Aya ya Siqayatu al-Hajji

Kutoka wikishia
Aya ya Siqayatu al-Hajji

Aya ya Siqayatu al-Hajji (Kiarabu: آية سقاية الحاج) ambayo ni Aya ya 19 ya Surat al-Tawba: inatanguliza imani ya kumwamini Mwenye Ezi Mungu, Siku ya Kiama na Jihad katika njia ya Mwenye Ezi Mungu kuwa ni amali bora zaidi kuliko kuwanywesha maji mahujaji na kushika funguo za Masjidi Al-Haram.

Sababu za kuteremshwa kwa Aya hiyo zimetajwa kuwani, pale Abbas bin Abdu al-Muttalib alipojivunia kupokea mahujaji, na Shaiba bin Othman kujivunia kushika funguo za Al-Kaaba. Imamu Ali (a.s) ameitangaza fakhari yake kuwa ni; kumwamini Mwenyezi Mungu, Siku ya Hukumu, na Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, mambo ambayo ni bora zaidi kuliko yale waliokuwa wakijifakharisha akina Shaiba bin Othman. Kwa hiyo Aya iliopo hapo juu, iliteremshwa katika kuunga mkono mtazamo wa imani ya Imamu Ali (a.s).

Baadhi ya wanazuoni wameichukulia Aya hii kuwa ni ushahidi wa ubora wa Imamu Ali (a.s) juu ya Masahaba wengine, na wamelichukulia jambo hili kuwa ndio sababu Imamu Ali (a.s), kuwa na kipaumbele katika uongozi na ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w). Imamu Ali (a.s) pia aliitumia Aya hii katika baraza la watu sita ili kuthibitisha ubora wa hadhi yake mbele ya wengine katika kushika nafasi ya uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w).

Pia Imamu Hassan (a.s) katika mkataba wa amani baina yake na Muawia, aliitumia Aya katika kuthibitisha hadhi na nafsi ya Imamu Ali (a.s.) kwa amani.

Maandishi na Tafsiri ya Aya ya Al-Hajj

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ لَا يَسْتَوُونَ عِنْدَ اللَّهِ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

Je, umeona kuwapa maji Mahujaji na kuushughulikia Msikiti wa Makka, kuwa sawa na anaye muamini Mwenye Ezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenye Ezi Mungu? (Wawili) hao hawafanani mbele ya Mwenye Ezi Mungu, na Mwenyezi Mungu huwaongoi watu madhalimu.



Utambulisho wa Aya

Aya ya 19 ya Surat Tawba inaitwa aya ya Siqayatu al-Hajj. [1] Maana ya Siqayatu Al-Hajj (سقایة الحاج) ni: kuwanywesha au kuwapa maji mahujaji. [2] Katika Aya hii, kuna dhana mbili zinazo kabilana; nazo ni dhana ya kuwanywesha maji mahujaji na kushika funguo na kuulinda Msikiti wa Makka, na dhana ya kumwamini Mwenye Ezi Mungu na Siku ya Kiyama na Jihadi katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. [3] Na Aya hii inawakadhibisha wale wanao jifakharisha kwa kunywisha mahujaji maji na kushika funguo za Masjid al-Haram, na kuhisabu mambo hayo kuwa ni bora zaidi kuliko kumwamini Mwenye Ezi Mungu, Siku ya Kiyama na Jihadi katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. [4]

Nafasi na hadhi ya kunywisha mahujaji maji, sambamba na kushikilia funguo za Al-Kaaba, ilizingatiwa kuwa ni moja ya nafasi zenye hadhi muhimu zaidi kabla ya Uislamu [5] na ilikuwa ni moja ya vitendo vya wazee (wakuu) wa Makka. [6] Nafasi ambazo zilishikiliwa na Bani Hashim [7] ambapo mhusika mkuu kwa wakati huo, alikuwa ni Abbas bin Abdul Muttalib [8] ambaye pia alishikilia nyadhifa hizo baada ya Uislamu, baada ya kupata idhini ya kushika nyadhifa hizo. [9]

