Nenda kwa yaliyomo

Laa Fataa Ilaa ‘Ali

Kutoka wikishia
Ibara ya «Laa Fataa Ilaa ‘Ali» iliyoandikwa katika ubao wa chuma, inayohusishwa na zama za Safawi

Laa Fataa Ilaa ‘Ali (Kiarabu: لا فَتَى إلاّ عَلي): Ni kauli ya mbinguni iliyotolewa na mmoja wa Malaika kuhusiana na fadhila na sifa za Imam Ali (a.s).[1] Kulingana na riwaya nyingi zilizosimuliwa kutoka pande zote mbili, za Shia na Sunni, ni kwamba; pale Imamu Ali (a.s) alipokuwa akimlinda na kumhami Bwana Mtume (s.a.w.w) katika vita vya Uhud, kulisikika sauti kutoka mbinguni isemayo:

(لا سَیفَ اِلاّ ذُوالفَقار و لا فَتی اِلاّ عَلی)

yaani Hakuna upanga kama Dhu al-Fiqar wala shujaa kama Ali.[2] Katika baadhi ya Riwaya, imeelezwa ya kwamba mtoaji wa sauti hii ya mbinguni alikuwa ni Jibril,[3] na katika baadhi ya Hadithi nyengine, ametajwa kuwa ni Malaika aitwaye Ridhwan[4] ila katika Riwaya nyingine jina la mwongeaji halijatajwa.[5] Katika baadhi ya ripoti, tukio hili pia linahusishwa na vita vya Badri[6] au Khaibar.[7] Allamah Amini (aliyefariki mwaka 1390 Hijiria), ambaye ni mwandishi wa kitabu al-Ghadir, akitegemea Hadithi kadhaa kuhusiana na suala hili, anaamini kuwa; tukio hili halikutokea mara moja tu, bali ni tukio lilijiri mara kadhaa.[8] Kulingana na baadhi ya Riwaya, Imamu Ali (a.s) aliitegemea sentensi hii na kuinukuu pale alipokuwa akielezea sifa zake.[9]

Ibara ya «Laa Fataa Ilaa ‘Ali» iliyoandikwa katika ubao, na mchoraji Farid-Din

Kwa mujibu wa mwanazuoni maarufu aitwaye Amini, ni kwamba; wataalamu wa elimu ya Hadithi wanakubaliana kuhusu ukweli wa Hadithi hii.[10] Katika kitabu cha Kifayat al-Talib fi Manaqib Ali bin Abi Talib amabacho ni miongoni mwa vyanzo vya Ahlu-Sunnah (kiliyoandikwa karne ya 7 Hijiria), kuna sura maalum ndani yake inayozungumzia nukuu tofauti za Hadithi hii, kisha ikaelezwa kuwa wanafani wa upande wa fani ya Hadithi (Ahlu-Hadith), wanakubaliana juu ya ukweli wa taarifa hii.[11] Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya waandishi wa upande wa Ahlu-Sunnah, Hadithi ambayo inaripoti tukio hili ni ya uongo,[12] pia wamesema kwamba; hata Ibn Taimiyyah pia naye aliona taarifa hii kuwa ni ya uongo.[13]

Ibara isemayo: «لا سیف الا ذوالفقار و لا فتی الا علی» (Hakuna upanga kama Dhu al-Fiqar, wala hakuna mtu shujaa kama Ali) ni ibara inayonekana kwenye panga tofauti.[14] Washairi kama Saadi,[15] Khaja Kermani,[16] na Attari Nishapuri[17] wametunga mashairi na tenzi mbalimbali zilizobeba ndani yake ibara hii maarufu isemayo: «hakuna shujaa kama Ali». Kulingana na maelezo ya Allamah Amini ni kwamba; Hassan bin Thabit kwa idhini ya Mtume (s.a.w.w), pia naye aliandika mashairi kuhusiana na ibara hiyo.[18]

