Nenda kwa yaliyomo

Miqdad bin Amru

Kutoka wikishia

Miqdad bin Amru, anayejulikana pia kama Miqdad bin Aswad (aliyezaliwa mwaka 33 Hijiria), alikuwa miongoni mwa masahaba wakubwa wa bwana Mtume (s.a.w.w) na ni miongoni mwa Mashia (wafwasi) wa kwanza wa Imam Ali (a.s). Miqdad alisilimu mwanzoni mwa Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) naye alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kudhihirisha Uislamu wao. Alishiriki katika vita vyote vya mwanzo vya Uislamu. Miqdad hutajwa na kusifiwa sambamba na Salman Farsi, Ammar bin Yasir na Abu Dharr kama ndiwo Mashia wa kwanza wa Imam Ali (a.s) ambao walijulikana kwa jina hilo (la Shia) hata wakati wa Mtume (s.a.w.w).

Baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w), Miqdad alimuunga mkono Imam Ali (a.s) katika kutetea haki ya nafasi ya ukhalifa wa Imamu Ali, na hakukubali kutoa kiapo cha utiifu cha kumtambua Abu Bakar kama na khalifa baada ya bwana Mtume (s.a.w.w). Yeye alikuwa miongoni mwa watu wachache waliohudhuria mazishi ya Bibi Fatima (a.s). Miqdad anachukuliwa kuwa mmoja wa wapinzani wakubwa wa ukhalifa wa Othman. Katika Hadithi za Ahlul Bayt, Miqdad anatajwa kwa sifa njema kabisa, pia anajulikana kama ni mmoja wa watu watakaorudi tena duniani wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.s). Kuna Hadithi kadhaa zinahusishwa na nukuu za Miqdad kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w).

Maisha yake

kuanzia kuzaliwa kwake hadi nasaba yake

Hakuna taarifa zilizopatika au kurikodiwa kuhusiana na tarehe ya kuzaliwa kwa Miqdad bin Amru bin Tha'laba anayejulikana pia kama Miqdad bin Aswad. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba; wanahistoria wamekadiria mwaka wa kifo chake kuwa ni mwaka wa 33 Hijiria, ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 70, [1] hivyo basi yawezekana kwamba yeye alizaliwa miaka wa 24 kabla ya utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), yaani ni miaka 37 kabla ya Hijra. Wnahistoria wametaja nasaba yake ya kifamilia hadi kufikia mababu ishirini. [2]

Inasemekana kwamba siku moja kulitokea ugomvi mjini Hadarimout, kati ya Miqdad na mtu mmoja aitwaye Abu Shimru bin Hajar, ambao ulisababisha majeraha kwa mtu huyo. Baada ya tukio hilo, Miqdad alikwenda Makka na akaungana na Aswad bin Abdu bin Yaghuthi al-Zahri, ambapo katika tukio hili, Miqdad alipata nasabu ya yeye kunasabishwa nasaba ya ubaba kwa bwana Aswad. Hivyo basi kuanzai hapo yeye, aliitwa Miqdad bin Aswad pia wakati mwingine aliitwa Miqdad al-Zahri. Hata hivyo, baada ya kushuka Aya isemayo (ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ) ; Waiteni kwa [majina] ya baba zao, [3] Kuanzia hapo Miqdad aliinza kuitwa Miqdad bin Amru. [4]

Majina ya kunia na lakabu

Miqdad alipewa majina kadhaa ya lakabu, nayo ni kama vile; Bahrai au Bahrawi, Kindi na Hadrami. [5] Kwa upande wa majina ya lakabu, yeye alijulikana kwa majina tofauti kama vile; Abu ma'abad, Abusaid na Abu al-Aswad yametajwa. [6]