Sababu ya Kushuka kwa Aya Hii

Wanazuoni wamesema kwamba; Sababu ya kuteremshwa kwa Aya ya Siqayatu al-Hajj, ni mazungumzo yaliopita kati ya Imamu Ali (a.s), Abbas bin Abd al-Muttalib na Shaiba bin Othman. Jambo hili lilitokea katika hali ambayo wawili hao walikuwa katika majigambo, huku kila mmoja wao akijivunia nafasi aliyokuwa nayo. Abbas alijifhakharisha kwa kawaribisha na kuwakirimu mahujaji, na Shiba bin Othman au Talha bin Shaiba, akielekeza majivuno yake katika kushika funguo na kulinda nyumba ya Mungu. Hatimae, walimteua Imamu Ali (a.s) kuwa ni hakimu, na wakamtaka atoe maoni yake kuhusu ubora wa mojawapo ya nafasi mbili hizo; Kwa kukataa na kukanusha ubora wa nafasi hizi, Imamu Ali (a.s) aliamua kuanzisha aina mpya ya majivuno, ambapo yeye aliamua kujivuni imani kumwamini Mwenye Ezi Mungu, Siku ya Kiyama na Jihadi katika njia ya Mwenye Ezi Mungu, mambo ambayo ni kigezo bora cha imani kwa wawili hao. Baada ya muda fulani, bwana Mtume (s.a.w.w) akapata habari kuhusiana na tukio hilo, na papo hapo ikateremshwa Aya ya Siqayatu al-Hajj na kuthibitisha rai na maoni ya Imamu Ali (a.s). [10]

Asili ya sababu ya kuteremshwa kwa Aya hii imesimuliwa kwa masimulizi kadhaa yenye baadhi ya khitilafu chache tu ndani yake. [11] Baadhi ya wanazuoni wamedai umaarufu wa ijmaa (makubaliano baina ya wanazuoni) juu ya sababu ya kuteremshwa kwake, [12] na wanaamini kwamba Aya hii ilimteremka kwa ajili ya kumuunga mkono Imamu Ali (a.s). [13] Pia Aya hii inachukuliwa kuwa ni miongoni mwa Aya zinazo ashiria hadhi na sifa zake maalum (a.s). [14] Katika Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Imamu Hassan (a.s), [15] Imamu Swadiq (a.s), [16] Abdullah bin Abbas na wengineo [17], imeelezwa ya kwamba; sababu ya kuteremshwa kwa Aya ni Imamu Ali (a.s).

Baadhi ya watu wanaamini kwamba; Aya ya Siqayatu Al-Hajj sio tu kueleza kaninu za msingi katika mambo ya kiitikadi, bali pia ina nia kuelezea tukio lililotokea katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w), na ina mahusiano kamili ya sababu zilizo peleka kushuka kwa Aya hii. [18] Hata hivyo, baadhi ya wengine, kwa kukiri kwamba Aya hii iliteremka kwa ajili ya Imamu Ali (a.s), ila bado waliichukulia marejeo ya Aya hiyo kuwa ni ya jumla, ambayo inaweza kujumuisha ndani yake mifano mingine tofauti, ukiachana na Imamu Ali (a.s). [19] Pia kuna uwezekano mwingine kuhusiana na sababu za kuteremshwa kwa Aya hii [20] ulio tajwa na kujadiliwa katika vitabu vya pande zote mbili za Shia pamoja na Sunni.

Tafakuri Katika Vyanzo

Adhama ya kuteremka kwa Aya hii inahusiana Imamu Ali (a.s), na ndio dhana iliyosimuliwa na kuungwa mkono na wanazuoni wengi kabisa. [22] Miongoni mwa wafasiri wa Kishia waliounga mkono na kunukuu nadharia hii ni; Furaat bin Ibrahim Kufi (aliyefariki mwaka wa 352 Hijiria), [23] na Fadhlu bin Hassan Tabarsi (aliyefariki mwaka 548 Hijiria). [24] Pia kuna wanazuoni kadhaa kutoka upande madhehebu ya sunni walio nukuu dhana hiyo vitabuni mwao, miongoni mwao ni; Fakhru Razi (aliye fariki mwaka 606 Hijiria), [25] Hakim Haskani (aliyefariki mwaka 490 Hijiria), [26] Muhammad bin Jarir bin Yazid Tabari (aliyefariki mwaka 310 Hijiria), [27] Ahmad bin Muhammad Qurtubi (aliyefariki mwaka 761 Hijiria), [28] Abdur Rahman Suyuti (aliyefariki mwaka 911 Hijiria) [29] na Ibn Abi Hatim (aliyefariki 327 Hijiria). [30] Hao ni miongoni mwa wafasiri wa Kisunni waliotaja adhama ya kuteremshwa kwa Aya hii, na kusema kwamba; lilishuka kuhuisana na Imamu Ali (a.s). Kuna zaidi ya vitabu 15 vya tafsiri vya Ahlu al-Sunna vilivyo tajwa katika kitabu Ihqaqu al-Haqqi, ambavyo vinazungumzia sababu ya kushuka kwa Aya hii, vitabu ambavyo pia vinasimulia Hadithi zihusianazo na tukio hilo. [31] Allameh Amini naye pia katika kitabu chake Al-Ghadir amenukuu idadi kubwa ya wanazuoni wa Kisunni walio nukuu riwaya kuhusiana na sababu ya kuteremshwa kwa Aya hii. [32]

