Aya ya Lailatu Al-Mabit
Aya ya Lailatu Al-Mabit au Ayah Shiraa (Kiarabu: آية ليلة المبيت أو آية الشراء) ni Aya ya 207 ya Suratu al-Baqarah. Aya hii inahusiana na kujitolea muhanga kwa Ali (a.s), nayo ni Aya iliyoteremka katika tukio la Lailatu Al-Mabit. Tukio hili ni lile tukio la Ali bin Abi Talib (a.s) kulala kitandani mwa Mtume (s.a.w.w). Aya hii imeteremka kwa ajili ya kuwasifu watu ambao wako tayari kujitolea muhanga maisha yao kwa ajili ya kupata radhi za Mungu.
Asili ya Aya na Tafsirir Yake
Aya ya 207 ya Surah al-Baqarah ni Aya maarufu ijulikanayo kwa jina la Ayatu Al-Shiraa(الشراء) au Ishtiraa, Maneno mawili haya yana ambayo yamo katika Qur'an, yana maana ya: Uuzaji au ufanyaji biashara. Aya hii ya 207 ya Surat al-Baqarah, imeteremka kama ifuatavyo:
و مِنَ النَّاسِ مَن یشْرِی نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَ اللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ
Na miongoni mwa watu kuna wanaouza nafsi zao (wanaozitoa muhanga nafsi zao) kwa ajili ya kupata radhi za Mwenye Ezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
(Surat al-Baqarah: 207)
Sababu ya Kushuka Kwake
- Makala Asili: Lailatu Al-Mabit
Allamah Tabatabai ameandika katika kitabu chake Al-Mizan ya kwamba: Kuna Hadithi nyingi zinazoeleza ya kwamba; Ayatu Al-Shiraa iliteremka kuhusiana na tukio la Lailatu Al-mabit.[1] Kwa mujibu wa kauli ya Ibnu Abi Al-Hadid, mwanachuoni wa madhehebu ya Ahlul-Sunna -mwenye kushikamana na nadharia za Mu’tazila- , katika maelezo yake ya tafsiri ya Nahju Al-Balagha, amesema: Wafasiri wote wa Qur'an wanaamini kwamba, Aya hii iliteremshwa kuhusiana na Imam Ali (a.s) katika tukio la Lailatu Al-Mabit.[2] Ambapo ilikuwa ni wakati wa usiku, usiku ambao washirikina wa kiqureish walikusudia kushikamana katika kundi moja na kumshambulia Mtume (s.a.w.w) na kumuuwa, huku akiwa amelala nyumbani kwake huko mjini Makka. Katika usiku huo, Imam Ali (a.s) alilala katika kitanda cha bwana Mtume (s.a.w.w) ili kuokoa maisha yake, na kwa njia hiyo basi, Mtume akawa ameokolewa na mpango huo muovu wa washirikina.[3]
Kwa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Kisunni, wakitegemea baadhi ya Hadithi fulani, wametoa mtazamo tofauti kuhusiana na sababu ya kushuka kwa Aya hii. Mtazamo wa wanazuoni hao wa Kisunni ni kwamba; Aya hii inahusiana na Masahaba kama vile Abu Dharr, Suhaib bin Sinaan,[4] Ammar Yasir na wazazi wake, Khabbaab bin Aratt na Bilal Al-Habshi[5]. Hata hivyo, kuna shaka kadhaa kuhusiana na umakini na umadhubuti wa riwaya hizo. Kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, riwaya hizo zimepotoshwa kwa sababu ya chuki na kwa malengo ya kufunika sifa na fadhila za Imam Ali (a.s).[6]
Vidokezo vya Tafsiri
Mizizi na shina la neno (یَشْری) katika Aya hii na neno (شِراء).[7] lenye maana ya kuuza.[8] Aya ya (شِراء) imeteremka kwa ajili ya kuwasifu wale walioko tayari kutoa maisha yao pamoja na roho zao kwa ajili kutafuta radhi za Mola wao.[9] Aina ya watu hawa iko kinyume kabisa na ile ya lile kundi la watu wa aina ya pili waliotajwa katika Aya ya 204 hadi 206 ya Suratu Al-Baqarah. Watu wa aina ya kundi hili la pili ni; Watu walio wabinafsi, wakaidi, wenye uadui na wanafiki, wanaojifanya kuwa ni watu wema, kumbe lengo lao ni kufanya ufisadi.[10] Kwa mujibu wa kauli ya Allamah Tabaatabai; Muktadha wa Aya hizi unaonyesha ya kwamba, makundi yote haya mawili yalikuwepo katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w).[11] Ijapokuwa baadhi ya wafasiri wameifasiri sentensi ya mwisho ya Aya hii isemayo; (وَالله رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ; Na Mwenyezi Mungu n Mwenye rehema na Mpole kwa waja wake) kuwa; Mwenyezi Mungu ni Mpole na Mwenye kurehemu kwa waja hao (wanaotafuta radhi za Mwenyezi Mungu). Lakini kwa mujibu maoni ya Allamh Tabatabai, maana ya sentensi hiyo ni kwamba; Mwenye Ezi amekuwa ni Mpole na Mrehemevu kwa waja wengine wote, kutokana na kule kuwepo kwa watu wanaojitolea miongoni mwao, ambao wapo tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya kupata radhi za Mola wao. Pia ni rehema ya Mwenye Ezi Mungu kuwepo kwa watu wa aina hiyo ndani ya jamii fulani.[12]
