Kisa cha kuzawadia pete

Kutoka wikishia

Kisa cha Kuzawadia Pete ni tukio la Imam Ali (A.S) ambapo mtukufu huyo alitoa pete yake akiwa kwenye rukuu akisali, na kumzawadia pete hiyo masikini aliyekuwa akiomba msaada. Tukio hili limesimuliwa katika vitabu mbali mbali vya Hadithi vya Waislamu wa madhehebu ya Shia pamoja na Sunni. Kwa mujibu wa kauli za wafasiri, Aya ya Wilaya iliteremshwa kuhusiana na tukio hili. Tukio hili linahisabiwa kuwa ni miongoni mwa matukio yanayoashiria sifa na hadhi aliyonayo Imam Ali bin Abi Talib (A.S).

Baadhi ya mafaqihi wa Kishia, wakitegemea kisa hicho cha Imam Ali (A.S) kinachohusiana na yeye kutoa pete yake na kumzawadia fakiri hali akiwa yupo katika hali ya kurukuu, wamesema kwamba: Kisa hichi kinaashira kwamba; baadhi ya vitendo vidogo vidogo katika mwili wa mwenye kusali, haibatilishi sala. Baadhi ya watu wamekosoa kwa kusema kwamba; Kusikiliza sauti za watu wengine wakati wa Sala hakuendani na hali za unyenyekevu wa Imamu Ali (A.S) zilizosimuliwa kutoka kwake, ambapo yasemekana yeye alikuwa na unyenyekevu wa hali ya juu kabisa katika sala zake. Katika kujibu ukosoaji huo, imejibiwa ya kwamba; Matendo yote mawili ya Imamu Ali (A.S), yaani sala pamoja na utoaji wake sadaka wa pete hali akiwa katika hali ya kusali, ni matendo yaliotendwa kwa ajili ya radhi za Mwenye Ezi Mungu; Kwa hiyo, hakuna mgongano kati ya matendo mawili hayo. Asili ya Tukio Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, siku moja maskini aliingia kwenye msikiti wa Mtume (S.A.W.W) na kuomba msaada; Lakini hakuna mtu aliyempa chochote. Katika hali hiyo yeye Akainua mikono yake mbinguni na kusema: Mungu! shuhudia ya kwamba niliomba msaada katika msikiti wa Mtume wako; Lakini hakuna mtu aliyenipa chochote. Wakati huohuo, Ali (A.S) ambaye alikuwa yupo mkatika hali ya kurukuu, akaashiria kwa kidole chake kidogo cha mkono wake wa kulia, yule maskini akakaribia na kuitoa pete ilioko kidoleni mwake. [1] Sheikh Mufid amezingatia tarehe ya tukio hil, kuwa ni tukio lililotokea mwezi 24 Dhul Hijjah. [2] Kwa mujibu wa riwaya nyingine, Mtume (S.A.W.W) alimtuma Imamu Ali (A.S) kwenda Yemen, alipofika Makka alikwenda kusali, na alipokuwa amerukuu katika sala yake, alitoa pete yake na kumpa masikini. [3] Faidhu Kashani (aliyefariki mwaka 1091 Hijiria) ametilia shaka ya kwamba; Aya inayohusiana na kisa hichi imeteremshwa baada ya yeye kutoa pete yake ya pili. [4]

Kuna washairi walotunga mashairi kuhusiana na tukio la Kisa cha Zawadi ya Pete, mmoja wa washairi waliotunga mashairi kuhusiana na kisa hicho, ni Mohammad Hossein Shahriyar aliyetunga shairi lake la Khatambakhshi Hazrat Ali (A.S) katika ubeti wa shairi lake hilo maarufu anasema:

برو ای گدای مسکین در خانه علی زن * که نگین پادشاهی دهد از کرم گدا را[5] Nenda, ewe mwombaji maskini, kwenye nyumba ya Ali na ugonge mlango wake, ambaye hutoa kito cha mfalme (pete) na kumpa mwombaji.

