Hadithi al-Wilaya
Hadith al-Wilaya (Kiarabu: حديث الولاية) ni hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na ni moja ya hoja zinazotumiwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa ajili ya kuthibitisha Uimamu na uongozi wa Ali bin Abi Talib (a.s). Hadithi hii imenukuliwa katika vitabu na vyanzo vya Kishia na Kisunni kwa ibara tofauti. Hata hivyo ibara mashuhuri zaidi miongoni mwazo ni: ("هُوَ وَلِیُّ کُلِّ مُؤْمِنٍ بَعْدی" ; Yeye (Ali) ni walii (kiongozi) wa kila muumini baada yangu).
Mashia wanaamini kuwa, neno walii lililotumika katika hadithi hii lina maana ya Imamu na msimamizi wa mambo na kupitia kwayo wanathibitisha Uimamu na uongozi wa Imamu Ali bin Abi Talib (a.s) na wanaami kuwa, “walii” katika lugha ina maana hii hii na imetumiwa katika maeneo mbalimbali na Sheikhein (Abu Bakr na Omar), masahaba, tabiina na baadhi ya Maulamaa wa Ahlu-Sunna; hata hivyo Masuni wanadai kwamba, neno hili lina maana ya rafiki na msimamizi na halina uhusiano wowote na Wilaya (uongozi) na Uimamu wa Al bin Abi Talib.
Andiko
Jafar bin Sulaiman amepokea kutoka kwa Imran bin Husayn kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alituma kundi kwenda kupigana vita na akamfanya Ali bin Abi Talib kuwa kamanda wao. Wakafanikiwa kupata ghanima na Imam Ali (a.s) akazigawa ghanima hizo kwa namna ambayo wao hawakufurahishwa na ugawaji huo. Watu wanne miongoni mwao wakakubaliana kwamba, watakapomuona Mtume (s.a.w.w) watamjuza kuhusiana na kitendo hiki cha Ali. Walipofika kwa Mtume mmoja baada ya mwingine alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je unatambua kwamba, Imamu Ali amefanya hivi? Mtume akiwa na sura ya kukasirika aliwaambia, mnataka nini kutoka kwa Ali? Mnataka nini kutoka kwa Ali? Ali anatokana na mimi, na mimi ninatokana na Ali, na Ali baada yangu ni walii wa kila muumini. [1]
Nukuu tofauti
Hadith al-Wilaya (Hadithi ya Wilaya/uongozi) imenukuliwa katika vyanzo vya Kishia na Kisunni kwa ibara tofauti. Miongoni mwanzo ni: ((علی ولیّ کل مؤمن بعدی ; Ali ni Walii wa kila muumini baada yangu)) [2], ((هو ولی کل مؤمن بعدی ; Yeye ni Walii wa kila muumini baada yangu))[3], ((انت ولی کل مؤمن بعدی ; Wewe ni Walii wa kila muumini baada yangu))[4], ((أنت ولی کل مؤمن بعدی ومؤمنه ; Wewe ni walii wa kila muumini mwanaume na muumini mwanamke baada yangu))[5], ((انت ولیی فی کل مؤمن بعدی ; Wewe ni Walii wangu katika kila muumini baada yangu))[6], ((فانه ولیکم بعدی ; Hakika yeye ni Walii wenu baada yangu)){7}, ((ان علیا ولیکم بعدی ; Hakika Ali ni Walii wenu baada yangu))[8], ((هذا ولیکم بعدی ; Huyu ni walii wenu baada yangu))[9], ((انک ولی المؤمنین من بعدی ; Hakika wewe ni Walii wa waumini baada yangu))[10], ((انت ولیی فی کل مؤمن بعدی ; Wewe ni Walii wangu katika kila muumini baada yangu))[11], ((و انت خلیفتی فی کل مؤمن من بعدی ; Na wewe ni Khalifa wangu katika kila muumini baada yangu))[12], ((و فهو اولی الناس بکم بعدی ; Na yeye (Ali) mbora miongoni mwa watu baada yangu))[13].