Katika vitabu vya hadithi kuna ithibati juu ya sababu ya kushuka kwa Aya hii kuhusiana na Imamu Ali (a.s). [33] Kitabu Sahih Muslim, ni moja ya vitabu vya Hadihti vilivyo nukuu na kuelezea sababu hiyo hiyo iliyo elezewa hapo juu kuhusiana na kushuka kwa Aya hii. Ila kitabu hichi kimenukuu tukio hilo bila ya kutaja majina ya watu ya waliomo katika tukio hilo, na imetosha kurekodi kisa cha tukio hilo kwa kutumia jina la "Rajul" (mtu). [34] Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wengine wa Kisunni wanaorejelea riwaya au tukio hili, wameashiria Hadithi nyingine ambapo ndani yake mmetajwa majina ya watu hao. [35] Hata hivyo, Ibn Taymia, mmoja wa wanazuoni wa Kiwahabi, amekanusha kuteremshwa kwa aya hii kwa ajili ya Imamu Ali (a.s). [37]

Uhalali wa Kisa cha Tukio Lililopelekea Kushaka kwa Aya Hii

Wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Imamiyyah wanakubaliana wote kwa paomja ya kwamba; Aya ya “Siqayah al-Hajji” iliteremka kuhusiana na Imamu Ali (a.s). [38] Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Ali Milani, ambaye ni mwanazuoni wa zama hizi, hati ya adhama ya kuteremshwa kwa Aya juu ya Imamu Ali (a.s), ni sahihi na vyanzo vya ripoti hii ni miongoni mwa vyanzo vinavyotegemewa sana katika elimu ya Hadithi na tafsiri, na ni ripoti iliyoripotia kupiti njia na matabaka mbali mbali ya wapokezi wa Hadithi. [39] Baadhi ya waandishi wanaamini ya kwamba; mwakisiko utokao katika vyanzo na vitabu mbali mbali kuhusiana na sababu ya kuteremka kwa Aya hii, unatoa mwanga tosha na kuondoa shaka juu ya uhalisia na sababu ya kushuka kwake. [40] Mwandishi wa kitabu Ihqaqu al-Haqqi ameandika akisema kwamba; sababu zilizonukuliwa juu ya kushuka kwa Aya hii ni sahihi, na akasema kwamba: hakuna khitilafu miongoni mwa wanazuoni juu ya kwamba Aya hii ilishuka kuhusiana na Imamu Ali (a.s. [41]

Je, Aya Hii Inahusiana na Makabiliano Baina ya Waumini na Makafiri?

Baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba; Aya ya Siqayatu al-Hajji inahusina na matokeo yaliotokea Madina baada ya kusilimu kwa Abbas bin Abd al-Muttalib. Kwa hiyo, makabiliano haya yametokea baina ya makundi mawili ya waumini wenyewe kwa wenyewe. [42] Hata hivyo, baadhi ya wengine wameona kwamba; Aya hii iliteremshwa kabla ya kusilimu kwa Abbas [43] na wameutambua mgongano huu kuwa ni mgongano wa makabilano baina ya waumini na makafiri. [44] Katika moja ya Riwaya imeelezwa ya kwamba; Abbas alikataa ombi la Imamu Ali (a.s) la kuhama Makka kwenda Madina akitoa hoja na kusema kunywesha maji mahujai, ni bora zaidi kuliko kuhajiri,[45] au pale Abbas alipotekwa katika vita vya Badri, alisema kuwaambai Waislamu; ikiwa nyinyi umetutangulia sisi kusilimu kwenu, basi tambueni ya kwamba, tumekutangulie katika kuwanywe maji mahujaji na kuimarisha Al-Kaaba. [46] Katika baadhi ya ripoti emeelezwa ya kwamba; makabiliano haya yalitokea kati ya kundi la Waislamu na Wayahudi ambao walidai kwamba; vitendo vya kuwanwisha maji mahujaji pamoja na kushika funguo za msikiti wa Makka, ni bora zaidi kuliko imani ya kumwamini Mungu na kushiriki Jihad. [47]

