Taiyyah Di'bil

Kutoka wikishia

Shairi la Taiyyah la Di'bil (Kiarabu: تائية دعبل) ni beti za mashairi za Di'bil bin Ali al-Khuza'i kuhusu Ahlul-Bayt (a.s). Shairi hili limezingatiwa kuwa mojawapo ya tenzi bora zaidi za kuwasifu Ahlul-Bayt. Shairi hili lina beti 120 na ndani yake kumezungumziwa ukhalifa na Wilaya (uongozi) ya Imam Ali (a.s) pamoja na fadhila na mateso waliyokumbana nayo Ahlul-Bayt (a.s).

Kwa mara ya kwanza Di’bil alimsomea Imamu Ridha (a.s) shairi hilo huko Marv na Imamu akampa sarafu za dhahabu au fedha ambazo zilikuwa na jina lake kama ambavyo alimzawadiia shati lake na kisha Imamu akaongeza beti kadhaa katika shairi hilo na hivyo kukamilisha zaidi maana na madhumini ya shairi hilo. Kumeandikwa vitabu mbalimbali kwa ajili ya kufafanua na kutoa maelezo kuhusiana na shairi hili na miongoni mwavyo ni: «Sherh va tarjume shi’r Taiyyah Di’bil» (Ufafanuzi na tarjumi ya shairi la Taiyyah la Di’bil) kilichoandikwa na Allama Majlisi.

Nafasi na Umuhimu Wake

Kaswida au shairi la Di’bil lililotungwa na Di'bil bin Ali al-Khuza'i mmoja wa masahaba wa Imamu Ridha (a.s), limetambuliwa kama mojawapo ya tungo bora na zenye fahari zaidi za kuwasifu Ahlul-Bayt (a.s) [1] Ja'afar Subhani, mwanahistoria na Marjaa wa Shia, amelitambua shairi hili kama hati ya kihistoria na ya milele ambayo ndani yake kumebainishwa sera ya Bani Umayyah na Bani Abbas dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s). [2] Kwa mujibu wa Sayyid Muhsin Amin katika kitabu cha A’yan al-Shiah, shairi hili ni mashuhuri mno kiasi kwamba, wanahistoria wote wamelijadili na washairi wameliashiria katika tungo za mashairi yao .[3]

Maudhui ya Shairi na Sababu ya Kupewa Jina Hilo

Kaburi linalohusishwa na Di'bil bin Ali al-Khuza'i katika mji wa Shush

Shairi hili limetungwa kwa ajili ya kuwasifu Ahlul-Bayt (a.s) na kubainisha masaibu na mambo yaliyowakumbwa. Wilaya (uongozi) ya Ali bin Abi Twalib (a.s), kuwa na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s), dhulma aliyoifanyiwa Imamu Ali (a.s) na watu wa nyumba yake baada ya kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w), tukio la Karbala na harakati na mapinduzi ya Alawi dhidi ya Ukhalifa wa Bani Umayyah na Bani Abbas ni miongoni mwa mambo yaliyozungumziwa katika shairi hili. [4]

Katika fasihi ya Kiarabu mashairi muhimu hupewa jina kulingana herufi ya mwisho inayomalizikia katika shairi. Kwa msingi huo, shairi la Di’bil limeitwa kwa jina la Taiyyah Di’bil kutokana na kumalizikia na herufi ya «ت». [5] Shairi hili ni mashuhuri pia kwa jina la «Madaris Ayaat» (mahali pa kujifunza Aya za Qur’ani). [6] Aidha shairi hili linatambulika kwa majina ya «al-Taiyyah al-Kubra» na «al-Taiyyah al-Khalidah». [7] Di’bil aliandika beti za shairi hili katika kitambaa na akafunga kitambaa hicho na ihram (vazi la mahujaji) na akausia kwamba, wakiweke kitambaa hicho katika sanda yake. [8]

