Nenda kwa yaliyomo

Saluni Qabl an Tafqiduni

Kutoka wikishia
Bango la Saluni Qabla an Tafqiduni lilochorwa na Muhammad al-Mushrifawi

Saluni Qabl an Tafqiduni (Kiarabu: سلوني قبل أن تفقدوني) ni maneno ya Imam Ali (a.s) yanayoashiria upana wa elimu yake. Kwa mujibu wa vyanzo vya Shia na Sunni, Imam Ali (a.s) alikuwa akiitamka sentensi hii mara nyingi tu. Miongoni mwa sehemu alizoitumia ibara hii, ni ndani ya moja ya hutuba zake, ambapo alitumia ibara hii Sa'd bin Abi Waqqas alimkabili kwa kumuuliza Ali (a.s); Hebu nieleze ni nywele ngapi nilizonazo kichwani pamoja na ndevuni mwangu? Imam Ali (a.s) alimjibu kwa kumwambia; Hakuna unywele wowote ule juu ya kichwa chako, isipokuwa kuna shetani anayeishi chini yake. Kisha akampa khabari kuhusiana na kifo cha kishahidi cha Imam Hussein (a.s), na kwamba jinai hiyo itafanywa kupitia mkono wa mwanawe, ambaye ni Omar bin Saad.

Kauli na ibara ya; ((سلونی قبل ان تفقدونی ; Niulizeni kabla hamjanipoteza)), ni moja ya ibara zinazohisabiwa kuashiria nafasi na hadhi ya Imamu Ali (a.s) mbele ya Masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) wengine.

Maelezo kwa ufupi

Ibara ya ((سَلُونِی قَبْلَ أَنْ تَفْقِدُونِی)) yenye maana ya niulizeni kabla hamjanipoteza, ni sentensi ya Imam Ali (a.s) [2] Kupitia msingi wa Hadithi iliyosimuliwa katika kitabu Yanabiu’ Al-Mawaddah, ni kwamba; Ali bin Abi Talib mara nyingi alionekana kuitumia ibara hii. [3] Moja ya nyakati ambazo Imamu Ali (a.s) aliisema ibara hii; ni baada ya watu kuweka kiapo cha utiifu kwake, cha kutambua yeye kuwa ni Khalifa, yeye aliitumia ibara hii katika khutba aliyowahutubia watu wa mji wa Kufa. [4] Pia aliitumia tena katika kipindi cha kati na kati cha baina ya vita vya Saffin na Nahrwan, alipokuwa kwenye moja ya kundi la masahaba zake. [5]

Maudhui ya sentensi hii imenukuliwa katika matini tofauti, kama vile; ((فَاسْأَلُونی قَبْلَ أَنْ تَفْقِدُونِی ; Basi niulizeni kabla sijakupooni)), [6] ((سَلُونِی عَمَّا شِئْتُمْ ; Niulize chochote kile mnachotaka kukiuliza)), [7] ((سَلُونِی قَبْلَ أَنْ لَا تَسْأَلُونِی ; Niulizeni kabla ya wakati ambao hamtaniuliza)), [8] na ((سَلونی ; Niulizeni mimi)). [9] Hizo ni matini tofauti zenye madhumuni ya maudhui moja.

Ashirio la Hadithi juu ya wingi wa elimu ya Imam Ali (a.s)

Katika baadhi ya maelezo ya Nahj al-Balaghah, imeelezwa kwamba sentensi isemayo ((سلونی قبل ان تفقدونی)) inathibitisha ya kwamba; Imam Ali (a.s) alikuwa ni mjuzi wa kila kitu [10] Pia, kwa mujibu wa kauli ya Mullah Saleh Mazandarani, mwanachuoni wa Kishia (aliyefariki maka 1081 Hijiri), ni kwamba; Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wameihisabu ibara hii, kuwa ni uthibitisho unaothibitisha wingi wa elimu ya Imam Ali (a.s). [11]

Imam Baqir (a.s) amenukuliwa akifafanua maana ya ((سلونی قبل ان تفقدونی)) kwa kusema; 'Hakuna mwenye elimu, isipokuwa amejifunza kutoka kwa Ali (a.s.)'. Waache watu waende waendapo. Ninaapa kwa Mungu kwamba, hakuna elimu ya haki wala ujuzi wa kweli isipokuwa upo hapa." Katika muendelezo wa riwaya hii, imesimuliwa ya kwamba; Imam Baqir (a.s) aliashiria nyumba yake kwa mkono wake. [12] Kwa mujibu wa maelezo ya Allamah Majlisi; Kule Imam Baqir (a.s) kuiashiria nyumba yake kwa mkono wake, alikuwa akimaanisha ya kwamba, nyumba yake ni nyumba yenye uhusiano wa Wahyi na Unabii. [13]

