Imamu Hassan Mujtaba (a.s)

Kutoka wikishia
Imam Hassan bin Ali bin Abi Talib(a.s), Imam wa pili wa wafuasi wa ahlul-bayt(a.s)

Hassan bin Ali bin Abi Talib (a.s) maarufu Imamu Hassan Mujtaba, aliyezaliwa (mwaka wa 3 Hijiria na kufariki mwaka wa 50 Hijiria), ni Imamu wa pili wa Kishia. Imamu ambaye alishika nasafi ya Uimamu kwa kipindi cha miaka 10. Aliwaongoza Waislamu baada ya kukubaliwa na kupata muwafaka wa kiapo cha utiifu kutoa kwao. Baada ya kiapo hicho, yeye alishika nafasi ya Ukhalifa kwa muda wa miezi 7. Muhula wa Uimamu wa Imamu Hassan Al-Mujtaba (a.s) ulianzia (mwaka wa 40 - hadi mwaka wa 50 Hijiria).

Hassan bin Ali ni mtoto wa kwanza wa Imamu Ali na bibi Fatima Zahraa (a.s), na ni mjukuu wa kwanza wa bwana Mtume (s.a.w.w). Kulingana na nukuu za kihistoria, jina hili la Hassan alichaguliwa na bwana Mtume (s.a.w.w), naye alikuwa akimpenda sana mjukuu wake huyu. Yeye aliishi pamoja na Mtume (s.a.w.w) kwa muda wa miaka saba. Yeye pia alishirika katika tukio la Baiatu Al-Ridhwaan na tukio la Mubahala baina ya Mtume na kizazi chake (a.s) na Wakiristo wa mji wa Najraan.

Sifa za Imamu Hassan (a.s)

Vyanzo vya kisunni na Kishia vyote kwa pamoja vimemtambua yeye kuwa ni miongoni mwa Ahlul Al-Kisaa (Watu Waliofinikwa Shuka na Mtume (s.a.w.w). Watu waliofinikwa shuka ndio watu walioshukiwa na Ayatu Al-Tathiir (Aya ya Utoharishaji). Kwa mujibu wa maoni ya wafuasi wa madhehebu ya Kishia, watu hawa ndio watu aliotoharishwa na kulindwa kutokana na maasi au kutenda dhambi. Imamu Hassan (a.s), mara mbili alitoa mali yake yote kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu, na mara tatu alitoa nusu ya mali yake kwenye njia hiyo, ambapo alitoa nusu ya mali yake hiyo kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza kujikimu kimaisha. Yasemwa kwamba, yeye alipewa jina la Karimu Ahlul-Bait kutokana na utowaji wake huo wa mali yake kwa ajili ya ridhaa za Mola wake. Yakadiriwa kwamba, mara 20 hadi 25 yeye alikwenda kutekeleza ibada ya hija kwa miguu.

Hakuna habari yoyote ile muhimu kuhusiana na maisha yake katika kipidi chote kile cha Ukhalifa wa Khalifa wa kwanza (Abu Bakar). Katika zama za khalifa wa pili (Omar), kupitia amri ya khalifa huyo, yeye alihudhuria kwenye shura ya watu sita (kikao cha majadiliano), akiwa ni kama shahidi katika tukio la kumteua Khalifa wa tatu (Othaman). Pia kuna nukuu kadhaa linazozungumzia namna ya yeye alivyoshiriki katika baadhi ya vita, ndani ya kipindi cha Ukhalifa wa Khalifa wa tatu. Katika Kipindi cha Ukhalifa wa Othman, Imamu Mujtaba (a.s) alitumwa na baba yake (Ali bin Abi Talib) katika vuguvugu na msongamano dhidi ya khalifa huyo wa tatu, tukio ambalo lilitokea mwisho cha maisha ya khalifa huyo. Amri hiyo iliyotoka kwa Imamu Ali (a.s), ilimtaka Imamu Hassan (a.s) aende kuilinda nyumba ya Othmani bin ‘Affaan, kutokana na machafuko ya kisiasa dhidi yake. Katika kipindi cha utawala wa Imamu Ali (a.s) yeye alifungamana naye kuelekea mji wa Kufa na kushiki pamoja naye katika vita vya Siffiin na Nahrewan, akiwa ni mmoja wa majemedari wa kijeshi ndani ya vita hivyo.

Hassan bin Ali alishika nafasi ya Uimamu tarehe 21 Ramadhani ya mwaka wa 40 Hijiria, baada ya kuuawa shahidi Imamu Ali (a.s). Siku hiyo hiyo, zaidi ya watu elfu arobaini walikula kiapo cha utiifu juu ya Ukhalifa wake. Kwa upande wa pili, Mu'awiyah hakukubaliana na Ukhalifa wake, hivyo basi aliliongoza jeshi lake kutoka Syria na kuelekea Iraq. Imamu Mujtaba (a.s) aliliamuru jeshi lake kukabiliana na Muawiyah chini ya uongozi wa ‘Ubaidullah bin Abbas, huku yeye mwenyewe akielekea Sabat pamoja na kundi jingine. Mu’awiyah alijaribu kutengeneza mazingira ya kusimamisha amani kwa kueneza aina tofauti za uvumi na fitina miongoni mwa askari wa Imamu Hassan (a.s). Katika hali hii, mmoja wa Makhawarij alikusudia kumuuwa Imamu Hassan (a.s), ila katika tukio hilo, Imamu Hassan (a.s) hakuuwawa, ila alijeruhiwa na kuhamishiwa Mada'in kwa ajili ya matibabu. Wakati huo huo, kundi la viongozi wa Kufa lilimwandikia barua Mu'awiyah na kumuahidi kumsalimisha Hasan bin Ali kwake yeye, au kumuua kabisa. Mu’awiyah naye akaituma barua hiyo kwa Hassan bin Ali (a.s) na kumuahidi kumpa amani. Imamu Mujtaba (a.s) alikubaliana na amani hiyo na kumkabidhi Mu'awiyah hatamu za Ukhalifa kwa sharti kwamba; Mu'awiyah aiongoze jamii kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume (s.a.w.w), na asimteue mrithi kwa ajili yake wa kuja kushika ukhalifa baada yake yeye. Pia Alimtaka awape amani watu wote, wakiwemo Mashia (wafuasi) wa Ali(a.s). Baadae Mu'awiyah hakutimiza hata moja miongoni mwa masharti hayo. Mkataba wa amani na Mu'awiyah ulisababisha kutoridhika kwa idaid kubwa ya wafuasi wa Imamu Hassan (a.s), na hata wengine miongoni mwao wakamwita "Mudhillu Al-Mu'minina" (mdhalilishaji wa waumini).

Baada ya tukio hilo la mkataba wa amani la mwaka wa 41 Hijiria, Imamu Hassan (a.s) alirejea Madina na akabaki huko hadi mwisho wa maisha yake. Yeye akiwa Madina alishika nafasi uongozi wa kielimu, na kulingana na baadhi ya nukuu za kihistoria, yeye alikuwa na nafasi na heshima maalumu katika jamii ya wakati huo.

Pale Mu’awiyah alipotia nia ya kumteuwa mwanawe kama ni mshika nafasi ya Ukhalifa baada yake, alitayarisha kiwango cha dirhamu laki moja akamtumia mke wa Imamu Hassan (a.s) aliyejulikana kwa jina (Ja’adah), ili amtilie sumu na kumuuwa. Wanahistoria wanasema ya kwamba; Imamu Hassan (a.s) aliishi kwa muda wa siku 40 baada ya kutiliwa sumu hio. Kulingana na baaddhi ya nukuu ni kwamba; Yeye aliusia azikwe pembeni mwa kaburi la Mtume (s.a.w.w), ila Marwan bin Al-Hakam akiambatana na baadhi ya ukoo wa Bani Ummayyah walizuia utekelezaji wa wosia huo. Hivyo basi Imamu Hassan (a.s) akazikwa katika mava ya Baqi’i mjini Madina.

Kuna jumla ya idadi kadhaa za maandiko ya Imamu Hassan (a.s) yaliyonukuliwa kutoka kwake, na kuna kiasi cha watu 132 walionukuu Hadithi kutoka kwake (a.s). Hadithi na riwaya hizo hatimae zilikusanywa katika kitabu kijulikanacho kwa jina la Musnadu Imamu Al-Mujtaba (a.s).

Mukhtasari wa Utambuzi

Hassan bin Ali bin Abi Talib, ni mtoto wa kwanza kabisa wa Imamu Ali na bibi Fatimah Zahraa (a.s) na ni mjukuu wa kwanza wa bwana Mtume (s.a.w.w) [1]. Nasabu yake inaishia kwa Bani Hashim na Qureish. [2]

Jina Kuniya na Lakabu za Imamu Hassan (a.s)

Neno na jina (Hassan) lina maana ya kitu kizuri, jina hili kachaguliwa na bwana Mtume (s.a.w.w). [3] Kuna riwaya isemayo kuwa; Mwenye Ezi Mungu ndiye aliyemchagulia jina hilo. [4] Jina Hassan na Hussein ni mbadala wa jina Shabbar na Shabiir au (Shabbiirun). [5] Nayo ni majina ya watoto wa Nabi Haarun (a.s) [6]. Kabla ya kuzaliwa kwa Hassan na Hussein (a.s), Majina ya Hassan na Hussein hayakuwepo na wala hayakuwa mashuhuri ndani ya jamii ya Waarabu.[7]

Imeelezwa ya kwamba kuniya zake ni (Abu Muhammad) na (Abu Qasim). [8] Pia kuna lakabu kadhaa zilizonasibishwa naye, nazo ni kama vile; Mujtaba (Aliyeteuliwa), Sayyied (Bwana) na kuniya ya Zakiyyun yenye maana ya (Msafi). [9] Lakabu za Imamu Hassan ni sawa na lakabu za Imamu Hussein (a.s), miongoni mwazo ni; (Sayyidu Shababu Ahlul Al-Jannah) na (Raihanatu Al-Nabiyyi). [10] na (Sibtun) [11]. Katika moja kati ya riwaya za Mtume (s.a.w.w) imeelezwa kwamba; (Hassan ni mmoja wa Asbati). [12] Neno (Asbati) kulingana na baadhi ya riwaya na Aya za Qur’an, lina maana ya Imamu na mrithi wa ukhalifa aliyechaguliwa na Mwenye Ezi Mungu anayetokana na kizazi cha Mitume. [13]

Uimamu

Hassan bin Ali ni Imamu wa pili wa Mashia. Yeye alikamata nafasi ya Uimamu na kushika wadhifa huo kwa muda wa miaka 10. Baada ya Imamu Ali (a.s) kuuawa shahidi, tukio ambalo lilitokea mnamo tarehe 21 Ramadhani ya mwaka wa 40 Hijiria. [14] Sheikh Kuleini (aliyefariki mnamo mwaka 329 Hijiri), amekusanya Hadithi kadhaa katika kitabu chake kiitwacho Al-Kafi kuhusiana na namna ya Imamu Hasssan alivyoshika nafasi ya Ukhalifa. [15] Kwa mujibu wa moja ya Hadithi hizo ni kwamba; Imamu Ali (a.s) kabla ya kifo chake cha kishahidi na mbele ya watoto wake na wakuu wa Kishia, alitoa kitabu na silaha (kutoka kwenye amana za Uimamu) na kumkabidhi mtoto wake. Baada ya kufanya hivyo, alisema na kuwambia ya kwamba; Mtume (s.a.w.w) alimuamuru amteue Hassan kuwa mrithi wa nafasi yake baada yake. [16] Kwa mujibu wa Hadithi nyingine, Imamu Ali (a.s) alipoondoka na kuelekea mji wa Kufa, alizikabidhi baadhi ya amana za Uimamu kwa Ummu Salama, kisha Imamu Hassan (a.s) akazichukua kutoka kwake baada ya Kurejea kutoka mji wa Kufa. [17] Sheikh Mufid (aliyefariki 413 Hijiria) pia katika kitabu chake Al-Irshaad anasema kwamba; Hassan (a.s) alikuwa mrithi halisi wa baba yake miongoni mwa watoto wake na masahaba zake. [18] [19] Kwa upande mwengine, pia ile Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inayozungumzia Makhalifa 12, [20] imetumika kama ni dalili ya Uimamu wake (a.s). [21] Katika kipindi cha miezi michache ya mwanzo ya Uimamu wake, Imamu Hassan (a.s) alikuwa ni mkaazi wa mji wa Kufa huku akishikilia nafasi hiyo ya ukhalifa.

