Aya ya al-Wilaya
Jina la Aya | Aya ya Wilaya] |
---|---|
Sura Husika | Maida |
Namba ya Aya | 55 |
Juzuu | 6 |
Sababu ya Kushuka | Imam Ali (a.s) Kutoa Sadaka Akiwa Amerukuu |
Mahali pa Kushuka | Madina |
Maudhui | Itikadi |
Mada Yake | Uimamu na Wilaya ya Imamu Ali (a.s) |
Aya Zinazofungamana Nayo | Aya ya al-Tabligh na Aya ya al-Ikmal |
Aya ya al-Wilaya (Kiarabu: آية الولاية) (Maida: 55) inabainisha Wilaya na uongozi wa Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na waumini ambao watoa Zaka hali ya kuwa wamerukuu. Kwa mtazamo wa wafasi wa Kishia na Ahlu-Sunna, sababu ya kushuka Aya hii ni kitendo cha Imamu Ali (a.s) cha kutoa (kutoa kitu -kutoa sadaka- katika njia ya Mwenyezi Mungu) hali ya kuwa amerukuu. Ni kwa msingi huo, ndio maana Mashia huitumia Aya hii kwa ajili ya kuthibitisha Wilaya na uongozi wa Imamu Ali (a.s) kwa umma wa Kiislamu baada ya Mtume (s.a.w.w).
Wanazuoni wa Kisuni wanasema kuwa, maana ya neno (ولیّ) katika Aya hii ni rafiki na hawakubaliani na hoja za Waislamu wa madhehebu ya Shia za kuonyesha na kuthibitisha Wilaya na uongozi wa Imamu Ali (a.s) kwa kutumia Aya hii. Mkabala na wao, wanazuoni wa Kishia wanasema kuwa, kwa kuangalia sababu za kushuka Aya hii na Ali (a.s) kuwa ndiye mfano pekee wa hili inafahamika kuwa, maana ya (ولیّ) katika Aya hii haiwezi kuwa “rafiki”; bali maana yake ni Wilaya, uongozi na usimamiaji mambo.
Aya hii inajadiliwa kwa mapana na marefu katika vitabu vya tafsiri, teolojia na Fiqhi. Mafakihi kupitia Aya hii wamenyambua na kutoa hukumu mbalimbali. Miongoni mwazo ni kuwa, kufanya kitendo kidogo cha ziada hakibatilishi Sala.
Andiko la Aya
Nafasi
Aya ya al-Wilaya ni miongoni mwa hoja zinazotumiwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa ajili ya kuthibitisha uwalii na uongozi wa Imamu Ali (a.s) kwa umma wa Kiislamu baada ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w). [1] Baadhi wameitambua Aya hii kuwa hoja kubwa na imara zaidi kwa ajili ya kuthibitisha Uimamu wa Imamu Ali (a.s). [2]
Wafasiri wa Qur’ani wa Kishia [3] na Kisunni [4] wameafikiana kuhusiana na sababu ya kushuka Aya hii kwamba, ni hatua ya Imamu Ali (a.s) ya kutoa na kumsaidia fakiri hali ya kuwa yumo katika hali ya kuswali. Kwa msingi huo Aya hii na kadhalika tukio la kutoa zawadi pete yanahesabiwa kuwa miongoni mwa fadhila za Imamu Ali (a.s) ambazo zimeashiriwa katika Qur’an. Imekuja katika kitabu cha al-Mustarshad fi Imamah kwamba: Imam Ali (a.s) aliitaja fadhila hii kwenye baraza la watu sita ambalo liliundwa kumteua khalifa baada ya Omar bin al-Khattab. [5]
Aya hii inajadiliwa katika vitabu vya teolojia, [6] tafsiri, [7] na fiq’h. [8] Hitilafu za kimitazamo baina ya Shia na Suni kuhusiana na maana ya Walii katika Aya hii zimepelekea kuweko na mjadala mrefu katika kufasiri Aya hii.
Sababu ya Kushuka Kwake
- Makala Asili: Kisa cha kuzawadia pete
Asili ya tukio kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, siku moja maskini aliingia kwenye msikiti wa Mtume (s.a.w.w) na kuomba msaada; lakini hakuna mtu aliyempa chochote. Katika hali hiyo yeye akainua mikono yake mbinguni na kusema: Mwenyezi Mungu! shuhudia ya kwamba niliomba msaada katika msikiti wa Mtume wako; lakini hakuna mtu aliyenipa chochote. Wakati huo, Ali (a.s) ambaye alikuwa yupo katika hali ya kurukuu, akaashiria pete kwa kidole chake kidogo cha mkono wake wa kulia, yule maskini akakaribia na kuitoa pete iliyoko kidoleni mwake na Aya hii ikashuka. [9] Sheikh Mufid amezingatia tarehe ya tukio hilo kuwa ni tukio hili na kushukwa kwa Aya hii kulitokea mwezi 24 Dhul-Hijja. [10].
