Nenda kwa yaliyomo

Al-Iradah al-Ilahi

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Matakwa ya Mwenyezi Mungu)

Al-Iradah al-Ilahi au Irada ya Kiungu (Kiarabu: الإرادة الإلهية) ni katika sifa thabiti za Mwenyezi Mungu na Mwenyezi ni Murid yaani mwenye irada. Maulamaa wa Kiislamu wana tofautiana kuhusiana na utambulisho wa irada ya Mwenyezi Mungu. Sheikh Mufid na Allama Tabatabai , miongoni mwa Maulamaa mahiri wa Kishia wanasema, irada ya Mwenyezi Mungu kuhusiana na Yeye ndio yale yale matendo ya Mwenyezi Mungu na irada Yake kuhusiana na wengine ni jambo la Mwenyezi Mungu; hata hivyo, Mu’tazilah na baadhi ya wanateolojia wa Kishia wanasema kuwa, irada ya Mwenyezi Mungu ni aina ya elimu yake.

Irada inagawanyika katika sehemu mbili, irada takwini (irada ya utashi wa kuumba) na tashri’i (utashi wa kisheria). Katika Aya za Qur’ani imezungumziwa pia irada takwini (utashi wa kuumba) na irada tashri’i (utashi wa kutunga sheria).

Nafasi

Iradah Ilahi ni katika sifa ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi ameitwa kuwa ni Murid yaani mwenye irada. [1] Katika Aya nyingi za Qur’ani Tukufu lmenasibishwa na irada na matakwa ya Mwenyezi Mungu; [2] Miongoni mwayo ni: (یعَذِّبُ مَنْ یشاءُ وَ یرْحَمُ مَنْ یشاءُ ; Humuadhibu amtakaye, na humrehemu amtakaye ) [3] na (إِنَّ رَبَّک فَعَّالٌ لِما یریدُ ; Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo). [4]

Irada ya Mwenyezi Mungu ni Nini?

Wanateolojia wa Kiislamu wana mtazamo mmoja kuhusiana na asili ya uwepo wa irada ya Mwenyezi Mungu, lakini wametofautiana kuhusiana na sifa maalumu pamoja na nukta zake za kina; [5] Miongoni mwazo ni: Irada ya Mwenyezi Mungu ni nini, kuwa ya dhati (asili) na kuwa kitendo irada ya Mwenyezi Mungu na kadhalika kuwa ya zamani au mpya irada ya Mwenyezi Mungu. [6]

Kwa mujibu wa Sheikh Mufid (aliyefariki dunia 413 Hijiria) [7] na Allama Tabatabai (aliyeaga dunia 1360 Shamsia), ni kwamba, irada ya Mwenyezi Mungu kuhusu matendo yake ni vile vitendo vyake (utashi wa uumbaji), na kuhusu matendo ya viumbe vingine, ni amri yake kwa matendo hayo ( utashi wa kutunga sheria). [8] Kwa msingi huo, "Mungu alitaka (alikuwa na irada) kumuumba mwanadamu", inamaanisha kwamba "Mungu alimuumba mwanadamu".[9] Kwa mujibu wa wawili hawa, irada ni moja ya sifa za kivitendo za Mwenyezi Mungu.[10] Sheikh Mufid aliuhesabu mtazamo na maoni haya kuwa yanaoana na rai ya Maimamu (a.s) na rai ya wanavyuoni wa Shia Imamiyyah.[11] Kuhusiana na hili, kumetumiwa pia hadithi kama hoja ya hilo; [12] na miongoni mwazo ni hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ambaye ametaja irada na matakwa ya Mwenyezi Mungu kuwa ni jambo la kutokea na sio la milele na la tangu na tangu. [13] Imam Kadhim (a.s) ameatambulisha irada ya Mwenyezi Mungu kuwa ni kile kile kitendo chake [14] ] na katika ibara ya Imamu Ridha (a.s) matkwa ya irada ya Mwenyezi Mungu imetambuliwa kuwa ni katika sifa za kivitendo za Mola Muumba. [15]

Kwa mujibu wa Allama Tabatabai, wanafalsafa mashuhuri kama Mulla Sadra wameihesabu irada na matakwa kuwa ni katika sifa za dhati na asili za Mwenyezi Mungu. [16] Kwa mujibu wa mtazamo mashuhuri baina ya wanafalsafa wa Kiislamu Iradadt Takwiniyah (utashi wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji) au ileile elimu ya Mwenyezi Mungu kwa vitendo mwafaka inawezekana kwa kwa nidhamu bora kabisa. [17] [18]. Kwa mtazamo wa Allama Tabatabai ni kuwa, kuitolea fasili na maana irada kuwa ni kuwa na elimu juu ya nidhamu bora sio sahihi na hakuna hoja ya hilo pia. [19] Kundi la Mu’tazilah na aktahri ya wanateolojian wa Kishia wanaamini kwamba, utashi wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji (الإرادة التكوينية) ni elimu yake kuhusiana na matendo ambayo yana maslahi na mwanadamu na viumbe wengine. [20] Kwa msingi huo basi kundi hili linaihesavbu irada kuwa ni katika sifa za dhati za Mwenyezi Mungu.

