Nenda kwa yaliyomo

Kufikisha Aya za Baraa

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na Iblagh Ayaat al-Baraah (kufikisha Aya za Baraa). Kama unataka kujua kuhusiana na Aya zenye jina kama hili, angalia makala ya Ayaat al-Baraa.

Iblagh Ayaat al-Baraa (Kiarabu: إبلاغ آيات البراءة) ni kusomwa Aya za mwanzo za Surat al-Tawba na Imamu Ali (a.s) katika mkusanyiko wa washirikina wa Makka mwaka wa 9 Hijiria. Awali Mtume (s.a.w.w) alimkabidhi jambo hilo Abu Bakr bin Abi Quhafa; lakini kwa amri ya Alla akabadilisha uamuzi huo na kumkabidhi Imamu Ali (a.s). Hadithi ambayo inabainisha tukio hili imenukuliwa kwa sura ya mutawatir (mapokezi mengi) katika vyanzo vya Shia na Sunni.

Tukio hili limetambuliwa katika vyanzo vya historia na hadithi kuwa ni katika fadhila za Imamu Ali (a.s). Kadhalika kwa mujibu wa hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya Kishia na Kisunni Imamu Ali akiwa na lerngo la kuthibnitisha ubora wake kwa masahaba wengine na kustahiki kwake Ukhalifa alitumia tukio hili kama hoja.

Umuhimu na nafasi

Kusoma Imamu Ali (a.s) Aya za Baraa (kujitenga) mwaka wa 9 Hijiria katika mkusanyiko wa washirikina mjini Makka kunahesabiwa kuwa ni katika fadhila zake. [1] Allama Amini amelitaja tukio hili katika kitabu chake cha al-Ghadir na kueleza kwamba, tukio hili limenukuliwa katika vyanzo mbalimbali vya Kishia na Kisunni. [2]

Ufafanuzi wa tukio

Aya za Baraa (kujitenga) zilishuka mwishoni mwa mwaka wa 9 Hijiria [3] na Mtume (s.a.w.w) alitakiwa kuzifikisha Aya hizo kwa washirikiana mwezi Dhul-Hijja mwaka huo huo wakati wa mkusanyiko wa washirikina mjini Makka. [4] Kuhusiana na namna ya kufikisha Aya hizi, hilo limeelezwa katika vyanzo vya kihistoria na hadithi vya Wasilamu wa Kishia na Kisuni. Baada ya Aya kumi za mwanzo katika Surat al-Tawbah kushushiwa Mtume, alichofanya Mtume ni kumuita Abu Bakar na kumtuma akawasomee watu wa Makka Aya hizi. Kisha Mtume akamuita Imamu Ali (a.s) na kumwambia amfuate na kumuwahi Abu Bakr na popote kabla hajafika Makka na atakampata achukue kutoka kwake Aya hizo na kisha aende Makka na kuwasomea wakazi wa huko. Imamu Ali (a.s) alifanikiwa kumkuta na kumuwahi Abu Bakr katika eneo la al-Juhfah na akachukua maandiko hayo kutoka kwake. Abu Bakr alirejea kwa Mtume na kusema: Ewe Mtume wa allahm je kuna kitu kimeshuka kuhusu mimi? Mtume akasema: Hapana, Jibril amenijia na kusema: Ujumbe huu wa Mwenyezi Mungu hawezi kuufikisha isipokuwa wewe au mtu kutoka katika familia yako. [5]

Allama Amini anasema, tukio hili limenukuliwa kwa sura ya mutawatir (mapokezi mengi) na wapokezi mbalimbali wa hadithi. [6] Hata hivyo kuna tofauti ndogo katika nukuu ya tukio hili; kama vile, awali Mtume aliwapa ujumbe huo Abu Bakr na Omar (sio Abu Bakr tu), kisha akamtuma Ali awafuate [7] au eneo ambalo Imamu Ali alimkuta na kumfikia Abu Bakr lilikuwa Dhul-Hulaifah. [8]

Sababu ya kushuka Aya za Baraa

Makala asili: Aya za Baraa

Makka ambayo ilikuwa kitovu kikubwa zaidi cha shirki mkabala wa Mtume (s.a.w.w), [9] mwaka wa 8 Hijiria mji huo uliangukia mikononi mwa Waislamu katika Fat’h Makka (kukombolewa Makka); [10] pamoja na hayo baadhi ya makabila yalikuwa yakisimama kidete kukabiliana na Uislamu. [11] Mpaka mwaka awa 9 Hijiria ambao ni mashuhuri kwa jina la Sannat al-Wufud (mwaka wa timu za wawakilishi), [12] makabila mengi yalituma timu za wawakilishi kwa Mtume (s.a.w.w) na kutangaza kusilimu kwao. [13] Baada ya kubadilika mahesabu ya kisiasa kwa maslahi ya Uislamu, Aya za Baraa (kujitenga) zikashuka ambapo zilikuwa zikieleza kutokubalika kuweko shirki na kutovumilika kwake. [14] Kadhalika imeelezwa kuhusiana na kushuka Aya hizi kwamba: Washirikina ambao walitiliana saini mkataba na Mtume (s.a.w.w) katika Sulhu ya Hudaibiya ya kwamba, wawachie fursa ya siku tatu Waislamu kwa ajili ya ibada ya Hija [15] walikiuka mkataba huo na walikuwa wakitufu wakiwa uchi katika msimu wa Hija. [16] Katika Tafsir Nemooneh na katika kufasiri Aya hizi, kumeelezwa na kubainishwa hatua ya washirikina ya kukiuka mara kwa mara mkataba huo. [17]