Itibari ya Hadithi za Sababu ya Kushuka kwa Aya Hii
Hadithi ya sababu ya kushuka Aya ya al-Wilaya imepokewa na masahaba kama Ibn Abbas, [11] Ammar, [12] Anas bin Malik, [13] Abu Rafi’ Madani, [14] na Miqdad. [15] Kwa mujibu wa Kadhi Aiji, mmoja wa wanazuoni wa Ahlu-Sunna ni kuwa, wafasiri wa Qur’an wameafikiana na wana kauli moja kuhusiana na sababu ya kushuka Aya hii ambayo ni tukio la Imamu (a.s) kumpatia pete masikini. [16] Pamoja na hayo, Ibn Taymiyya, [17], Ibn Kathir [18] na Fakhrurazi [19 wameihesabu hadithi inayohusiana na Aya hii kuwa ni dhaifu. Kadhalika katika baadhi ya tafsiri za Ahlu Sunna kuhusiana na kwamba, sababu ya kushuka Aya hii ni nani, kumezungumzia mitazamo minne: Imam Ali (a.s), Ubadah bin Samit, Abu Bakar bin Abi Quhafa na Waislamu wote. [20]
Ibn Shu’bah Harrani katika kitabu chake cha Tuhaf al-Uqul, amezitambua hadithi zinazohusiana na sababu ya kushuka Aya ya al-Wilaya kuwa ni sahihi na miongoni mwa hadithi ambazo Maulamaa wameafikiana kwa kauli moja. [21] Kwa mtazamo wa Allama Tabatabai katika tafsiri ya al-Mizan ni kuwa, hadithi zinazozungumzia sababu ya kushuka Aya hii zinaafikiana na Qur’an. [22] Kwa mujibu wake ni kuwa, shakhsia wakubwa wa tafsiri na hadithi, wamenukuu hadithi hizi na hawakuzipinga na baadhi yao kama Ibn Taymiyya ambao walipinga, wamefikia kilelele cha uadui. [23]
Hoja ya Uongozi wa Imamu Ali (a.s)
Maulamaa na wanazuoni wa Kishia wanasema kuwa, Aya hii ni ithbati na hoja juu ya Wilaya, uongozi na ukhalifa wa Imamu Ali (a.s). Kwa mtazamo wao ni kuwa, neno اِنّما (hakika) katika fasihi ya Kiarabu, sentensi inapoanza na (اِنّما) hufanya maana ya sentensi kuwa ya kipekee; [24] yaani kartika Aya hii suala la al-Wilaya na uongozi limefanywa kuwa la kipekee kwa Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na wanaotoa huku wakirukuu. [25] Kwa mujibu wa sababu ya kushuka Aya hii, mfano wa mtu anayetoa huku akirukuu ni Imamu Ali (a.s). [26] Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s). Aya hii pamoja na Aya ya Ulul Amr zimetumiwa kwa ajili ya kuonyesha wajibu wa kuwatii mawasii wa Mwenyezi Mungu. [27]
Tofauti ya Maana ya Walii Baina ya Shia na Sunni
Maulamaa wengi wa Ahlu-Sunna wanaitambua Aya hii kwamba, ilishuka baada ya Imamu Ali kutoa zawadi ya pete; lakini kwa mtazamo wao ni kwamba, neno (ولیّ) maana yake ni rafiki au msaidizi na sio msimamizi na kiongozi. [28] Lakini Maulamaa wa Kishia wanasema kuwa, neno (ولیّ) lina maana ya “uongozi” na “mtu mwenye mamlaka”. [29] Ayatullah Makarim Shirazi anasema, sio mahususi kwa watu ambao wanatoa Zaka hali ya kuwa wamerukuu; bali ni hukumu ya jumla na Waislamu wote wanapaswa kuwa na urafiki baina yao na kusaidiana. Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa sababu ya kushuka Aya hii misdaq na mfano wa (ولیّ) katika Aya ni Ali (a.s) peke yake. Hivyo basi (ولیّ) katika Aya hii ina maana ya Wilaya, uongozi, mamlaka na usimamizi wa mambo; hususan kwa kuzingatia kwamba, uongozi huu uko katika safu moja na uongozi wa Mtume (s.a.w.w) na Mwenyezi Mungu. [30]
Matumizi ya Kifiq’h
- Kutobatilika Sala kwa kufanya kitendo kidogo: Baadhi ya mafakihi wa Kishia wakiwa na lengo la kuthibitisha kwamba, harakati ndogo au kitendo kidogo cha (kutikisika) mwili hakibatilishi Sala, hutumia kama hoja kitendo cha Imamu Ali (a.s) cha kutoa zawadi ya pete kwa masikini hali ya kuwa yupo katika hali ya kurukuu. [31]
- Zaka inajumuisha pia sadaka ya mustahabu: Katika Aya hii zawadi ya pete imetajwa kuwa ni Zaka. Baadhi ya wanazuoni wa Sheria za Kiislamu wamefikia natija hii kwamba, Zaka inajumuisha pia sadaka ya mustahabu. [32]
- Baadhi ya mafakihi wakiwa na lengo la kuthibitisha kwamba, nia ni kitendo cha moyoni na hakuma ulazima wa kuitamka kwa ulimi, wanaitumia Aya hii kama hoja ya hilo. [33]
- Kutokinzana kutoa katika Sala na mahudhurio ya moyo katika Sala: Allama Majlisi anasema kuwa, kuzingatia ibada nyingine katika Sala hakugongani na suala la kuswali Sala katika hali ya mahudhurio ya moyo kikamilifu. [34] Kadhalika amesema, Sala na kutoa sadaka yote mawili yalifanywa na Imamu Ali (a.s) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa msingi huo hakuna mgongano kwa Imamu Ali kusikia sauti ya fakiri na atoe kwa ajili ya kupata radhi za Allah. [35] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa katika kitabu cha Ilal Shara'i ni kwamba, kila wakati Mtume aliposikia sauti ya kulia mtoto akiwa katika hali ya kuswali alikuwa akiharakisha kumaliza Sala kuliko wakati mwingine ili mama mwenye mtoto aweze kumchukua mwanawe huyo. [36]