Sifa na wasifu wa Imamu Ali (a.s)
Sifa na wasifu wa Imamu Ali (a.s) (Kiarabu: فضائل الإمام علي (ع)). Imamu Ali (a.s) ni mwenye wasifu na sifa mbali. Ali bin Abi Talib ni Imamu wa kwanza wa Madhehebu ya Shia, ambaye sifa zake zimeashiriwa na Aya mbaimbali za Qu’ani pamoja na Hadithi pia ndani ya matokeo mbalimbali ya kihistoria. Kuna kauli iliyopokewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) isemayo kwamba; Ni vigumu kuzihesabu sifa za Ali bin Abi Talib (a.s). Kulingana na Hadithi nyingine ni kwamba; Kuzitaja sifa zake, kuziandika, kuzitafakari pamoja na kuzisikiliza, ni miongoni mwa matendo ya ibada na hupelekea mtu kusamehewa makosa yake.
Kuna aina mbili za sifa za Imamu Ali (a.s): Sifa na wasifu makhususi na sifa za kijumla jamala, ambazo zinamshirikisha yeye pamoja na Ahlul-Bayt (a.s) wote. Aya ya Wilaya, Aya ya Shiraa, Aya ya Infaq, Hadithi ya Ghadir, Hadithi Al-tair Al-Mashwi, Hadithi Al-Manzilah na Hadithi ya Kuzawadia Pete, ni maalumu juu ya sifa na wasifu wake makhususi.
Katika kipindi cha Banu Umayyah, ilikuwa ni kosa kutangaza na kueneza sifa zinazohusiana na wasifu wa Imam Ali (a.s). Yeyote yule aliyekuwa akieneza sifa za Ali bin Abi Talib Katika kipindi hicho ima aliuwawa au aliwekwa kiziwizini. Pia, kupitia amri za Muawiya, wale waliozibandikiza sifa za Imam Ali (a.s) kwa makhalifa watatu walitiwa moyo na kutunzwa. Baadhi, kama vile Ibn Taymiyyah, kiongozi wa Usalafi na wanafunzi wake, kama vile Ibn Kathir na Ibn Qayyim Al-Jozi, wamezingatia idadi kadha ya Aya na Hadithi kuhusu sifa za Imam Ali (a.s) kuwa ni potofu ambazo ni za uongo au bandia.
Licha ya juhudi za wapinzani za kuzuia kuenezwa sifa za Imam Ali (a.s), fadhila nyingi za Ali bin Abi Talib (a.s) zimenukuliwa na wanazuoni wa madhehebu ya pande zote mbili, za Shia na Sunni. Wanazuoni hao wameandika na kuorodhesha vitabuni mwao sifa kadhaa makhususi za Imamu Ali (a.s). Miongoni mwa vitabu hivyo ni Fadhailu Amirul-Mu'minina cha Ibn Hanbal, Khasaisu Amir Al-Mu'minina cha Nasa'i na 'Umdatu 'Uyuni Sahihi Al-Akhbar fi Manaqib Imami Al-Abrari cha Ibn Batriq.
Maana, umuhimu na vigao
Maana ya sifa ni aina maalumu za wasifu zinazomfanya mtu binafsi au kundi fulani kuwa na ubora kuliko kundi au watu wengine. [1] Hivyo basi, (فضایل امام علی(ع) ; sifa za Imam Ali (a.s)) ni mkusanyiko wa sifa zenye kujenga wasifu wa Imamu Ali (a.s). Sifa ya kwanza kabisa, ni kwamba yeye ni Imamu wa madhehebu ya Shia, ambaye ametajwa katika Aya, Hadithi na nukuu mbalimbali za Kihistoria. Sifa hizo ndizo ndizo zilizomboresha na kumfanya awe juu zaidi kuliko wengine. Katika vitabu vya kitheolojia vya Shia, sifa za Ali bin Abi Talib (a.s), zimetumika katika kuthibitisha Uimamu na ubora wake katika nafasi ya Ukhalifa. [2] Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ya kwamba; Sifa za Imamu Ali (a.s) ni nyingi sana kiasi ya kwamba haziwezi kuhisabika. [3] Sunni pia wanakubaliana na hili; Kwa mfano, imepokewa kutoka kwa Ahmad bin Hambal, kiongozi wa madhehebu ya Hambali kwamba; Kuna kiasi kikubwa cha sifa zilizonukuliwa kuhusiana na Ali bin Abi Talib, kiasi ya kwamba hakuna mfano wa Swahaba mwingine yeyote yule mwenye kiwango kikubwa cha sifa kama hicho. [4]
Sifa za Imamu Ali (a.s) zimegawika katika vigao viwili:
- Sifa makhususi za Ali (a.s): Sifa makhususi ni zile sifa kuhusiana na wasifu wake yeye peke yake, kama vile yeye kulala kwenye kitanda cha Mtume (s.a.w.w) katika usiku ujulikanao kwa jina la Lailat Al-Mubit, ambapo Allah aliteremsha Aya maalumu kuhusiana na tukio hilo.
- Sifa enevu (sifa shirikisho): Sifa enevu au sifa shirikishi ni sifa zilizowaenea watu wa Shuka (Ahlu Al-kisaa) pamoja na Maasumina wote waliobakia. Aina ya sifa kama hizi utakuta zimetajwa katia Hadithi tofauti, kama vile; Hadithi ya Thaqalaini, ambayo ndani yake inawajumuisha Ahlul-Bayt wote kwa jumla, ambapo Hadithi ya Kisaa, ni makhususi kwa watano tu waliofinikwa shuka na bwana Mtume (s.a.w.w).