Pia, katika muendelezo wa matini inayohusiana na ibara iseayo; ((سلونی قبل ان تفقدونی)) kuna tungo na ibara mbalimbali zinazoashiria upana wa elimu ya Imam Ali (a.s). Ikiwa ni pamoja na ibara zifuatazo:

  • Hakika elimu ni ya waliotangulia na ya watakaokuja, ziko kwangu. Natoa fatwa kwa watu wa Taurati kwa mujibu wa Taurati, kwa watu wa Biblia kwa mujibu wa Biblia, na kwa watu wa Qur’an kwa mujibu wa Qur’ani.” [14]
  • Kwa nini usimuulize yule ambaye ana elimu ya wakati wa vifo, misiba na nasaba? [15]
  • Nazijua njia za mbinguni (maarifa ya kiroho) kuliko njia za ardhini. [16]
  • Naapa kwa Mungu, nitajibu kila mtakaloliuliza. Ulizeni kuhusiana na kitabu cha Mwenye Ezi Mungu, naapa kwa Mwenye Ezi Mungu, nazifahamu hali za Aya zote za Qur'an, kwamba ziliteremshwa usiku au mchana; zimeteremshwa kwenye ardhi tambarare au juu ya mlima. [17]
  • Naapa kwa Mwenye Ezi Mungu, nitajibu kila swali mlilo nalo kuhusiana na yaliyopita, yaliyopo na yajayo. [18]

Sifa pekee za Imam Ali (a.s)

Kwa mujibu wa maelezo ya Ibnu MardawaIhi Esfahani, mpokezi wa Hadithi wa madhehebu ya Kisunni wa karne ya 4 na 5, ni kwamba; Kauli isemayo; ((سلونی قبل ان تفقدونی)) yenye maana ya "Niulizeni kabla sijakupoteeni" ni uthibitisho unaothibitisha kwamba, Imam Ali (a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kuliko masahaba wengine wote. Katika kitabu cha Faraidu Al-Simataini, kauli hii imehisabiwa kuwa ni ishara inayoashiria sifa maalumu za Imam Ali (a.s), sifa ambazo maadui na wapinzani wake hawana budi ila kuzikubali. [20] Kwa mtazamo wa Sayyid bin Taawus ni kwamba; Kutokana na kule Imamu Ali (a.s) kuitamka ibara yake ya kuwataka watu, wamuulize swali walitakalo, na kwamba aliitamka ibara hiyo mbele ya watu wote wakiwemo maadui zake. Kufanya kwake hivyo, ni aina ya changamoto katika kwenye uwanja wa kielimu. [21] ] Hata hivyo, kuna baadhi ya watu, kama vile Shamsu Al-Din Dhahabi [22] na Ibnu Taimiyyah [23], ambaye ni mmoja wa wanachuoni wa Kisalafi, wote wawili wamesema wamejaribu kukanusha sifa zivunywazo kwa ajili Imamu Ali (a.s) kupitia ibara yake ambayo ni changamoto kwa kila mwenye kudhani kuwa ni mwanazuoni au ni mjuzi wa elimu. Wao wamedai ya kwamba; Ibara ya Imamu Ali (a.s) aliitamka kuwahutubia wajinga waliokuwa wakiisha katika mji wa Kufa nchini Iraq.

Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, Imam Baqir [24] na Imam Swadiq (a.s) [25] wao pia katika baadhi ya matukio, walionekana kutamka ibara isemayo; ((سَلُونی قَبْلَ أَنْ تَفْقِدُونِی)). Au pia, wakati mwingine walisema kuwambia watu; ((سَلُونِی عَمَّ شِئْتُمْ)). Kuna Hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo ndani yake Mtume (s.a.w.w) aliitamka ibara hiyo. [26] Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wameripotiwa wakisema ya kwamba; Hakukuoneka mtu mwingine yeyote aliyeitumia ibara hiyo isipokuwa Imamu Ali (a.s). [27] Kwa upande mwingine, pia baadhi ya vyanzo vya Kisunni vimesema kwamba; Hakuna Sahaba yeyote isipokuwa Ali (a.s) aliyewahi kusema neno kama hilo. [28]


Waliojidai Majivuno ya Uongo

Wanazuoni wa Kiislamu wameripoti kwamba; Kuna watu waliodai na kujivuna kwa majivuno ya uongo, waliojaribu nao kusema; (سلونی قبل ان تفقدونی). Ila walipokabiliwa na maswali kutoka watu waliojidai mbele yao, wao walishindwa kutoa jawabu za maswali hayo. Miongoni mwao, ni Qatada bin Di'aamah aliyekuwa ni mmoja wa wafuasi wa Masahaba (Taabi'iina) na ni faqihi wa mji wa Basra. [29] Wa katika majivuno hayo, ni Ibnu Jauzi aliyekuwa ni faqihi wa Kihanbali aliyeishi katika karne ya sita. [30]

