Nenda kwa yaliyomo

Hadithi al-Wisayah

Kutoka wikishia

Hadith al-Wisaya (Kiarabu: حديث الوصاية) ni hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo ndani yake inamtaja Imamu Ali bin Abi Talib (a.s) kuwa ni wasii, mrithi na kiongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w). Madhumuni ya hadithi hii imekuja kwa ibara na maneno tofauti katika vitabu vya hadithi vya Waislamu wa Kishia na Kisuni. Miongoni mwa nukuu mashuhuri zaidi ya Hadithi hii ambayo imenukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Buraydah ibn Husayb inasema: ((لِكُلِّ نَبِيٍّ وَصِيٌّ وَ وَارِثٌ وَ إِنَّ عَلِيّاً وَصِيِّي وَ وَارِثِي‏)) ; Kila Nabii ana wasii na mrithi, na kwa hakika Ali ni wasii na mrithi wangu.

Andiko la hadithi

Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ya kwamba amesema:

لِكُلِّ نَبِيٍّ وَصِيٌّ وَ وَارِثٌ وَ إِنَّ عَلِيّاً وَصِيِّي وَ وَارِثِي‏



Kila Nabii ana wasii na mrithi, na kwa hakika Ali ni wasii na mrithi wangu. [1]

Hadithi ya al-Wisayah katika vitabu vya hadithi

Hadithi ya al-Wisayah imekuja katika vyanzo vya hadithi vya Waislamu wa Kishia na Kisuni kama Fadhail al-Sahabah cha Ibn Hambal, [2] Manaqib cha Ibn Maghazil, [3] al-Mu'jam al-Kabir cha Tabarani, [4] Tarikh Madinat Dimashq, [5] Manaqib al-Khwarazmi, [6] al-Kamil cha Jurjani, [7] Tadhkirat al-Khawas, [8] Kifayat al-Athar, [9] Man la yahdhuruh al-Faqih, [10] Dalail al-Imamah, [11] Manaqib Ibn Shahrashub [12] na Bihar al-Anwar. Burayd ibn Husayb amepokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba: ((لِكُلِّ نَبِيٍّ وَصِيٌّ وَ وَارِثٌ وَ إِنَّ عَلِيّاً وَصِيِّي وَ وَارِثِي‏ ; Kila Nabii ana wasii na mrithi, na kwa hakika Ali ni wasii na mrithi wangu)). [14]Mtume (s.a.w.w) alimjibu Salman Farsi alipomuuliza kuhusiana na wasii na mrithi wake ya kwamba: Wasii na mrithi wangu na mtu ambaye atalipa deni langu na ambaye atatekeleza ahadi zangu ni Ali ibn Abi Talib. [15]

Kadhalika kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa na Ali ibn Ali Hilali, Mtume (s.a.w.w) alimhutubu binti yake Fatma (a.s) kwa kumwambia: ((وَصِيِّي خَيْرُ الْأَوْصِيَاءِ وَ أَحَبُّهُمْ إِلَى اللَه وَ هُوَ بَعْلُكِ ; Wasii wangu ni wasii bora kabisa miongoni mwa mawasii na mpendwa zaidi na Mwenyezi Mungu naye ni mumeo)). [16]

Madhumuni ya hadithi

Maudhui na madhumuni ya hadithi ya al-Wisayah inahusiana na kadhia ya uwasii, urithi na ukhalifa wa Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s). Maulamaa wa Kishia wanaitambua hadithi hii kwamba, inatoa ishara na dalili ya Uimamu wa Ali ibn Abi Talib; wao wanatambua kwamba, al-Wisayah maana yake ni kurithi uongozi na wanaamini kwamba, kwa mujibu wa hadithi, Bwana Mtume (s.a.w.w) alimtambuliisha Imamu Ali ibn Abi Talib (a.s) kuwa, mrithi na kiongozi wa umma wa Kiislamu baada yake. [17] Hata hivyo baadhi ya Maulamaa wa Ahlu-Sunna wamesema kuwa, al-Wisayah katika hadithi hii haina maana ya ukhalifa na uongozi bali Mtume alimuagizia Imamu Ali kuhusiana na familia yake. [18] Katika kuwajibu wenye nadharia na madai haya imeelezwa kwamba, Mtume (s.a.w.w) alimfanya Imamu Ali kuwa wasii wake kwa sura mutlaki na hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba, alipambanua kwamba, uwasii huo unahusiana na suala la familia yake tu. [19] Hamdi bin Abdul-Majid Salafi, amesema katika nakala ya al-Mu'jam al-Kabir ya kwamba, kama sanadi na mapokezi ya hadithi yangekuwa sahihi, basi maudhui ya ukhalifa na urithi wa uongozi baada ya Mtume hilo lingethibitika.