Kwa kuzingatia Hadithi iliyopokewa na Ibn Shaadhan Qommiy kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), ni kwamba; Mtu ambaye ataandika sifa za Imam Ali (a.s), Malaika watamuombea msamaha, na wataendelea kufanya hivyo mpaka athari ya maandishi hayo itakapofutika. Pia mwenye kusikiliza utajo wa sifa zake, Mwenyezi Mungu atamfutia madhambi alizoyafanya kupitia masikio yake, na mwenye kuangalia kuziangalia sifa za Imamu Ali (a.s), atasamehewa madhambi zake alizoyafanya kupitia macho. [5]
Sifa alizosifiwa kupitia Qur'ani
Sifa za alizosifiwa na Qur'an: Sifa hizi zinahusiana na sifa zilizotajwa na Aya za Qur'an, ambazo ima ziliteremshwa kuhusiana na Imamu Ali (a.s) au mfano hai kuhusiana na Aya hizo ni Imamu Ali (a.s). Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba; Kiasi cha Qur’an kilichoteremshwa kuhusiana na Ali (a.s) hakikuteremshwa kuhusiana na mtu mwingine yeyote yule. [6] Pia, Ibn Abbas amenukuu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwamba; Mwenyezi Mungu hakuteremsha Aya ambayo ndani yake mna ibara ya ((یا أیها الذین آمنوا ; Enyi mlioamini)), isipokuwa Ali ndiye kiongozi wa waumini na ndiye mtu wa mwanzo miongoni wao. [7] Alizingatia ya kwamba; Kuna kiwango cha zaidi ya 300 kilichoteremshwa kuhusiana na sifa za Ali (a.s). Baadhi ya sifa za Qur'an juu ya Imam Ali ni:
- Aya ya Wilayat: Aya ya Wilaya ni Aya ya 55 ya Surat Al-Maidah, isemayo kwamba Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na wanaoswali na kutoa zaka wakiwa wamerukuu, ndiwo wenye mamlaka juu ya watu (Waislamu). [9] Wafasiri wa Shia na Sunni wamewafikiana ya kwamba; Sababu ya kuteremka kwa Aya hii, ni kitendo cha Ali ((a.s)) cha kutoa pete yake na kumpa fakiri hali akiwa yupo kwenye rukuu ya sala yake. [10]
- Aya ya Shiraa (Uuzaji wa Nafsi): Ni Aya ya 207 ya Surat Al-Baqarah, Aya hii inawasifu na kuwapa pongezi wale ambao wako tayari kutoa maisha yao kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu [11] Kwa mujibu wa maoni ya Ibn Abi Al-Hadid, mwanachuoni wa kundi la Al-Mu'utazilah, ni kwamba; Wafasiri wote wanaamini ya kwamba Aya hii iliteremshwa kwa ajili ya Imam Ali ((a.s)). [12] Allameh Tabatabai ameandika kuhusiana na Aya hii akisema: Kwa mujibu wa Hadithi Aya Aya hii, iliteremka kuhusiana na tukio la Lailat Al-Mabit. [13] Wakati wa Lailat Al-Mabit, washirikina walipanga kuishambulia nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) huko Makka na kumuua akiwa amelala nyumbani kwake. Katika usiku huu, Imam Ali ((a.s)) alilala kwenye kitanda cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ili kuokoa maisha ya Mtume (s.a.w.w). [14]
- Ayah Tabligh (Aya ya Kuutangaza Ujumbe : Ni Ayah ya 67 ya Surat Al-Maida, ambayo kwa mujibu wake, Mtume Muhammad (s.a.w.w), alilazimika kufikisha ujumbe kwa watu, na ikiwa atashindwa kuufikisha, basi atakuwa hajatimiza na hajafikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu. [15] Kwa mujibu wa maoni ya wafasiri wa Shia na Sunni, Aya ya Tabligh iliteremka katika bonde la Ghadir Khum wakati Mtume akiwa narudii kutoka Hijjatu Al-Wida'a. [16] Hadhithi zimeeleza ya kwamba Aya hii iliteremka kuhusiana na tukio la Ghadir na tangazo la kumtanga Ali ((a.s)) ni ndiye mrithi wa nafasi ya bwana Mtume endapo Mtume Muhammad (s.a.w.w) atafariki dunia. [17]
- Aya ya Ikmal: Aya ya Ikmal ni Aya ya 3 ya Surat Al-Maida inayozungumzia kukamilika kwa dini ya Kiislamu. [18] Kwa mujibu wa tafsiri ya Nasir Makarim Shirazi, ambaye ni mfasiri wa madhehebu ya Shia ni kwamba; Katika tafsiri za Kihia, kukamilika kwa dini kunamaanisha tangazo la kutangaza mamlaka na nafasi ya ukhalifa wa Imam Ali (a.s) juu ya Waislamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kufariki. Jambo ambalo pia limethibitishwa na Hadith mbali mbali. [19] Wanachuoni wa Kishia wanaamini kwamba; Aya ya Ikmal iliteremka kuhusiana na tukio la Ghadir. [20]
- Aya Sadiqiin: Aya ya Sadiqiina ni Aya ya 119 ya Surat Al-Tawba ambayo inawausia waumini kuwa pamoja na Sadiqiina (Wasemakweli) na kushikamana nao.” [21] Katika Hadith za Shia, neno Sadiqeen (Wasemakweli) limefasiriwa kwa maana ya Ahlul-Bait (a.s), Muhaqqiq Tusi amesema kwamba Aya hii ilishuka kuhusiana na Imamu Ali (a.s). 23]
- Aya ya Khairu Al-Bariyyah: Ni Aya ya saba ya Surat Al-Bayyinah, inayowatambulisha wale walioamini na wakatenda mema kuwa ni ndiwo viumbe bora. [24] Kwa mujibu wa Hadith za Shia na Sunni, kundi hili hili la viumbe bora, ni Imam Ali (a.s) na wafuasi wake. [25]
- Aya ya Salihul-Muuminiina: Ni Aya ya 4 ya Surat Al-Taharim, ambapo Mwenyezi Mungu alimweka Ali (a.s), Jibril na Malaika wengine kama tegemeo la Mtume Muhammad (s.a.w.w). Katika tafsiri, kupitia Hadithi kutoka pande zote mbili za Sunni na Shia, [26] ni kwamba; Mfano mfano hai pekee wa Salihul-Muuminiina katika Aya hii, ni Imam Ali (a.s). [27]
- Aya ya Infaq (Sadaka): Ni Aya ya 274 ya Surat Al-Baqarah. Aya hii inaelezea malipo ya wale watoawo sadaka usiku na mchana kwa siri na dhahiri mbele ya Mola wao Mlezi. [28] Kwa mujibu wa maelezo ya wafasiri, Aya hii iliteremka kuhusiana na Ali (a.s), ambaye alikuwa na dirham nne, moja akaitoa sadaka wakatika wa usiku, ya pili akaitoa mchana, moja akaitoa kwa siri na moja kwa dhahiri. [29]
- Aya ya Naj'wa: Aya ya Najwa ni Aya ya 12 ya Surat Al-Mujadalah ambayo inawaelekeza na kuwahimiza Waislamu matajiri kutoa sadaka wakiwa kwenye mazungumzo (mazungumzo ya siri) na Mtume wa Muhammad (s.a.w.w). [30] Kulingana na maelezo ya Tabarsiy ni kwamba; Wengi miongoni mwa wafasiri wa Kishia na Kisunni wamesema ya kwamba, mtu pekee aliyefanyia kazi Aya hii, ni Imamu Ali (a.s). [31]
- Aya ya Wuddi: Nayo ni Aya ya 96 ya Surat Maryam ambayo kwa mujibu wake Mwenyezi Mungu anaingiza mapenzi ya waumini ndani nyoyo za watu wengine.” [32] Kwa mujibu wa baadhi ya Hadith, kuhusiana na Aya hii ni kwamba; Mtume (s.a.w.w) alimtaka Ali aseme; Ewe Mweny Ezi Mungu, weka upendo wangu katika mioyo ya waumini. Baada ya ombi hilo, Aya hii iliteremshwa. [33]
