Nenda kwa yaliyomo

Saqi Kawthar

Kutoka wikishia

Saqi Kawthar (Kiarabu: ساقي الكوثر) Katika Uislamu bali katika istilahi za upande wa madhehebu ya Shia, jina Saqi Kawthar ni jina maarufu la Ali bin Abi Talib. Jina hili linamaanisha kwamba yeye ni mnyweshaji atakaye wanywesha watu maji kutoka katika chemchemi ya Kawthar.

Saqi Kawthar ni mchanganyiko wa maneno mawili; Saqi na Kawthar. Saqi inamaanisha mnyweshaji au anayetoa kinywaji (pombe) na kuwapa wengine. [1] Hapo zamani neno, Saqi lilikuwa ni jina apewalo mtu mwenye kumimina maji kwenye kikombe na kumpa mtu mwingine. Neno Kawthar nalo lina maana ya neema nyingi au kheri nyingi. [2]

Baadhi ya wafasiri wamelifasiri neno Kawthar lililoka katika Aya ya kwanza ya Surat al- Kawthar kwa maana ya hodhi maalumu ambalo ametunukiwa bwana Mtume (s.a.w.w) na Mola wake, ambapo maji yake ni meupe zaidi kuliko maziwa, na ni matamu zaidi kuliko asali. [3] [Maelezo 1] Kulingana na Riwaya za pande zote mbili Shia na Sunni, ni kwamba; Imam Ali (a.s) ndiye “Saqi” wa Hodhi hiyo Kawthar. [4] Muhyiddin Arabi katika tafsiri yake amelifasiri neno “Kawthar” kama ni mto wa Peponi ambao yeyote anayekunywa kutoka katika mto huo, kamwe hatapatwa na maishani mwake. [5] Katika mashairi pia, Imam Ali (a.s) ametajwa kuwa ndiye “Saqi Kawthar”. [6]

Maelezo

  1. (نهر فِي الْجنَّة أعطانيه رَبِّي لَهو أَشد بَيَاضًا من اللَّبن وَأحلى من الْعَسَل) Yaani bwana Mtume (s.aw.w) amesema: “Kawthar ni mto wa Peponi niliopewa na Mola wangu, maji yake ni meupe kuliko maziwa na ni matamu kushinda asali”.

Vyanzo

  • ʿAṭṭār Neyshābūrī, Farīd al-Dīn Muḥammad. Manṭiq al-ṭayr. Edited by Sayyid Sādiq Guharīn. Tehran: Bungāh-i Tarjuma wa Nashr-i Kitāb, 1356 Sh.
  • ʿAmīd, Ḥasan. Farhang-i lughāt-i ʿAmīd. Edited by Farhād Qurbānzāda. 1st edition. Publisher: Ashjaʿ, 1389 Sh.
  • Dīwan-i Khawja Shams al-Dīn Muḥammad Ḥāfiz Shīrāzī. Edited by Muḥammad Riḍā Jalālī Naʾīnī and Nadhīr Aḥmad. Tehran: Amīr Kabīr, 1361 Sh.
  • Khurramshāhī, Bahāʾ al-Dīn. Dānishnāmah-yi Qurʾān wa Qurʾān pazhūhī. Entry Al-Batul. Tehran: Dūstān wa Nāhīd, 1377 Sh.
  • Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Al-Manāqib. Edited by Mālik Mahmūdī. Qom: 1414 AH.
  • Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Edited by Najdat Najīb. Beirut: 1421 AH/2001.
  • Ṭabarī, Aḥmad b. ʿAbd Allāh. Dhakhāʾir al-ʿuqbā fī manāqib dhawi al-qurbā. Cairo: 1356. Beirut: lithography, [n.d].