Hasan bin Thabit, mshairi wa karne ya kwanza ya Hijiria, naye pia kuhusu hili aliandika mashairi yafuatayo:


أبا حَسَنٍ تَفدیکَ نَفسی ومُهجَتی * وکُلُّ بَطیءٍ فِی الهُدی ومُسارِعِ أیَذهَبُ سَعیٌ فی مَدیحِکَ ضائِعا ؟!* ومَا المَدحُ فی جَنبِ الإِلهِ بِضائِعٍ فَأَنتَ الَّذی أعطَیتَ إذ کُنتَ راکِعاً * فَدَتْکَ نُفوسُ القَومِ یا خَیرَ راکِعٍ فَأَنزَلَ فیکَ اللّهُ خَیرَ وِلایَة * فَثَبَّتَها فی مُحکَماتِ الشَّرائِعِ.]۶[

Ewe Abul Hasan! Maisha yangu na familia yangu viwe muhanga kwa ajili yako, na yeyote aliye kwenye njia ya uongofu, awe mpole na mwepesi kujitoa muhanga kwako. Je, hivi sifa za wapenzi wako kwako juu yako zitaweza kuharibiwa (kupotoshwa)? Kamwe sifa hii (ya kutoa pete), haififii mbele ya Mungu wala haziwezi kutoweka. Wewe ndiye uliyetoa ukiwa katika rukuu. Ewe Ali! roho za watu wote ziwe ni muhanga kwako, Ewe mbora wa kurukuu mbele ya Mwenye Ezi Mungu. Mungu akakupa cheo bora na utukufu zaidi katika utukufu wako na akauelezea na kukuthibitisha katika sheria madhubuti za dini.

Nasser Khosrow pia katika beti mbili zake za mashairi yake anasema: آنچه علی داد در رکوع فزون بود * زانکه به عمری بداد حاتم طائی گر تو جز او را به جای او بنشاندی * والله والله که بر طریق خطائی Alichotoa Ali akiwa katika Rukuu kimepindukia, kiwango alichotoa Hatim Ta'i katika uri wake mzima. Ukiwa wewe umekali nafasi ambayo ni mahali pake yeye, Wallahi, Wallahi, Elewa kwamba wewe uko kwenye kwenye kosa adhima.

Kuteremka kwa Aya ya Wilayah Makala asili: Aya ya Wilayah Tafsiri kuhusiana na sababu ya kuteremshwa kwa Aya isemayo:

«إِنّما وَلیکُمُ اللهُ و رَسولُهُ والّذینَ ءَامَنوا الَّذینَ یقِیمُونَ الصَّلوةَ و یؤتُونَ الزَّکوة و هُم راکِعونَ»

“Hakika kiongozi wenu (mwenye mamlaka juu yenu) ni za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na walioamini, ambao wanasimamisha sala, na wakatoa sadaka hali wakiwa katika hali ya kurukuu." [8] Wafasiri mashuhuri wa Qur'ani wanakubaliana kuwa Aya hii iliteremka  kuhusiana na kisa cha Ali (A.S) kutoa pete yake hali akiwa katika sala. [9] Kulingana na kauli ya mwanatheolojia wa Kisunni, Qadhi 'Adh-du Al-Diin Iijiy ni kwamba; Wafasiri wa Qur'rani wana kauli moja (wana ijmaa) ya kwamba Aya hii imemshukia Ali bin Abi Talib (A.S),[10] ingawaje baadhi ya wafasiri wa madhehebu ya Kisunni wana dhana ya kwamba; Aya hii imewashukia waumini wengine. [11]

Wengi miongoni mwa Masahaba akiwemo Ibnu Abbas, [12] Ammar, [13] Abu Dharr, [14] Anas Ibnu Malik, [15] Abu Raafi'i Madani [16] na Miqdad [17] wamesema kwamba; Aya ya Wilayah inahusiana na Imamu Ali (A.S) ambapo imeteremka baada ya Ali kutoa pete yake na kumpa maskini. Vitabu vya Hadithi pamoja na tafsiri za kutoka pande zote mbili zimenukuu kisha hichi cha Hadhrat Ali (A.S) kutoa pete yake na kumpa maskini huku akiwa katika hali ya kurukuu. [18]