- Aya ya Mubaahalah: Ambayo ni Aya ya 61 ya Surat Al-Imran Aya hii inaelezea kisa cha Mubaahalah (kula kiapo cha maapizano) wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na Wakristo wa Najran. Kwa mujibu wa tafsiri ya Aya hii ni kwamba; Imam Ali (a.s) ametambulishwa katika Aya hii kuwa yeye ni nafsi ya Mtume (s.a.w.w). [34]
- Aya ya Tat'hiir (Utakaso): Ni sehemu ya Aya ya 33 ya Surat Al-Ahzab, ambamo ndani yake imeelezewa matakwa ya Mwenyezi Mungu juu ya kuwatakasa Ahlul-Bait (a.s) kutokana na uchafu na uchafu. Wafasiri wa Kishia wanaamini kwamba; Aya hii iliteremshwa kuhusiana na As'habu Al-Kisaa (Watu Waliofunikwa Shuka). [35]
- Aya ya Uli Al-Amri: Ambayo ni 59 ya Surat Al-Nisa, inayowaamrisha waumini kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w) na wenye mamlaka miongoni mwao. [36] Kwa mujibu wa wafasiri wa Shia na Sunni, Aya hii inaashiria umaasumu wa wenye mamalaka. [36] 37] Katika Hadith imeelezwa ya kwamba; Maana halisi ya neno "ulil-amri katika Aya hii, ni maimamu wa Kishia. [38]
- Aya ya Mawaddah: Ni Aya 23 ya Surat Shura. Katika aya hii, imetakiwa kuwafanyia wema na kuwa na mapenzi na «اَلْقُرْبیٰ» "Al-Qurba" (watu wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w) iwe ndiyo malipo ya ujumbe wa Mtume (s.a.w.w) na kufanya hivyo ni wajibu kwa Waislamu wote duniani. [39] Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba; Mtume alimchukulia Ali, Fatimah, Hassan na Hussein kuwa ndiwo waliokusudiwa katika neno "Al-Qurba". [40]
- Aya ya It-'aamu (kulisha maskini): Aya hii ambayo ni Aya ya 8 ya Surat Al-Insan, inawatambulisha wafadhili wa kweli kuwa ni wale ambao, ingawa wao wenyewe wanahitaji chakula, ila wao hujinyima na badala yake, chakula cha huwapa masikini, mayatima na mateka kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Kulingana na maelezo ya Hadithi, Aya ilimteremkia Ali pamoja na bibi Fatima. [42] Kwa mujibu wa Hadithi ni kwamba; Ali na Fatima (a.s) walifunga siku tatu kwa ajili ya nadhiri ya kupata ponyo la Hasanain (Hassan na Hussein) (a.s), na katika siku zote tatu, kila ulipofika wakati wa kufutari, walibaki na njaa zao, kwa sababu chakula chao walikitoa na kuwapa masikini, mayatima, na mateka, huku wao wenyewe wakisamehe kula na kubaki na njaa. 43]
- Aya ya Ahlul-Dhikri: Hii ni Aya ya 43 ya Surat Nahli na pia ni Aya ya 7 ya Surat Anbiyaa, aya hizi zinasisitiza juu ya kuwauliza maswali Ahlul-Zikr (watu wenye elimu). [44] Kwa mujibu wa baadhi yaHadithi,, Ahlu Al-Dhikri Ahlul-Bait wa Mtume Muhammad tu peke yao. [45]
- Aya ya Nasri: Nayo ni Aya ya 62 ya Surat Anfal. Kwa mujibu wa tafsiri ya Ayatullah Makarim Shirazi, kila muumini aliyemsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) amejumuishwa katika aya hii, lakini hapana shaka kwamba, mfano kamili na mtu mashuhuri miongoni mwa waumini katika Aya hii ni Ali (a.s). [46] Ayatullah Makarim Shirazi katika kitabu chake Ayat Wilayat Dar Qur'an, anasema kwamba; Aya ya Nasri ni mojawapo wa Aya zinazohusiana na sifa za Amirul-Mu'minin (a.s). [47]
- Siratu Al-Mustaqiim: Ni Aya katika Surat Al-Fatiha, katika Hadithi kadhaa imeelezwa ya kwamba; Ali na muongozo wa Ali ndiyo maana ya Siratu Al-Muistaqiim ndani ya Qur'ani Karim. [48]
Sifa katika simulizi za Hadithi
Katika mada hii, tukizungumzia sifa katika simulizi za Hadith, tunakusudia zile sifa zlilizonukuliwa kutoka katika Hadithi za bwana Mtume (s.a.w.w), zenye kumsifu Imam Ali (a.s). Baadhi ya Hadithi hizo ni pamoja na:
- Hadithi ya Ghadir: Hadithi ya Ghadir, ni Hadithi iliyonukuu hotuba ya Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) katika bonde la Ghadir Kham. Hotuba ambayo inamtambulisha Ali (a.s) kuwa ndiye kiongozi mwenye mamlaka ya kuwaongoza Waislamu baada kufariki kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Hadithi hii imenukuliwa kutoka katika vyanzo vya pande zote mbili, za Shia na Sunni. [49] Hadhithi hii inachukuliwa kuwa ni mojawapo ya ithibati na vielelezo vya Shia katika kuthibitisha Uimamu na Ukhalifa wa Imamu Ali. (a.s). [50]
- Hadithi ya Manzlah: Hadithi ya Manzlah ni hadithi inayoitambulisha nafasi ya Imam Ali (a.s) mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja ukaribu uliopo baina yao, ambapo Hadithi hii imesema kuwa; Nafasi ya Imamu Ali mbele ya Mtume (a.s), ni sawa na nafasi ya Harun mbele ya na Nabii Musa (a.s). [51]
- Hadithi ya Madinatu Al-Elimu: Hii ni Hadith ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambayo inamtambulisha Imamu Ali (a.s), kuwa yeye ndiye mlango wa mji wa elimu. [52] Kitabu cha Al-Ghadir kimewataja wapokezi 21 wa Kisunni walioikubali Hadithi hii kuwa ni miongoni mwa Hadith sahihi. [53]
- Hadithi ya Yaumu Al-Daar: Hii nayo ni Hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambapo aliwataka jamaa za kuukubali na kuupokea ujumbe wake, wakati huo huo akabainisha urithi na ukhalifa wa Ali Ibn Abi Talib (a.s) katika Hadithi hiyo. [54] Wanatheolojia wa Kishia wameitegema Hadithi hii, ikiwa ni miongoni mwa ithibati na vielelezo katika kuthibitisha Uimamu wa Ali bi Abi Talib (A.S). [55]
- Hadithi ya Wasiyyat: Hii nayo ni Hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambamo ndani ya Hadithi hii, amemtambulisha Imam Ali (a.s) kama mrithi na ni mshika nafasi ya Mtume (s.a.w.w) baada yake. [56] Pia Hadithi hii ni miongoni mwa Hadithi zinazotegemewa na Mashia katika kuthibitisha Uimamu wa Imamu Ali (a.s). [57]
- Hadithi ya Wilayah: Hadithi ya Wilayah ni Hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) inayomtambulisha Ali bin Abi Talib kuwa ndiye mwenye mamlaka juu ya waumini baada yake (s.a.w.w). Hadithi hii imesimuliwa katika maneno na ibara tofauti katika vyanzo vya pande zote mbili, za Shia na Sunni. [58] Mashia wanalichukulia neno "mamlaka" ambalo limetumika katika ibara isemayo عَلِیٌّ وَلِیُّ کُلِّ مُؤْمِنٍ مِنْ بَعْدِی) [59]) kuwa, linamaanisha maana ya Uimamu na ushikaji hatamu za uongozi, na kupitia njia hiyo wanathibitisha Uimamu na mamlaka ya uongozi kwa Imamu Ali (a.s). [60]