Mapokezi

Hadithi ya al-Wisayah imepokelewa kwa mapokezi tofautii kutoka kwa Buraydah, [21] Salman, [22] Abu Ayub Ansari na Anas ibn Malik [23] katika vyanzo na vitabu vya hadithi vya Waislamu wa madhehebu ya Kisuni. Sibt ibn al-Jawzi (mwandishi wa kitabu cha Tadhkirat al-Khawas) amenukuu hadithi ya Salman kwa mapokezi mawili. Yeye ameyatambua mapokezi yaliyokuja katika kitabu cha Fadhail al-Sahabah cha Ibn Hambal kwamba, ndio sahihi. [24]

Baadhi ya Maulamaa wa Kisuni kama Ibn al-Jawzi, [25] Jalal al-Din al-Suyuti, [26] na Haythami [27] wametilia shaka katika itibari ya sanadi na mapokezi ya hadithi hii kutokana na kuweko Muhammad bin Hamid Razi au Ali Mujahid katika mapokezi ya hadithi hii na hivyo wameikataa. Hii ni katika hali ambayo, Sayyid Ali Milani anasema, Muhammad bin Hamid ni katika wapokezi wa hadithi wa Sihah al-Sittah (Sahihi Sita) na baadhi ya wanazuoni wa elimu ya Rijal akiwemo Yahya bin Muin wamemtaja kuwa mtu wa kuaminika. [28] Kadhalika imeelezwa kwamba, Tirmidhi mwandishi wa kitabu cha Sunan Tirmidhi moja ya vitabu vya Sahihi Sita na Ahmad bin Hambal wamenukuu hadithi kutoka kwa Ali bin Mujahid. [29]

Rejea

Vyanzo

  • Haythamī, ʿAlī b. Abī Bakr b. Sulaymān al-. Majmaʿ al-zawāʾid wa manbaʿ al-fawāʾid. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1408 AH.
  • Ibn al-Jawzi,. ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Mawḍūʿāt. Edited by ʿAbd al-Raḥmān Muḥammad ʿUthmān. Madina: al-Maktabat al-Salafīyya, 1386 AH.
  • Ibn al-Maghāzilī, ʿAlī b. al-Ḥasan. Manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. Qom: Intishārāt-i Sibṭ al-Nabī, 1426 AH.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. Ḥasan. Tārīkh Madīna Dimashq. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
  • Jurjānī, ʿAbd Allāh b. ʿAdīy al-. Al-Kāmil fī ḍuʿafāʾ al-rijāl. Edited by Mukhtār Ghazāwī. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Khawārazmī, Al-Muwaffaq b. Aḥmad al-. Al-Manāqib. Edited by Mālik Maḥmūdī. Beirut: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1414 AH.
  • Khazzāz al-Rāzī, ʿAlī b. Muḥammad al-. Kifāyat al-athar fī l-naṣ ʿalā l-aʾimmat al-ithnā ʿashar. Edited by ʿAbd al-Laṭīf Ḥusaynī. Qom: Nashr-i Bīdār, 1401 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar al-Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1413.
  • Sibṭ b. al-Jawzi, Yusuf b. Ḥisām. Tadhkirat al-khawāṣ. Qom: Manshūrāt al-Sharīf al-Raḍī, 1418 AH.
  • Suyūtī, ʿAbd al-Raḥman al-. Al-Āliʾ al-maṣnūʿa fī aḥādīth al-mawḍūʿa. Beirut: Dār al-Maʿrifa, n.d.
  • Ṭabarānī, Sulaymān b. Muḥammad al-. Al-Muʿjam al-awsaṭ. Edited by Qism al-Taḥqīq bi-Dār al-Ḥaramayn. Cairo: Dār al-Ḥaramayn li-l-Ṭibāʿa wa l-Nashr, 1415 AH.
  • Ṭabarānī, Sulaymān b. Muḥammad al-. Al-Muʿjam al-kabīr. Edited by ʿAbd al-Majid al-Salafī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Ṭabari al-Saghīr, Muḥammad b. Jarir al-. Dalā'il al-Imāma. Qom: Nashr-i Biʿthat, 1413 AH.