Nenda kwa yaliyomo

Hadithi ya Ali Yupamoja na Haki

Kutoka wikishia

Hadithi ya Ali Yupo Pamoja na Haki na Haki Ipo na Ali (Kiarabu: حديث عَلِيٌّ مَعَ الْحَقِّ وَالْحَقُّ مَعَ عَلِيٍّ) inaashiria maneno yaliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo yanamtambulisha Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) kwamba, daima yupo pamoja na haki na haki ipo pamoja na yeye. Madhumuni ya hadithi hii imenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kwa ibara na maneno tofauti tofauti. Baadhi ya nukuu hizo zimekuja katika vyanzo na vitabu vya Shia na Sunni na kutambuliwa kuwa mutawatiir (hadithi ambayo imepokewa kwa wingi kiasi cha kupatikana uhakika wa usahihi wake). Pamoja na hayo, Ibn Taymiyyah Harrani amekana hadithi kama hizi hata kwa sura dhaifu na kutokubali kwamba zimetoka kwa Mtume (s.a.w.w).

Katika Baraza la Watu Sita la kuianisha Khalifa lililoundwa baada ya Khalifa Omar ibn al-Khattab, Imamu Ali (a.s) akiwa na lengo la kuthibitisha ustahiki wake kwa Ukhalifa alitumiai hadithi hii kama hoja. Kadhalika baadhi ya masahaba na wasomi wa Kisuni, wametumia hadithi hii wakiwa na lengo la kuthibitisha kwamba, amalii na matendo ya Imamu Ali yalikuwa sahihi. Hadithi hii inatumiwa kuonyesha kwamba, Imamu Ali (a.s) ni mbora kuliko masahaba wengine, nii maasumu, kuna ulazima wa kumtii na kwamba, ni mtu anayestahiki Uimamu na kuwa kiongozi wa Waislamu baada ya Mtume na vilevile inazuia kutukanwa kwake.

Matini na Maudhui

Kuwa pamoja na haki ni miongoni mwa sifa na fadhila za Amirul-Muuminin Ali (a.s) ambayo imeashiriwa katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w). Imekuja katika hadithi hii kwamba: «Ali yupo pamoja na haki, na haki ipo pamoja naye». [2] Madhumuni ya hadithi hii imenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kwa ibara na maneno tofauti na katika minasaba mbalimbali. [3] Allama Hilli anaamini kuwa: Kuna hadithi nyingi kuhusiana na maudhui hii kiasi kwamba, haiwezekani kuzihesabu. [4] Kuna Nukuu mbalimbali za hadithi hii zilizokuuja katika vitabu kama Kashf al-Yaqin, [5] Kashf al-Ghummah, [6] Bihar al-Anwar, [7] al-Ghadir [8] na Mizan al-Hikmah [9]. Sayyid Hashim Bahrani katika kitabu cha Ghayat al-Maram amezungumzia hadithi hii na hadithi zinazofanana nayo katika milango miwili na katika kalibu na fremu 26. [10]

Itibari

Baadhi wanaamini kuwa, baadhi ya hadithi ni thabiti na hazina shaka [11] na zimeafikiwa [12] na pande mbili [13] na kwamba, ni mutawatir. [14] Kadhalika inaelezwa kuwa, sehemu ya matini ya hadithii hizi, zina daraja ya juu kabisa ya itibari na kuwa kwake mutawatir na kutokuwa na shaka juu yake ni jambo ambalo linakubaliwa na wapokezi wa hadithi wa Kishia na Kisuni. [15] Vievile hakujatolewa ukosoaji dhidi ya wapokezi na sanadi (mapokeo) ya hadithi hii. [16].

Ibn Abil Hadid ameitambua sanadi yake kuwa sahihi na kwamba, hadithi hii haina shaka; [17] kiasi kwamba, hadithi yenye madhumuni ya «Ali yupo pamoja na haki» iipo katika baadhi ya vitabu vya al-Sihah al-Sittah (Sahihi Sita) [18] na katika athari na vitabu vingine vya Waislamu wa Ahlu Sunna ambapo idadi yake inafika takribani 130. [19]

Madai ya Ibn Taymiyyah

Katika kitabu chake cha Minhaj al-Sunnah Ibn Taymiyyah anaamini kuwa, hakuna mtu aliyenukuu hadithi hii kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) hata kwa sanadii na mapokeo dhaifu. Anamlaumu Allama Hili kwa sababu ya kunukuu hadithi hii na kumtaja kama mtu muongo. [20] Wahakiki wa Kishia katika kumjibu Ibn Taymiyyah wanaashiria hadithi za Masahaba walizonukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na kadhia hii. [21] Vilevile Allama Amini katika kitabu chake cha al-Ghadir baada ya kunukuu matamshi ya Ibn Taymiyyah, amenukuu hadithi nyingi ambazo zimenukuliwa na shakhsia wakubwa wa Ahlu-Sunna pamoja na vitabu vyao vyenye itibari na vya kutegemewa. [22]