- Hadithu Al-Tair (حدیث الطیر): Hadithu Al-Tair ni Hadithi inayohusu sifa za Imamu Ali (a.s), kwa mujibu wa muqtadha wa Hadithi hii, Mtume (s.a.w.w) alikusudia kula nyama ya ndege wa choma (ndege wa kubanika) na akamwomba Mungu ale ndege huyo pamoja na mbora wa wanadamu, naye akala na Imamu Ali (a.s). [61] Riwaya hii inapatikana katika vyanzo vya Shia na Sunni. [62]
- Hadithu Al-Rayah (حديث الراية): Kuna Hadith maarufu kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhusu Imam Ali (a.s) katika vita vya Khaibar, ambapo aliwambia Masahaba zake kwa kusema: "Kesho nitampa bendera mtu ambaye Mungu ataleta ushindi dhidi ya ngome ya Khaibar kupitia mkononi mwake, yeye ni mwenye mapanzi juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mungu na Mtume wake ni wenye mapenzi naye." [63]
- Hadithu Al-Thaqlain (حديث الثقلين): Ni hadithi mashuhuri ya Mtume (s.a.w.w) kuhusu nafasi ya Qur'an na Ahlul-Bait. Imeelezwa katika Hadithi hii ya kwamba, bwana Mtume (s.a.w.w) aliwambia Masahaba wake: “Mimi ninakuachieni vizito viwili (johari mbili) ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, navyo ni: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na 'Itra yangu (watu maalumu wa kizazi changu), ambao ni Ahlul-Bait.” [64] Hadithi hii imenukuliwa kutoka katika vyanzo vya Shia pamoja na Sunni. [65]
- Hadithu Al-Kisaa (حديث الكساء) : Hadithi hii Hadithi inayohusiana na sifa za watu watano maalumu. Kwa mujibu wa Hadithi hii, ambayo imetajwa katika vyanzo vya Shia [66] na Sunni [67], Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliifunika familia yake kwa shuka na akamuomba Mola wake akisema: "Ewe Mola wangu, hawa ndio Ahlul-Bait wangu, basi waondolee uchafu na uwatakase.” [68]
- Hadithi Al-Safina (حديث السفينة): Hadithi Al-Safina ni Hadithi mashuhuri ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambamo Ahlul-Bait (a.s) wamefananishwa na safina ya Nuhu, ambayo atakayeingia ndani yake ataokoka na anayebaki nyuma (atakaye achana nayo) ataghariki. [69] ] Hadithi hii imesimuliwa katika vyanzo vya Shia na Sunni. [70]
- Hadithu Al-Shajarah (حديث الشجرة): Katika Hadithi hii Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mimi na Ali tumeumbwa kutokana na mti mmoja na watu wengine wameumbwa kutokana na miti mingine mbalimbali. [71] Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba; Kwa vile Mtume na Imam Ali (a.s) wameumbwa kutokana na chanzo kimoja, hiyo ni dalili ya wao huwa ni sawa, basi kama ilivyokuwa ni wajibu kumtii Mtume (s.a.w.w), pia ni wajibu kumtii Ali (a.s). [72]
- Hadithu Al-Lauh (حديث الوح): Ni moja ya hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika kuthibitisha Uimamu wa Maimamu kumi na mbili, ambamo ndani yake yametajwa majina ya warithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuanzia Imamu wa kwanza, ambaye ni Ali (a.s) hadi Imam wa kumi na mbili, ambaye ni Imam Mahdi (a.j.t.f). [73]
- Hadithu Al-Haqqi "حديث الحق": Ni moja ya Hadithi maarufu za Mtume zinazomtambulisha Ali (a.s) kama ndiye mizani ya haki. Moja ya nukuu za Hadithi hii ni kama ifuatavyo: (( عَلِی مَعَ الحَقِّ وَالحَقُّ مَعَ عَلِی، ولَن یفتَرِقا حَتّى یرِدا عَلَی الحَوضَ یومَ القِیامَةِ ; Ali yuko pamoja na Haq, na Haq iko pamoja na Ali, na viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikia mimi kwenye hodhi la Kauthar)). [74]
- Hadithu Al-Tashbiih (حديث التشبيه): Ni Hadith ambayo Mtume (s.a.w.w) alimlinganisha Ali (a.s) na Mitume wengine. Hadith hii imesimuliwa katika vyanzo vya Shia [75] na Sunni. [76]
- Hadithu La Fataa illa Ali (لا فَتَى إِلّا عَلِی): Hadithi hii ina maana kwamba hakuna mwanamume (muungwana) isipokuwa Ali. Kwa kuzingatia vyanzo vya Hadithi na kihistoria, Hadithi hii inatokana na maneno ya Jibrail kuhusiana na ushujaa wa Imam Ali (a.s.) na kujitolea kwake mhanga katika vita vya Uhud. [77] Hadithi hii imesimuliwa katika vyanzo vya Shia na Sunni.[78]
- Hadithi ya Qasim Al-Annar wa Jannah (حدیث قسیم النار و الجنة): Ni Hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) inayomtambulisha Ali kama ni mgawaji wa pepo na moto. [79] Hadithi hii imepokewa kwa njia tofauti, na wapokezi wengi ndani ya vyanzo mbali mbali vya Kishia [80] na pia vyanzo vya Kisunni. [81]
- Hadithi ya Khasif Al-Na'al (خاصِف النَعل): Ni ibara ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika kuelezea nafasi, hadhi na sifa za Imamu Ali (a.s), ambapo katika mazungumzo yake, alimpa Imam lakabu ya Khasif Al-Na'al (mshona au mkarabati wa viatu) kwa sababu, pale Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akizungumza na washirikina na kuashiria moja ya sifa na nafsi ya Imamu Ali (a.s), wakati huo Imamu Ali (a.s) alikuwa ameshughulika kushona viatu vya Mtume (s.a.w.w). [82]
Pia kuna Riwaya nyingine nyingi zaidi ya hizi zilizopokewa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), kuhusu siza za Imamu Ali (a.s); Miongoni mwazo ni kuhsiana vita vya Khandaq, ambapo imesemwa ya kwamba, "Shambulio la Ali katika vita vya Khandaq ni bora kuliko ibada ya majini na wanadamu." [83] Katika Riwaya nyengine Mtume anasema: "Yeyote atakayemtukana Ali, huyo atakuwa ametutaka sis." [84] Katika ibara nyingine Mtume (s.a.w.w) amesema: "Yeyote yule atakayemuudhi Ali, atakuwa ametuudhi sisi." [45] Kwenye ibara nyingine anasema: "Kwa kumpenda Ali ndiko kunakomtofautisa muumini kutokana na mnafika". [86] Pia Mtume (s.a.w.w) amesema: "Ali anatoka nami na mimi ninatokana na Ali." [87] Ibara nyingine inasema “Kumkumbuka (kumtaja) Ali ni ibada.” [88] Pia kwenye ibara nyingine imesewa kwamba: “Kumtazama Ali ni ibada.” [89]