Maisha ya utotoni

Kulingana na kauli iliyo mashuhuri zaidi [22] ni kwamba; Imamu Hassan (A.S) alizaliwa mwezi 15 Ramadhani mnamo mwaka wa 3 Hijiria. Ila maoni ya Sheikh Kulaini pamoja na Sheikh Tusi, ni kwamba; Yeye alizaliwa mwaka wa pili Hijiria. [23] Imamu huyo alizaliwa katika mji wa Madina [24], na Mtume (s.a.w.w) mwenyewe ndiye aliyemsomea adhana sikioni mwake. [25] Baada ya siku 7 za tokeo hilo la kuzaliwa kwake, Mtume (s.a.w.w) alimchinjia kondoo kwa ajili ya akiki yake. [26]

Kulingana na vielelezo kadhaa kutoka kwa upande wa Kisunni, kabla ya Mtume (s.a.w.w) kumchagulia jina la Hassan, Ali (a.s) ima alikuwa amemchagulia jina la Hamza [27] au Harbu [28], ila baada ya Mtume (s.a.w.w) kumuuliza jina lake, alimjibu kwa kusema; “mimi sina haki ya kumtangulia Mtume wa Mungu katika hilo”, hapo basi ndipo Mtume alipompa jana la Hassan. [29] Baqiri Al-Sharif ambaye ni Mtafiti wa Kishia, ametoa dalili kadhaa kupingana na kauli hiyo. [30]

Mila za Gorgiian

Mila za Gorgiian ni mila za kale mno za wakazi wa Kusini mwa Iran. Mila hizo huchukua nafasi yake kila mwaka mnamo mwezi 15 Ramadhani, sambamba na tarehe ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s). [31] Yasemekana kwamba mila hizi zilirithiwa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Mila hizo zinahusishwa moja kwa moja na tukio la furaha ya Mtume (s.a.w.w), kutokana na kuzaliwa kwa mjukuu wake, ambapo watu wa zama hizo wanamiminika kwa Imam Ali (a.s) na bibi Fatimah (a.s), kwa ajili ya kuwapa hongera na mkono wa baraka kutokana na tukio hilo jema. Na baada ya hapo jambo hilo likageuka kuwa ndio mila na desturi ya kila mwaka miongoni mwa Waislamu. [32]

Maisha ya utotoni mwake

Hakuna ripoti muhimu zilizoripotiwa kuhusiana na maisha ya uotoni mwa Imamu Hassan Mujtaba (a.s). [33] Imamu Hassan Mujtaba (a.s) hakuishi kipindi kirefu na bwana Mtume (s.a.w.w), ni chini ya kipindi cha miaka 8 tu ndicho alichoishi pamoja naye (s.a.w.w). Hiyo ndiyo sababu hasa iliyopelekea jina lake liorodheshwe na kuwekwa kwenye tabaka la mwisho la ya majina Masahaba walioishi pamoja na Mtume (s.a.w.w). [34] Kuna nukuu kadhaa lilizopokewa kutoka pande zote mbili za Kisunni na Kishia kuhusu mapenzi ya dhati ya Mtume (s.a.w.w) juu yake pamoja na nduguye Hussein (a.s). [35]

Miongoni mwa matukio muhimu yanayohusiana na kipindi alichoishi pamoja na bwana Mtume (s.a.w.w), ni kuhudhuria kwake pamoja na baba, mama na kaka yake, katika tukio muhimu la Mubahala baina ya Mtume (s.a.w.w) na Wakiristo wa mji wa Najrani. Yeye na kaka yake walikuwa ndiyo nembo ya na tafsiri halisi ya neno «أَبْنَاءَنَا» lililoko kwenye Aya ya Mubahala (Aya ya 61 ya Suratu Al-Imran). [36] Kwa mujibu wa kauli ya Sayyid Ja’afar Murtadha, Imamu Hassan pia alikuwepo katika tukio la Bai’atu Al-Ridhwan naye pia alikuwa ni miongoni mwa Masahaba waliokula kiapo cha utiifu kwa Mtume (s.a.w.w). [37] Kuna Aya za Qur’an zilizomshukia yeye akiwa ni mmoja wa wa Ahlul Kisaa (Watu Waligubikwa Shuka). [38] [39] Imesemwa ya kwamba; Yeye alikuwa akihudhuria vikao vya elimu vya Mtume tokea akiwa na umri wa miaka 7, na alikuwa akimsimulia mama yake kila kilichokuwa kikimshukia bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na Wahyi. [40]

Imepokewa kutoka kwa Suleim bin Qaisi (aliyefariki mwishoni mwa karne ya kwanza Hijiria) akisema; “Baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), ambapo Abu Bakar alichukuwa nafasi ya Ukhalifa, katika kipindi hicho Hassan bin Ali akishirikiana na baba yake, mama yake pamoja na kaka yake (a.s), walikuwa wakitoka usiku na kuwafuata Maansari majumbani mwao, wakiwataka wamuunge mkono Imamu Ali (a.s). [41] Pia imesemwa ya kwamba; Imamu Hassan (a.s) hakuridhika kumuona Abu Bakar akipanda juu ya jukwaa la Mtume (s.a.w.w). [42]

Maisha ya Ujanani

Kuna ripoti chache tu zilizorikodiwa kuhusiana na maisha ya ujana wa Imamu Hassan (a.s). Miongoni mwa ripoti chache hizo, ni ropoti iliyonukuliwa katika kitabu “Al- Imaamatu wa Al-Siasah” cha Ibnu Kutaibah, kilichoripoti ya kwamba; Kupitia amri na matakwa ya Khalifa wa pili, Imamu Hassan bin Ali (a.s) alihudhuria katika timu ya kikao cha watu sita cha kumteuwa Khalifa wa tatu, yeye alihudhuria kikaoni humo akiwa ni kama shahidi katika tukio hilio. [43]

Imeelezwa katika baadhi ya vyanzo vya Kisunni kwamba; Hasanain (Hassan na HUssein) walishiriki katika vita vya Afriiqiyah, vya mwaka wa 26 Hijiria, [44] na vita vya Tabaristan vya mwaka wa 29 au 30 Hijiria [45]. Ila kuna wanaoziunga mkono riwaya hizo, na pia kuna wanaopingana nazo. Jafar Morteza Aamuli, amezihisabu riwaya hizo kuwa ni za kutunga na zisizo na mashiko imara. Ametoa mtazamo huo kutokana na mikinzano na pingamizi kadhaa zilizomo katika mapokezi yake. Jambo jengine lililomfanya asikubalianae na riwaya hizo, kunatokana na kukinzana kwa riwaya hizo na mifumo ya uenezaji na utangazaji wa dini wa Maimamu (a.s). Kule Imamu Ali (a.s) kutowaruhusu Hasanaini kuingia kwenye uwanja wa vita vya Siffin ni moja ya uthibitisho unaotilia mkazo na kuthibitisha jambo hilo [46]. Wilfred Madelong anaamini ya kwamba; Imamu Ali (a.s) pengine alitaka kumpa Hassan uzoefu kwenye masuala ya vita akiwa bado ni kijana umri mdogo ili aongeze uzoefu wake huo wa vita. [47]

Miongoni mwa ripoti nyengine zinazohusiana na kipindi hichi ni kwamba; Kila pale watu walipomlalamikia Ali (a.s) juu ya matatizo ya Othman, yeye alimtuma mwanawe Hassan nyumbani kwa Othman kwa ajili ya kutatua matatizo hayo au kwa ajili ya sababu nyingine kadhaa. [48] Kulingana na nukuu kutoka kwa Biladhiriy ni kwamba; "Katika vuguvugu na maandamano dhidi ya uongozi wa Othmani, yaliyotokea mwishoni mwa kipindi cha maisha na Ukhalifa wake, nyumba yake ilizungukwa na waasi na akafungiwa njia ya kupata maji na hatimae kuuwawa. Katika hali kama hiyo, Imamu Hassan akiwa pamoja na nduguye Hussein, wakishirikiana na baadhi ya watu kadhaa, walikwenda kulinda nyumba ya Othmani kupitia amri ya baba yao Imamu Ali (a.s)". [49] Kulingana na kauli ya Kadhi Nuumani Al-Maghribiy, mwandishi wa kitabu Dalaa-ilu Al-Imaamah (aliyefariki mwaka 363 Hijiria) ni kwamba; "Baada ya waasi kumfungia maji Othman, Imamu Mujtaba (a.s) alipeleka maji nyumbani kwa Othman kupitia amri ya baba yake (a.s)". [50] Pia kuna ripoti zesemazo kwamba; Imamu Hassan Mujtaba (a.s) alijeruhiwa katika tukio hilo la kupeleka maji na chakula nyumbani kwa Othmani. [51] Ila baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Shia, kama vile Allaamah Amiiniy, hawakulitilia maanani tamko hilo. Allaamah Amiiniy anaamini kuwa, tamko hilo ni tamko la kutungwa tu na halina ukweli wowote ule ndani yake. 52 Sayyied Murtadha, baada ya kutilia shaka kwamba; Amirul-Mu'minin (a.s) alimtuma Hasnain (a.s) kumtetea Othman, alisema kwamba; "sababu ya kitendo hiki ni kuzuia kuuawa kwa Khalifa huyo kwa makusudi, yaani kama asingemtetea, basi angelikuwa kama vile Imamu Ali (a.s) pia ameshiriki katika mauwaji hayo kwa makusudi. Ama kuhusiana na kumtuma Hassan awapelekee chakula na maji, alikuwa na nia ya kuipelekea maji na chakula familia ya Othmani, na si kumpelekea Othmani mwenyewe. Na sio kwamba alifanya hivyo kumzuia asiondolewe katika Ukhalifa wake, kwa sababu -kiuhalisia Othmani- alistahiki kuondolewa katika Ukhalifa huo kutokana na makosa yake. [53]

Wake na watoto wa Immu Hassan (a.s)

Makala ya asili: Wake wa Imam Hassan (a.s)

Kuna vielelezo tofauti kuhusiana na idadi ya wake na watoto wa Imamu Hassan (a.s). Ingawaje kuna vyanzo vingi vya kihistoria vilivyotaja kwa majina idadi ya wanake 18 ambo ni wake wa Imamu Hassan (a.s), [54] huku vikiashiria kuwepo kwa idadi ya wake 250, [55] au 200, [56] 90, [57] na 70. [58] Ila kuna vyanzo vyengine vinavyodai kuwa, Imamu Hassan (a.s) alikuwa ni mwingi wa kuowa na kuacha, na kumpachika jina la (Tallaaq) lenye maana ya mfanya israfu katika kuowa na kuacha. [59] Zaidi ya hayo pia kuna waliosema kwamba, Imamu Hassan alikuwa na Masuria kadhaa na aliwahi kazaa nao. [60]

Suala la Imamu Hassan kuwa ni mfanya israfu katika kuowa na kuacha limejadiliwa na kuchakatuliwa kihistoria pia kutenguliwa na vyanzo tofauti vya zamani na vya zama hivi sasa. [61] Kwa mujibu wa mtazamo wa Madelong; Mtu wa kwanza aliyeeneza uvumi usemao kwamba, Imamu Hassan (a.s) alikuwa na wake 90 alikuwa "Muhammad Bin Kalbi" na "Madaaini" (aliyefariki mwaka wa 225 Hijiria) ndiye aliyetengeneza na kuzua idadi hii. Wakati huo huo, Kalbi mwenyewe aliwataja wanawake kumi na moja tu kuwa ni wake wa Imamu Hassan (a.s), ambapo watano kati yao wanashukiwa, na hakuna uhakika kuhusu kuolewa kwao na Imamu Hassan (a.s). [62] Qureishiy amezihisabu khabari hizi kuwa ni miongoni mwa khabari zilizotungwa na viongozi wa ukoo wa Bani Abbas, ili kukabiliana na kizazi cha Imamu Hassan (a.s). [63] Pia kuna khitilafu katika idadi ya watoto wa Imam Mujtaba (a.s). Sheikh Mufid alitaja idadi yao kuwa ni watoto 15. [64] Kwa maoni ya Tabarsi Imam Hasan (a.s) alikuwa na watoto 16, pia akamhesabu Abu Bakr ambaye aliuawa kishahidi katika tukio la Ashura kuwa ni mmoja wa watoto wake. [65]

Kizazi cha Imam Hassan

Makala asili: Saadaati Hassaniy

Kizazi cha Imam Hasan (a.s) kiliendelea kutoka kwa Hassan Muthanna, Zayd, Umar na Hussein Athram. Kizazi cha Hussein na Omar kilitoweka baada ya muda, na kizazi cha Hassan Muthanna na Zaid bin Hassan ndivyo vilichobakia. [66] Watoto wake wanaitwa Saadaati Hassaniy. [67] Wengi wao walikuwa na harakati za kijamii na kisiasa katika historia yao yote, na mnamo karne ya pili Na tatu, walisimama dhidi ya serikali ya Bani Abbas na kuanzisha serikali katika sehemu mbalimbali za nchi za Kiislamu. Nasaba hii ya Saadaat inajulikana kwa jina la Shurafaa (Masharifu) katika baadhi ya maeneo kama vile Morocco. [68]