Pia, Allamah Amini alitaja visa vyengine vitano katika kitabu chake Al-Ghadir vinavyohusiana na waliodai na kujivuna kwa kauli isemayo: ((سلونی ; Niulizeni swali mlitakalo)), hatimae wakafedheheka.” [31] Kwa mujibu wa maelezo ya Allamah Majlisi na Mulla Saleh Mazandarani, yeyote yule aliyetoa aliyejidaia mada hayo, hatima yake ilikuwa ni kufedheheka tu, isipokuwa Imam Ali (a.s). [32]

Hadhi ya Hadithi na wapokezi wake

Kuna wapokezi wengi wa Hadithi waliosimulia ibara isemayo; ((سلونی قبل ان تفقدون ; Niulizeni kabla sijakupoteeni)). Miongoni mwao ni Amer bin Waathilah, [33] Abdullah bin Abbas, [34] Sulaim bin Qais Al-Helali, [35] Asbagh bin Nubatah, [36] na Abaaya bin Rab-'iy.

Mwitikio au Radiamali ya Saad bin Abi Waqqas

Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, ni kwamba; Baada ya Imam Ali (a.s) kutamka sentensi iliyosema: Niulizeni kabla hamjanipoteza au kabla sijakupoteeni hii katika khutba yake, Sa'd bin Abi Waqqas alimuuliza ni nywele ngapi zilizomo kichwani kwangu na ndevuni mwangu? Imam Ali (a.s) akimjibu swali lake, kwanza aliapa ya kwamba tokea zamani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alikwisha mjuilisha ya kwamba, yeye utamiuliza swali kama hilo. Kisha akaendelea kumwambia; Hakuna unywele hata mmoja katika kichwani na ndevuni mwako, isipokuwa kama kuna shetani anayeishi chini yake. Pia nyumbani kwako kuna mtoto wa mbuzi (akimkusudia Omar bin Sa'ad ambaye ni mwanawe), ambaye atamuua mwanangu Hussein (a.s). [39] Wapo baadhi walionukuu kisa hichi na kukinasibisha na baba wa Sanaan bin Anas ambaye ni miongoni mwa wauwaji waliomuuwa Imamu Hussein. [40]