Pia kupitia Hadithi mbalimbali, bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) amempa Ali bin Abi Talib majina kadhaa yanayotoa tafsiri ya wasifu wake, kama vile: Sadiq Akbar, [90] Farooq Azam [91] na Abu Turab. [92]
Sifa nyingine pambanuzi za Imamu Ali (a.s)
Baadhi ya matukio na sifa pekee kuhusiana naye, ambazo zimehisabiwa kuwa ni sifa pambanuzi zinazompambanua Imam Ali (a.s) na watu wengine ni:
- Ndoa yake na bibi Fatima Zahraa: Moja ya sifa maalum za Imam Ali (a.s), ni ndoa yake na binti ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambayo ilifanyika kwa amri ya Mwenye Ezi Mungu mwenyewe. [93] Ilisemwa ya kwamba lau isingekuwepo Ali (a.s), basi kusingekuwepo mtu mwenye kulingana hadhi na Fatima (a.s) ambaye angeliweza kufunga ndoa naye. [94]
- Mzaliwa wa Al-Kaaba (مولود الكعبة) Mzaliwa wa ndani ya Kaaba: Ibara ya "Mzaliwa wa Al-Kaaba", inaashiria tukio la kuzaliwa Imam Ali (a.s) ndani ya Al-Kaaba, jambo hili linachukuliwa kuwa mojawapo ya sifa zake maalum za Imamu Ali (a.s). [95]
- Lakabu ya "Amirul-Mu'minina (أمير الموًمنين): lenye maana ya kiongozi, wa Waislamu, kwa imani na itikadi ya Mashia, lakabu hii ni lakabu maalumu kwa ajili ya Ali (a.s). Kwa mujibu wa itikadi ya Mashia, jina hili lilitumika kwa mara ya kwanza kabisa wakati wa Mtume kwa ajili ya Ali bin Abi Talib. [96] Sayyid Ibn Taawuus, mwanahadithi wa Kishia wa karne ya 7, katika kitabu Al-Yaqiin cha Al-Yaqiin Bi-ikhtisaasi Maulana Ali Bi-imrati Al-Muuminiin, kwa kutegemea Hadithi 220 kutoka vyanzo vya Sunni, jina Amiru Al-Mu'minin amelizingatia kuwa ni jina makhususi kwa Imam Ali (a.s). [97]
- Kisa cha Saddu Al-Abwaabi (سدّالاَبواب): Maana yake ni kufunga milango, kisa hichi kinahusiana na tukio la amri ya Mtume kunga milango ya nyumba ambazo zlikuwa zimeuzunguka msikiti wa Mtume (s.a.w.w). Nyumba hizo milango yake ilikuwa ikifungukia kuelekea ndani ya msikiti, bwana Mtume (s.a.w.w) akatoa amri kufungwa milango ya nyumba hizo, ila mlango wa nyumba ya Ali bin Abi Talib peke yake (a.s). [98]
- Udugu bina yake na Mtume (s.a.w.w): Mtume (s.a.w.w) alianzisha udugu miongoni mwa wahajiri kabla ya kuhamia Madina. Pia, huko Madina, pia alifanya mafungamano ya udugu baina ya wahajiri na Ansari, na katika nyakati zote mbili, yeye aliweka mafungamano ya udugu baina yake na Imam Ali (a.s) na akamtambua Ali bin Abi Talib kuwa ni nduguye. [99]
- Wa kwanza katika Uislamu: Kwa mujibu wa maoni ya Shia na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni, Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza kumwamini bwana Mtume (s.a.w.w). [100]
- Utangazaji wa Aya za kuchanganuka (آيات برائة): Kwa mujibu wa maelezo ya kitabu cha tafsiri ya Qur'ani cha Tafsire Nemune, ni kwamba; Takriban wafasiri na wanahistoria wote wanakubali ya kwamba pale zilipoteremshwa Aya za kwanza za Surat Tawbah zilizokuja kufuta mkataba wa makubaliano baina ya washirikina na Mtume Muhammad kuchanganuka, Mtume (s.a.w.w) kwanza alimpa Abu Bakar jukumu la kufikisha amri hii, lakini baadae alighairi na akalichukua jukumu hilo kutoka kwa Abu Bakar na kumpa Ali (a.s), na Ali (a.s) akawatangazia watu wakati wa ibada ya Hijja. [101] Tukio hili limesimuliwa katika vyanzo vya Sunni. [102]
- Kisa cha Sadaka ya Pete: Kisa hichi kinatokana na tukio la Imam Ali (a.s) kumpa masikini pete yake huku akiwa amerukuu katika swala. Tukio hili limesimuliwa katika vitabu vya Hadithi za Shia na Sunni.[103]
- Raddu Al-Shamsi (ردّ الشمس) kurudishwa kwa jua: Katika tukio hili, jua lililokuwa linatua lilirudishwa tena kupitia dua ya Mtume (s.a.w.w), ili Ali bin Abi Talib (a.s) aweze kuswali sala yake ya Alasiri. [104] Kulingana na nukuu ya Sheikh Mufid, katika moja ya vita, ndani ya zama za Ali bin Abi Talib, kuliwa na majeshi ambao walipitwa na sala ya Alasiri, ambapo kupitia dua ya Imamu Ali (a.s), jua lilirudi tena nao wakadiriki kusali sala yao ya Alasiri. [105]
Pingamizi juu ya utangazaji wa sifa za Ali (a.s)
Kwa mujibu wa ripoti za kihistoria, katika kipindi cha Bani Umayyah, Mu’awiya aliamuru kuweka pingamizi na vizuizi juu ya uenezaji na utangazaji wa sifa za Imam Ali (a.s). Kwa mujibu wa maelezo ya Ali bin Muhammad Madaa-iniy, mwanahistoria wa karne ya tatu, Mu’awiya aliwaandikia mawakala wake kwamba; Mtu yeyote yule asimuliaye sifa fulani kuhusiana na wasifu wa Imam Ali (a.s), roho yake na mali zake nitakuwa ni halali, yaani ni halali kumuuwa na kutaifisha mali yake. [106]
Pia, ilikuwa ni haramu kunukuu Hadithi zake, kumtaja kwa wema na kuwapa watoto jina la Ali. [107] Mu'awiya alikuwa akimtukana Imam Ali na kusema: "Sitaacha kufanya hivi mpa ifikia hali ya kutopatikana mtu atakayemtaja Ali kwa sifa njema." [108] Kwa amri ya Muawiya, kumtukana Ali kwenye mimbari kukaanza rasmi [109], jambo ambalo liliendelea kwa takriban miaka 60 mpaka wakati wa Omar bin Abdul Aziz. [110] Kwa mujibu wa maelezo ya Allama Hilliy (aliyezaliwa mwaka 648 na kufariki 726 Hijiria) ameandika katika kitabu cha Kashfu Al-Hakika ya kwamba; marafiki wa Imam Ali (a.s) hawakutangaza sifa zake kutokana na khofu, maadui zake hawakuzitangaza kutokana na husuda. Hata hivyo sifa zake zilitanda mashariki na magharibi. [111] Kwa mujibu maelezo ya Muhammad Jawad Mughniyah; Bani Umayya waliwatesa wale wote waliokuwa wakieneza sifa au kunukuu Hadithi kutoka kwa Imam Ali (a.s). Wao pia waliwaua wanafunzi na watu karibu wa Imam Ali (a.s), ambao miongoni mwao ni kama vile: Maitham Tammar, Amru bin Hamiq Khuzai, Rashiid Hijriy, Hujar bin 'Uday, na Kumail bin Ziad. Walifanya hivyo ili kuhakikisha ya kwamba, kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kupata habari au kupokea nukuu za kielimu kutoka kwao. [112]
Pia, kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Muhammad Abu Zuhra, mwanachuoni wa Kisunni, ni kwamba; Serikali ya Bani Umayyah ilikuwa na athari kubwa katika kuficha elimu na mafunzo ya Imamu Ali (a.s), ndio maana kukawa na Hadithi chache kutoka kwake ziliripotiwa katika vyanzo vya Sunni. [113]