Maudhui ya ujumbe wa Mtume (s.a.w.w)

Imamu Ali bin Abi Talib (a.s) aliwasili Makka baada ya adhuhuri ya siku ya Eidul al-Adh’ha (Idi ya kuchinja) na akajitambulisha kuwa ni mjumbe wa Mtume wa Allah na kisha akawasomea washirikina wa Makka Aya za mwanzo katika Surat Tawba na kisha akasema: “Kuanzia sasa na kuendelea hakuna mtu kutufu Kaaba akiwa uchi, na hakuna mtu yeyote miongoni mwa washirika ambaye ana haki ya kufanya ziara katika Kaaba mwaka ujao na kila mtu miongoni mwa washirikina ambaye alifunga mkataba na Mtume (s.a.w.w), itibari na muda wake ni miezi minne.” [18] Imekuja katika kitabu cha Tarikh Ya’qubi: Imamu Ali (a.s) aliwasome watu wa Makka Aya za Baraa na akawapa amani na kisha akasema: “Kila ambaye ana mkataba na Mtume wa miezi minne, basi Mtume yupo thabiti katika mkataba wake na kila ambaye hana mkataba naye, Mtume amempatia siku 50. [19]

Inaelezwa kuwa, kuondolewa suala la amani kwa washirikina kulitokana na wao kukiuka mkataba na kutotekeza ahadi. Kwani Aya za mwanzo katika Surat Tawba zinaonyesha kuwa, washirikina ambao hawakuvunja mkataba basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. [20]

Miongoni mwa fadhila za Imamu Ali (a.s)

Tukio hili limenukuliwa katika vitabu mbalimbali ambapo Imamu Ali alilitumia hili kama hoja ya kuthibitisha fadhila na ubora wake kwa masahaba wengine na kwamba, alikuwa akistahiki ukhalifa na kuwa kiongozi wa Waislamu baada ya Mtume kuliko sahaba mwingine yeyote. Baadhi ya vitabu vilivyonukuu tukio hili kwa madhumuni haya ni: Al-Ihtijaj [21] cha Tabarsi, mmoja wa wanazuoni wa Kishia na Manaqib al-Imam Ali bin Abi Talib (22] cha Ibn Maghazili mmoja wa wanazuoni wa Kisunni.

Kadhalika ufikishaji wa Aya za Baraa umebainishwa katika athari na vitabu vya Kishia na Kisuni kwamba, ni miongoni mwa fadhila za Imamu Ali (a.s). Miongoni mwa athari za Kishia ambazo tunaweza kuziashiria ni Kitab al-Irshad cha Sheikh Mufid (aliaga dunia 413 Hijiria), [23] Kash al-Yaqin cha Allama Hilli (aliaga dunia 726 Hijiria), [24] na Manaqib cha Ibn Shahrashub (aliaga dunia 488 Hijria), [25] na miongoni mwa athari na vitabu vya Kisunni tunavyoweza kuashiria kuhusiana na muadhui hii ni al-Bidayah Wan-Nihayah cha Ibn Kathir [26] na al-Manaqib cha Muwafffaq bin Ahmad Khwarizmi (aliaga dunia 568 Hijiria). [27]

Baadhi ya Maulamaa wa Kisuni wamesema kuwa, kupokonywa Abu Bakr jukumu hilo baada ya kuwa hapo awali amepatiwa hilo na kisha kutumwa Imamu Ali (a.s), sio kitu na hoja ya kuonyesha ubora wa Ali kwa Abu Bakr; kwani zama hizo ilikuwa ni ada na mazoea baina ya Waraabu kwamba, kufutwa mkataba kunapaswa kufanywa na mtu aliyeuweka au mtu kutoka katika jamaa zake; [28] hata hivyo Maulamaa wa Kishia wanaamini kwamba, kutumwa Imamu Ali na kupewa jukumu hilo kunaonyesha juu ya kuweko ushirikiano wa risala na jukumu baina Imamu Ali na Mtume (hii inaonyesha kuwa, Imamu Ali ndiye mrithi na kiongozi wa Waislamu baada ya Mtume); kwani jukumu hili halikuwa tu ni kutangaza kujibari na kujitenga na washirikina ambalo ni jukumu la Waumini wote, bali kulikuweko na suala la kutangaza na kufikisha sheria mpya za Mwenyezi Mungu. [29]

Rejea

Vyanzo