Nenda kwa yaliyomo

Aya za Bara-a

Kutoka wikishia
Aya za Bara-a
Jina la AyaAya za Bara-a
Sura HusikaTawba
Namba ya Aya1
Juzuu10
Mahali pa KushukaMadina
MaudhuiItikadi na Fiqhi
Mada YakeKutangaza Kuingia Makubaliano na Washirikina


Aya za Bara-a (Kiarabu: آيات البراءة) Ni Aya za kwanza katika Surat al-Tawba ambazo zimeelezea hukumu za mwisho kuhusu uhusiano wa Waislamu na washirikina. Katika Aya hizi, Mwenye Ezi Mungu amemuaru Mtume wake (s.a.w.w) na Waislamu kudhihirisha hasira na kujitenga kwao dhidi ya washirikina, kuachana na mikataba waliyofunga nao, na ikiwa washirikina hawataingia katika Uislamu, basi watamgaze vita dhidi yao. Aya hizi ziliwasilishwa kwa washirikina siku ya sikukuu ya kuchinja (Idu al-Adh-ha) kupitia Imam Ali (a.s).

Kulingana na maelezo ya wafasiri wa Qur’ani ni kwamba; kuvunjwa kwa mikataba baina ya Waislamu na washirikina kupitia upande mmoja (wa Waislamu), haukuwa ni uamuzi usio na sababu, bali uvunjaji huo wa mikataba kwanza ulianza kutoka upande wa washirikina. Hivyo basi, ile mkataba ambayo washirikina hawakukiuka ahadi zao juu yake, Waislamu waliihisabu mikataba hiyo kuwa ni halali hadi muda wake ulipo malizika kulingana na Aya hizo hizo za Bara-a. Pia imesemwa ya kwamba; tokea awali mikataba hii baina ya Waislamu na washirikina, ilikuwa ni mikataba ya muda mfupi.

Kwa mujibu wa maoni ya Muhammad Jawad Maghniyya ni kwamba; Msisitizo wa Aya za Bara-a juu ya kulazimisha washirikina wa Bara Arabu kuukubali Uislamu au kuwa tayari kwa ajili ya vita, hauendani na dhana ya uhuru na hiari ya mtu katika kuikubali au kuikataa dini, dhana ambayo inapatikana katika Aya nyingine za Qur’ani. Hii ni kwa sababu washirikina wa Bara Arabu, walikuwa daima wakivunja mikataba yao, na pia walikuwa wanatishia amani ya jamii ya Waislamu. Hivyo basi huku hii ni hukumu makhususi kwa ajili ya washirikina hao wa Bara Arabu walio kuwa na sifa hizo.

Aya za Bara-a na Tafsiri Yake

Aya za mwanzo za Surat al-Tawba kiumaarufu hujulikana kwa jina la Aya za Bara-a[1] Aya hizo na tafsiri yake ni kama ifuatavyo:

بَرَ‌اءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَ‌سُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِ‌كِينَ ﴿1﴾ فَسِيحُوا فِي الْأَرْ‌ضِ أَرْ‌بَعَةَ أَشْهُرٍ‌ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ‌ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِ‌ينَ ﴿2﴾ وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَ‌سُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ‌ أَنَّ اللَّـهَ بَرِ‌يءٌ مِّنَ الْمُشْرِ‌كِينَ ۙ وَرَ‌سُولُهُ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ‌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ‌ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ‌ الَّذِينَ كَفَرُ‌وا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿3

Maana ya Aya hizi ni kwamba:

  1. (Aya hizi) ni tangazo la kujitenga (na kutokuwa na uhusiano) kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu na Mtume wake, kwa wale washirikina mliofunga nao mikataba ya mapatano.
  2. Kwa hivyo, (enyi washirikina), kueni huru katika tembea kwenye ardhi hii hadi muda wa miezi minne (ijayo) na mujue ya kwamba hamwezi kumshinda Mwenye Ezi Mungu, na Mwenye Ezi Mungu Ndiye anaye waaibisha makafiri.
  3. Na (Aya hizi) ni tangazo kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu na Mtume wake kwa watu katika siku ya Hija Kuu, ya kwamba; Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana uhusiano wowote ule na makafiri. (Hata hivyo) ikiwa mtatubu hilo litakuwa ni bora kwenu; na ikiwa mtageuka na tutakabari, basi jueni ya kwamba; hamtamdhoofisha au kumshinda Mwenye Ezi Mungu, na wape makafiri bishara ya adhabu ya chungu iumizayo.