Maudhui
Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba, muhtawa na maudhui ya hadithi ya al-Wilaya inahusiana na kadhia ya Uimamu na Wilaya (uongozi) ya Ali (a.s). [14] Wao wanalitambua neno Walii kwamba, linaa maana ya msimamizi, Imamu, kiongozi na khalifa. [15] Hata hivyo, Waislamu wa Ahlu-Sunna, wao wanaamini kwamba, hadithi hii haina dalili na ishara za suala la uongozi wa Ali bin Abi talib baada ya Mtume, kwani wanadAi kwamba, neno Walii katika lugha lina maana ya rafiki na kusaidia. [16] Waislamu wa Kishia wakiwa na lengo la kuthibitisha madai yao wanasema: Neno Walii katika lugha lina maana ya msimamizi, kiongozi, khalifa, mtu mwenye mamlaka na Imamu na kwamba, mwanzoni mwa Uislamu na baada ya kipindi hicho pia, neno hili lilikuwa likitumika kwa maana ya khalifa na msimamizi. Kadhalika Mashia wanashiria kutumiwa neno hili kwa maana hii na khalifa na msimamizi na Khalifa wa kwanza, [17] khalifa wa pili, [18], masahaba, [19] tabiina [20] na baadhi ya Maulamaa wa Kisuni. [21]
Itibari
Abdul-Qadir Baghdadi na Ibn Hajar al-Asqalani wamesema, hadithi ya Wilaya imenukuliwa na Tirmidhi ikiwa na mapokezi na sanadi imara kutoka kwa Imran Husayn. [22] Mutaqi Hindi pia ameitambua hadithi hii kuwa ni sahihi. [23] Hakim Neyshapour amesema kuwa, hadithi hii sanadi yake ni sahihi. Hata hivyo, Muslim na Bukhar hawajaileta hadithi hii katika vitabu vyao vya Sahihein. [24] Kadhalika, Shams al-Din Dhahabi na Nasser al-Din al-Bani wameitambua hadithi hii kuwa ni sahihi. [25]
Vyanzo
Hadithi ya Wilaya imenukuliwa na kuletwa katika vyanzo na vitabu mbalimbali kama: Sahih Tirmidhi, Musnad Ahmad bin Hanbal; [26] Jamiu al-Ahadith Suyuti; [27] Kanzul Ummal’ [28] Musnad Abi Dawud; [29] Fadhail al-Sahabah; [30] al-Aaahad wal-Mathani; [31] Sunan Nasai; [32] Musnad Abu Ya’la; [33] Sahih ibn Habban; [34] al-Mu’jam al-Kabir Tabarani; [35] Tarikh Madinat Dimashq; [36] al-Bidayat wal-Nihayat; [37] al-Isabah; [38] al-Jawharah fi Nasb al-Imam Ali Waalih; [39] Khazanat al-Adab Walubb Lubab Lisan al-Arab; [40] al-Ghadir; [41] al-Isti’ab; [42] na Kash al-Ghummah. [43].
Uchunguzi wa sanadi (mapokezi)
Mubarakfuri anadai kwamba, neno "baadi" yaani "baada yangu" halipo katika baadhi ya nakala za hadithi ya Wilaya na limeongezwa na wapokezi wa hadithi wa Kishia. Akiwa na nia ya kuthibitisha madai yake haya anatumia Musnad ibn Hambal kama hoja ya ambapo ndani yake hadithi hii imekuja ikiwa na sanadi na mapokezi mbalimbali lakini anadai kwamba, hakuna hata moja kati ya hadithi hizo ambayo ina nyongeza hii. [44] Hata hivyo, Ahmad Hambal ameileta hadithi hii katika Musnad [45] na Fadhail al-Sahabah ikiwa na nyongeza hii (neno: "baadi" yaani baada yangu". [46]
Kadhalika Mubarkfuri (Abul-Alaa Muhammad bin Abdul-Rahman 1353-1283 Hijria) amedai kwamba, hadithi hii imepokewa na kusimuliwa na watu wawili tu, Ja'far bin Suleiman na Ibn Aljah al-Kindi na kwamba, kutokana na kuwa kwao Mashia, hadithi zao hazikubaliki. Yeye anawatambua Mashia kuwa ni watu wa bidaa na anasema kwamba, ikiwa mzushi na mtu wa bidaa atanukuu hadithi ambayo itapelekea kuimarika madhehebu yake, basi hadithi hiyo haikubaliki. [47] Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa al-Bani ni kwamba, kigezo pekee cha kukubaliwa hadithi na masuni ni ukweli na umakini wa mpokezi katika kunukuu hadithi na kwamba, madhehebu ya mpokezi wa hadithi, hayana taathira yoyote katika kukubaliwa au kukataliwa hadithi yake. Ni kutokana na sababu hiyo, ndio maana Bukhari na Muslim wamenukuu katika vitabu vyao vya sahihi mbili (Sahihein) hadithi kutoka kwa wapokezi ambao madhehebu yao yanapingana na madhehebu ya Ahlu-Sunna kama makhawarij na Mashia. [48]