Maisha mjini Kufa, ndani ya Ukhalifa wa Imam Ali (a.s)

Wakati wa ukhalifa wa miaka mitano wa Amirul-Mu’minin (a.s), Imam Mojtaba (a.s) alikuwa yupo pamoja na baba yake katika harakatika zote za kidini na kisiasa. [69] Kwa mujibu wa kitabu Al-Ikhtasas baada ya watu kutoa ahadi na kiapo cha utiifu kwa Imam Ali, Hassan bin Ali (a.s), alikwenda kwenye mimbari kwa ombi la baba yake na akawahutubia watu. [70] Kulingana na ripoti ya tukio la vita vya Sifiin, yaonekana kwamba, Imamu Hassan alikuwa pamoja na Imamu Ali (a.s) huko mjini Kufa, tokea mwanzoni mwa tukio hilo, ambapo Imamu Ali aliwasili huko na kuweka kambi yake mjini humo (a.s). [71]

Maisha ya mjini Kufa, ndani ya Ukhalifa wa Imam Ali (a.s)

Wakati wa ukhalifa wa miaka mitano wa Amirul-Mu’minin (a.s), Imam Mujtaba (a.s) alikuwa yupo pamoja na baba yake katika harakatika zote za kidini na kisiasa. [69] Kwa mujibu wa kitabu Al-Ikhtasas baada ya watu kutoa ahadi na kiapo cha utiifu kwa Imam Ali, Hassan bin Ali (a.s), alikwenda kwenye mimbari kwa ombi la baba yake na akawahutubia watu. [70] Kulingana na ripoti ya tukio la vita vya Sifiin, yaonekana kwamba, Imamu Hassan alikuwa pamoja na Imamu Ali (a.s) huko mjini Kufa, tokea mwanzoni mwa tukio hilo, ambapo Imamu Ali aliwasili huko na kuweka kambi yake mjini humo (a.s). [71]

Katika vita vya Jamali

Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, imeelezwa ya kwamba; Baada ya waasi wa Naakithiin na harakati za Imam Ali (a.s) na askari wake kukabiliana nao, Hassan bin Ali alimuomba baba yake wakiwa njiani na kumtaka aepukane na vita hivyo. [72] Wakati huo Imam Hassan (a.s) alipewa amri na baba yake yeye pamoja na Ammar bin Yasir na Qais bin Saad, kuwakusanya watu wa Kufa na kuwataka kujiunga na jeshi la Imam Ali (a.s). [73] Yeye akawahutubia watu wa mji wa Kufa na kuwasomea sifa za Imamu Ali (a.s) na kuwapa habari za wakivunja makubaliano kwa Talha na Zubeir, katika hotuba hiyo aliwaita watu hao kumsaidia Imam Ali (a.s) katika mapambano yake. [74]

Katika Vita vya Jamal, wakati Abdullah bin Zubeir alipomtuhumu Imamu Ali (a.s) kumuua Othman, Hassan bin Ali (a.s) alitoa khutba na akabainisha wazi nafasi ya Zubeir na Talha katika kumuua Othman. [75] Imam Mujtabi (a.s) katika vita hivyo alikuwa ni amiri wa upande wa mkono wa kulia wa vita hivyo. [76] Ibn Shahr Ashub amesimulia kwamba Imam Ali (a.s) alimkabidhi mkuki wake Muhammad Hanafiyyah katika vita hivyo, na akamtaka amuue ngamia wa Aisha, Ila Muhammad bin Hanafiyyah alifeli na hakuweza kukamilisha jambo hilo. Hapo basi Hassan bin Ali Akauchukua mkuki huyo na akaweza kumjeruhi ngamia ngamia huyo. [77] Imepokewa ya kwamba, baada ya Vita vya Jamal, Imam Ali (a.s) aliugua na kumwachia mwanawe Hasan kuswalisha swala ya Ijumaa mjini Basra. Katika khutba yake ya ya swala hiyo, alisisitiza msimamo wa Ahlul-Bayt na hatima mbaya ya kutoshikamana na kizazi cha bwana Mtume (s.a.w.w). [78]

Vita vya Siffin

Katika Vita vya Siffin, Imamu Ali (a.s) alipopata taarifa ya kwamba Imamu Hassan (a.s) ameingia katika uwanjani wa vita, alisema:


Nichungieni kijana huyu (ili asiingie katika vita) asivunje uti wa mgongo wangu. Hakika nasikitika na kuhofia vijana hawa wawili (Hassan na Hussein) kufikwa na umauti au kuuawa kwao ni kukatika kwa kizazi cha Mtume (s.a.w.w).

Nahjul Balaghah, Tafsiri ya Shahidiy, uk. 240

Kwa mujibu maoni ya Nasr bin Muzaahim (aliyefariki mwaka wa 212 Hijiria), Hassan bin Ali alitoa khutba kabla ya jeshi la Imam Ali (a.s) kuondoka na kuelekea Siffin, na akawahimiza na kuwatia watu motisha wa kufanya jihadi. [79] Kulingana na baadhi ya vyanzo vya historia, yeye katika vita hivyo vya Siffin alishirikiana na kaka yake Hussein bin Ali (a.s) wakiwa ni kama maamiri jeshi wa upnde wa kuliani mwa vita hivyo. [80] Katika ripoti iliyoripotiwa na Askafi (aliyefarika mwaka 240 Hijiria) imeelezwa kwamba, Hassan bin Ali alipokabiliana na mmoja wa wazee katikati ya vita hivyo, mzee huyo alikataa kupigana na Imam Hassan (a.s) huku akisema; Kwa hakika nimemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akiwa amepanda ngamia wake na wewe ulikuwa umempanda mbele yake. Mimi sitaki kukutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na damu yako iko shingoni mwangu. [81]

Katika kitabu kijulikanacho kwa jina la Waqi'atu Siffin, imeelezwa kwamba; Ubaidullah bin Omar (mtoto wa khalifa wa pili) alikutana na Hassan bin Ali (a.s) wakati wa vita hivyo na akapendekeza kuwa Imamu Hassan (a.s) achukue ukhalifa badala ya baba yake, kwa sababu Maquraishi wanamuhisabu Imamu Ali (a.s) kuwa ni adui yao. Imam Hassan (a.s) akajibu: Ninaapa kwa Mungu, hili halitatokea kamwe. Kisha akamwambia: Naona kama vile utauawa leo au kesho, na shetani amekuhadaa. Kwa mujibu wa maelezo ya kitabu Waqqiatu Siffin, Ubaidullah bin Omar aliuawa katika vita hivyo. [82] Baada ya kumalizika vita na kuzuka kwa Kauli mbiu ya Hakimiyyah (ya Makhawarij), Hassan bin Ali (a.s) alitoa aliwahutubia watu kupitia amri ya baba yake. [83]

Imamu Ali (a.s.) akiwa njiani akirudi kutoka Siffin, aliandika barua yenye maudhui ya kimaadili na kielimu kwa ajili ya mwanawe Imamu Hassan (a.s). [84] barua ambayo katika kitabu kijulikanacho kwa jina la Nahjul Balaghah, mara nyingi barua hiyo huwa na anwani ya nambari 31. [85]

Imeelezwa katika kitabu Al-Istii'aab ya kwamba Hassan bin Ali (a.s) pia alishiriki katika vita vya Nahrwan. [86] vile vile imeelezwa katika baadhi ya riwaya kwamba; Imam Ali (a.s) katika siku za mwisho za uhai wake, alipokuwa anatayarisha jeshi lake kumkabili Mu'awiyah kwa mara nyengine tena, alimteua mwanawe Hassan (a.s) kuwa kiongozi wa jeshi la watu elfu kumi. [87]

Kipindi kifupi cha Ukhalifa

Imamu Mojtab (a.s) alikuwa khalifa wa Waislamu kuanzia mwezi 21 Ramadhani mwaka wa 40 Hijiria [88] kwa muda wa miezi 6 hadi 8. [89] Kwa mujibu wa hadithi iliyonasibishwa kwa bwana Mtume (s.a.w.w), Sunni wanamuhisabu yeye kuwa ndiye khalifa wa mwisho miongoni mwa makhalifa wa haki (Kulafau Al-Rashidina). [90] ] Ukhalifa wake ulianza kupitia kiapo cha utii cha watu wa Iraq na kufuatiwa na miji mingine jirani [91] Watu wa Syria, wakiongozwa na Muawiyah, walipingana na ukhalifa huu. [92] Muawiyah akiambatana na wanajeshi kutoka Sham (Syria) aliondoka mjini Sham akaelekea Iraq kwa ajili ya kupigana na wa watu wa Iraq .[93] Mwisho wa Vita hivi ikwa ni suluhu ya Muawiyah kukabidhiwa ukhalifa, na huo ndio ukawa khalifa wa kwanza wa Bani Umayya. [94]

Kiapo cha utii cha Waislamu na upinzani wa watu wa Syria

Kwa mujibu wa vyanzo vya Shia na Sunni, baada ya kifo cha kishahidi cha Amiru Al-Muuminiina (cha mwaka wa 40 Hijiria). Watu walikula kiapo cha utiifu cha kumuunga mkono Hassan bin Ali (a.s) kwa ajili ya ukhalifa. [95] Kulingana na maandiko ya Bilaadhariy (aliyefariki mwaka 279 Hijiria), Ubaidullah bin Abbas alikuja mbele ya watu baada ya kuuzika mwili wa Imam Ali (a.s) na akawapa taarifa ya kifo cha kishahidi cha Imamu Ali (a.s) Na akasema ya kwamba: "Imamu Ali (a.s) ameacha wasii mvumilivu naanayestahiki kushika nafsi ya baba yake, basi mkipenda mpeni kiapo chenu cha utiifu kwake".[96] Pia kitabu cha Al-Arshad kimeeleza kwamba; Asubuhi ya Ijumaa ya tarehe 21 Ramadhani, Hassan bin Ali (a.s) alitoa khutba msikitini na kutaja sifa na ubora wa baba yake, akasisitiza mafungamano baina ya baba yake na Mtume (s.a.w.w) na akaashiria pointi muhimu za nafasi yake, katika hotuba yake hiyo alitaja Aya za Qur'an kuhusu nafasi maalum ya Ahlul-Bayt ndani ya jamii ya Kiislamu. [97] Baada ya kumaliza maneno yake, Abdullah bin Abbas alisimama na kuwaambia watu: "Kuleni kiapo cha utiifu kwa ajili mtoto wa Mtume wanu (s.a.w.w), na wasii wa Imamu wenu (a.s). Kisha watu wakala kiapo cha utii kwa Imamu Hassan (a.s)". [98] Vyanzo vya kihistoria vimenukuu zaidi ya idadi ya watu arobaini elfu waliokula kiapo cha utiifu juu yake. [99] Kwa mazingatio ya riwaya ya Tabari ni kwamba, Qays bin Saad bin Ubaada, kamanda wa jeshi la Imam Ali (a.s), alikuwa ndiye mtu wa kwanza aliyekula kiapo cha utiifu. [100]

Kulingana maoni ya Hussein Muhammad Jafari katika kitabu chake "Tashayyu'u Dar Massire Taariikh" ni kwmba; Masahaba wa Mtume (s.a.w.w) wengi waliohamia katika mji wa Kufa baada ya kujengwa kwa mji huo, ambao wailiufanya mji huo kuwa ndio makazi yao, pamoja na wale waliokuja katika zama za Ukhalifa wa Imam Ali (a.s) wote kwa pamoja ima walikuja kumpa kiapo cha utiifu Imam Hassan (a.s), au kidhahiri walikubaliana na ukhalifa wake huo. [101] Jafari, akitegemea ushahidi moja kati ya dalili za kihistoria, anaamini kwamba; Watu wa Makka na Madina pia walikubaliana na ukhalifa wa Hassan bin Ali (a.s) na watu wa Iraq walimuona yeye kuwa ndiye chaguo pekee katika nafasi hiyo ya Ukhalifa. [102] Maoni ya Ja'afari ni kwamba; Hata watu wa Yemen na Iran pia kidhahiri waliridhika na Uimamu wa Hassan (A.S), na hapakuonekana kutokea upinzani wowote ule kutoka kwao. [103]