Wapokezi

Hadithi ya: Ali yupo pamoja na haki imenukuliwa kutoka kwa Imamu Ali na masahaba 23 [23] ambapo miongoni mwao yumo Khalifa wa Kwanza, [24] Saad ibn Ubadah, [25] Abu Dharr al-Ghifari, [26] Miqdad, [27] Salman Farsi, [28] Ammar Yassir, [29] Abu Mussa Ash'ari, [30] Abu Ayyub Ansari, [31] Saad bin Abi Waqqas, [32] Abdullah ibn Abbas, [33] Jabir ibn Abdillah Ansari, [34] Hudhaifah ibn al-Yaman, [35] Bibi Aisha, [36] na Ummu Salamah.[37]

Katika hadithi za Ahlul-Bayt (a.s), Imamu Swadiq (a.s) anaashiria hadithi hii akinukuu kutoka kwa mababu zake. [38].

Kujengea Hoja

Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) na masahaba wengine walitumia hadithi ya "Ali yupo pamoja na haki" na kujengea hoja katika matukio mbalimbali.

  • Katika Baraza la Watu Sita; ambalo liliundwa kwa ajili ya kuianisha Khalifa baada ya kifo cha Khalifa wa Pili Omar bin al-Khattab, Imamu Ali (a.s) akiwa na lengo la kuthibitisha ustahiki wake kwa Ukhalifa alitumia hadithi hii kama hoja kwamba, yeye anastahiki zaidi nafasi hiyo na akawataka watu wa baraza hilo kutoa ushahidi wa usahihi wake, na kisha watu hao wakaunga mkono na kuthibitisha hilo. [39]
  • Vita vya Jamal; Muhammad bin Abi Bakr, [40] Abdullah ibn Budayl na kaka yake Muhammad [41], baada ya vita vya Jamal walimuendea Bibi Aisha na kumhoji wakimuuliza kuhusiana na hadithi iliyonukuliwa na yeye kuhusiana na haki kuwa pamoja na Ali. Baada ya vita vya Nahrawan Bibi Aisha alikuwa ametumia hadithi ya "Ali yupo pamoja na haki, na haki ipo pamoja na Ali" na kuthibitisha kwamba, matendo na mambo yaliyofanywa na Imamu Ali (a.s) yalikuwa sahihi na kwamba, Ali alikuwa mkweli katika vitendo. [42]
  • Vita vya Siffin; Abu Ayyub Ansari, mmoja wa masahaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w) alipigana dhidi ya wapinzani wa Imamu Ali (a.s) katika vita vya Siffiin akiwa pamoja na Ammar bin Yassir pamoja na Imamu Ali na wengineo, na kwa msingi huo alikuwa pamoja na haki kwa mujibu wa maneno ya Bwana Mtume (s.a.w.w) ya kwamba: Ali yupo pamoja na haki, na haki ipo pamoja na Ali. [43] Vilevile Saad bin Abi Waqqas ambaye hakuwa na uhusiano mzuri na Imamu Ali (a.s) alijengea hoja hadithi hii mbele ya Muawiyah bin Abi Sufyan. [44]

Ahmad bin Hanbal, [45] Ibn Abil al-Hadid, [46] Ibn Jawzi, [47] na Sibt bin Jawzi [48] ni miongoni mwa Maulamaa wa Ahlul-Sunna ambao walimsifia Imamu Ali (a.s) wakitumia hadithi hii kama hoja au walitoa ushahidi wa kuthibitisha kuwa sahihi amali, matendo na mambo yaliiyofanywa na Imamu Ali (a.s).

Kilichoeleweka

Naqsh ya Hadithi ya Ali yupo pamoja na haki, kwenye kaburi la Imam Ali (a.s) [49]

Maulamaa wa Kiislamu wamefahamu na kuuelewa yafuatayo kuhusiana na hadithi ya Ali yupo pamoja na haki:

Ali Kigezo cha Haki na Batili

Imamu Ali (a.s) ametambulishwa na kuarifishwa kama mtu anayelazimiana na haki na yupo pamoja na haki, msema haki na kigezo cha kutambua haki kutoka katika batili. [50] Kwa mujibu wa hadithi hizi, baadhi wanawaona wapinzani wa Imamu Ali kuwa ni watu waliopotea na kutoka katika haki, [51]. Baadhi ya watu wengine wakitumia hadithi hizi kama hoja wanaamini kuwa, kundi pekee litakaloongoka na kufuzu ni wafuasi wa Imamu Ali (a.s). [52] Fakhrurazi, mfasiri wa Qur'ani wa Kisunii akitumia hadithi hii kama hoja anaamini kwamba, kila ambaye katika dini yake atamfuata Ali (a.s) amepata uongofu. [53] Katika mwendelezo wa hadithi, imekuja ya kwamba, Mtume (s.a.w.w) alimwambia Ammar Yassir ya kwamba: Kama watu wote watakuwa upande mmoja na Imamu Ali akawa upande mwingine, basi wewe nenda upande wa Ali, njia ya Ali itakuwa njia ya haki. [54]