Al-Bani (Muhammad Nassir-al-Din 1914-1999 Miladia) amesema, hadithi hii imenukuliwa katika vyanzo vya Ahlu-Sunna kwa sanadi na mapokezi mengine ambapo katika mlolongo wa mapokezi yake hakuna mpokezi wa Kishia. [49] Sayyied Ali Milani amesema, hadithi hii imenukuliwa kutoka kwa masahaba [50] 12 akiwemo Imamu Ali (a.s), Imamu Hassan (a.s), Abu Dharr, Abu Said al-Khudhri na Baraa bin Azib [51] ambapo akthari ya nukuu zake zinaishia kwa Imran bin Husayn na Burayda bin Husayb. [52]
Kadhalika Ja'fara bin Suleyman, ni mmoja wa wapokezi wa Sahih Muslim [53] ambaye al-Dhahabi anamtaja kwa ibara ya Imamu [54] na amenukuu kutoka kwa Yahya bin Muin ya kwamba, alikuwa akimtambua kuwa ni mtu wa kuaminika. [55] Al-Bani anamtambua Ja'far kuwa ni mmoja wa wapokezi wa hadithi anayeaminika na mwenye hadithi imara ambaye alikuwa akimili upande wa madhehebu ya Ahlu-Sunna na hakuwa akilingania madhehebu yake. Yeye anasema: Hitilafu baina ya viongozi wetu haipo katika suala hili kwamba, mkweli atakuwa ni katika watu wa bidaa na uzushi, lakini hakulingania na kuegemea upande wa madhehebu yake, basi ni sahihi kushikamana na hadithi yake. [56]
Baadhi ya Maulamaa wa Ahul-Sunna, wamemtaja Ibn Ajlah kuwa ni katika watu waaminifu na kuzitambua hadithi zake kuwa ni Hasan (nzuri). [57] Al-Bani anatambua kuwa, hadithi ya Ajlah ni ushahidi wa kuwa sahihi hadithi ya Ja'far bin Suleyman. [58]
Mubarakfur amesema, Ibn Taymiyah alikuwa akidai kwamba, hadithi hii ni ya uongo ambayo ndani yake amenasibishwa Mtume wa Allah. [59] Al-Bani ni katika Maulamaa wa Ahlu-Sunna ambaye ameshangazwa mno na hatua ya Ibn Taymiyah ya kukana hadithi hii. [60]
Monografia
- Hadith al-Wilayah Waman Rawaa Ghadir Khum Mina al-Sahabah; Ibn Uqdah al-Kufi.
- Hadith al-Wilayah, Seyyid 'Ali Husayni Milani; Markaz al-Haqa'iq al-Islamiyya.
Rejea
Vyanzo
- Abū Yaʿlā al-Mūṣilī, Aḥmad b. ʿAlī. Musnad Abī Yaʿlā. Edited by Ḥasan Salīm Asad. Damascus: Dār al-Maʾmūn li-l-Turāth, n.d.
- Abū Bakr al-Shaybānī, Aḥmad b. ʿAmr. Al-Āḥād wa l-mathānī. Edited by Bāsim Fiyṣal Aḥmad Jawābira. Riyadh: Dār al-Dirāya, 1411 AH.
- Albānī, Muḥammad Naṣir al-Dīn al-. Silsilat al-aḥādīth al-ṣaḥīḥa wa shayʾ min fiqhihā wa fawāʾidihā. Beirut: Maktabat al-Maʿārif, 1415 AH.
- Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn al-. Al-Ghadīr. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1397 AH.
- Baghdādī, ʿAbd al-Qadir al-. Khazānat al-adab wa lub lubāb lisān al-ʿArab. Edited by Muḥammad Nabīl Ṭarīqī & Amīl Badīʿ Yaʿqūb. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1998.
- Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Ḥamīd Allāh. Egypt: Dār al-Maʿārif, 1959.
- Dhahabī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Siyar iʿlām al-nubalāʾ. Edited by Shuʿayb Arnāʾūṭ & Muḥammad Naʿīm ʿArqasūsī, Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1413 AH.
- Dhahabī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām wa waffayāt al-mashāhīr wa l-aʿlām. Edited by ʿUmar ʿAbd al-Salām Tadmurī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1413 AH.