Maudhui zinazo fungamana

Rejea

  1. Kulaini, al-Kafi, juz. 8, uk. 110.
  2. Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 8, uk. 110; Sheikh Saduq, Amāli, uk. 200; Sheikh Mufid, al-Irshad, juz. 1, uk. 87, Sheikh Tusi, Amāli, uk. 143; Ibnu Hisham, al-Sirah al-Nabawiyah, juz. 2, uk. 100; Tabari, Tarikh al-Tabari, juz. 2, uk. 514.
  3. Sheikh Saduq, 'Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), 1378 S, juz. 1, uk. 85.
  4. Sheikh Mufid, 1413 H, al-Irshad, juz. 1, uk. 87; Fatal Neishaburi, Raudhat al-Wa'idhin, juz. 1, uk. 128.
  5. Sheikh Saduq, 'Ilal al-Sharai' , juz. 1, uk. 7.
  6. Khawarizmi, al-Manaqib, uk. 167, Hadithi no. 200.
  7. Sibt Ibnu Jauzi, Tadhkirat al-Khawas, uk. 26.
  8. Amini, al-Ghadir, juz. 2, uk. 104.
  9. Sheikh Saduq, al-Khisal, 1362 H, juz. 2, uk. 550; Ibnu Asakir, Tarikh Madinah Dimascus, juz. 39, uk. 201.
  10. Amini, al-Ghadir, juz. 2, uk. 104.
  11. Ganji, Kifayat al-Talib, uk. 277-280.
  12. Ibnu Jauzi, al-Maudhu'at, juz. 1, uk. 381-382.
  13. Halabi, al-Sirat al-Halabiyah, juz. 2, uk. 321.
  14. Zarwani, «Dhulfiqar», uk. 849.
  15. Sa'di, Kuliyat Sa'di, 1365 S, Qasideh 1.
  16. Khawajah Kermani, Divan Ash'ar, 1369 S, uk. 133.
  17. Atar Neishaburi, Musibat-nameh, uk. 34.
  18. Amini, al-Ghadir, juz. 2, uk. 105.

Vyanzo

  • Amini, Abdul-Hussein, al-Ghadir fi al-Kitab wa al-Sunnah wa al-Adab, Qom: Markaz al-Ghadir li al-Dirasat al-Islamiah, 1416 HS.
  • Atar Neishaburi, Muhammad, Madzhar al-'Ajaib wa Madh-har al-Asrar, Tehran: Sinai, 1376 S.
  • Athar Neishaburi, Muhammad, Musibat-nameh. Mhariri: Nurani Wasal, Tehran: Zuwwar, 1356 S.
  • Fatal Neishaburi, Muhmmad bin Ahmad, Raudhah al-Wa'idhin wa Bashirat al-Muta'adhin, Qom: Intisharati Ridha, 1375 S.
  • Ganji, Muhammad bin Yusuf, Kifayat al-Talib fi Manaqib Ali bin Abi Talib, Tehran: Dar Ihya al-Turath Ahlul-bait, 1404 HS.
  • Halabi, Ali bin Ibrahim, al-Sirat al-Halabiyah, Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiyah, 1427 HS.
  • Ibnu Asakir, Ali bin Hassan, Tarikh Madinah Damascus wa Dhikr Fadhlha wa Tasmiyat man Hallaha min al-Amathil, Mhakiki: Omar bin Gharamah Omari, Beirut: Dar al-Fikr, 1995 M
  • Ibnu Hisham, Abdul-Malik, al-Sirat al-Nabawiyah, Beirut: Dar al-Ma'rifah.
  • Ibnu Jauzi, Abdul-Rahman bin Ali, al-Maudhu'at, Madinah, Al-maktaba al-Salafiyah, 1386 S.
  • Khawajah Kermani, Mahmud, Divan Ash'ar. Mhakiki: Ahmad Suhaili Khunsari. Tehran: Pazhank, 1369 S.
  • Khawarizmi, Muwafiq bin Ahmad, al-Manaqib, Qom: Jamiah Mudarrisin, 1411 HS.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub, al-Kafi, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, Chapa ya nne, 1407 HS.
  • Muhtasham Kashani, Ali bin Ahmad, Divan Muhtasham Kashani. Tehran: Tazama, 1387 S.
  • Sa'di, Muslih ad-Din, Kuliyat Sa'di, Tehran: Amir Kabir, 1365 S.
  • Sibt Ibnu Jauzi, Tadzkirah al-Khawash, Qom: Intisharat al-Sharif Al-Radhi, 1418 HS.
  • Shah Niimatullah Wali, Shah Niimatullah Wali, Divan Hazrat Shah Niimatullah Wali, Kerman: Intisharat Khidmat Farhangi Kerman, 1380 S.
  • Shahriyar, Muhammad Hussein, Divan Shahriyar. Tehran: Tazama, 1385 S.
  • Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad. al-Irshad fi Ma'rifah Hujajillah ala al-Ibad, Qom: Congress Sheikh Mufid, 1413 HS.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, 'Uyun Akhbar al-Ridha, Teheran: Penerbit Jahan, 1378 S.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, al-Āmali, Teheran: Kitabci, 1376 S.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, al-Khishal, Qom: Kantor penerbit Islami, 1362 S.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali, Ilal al-Sharai', Qom: Toko buku Davari, 1385 S.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, al-Āmali, Qom: Dar al-Tsaqafah, 1414 HS.
  • Tabari, Muhammad bin Jarir, Tarikh Tabari, Mhakiki: Muhammad Abu al-Fadhl Ibrahim. Beirut: Dar al-Turath, 1387 HS.
  • Zarwani, Mujtaba, Dhulfiqar, Dar Jild 18 Daneshname Jahan Islam. Teheran: Buniyad Dairat al-Ma'arif Islami, 1392 S.