Nakala Mbalimbali za Shairi

Allama Amini anasema katika kitabu chake cha al-Ghadir kwamba: Imeelezwa katika ripoti na nukuu mbalimbali kwamba, idadi ya beti za shairi hili ilikuwa 120. [9] Hata hivyo, Yaqut Hamawi, mwandishi wa historia wa karne ya sita na ya saba anaamini kwamba, kuna nakala tofauti za shairi hili na anasema kuwa, kuna uwezekano baadhi ya Mashia waliongezea beti za shairi hili. [10] Sayyid Muhsin Amin anasema, uwezekano huo uliozungumziwa na Yaqut Hamawi sio sahihi na akasema kwamba, tofauti ya nakala za shairi hili sababu yake ni tofauti za dhuku za walionukuu shairi hili katika kupanga beti za mashairi haya; kwani shairi la Taiyyah ni refu na baadhi ya watu katika kunakili shairi hili, walifuta baadhi ya beti na hivyo kunukuu badhi tu ya beti zake. [11]

Msimamo wa Imamu Ridha kwa Shairi Hili

Baada ya Di’bil kutunga shairi hili la Taiyyah alijiwekea ahadi ya kutolisoma kwa ajili ya mtu mwingine yeyote kabla ya Imamu Ridha (a.s). Kwa hiyo, alikwenda Marv na kumsomea Imamu (a.s). [12] Imamu Ridha (a.s) alionyesha kuridhika mno na shairi hili. [13] Wakati Di’bil alipomsomea Imam Ridha shaili hili, Imamu alilia sana. [14] Imamu Ridha alimtaka Di’bil asome tena shairi hilo na alifanya hivyo mara tatu na Di’bil alatekeleza takwa hilo la Imamu. [15]

Zawadi ya Imamu Ridha kwa Di’bil

Sherhe ya Mashairi ya Taaiyyah Di'bil, iliyoandikwa na Allamah Majlisi

Baada ya Di’bil kusoma shairi hilo, Imamu akampa sarafu za dhahabu au fedha ambazo zilikuwa na jina lake kama ambavyo alimzawadia shati lake. [19] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa na Sheikh Tusi katika kitabu cha Amali kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) ni kwamba, Imamu Ridha alikuwa ametumia vazi hilo kuswalia kwa muda wa siku elfu moja na katika kila usiku mmoja aliswali rakaa elfu moja. Aidha akiwa amevaa vazi hilo, Imamu Ridha alihitimisha kusoma Qur’ani mara elfu moja. [20] Watu wa Qum walimtaka Di’bil awazuie shati hilo kwa dirihamu 30,000, lakini Di’bil alikataa na badala yake alikata mikono ya shati hilo na kuwapatia na akausia kwamba, sehemu ya nguo iliyobakia atakapokufa iwekwe katika sanda yake. [21] Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, Mashia walinunua kutoka kwa Di’bil kila sarafu moja ya dhahabu ambayo Imamu Ridha alimpatia kwa bei ambayo ni mara kumi ya thamani yake ya kawaida. [22]

Vitabu Vilivyoandikwa Kufafanua Shairi la Taiyyah

Shairi la Taiyyah la Di’bil limeafanunuliwa na watu mbalimbali. [23] Miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kufafanua shairi hili ni:

  1. «Sherh va tarjume shi’r Taiyyah Di’bil» (Ufafanuzi na tarjumi ya shairi la Taiyyah la Di’bil) kilichoandikwa na Allama Majlisi kwa lugha ya Kifarsi. Kitabu hiki kimesahihishwa na kuhakikiwa na Muhammad Lutfzadeh na kusambazwa na Taasisi ya Uchapishaji ya Dar al-Mujtaba, Qum, Iran mwaka 2014 kikiwa na kurasa 200. [24] Masahihisho mengine ya kitabu hiki yamefanywa na Ali Muhadith. [25]
  2. «Sherh Qasidah Di’bil al-Taiyyah», mwandishi Muhammad bin Fasawi (mkwe wa Allama Majlisi): Kitabu hiki kilisambazwa na Taasisi ya al-Balagha ya Beirut, Lebanon mwaka 1436 Hijria kikiwa na kurasa 487. [26]
  3. «Sharh Qasidah Di’bil», Mwandishi Neematullah Jazayri. [27]

Rejea

Vyanzo