Familia yake

  • Mke: Mke wa Miqdad alikuwa ni; Dhubaa’ah binti wa ami ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni binti wa Zubair bin Abdulmuttalib. [7] Inagwa Dhubaa’ah kinasaba alikuwa ni mwanamke mwenye nasaba ya daraja za juu, ila bwana bwana Mtume (s.a.w.w) alimfanya Dhababah kuwa mke wa Miqdad. Katika tukio hili bwana Mtume (s.a.w.w) akasema: "Sikumfanya binti ya ami yangu Dhababah kuwa ni mke wa Miqdad, isipokuwa nimefanya hivyo ili watu warahisishe masuala ya ndoa, na weweze kumwozesha binti yao kila Muamini, na wala wasiangaze masuala ya nasaba katika ndoa".[8]
  • Watoto: Miqdad alikuwa na watoto wawili, Abdullah na Karima. Katika vita vya Jamali, Abdullah alikuwa ni miongoni mwa watu wa kundi la Aisha waliopambana dhidi ya Imam Ali (a.s), naye aliuawa katika vita hivyo. Baada kumalizika kwa vita hivyo, Imam Ali (a.s) alipoina maiti ya Abdullah, alaliielekea maiti ya Abdullah na kuiambia: "Ulikuwa ni mwana mbaya wa dada."[9] Wengine badala ya jina la Abdullah, walimtambua mtoto huyu wa Miqdad kwa jina la Ma'abad. [10]

Kifo na mahali alipozikwa

Miqdad katika maisha ya uzeeni mwake aliishi katika kitongoji cha "Jaraf" (eneo ambalo liko umbali wa maili moja kutoka Madina kuelekea ardhi ya Sham). Miqdad alifariki dunia mnamo mwaka wa 33 Hijiria alipokuwa na umri wa miaka 70. [11] Waislamu waliupeleka mwili wake Madina na Othman bin Affan akausalia mwili huo na hatimae akazikwa katika mava ya Baqi'. [11] Pia katika mji wa Van nchini Uturuki kuna kaburi linalohusishwa na Miqdad, ambalo baadhi ya wanazuoni wamelihusisha kaburi hilo na Faadhil bin Miqdad au mmoja wa masheikh wa Kiarabu aliyekuwa akiishi katika mji huo. [12] Kulingana na Hadithi, Miqdad alikuwa mtu tajiri na katika wasia wake aliandika akiusia ya kwamba; dirhamu 36,000 kutoka katika mali yake zitolewe kwa ajili ya kupewa Hasan na Hussein (a.s). [13]

Wakati wa Mtume

Kusilimu kwake

Miqdad bin Amru (r.a) aliingia Uislamu tokea zama za awali za Utume wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuvumilia mateso ya makafiri wa Kiquraish. Wanahistoria wanamchukulia kama ni mmoja wa watu wa mmwazoni (al-Sabiquna) kabisa katika Uislamu; lakini hakuna maelezo ya kina kuhusiana na jinsi yay eye alivyoingia katika Uislamu. Imenukuliwa kutoka kwa Abdullah bin Mas'ud ya kwamba; Miqidad ni miongoni mwa watu saba kwanza kabisa kudhihirisha Uislamu wao mbele ya jamii. [14]

Uhamiaji na harakati za kuhajiri

Miqdad bin Amru (r.a.) alihama mara mbili kutoka sehemu moja kwenda nyengine: mara moja ni safari yake ya kuhamia Habasha, ambapo Miqdad alikuwa miongoni mwa kikundi cha tatu cha Waislamu kilichoelekea Habasha, na mara ya pili ni safari ya kuhamia Madina, ila mudai halisi wa uhamiaji kwake kwenda Madina haukubainika; lakini kwa kuzingatia kuwepo kwa dalili nyingi, yaonekena kwa yeye alielekea mji huo katika mwaka wa kwanza wa Hijiria, ndani ya mwezi wa Shawal katika kikosi cha Abu Ubaida, ambapo alijiunga na Waislamu wengine na akahamia Madina pamoja nao. [15]