Sababu ya Kuteremka kwa Aya za Bara-a

Aya za Bara-a ziliteremshwa mwishoni mwa mwaka wa 9 Hijiria baada ya Waislamu kurudi kutoka vita vya Tabuk.[2] Bwana Mtume (s.a.w.w) aliamuriwa na Mola wake kuzisoma na kuwafikishia Aya hizi washirikina waliokuwa wakikusanyika katika mji wa Makka ndani ya mwezi wa Dhul-Hijjah mwaka huo huo.[3] Sababu za Kuteremshwa kwa Aya za Aya za Bara-a, Inasemekana kwamba licha ya ushindi wa Waislamu katika Fat-hu Makka mwaka wa 8 Hijiria,[4] ila bado kulikuwa na makabila fulani pamona na washirikina wengine waliokuwa wakipingana na kusimama dhidi ya Uislamu.[5] Pia, washirikina waliokuwa wametia mikataba ya mapatano na Mtume (s.a.w.w) walikuwa wakivunja mikataba ya mapatano hayo mara kwa mara.[6] Kwa kubadilika kwa hali na kuenea kwa Uislamu,[7] Aya hizi ziliteremshwa na kutangaza kwamba; uwepo wa shirki hauwezi kuvumiliwa.[8]

Matukio ya ufikishaji wa Aya za Aya za Bara-a Mbele ya Makafiri; Katika vyanzo vya kihistoria na Hadithi za Shia na Sunni, inaelezwa kwamba; wakati Aya za kwanza za Surat al-Tawba ziitwazo Aya za Bara-a zilipo teremshwa, bwana Mtume (s.a.w.w) alimtuma Abu Bakar ibnu Abi Quhafa kwenda kwa watu wa Makka ili awasomee Aya hizo. Hata hivyo, baada ya Abu Bakar kuondoka Madina, Jibril alimteremkia bwana Mtume (s.a.w.w) na kumwambia kwamba; Aya hizo ima anapaswa kuzisoma yeye mwenyewe au mtu kutoka katika familia yake. Kwa kufuata amri hiyo ya Mwenye Ezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) alimtuma Imam Ali (a.s) badala ya Abu Bakar kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza amri hiyo.[9]

Abu Jafar Muhammad ibn Jarir al-Tabari katika kitabu chake cha Tafsir al-Tabari anasema kwamba; Imam Ali (a.s) alifika Makka wakati wa alasiri ya siku ya Eid al-Adh-ha kisha akazisoma Aya za hizo za Aya za Bara-a na kuufikisha ujumbe wa bwana Mtume (s.a.w.w.) mbele ya watu. Baada ya hapo, alisema na kuwaambia ya kwamba; kuanzia sasa hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya ibada ya kuzunguka Kaaba akiwa uchi, na kwamba hakuna mshirikina anayeruhusiwa kuja kufanya ibada katika Kaaba mwaka ujao. Kwa mujibu wa kauli ya al-Tabari, ni kwamba; Baada ya hapo Imam Ali (a.s) aliwapa amani watu hao na kusema: wale washirikina waliotia mikataba mapatano na Mtume (s.a.w.w) wataendelea kuwa na amani kwa miezi mine, na yeyote yule ambaye hawakuwa na mikataba ya mapatano atapewa muhula wa muda wa siku hamsini.[10]