Kundi la Asha’ira lenyewe linaamini kwamba, irada ni tofautio na elimu na nguvu na sifa zingine za Mwenyezi Mungu; [22] lakini wanaitambua hiyo kuwa ni sifa ya dhati au ya ziada katika dhati, lakini kongwe na ya milele. [23] [24].

Tofauti ya Irada na Matakwa (Mashiyah)

Makala Asili: Matakwa

Inaelezwa kuwa, akthari ya wataalamu wa lugha na wanateolojia wanaona kuwa, Mashiyyah ina maana ya Irad [25] na wanaamini kwamba, irada na mashiyyat ni sifa moja; hata hivyo kundi jingine lenyewe linaona kuwa, kwa kuzingatia kuwa, Qur’an imetumia neno mashiyyah (matakwa) katika masuala ya tak’wini (uumbaji) hivyo irada na mashiyyah ni sifa mbili tofauti. [26] Ayatullah Makarem Shirazi anasema kuwa, uchunguzi kuhusiana na Aya za Qur’an unaonyesha kuwa, neno irada limetumika katika sehemu zote mbili za utashi wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji (الإرادة التكوينية) na utashi wa kisheria wa Mwenyezi Mungu (الإرادة التشريعية); lakini aghalabu hutumika katika masuala ya uumbaji na imetumika kidogo tu katika masuala ya utungaji sheria. [27]

Irada ya Utashi wa Uumbaji na Utashi wa Kisheria

Makala Asili: Utashi wa Uumbaji na Utashi wa Kisheria

Irada ya Mwenyezi Mungu imegawanywa katika sehemu mbili za Iradah Tak’wini (utashi wa Mwenyezi Mungu katika kuumba) na Iradah Tash’ri’i (utashi wa kisheria wa Mwenyezi Mungu. [30]Ayatullah Sobhani anasema, kama irada ya Mwenyezi Mungu itakuwa na suala la kutokea kitu, hujulikana kama irada ya utashi wa uumbaji. [32] Irada ya utashi wa kisheria ni mtu kutaka mtu mwengine afanye jambo fulani kwa irada ya hiari yake; kama vile Mwenyezi Mungu kutunga sheria za mambo ya wajibu na kiibada ambayo hufanywa na waja wake kwa irada yao binafsi au irada binafsi ya mtoto au hadimu kufanya jambo au kitu fulani bila ya mtu kumlazimisha. [33] Kwa maneno mengine ni kuwa, irada ya mtungaji sheria ya kufanywa amali au jambo fulani na mukallafu na hiari yake mwenye inajulikana kwa jina la Irada ya utashi wa kisheria au irada ya utashi katika utungaji sheria. [34]

Katika utashi wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu kila akitakacho Allah bila shaka hutokea; lakini katika utashi wa kisheria, kuna uwezekano wa kutokea ukiukaji. [36] Katika utashi wa kisheria tofauti na utashi wa uumbaji linalohusika pekee hapo ni matendo ya hiari. [37]

Utashi wa uumbaji na utashi wa kisheria umetumika sana katika Aya za Qur’an. [38] makusudio ya matakwa katika Aya kama za 82 Surat al-Nisaa, [39] Ayat Tat’hir, [40] aya ya 41 katika Surat al-Maidah, [41] Aya ya 5 ya surat al-Qasas, [42] na Aya ya 7 katika Surat al-Anfal [43] ni takwa la utashi wa uumbaji na makusudio ya irada katika Aya ya 185 ya Surat al-Baqarah, [44] Aya ya kwanza na ya sita ya Surat al-Maidah, [45] na Aya ya 7 ya surat al-Anfal [46] ni irada ya utashi wa kisheria.

Bibliografia

Kumeandikwa vitabu vya kujitegemea kuhusiana na irada na matakwa ya Mwenyezi Mungu na miongoni mwavyo ni:

  • Irade Khuda az didgah filosofan, motakalimin va muhadesin, mwandishi Ali Bedashti. [47]
  • Elm va Eradeh Elahi, mwandishi: Muhammad Hassan Qadardan Qaramalaki. [48]

Masuala Yanayo Fungamana

Rejea

Vyanzo