwanza ambaye alikuwa na uwezo wa kumuunga mkono na kumsaidia Mtume wa Uislamu (s.a.w.w). [20] Ibn Hajar Katika kitabu "Al-Isaba", yeye alimchukulia Imam Ali (a.s) kuwa ndiye Mwislamu wa kwanza miongoni mwa watoto, Khadijah miongoni mwa wanawake, Zaid bin Harith miongoni mwa wamiliki wa watumwa na Bilal Habashiy ni miongozi mwa watumwa. Yeye amechukulia Abu Bakar kuwa ndiye mtu huru wa kwanza aliyesilimu. [21] Hata hivyo, Muhammad bin Jarir al-Tabari amesimulia kutoka kwa Muhammad bin Sa'ad kwamba; Abu Bakr alisilimu baada ya watu 50 kuingia Uislamu. [22]

Kulingana na maoni ya Rasul Jafarian, mwanahistoria wa Shia; Baadhi ya vyanzo vya kihistoria vilivyomchukulia Abu Bakar kuwa Mwislamu wa kwanza, kwa mujibu wa historia, vyanzo hivyo havina na msingi wowote katika mashiko ya histyoria, ila jambo hilo linatokana na migogoro ya kimadhehebu miongoni mwa Waislamu. [23]

Mpangilio wa orodha ya waliosilimu

Ibn Athir, mwanahistoria wa Kisunni, amewaorodhesha kwa mpangilio; Khadija (a.s), Ali (a.s), Zayd bin Haritha na Abu Bakar kuwa ndio Waislamu wa mwanzo.[24] Muhammad Baqir Majlisi, amewaorodhesha kwa mpangilo; Ali (a.s), Khadijah (a.s) na Ja'afar bin Abi Talib kwa ndiwo waumini wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w). [25]

Vyanzo

  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Riyāḍ al-Ziriklī. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām. Edited by ʿUmar ʿAbd al-Salām al-Tadmurī. 2nd edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1409 AH.
  • Ḥusaynī, Sayyid Karam Ḥusayn. Nakhustīn muʾmin wa agāhānatarīn īmān. Ṣirāṭ, No 10. Fall 1392 Sh.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1385 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd and ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd l-Raḥmān b. Muḥammad. Tārīkh Ibn Khaldūn. Edited by Khalīl Shaḥāda. 2nd edition. Beirut: Dār al-Fikr, 1408 AH-1988.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad b. Manīʿ al-Ḥāshimī al-Baṣrī. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. 1st edition. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1410 AH-1990.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. 1st edition. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. 1st edition. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allah b. Muslim . Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkkāsha. Cairo: Al-hayʾa al-Misrīyya al-'āmma li l-kitāb. 1992 CE.
  • Ibn ʿUqda al-Kūfī, Aḥmad b. Muḥammad. Faḍaʾīl Amīr al-Muʾminīn. Edited by ʿAbd al-Razzāq Muḥammad Ḥusayn Hirz al-Dīn. 1st edition. Qom: Dalīl-i Mā, 1424 AH.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Tārīkh sīyāsī-yi Islām; sīra-yi Rasūl-i Khudā. Qom: Intishārāt-i Dalīl-i Mā, 1380 Sh.
  • Khuṣaybī, Ḥusayn b. Ḥamdān al-. al-Hidāya al-kubrā. Beirut: al-Balāgh, 1419 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. 2nd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Murawwijī Ṭabasī, Muḥammad Jawād. Amīr Muʾminān wa pīshtāzī dar Islām. Farhang-i Kawthar, No 75. Fall 1387 Sh.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī. Imtāʿ al-asmāʾ bimā li-Nabī min al-aḥwāl wa al-amwāl wa al-ḥafda wa al-matāʾ. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Ḥamīd al-Namīsī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1420 AH.
  • Ṣāliḥī Damishqī, Muḥammad b. Yusuf. Subul al-hudā wa al-rashād fī sīrat khayr al-ʿibād. 1st edition. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1414 AH.
  • Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣā'ir al-darajāt fī faḍāʾil-i Āl-i Muḥammad. Edited by Muḥsin Kūchabāghī. 2nd edition. Qom: Kitābkhāna-yi Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. 1st edition. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. 1st edition. Beirut: Dār Ṣādir, n.p.