Daraja Tatu za Uuzaji wa Roho (Kujitolea Muhanga)
Katika tafsiri ya Aya ya (شِراء), baadhi ya wafasiri wameugawa uuzaji wa roho katika daraja tatu tofauti, nazo ni: Uuzaji wa roho kwa sababu ya kuogopa moto wa Jahannamu, uuzaji wa roho kwa tamaa ya kupata Pepo, na uuzaji wa roho kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Wao wameihisabu daraja ya tatu, kuwa ndiyo daraja yenye kiwango cha juu kabisa katika daraja hizo tatu za uuzaji wa roho. Ambapo katika daraja hiyo ya tatu, mtu huwa hana nia wala tamaa yoyote ile juu ya malipo ya uuzaji wa roho yake. Wafasiri hawa wamelihisabu lile tendo la Imamu Ali (a.s) la kulala katika kitanda cha Mtume (s.a.w.w) katika usiku wa Lailatu Al-Mabit, kama ndio mfano mmoja wa daraja hiyo ya tatu ya uuzaji wa nafsi.[13] Kwa mujibu wa maneno ya Allamah Tabaatabai ni kwamba; Kule mja kuuza maisha yake kwa ajili ya kumridhisha Mola wake, kunamaanisha ya kwamba, watu wa aina hii hawataki kito chochote kila katika matendo yao hayo ya kujitoa muhanga na kuuza roho zao, isipokuwa ni kupata radhi za Mola wao, na matakwa yao wao yanaendana na matakwa ya Mola wao, na wala hayaendani na matakwa ya nasfi zao.[14]
Rejea
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 2, uk. 100.
- ↑ Ibn Abī l-Ḥadīd, Sharḥ Nahj al-balāgha, juz. 13, uk. 262.
- ↑ Ṭūsī, al-Amālī, uk. 466.
- ↑ Ṭabarī, Jāmiʿ al-Bayān, juz. 3, uk. 591.
- ↑ Fakhr al-Razi, al-Tafsīr al-kabīr, juz. 5, uk. 350.
- ↑ Hashimi, ((Baresi sababu nuzul aye ishtirai nafsi)),uk. 153
- ↑ Ṣādiqī Tihrānī, al-furqān, juz. 3, uk. 225.
- ↑ Makarim Shiraz, Tafsiri nemune,1371 S, juz. 2, uk. 78
- ↑ Ṭaliqānī, Partuwī az Qurʾān, juz. 2, uk. 100.
- ↑ Makārim Shīrāzī, Tafsīr-i nimūna, juz. 2, uk. 79.
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 2, uk. 98.
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 2, uk. 98.
- ↑ Ṣādiqī Tihrānī, al-furqān, juz. 3, uk. 225-226.
- ↑ Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān, juz. 2, uk. 98.
Vyanzo
- Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-kabīr). Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
- Ḥākim al-Nayshābūrī, Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak 'alā l-ṣaḥīḥayn. Edited by Muṣṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭāʾ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1411 AH.
- Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balāgha. Qom: Maktabat Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
- Ibn Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī al-Karam. Usd al-ghāba fī Maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1371 Sh.
- Ṣādiqī Tihrānī, Muḥammad. Al-furqān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Farhang-i Islāmī, 1406 AH.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jāmiʿ al-Bayān. Edited by ʿAbd Allāh b. ʿAbd al-Muḥsin b. al-Turkī. al-Jiza: Dār al-Hijr li-l-Ṭabāʿat wa l-Nashr wa l-Tawzīʿ wa l-Iʿlān, 1422 AH.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1393 AH.
- Ṭaliqānī, Maḥmūd. Partuwī az Qurʾān. 4th edition. Tehran: Shirkat-i Sahāmī-yi Intishār, 1362 Sh.
- Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by Muʾassisat al-Biʿtha. Qom: Dār al-Thiqāfa li-ṭibaʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1414 AH.