Kwa mujibu wa maoni ya Sheikh Tusi juu ya Aya hii ni kwamba;, Mwenye Ezi Mungu katika aya hii amelihutubu kundi maalumu la makafiri waliokuwa wakijishughulisha katika kuwapa maji mahujaji na kuitunza Masjid al-Haram, ambao waliona kuwa; vitendo hivyo ni sawa au ni bora zaidi kuliko imani ya kumwamini Mungu na kushiriki jihadi. [48] Hapa inafahamika ya kwamba; Aya ya Siqayatu al-Hajji ina nia ya kusema kuwa, tendo lolote lile litendwalo bila kushikamanishwa na imani ya kumwamini Mwenye Ezi Mungu, hata kama litakuwa ni tendo jema kiasi gani mbele ya watu, ila mbele ya Allah halitaweza kuhimidiwa wala kupewa thamani. [49]

Qur'an na Kuhifadhi Heshima za Watu

Allameh Tabatabai anasema kuwa; Aya hii imekuja kufafanua na kutathimini matendo mawili, mojawapo ni tendo la kijahilia ambalo ni tendo la yule mtu asiyekuwa na imani juu ya Allah, na la pili ni la yule mtu mwenye ya kumwamini Mwenye Ezi Mungu na Siku ya Kiyama. Kulingania na tathmini ya Aya hii; kile kitendo cha asiyekuwa na imani, ni kitendo kisicho kuwa na uhai, ambacho hakiwezi kutoa matunda endelevu. Kwa upande wa pili kitendo kilicho hai chenye athari na manufaa endelevu, ni kile kitendo kilicho shikamanishwa na imani safi ya kumwamini Mwenye Ezi Mungu. Hivyo basi, madai ya usawa huu au malinganisho mawili haya yalio fanya, kati ya kazi yausambazaji wa maji na ukarabati uhifadhi wa Msikiti Mkuu Makka, hayawezi kuwa ni malinganisho ya kimantiki. Lakini ili Mwenyezi Mungu kutoa uwamuzi wa wazi juu ya malumbano hayo, pamoja na kuhifadhi hadhi pamoja na majina yao, ilibidi ateremshe Aya hii ambayo mwisho wake imemalizia kwa kusema:

«وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ»
Na Mwenye Ezi Mungu haliongozi kundi la madhalimu

Amefanya hivyo bila ya kumtuhumu yeyote yule kati yao, na kumpa sifa ya udhalimu. Lakini alifafanua na kuweka wazi ya kwamba; katu amali hizo haziwezi kulinganishwa na amali za waumini (kumwamini Mungu, jihadi, na kuhajiri). [50]

Malumbano

Pale Imamu Ali (a.s) alipokuwa katika baraza la watu sita lililo undwa baada ya kifo cha khalifa wa pili ili kuamua ni nani wa kushika nafasi ya khalifa, yeye aliisoma Aya hii mbele ya baraza hilo, ili kuthibitisha namna ya kustahiki kwake na ubora wake juu ya kushika nafasi ya ukhalifa. [51] Vile vile aliitaja Aya hii katika kujibu swali aliloulizwa kuhusiana na hadhi na bora wake. [52]

Imamu Hassan (a.s) pia aliitaja Aya hii katika khutba yake kwenye mkataba wa amani baina yake na Muawia. [53] Maamun Abbasi pia aliitaja Aya hii katika barua yake kwa Mahashimu (ukoo wa bwana Mtume (s.a.w.w)), ambapo ndani yake alimsifu Imamu Ali (a.s) na kuzungumzia ubora wake juu ya Abbas bin Abdul Muttalib. [54] Pia kisa hichi cha kujifakharisha kilichopelekea kuteremshwa kwa Aya hii kinapatika ndani maandishi ya washairi kama vile; Sayyid Hamyari, Al-Naashi, na Al-Bashnawi. [55]