Ushirikiano wake katika vita

Miqdad alishiriki katika vita vyote vya bwana Mtume (s.a.w.w) na alikuwa miongoni mwa mashujaa wa masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w). [16] katika vita vya Badri, Miqdad alikuwa katika kikundi cha jeshi la wapanda farasi vitani humo. Farasi wake alijulikana kwa jina la "Sabha", likimaanisha "mwogeleaji". Yawezekana kuwa alipewa jina hilo kwa sababu kule Miqdad kupigana kwa ushupavu na ujasiri, yaani ni kama vile yeye alikuwa akivikogo vita pale alipokuwa vitani. [17]

Pia Miqdad alishika jukumu muhimu katika vita vya Uhud, kwani mwishoni mwa vita wakati kila mtu alipokimbia, kulingana na vyanzo vya kihistoria, hakubaki mtu yeyote yule pamoja na Mtume (s.aw.w), isipokuwa Ali (a.s), Talha, Zubair, Abu Dujana, Abdullahi bin Mas'ud, na Miqdad. [18] Baadhi ya Hadithi zimemtaja Miqdad katika vita hivi kama mmoja wa wapiga mishale wa jeshi la Waislamu. [19] Hata hivyo, wengine wanamchukulia kuwa yeye alisimama sambamba na Zubair akiwa ni kamanda wa wapanda farasi wa jeshi la Waislamu. [20]

Miqdad pamoja na Salman, Ammar, na Abu Dhar walikuwa ni miongoni mwa Mashia wa kwanza ambao walijulikana kwa jina hili tokea zama za bwana Mtume (s.a.w.w). [21]

Utetezi wake katika kuunga mkono Ukhalifa wa Imam Ali (a.s)

Baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuchaguliwa kwa Abu Bakar kama ni khalifa na mrithi wa nafasi ya bwana Mtume(s.a.w.w), ni idadi ndogo ya Waislamu walimbakia kuwa ni waaminifu kwa Imamu Ali (a.s) ambao hawakukubali kutoa kiapo cha kumtambua Abu bakar kama ni khalifa wa Waislamu. Miongoni mwao walikuwa Salman, Abu Dhar, na Miqdad. Muqdad hakushiriki katika tukio la Saqifa bali alikuwa pamoja na Amirul Muminiin (a.s.) akiungana na baadhi ya masahaba katika kazi na wajibu wa kuosha maiti ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kisha kuisalia maiti hiyo takatifu. [22] Kulingana na maelezo ya Hadithi; Yeye ni miongoni mwa Waislamu wachache walio usalia wa mwili wa bibi Fatima (a.s). [23] Baadhi ya vyanzo vinamchukulia kuwa alikuwa mmoja wa kikosi cha Shurtatu al-Khamis (شُرْطَةُ الخَمیس). [24] [Maelezo 1]

Miqdad katika hali tofauti, alikuwa akijitahidi kuwakumbusha kwa Abu Bakar na wafwasi wake juu ya suala la ukhalifa wa Imam Ali (a.s) pia alichukua hatua kadhaa katika kuwaelimisha watu juu ya suala hilo. Baadhi ya vitendo na shughuli za Miqdad katika utetezi wa Ali (a.s) ni kama ifuatavyo:

  1. Baada ya watu kumpa Abu Bakar kiapo cha kumtambua kwama ni khalifa wa Waislamu, kikundi cha Muhajir na Ansar walikataa kumuunga mkono Abu Bakar, na badala yake walijiunga na Ali (a.s.) ambapo mmoja wao alikuwa ni Miqdad. [25]
  2. Wakati kikundi cha watu 40 walipoenda kwa Imamu Ali (a.s), na kumwambia kwamba; “Sisi tuko tayari kupigana na kukulinda.” Imam Ali (a.s.) aliwajibu akisema: "Kama kweli muko tayari kusimamia kauli yenu hii, basi nendeni kisha kesho muje hapa hali kimmoja wenu akiwa ni kipara (ameshanyoa nwele zake).” Kesho ilipofika hakuhudhuria isipokuwa; Salman, Miqdad na Abu Dhari, ambao walifika wakiwa tayari wameshanyoa nyewe zao. [26]
  3. Katika mchakato wa uchaguzi wa Khalifa kupitia kikosi cha watu sita, wakati Abdurrahman bin Auf alipo mwambia Imamu Ali (a.s) "Nitakupa kiapo cha utiifu iwapo tu utakubali kutafuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sunna za Mtume (s.a.w.w), na kupitia njia na sunna za Abu Bakr," ambapo Imamu Ali (a.s), alikubali tu masharti mawili ya kwanza, Maqdad alimgeukia Abdurrahman na kusema: "Kwa jina la Mwenye Ezi Mungu, mmemwacha Ali, ambaye alikuwa akihukumu kwa haki na uadilifu." Kisha akaendelea akisema: "Sijaona mtu au familia yoyote iliyodhulumiwa na kukandamizwa baada ya kuondokewa na Mtume wao kama walivyodhulumiwa Ahlul-Bayt (a.s)." [27]