Sayyid Ali Shahrashtani katika kitabu cha “Man'u Tahriri Al-Hadithi” ya kwamba: Wengi wa waandishi wa Shia wanaamini kwamba moja ya sababu za kuharamishwa uwandishi wa rikodi za Hadithi, ilikuwa ni kwa ajili ya kuzuia kuenea na kusambaa kwa sifa za Imam Ali (a.s). [114] Hii ni kutokana na kule Hadithi za Mtume (s.a.w.w) kuweka wazi juu hadhi ya Ahlul-Bait (a.s), na nafasi yao katika suala Ukhalifa na uongozi wa juu ya Waislamu, jambo ambalo linakwenda kinyuma na maslahi ya tawaza za Bani Umayyah.[115]
Kuiba sifa za Ali (a.s) na kuzipachika kwa wengine
Kama vile alivyo nukuu Ibnu Abi Al-Hadid mwanatheolojia wa fikra za Mu'tazili wa karne ya 3 Hijiria, kutoka kwa Abu Ja'afar Eskafi ya kwamba; Mu'awiya aliagiza kundi la masahaba na wafuasi wa Masahaba (Mataabi'ina) kuunda Hadith zinazomlaani na kumtuhumu Imam Ali (a.s). [116] Muawiya katika barua aliyowaandikia mawakala wake, aliwataka kuwatafuta wapenzi wa Othmani bin Affan na wafanye urafiki nao, kisha wamrikodie sifa wanazomsifu nazo Othman. [117]
Kwa mujibu wa kauli ya Ali bin Muhammad Madaa-iniy, mwanahistoria wa karne ya tatu Hijiria; katika kipindi hicho watu walinukuu Hadithi chungu nzima za bandia katika kumsifu Othmani kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kidunia na kujipatia. [118] Baada ya hapo, Muawiya aliandika barua nyingine kwa mawakala wake akiwaamrisha mawakala hao wawatake watu kunukuu sifa bandia kwa ajili ya kuwasifu masahaba na Makhalifa watatu, mpaka isiwepo Hadithi hata moja kuhusu sifa za Imamu Ali (a.s), isipokuwa iwe na mbadala wake bandia katika kuwasifu Makhalifa waliotangulia pamoja na masahaba, au kinyume chake, yaani wanukuu Hadhithi ya kumponda inayokabiliana na Hadhithi inayomsifia.Muawia Aliiona kazi hii kama ni chanzo cha kuharibu njia zinazopelekea kueleweka kwa Abu Tarab (Ali) na wafuasi wake. [119]
Kukanusha sifa za Imam Ali (a.s)
Ibn Taimiyyah (aliyezaliwa mwaka 661 na kufariki 728 Hijiria), ambaye ni kiongozi wa Salafiyyah, amezingatia baadhi ya Hadith kuhusianana sifa za Imam Ali (a.s) kuwa ni Hadithi potofu au bandia.[120] Pia mwanafunzi wake, ambaye ni Ismail bin Omar ajulikanaye kwa umaarufu wa Ibn Kathir wa Damashqiy (aliyezaliwa mwaka 774 na kufariki 701 Hijiria) amesema; Haikuteremshwa Aya hata moja kuhussiana na Ali (a.s) peke yake, na Aya zinazotajwa ni kuhusiana na Ali (a.s), si kwamba zimeteremka kuhusiana naye tu, bali kuhuisiana naye pamoja na Masahaba wengine kadhaa. [121] Kwa mujibu wake, Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Ibn Abbas na wengineo kuhusiaana na suala hili, si Hadithi sahihi. [122] Yeye pia ameidhoofisha Milolongo kadhaa ya wapokeza Hadith kuhusiana na sifa za Imam. [123]
Ibn Qayyim Jozi (aliyefariki mwaka 751 Hijiria), ambaye ni mwanafunzi mwingine wa Ibn Tamiyyah, alichukulia tukio la kuutangaza Uimamu wa Ali (a.s) katika Ghadir Khum kuwa ni la uongo; [124] ingawa kwa mujibu wa maelezo ya Allameh Amini, Hadithi inayohusiana na tukio la Ghadir imenukuliwa katika vyanzo vya Shia na Sunni kupitia njia na milolongo tofauti ya wapokezi wa Hadithi (Mutawatir). [125] Pia, Ibnu Jauzi (aliyefariki mwaka 597 Hijiria), ambaye ni mwanachuoni wa Kisunni, katika kitabu cha Al-Maudhuu'at, amenukuu baadhi ya Hadithi zinazohusiana na sifa za Imam Ali (a.s), na akazitumbukiza katika kikapu cha Hadithi za uongo. [126]
Orodha ya vitabu
Kuna vitabu vingi vya Hadith miongoni mwa vitabu sahihi sita vya Kisunni vilivyoandikwa kuhusiana na sifa za Imamu Ali (a.s). [127] Pia, katika vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na sifa na wasifu wa Ahlul-Bait, miongoni mwao kuna vitabu vilivyojikita katika kuzungumzia sifa za Imam Ali (a.s). Wanachuoni wa Shia na Sunni pia wameandika vitabu makhususi vilivyojitenga katika kuzungumzia wasifu na sifa za Imam Ali (a.s). Agha Bozurge Tehrani katika kitabu chake Al-Dhari'a ameviorodhesha na kuvitambulisha vitabu 15 vilivyoandikwa makhususi kuhusiana na sifa za Imamu Ali (a.s) vyenye jina la "Fadhaailu Amirul-Muuminina". [128] Vile vile ameordhesha vitabu kadhaa vyengine vyenye majina mengine ambavyo pia vimeandikwa kuhusiana na sifa za Imam Ali (a.s). Kwa mfano: "Nahju Al-'Adaalah fi dhaili Al-Imami Amiri Al-Mu'minina Ali bin Abi Talib", kiliyoandikwa na Abdu Ali bin Al-Hussein Al-Lubnani Al-Najafiy. [129] na "Misbahu Al-Anwar fi Fadhaili Imami Al-Abrari", kiliyoandikwa na Hashim bin Muhammad. [130]
Vitabu vya Kisunni
- Fadhailu Amirul-Mu’minina, cha Ahmad Ibn Hanbal Shaibani (aliyefariki mwaka 241 Hijiria), ambaye ni mmoja wa viongozi wanne wa madhehebu ya Kisunni. Katika kitabu hichi, kuna Hadithi 369 juu zilizo orodheshwa kuhusiana na sifa za Imam Ali (a.s). [131] Katika kitabu hichi, Ibn Hanbal amesimulia kisa cha Khalifa wa pili akimpongeza Imam Ali (a.s) katika siku ya Ghadir. [132]
- Khasaa-isu Amiril-Mu’minina, ni kitabu cha Ahmad bin Shu'aib Nasa-iy (aliyefariki mwaka wa 303 Hijiria), ambaye ni mwanahadithi na mtunzi wa kitabu cha Sunanu Al-Nasaa-iy, ambacho ni miongoni mwa vitabu sahihi sita vya Hadithi vya Ahlu Al-Sunna. Katika kitabu hichi, ambacho kimeandikwa kwa lugha Kiarabu, ni kitabu kinachozungumzia Uislamu wa Ali (a.s), hadhi na nafasi yake mbele ya Mtume (s.a.w.w), uhusiano wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) pamoja na nafasi ya mkewe na watoto wake.
- Manaqib Al-Imami Ali bin Abi Talib, cha Ibn Maghazili (aliyefariki 483 mwaka Hijiria). Kitabu hichi kimeandikwa kwa lugha Kiarabu na kimetaja sifa kadhaa za Imamu Ali ndani yake, kama vile; Kuzaliwa katika Al-Kaaba, kushika nafasi ya kwanza katika kusilimu, kupanda juu ya mabega ya Mtume (s.a.w.w), pia kimenukuu Hadithi na Aya kadhaa kuhusiana na Imamu Ali (a.s).