Yaliomo Katika Ujumbe wa Aya za Bara-a

Muhammad Jawad Maghniyyah katika tafsiri yake ya al-Kasshaf anaamini kwamba; Aya za Bara-a, ambazo ziliteremshwa ndani ya Surat al-Tawba, zilifafanua hukumu za mwisho kuhusiana na mahusiano kati ya Waislamu na washirikina.[11] Kwa mujibu wa maoni ya wafasiri wa Qur’ani ni kwamba; katika aya za mwanzo za Surat al-Tawba, Mwenye Ezi Mungu anamwamuru bwana Mtume wake (s.a.w.w) akiwa pamoja na Waislamu watangaze kujitenga na kusimama kwao dhidi ya washirikina, na waondoke kwenye mikataba ya mapatano waliyowafunga nao, na ikiwa hawatatubu, watangaze vita dhidi yao. Onyo hili lilijumuisha washirikina wote, hata wale waliotia saini mikataba ya amani na maelewano na bwana Mtume (s.a.w.w). Ilitangazwa kwamba baada ya muda wa miezi minne ya kutafakari kuhusu hali yao, wanapaswa kubaini wajibu wao kuhusu kuingia katika Uislamu au kupigana na Waislamu.[12]

Sababu ya Upande Mmoja Kuvunja Mkataba wa Mapatano

Suala la amri ya kuvunja kwa mikataba ya mapatano na washirikina kupiti maamuzi ya upande mmoja, yaliokuja kupitia Aya za Bara-a, limekuwa ni suala linalodadisiwa na watu mbali mbali, na kwamba licha ya kuwepo kwa maagizo kadhaa yanayo sisitizwa mno suala la uaminifu na kushikamana na ahadi katika dini ya Kiislamu, ni kwa nini hali kama hiyo imeweza kutokea katika jamii ya Wasilamu.[13] Katika jitihada za kujibu utata huu, Ayatullahi Tabatabai, ambaye ni mwandishi wa Tafsiru al-Mizanametoa maoni yasemayo kwamba; Uasi wa washirikina ulikuwa ndiyo sababu ya kuondolewa kwa mikataba ya amani juu yao, na ndio kibali cha kutoa idhini kwa Waislamu kukabiliana nao jinsi ya wao wanavyo amiliana na Waislamu, yaani kuvunja mikataba ya mapatano iliyopo baina yao na washirikina.[14] Kulingana na Tafsiri ya Majma al-Bayani ya Tabarsi ni kwamba; Kulikuwa na sababu tatu zilizopelekea kuvunjwa kwa mikataba ya mapatano ya amani kutoka upande wa bwana Mtume (s.a.w.w), nazo ni kama ifuatavyo:

A- Mikataba hiyo ilikuwa ni mikataba ya kipindi cha muda mfupi
B- Mikataba hiyo ya mapatano ya amani na washirikina, ilikuwa uhai kwa sharti ya kuto kuja amri kutoka kwa Mwenye Ezi ya kuvuja mikataba hiyo.
C- Kudumu kwa mikataba hiyo kulitegemea kudumu kwa uamninifu na ukweli wa washirikina katika kuamiliana na makubaliano ya mikataba yao.[15]

Makarimu Shirazi pia anaamini kwamba; kuvunjwa kwa mikataba ya mapatano kutoka kwa Waislamu, hakukuwa bila utangulizi wowote; kwani kulingana na ushahidi, ilikuwa wazi kwamba washirikina, ikiwa wangeweza kuvunja mikataba ya mapatano, basi wangewasababishia Waislamu pigo kubwa kabisa. Kulingana na maoni yake ni kwamba; mapatano ambayo yanalazimishwa dhidi ya taifa au kundi fulani, huweza kudumu katika hali maalum tu, na baada ya wao kupata nguvu, mikataba hiyo inaweza kukiukwa mara moja.[16]

Kwa mujibu wa maoni ya wafasiri mbali mbali ni kwamba; Kutangaza hadharani kuvunjwa kwa mikataba yamapatano baina ya Waislamu na washirikina, katika kitovu cha mkusanyiko wa washirikina hao huko Makka na katika siku ya Eid al-Adh-ha, na pia kuwapa muda wa miezi minne ili kujitafakari, Ilikuwa ni ajili ya kuwashitukizia washirikina hao kwa ghafla, na hii inaonyesha heshima ya Uislamu katika kuheshimu na kuzingatia kanuni za kibinadamu.[17] Kulingana na maoni ya Ayatullah Tabatabai ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu kwa amri yake hii, amewazuia Waislamu kuto fanya usaliti hata kwa kiwango cha kidogo.[18]