Ndani ya baadhi ya vyanzo imeelezwa ya kwamba; Pale watu walipokuwa wakila kiapo cha utiifu juu yake, Imamu Hassan (a.s) aliweka masharti maaluumu kwa wanaotaka kula kiapo cha utiifu juu yake. Kwa mfano katika kitabu Al-Imaatu wa Al-Siasah cha Ibnu Kutaibah, imeelezwa ya kwamba; Imamu Hassan aliwaaambia walaji kiapo hao ya kwamba, je, mupo tayari katika kiapo chenu hichi kupambana na yule nitakayepambana naye, na kumjengea Amani yule nitakaye mjengea Amani? Baada ya wao kusikia kauli hiyo wakaingia wasiwasi, kisha wakenda kwa Imam Hussein (a.s) ili kulia yeye kiapo cha utiifu. Ila Imamu Hussein aliwajibu kwa kusema; “Kwa hakika na namuomba Allah anilinde, katu mimi sikubaliani na viapo vyenu juu yangu, hali ya kwamba Hassan (a.s) bado yupo hai”. Waliposikia hayo wakarudi kwa Imamu Hassan na kumpa kiapo chao cha utiifu. [104] Mwanazuoni wa kihistoria ajulikanaye kwa jina Tabari (aliyefariki mwaka wa 10 Hijiria), amenukuu kwa kusema; “Pale Qais bin Sa’ad alipomlia kiapo cha utiifu Imam Hassan (a.s) alikubaliana na mashati maalumu akisema, yeye anakula kiapo cha kusimama na Hassan bin Ali (a.s) kupitia misngi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kwamba yeye yupo tayari kupigana na yeyote yule anayehalalisha damu za Waislamu. Ila Imamu Hassan (a.s) alikubaliana na masharti yake mawili tu, nayo ni kusimama na kitabu cha Mwenye Ezi Mungu na Sunna za Mtume (s.a.w.w). Na kama kuna sharti nyengine zozote zile ambazo Imamu alikubaliana nazo, basi zitakuwa chini ya sharti mbili hizo msingi. [105] Wengi kutokana maandiko ya vyanzo hivi vya kihistoria, wamemuhisabu Imamu Hassan (a.s) kuwa ni kiongozi mwenye siasa za katika na kati asiyependa vita, na kwamba nyenendo zake yeye kisiasa, zinatofautiana kabisa na nyenendo za baba yake pamoja na ndugu yake. [106], [107].

Rasul Ja’afarian anaitakidi ya kwamba; Masharti ya Imamu Hassan hayakuwa na nia ya kutopambana kivita, bali alikuwa na nia ya kuhifadhi mhimili wake wa kisiasa akiwa ni kiongozi wa wa jamii, na alitaka watu wawe huru katika chaguo la kiongozi wao, na hata hatua zilizofuatia baadae pia zilionesha nia yake ya kupambana kivita na maadui zake. [108] Abu Faraji Isfahani amenukuu akisema; “Moja kati ya hatua muhimu baada yay eye kukamata hatamu za Uimamu, ilikuwa ni kuengeza posho la mishahara ya wanajeshi wake. [109]

Vita vya amani baina yake na Muawiyah

Moja kati ya matukio muhimu baina ya Imamu Hassan na Muawiyah, ni vita baina yao, vita ambavyo hatimae vilimalizika kwa suluhu na amani. [110] Tukio muhimu zaidi la kisiasa katika maisha ya Hassan bin Ali (a.s) ni vita baina yake na Mu'awiyah, vita ambavyo viliisha kwa suluhu na amani. [110] Wakati huo huo watu wa Hijazi, Yemen na Uajemi, kidhahiri walionekana kukubaliana na Ukhalifa wa Imamu Hassan bin Ali (a.s)[111] Kwa upande wa pili, watu wa Shamu walikula kiapo cha kutii Mu'awiya kama ndiye kiongozi wao. [112] Muawiyah katika hotuba yake na barua alizokuwa akimwandikia Imam Hassan (a.s), alisisitiza uamuzi wake mzito wa kutokitambua kiapo hiki cha utiifu wa watu waliokubaliana na Ukhalifa wa Hassan bin Ali (a.s). [113] Muawiyah tokea mwanzoni mwa kifo cha Othmani alikuwa tayari ameshajitayarisha kwa ajili ya kushika Ukhalifa. [114] Hapo basi akaamu kukusanya jeshi lake na kuelekea Iraq. [115] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti za kihistoria ni kwamba, kwa kiasi cha kipindi cha siku 50 hivi baada ya kifo cha baba yake kishahidi na tukio la yeye kupewa viapo vya utiifu, Imam Hassan (a.s) hakuchukua hatua yoyote katika juhudi za kujitayarisha kivita au za kuleta amani. [116] Na pale alipopata habari kuhusu harakati za jeshi la Syria, aliondoka kutoka mji wa Kufa pamoja na askari wake na kutuma jeshi lake chini ya uongozi wa Ubaidullah bin Abbas kumuelekea Muawiya. [117]

Nafasi ya Iman Hassan (a.s) katika mji wa Sabat

Kwa upande mwingine, Imam Hassan (a.s) alikwenda Sabbat (Kaskazini mwa Baghda) na jeshi lake. Kwa mujibu wa mtazamo wa Sheikh Mufid, Imam Hassan (a.s), ili kuwajaribu maswahaba zake na kupima utiifu wao juu yake, aliwasomea khutba na akiwambia: “Umoja na mshikamanu wa kiroho ni bora kwenu kuliko utengano na mparaganyiko...; Hakika mipango niliyokupangieni ni bora kwenu kuliko mpango mliojipangia nyinyi wenyewe nafsini mwenu...” Baada ya maneno yake hayo, watu wakasemezana kwamba, Imamu (a.s) ana nia ya kufanya suluhu na Mu’awiyah na kumawachia yeye ukhalifa. Mara tu baada ya hapo, baadhi ya watu wakalivamia hema lake na kupora vitu vyake, na hata mkeka wake ulioko chini ya miguu yake pia wakauvuta na kuupora. [120] Ila Yaqoubi ambaye ni mwana historia maarufu (aliyefariki mwaka 292 Hijiria), yeye anasema; "Sababu ya tukio hilo ni pale Muawiya aliwatuma baadhi ya watu waende kujadiliana na Imamu Hasan bin Ali (a.s) na kufanya mazungumzo naye kuhusiana na suala la kusimamisha vita na kuleta suluhu ya amani.... Na pale watu hao walipokuwa wakirudi kutoka kwake, wakaanza wakiambizana wao kwa wao kwa sauti kubwa ili watu wasikie: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameziokoa damu za Waislamu na kuzima fitna kupitia mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kukubali kwake amani na kuleta suluhu". Baada ya askari wa Imam Hassan (a.s) kusikia maneno haya, wakafadhaika na kulishambulia hema lake." [121] Baada ya tukio hilo masahaba wa karibu wa Imam Hassan (a.s) walimlinda kutokana na balaa hilo, lakini katika giza la usiku huo, mmoja wa Khawarij [122] alikaribia na kusema: "Ewe Hassan, umekuwa mshirikina kama yako alivyo kuwa baba" Kisha akampiga panga pajani mwake, na imamu aliyekuwa amepanda farasi akaanguka chini. [123] Wafuasi wake Wakamchukua kitandani na kwenda naye Madain, kisha wakampatia makazi katika nyumba ya Sa'ad bin Masoud Thaqafi ili aweze kutibiwa. [124]

Vita kati ya Muawiya na Imam Hassan (a.s) hatimaye vilipelekea kusainiwa kwa makubaliano wa amani baina yao. Kwa mujibu wa maoni ya Rasul Jafarian, sababu zilizopelekea kusainiwa kwa mkataba huo, kama vile uvivu wa watu, hali mbaya za nyakati, na khofu juu ya roho za Mashia. Kwa mtazamo wake, hizo ndizo sababu hasa zilizomfanya Imam Mojtab (a.s) kukubali kusaini mkataba wa amani.[125] Na kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, Ukhalifa ulikabidhiwa kwa Muawiyah naye akawa ndiye Khali kwa kipindi hicho. [126]

Tukio kusimamisha suluhu (amani) na Mu'awiyah

Makala asili: Suluhu ya Imam Hassan (a.s)

Sambamba na wakati ambao majeshi mawili ya Iraq na Syria yalipopambana, Imam Hassan (a.s) alidhamiriwa kuuwawa, ila dhamira hiyo haikufanikiwa, na badal yake alijeruhiwa na kuelekea Mada'in kwa matibabu. Kundi fuani liliko ndani ya Kufa lilimuandikia barua ya Mu'awiyah na kutangaza utiifu wao juu yake. Walimhimiza Mu’awiyah aje kwao, na wakaahidi kumsalimisha Hasan bin Ali (a.s) kwake yeye au kumuua kabisa. [128] Mtazamo Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka wa 413 Hijiria), ni kwamba; Pale Imam Hassan (a.s) aliposikia habari hiyo na pia habari ya Ubaidullah bin Abbas kuungana na Mu'awiyah, na kwa upande mmoja alipouona udhaifu wa masahaba zake, alitambua ya kwamba kwa idadi ndogo tu ya Mashia (Wafwasi) wake, katu hawezi kupambana na jeshi kubwa la watu wa Syria wanaoongozwa na Mu'awiyah. [129] Zaid bi Wahab ameripoti akisema "Wakati Imamu Hassan (a.s) alipokuwa matibabuni mwake huko Mada-in, akamwambia akisema: "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, iwapo nitapigana na Mu'awiyah, basi watu wa Iraq watanishika shingo yangu na kunikabidhisha kwake." Wallahi iwapo nitafanya suluhu na Mu’awiyah nikiwa katika heshima bila ya fedheha, ni bora zaidi kuliko kuuwawa mikononi mwake huku nikiwa ni mateka wake, au anisimbulie kutokana na kunisamehe kwake, jambo ambalo litabaki kuwa ni fedheha kwa Banu Hashim milele na milele...." [130]

Pendekezo la amani la Mu'awiyah

Kwa mujibu wa riwaya ya Ya'aqubi, moja ya hila za Mu'awiya ili kuvibadili vita na kuvielekeza kwenye gurudumu la sulusuhu na amani ni kwamba; Mu'awiyah alitumia mbinu ya kuwatumia watu miongoni mwa askari wa Imam Hassan (a.s), ili kueneza uvumi kwamba Qais bin Sa'ad pia naye amejiunga na Mu'awiyah, na kwa upande mwingine, akawatuma baadhi ya askari wa Qays kueneza uvumi wa kwamba, Hasan bin Ali ameikubali kuleta suluhu na kujenga amani. [131] Vile vile akatumia Hassan bin Ali (a.s) zile barua kutoka kwa watu mji wa Kufa waliojitangazia kula kiapo cha utiifu wao kwa Mu'awiyah, huku akimpa Hassan bin Ali (a.s) ushauri na pendekezo la makubaliano ya amani huku akijipangia masharti maalumu juu ya suala hilo la kusimamisha amani. Kwa mujibu nukuu kutoka kwa Sheikh Mufid, yaonekana ya kwamba; Imam Hassan (a.s) hakumwamini Mu'awiyah na alifahamu fika hila yake, lakini hakuwa na chaguo jingine ila kukubali amani. [132] Imeelezwa katika ripoti ya Biladhari ya kwamba; Mu'awiyah alimtumia Imamu Hassan (a.s) karatasi nyeupe pepepe ambayo tayari imeshagongwa muhuri, ili Imamu Hassan (a.s), aandike masharti ayatakayo mwenyewe juu ya suala hilo la kusimamisha vita na kuleta suluhu ya amani.[133] Imam Hassan (a.s) ambaye aliona hali kama hii, alizungumza na watu na akawataka watoe maoni yao kuhusu kuendelea na vita hivyo, au kuleta amani. Watu hao wakana na kauli mbio isemayo “Al-Baqiya al-Baqiyya” (yaani tunataka kubaki na kuendelea kuishi). [134] Hivyo basi Imamu Hassan (a.s) akaikubaliana na amani hiyo. Amani hiyo ilitiwa mkataba na kusimama mnamo mwezi 25 Rabiu Al-Awwal [135] na katika baadhi ya vyanzo, ni Rabiu Al-Akhar au Jumadu Al-Awali [136] ya mwaka wa 41 Hijiria.