Vyanzo

  • Amini, Abdul Hussein, Al-Ghadir. Qom: Markaz al-Ghadir, cet. I, 1416 H.
  • Dzahabi, Shamsuddin, Al-Muntaqa min Minhaj al-I'tidal fi Naqd Kalami Ahl al-Rafdh wa al-I'tizal, Riset Muhibbuddin Khatib, tanpa nama, tanpa tahun.
  • Dzahabi, Shamsuddin, Tarikh al-Islam wa Wafayat al-Mashahir wa al-A'lam, Riset Bashshar Awwad Ma'ruf, Dar al-Gharb al-Islami, cet. I, 2003 M.
  • Hakim Naishaburi, Muhammad bin Abdullah, Al-Mustadrak ala al-Shahihain, Riset Musthafa Abdul Qadir Atha. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiah, 1411 H/ 1990 M.
  • Haskani, Ubaidullah bin Abdullah, Shawahid al-Tanzil li Qawa'id al-Tafdhil, Riset dan revisi Muhammad Baqir Mahmudi, Teheran: Wizarate Fathangg wa Irshad Islami, cet. I, 1411 H.
  • Hilali, Sulaim bin Qais, Kitab Sulaim bin Qais al-Hilali, Riset dan revisi Muhammad Anshari Zanjani Khuini, Qom: al-Hadi, cet. I, 1405 H.
  • Ibnu Abdilbar, Yusuf bin Abdullah. Al-Isti'ab fi Ma'rifat al-Ashhab. Riset Ali Muhammad al-Bajawi, Beirut: Dar al-Jail, cet. I, 1412 H.
  • Ibnu Abi al-Hadid, Abdulhamid bin Hibatullah, Sharh Nahj al-Balaghah, Riset Muhammad Abul Fadhl Ibrahim, Qom: Perpustakaan Ayatullah Marashi Najafi, cet. I, 1404 H.
  • Ibnu Abi Zainab, Muhammad bin Ibrahim, Al-Ghaibah li al-Nu'mani, Riset dan revisi Ali Akbar Ghaffari, Teheran: Penerbit Shaduq, cet. I, 1397 H.
  • Ibnu Asakir, Ali bin Hassan, Tarikh Dimashq, Riset 'Amr bin Gharamah 'Amrawi, Beirut: Dar al-Fikr, 1415 H/ 1995 M.
  • Ibnu Athir, Muhammad bin Muhammad, Usd al-Ghabah, Beirut: Dar al-Fikr, 1409 H/1989 M.
  • Ibnu Hambal, Ahmad bin Hambal, Fadhail al-Shahabah, Riset Washiyullah Muhamma Abbas, Beirut: Muassasah al-Risalah, cet. I, 1403 H.
  • Ibnu Hayyun, Nu'man bin Muhammad Maghribi, Sharh al-Akhbar fi Fadhail al-Aimmah al-Athhar as, Riset dan revisi Muhammad Husain Husseini Jalali, Qom: Jamiah Mudarrisin, cet. I, 1409 H.
  • Ibnu Mardawaih Isfahani, Ahmad bin Mussa, Manaqib Ali bin Abi Thalib wa ma Nazala min al-Quran fi Ali, Riset Abdurrazzaq Muhammad Hirzuddin, Qom: Dar al-Hadits, cet. II, 1424 H.
  • Ibnu Quliwaih, Jakfar bin Muhammad, Kamil al-Ziyarat, Riset dan revisi Abdul Husain Amini, Najaf: Dar al-Murtadhawiyah cet. I, 1366 HS.
  • Ibnu Taimiyah, Minhaj al-Sunnah al-Nabawiyah fi Naqdi Kalam al-Shiah al-Qadariyah, Riset Muhammad Rasyad Salim, Jamiah al-Imam Muhammad bin Sa'ud al-Islamiyah, cet. I, 1406 H.
  • Juwaini, Ibrahim bin Muhamamd, Faraid al-Simthain, Riset Muhammad Baqir Mahmudi, Beirut: Muassasah Mahmudi, 1400 H.
  • Kharazmi, Muwaffaq bin Ahmad, Manaqib, Qom: Muassasah Nashre Islami, tanpa tahun.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub, Al-Kafi, Riset dan revisi Ali Akbar Ghaffari dan Muhammad Akhundi, Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. IV, 1407 H.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Mir'at al-Uqul fi Sharh Akhbar Al al-Rasul, Riset dan revisi Sayyid Hashim Rasuli Mahallati, Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. II, 1404 H.
  • Mazandarani, Muhammad Shaleh bin Ahmad, Sharh al-Kafi (Ushul wa Raudhah), Riset dan revisi Abul Hassan Sha'rani, Teheran: Maktabah al-Islamiyah, cet. I, 1382 H.
  • Mufid, Muhammad bin Muhammad. Al-Irshad fi Ma'rifat Hujajillah ala al-'Ibad, Qom: Kongres Sheikh Mufid, cet. I, 1313 H.
  • Nabathi Amili, Ali bin Muhammad. Al-Shirat al-Mustaqim ila Mustahiqqi al-Taqdim, Revisi Muhammad Baqir Behbudi. Teheran: al-maktabah al-murtadhawiyah, 1384 H.
  • Naishaburi, Muslim bin Hajjaj, Sahih Muslim. Riset Muhammad Fuad Abdul baqi, Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, tanpa tahun.
  • Qunduzi, Suleiman bin Ibrahim, Yanabi' al-Mawaddah li Dzawi al-Qurba, Qom: Dar al-Uswah, tanpa tahun.
  • Shaduq, Muhammad bin Ali bin Babawaih, Al-Amali, Teheran: Ketabchi, cet. VI, 1376 H.
  • Shaffar, Muhammad bin Hassan, Bashair al-Darajat fi Fadhail Al Muhammad, Qom: Maktabah Ayatullah Marashi Najafi, cet. II, 1404 H.
  • Sharif Radhi, Muhammad bin Hussein, Nahj al-Balaghah, Revisi Shubhi Saleh, Qom: Hijrat, cet. I, 1404 H.
  • Tabari, Muhibbuddin, Dzakhair al-'Uqba fi Manaqib Dzawi al-Qurba, Qom: Dar al-kutub al-Islamiyah, cet. I, 1428 H.
  • Tusi, Muhammad bin Hassan, Rijal al-Thusi. Riset Jawad Qayyumi Isfahani, Qom: Muassasah Nashre Islami, cet. III, 1373 HS.
  • Zamakhshari, Mahmud bin Umar, Al-Kashshaf an Haqaiq Ghawamidh al-Tanzil wa Uyun al-Aqawil fi Wujuh al-Ta'wil, Revisi Musthafa Hussein Ahmad. Beirut: Dar al-Kutub al-Arabi, cet. III, 1407 H.