Kuheshimu Ahadi ya Wasiovunja Ahadi

Kwa kuzingatia Aya ya nne Surat al-Tawba, Ayatullah Tabatabai anatofautisha kati ya washirikina wanaovunja ahadi na washirikina wanaozingatia ahadi zao. Yeye Anasema kwamba; washirikina ambao walishikamana na ahadi zilizopo baina yao na Waislamu, na wakawa hawakuivunja ahadi zao, si kwa njia ya moja kwa moja wala kwa njia isiyo ya moja kwa moja, wao hawaingii katika hukumu zilizokuja katika Aya za Bara-a. Waislamu nao wanapaswa kuheshimu ahadi na mikataba waliotiliana na watu kama, na Wislamu wanalazimika kubaki ndani ya mikataba hiyo hadi kumalizika muda wake.[19] Hata hivyo, kwa mujibu wake ni kwamba; wengi wa washirikina walivunja ahadi zao na kuwafanya Waislamu kuto kuwa na uhakiwa.[20]

Sababu ya Kuwalazimisha Makafiri Kukubali Dini ya Kiislamu

Ni sababu gani hasa iliyo pelekea kuwalazimisha washirikina kuingia katika dini ya Kiislamu, licha ya kuwepo kwa Aya katika Qur'an Tukufu ziendazo kinyume na jambo hilo, kama vile Aya ya 256 Surat al-Baqara ambayo inakataza kulmazimisha kuingia katika dini kwa nguvu? Katika kujibu swali hili, imeelezwa ya kwamba; Dini ya Kiislamu inawaita watu kwenye dini kwa njia ya hekima na hoja madhubuti, na hailazimishi mtu yeyote yule kukuibali dini kwa nguvu; lakini wakati mwingine ni lazima kuhakikisha kwamba; washirikina wapo nje ya jamii ya Kiislamu, na kinyume chake itakuwa ni vigumu kabisha kuhakikisha uwepo wa maslahi ya jamii ya Kiislamu. Hii ni kwa sababu uwepo wao husababisha madhara kwa jamii na ufisadi ndani yake. Kulingana na maelezo ya Muhammad Jawad Maghniyah, hukumu ya kuwalazimisha washirikina kuikubali dini ya Kiislamu ilihusiana na washirikina wa Bara Arabu; hii ni kwa sababu wao, licha ya kuwa na mikataba wa amani baina yao na Waislamu, ili walikuwa wakivunja mikataba hiyo mara kwa mara na kuidhuru jamii changa ya Kiislamu, hivyo basi hukumu ya Mungu kuhusiana nao, ilikuwa kwamba; ama wauawe au waingie katika dini ya Kiislamu.[21]