Masharti ya makubaliano ya amani

Kuna riwaya mbalimbali zilizonukuu masharti ya makubaliano ya amani. [137] Miongoni mwa masharti yaliyonukuliwa katika riwaya hizo ni kwamba; Ukhalifa ukabidhiwe kwa Mu'awiyah kwa sharti la kwamba undendaji wake akiwa katika nafasi hiyo ya Ukhalifa, uwe ni kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume (s.a.w.w) na kulingana na nyenendo za makhalifa waongofu. Jingine ni kwamba, asiteue mrithi baada yake, na watu wote, wakiwemo Mashia(wafuasi) wa Ali (a.s), wapewe amani ya kuishi salama. [138] Sheikh Swaduq alisema: "Pale Imam Hassan (a.s) ) alipoukabidhi Ukhalifa kwa Mu'awiyah, alimpa kiapo cha kumtii chini ya sharti la kwamba yeye (Imamu Hassan (a.s) hatamuita Mu'awiyah kwa jina la Amirul-Mu'minin. [139]

Katika baadhi ya vyanzo, imeelezwa kwamba; Imam Hassan (a.s) aliweka sharti la kwamba, ukhalifa urudi tena kwake yeye baada ya kumalizika kipindi cha Mu'awiyah, akiongezea, kwamba Mu'awiyah anatakiwa amlipa Immu Hassan (a.s) dirham milioni tano. [140] Kwa mujibu wa maoni ya Jafari, masharti mawili hayo yalitolewa na mwakilishi wa Imam Hassan (a.s) katika suala hilo la kusimamisha amani. Ila Imam hakukubali na akasisitiza kwamba uteuzi wa Khalifa baada ya Mu'awiyah uwe kupitia baraza la Waislamu (Shura). Na kuhusu suala malipo ya dirhamu milioni tono, Imamu alisistiza ya kwamba, Mu'awiyah hana haki yoyote ile ya kumiliki fedha ndani ya hazina ya Waislamu. [141] Wengine pia wamesema kwamba sharti hilo la kumlipa kifedha Imamu Hassan (a.s), liliwekwa na Mu'awiyah mwenyewe au wawakilishi wake. [142]

Imamu Hasan (a.s) licha ya kung'atuka kutoka katika nafasi ya Ukhalifa, ila bado aliendelea kuwa ni Imamu wa Mashia, na hata Mashia waliopinga amani ya Imamu Hassan (a.s), hawakuwahi kuukana Uimamu wake. Naye aliendelea kubaki kuwa ni mkuu wa familia ya Mtume (s.a.w.w) hadi mwisho wa maisha yake. [143]

Athari na akisiko ya matokeo

Kuna ripoti zilizorikodiwa zikisema kwamba; Baada ya suluhu ya Imam Hassan (a.s) na Mu'awiyah, kundi la Mashia lilonesha masikitiko na kuchukizwa kwao kwa makubaliano hayo ya suluhu. [144] Hata baadhi yao walimlaumu Imamu Hassan (a.s) na kumwita “Mudhillu Al-Muuminiina” (mwenye kuwadhalilisha waumini). [145] Imam Hassan akijibi lawana na shutuma hizo, alisisitiza ulazima wa kukukbaliana uamuzi wa Imam (a.s), na kunasibisha sababu ya suluhu yake na suluhu Hudaybiyah, na kuifananisha hekima ya suluhu hiyo kuwa ni sawa na hekima ya Khidri (a.s) katika hadithi ya safiri Nabi Musa na Khidhri (a.s). [146]

Imeelezwa katika vyanzo vingi vya kihistoria kwamba; Mu'awiyah hakuzingatia masharti ya makubaliano hayo ya amani(suluhu). [147] Badala yake akawageukia na kuwaua Mashia wengi wa Imam Ali (a.s), akiwemo Hajar bin Adiy [148]. Imepokewa kwamba Mu'awiyah aliingia katika mji wa Kufa baada ya suluhu hiyo, na akawahotubia watu akisema: Nitaitengua kila sharti nililoweka na nitavunja kila ahadi niliyoitoa. [149] Pia akawambia: "Sikupigana nanyi ili msimamishe swala na kufunga au kuhiji, bali nilipigana nanyi ili niwatawale. [150]

Maisha yake mjini Madina na mamlaka ya kidini

Baada ya Hassan bin Ali (a.s) kufanya suluhu na Mu'awiyah, licha ya ombi la baadhi ya Mashia wake kumtaka akae mji wa Kufa, yeye alirejea Madinah, [151] na akakaa huko hadi mwisho wa maisha yake, safari alioifunga ni ile safari ya kwenda Makka tu na Syria[153]. Baada ya kifo cha cha Imam Ali (a.s) kishahidi na kwa mujibu wa wosia wake, Imam Mujtabi (a.s) ndiye aliyekuwa wasii na mdhamini na msimamizi wa waqfu na sadaka zake. Kwa mujibu wa nukuu za Kitabu Al-Kafi, wasia huo uliandikwa mnamo tarehe 10 Jumadu Al-Aawali ya mwaka wa 37 Hijiria. [154]

Rejeo la kielimu (Mwanazuoni mkuu)

Zipo ripoti kadhaa zilizoashiria kuwepo kwa vikao vya kielimu vya Imam Hasan (a.s) vinavyoendelea vikiendelea mjini Madina kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwaongoza watu kwenye haki. Miongoni mwa watu walioripoti ripoti hizo ni; Ibn Saa'd (aliyefariki mwaka wa 230 Hijiria), Biladhiri (aliyefariki mwaka wa 279 Hijiria), na Ibn Asaaker (aliyefariki mnamo mwaka wa 571 Hijiria), ambaye amesimulia kuwa; Hassan Ibn Ali (a.s) akisali Swala ya Asubuhi kwenye msikiti wa Mtume (s.a.w.w) kisha alikuwa akiendelea kuabudu mpaka jua linapochomoza. Na baada ya hapo wazee waliokuwepo msikitini walikuwa wanakaa karibu naye na kujadiliana pamoja katika masuala mbali bali. Pia baada ya sala ya Adhuhuri alikuwa na kwaida hiyo hiyo. [155] Pia katika kitabu cha Al-Fusul Al-Muhimmah meelezwa ya kwamba; Hassan bin Ali (a.s), alikuwa akikaa katika msikiti wa Mtume pamoja na watu kwa mfumo wa duara na kujibu maswali yao. [156] Wakati huo huo, Kwa mujibu wa maoni ya Mahdi Pishwai, Hassan bin Ali (a.s) alikabiliana na aina fulani ya kutengwa katika jamii na pia kutokubalika mbele ya watu katika kipindi hicho, jambo ambalo lilichangia kupotoka kwa maadili ya jamii ya siku hizo. [156] Allaamah Tehraniy anaamini ya kwamba; Kipindi cha Uimamu wa Hassan bin Ali na Imamu Husein (a.s) ndio kipindi kilichogubikwa na giza kubwa zaid, kutokana shinikizo la kidhalimu la utawala dhalimu wa Bani Umayya. Tuzingatia urefu wa maisha ya Maimamu wawili hawa, pamoja na muda wa uimamu wao, ni lazima kwa kawaida ni lazima kungelikuwa na maelfu ya hadithi, mawaidha, khutba pamoja na tafsir ya Qur'an mkononi mwetu, lakini kuna khutba na maneno machache mno yaliorikodiwa kutoka katika kipindi hicho. [158]

Nafasi ya kijamii

Kutokana na habari za kihistoria, inaonekana kwamba Imam Hassan (a.s) alikuwa na nafasi maalum katika kijamii. Kwa mujibu wa riwaya ya Ibn Sa'ad (aliyefariki mwaka wa 230 Hijiria), watu walipomuona Hassan bin Ali (a.s), wakati wa ibada ya Hijja, walimkimbilia ili kupata baraka zake mpaka wakati mwengine Husein bin Ali (a.s) akisaidiana na watu wengine wakawa wanamsaidia kuutawanya umma wa watu hao. [159] Imepokewa pia kwamba Ibn Abbas, licha ya kwamba yeye alikuwa ni mmoja wa wazee wa Maswahaba [160] na alikuwa ni mkubwa kiumri kuliko Imam Hassan (a.s), ila alikuwa akimuona Imamu Hassan (a.s) anataka kupanda farsi wake, alikuwa akienda kumsaidia ili apande bila ya tabu. [161]

Kutoingilia mambo ya kisiasa na kutoshirikiana na Mu'awiya

Inasemekana ya kwamba; baada ya Imam Hassan (a.s) kuondoka Kufa, kundi la Khawariji lilikusanyika kitongoji cha Nakhila ili kupambana dhidi ya Mu'awiya. Jambo hilo lilimfanya Mu'awiyah amwandikie barua Hassan bin Ali (a.s) na kumtaka arejee na kupigana nao. Ila Imam hakukubali naye na katika jibu lake alimwandikia akisema: “Lau ningetaka kupigana na mmoja wa watu wa Qibla (Muislamu), basi ningelipigana na wewe.” [162] Pia, wakati kundi jingine la Khawariji lililokuwa likiongozwa na Hauthrah Asadi lilipoinuka dhidi ya Mu'awiyah, Muawiyah alimtaka Imam Hassan (a.s) apambane nao ila hakukukabaliana naye, na akamji jibu lile lile la awali lililosema kwamba; Ingelikuwa Imamu Hassan ana nia ya kupigana na mmoja ya Waislamu, basi wa kwanza kupigana naye angeliku ni Mu'awiya. [163]

Imeelezwa katika baadhi ya Hadithi kwamba Imamu Mujtab (a.s) alikubali na kupokea zawadi kutoka kwa Mu'awiyah licha ya kutofuatana naye na kupingana na matendo yake. [164] Mu'awiya kila mwaka alikuwa akimpelekea Imamu Hassan zawadi kadhaa sambamba na kiwango cha fedha zinazokadiriwa kuwa ni dirhamu milioni moja [165] au lakimoja. [166] Kutokana na nukuu za baadhi ya riwaya, yaonekana kwamba, wakati mwingine Imamu Hassan (a.s), alizitumia fedha hizo kwa ajili ya kulipa deni lake na kilichobaki alikuwa akikigawa baina ndugu, jamaa zake, na wasaidizi wake. [167] Pia wakati mwingine alikuwa akizigawa fedha hizo zote na kuwazawadia watu. [168] Pia kuna ripoti isemayo kwamba; Hassan bin Ali (a.s) wakati mwingine hakubali kupokea zawadi hizo kutoka kwa Mu'awiyah. [169] Habari kama hizo zimesababisha utata na mashaka kutoka kwa wahakiki mbali mbali. [170] na miongoni mwa mijadala ilioibuka kuhusu hilo, ni ileikijumuisha mijadala inayojadiliwa ndani ya elimu ya fani ya theologia (akida). Kwa mfano, Sayyied Murtaza anaamini ya kuwa inaruhusiwa tu, bali ni wajibu kwa Imamu Hassan (a.s) kupokea fedha na zawadi kutoka kwa Mu'awiya. Uelewa wake huo unatokana na nukta ya kwamba, ni lazima mali ya mtawala aliyetawala taifa kwa mabavu ichukuliwe. [171]

Miamala ya Bani Umayyah kwa Imamu Hassan

Kuna ripoti zinazoonesha Bani Umayya kutoamilana vizuri na Imam Hassan (a.s). [172] Pia, katika kitabu Al-Ihtijaaj, kumeripotiwa mijadala mbalimbali iliyotokea kati ya Mu'awiya na wafuasi wake na Imam Hassan (a.s). Katika mijadala hiyo, Imamu Hassan (a.s) alitetea msimamo na nafasi ya Ahlul-Bayt na akafunua pazia na akadhihirisha asili na nafasi ya maadui zake. [173] Ingawaje kulikuwa na shinikizo kubwa la propaganda za Bani Umayya na njama mbalimbali dhidi ya Ahlul-Bayt(a.s) wote kwa jumla, pamoja na njama maalumu dhidi ya Imam Mujtaba (a.s.), ila daima yeye alikuwa ni mwenye busara, werevu, na ubingwa wa hali ya juu katika kuzitengua na kuzibatilisha njama hizo. Ripoti kadhaa za kihistoria zimeripoti kuwepo kwa mijadala yenye utata iliyomuelemea Imamu kutoka kwa wapinzani na maadui zake. Mijadala hiyo inaonyesha wazi jinsi ya Imamu Hassan (a.s), alivyokuwa ni mjuzi mwenye hekima mwenye tahadhari ya kutosha katika nyenendo zake. Katika mkusanyiko ambapo watetezi na wafuasi wa serikali ya Mu'awiyah, kama vile Amru bin Othman, Amr bin As, Utbah bin Abi Sufyan, Walid bin Uqbah na Mugheirah bin Shu'abah walikuwa mbele ya Mu'awiyah, huku Imam Mujtaba (a.s) akiwa peke yake, aliwasimamishia hoja na dalili kupitia Aya za Qur'an na Hadithi na nukuu za kihistoria. Dalili ambazo zilifichua uhalisia wao na kuwahukumu kwa matendo yao. Kupitia dalili hizo aliwaonesha ukweli wa haki ya Amirul-Mu'minin na Ahlul-Bayt (a.s) na nafasi yao katika Uislamu, kiasi ya kwamba, hata kabla ya mjadala huo kuanza, tayari Mu'awiyah akawa ameshafedheheka na kuadhirika mbele ya watu walihudhuria katika mjadala huo, naye ndiye akawa mhukumiwa katika mjadala huo. [174]

Tukio la kifo cha kishahidi na mazishi yake (a.s)

Faili:Shahadate emam hasan.jpeg
Imam Hassan (a.s.) kwenye kitanda cha kifo cha kishahidi, toleo la "Hadiqah al-Suadaa" katika karne ya 16 AD.