Maqdad alipingana na ukhalifa wa Othmani na kutangaza kukataa kwake kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye Msikiti wa Madina. [28]

Ya'aqubi ambaye ni mmoja wa wanahistoria wa Kiislamu, akinukuu kutoka kwa baadhi ya watu ya ameswma kwamba; Othmani, katika usiku huo huo aliotawalishwa ndani yake, alitoka kwa ajili ya Sala ya Isha, huku mbele yake kukiwa na mshumaa unaowaka, Maqdad bin Amru akamwandama na kuwambia: “Huu ni uzushi gani tena? [29] Kulingana na maelezo ya Ya’aqubi, Miqdad alikuwa ni mdadisi na mkosoaji dhidi ya Othmani, na hakukubali kuungana na Othman, na badala yake akashikamana na Imamu Ali (a.s). [30]

Miqdad katika hadithi za Ahlul Bait (a.s)

Kuna Hadithi nyingi kuhusiana na Miqdad zilizonukuliwa kutoka kwa Ma'asumina (a.s), ambazo nyingi miongoni mwazo, zinazungumzia sifa zake, khulka zake njema pamoja na imani yake. Baadhi ya Hadithi hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Upendo wa bwana Mtume (s.a.w.w) kwa Maqdad: Bwana Mtume (s.a.w.w) amesema: "Mungu ameniamrisha kuwa na rafiki na watu wanne. Mtu mmoja miongoni wa masahaba aliuliza kwa kudadisi ili kuwajuwa watu hao: Bwana Mtume (s.a.w.w) naye akamjibu kwa akasema: "Ni Ali, Salman, Maqdad na Abu Dharri." [31]
  2. Kuingia Peponi kwa Miqdad: Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (r.a) ya kwamba; siku moja Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) alisema: "Pepo inawatamani watu wanne kutoka katika umma wangu, na pale Ali (a.s) alipomuuliza bwana Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na watu hao, bwana Mtume (s.a.w.w) alimjibu akisema: " Naapa kwa jina la Mwenye Ezi Mungu kwamba; wewe ndiye wa kwanza wao na wale watatu wanaofuatia ni; Miqdad, Salman na Abu Dhar." Pia Imam Sadiq (a.s) katika tafsiri ya Aya isemayo: ((إِنَّ الَّذِینَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ کانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا)) [32] Alisema kwamba: Aya hii imeteremka kuhusiana na Abu Dhar, Miqdad, Salman na 'Ammar. [33]
  3. Imani yake: Imepokewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) ya kwamba: Imani ina daraja kumi, katika daraja hizo, Miqdad yupo katika daraja ya nane na Abu Dhar katika daraja ya tisa na Salman katika daraja ya kumi. [34]
  4. Kushikamana na amri ya Aya ya Mawaddah: Imamu Swadiq (a.s) kuhusiana na Aya ya Mawaddah isemayo قُل لا أَسئَلُکم عَلَیْهِ أَجْراً إِلاَّ المَوَدَّةَ فِی القُربی)) [35])) amesema: Naapa kwa jina la Mwenye Ezi Mungu ya kwamba; hakuna mtu aliye ifanyia kazi Aya hii, isipokuwa watu saba, ambapo Miqdad ni mmoja miongoni mwao. [36]
