Aya ya Mawaddah

Kutoka wikishia

Aya ya Mawaddah (Kiarabu: آية المودة) ni sehemu ya Aya ya 23 ya Surat al-Shura, ambayo inasititiza ya kwamba; Malipo ya kazi ya Mtume (s.a.w.w) katika kutufikishia ujumbe wa Allah, ni kuwapenda mapenzi pekee Ahlul Bait wake (a.s) Kwa mujibu wa wafasiri wa Kishia, Aya hii inaashiria nafasi na umuhimu wa Ahlul Bait wa Mtume (s.a.w.w) katika suala zima la dini na jamii. Kwa mujibu wa riwaya zilizosimuliwa na wafasiri wa Kishia na Kisunni; Aya ya hii iliteremka baada ya kuhama Mtume (s.a.w.w) kutoka Makka kwenda Madina, ambapo kundi la Ansari lilimwomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.W) awape khabari iwapo kutahitajika mchango wao mali, ili watoe mali yao pale itakapohitajika na kumpelekea bwana Mtume (s.a.w.w).

Wanachuoni wa Kishia na baadhi ya wanazuoni wa Kisunni wakizingatia Hadith kadhaa kuhusiana na Ahlul-Bait, wamesema; Makusudio hasa ya neno “القربی” lililopo katika Aya hii ni Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w). Yaani ni Ali bin Abi Talib na bibi Fatima (a.s) pamoja na Maimamu wa Kishia ambao wanatokana na vizazi vyao. Allamah Tabaatabai akitoa ufafanuzi wake juu ya Aya hii amesema:, "Falsafa ya amri ya Mtume juu ya kuwapenda na kushikamana na Ahlul-Bait (a.s), ilikuwa na nia ya kuwaelekeza watu kwa Ahlul-Bait ili wasome kutoka kwao maana na tafsiri ya Qur’an pamoja na welewa wa dini yao.


Andiko la Aya na Tafsiri Yake

قُل لَّا أَسْأَلُکُمْ عَلَیهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِی الْقُرْبَی


...Sema na uwaambie: (Mimi sitaki ujira wowote ule kutoka kwenu kuhusiana na ujumbe ninaokuleteeni kutoka kwa Mola wenu, ila nakutakeni muwapende watu wa karibu yangu).



(Quran: 42: 23)


Nafasi ya Aya

Kwa mujibu wa mtazamo wa Mashia, Aya ya Mawaddah ni miongoni mwa Aya ziliteremshwa kuhusiana umuhimu na nafasi maalumu waliyonayo Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w), na inaashiria ulazima wa kuwapenda Ahlul-Bait (a.s). [1] Pia, wengine wanaihisabu Aya hii kama ni moja ya dalili za Uimamu na ubora wa Imamu Ali (a.s).

Maana ya Maneno

Neno Mawaddah «مَوَدَّه» lina maana ya upendo na mapenzi. [3] Miongoni mwa maana za neno hili zilizotajwa na Raghib Esfahani ni; Mapenzi yenye daraja ya juu kabisa pamoja na kuwepo mshikamano baina ya mpendwa apendwaye na mpenda apendaye. [4] Neno Qurba«قُربی» nalo lina maana ya jamaa wa mtu, anaohusiana nao kwa damu.

Sababu ya Kushuka kwa Aya

Wafasiri wa Kishia [6] na Kisunni [7] wamemnukuu Ibn Abbas akisema ya kwamba; Baada ya Mtume (s.a.w.w) kuhama kutoka Makka kwenda Madina, na baada ya kuimarika kwa misingi ya Uislamu, kundi la Ansari lilimwomba Mtume (s.a.w.w), ikiwa kutatokea tatizo linalohitaji mali, basi bila ya pingamizi yoyote ile, yeye achukuwe mali zao na kuzitumia katika kutatua tatizo hilo. Hapo ndipo iliposhuka Aya ya Mawaddah, ikiwaeleza ya kwamba; ujira wa bwana Mtume (s.a.w.w) ni wao kuwapenda Ahlul-Bait wake (a.s) na sio kutoka mali zao na kumpa yeye.

Mifano Hai ya Qurba

Mtazamo wa Shia

Wanachuoni wa Kishia wakitegemea Hadithi kadhaa, wanaamini ya kwamba; Makusudio ya «القربی» yaliokusudiwa katika Aya ya Mawaddah ni Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w). Yaani Ali na Fatima (a.s) pamoja na Maimamu 12 wanaotokana na katika kizazi chao. Kwa mujibu wa tafsiri hii, maana ya “Al-Mawaddah fi Al-Qurba” «المَوَدَّةَ فِی الْقُرْبَی» ni kuwapenda Ahlul-Bait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.W). [8] Kupitia mtazamo wa Fadhlu bin Hassan Tabrasi, ni kwamba; Kuna Hadithi mutawaatir -zilopokewa kupitia njia kadhaa, na sio kupitia njia ya mtu mmoja tu- kutoka pande zote mbili za Shia na Sunni, zinazotia mkazo wajibu wa kuwapenda Ahlul-Bait (a.s). Hadithi hizo ni miongoni mwa dilili zinazotilia mkazo maoni ya tafsiri hiyo. [9] Pia, kuna Hadithi nyingi zitokazo kwa Maasumina (watu waliotakaswa) kuhusiana na tafsiri ya Aya hiyo. Miongoni mwazo ni kama ifuatavyo:

  • Baada ya Imamu Hussein (a.s) kuuliwa baba yake kishahidi (Imam Ali (a.s)), yeye aliwahutubia watu, na miongoni mwa maneno aliyoyasema ni kwamba: "Sisi ni miongoni mwa Ahlul-Bait na ni familia ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni wajibu kwa kila Muislamu kuipenda. Ambapo Mwenyezi Mungu amesema: «قُلْ لا أَسْئَلُکُمْ عَلَیْهِ أَجْراً إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِی الْقُرْبی...‏» ; "Sema, (ewe Muhammad)``Sikuombeni ujira isipokuwa nakutakeni muwapende watu wangu wa karibu."[10]
  • Imamu Sajjad (a.s.) aliulizwa kuhusu Aya ya Mawaddah, na Imamu (a.s) naye alijibu kwa kusema: "Maana ya Aya hii ni kutupenda sisi Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w). [11]
  • Imepokewa kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) kwamba; Maimamu watoharifu (Maasumina) ndio mfano hai wa Aya ya Mauddah. [12]

Mtazamo wa Kisunni

Wanazuoni wa Kisunni wamekhitalifiana juu ya tafsiri na mifano hai ya «قربی» (watu wa karibu); Hakim Hasakani, mmoja wa wanazuoni wa Kisunni wa karne ya 5 Hijiria, katika kitabu chake Shawahidu Al-Tanzil, amesimulia riwaya saba ambazo kwa mujibu wake makusudio ya «القربی» yatakuwa ni Imamu Ali, bibi Fatima na Hassanein (Hassana na Hussein) (a.s). [13] Pia kwa mtazamo wa Zamakhshari, neno «القربی» halina maana ya ukaribu wa damu, bali ni ujamaa na udugu. [14] Hivyo basi, Mwenyezi Mungu atakuwa amemuamuru Mtume wake (s.a.w.w) awatake Maquraishi, ikiwa hawamuamini, basi angalau wauheshimu udugu na ujamaa uliopo baina yao na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). [15] Alousi anaamini wajibu wa kuwapenda Ahlul-Bait unajumuisha jamaa wa Mtume pamoja na watoto wote wa Abud Al-Muttalib. [16] Ukiachana na kile alichokisema Alousi, ambaye ni mmoja wa wafasiri wa Kisunni, pia kuna mitazamo mengine isiyokuwa hiyo. Kuna waliosema kwamba aliyekusudiwa katika neno «قربی» ni bibi Amina, mama wa Mtume (s.a.w.w). [17] Pia kuna waliosema ya kwamba; Kiinachokusudiwa katika Aya hiyo ni Waislamu kuwapenda jamaa na ndugu zao, kwa maana ya kuunga udugu. [18]

Falsafa ya Kuwapenda Ahlul-Bait (a.s)

Sayyied Muhammad Hussein Tabatabai, mmoja wa wafasiri wa Kishia, akitegemea baadhi ya Hadithi kama vile Hadithi ya Thaqalain (Hadithi yenye kuzungumzia vizito viwili navyo ni Qur'ani na Ahlul-Bait) na Hadithi ya Safina (Jahazi), ameyahisabu mapenzi juu Ahlul-Bait, kuwa ni wajibu juu ya kila Muislamu. Wajibu huo unatokana na kule wao kuwa ndio kimbilio na rejeo tegemezi la watu la kielimu. Ambapo kuwapenda Ahlul-Bait kutapelekea kubaki na kuendelea ujumbe aliokuja nao Mtue Muhammad (s.a.w.w). Ingawaje mapenzi kwa Ahlul-Bayt yanaitwa kuwa ni "malipo", ya ujumbe wa bwana Mtume (s.a.w.w), ila faida za mapenzi hayo zinamrudia mwadamu mwenyewe, na sio kwamba kuna faida wanayoipata Ahlul-Bait (a.s). [19] Mfano wa Aya hiyo ni kama wa Aya ya 47 ya Surat al-Sabai ambapo ndani Aya hii imeelezwa ya kwamba; Ujira kwa ajili ya ujumbe wa Allah unawarudia Waislamu wenyewe. [20]

Tafiti Husika

Kitabu «Mu'utayat Ayatu Al-Muwaddah» kilichoandikwa na Sayyied Mahmud Hashimiy Shahrudiy; Mohammad Hossein Bayatiy amekifasiri kitabu hichi katika lugha ya Kiajemi kwa la "Darshaye az Aye Muwaddat". "Mahrvarzi Ahl-Al-Bait (a.s) az Diidgahe Qu'ani wa Sunnat" kilichoandikwa na Ali Hosseiniy Milaniy; caha ya Intisharate Markaze Haqaaiq Islamiy. Kitabu hichi kilichapishwa mnamo mwaka 1389 Shamsia kikiwa na idadi ya kurasa 248. [21] "Fardhu Al-Mahabbah fi Tafsiri Ayatu Al-Mawaddah" kilichoandikwa na Shihabuddin Khafaajiy, bwaba Ali Raad amekitafsiri kitabu hichi kwa ya Kiajemi kwa jina la «Mawaddate Ahlul-Bait dar Aineye Wahyi». Tafsiri hii ilichapishwa mwaka wa 2004 kwa juhudi za Taasisi ya Uchapishaji ya Behnashr. «Mudat Ahlu Al-Bait (a.s)» kilichondikwa na MUhammad Mohssien Haji Haidarii; Kitabu hiki kilichapishwa na shirika la uchapishaji la Aaraste mwaka wa 1392 Shamsia, kikwa na kurasa 188. [22]