Katika vyanzo vingi vya Kishia na Kisunni, imeelezwa kwamba; Imamu Hassan (a.s) aliuawa kishahidi kwa njia ya sumu.[175] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, alitiliwa sumu mara kadhaa, ila Mungu alimuokoa na kifo. [176] Kuhusiana na sumu ya mwisho iliyopelekea kuuawa kwake kishahidi, Sheikh Mufid amenukuu akisema; Pale Mu’awiyah alipodhamiria kukusanya viapo vya utiifu kwa ajili ya kumweka mwanawe (Yazid) katika kiti cha Ukhalifa, alituma kiwango cha dirham laki moja kumpelekea Ja'adah binti Ash’ath bin Qais (mke wa Imamu Hassan (a.s)) , na akamuahidi iwapo atatimiza kazi yake ya kumuuwa Imamu Hassan (a.s) kupitia sumu, basi atamuozesha mwanawe (Yazid). [177] Pia Jina la Ja'adah limenukuliwa na vyanzo vya kihistoria vya upande Kisunni akitambuliwa kuwa ndiye muuaji wa Hassan bin Ali (a.s). [178] Madelong anaamini kwamba suala la urithi wa ukhalifa wa Mu'awiyah na jaribio lake la kutawazisha Yazid kuwa ndiye Khalifa, linatilia mkazo suala la Imamu Hassan (a.s) kupewa sumu na Ja'adah kupitia ushawishi wa Mu'awiyah. [179] Pia kuna ripoti zinazoashiria kuwa Imamu Hassan (a.s) alitiliwa sumu na mmoja wa wake zake ajulikanaye kwa jina la Hindu, [180] au sumu hiyo alitiliwa na mmoja wa wajakazi wake. [181] Inasemekana kwamba Hassan bin Ali (a.s) alikufa baada ya siku 3[182] au siku 40[183] au miezi miwili [184] baada ya kupewa sumu hiyo.

Imepokewa kwamba baada ya Imam Mujtaba (a.s) kuuawa shahidi, mji wote wa Madina uliingia katika maombolezo. [185] Pia inasemekana kwamba wakati wa mazishi, eneo la makaburi ya Baqii lilijaa watu na masoko yalifungwa kwa muda wa siku saba. [186] Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya Kisunni, Imesimuliwa kwamba fedheha ya kwanza kwa Waarabu ilikuwa ni kifo cha Hassan bin Ali (a.s). [187]

Kuzikwa karibu na kaburi la Mtume

Katika baadhi ya vyanzo, imeelezwa kwamba Imamu Hassan (a.s) alimuusia kaka yake baada ya kifo chake amzike karibu na kaburi la babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). [188] Kwa mujibu wa riwaya zisemavyo, Hassan bin Ali alimjulisha Aisha kuhusiana na wosia wa nduguye, Naye akakubaliana na wosia huo. [189] Na kwa mujibu wa riwaya ya kitabu kiitacho “Ansab Al-Ashraaf”, pale Marwan Ibn Al-Hakam alipopata habari kuhusu wosia huo, aliripoti kwa Mu’awiyah na Mu’awiyah akamtaka apingane na wosia huo na asiruhuru wosia huo kutendeka. [190]

Katika riwaya za Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka wa 413 Hijiria), Tabrasi (aliyefariki mwaka wa 548 Hijiria) na Ibn Shahr Ashub (aliyefariki mwaka wa 588 Hijiria) imeelezwa kwamba; Imam Hassan Mujtaba (a.s) alitaka jeneza lake lipelekwe kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w) kwa nia ya kuweka upya kiapo cha kumuunga mkono babu yake. Kisha azikwe pembeni mwa kaburi la bibi yake Fatima binti Asad. [191] Katika ripoti hizi, imeelezwa kwamba Hassan bin Ali (a.s), aliamuru kuepukana na aina zote za mgogoro wakati wa maziko yake [192] ili kuepusha umwagaji damu. [193]

Bani Hashim walipolipeleka jeneza la Imamu Mujtabi (a.s) kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w), Marwan pamoja na baadhi ya Bani Umayya walishika silaha na kuziba njia ili asizikwe karibu na kaburi la Mtume (s.a.w.w). [194] Abul Faraj Isfahani (aliyefariki mwaka wa 356 Hijiria) ameripoti kwamba Aisha alipanda mnyama -ambaye baba ni punda na mama ni farasi- na akamtaka Marwan na Bani Umayyah wampe msaada. Pale Aisha alipoona mgogoro umewaka moto na tayari watu wanakaribia kumwaga, alisimama na kunadi akisema "Nyumba ni nyumba yangu na sitaruhusu mtu yeyote kuzikwa ndani yake". [196] Ibn Abbas alimkabili Marwan, ambaye alikuwa na silaha na alikuwepo katika eneo hilo kwa ajili ya kuleta fitna, akimwambia; "Sisi hatukusudii kumzika Imamu Hasan (a.s) karibu na Mtume (s.a.w.w), ila tunakusudia kuikariri ahadi ya kumuunga mkono bwana Mtume (s.a.w.w) na kumuaga, ila kama imamu angekuwa ametuusia tumzike karibu na Mtume (s.a.w.w), basi tungefanya hivyo na hakuna ambaye angeliweza kutuzuia. Papo hapo Ibnu Abbas atumia lugha ya kinaya akaashiria tukio la Aisha kushiriki katika vita vya Jamal huku akiwa na nia ya kumfuja na kumkana. [197]

Pia imeripotiwa ya kwamba; Marwan alijibizana na wazishi wa Imamu Hassan (a.s) akisema: "Sisi hatukubali kumuona Othman amezikwa mwishoni mwa mji, lakini mnataka kumzika Hassan bin Ali karibu na Mtume. [198] Katika mzozano huo, ilikaribia kutokea mapigano baina ya Bani Hashim na Bani Umayyah. Ila Imamu Hussein (a.s) kwa mujibu wa wosia wa kaka yake, alijizuia na akaepukana mzozo huo. [199] Hivyo basi mwili wa Hassan bin Ali (a.s) ulipelekwa Baqi'i na kuzikwa karibu na kaburi la bibi Fatima binti Asad. [200][201]

Katika riwaya ya Ibn Shahar Ashub, imeelezwa kwamba; Bani Umayya walirusha mishale kwenye maiti ya Imam Mujtaba (a.s). Kulingana na nukuu hii, kiasi ya mishale 70 ilitolewa kutoka kwenye mwili wa Hassan bin Ali (a.s.) kabla ya kuzikwa kwake. [202]

Tarehe ya kufa kishahidi

Vyanzo tofauti vya kihistoria vimenukuu ya kuwa; Imam Hassan (a.s) ameukufa kishahidi katika mwaka wa 49, 50 au 51 Hijiria. [203] Pia kuna ripoti zingine zilizonukuu habari zinazotofautiana na hizi. [204] Baadhi ya wahakiki wakitegemea nukuu tofauti, wamechagua kauli isemayo kuwa, yeye amekufa kishahidi mnamo mwaka wa 50 hijiria. [205] Tukio hilo limetokea mwezi gani? Vyanzo vya Shia vimeripoti kutokea kwa tukio hilo ndani ya mwezi wa Safar [207], na vyanzo vingi vya Sunni vimeripoti kutokea kwa tukio hilo ndani ya mwezi wa Rabi'u Al-Awwal. [209]

Pia kuna nukuu tofauit kuhusiana na siku ya kufa kwake kishahidi: Wanazuoni wengi akiwemo Sheikh Mufid [210], Sheikh Tusi [211] (aliyefariki mwaka 460 Hijiria) Sheikh Tabrasi [212] (aliyefaki mwaka 548 Hijiri), pamoja na Ibnu Shahar Ashub [213] (aliyefariki mwaka 588), wote kwa pamoja wamesema kuwa; Imamu Hassan (a.s) alifariki mwezi 28 Safar. Ama Shahidu Al-Awwal (aliyefariki mwaka 786 Hijiria) amesema kwamba Imamu Hassan (a.s), amefariki tarehe 7 ya mwezi wa Safar [214], Sheikh Kulaini naye amesema kuwa, yeye alifariki siku ya mwisho ya mwezi wa Safar. [215] Yadu Llahi Muqaddasi baada ya utafiti madhubuti kutoka katika vyanzo tofauti, amesema ya kwamba, kauli madhubuti zaidi juu ya kutokea kwa tukio hilo, ni mwezi 28 Safar. [216]

Nchini Iran, mwezi 28 Safar ni siku ya mapumziko kutokana na siku hiyo kuwafikiana na ni siku ya kufariki kwa bwana Mtume (s.a.w.w) sambamba na Imamu Mujtaba (v), na watu wa Iran katika siku kama hiyo hujishighulisha na maombolezo ya matukio mawili hayo. Ila baadhi ya nchi nyingine kama vile Iraq, siku ya kuomboleza kifo cha Imam Hassan (a.s), huwa ni siku ya mwezi 7 Safar. [217] Tokea zama za kale chuo cha Kiislamu cha Najaf, kilikuwa kikiomboleza kifo cha Imamu Hassan (a.s), katika siku ya mwezi 7 Safar. Na katika chuo cha Kiislamu kilichoko Qom Iran, kuanzia zama za Sheikh Abdulkarim Haairiy, siku ya mwezi 7 Safar ilihisabiwa kuwa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya maombolezo hayo. [218] [219] Kulingana na tofauti zilizopo juu ya siku halisi ya kifo cha kishahidi cha Imamu Hassan bin Ali (a.s), pia kumetokea khitilafu kuhusiana na umri wake. Hivyo makadirio ya umri wake pale alipokufa kishahidi, yatakuwa ima ni miaka 46 [220] ima 47 [221] au 48. [222]

Sifa na vigezo alivyokuwa navyo

Kwa mujibu wa maoni ya Ya'aqubi (aliyefariki mwaka wa 292 Hijiria), ni kwamba; Hassan bin Ali (a.s) alikuwa ndiye mtu anayefanana zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.W) kisura na kitabia. [223] Alikuwa na kimo cha wastani na sifa na vigezo tofauti. [224] Alipaka rangi nyeusi ndevuni mwake. [225] Ana sifa kibinafsi na za kijamii zimeripotiwa katika vyanzo vya Kiislamu:

Sifa zake binafsi

Kura riwaya kadhaa zinazozungumzia muqtadha wa sifa zake binafsi, miongoni mwazo ni kwa ifuatavyo:

Sifa ya kupendwa na Mtume (s.a.w.w)

Kuna riwaya nyingi kuhusu mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) juu mjukuu wake Hassan bin Ali (a.s). Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ya kuwa; Siku moja akiwa amembeba Hassan (a.s) mabegani mwake, alisema: “Ewe Mola wangu, mimi nampenda huyu, basi na wewe pia umpende. [226] Baadhi ya wakati fulani, Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akisujudu alipokuwa katika swala ya jamaa, basi Hassan (a.s) alikuwa akipanda juu ya mgongo wake, na Mtume (s.a.w.w) akawa hainui kichwa chake kutoka katika sijda mpaka yeye ateremke, Maswahaba walipokuwa wakiuliza kwa nini amerefusha sijda yake, alikuwa akisema kwamba; anataka ashuke kutoka mgongoni kwangu kwa hiari yake mwenyewe. [227]

Imeelezwa katika kitabu Faraid Al-Simtain kwamba; Mtume (s.a.w.w) amesema kuhusu yeye ya kwamba: "Yeye (Hassan) ni mmoja wa vijana wa Peponi na Khalifa wa Mwenyezi Mungu juu ya Ummah... Yeyote anayemfuata yu pamoja nami na anayemuasi hayupo pamoja nami". [228]