Ashirio Juu ya Unaibu wa Imamu Ali (a.s)

Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba; Aya ya Siqayatu al-Hajji iliteremka ili kueleza na kuonesha ubora wa Imamu Ali (a.s) [56] ambapo Aya hii inaonyesha ubora alio nao Imamu Ali (a.s) juu ya masahaba wengine, [57] na pia anaonesha na kuthibitisha kipaumbele cha Imamu Ali (a.s) katika uongozi na ukhalifa baada ya bwana Mtume (s.a.w.w). [58] Pia imesemwa ya kwamba; maana ya Aya hii iko wazi kabisa juu ya kuthibitisha haki ya Imamu Ali (a.s.) katika uongozi. [59] Hii ni kwa sababu ya kwamba; kwa mujibu wa maoni ya kila mtu, Imamu alikuwa ni mbora zaidi kuliko masahaba wengine wote katika suala la imani ya Mwenye Ezi Mungu, na pia katika uhajiri na jihadi. [60]

Mfasiri wa Kishia ajulikanaye kwa jina la Makarimu Shirazi anaamini ya kwamba; kwa kuzingatia ubora wa Imamu Ali (a.s) katika imani na jihadi juu ya wengine, ikiwa Mungu atataka kumchagulia mrithi wa Mtume (a.s), bila shaka atamtanguliza yule aliye bora zaidi kuliko mbora wa kawaida na atamweka yeye mbele kuliko yule ubora wa daraja ya chini. Hii ni kwa sababu Mungu ni mwenye hekima, na kumtanguliza mwenye ubora wa kawaida na mwenye ubora wa chini mbele ya aliye na ubora wa hali ya juu, ni kinyume na hekima. Na ikiwa suala la kumchagua ukhalifa liko mikononi mwa watu, basi katu wenye akili hawamchagua mwenye draja ya kawada au mwenye daraja ya chini licha ya kuwepo mwenye daraja ya juu zaidi. [61]