Manaqibu Ali bin Abi Talib, cha Ahmad bin Musa bin Murdawieh (aliyefariki mwaka 410 Hijiria), Al-Mi'iyaaru wa Al-Mawazinu fi Fadhail al-Imam Amiri Al-Mu'minina Ali bin Abi Talib (a.s), kilichoandikwa na Muhammad bin Abdullah Eskafi, mwanachuoni wa nadharia za Mu'tazili (aliyefariki mwaka 240 Hijira), Al-Jawhara fi Nasabi Al-Imami Ali wa Aalihi, cha Muhammad bin Abi Bakar Tilmisani, ambaye ni mwanazuoni wa karne ya 7 Hijria, Jawahiru Al-Matalibi fi Manaqibi Al-Imami Ali bin Abi Talib, kilichoandikwa na Shamsu Al-Dini Baauniy (aliyefariki mwaka 871 Hijiria), Kefayatu Al-Matalibi fi Manaqibi Ali bin Abi Talibi, cha Muhammad bin Yusuf Ganji (aliyefariki mwaka 658 Hijiria), Manaqibu Al-Imami Amiri Al-Mu'minina kilichoandikwa na Muwaffaq bin Ahmad Khaarazmiy (aliyefariki mwaka 568 Hijiria ) na Manaqibu Mortazawiy, kiliyoandikwa na Mir Mohammad Saleh Tirmidhiy (aliyefariki mwaka1060 Hijiria). Hivyo basi ni miongoni mwa vitabu vyengine vya wanazuoni wa Kisunni kuhusu sifa za Imam Ali (a.s).
Vitabu vya Shia
- Al-Maratibu fi Fadhaili Amiril-Mu’minina. Kitabu hichi kimeandikwa na Abu Al-Qasim Bustiy, mwanachuoni wa madhehebu ya Zaidiyyah wa karne ya nne ya Hijiria. Kazi hii imeorodhesha ndni yake sifa 450 za Ali bin Abi Talib (a.s).
- Tafdhilu Amiri Al-Mu'minina, cha Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 Hijiria), katika kitabu hichi, akinukuu Hadithi za Shia na Sunni, mwandishi huyu amethibitisha ubora wa Ali (a.s) juu ya mitume wote isipokuwa Mtume wa Muhammad (s.a.w.w). Kazi hii pia imetafsiriwa katika lugha Kiajemi.
- Al-Rissalatu Al-Alawiyyah fi Fadhli Amirul-Mu'minina (a.s) Ali 'Ala Saa-iri Al-Bariyyah Siwaa Sayyidina Rasuulu Allahi (s.a.w.w). Kitabu hichi kiliandikwa kwa lugha ya Kiarabuna Abulfath Karaajki (aliyefariki mwaka 449 Hijiria). Ndani yake mmeorodheshwa sifa ubora wa Ali (a.s) kwa mujibu wa Aya za Qur'ani, pia ndani yake mmna jawabu kuhusiana na ukosowaji wa watiaji dosari na shaka juu ya suala hilo.
- Al-Yaqin Bi-iKhtisasi Maulana Ali Bi-imrati Al-Muuminiina. Mwandishi wa kitabu hichi ni Sayyid Ibn Tawus (aliyefariki mwaka 664 Hijiria). Katika kitabu hichi, akinukuu Hadithi 220 kutoka vyanzo vya Sunni, alilichukulia jina la “Amirul-Muuminina” kuwa ni la kipekee na maalumu kwa ajili ya Ali (a.s), alilopewa na bwana Mtume (s.a.w.w).
Pia vitabu kama vile: Umda 'Uyuni Sihahi Al-Akhbari fi Manaqibi Imami Al-Abrari kinachojulikana kwa jina la "Ummada", ambacho kimeandikwa na Ibn Batreeq (aliyefariki mwaka 600 Hijiria), Mi-atu Manqabati Amiri Al-Muuminina wa A-immati Min Wuldihi (a.s) Min Tariqi Al-Aama, cha Ibn Shaadhaan, Tarafu Mina Al-Anbiyaa-i wa Al-Munaqibi, cha Sayyid Ibnu Tawus, Al-Raudha fi Fadhaa-ili Amiri Al-Muuminina, cha Shaadhan bin Jibra-il Qomi, Kashfu Al-Yaqin Fi Fadhaili Amiril-Mominina, kilichoandikwa na Allamah Halliy na Qadhaa-u Amiril-Mominina cha Muhammad Taqi Shushtari, pia Fadaailu Al-Khamsa Mina Al-Sihahi Al-Sattah, cha Fairuz Abaadiy, ni miongoni mwa kazi zilizoandikwa na wanazuoni wa Kishia kuhusiana na sifa na wasifu wa Imamu Ali (a.s).
Masuala yanayo fungamana
Vyanzo
- Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn. Al-Ghadīr fī al-kitāb wa al-sunna wa al-ʾadab. [n.p]. [n.d].
- Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. [n.p]. [n.d].
- Abū Zahrā, Muḥammad. Al-Imām al-Ṣādiq, ḥayātihi wa ʿaṣrihi wa ārā'ih. [n.p]. Maṭbaʿat Muḥammad ʿAlī Mukhayyam. [n.d].
- Aṣgharpūr, Ḥasan. Darāmadī bar manāqibnigārī-i Ahl Bayt. [n.p]. [n.d].
- Al-Tafsīr al-mansūb ilā al-Imām al-Ḥasan b. ʿAlī al-ʿAskarī. 1st edition. Qom: Madrisat al-Imām al-Mahdī, 1409 AH.
- ʿĀṣimī, Aḥmad b. Muḥammad. Al-ʿAsal al-muṣaffā min tahdhīb zayn al-fatā fī sharḥ sūrat hal atā. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Qom: Majmaʿ Iḥyāʾ al-Thiqāfat al-Islāmiya, 1418 AH.
- ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmiyya, 1380 Sh.
- Baḥrānī, Hāshim b. Sulaymān al-. Al-Burhān fī tafsīr al-Qurʾān. [n.p]. [n.d].
- Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Edited by Muḥammad Zuhayr b. Nāṣir al-Nāṣir. [n.p]. Dār Ṭawq al-Najāt, 1422 AH.
- Bayāḍī, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Ṣirāṭ al-mustaqīm ilā mustaḥaqqay al-taqdīm. Edited by Ramaḍān Mikhāil. Najaf: al-Maktaba al-Ḥaydariyya, 1384 AH.
- Fattāl al-Nayshābūrī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Rawḍat al-wāʿiẓīn wa baṣīrat al-muttaʿzīn. Qom: Intishārāt-i al-Raḍī, 1375 Sh.
- Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
- Ganjī al-Shāfiʿī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Kifāyat al-ṭālib fī manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by Muḥammad Hādī Amīnī. Tehran: Dār Iḥyāʾ al-Turāth Ahl al-Bayt, 1404 AH.
- Ḥibarī, Ḥusayn b. al-Ḥakam al-. Tafsīr al-Ḥibarī. Beirut: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1408 AH.
- Ḥākim al-Nayshābūrī. Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Edited by Musṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1411 AH.
- Ḥaskānī, ʿUbayd Allāh b. ʿAbd Allāh al-.Shawāhid al-tanzīl li-qawāʿid al-tafḍīl. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. Tehran: Sāzmān-i Chāp wa Intishārāt-i Wizārat-i Irshād-i Islāmī, 1411 AH.
- Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Kashf al-murād fī sharḥ tajrīd al-iʿtiqād. Edited by Ḥasan Ḥasanzāda Āmulī. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1413 AH.
- Ḥimawī Shāfiʿyī, Ibrāhīm b. Saʿd al-Dīn. Farāʾid al-samṭayn. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. [n.p]. Muʾassisa al-Maḥmūd, [n.d].
- Ḥimawī Shāfiʿyī, Ibrāhīm b. Saʿd al-Dīn. Farāʾid al-samṭayn. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. 1st edition. Beirut: Muʾassisa al-Maḥmūd, 1398 AH.
- Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balāgha. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Qom: Maktabat Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1404 AH.
- Ibn Baṭrīq, Yaḥya b. Ḥasan. Khaṣāʾiṣ al-waḥy al-mubīn fī manāqib Amīr al-Muʾminīn. Qom: Dār al-Qurʾān al-Karīm, 1417 AH.
- Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Minhāj al-sunna al-nabawīyya fī naqd kalām al-shīʿa al-qadarīyya. Edited by Muḥammad Rashād Sālim. [n.p]. Jāmiʿat al-Imām Muḥammad b. Saʿūd al-Islāmiyya, 1406 AH/1986.
- Ibn Ḥanbal, Aḥmad b. Muḥammad. Faḍaīl Amīr al-Muʾminīn ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by ʿAbd al-ʿAzīz Ṭabaṭabaʾī. Qom: Dār al-Tafsīr, 1433 AH.
- Ibn Ḥanbal, Aḥmad b. Muḥammad. Musnad al-Imām Aḥmad b. Ḥanbal. Edited by Shuʿayb al-Arnaʾūt and ʿĀdil Murshid. Beirut: Al-Risāla, 1421 AH.
- Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Mawḍūʿāt. Edited by ʿAbd al-Raḥmān Muḥammad ʿUthmān. Medina: Al-Maktabat al-Salafiyya, 1386 AH.
- Ibn Shādhān al-Qummī, Muḥammad. Miʾat manqaba min manāqib Amīr al-Muʾminīn. Qom: Madrisat al-Imām al-Mahdī, 1407 AH.
- Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: ʿAllāma, 1379 AH.
- Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
- Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
- Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tarjumat al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib (a) min tārīkh madīnat Dimashq. Edited by Muḥammad Bāqir Maḥmūdī. 2nd edition. Beirut: Muʾassisa-yi Maḥmūdī, 1400 AH.
- Ibn Qayyim al-Jawziyya, Muḥammad ibn Abī Bakr. Al-Manār al-munīf fī al-ṣaḥīḥ wa al-ḍaʿīf. Edited by ʿAbd al-Fattāḥ Abū Ghudda. [n.p]. Maktabat al-Maṭbūʿāt al-Islāmiyya, 1390 AH-1970.
- Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407 AH-1986.
- Ibn Mardawayh, Ahmad b. Mūsā. Manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1424 AH.
- Ibn Maghāzīlī, ʿAlī b. Muḥammad. Manāqib ʿAlī b. Abī Ṭālib. 3rd edition. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1424 AH.
- Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Mūkhtasar tārīkh Dimashq li-Ibn ʿAsākir. Edited by Ruḥiyat al-Nuḥas and Riyādh ʿAbd al-Ḥamīd Murād and Muḥammad Muṭīʿ. Damascus: Dār al-Fikr li-Ṭabʿat wa al-Tawzīʿ wa al-Nashr, 1402 AH-1989.
- Istarābādī, Muḥammad Jaʿfar. Al-Barāhīn al-qāṭiʿa fī sharḥ tajrīd al-ʿaqāʾid al-sāṭiʿa. Edited by Markaz Muṭāliʿat wa Taḥqīqāt-i Islāmī. Qom: Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1382 Sh.
- Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Edited by Bashār ʿAwād Maʿrūf. Beirut: Dār al-Gharb al-Isālmī, 1422 AH-2002.
- Khwārizmī, Muwaffaq b. Aḥmad al-. Al-Manāqib. Edited by Mālik Mahmūdī. 2nd edition. Qom: Muʾassisa al-Nashr al-Isālmī, 1411 AH.
- Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhundī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
- Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Al-Ḥusayn wa baṭalat Karbalā. Edited by Sāmī ʿAzīzī. Qom: Dār al-Kitāb al-Islāmī, 1426 AH.
- Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Kitāb al-amālī. Edited by Ḥusayn Ustād Walī and ʿAlī Akbar Ghaffārī. 1st edition. Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
- Muslim Nayshābūrī. Ṣaḥīḥ Muslim. Edited by Muḥammad fuʾād ʿAbd al-Bāqī . Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
- Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Dānishnāma-yi Amīr al-Muʾminīn (a). [n.p]. [n.d].
- Nasā'ī, Aḥmad b. Shuʿayb. Sunan al-kubrā. Edited by Ḥasan b. ʿAbd al-Munʿim ʿAlī Khurāsānī. Beirut: Muʾassisat al-Risāla, 1421 AH-2001.
- Nasā'ī, Aḥmad b. Shuʿayb. Khaṣāʾiṣ Amīr al-Muʾminīn ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by Aḥmad Mīrīn Balūshī. Kuwait: Maktabat al-Muʿllā, 1406 AH.
- Nuʿmānī, Muḥammad b. Ibrāhīm al-. Kitāb al-Ghayba. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Nashr-i Ṣadūq, 1397 Sh.
- Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Ṭayyib Mūsawī Jazāʾrī. Qom: Dār al-Kitāb, 1404 AH.
- Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm. Yanābīʿ al-mawadat li-dhi l-qurbā. Qom: Uswa, 1422 AH.
- Rahīmī Iṣfahānī, Ghulām Ḥusayn. Wilāyat wa rahbarī. [n.p]. [n.d].
- Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Qom: Maktabaṭ Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
- Shablanjī, Muʾmin b. Ḥasan. Nūr al-abṣār fī manāqib Āl Bayt al-Nabī al-mukhtār. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, [n.d].
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Amālī. Tehran: Kitābchī, 1376 Sh.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. 1st edition. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Kamāl al-dīn wa itmām al-niʿma. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. 2nd edition. Tehran: Islāmiyya, 1395 AH.
- Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣā'ir al-darajāt fī faḍāʾil-i Āl-i Muḥammad. Edited by Muḥsin Kūchabāghī. 2nd edition. Qom: Kitābkhāna-yi Āyatullāh al-Marʿashī, 1404 AH.
- Taqaddumī Maʿṣūmī, َAmīr. Nūr al-amir fī tathbīt khuṭbat al-ghadīr. [n.p]. [n.d].
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Muḥammad Jawād Balāghī. 3rd edition. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
- Ṭabarī Āmulī, ʿImād al-Dīn al-. Bishārat al-Muṣṭafā li Shīʿat al-Murtaḍā. 2nd edition. Najaf: al-Maktaba al-Ḥaydarīyya, 1387 AH.
- Ṭabarī, Aḥmad b. ʿAbd Allāh. Dhakhāʾir al-ʿuqbā fī manāqib dhawi al-qurbā. Cairo: Maktabat al-Qudsī, 1354 AH.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Al-Mustarshid fī Imāmat ʿAlī b. Abī Ṭālib. Edited by Aḥmad Maḥmūdī. Qom: Kūshānpūr, 1415 AH.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. 2nd edition. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
- Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by Muʾassisa al-Biʿtha. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
- Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Tafsīr al-kashshāf. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿArabī, 1407 AH.