Rejea

  1. Ṣādiqī Tehrānī, al-furqān fī tafsīr al-Qurʾān, juz. 7, uk. 202; Ḥākim al-Ḥaskānī, Shawāhid al-tanzīl, juz. 1, uk. 305; Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 69, uk. 152.
  2. Ṭabrasī, Majmaʿ al-bayān, juz. 5, uk. 3; ʿAyyāshī, Tafsīr al-ʿAyyāshī, juz. 2, uk. 73.
  3. Rajabī, «Imām ʿAlī dar ʿahd-i payāmbar», uk. 209; Ibn Kathīr, al-Bidāya wa l-nihāya, juz. 5, uk. 36-37.
  4. Ṭabarī, Tārīkh al-umam wa l-mulūk, juz. 3, uk. 42.
  5. Rajabī, «Imām ʿAlī dar ʿahd-i payāmbar», uk. 209.
  6. Shubbar, Tafsīr al-Qur'ān al-karīm, juz. 1, uk. 199; Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nemūne, juz. 7, uk. 272.
  7. Mughnīya, Tafsīr al-Kāshif, juz. 4, uk. 9.
  8. Rajabī, Imām ʿAlī dar ʿahdi payāmbar, uk. 209.
  9. Ibn Ḥanbal, Musnad, juz. 2, uk. 427; Ibn Ḥanbal, Faḍhāʾīl al-ṣaḥāba, juz. 2, uk. 703; Ibn ʿAsākir, Tārīkh madīnat Dimashq, juz. 42, uk. 348; Ibn Saʿd, al-Ṭabaqāt al-kubrā, juz. 1, uk. 168; Mufīd, Kitāb al-amālī, uk. 56.
  10. Yaʿqūbī, Tārīkh al-Yaʿqūbī, juz. 2, uk. 76.
  11. Mughnīya, Tafsīr al-Kāshif, juz. 4, uk. 8.
  12. Mughnīya, Tafsīr al-Kāshif, juz. 4, uk. 8; Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nemūne, juz. 7, uk. 272.
  13. Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nimūna, juz. 7, uk. 282.
  14. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 147.
  15. Ṭabrasī, Majmaʿ al-bayān, juz. 5, uk. 5.
  16. Makārim Shīrāzī, Tafsīri nemūne, juz. 7, uk. 283.
  17. Riḍhāʾī Iṣfahānī, Tafsīri Qurʾāni mehr, juz. 8, uk. 145; Makārim Shīrāzī, Tafsīri nemūne, juz. 7, uk. 284.
  18. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 147.
  19. Mughnīya, Tafsīr al-Kāshif, juz. 4, uk. 9-10.
  20. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 150.
  21. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 9, uk. 147.

Vyanzo

  • ʿAyyāshī, Muḥammad bin Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Mhakiki: Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmiyya al-Islāmiyya, 1380 Sh.
  • Ḥākim al-Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh bin ʿAbd Allāh al-. Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
  • Ḥusseinī Rashād. Tehran: Intishārāt-i Pazhūhishgāh-i Farhang wa Andīsha, 1380 Sh.
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī bin al-Ḥassan. Tārīkh madīnat Dimashq. Mhakiki: ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1425 AH.
  • Ibn Ḥanbal, Aḥmad bin Muḥammad. Faḍāʾīl al-ṣaḥāba. Mhakiki: Muḥammad ʿAbbās Waṣī Allah. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1403 AH.
  • Ibn Ḥanbal, Aḥmad bin Muḥammad. Musnad al-Imām Aḥmad bin Ḥanbal.Mhakiki: Shuʿayb al-Arnaʾūt and ʿĀdil Murshid and Wenzake. Beirut: Al-Risāla, 1421 AH.
  • Ibn Kathīr, Ismāʿīl bin ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Mhakiki: Khalīl al-Shaḥāda Beirut: Dār al-Fikr, 1398 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Beirut: Dār Beirut, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Chapa ya pili. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Mufīd, Muḥammad bin Muḥammad al-. Kitāb al-amālī. Mhakiki: Ḥussein Ustādh Walī and ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmiyya, [n.
  • Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1424 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 Sh.
  • Rajabī, Muḥammad Ḥussein. Imām ʿAlī dar ʿahd-i payāmbar In dānishnāma-yi Imām ʿAlī (a.s). Chini ya uangalizi wa ʿAlī Akbar
  • Riḍhāyī Iṣfahānī, Muḥmmad Alī. Tafsīr-i Qurʾān-i mihr. Qom: Pazhūhish-hā-yi Tafsīr wa ʿulūm-i Qurʾān, 1387 Sh.
  • Ṣādiqī Tihrānī, Muḥammad. Al-furqān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Farhang-i Islāmī, 1406 AH.
  • Shubbar, Sayyid ʿAbd Allāh. Tafsīr al-Qur'ān al-karīm. Beirut: Dār al-Hujra, 1410 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad bin Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Mhakiki: Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Beirut: [n.n], [[n.d].
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥussein al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
  • Ṭabrasī, Faḍhl bin al-Ḥassan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Naṣir Khusruw, 1372 Sh.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad bin Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār Beirut, [n.p].