Aya kadhaa kuhusiana naye

Hassan bin Ali (a.s) ni miongoni mwa Ahlul-Bait (a.s), na kwa mujibu wa wafasiri wa Qur'an, Aya kadhaa za Qur’an ziliteremshwa kuwahusiana naye, moja wapo ikiwa ni ile Aya ya kulisha maskini (Aya ya 8 ya Suratul Insan), ambayo kwa mujibu wa Hadith za Shia na Sunni, iliteremka kuhusiana na Ahlul-Bayt na kuteremkiwa na Aya hiyo ni miongoni sifa zao (a.s). [229] Pia wafasiri wengi, wakinukuu Hadith, wamesema kwamba; Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w) ndio sababu ya kuteremshwa Aya ya Mawaddah (Aya ya 23 ya Suratu Shura). Katika Aya ya Mubahalah (Aya ya 61 ya Suratu Al-Imran), iliyoteremka katika kisa cha Mubahalah (Kulishana kiapo cha maapizo) baina ya Mtume na Wakristo wa Najran, Imamu Hassan na Hussein (a.s) wanatambuliwa kuwa ndiyo maana na nembo halisi ya neno "Ab-naa-ana" lenye maana ya watoto wetu, liliko ndani ya Aya hiyo. [231]

Pia, Aya ya utakaso iliteremka kuhusiana na As-habu Al-Kisaa wa watu waliofunikwa na shuka la Mtume (s.a.w.w), ambapo Imam Mujtaba (a.s) alikuwa mmoja wao. Aya hii inategemewa kama ndio dalili na hoja ya kuthibitisha umaasumu (utakaso) wa Ahlul-Bayt. [232]

Ibada na mafungamano na Mungu

Imam alipokuwa anatawadha na kujiandaa kwa ajili ya Swala, miguu yake ilikuwa ikitetemeka na kugeuka manjano. Pale alipoulizwa kuhusiana na hilo Imamu Hassan (a.s) alisema: “Anayesimama mbele ya Mola wake Mlezi anastahikina miguu yake kutetemeke". [233] Abu Khaythamah anasema: " Imamu Hassan (a.s), alipokuwa akisali, alikuwa akichagua nguo zilizo bora zaidi kwa ajili ya kusalia, alipoulizwa, ni kwa nini unavaa nguo zilizo bora zaidi? Alijibu kwa kusema: "Mwenyezi Mungu ni mzuri na anapenda uzuri, na mimi hupenda kuvaa nguo zangu bora na kujidhihirisha kwa Mola wangu Mlezi"". [234] Imamu Sajjad (a.s) amesema kwamba; Imam Hassan (a.s) katika hali zake zote zile maishani mwake, hakuonekana akijishughulisha na jambo jingine lile isipokuwa la kumdhikiri Mwenye Ezi Mungu. [235]

Mara kadhaa alikwenda Hija kwa mguu

Mara kadhaa Imamu Mujtab (a.s) alikuwa akienda Hija kwa miguu. imepokewa ya kwamba; Yeye alikuwa akisema kwamba, kwa hakika mimi ninaona haya kukutana na Mola wangu Mlezi huku nikiwa sikupiga hatua kuielekea nyumba yake. [239] yasemekana ya kwamba mara 15 [237], au 20 [238] au 25 [239] alikwenda Hija kwa miguu huku ngamia walio bora zaidi wakimfuatana naye pembeni mwake. [240]

Sifa za kijamii

Tabia zake za kijamii pia zinajadiliwa katika vyanzo:

Imamu Hassan (a.s) alisifika kwa uvumilivu

Katika vyanzo vya Kiislamu, kuna ripoti nyingi kuhusiana uvumilivu wake hadi akaitwa Halim (mvumilivu). [241] Katika baadhi ya vyanzo vya Sunni, imeelezwa kwamba; Marwan bin Hakam, ambaye alikuwa na uadui naye ambaye alimzuia asizikwe karibu na Mtume (s.a.w.w), alishiriki katika mazishi yake naye amelichukua kwa sehemu ya mvunguni mwa jeneza hilo. Watu walipotaka kumzuia na kumuondoa katika jeneza hili wakimwambi; wewe hustahiki kushikilia jeneza hili, kwa sababu ulikuwa ukimuudhi Hassan bin Ali wakati wa uhai wake, yeye alijibu kwa kusema: “Mimi nilikuwa ninamuudhi mtu ambaye subira yake ilikuwa ni pevu kama milima. [242] Imepokewa kwamba mtu mmoja wa Sham alimuona Imam Hassan (a.s) na akaanza kumlaani. Baada ya mtu huyo kunyamaza, Imam Mujtabi (a.s) alimsalimia na kumsemeza kwa tabasamu akimwambia: "Wewe unaonekana ni mgeni katika mji huu." Kisha akamwambia kwamba, kama una haja yoyote ile, basi sema tukutatulie haja yako". Mtu huyo alilia na kujibu kwamba, Mungu ndiye anayejua zaidi mahali pa kuuweka Utume wake. [243] Katika Dua zinazonasibishwa na Khawaja Nasir Al-Din Tusi, ambapo yeye alimsifu Imam Zaman (a.s), kwa sifa mbali mbali, amesema kwamba sifa ya Halim aliyonayo Imam Zaman (Imamu Mahdi) (a.s) ameirithi kutoka kwa Imamu Hassan (a.s).

Alikuwa ni maarufu kwa ukarimu na kusaidia watu

Vyanzo vya Kiislamu vimesifu Imam wa pili wa Mashia kuwa; Ni mtu mwenye mkono mkunjufu na mkarimu, na kumpa jina la Jawadun (Mtoaji) na Sakhiyyun “Mkarimu”. [244] Imenukuliwa kwamba; Yeye mara mbili alijitolea kwa kutoa mali yake yote kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. Na mara tatu alijitolea kwa kuigawa mali yake nusu mbili, kisha nusu moja akaitoa kuwapa watu wasiojikimu kimaisha. [245] Katika kitabu Al-Manaqib cha Ibn Shahar Ashob, imeelezwa kwamba; katika safari ya Imam Hassan (a.s) kwenda Syria, Mu'awiyah alimpa hati iliyosajiliwa ndani yake shehena ya mali nyingi mno. Na pindi tu alipotoka kwa Muawiyah, mtumishi wake mmoja akamkarabatia viatu vyake na baada ya kufanya hivyo, Imam akamkabidhi hati hiyo iliyojaa shehena za mali mbali mbali. [246] Pia inasemekana kwamba siku moja Imam Hassan (a.s.) alimsikia mtu mmoja akimuomba Mungu ampe dirham elfu kumi. Imamu Hassan (a.s) akaenda nyumbani kwake kisha akampatia kiwango hicho alichokuwa akikiomba. [247] Inasemekana kwamba kutokana na ukubwa wa ukarimu, yeye alipewa lakabu ya “Karim Ahl al-Bayt”. [248] Ila ibara hiyo haikunukuliwa ndani ya Hadithi yoyote ili.

Vile vile kuna ripoti zinazoashiria kusaidia kwake watu, hata imepokewa kwamba; alikuwa akiacha I'tikafu na Tawafu nusu-nusu ili kwenda kuwatimizia watu haja zao, na sababu hasa ya kufanya hivyo, ni Hadith ya Mtume (s.a.w.w), isemayo kwamba; "Mtu yeyote yule anayetimiza mahitaji ya ndugu yake Muumini, ni sawa na mtu ambaye anayefanya ibada kwa muda miaka mingi. [249]


Aliamiliana na wasaidizi wake kwa unyenyekevu

Imesemekana kwamba siku moja alikuwa akuwa juu ya farasi wake akakutana na maskini ambao walikuwa wakila vipande vya mkate. Walipomuona, walimualika kula chakula pamoja nao. Akashuka kutoka kwenye farasi wake na kula mikate pamoja nao na wote wakashiba. Kisha akawaaga nyumbani na akawapa chakula na nguo. [250] Vile vile imesimuliwa kwamba mmoja wa watumishi wake alifanya kosa lililostahiki adhabu. Mtumishi huyo akamsomea Imam Hassan (a.s) Aya isemayo: «والعافین عن الناس» “Na wenye kuwasamehe watu.” Hassan bin Ali (a.s) akasema: “Nimekusamehe". Mtumishi akaendelea: «الله یحب المحسنین» “Na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema.” Imam Mujtaba (a.s) akamwambia: Wewe uko huru katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nitakupa mara mbili ya mshahara niliokuwa nakupa. [251]

Urithi Unaohusiana na Masuala Kiroho

Mkusanyiko wa maneno ya Hassan bin Ali (a.s.) umekusanywa katika kitabu cha Musnad al-Imam al-Mujtabi.

kuna karibu ya Hadith 250 katika nyanja mbamimbali zilizosimuliwa kutoka kwake. [252] Baadhi ya Hadith hizo ni kutoka kwake yeye mwenyewe (a.s) na baadhi ya nyingine amezinukuu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Imamu Ali pamoja na bibi Fatima Zahraa (a.s). [253]

Maneno yaliyonukuliwa kutoka kwake pamoja na barua zake, yamerikodiwa katika kitabu Musnad Al-Imam Al-Mujtabi (a.s). Maneno hayo yamerikodiwa pamoja na mlolongo wa wapokezi wake, nayo yamekuja katika mfumo wa khutba, mawaidha, mazungumzo tofauti, dua, mijadala, masuala ya kidini na kifiqhi. [254] Pia katika kitabu Balaghatul Imam Hassan, kuna Hadithi na mashairi yaliyonasibishwa na Imam Mujtaba (a.s).

Ahmadi Mianji, ameorodhesha barua 15 kutoka kwa Hassan bin Ali (a.s.), katika kitabu chake kiitwacho Makatib Al-a-immah, ambapo barua alimwandikia Muawiya, barua 3 zinahusiana na Ziyad bin Abayyah, barua moja kwa watu wa Kufa, na barua moja kwa Hassan Al-Basri. [255] Vile vile Ahmadi Mianji amekusanya idadi 7 za wosia kutoka kwa Imam Hassan (a.s) kwenda kwa Imamu Hussein (a.s.), Muhammad Hanafiyah, Qasim bin Hassan na Junada bin Abi Umayyah. [256]

Azizullah Ataardi amekusanya majina ya watu 138 ambao wamesimulia Hadhithi kutoka kwa Imam Mujtaba (a.s). [257] Sheikh Tusi pia ameratibu idadi ya watu 41 aliyowarikodi kama ni masahaba na wafuasi wake (a.s). [258]

Utamaduni na sanaa

Nafasi ya Imam wa pili wa Shia ana nafasi kubwa yenye kustahiki kuhimidiwa, katika nyanja tofauti za kitamaduni, zikiwemo sherehe kadhaa za kidini na kazi za sanaa. Baadhi yake ni kama ifuatavyo:

Karamu ya Imam Hassan

Moja ya mila za kidini nchini Iran ni karamu ya Imam Hassan (a.s), ambapo sadaka hutolewa kama nadhiri ya watu kukubaliwa muradi na maombi yao. Rikodi ya historia ya kuanzishwa kwa aina kama hiyo ya karamu, inarudi kabla ya zama za utawala Safawiyyah. Rangi ya chakuka kwenye karamu hii hupaswa kuwa na rangi ya kijani kibichi. Karamu hiyo huliwa baada ya kuomboleza maombolezo ya kifo cha Imam Hassan (a.s). Karamu hii ni maarufu na ina nafsi kubwa zaidi katika jamii ya wanawake. Mbali na vyakula mbalimbali vya rahisi na vilivyozoeleka katika karamu hiyo, pia kwa kawaida huwekwa Qu'ran, mishumaa, mswala na pamoja na tasbihi, kama ni nembo ya dini. [264]

Kongamano la Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w)

Kongamano la Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), lilifanyika mjini Tehran mwezi Julai 2014 kupitia Baraza la Dunia la Ahlul-Bait na jumuiya nyingine kadhaa. Katika kongamano hili, kati ya takriban makala 130 zilizopokelewa, makala 70 zilichaguliwa kwa ajili ya kuchapishwa na kusambazwa. 266]

Filamu ya kamanda mpweke zaidi

Filamu ya Kamanda Mpweke Zaidi mnamo, ya mwaka 1375. Ilitangazwa kwenye Idhaa ya Kwanza ya TV, ilionyesha maisha ya Imam Hassan (a.s) na riwaya ya suluhu na Mu'awiyah na hali za jamii ya Kiislamu na Mashia ya wakati wa uhai wake na muda mfupi baada ya kifo chake cha kishahidi. [267]

Orodha ya maandiko na vitabu

Makala kuu: Orodha ya vitabu kuhusu Imam Hassan (a.s)
Mkusanyiko wa makala zilizochapishwa katika juzu nne juu ya Mjukuu wa Mtume

Kuna vitabu na makala nyingi zimechapishwa kuhusu Imam Hassan (a.s). Takriban kuna vitabu 130 vilivyochapishwa na kuandikwa kwa kwa lugha za Kiajemi, Kiarabu, Kituruki na Kiurdu. Vitabu hivyo vimeorodhesha na kusajiliwa katika makala yaliyoandikwa kwa jila la "Kitabshenasiy Imam Mojtabi (a.s)". [268]

