Ha Ali Bashar Kayfa Bashar

Kutoka wikishia

Ha Ali Bashar Kayfa Bashar (Kiarabu: ها عليٌّ بَشَرٌ کَيْفَ بَشَر) (Ali ni mwanadamu; lakini ni mwanadamu gani) ni ubeti wa shairi mashuhuri la Mad’hiyyah (wasifu) au Ghadiriyyah tungo zilizotungwa kwa lugha ya Kiarabu kwa ajili ya kumsifu Imamu Ali (a.s). Mshairi wa tungo hizi ni Mullah Mehrali Tabrizi Khui, malenga na mshairi wa tungo za Ghadir wa karne ya 13 Hijiria na umashuhuri wake umetokana na kaswida na mashairi haya. Alitunga pia shairi la beti 18 kwa lugha ya Kifarsi akimsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Shairi hili lina beti 20 hadi 40 na lilitungwa mwaka 1216 na 1240 Hijiria na likatarjumiwa na Mirza Muhammad-Reza Shirazi kwa kwa vina na urari. Kadhalika nudhumu na shairi hili limezingatiwa na mahatibu na washairi wa Kishia na kuna mashairi kadhaa mzani huu ambayo yametungwa kwa kutumia ubeti huu au beti za shairi hili.

Kaswida ya Mad’hiyyah au Ghadiriyyah

Kaswida au shairi la Ha Ali Bashar Kayfa Bashar ambalo ni mashuhuri kwa jina la kaswida ya Mad’hiyya au Ghadiriyyah, [1] ni kaswida iliyotungwa kwa lugha ya Kiarabu kwa ajili ya kumsifu Imamu Ali (a.s). [2]

Imeelezwa kuwa, shairi hili lina beti 20 hadi 40 na lilitungwa mwaka 1216 na 1240 Hijria. [3] Farhad Mirza ambaye aliishi katika zama moja na Mullah Mehrali amenukuu shairi hili katika kitabu chake cha Zanbil likiwa na beti 29. [4]

Kaswida ya Ha Ali Bashar Kayfa Bashar imezingatiwa na mahatibu na washairi wa Kishia na kuna mashairi kadhaa ambayo yametungwa kwa kutumia ubeti huu au beti za shairi hili. [5] Kadhalika kaswida hii imetarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi na Mirza Muhammad-Reza Basirat Shirazi kwa vina na urari huo huo katika majimui ya beti 40. [6]

Mshairi

Makala kuu: Mehrali Tabrizi

Mullah Mehrali Tabrizi Khui (1182-1262 Hijiria) anayejulikana kama Fadavi, ni mshairi na mtunzi wa tungo za ghadir wa karne ya 13, ambaye alikuwa akitunga mashairi katika lugha tatu: Kituruki, Kiajemi na Kiarabu. [7] Alikuwa mmoja wa wasomi wa elimu ya irfani na alitambuliwa kama msomi aliyekuwa na ujuzi wa elimu zilizokuwa zimeenea katika zama zake. [8] Hata hivyo, umaarufu mkubwa wa Mulla Mehrali unatokana na Mad’hiyyah au Ghadiriyyah yake (shairi lake hili la kumsifu Imamu Ali). [9] Kadhalika alitunga pia mashairi ya beti 18 kwa lugha ya Kifarsi akimsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w). [10]

Kumuona Mtume katika ulimwengu wa ndoto

Katika kitabu cha Velayat Nameh Ghadiriyeh imenukuliwa kutoka kwa Mullah Waiz Khiyabani mwandishi wa kitabu cha Ulamaa Muasirin kwamba, Mulla Mehrali baada ya kutunga kaswida au shairi la Ha Ali Bashar Kayfa Bashar alimuona Mtume (s.a.w.w) katika ndoto ambapo Imamu Ali (a.s) alikuwa pembeni yake. [11] Mtume (s.a.w.w) alimwambia Mullah Mehrali: “Soma, mashairi uliyotunga kumsifu binamu yangu”. Mullah Mehrali akaanza kusoma beti za shairi hilo na baada ya kumaliza beti ya kwanza, Mtume (s.a.w.w) alisema: Kayfa Bashar, Kayfa Bashar, Kayfa Bashar (mwanadamu gani, mwanadamu gani, mwanadamu gani). [12]

Vyanzo

  • Fadawī Khoeī, Mullā mihrʿAlī. Wilāyatnama(Ghadīrīya). Edited by ʿAlī Ṣadrāiy Khoeī, Qom: Ansārīyān, First edition, 1376 sh.
  • Farhād Mīrzā, Muʿtamad al-Dawla. Zanbīl. Tehran: Padīda, Secound edition, 1367 sh.
  • Mujāhidī, Muḥammad ʿAlī. Siyrī dar qalamruw-i shʿr-i nabawī. Qom: Majmʿ-i Jahānī-ie ahl al-bayt(a), First edition, 1387 sh.
  • Mullā Zāda, Muḥammad Hānī. Tabrīzī Khoeī, Mullā mihrʿAlī. https://rch.ac.ir/article/Details/7372. In Encyclopaedia of the World of Islam, vol. 6, Tehran: Encyclopedia Islamica Foundation, Secound edition, 1388 sh.