Wasifu wa Pete Imepokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (A.S) ya kwamba; Uzito wa pete ya Imamu Ali (A.S) aliyoitoa na kumpa maskini, ilikuwa na uzito wa kiasi cha gramu 20.20, na uzito wa kito chake ni kiasi cha gramu 24.25, na asili ya kito chake ilikuwa ni yakuti nyekundu. Pete hii ilikuwa ni ya Marwan Bin Touq, ambaye aliuawa na Imamu Ali (A.S) katika vita. Kisha Ali akaichukua pete hiyo na kuipeleka kwa Mtume (S.A.W.W) kama ngawira ya vita. Mtume (S.A.W.W) pia akampa yeye kama zawadi. [19] [Maelezo 1] Katika Hadithi za kitabu Majma'u Al-Bayan, hakuna maelezo zaidi kuhusiana na wasifu wa pete hiyo, ispokuwa kilichoelezewa kuhusiana na wasifu wake, ni kwama ilikuwa ni pete inayotokana na madini ya fedha. [21]

Hadhi ya Kisa cha Pete Katika Matumizi ya kisheria Baadhi ya mafaqihi wa Kishia wamekitegemea kisa hichi cha Imamu Ali (A.S) cha kutoa pete hali akiwa katika sala, kuwa ni moja za ithibati katika kuthibitisha kwamba; Mtu anaweza kuvishughulisha baadhi ya viungo vya mwili wake huku akiwa katika sala. [22] Pia kwa kuzingatia tukio la kisa hicho, wamehitimisha kwamba; Nia ya moyoni inatosha katika kutekeleza ibada, na wala hakuna ulazima wa kutamka kwa mdomo. [23] Pia kutoka na kule Aya kutambua sadaka ya Imamu Ali (A.S) kwa jina la zaka, baadhi ya wanazuoni wamesema sadaka ya kawada pia ni moja ya aina za zaka. [24] Kuna wengine waliosema kuwamba; Hakuna uwiyano baina ya umakini na unyeyekevu wa Imamu Ali (A.S) katika sala, ulionukuliwa na riwaya kadhaa, na kule yeye kusikia sauti ya masikini aliyekuwa akiomba, hali akiwa yeye yumo kwenye sala. Walioijibu hoja hii wamesema ya kwamba; Sala ya Imamu Ali (a.s.) na tendo lake la kutoa sadaka pete yaka hali akiwa yumo kwenye sala, yote mawili yametendeka chini ya msingi mmoja, nao ni kutaka radhi za Mwenye Ezi Mungu. Pia kuna Hadithi zilizosema ya kwamba; Pale Mtume (S.A.W.W) alipoisikai sauti ya kilio cha mtoto alikuwa akifanya haraka kuimaliza sala anayosalisha ili mama wa mtoto awahi kumshughulikia mwanawe. [25] [Maelezo 2] Allama Majlisi amesema kwamba; kule mtu kujishighulisha na ibada nyengine hali akiwa katika sala, haipingani na ukamilifu wa swala na hudhurio la moyo wake katika sala hiyo [26] Baadhi ya wanafikra wa fani ya tasawwuf pia wamehalalisha tendo la Imamu Ali (A.S) la kutoa sadaka huku akiwa yumo kwenye sala. Wao wametumia hoja ya kwamba nafsi zenye nguvu na zilizokomaa kiuchamungu, zinaweza kufanya ibada zaidi ya moja kikamilifu kwa wakati mmoja na kwa uangalifu kamili. Kwa hiyo Imamu Ali (A.S) hakupoteza umakini na unyenyekevu wake pale alipotoa sadaka pete yake hali akiwa yupo katika hali ya kurukuu, bali yeye aliendelea kumuabudu Mungu kiukamilifu bila ya kupoteza ubora na umakini wa sala yake. [chanzo kinahitajika]