- Ḥākim Nayshābūrī, Muḥammad b. ʿAbd Allāh. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Edited by ʿAbd al-Raḥmān Marʿashī. n.p, n.d.
- Hindī, Muttaqī al-. Kanz al-ʿummal. Edited by Shaykh Bakrī al-Ḥayyānī. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1409 AH.
- Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad Bajāwī. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
- Ibn Abī Shayba al-Kūfī, ʿAbd Allāh b. Muḥammad. Al-Muṣannaf fī aḥādīth wa l-Āthār. Edited by Saʿīd al-Liḥām. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
- Ibn ʿAsākir,ʿAlī b. Ḥasan. Tārīkh Madīna Dimashq. Edited by Muḥib al-Din ʿumar b. Gharāma. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
- Ibn Ḥabbān, Muḥammad. Ṣaḥīḥ Ibn Ḥabbān. Edited by Shuʿayb Arnāʾūṭ. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1414 AH.
- Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣahāba. Edited by ʿĀdl Aḥmad ʿAbd al-Mujūd & ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
- Ibn Ḥanbal, Aḥmad. Faḍāʾil al-Ṣaḥāba. Edited by Waṣī Allah Muḥammad ʿAbbas. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1403 AH.
- Ibn Ḥanbal, Aḥmad. Masnad. Egypt: Muʾassisat al-Qurtuba, n.d.
- Ibn Kathīr, Ismāʾīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH.
- Ibn Saʿd, Muḥammad b. Manīʿ al-Ḥāshimī al-Baṣrī. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1410 AH.
- Ījī, ʿAbd al-Raḥmān al-. Sharḥ al-mawāqif. Edited by Badr al-Dīn al-Ḥalabī. Qom: Al-Sharīf al-Raḍī, 1325 AH.
- Irbili, ʿAlī b. Abī al-Fatḥ al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1405 AH.
- Khaṭīb al-Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh Baghdād. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmayyya, n.d.
- Manāwī, ʿAbd al-Raʾūf al-. Fayḍ al-qadīr fī sharḥ jāmiʿ al-ṣaghīr. Edited by Aḥmad ʿAbd al-Salām. Beirut: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1415 AH.
- Masʿūdī, ʿAlī b. al-Husayn. Murūj al-dhahab wa maʿādin al-Jawāhir. Edited by Asʿad Dāghir. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
- Mīlānī, Sayyid ʿAlī. Tashyīd al-murājiʿāt wa tanfīdh al-mukābirāt. Qom: Markaz al-Ḥaqāʾiq al-Islāmīyya, 1427 AH.
- Mubārakfurī, Muḥammad b. ʿAbd al-Raḥmān al-. Tuḥfat al-aḥwadhī bi-sharḥ jamiʿ al-Tirmidhī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1410 Ah.
- Nayshābūrī, Muslim b. Ḥajāj al-. Saḥīḥ Muslim. Beirut: Dār al-Fikr, n.d.
- Nisāʾī, Aḥmad b. Shuʿayb al-. Al-Sunan al-Kubrā. Edited by ʿAbd al-Ghaffār Sulaymān Bindārī & Sayyid Ḥasan Kasrawī. Beirut: Dār al-kutub al-ʿIlmīyya, 1411 AH.
- Nisāʾī, Aḥmad b. Shuʿayb al-. Khaṣāʾiṣ amīr al-muʾminīn. Qom: Būstān-i Kitāb, 1383 Sh.
- Raḥīmī Iṣfahānī, Ghulām Ḥusayn. Wilāyat wa rahbarī. Tafresh: Intishārāt-i ʿAskarīyya, 1374 Sh.
- Shaybānī, ʿAmr b. Abī ʿĀthim al-. Al-Sunna. Edited by Muḥammad Nāṣr al-Din al-Albānī. Beirut: Al-Maktab al-Islāmī, 1413 AH.
- Ṭabarānī, Sulaymān b. Muḥammad. Al-Muʿjam al-kabīr. Edited by Ḥamdī b. ʿAbd al-Majīd Salafī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, n.d.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu al-Faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dār al-Turāth, 1387 AH.
- Tiālasī, Sulaymān b. Dāwūd. Musnad Abī Dāwūd. Beirut: Dār al-Maʿrifa, n.d.
- Tilmisānī, Muḥammad b. Abī Bakr. Al-Jawhara fī nisab al-Imām ʿAlī wa Ālih. Qom: Anṣārīyān, n.d.