Vyanzo

  • A Group of Authors. Fī riḥāb Ahl al-Bayt. 2nd edition. Qom: al-Majmaʿ al-ʿĀlamī li Ahl al-Bayt, 1426 AH.
  • Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn. Al-Ghadīr fī al-kitāb wa al-sunna wa al-ʾadab. Qom: Markaz al-Ghadīr li-l-Dirāsāt al-Islāmiyya, 1416 AH.
  • ʿAskarī, Sayyid Murtaḍā. Maʿālim al-madrasatayn. 4th edition. Tehran: Muʾassisat al-Biʿtha, 1412 AH.
  • Astarābādī, Muḥammad Jaʿfar. Al-Barāhīn al-qāṭiʿa fī sharḥ tajrīd al-ʿaqāʾid al-sāṭiʿa. Edited by Markaz Muṭāliʿat wa Taḥqīqāt-i Islāmī. Qom: Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1382 Sh.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmiyya al-Islāmiyya, 1380 Sh.
  • Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Bunyād-i Biʿthat, 1416 AH.
  • Daylamī, Ḥasan b. Abī l-Ḥasan al-. Irshād al-qulūb. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1412 AH.
  • Faḍl Allāh, Sayyid Muḥammad Ḥusayn. Tafsīr min waḥy al-Qur'ān. Beirut: Dār al-Milāk li-Ṭabā'at wa al-Nashr, 1419 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Furāt al-Kūfī, Abu l-Qāsim Furāt b. Ibrāhīm. Tafsīr furāt al-kūfī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1410 AH.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. ʿAbd Allāh al-. Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
  • Hilālī, Sulaym b. Qays. Kitāb Sulaym b. Qays. Qom: Al-Hādī, 1405 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Minhāj al-karāma fī maʿrifat al-imāma. Mashhad: Muʾassisa ʿĀshūrā, 1379 sh.
  • Ḥusaynī astarabādī, Sharaf al-Dīn ʿAlī . Taʾwīl al-āyāt al-ẓāhira. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1409 AH.
  • Ḥuwayzī, ʿAbd ʿAlī b. al-Jumʿa al-. Tafsīr nūr al-thaqalayn. Qom: ʿIsmā'ilīyān, 1415 AH.
  • Ibn ʾAbī Ḥātam, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad. Tafsīr al-Qurān al-ʿAẓīm. Edited by ʾAsʿd Muḥammad al-Ṭayyib. 3rd edition. Saudi Arabia: Maktabat Nazār Muṣṭafā al-Bāz, 1419 AH.
  • Ibn ʿAṭiyya, ʿAbd al-Ḥaqq b. Ghālib. Al-Muḥarrar al-wajīz fī tafsīr al-kitāb al-ʿazīz. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1422 AH.
  • Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Zād al-masīr fī ilm al-tafsīr. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1422 AH.
  • Ibn Ḥayyūn, Nuʿmān b. Muḥammad. Daʿāʾim al-islām wa dhikr al-ḥalāl wa al-ḥarām wa al-qaḍāyā wa al-aḥkām. 2nd edition. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt(a), 1385 AH.
  • Ibn Ḥayyūn, Nuʿmān b. Muḥammad. Sharḥ al-akhbār fī faḍāʾil al-aʾimmat al-aṭhār (a). First edition. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1409 AH.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH-1986.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. 1st edition. Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiyya, 1419 AH.
  • Ibn Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā. Al-Taraʾif fī maʿrifat madhāhib al-ṭawāʾif. Qom: Khayyām, 1400 AH.
  • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Minhāj al-sunna al-nabawīyya fī naqd kalām al-shīʿa al-qadarīyya. Edited by Muḥammad Rashād Sālim. [n.p]: Jāmiʿat al-Imām Muḥammad b. Saʿūd al-Islāmīyya, 1406 AH/1986. [n.p].
  • Jaʿfarī, Yaʿqub. Tafsīr kawthar. Qom: Muʾassisat Intishārāt-i Hijrat, 1376 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Āyāt al-wilāya fī l-Qurʾān. Qom: Madrasat al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib (a), 1383 sh.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 Sh.
  • Mīlānī, Sayyid ʿAlī al-. Sharḥ minhāj al-karāma. Qom: Markaz al-Ḥaqāʾiq al-Islāmiyya, 1386 sh.
  • Muqaddas al-Ardibīlī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Ḥadīqat al-shīʿa. Third edition. Qom: Intishārāt-i Anṣārīyān, 1383 sh.
  • Muslim b. Ḥajjāj. Ṣaḥīḥ Muslim. Edited by Muḥammad Fuʾād ʿAbd al-Bāqī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabiyya, 1412 AH.
  • Muzaffar, Muḥammad Ḥasan. Dalāʾil al-ṣidq. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1422 AH.
  • Qirāʾatī, Muḥsin. Tafsīr-i nūr. Tehran: Markaz-i Farhangī-yi Dars-hā-yi az Qurʾān, 1388 Sh.
  • Qurtubī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Al-Jāmiʿ li-aḥkām al-Qurʾān. 2nd edition. Cairo: Dār al-Kutub al-Miṣriyya, 1384 AH.
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Third edition. Qom: Dār al-Kitāb, 1363 Sh.
  • Shūshtarī, Nūr Allāh al-Ḥusaynī al-. Iḥqāq al-ḥaqq wa izhāq al-bāṭil. Edited by Marʿashī al-Najafī. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatollāh Marʿashī al-Najafī, 1409 AH.
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatollāh Marʿashī al-Najafī, 1404 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Al-Mustarshid fī imāmat Amīr al-Muʾminīn ʿAlī b. Abī Ṭālib. Qom: Muʾassisat al-Wāṣif, 1415 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jāmiʾ al-bayān fi tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʾrifa, 1412 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abū l-Faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dār al-Turāth, 1387 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. 2nd edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Muḥammad Jawād Balāghī. 3rd edition. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
  • Ṭabrisī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Al-Iḥtijāj. Mashhad: Nashr al-Murtaḍā, 1403 AH.
  • Thaʿālibī, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad al-. Tafsīr al-thaʿālibī al-musammā bi l-jawāhir al-ḥisan fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
  • Thaʿlabī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Al-Kashf wa l-bayān ʿan tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1422 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Aḥmad Qaṣīr al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī yaʿqūb.Tārīkh-i yaʿqūbī. Beirut: Dār Ṣādir, [n.d]
  • Ziriklī, Khayr al-Dīn al-. Al-Aʿlām. Eighth edition. Beirut: Dār al-ʿIlm li-l-Malāyyīn, 1989.