Uimamu na Uongozi wa Waislamu ni wa Ali (a.s) Baada tu ya Mtume (s.a.w.w)

Wasomi na wanazuoni wa Kishia wanaamini kuwa, miongoni mwa matokeo na natija ya hadithi za haki kuwa pamoja na Ali (a.s) ni kukubalika kila upande sifa bora na ustahiki wa Ali ukilinganisha na masahaba wengine. Miongoni mwa ustahikii huo mutlaki ni katika suala la Uimamu, uongozi na kuwa Khalifa mstahiki wa Umma wa Kiislamu mara tu baada ya kufariki dunia Bwana Mtume. Kwa maana kwamba, yeye ndiye mrithi na kiongozi wa Waislamu baada tu ya kuaga dunia Mtume na kurejea kwa Mola wake, [55] na kama Ali hakuwa na daraja aali na ya juu ya kukusanya elimu zenu (kutamalaki elimu zote), kuwa na maadili mema na kuwa mweledi wa masuala ya kisiasa, basi asingekuwa mlengwa na mkusudiwa au misdaqi na mfano wa wazi wa hadithi hii ya Bwana Mtume (s.a.w.w). [56]

Wote wanakiri hata masahaba wenyewe ya kwamba, Ali alikuwa mbora na aliyewazidi wao kila kitu, kielimu, kimaadili, ujuzu wa mambo na kadhalika. Allama Muhammad Baqir Majlisi anasema, Muutazilah pia wakitumia hadithi hizi wanaamini kwamba, Imamu Ali (a.s) alikuwa sahaba bora kabisa miongoni mwa masahaba wa Bwana Mtume. [57]

Umaasumu (kinga ya kutotenda dhambi) wa Imamu Ali (a.s)

Sheikh Mufidu anaamini kuwa, Imamu Ali kutokana na kutajwa kwa sifa kama hii na Mtume (s.a.w.w), hawezi kuwa mtu ambaye anakosea au kuwa na shaka katika hukumu za Mwenyezi Mungu [58] na hawezi kutumbukia katika upotofu. [59] Baadhi wanaamini kuwa, kutokana na hadithi hii kutokuwa na sharti ndani yake katika suala la Imamu Ali kuwa pamoja na haki, [60], hiyo ni moja ya sababu za Imamu Ali kuwa ni Maasumu (asiyetenda dhambi) [61[ na kwamba, hilo linajumuisha nyanja zote za kielimu, kivitendo, kisheria, kiada, kijamii na kimaadili pia; [62] na kwa muktadha huo wanaamini kuwa, ni muhali kwa Imamu Ali kufanya kosa au kutenda dhambi;[64] hii ni kutokana na kuwa, kwa kufanya dhambi au hata kosa, hali ya kulazimiana na kuwa pamoja haki na Ali itaondoka na hivyo maneno ya Mtume yatakuwa yamekwenda kinyume na uhalisia. [65]

Wajibu wa Kumtii Ali (a.s) na Marufuku ya Kumfanyia Uadui

Kwa kutumia hadithi hii, imekuwa wajibu kwa wengine kumtii Imamu Ali (a.s) mutlaki. [66] Baadhi ya wanasema kuwa, hadithi hizi zimetambua suala la kuifikia kilele fadhila, karama na adhama ya Imamu Ali na wanaamini kwamba, kinachofahamika kwa akali kabisa kupitia hadithi hizi ni marufuku ya kupigana vita na Ali, kumlaani na kuonyesha uadui dhidi yake. [67]

Kuleta Mshabaha Kwa Ajili ya Khalifa wa Pili

Baadhi ya Waislamu wa Kisuni wamezungumzia juu ya kunukuliwa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kumhusu Khalifa wa Pili Omar bin al-Khattab ambayo inashabihiana na kufanana na hadithi tuliyotangulia kuijadili ya "Ali yupo pamoja na haki na haki iko pamoja naye. Wanadai kwamba, Mtume Muhammad (s.a.w.w) sambamba na kumtakia rehma Omar alimtambua kuwa, msemaji wa haki hata kama haki itamuacha. [68]

Katika uga huu, baadhi ya wahakikiki wanaamiini kwamba, thamani ya muhtawa (maudhui) na sanadi (mapokeo) ya hadithi ya Ali yupo pamoja na haki, ilikuwa ikizuia na kukataza kukana na kuihesabu hadithi hii kwamba, ni dhaifu; kwa msingi huo, maadui wa Imamu Ali wakafanya hima na juhudi ili kuandaa na kutunga hadithi zenye fadhila zinazoshabihiana na hadithi hii kwa ajili ya washindani wa Ali au katika muendelezo wa hadithi zenye fadhila kumhusu Imamu Ali waongezee kitu ili ziwe na ushahidii na ishara pia kwa watawala wa kabla ya Imamu Ali, na kwa msingi huo, fadhila hiyo isiwe ni makhsusi tu kwa Imamu Ali (a.s) peke yake. [69]

Masuala Yanayo Fungamana

Rejea

Vyanzo