Baadhi ya maandiko muhimu zaidi juu ya kazi hizo ni:

  • Akhbar Al-Hasan bin Ali (a.s), kilichoandikwa na Suleiman bin Ahmad Tabarani (aliyefariki mwaka 360 AH)
  • Al-Hayat Al-Siyasiyah Lil Imam Al-Hasan kilichoandikwa na Jafar Murteza Ameliy
  • Hayatu Al-Imam Al-Hasan bin Ali (a.s) cha Baqir Sharif Qurashiy
  • Sulhu Al-Hasan (a.s) kilichoandikwa na Razi Aal Yaasiin, ambacho Ayatollah Sayyied Ali Khamenei alikitafsiri kwa Kiajemi mwaka 1348 kwa jina la "Porshukuuhtarin Narmesh Qahremanane Tarekh"
  • Zindegi Imam Hassan (a.s) cha Hashim Rasoli Mahallatiy
  • Al-Hassan bin Ali Dirasatu Tahliiliyyah cha Kaamil Suleiman
  • Al-Imamu Al-Hassan wa Nahju Al-Binaa Al-Ijtima'i kilichoandikwa na Hasan Musa Al-Saffaar
  • Haliim Ahlu Al-Bait kilichoandikwa na Musa Muhammad Ali
  • Al-Imam Al-Mujtaba (a.s) Mahjatu Qalbi Al-Mustafa (s.a.w.w) kilichoandikwa na Ahmad Rahmani Hamdani na kutafsiriwa na kufupishwa na Hussein Ustad Wali, kilichochapishwa na Taasisi ya Munir mwaka 1392 Shamsia.
  • Farhange Jaami'i Imam Hassan Mujtaba (a.s) kilichoohaririwa na kundi la wataalamu wa Hadith la taasisi ya utafiti ya Baqiril Uluum na kutafsiriwa na Ali Muayyidiy.
  • Pia, kuna mkusanyiko wa makala zilizochaguliwa katika "Kongamano la Sabbat Al-Nabi" yaliochapishwa katika juzuu tatu.
  • Haqaaiqi Penhaan: Ni kitabu juu ya utafiti kuhusu maisha ya kisiasa ya Imam Hassan Mujtab (a.s) kilichoandikwa na Ahmad Zamani, na kuchapishwa na Taasisisi ya Bustan Kitab Qom, toleo la 8 la 1394.

Vyanzo

  • Abū Yaʿqūb al-Sijistānī. Kitāb al-iftikhār. Published by Ismāʿīl Qurbān Ḥusayn Punāwālā. Beirut: 2000.
  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Edited by Sayyid Aḥmad al-Ṣaqar. Beirut: 1408 AH.
  • Āl Yāsīn, Raḍī. Ṣulh al-Ḥasan. Beirut: Aʿlamī, 1412 AH.
  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Tʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Amīnī, ʿAbd al-Ḥusayn. Al-Ghadīr fī al-kitāb wa al-sunna wa al-ʾadab. Qom: Markaz-i al-Ghadīr li-l-Dirāsāt al-Islāmīyya, 1416 AH.
  • Āmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Al-Ḥayāt al-sīyāsiyya li-l-Imām al-Ḥasan. Beirut: Dār al-Sīra, [n.d].
  • Aṭārudī, ʿAzīz Allāh. Musnad al-Imām al-Mujtabā. Qom: ʿAṭārud, 1373 SH.
  • Aḥmad b. Ḥanbal. Musnad al-Imām Aḥmad b. Ḥanbal. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • Balādhurī, Aḥmad b.Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Dār al-fikr, 1417 AH-1996.
  • Balādhurī, Aḥmad b.Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1397 Sh.
  • Bayḍāwī, ʿAbd Allāh ibn ʿUmar al-. Anwār al-tanzīl wa asrār al-taʾwīl. Beirut: Dār al-fikr, 1429 AH.
  • Dīyārbakrī, Ḥusayn. Tārīkh al-khamīs fī aḥwāl anfas al-nafīs. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • Dīnawarī, Aḥmad b. Dāwūd al-. al-Akhbār al-ṭiwāl. Qom: Manshūrāt al-Sharīf al-Raḍī, 1368Sh.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām wa wafayāt al-mashāhīr wa l-aʿlām. 2nd edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1409 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Al-Tafsīr al-Kabīr. Beirut: Dār al-Fikr, 1405 AH.
  • Ḥākim al-Nayshābūrī. Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Edited by Yusuf ʿAbd al-Raḥmān al-Marʿshlī. Beirut: 1406 AH.
  • Ḥalabī, Abu l-Faraj. Al-Sīra ḥalabīyya. 2nd ed. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1427 AH.
  • Ḥimawī Shāfiʿyī, Ibrāhīm b. Saʿd al-Dīn. Farāʾid al-samṭayn. Beirut: Muʾassisa al-Maḥmūd, 1400 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Qom: Raḍī, 1421 AH.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-balagha. Qom: Maktabat Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1385 Sh.
  • Ibn al-Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Aʿtham al-Kūfī, Aḥmad b. Aʿtham. Kitāb al-Futūḥ. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1411 AH-1991.
  • Ibn Bābawayh, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Al-Imāma wa al-tabṣira min al-ḥīra. Qom: 1363 Sh.
  • Ibn Khalkān, Aḥmad b. Muḥammad. Wafayāt al-aʿyān wa ʾanbāʾ ʾabnāʾ al-zamān. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1364 Sh.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. 2nd ed. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1418 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Published by Iḥsān ʿAbbās. Beirut: 1968-1977.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: Nashr-i ʿAllāma, 1379 Sh.
  • Ibn Ṣabbāgh Mālikī. Al-Fuṣūl al-muhimma. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1422 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jail, 1412 AH.
  • Ibn ʿAbd Rabbih. Al-ʿIqd al-farīd. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, [n.d].
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allah b. Muslim . Al-Imāma wa l-sīyāsa al-mʿrūf bi-tārīkh al-khulafāʾ. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Awḍāʾ. 1410 AH-1990.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, [n.d].
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Tafsīr al-Qurʾān al-ʿazīm. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1419 AH.
  • Iskāfī, Muḥammad b.ʿAbd Allāh. Al-Miʿyār wa al-muwāzina. Beirut: 1402 AH.
  • Jaʿfarī, Ḥusayn Muḥammad. Tashayyuʿ dar masīr-i tārīkh. Translated by Muḥammad Taqī Āyatullāhī. Tehran: Daftar-i Nashr-i Farhang-i *Islāmī, 1382 Sh.
  • Jaʿfarī, ʿAbbās. Guzārish-i congira-yi bayn al-milalī sibṭ al-nabī haḍrat-i imām Ḥasan Mujtabā. Qom: Khātam al-Anbīyāʾ, 1393 Sh.
  • Jaʿfarīyan, Rasūl. Ḥayāt-i fikrī wa sīyāsī-yi aʾimma. 6th ed. Qom: Anṣārīyān, 1381 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Furūʿ min al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1362 Sh.
  • Muḥammadī Rayshahrī. Dānishnāma-yi Imām Ḥusayn. Translated by Muḥammad Murādī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1430 AH.
  • Maghribī, Qāḍī Nuʿmān al-. Al-Manāqib wa al-mathālib. Beirut: al-Aʿlamī inistitute, 1423 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Ikhtiṣāṣ. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Masāʾil al-ʿukbariya. Edited by ʿAlī Akbar Khurasān Ilāhī. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamī li-Alfīyat al-Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Masār al-Shīʿa fī tawārīkh al-sharīʿa. Edited by Mahdī Najaf. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamī li-Alfīyat al-Shaykh al-Mufīd, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Tehran: Intishārāt-i Islāmiya, 1363 Sh.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Murūj al-dhahab wa maʿadin al-jawhar. Edited by Asʿad Dāghir. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Maqdisī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Al-Bidaʾ wa tārīkh. Port Said: Maktabat al-Thaqāfa al-Dīnīyya, n.d.
  • Muqaddasī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Barrasī wa naqd-i guzārishā-yi tārīkh-i shahādat-i Imam Ḥasan Mujtabā. Year 11. Fall and Winter, 1389 Sh.
  • Muqaddasī, Muṭahhar b. Ṭāhir. Bāzpazhūhī-yi tārīkh-i wilādat wa shahādat-i maʿṣūmān. Qom: Pazhūhishgāh-i ʿUlūm wa Farhang Islāmī, 1391 Sh.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī. Imtāʿ al-asmāʾ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1420 AH.
  • Mahdawī Dāmghānī, Mahmud and Baghistani Isma'il. Ḥasan b. Alī, Imām in Dānishnāma-yi jahān-i Islām. volume 13. Tehran: Bunyād Dāʾirat al-Maʿārif al-Islāmī, 1388 SH.
  • Naṣr b. Muzāhim Minqarī. Waqʿat Ṣiffīn. Qom: Manshūrāt Maktabat Āyatullāh Marʿashī al-Najafī, 1404 AH.
  • Nuwayrī, Aḥmad b. ʿAbd al-Wahhāb. Nihāyat al-ʾarab fī funūn al-ʾadab. Cairo: Dār al-Kutub wa al-Wathāʾiq al-Qawmīyya, 1423 AH.
  • Pīshwāyī, Mahdī. Tārīkh-i islām az saqīfa ta Karbalā. Qom: Dafter-i Nashr-i Maʿārif, 1393 Sh.
  • Qarashī, Bāqir Sharīf al-. Ḥayāt al-Imām al-Ḥasan. Beirut: Dār al-Balāgha, 1413 AH.
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm. Yanābīʿ al-mawadat li-dhi l-qurbā. 2nd edition. Qom: Uswa, 1422 AH.
  • Sulaym b. Qays. Kitāb sulaym b. qays al-hilālī. Qom: Hādī, 1405 AH.
  • Sayyid b. Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā al-. Kashf al-maḥajja li thamarat al-mahajja. Najaf: Maṭbaʿat al-Ḥaydarīyya, 1370 AH.
  • Sayyid al-Raḍī. Nahj al-balāgha. Translated by Sayyid Jaʿfar Shahīdī. ed 14th. Tehran: Intishārāt-i Ilmī wa Farhangī, 1378 Sh.
  • Sayyid Murtaḍā. Al-Shāfī fī al-imāma. 2nd ed. Qom: Muʾassisa-yi Ismāʿīlīyān, 1410 AH.
  • Sayyid Murtaḍā. Tanzīh al-anbīyā'. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, [n.d].
  • Shahīd Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Durūs al-sharʿīyya fī fiqh al-imāmīyya. 2nd ed. Qom: Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn, 1417 AH.
  • Shūshtarī, Qāḍi Nūr Allāh al-. Iḥqāq al-Ḥaqq wa Izhaq al-Bāṭil. Qom: Maktabaṭ Āyat Allāh al-Marʿashī, 1409 AH.
  • Shūshtarī, Muḥammad Taqī. Risālat fī tawārīkh al-Nabī wa al-Āl. Qom: Intishārāt-i Jāmiʿa-yi Mudarrisīn, 1423 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥaasn al-. Al-Rijāl. Edited by Jawād Qayyūmī al-Iṣfahānī. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1415 AH.
  • Ṭabāṭabā'ī, Mūhammad Ḥusayn. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Translated to Farsi by Mūsawī Hamidānī. Fifth edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1374 Sh.
  • Ṭabrisī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Al-Iḥtijāj. Mashhad: Nashr al-Murtaḍā, 1403 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1417 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʿrifa, [n.d].
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. 2nd edition. Beirut: Dār al-Turāth, 1387 AH.
  • Tirmidhī, Muḥammad b. ʿĪsā al-. Sunan al-Tirmidhī. published by ʿAbd al-Wahāb ʿAbd al-laṭīf. Beirut: 1403 AH.
  • Wilferd Madelung. The succession to Muhammad. Cambridge: 1997.
  • Wilferd Madelung. Jānishīnī-yi Muḥammad. Translated to Farsi by Aḥmad Nimāʾī and others. Mashhad: Bunyād-i Pazhūhishhā-yi Islāmī, 1377 Sh.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār Ṣādir, [n.d].
  • Zamānī Aḥmad. Ḥaqāyiq-i pinhān, pazhūhishī dar zindigānī-yi sīyāsī-yi Imām al-Ḥasan. Qom: Markaz-i Intishārāt-i Daftar-i Tablīghāt-i Islāmī, 1380 Sh.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Al-Kashshāf an ḥaqāiq ghawāmiḍ al-tanzīl. Second edition. Qom: Bilāghat. 1415 AH.