  5. Miqdad ni miongoni mwa Ahlul Bait: Siku moja Jabir bin Abdullah Ansari aliuliza kuhusu Salman, Miqdad na Abu Dharri kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Bwana Mtume (s.a.w.w) naye alijibu moja baada ya jengine kuhusiana na maswali juu ya watu hao, na ilipofika zamu ya kujibu maswali yilohisiana na Miqdad alisema: "Maqdad ni mtu wetu sisi. Mungu ni adui wa yule ambaye ni adui wake na ni rafiki wa yule ambaye ni rafiki yake. Ewe Jabir! Kila unapotaka kuomba dua ambayo itakayojibiwa na Mwenye Ezi Mungu, basi omba dua yako kwa kumtaja yeye (Miqdad) ndani ya dua hiyo, kwani majina haya (ya Ahlu al-Bait pamoja na Miqdad) ni bora zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu". [37]
  6. Ushikamanifu wake kwa Imam Ali (a.s): Imam Baqir (a.s) amesema: Watu baada ya Mtume wa Mungu (s.a.w.w) walirudi nyuma kutoka katika njia na mwendo wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w) isipokuwa watu watatu: Salman, Abu Dhar na Maqdad. [38] Pia katika baadhi ya Hadithi, Miqdad ametambuliwa kuwa ndiye mfwasi mtiifu zaidi wa Imamu Ali (a.s) kuliko wengine. [39]
  7. Kufufuliwa kwa Maqdad katika zama za Imamu Mahdi (a.s): Kulingana na Hadithi; Miqdad ni miongoni mwa wali watakao fufuliwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.f), naye atakuwa ni miongoni mwa washirika na wakuu wa serikali ya Imamu Mahdi (a.s). [40]
  8. Ulazima wa kumpenda na kufanya urafiki na Miqdad: Imamu Swadiq (a.s) amesema: "Ni wajibu kwa Waislamu kuwapenda na kuwa na urafiki na watu ambao hawakupotoka baada ya kufariki bwana Mtume (s.a.w.w). Kisha akaorodhesha baadhi yao, ambao ni pamoja na Salman, Abu Dhar na Maqdad. [41]
  9. Kuwa na mke maalum Peponi: Siku moja bibi Fatima alimwambia Salman kwa kusema: "Siku moja baada ya kifo cha baba yangu, (Mtume wa Mungu (s.a.w.w)), ambapo ilikuwa ni wakati wa jioni, walikuja kwangu wanawake watatu warembo, wakaniambia kwamba wao ni wanawake wa Peponi, na majina yao ni Dharrah (ذرّه) ambaye ni kwa ajili Abu Dharri, Midudah (مقدوده) ambaye ni kwa ajili ya Miqdad na Salam (سَلمی) kwa ajili ya Salman. Wao Walisema kwamba Mwenye Ezi Mungu Mtukufu aliwaumba makhususi kwa ajili ya Abu Dhar, Maqdad, na Salman." [42]

Upokezi wake wa Hadithi

Miqadad alinukuu Hadithi kadhaa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Pia kuna wapokezi kadhaa wa Hadithi walionukuu Hadithi kutoka kwake, ambao miongoni mwao kama vile:

Bibliografia (seti ya vitabu kuhusiana na Wasifu wa Miqadad)

  • Kitabu cha Wasifu wa Miqadad (سیمای مقداد) kilicho andikwa na Muhammad Mahammediy Eshterhaardiy na kuchapishwa na Intishaarat Peyame Islam.
  • Kitabu cha Miqadad (مقداد) kilicho andikwa na Muhammad Kamrani Aqdam na kuchapishwa na Kitengo cha Uchapishaji cha Hadithi Ninawaan.
  • Kitabu cha Ilikuwa ni Miaka Migumu (سال‌های سختی بود) ambacho kinaelezea maisha ya Miqadad kwa njia ya visa (riwaya), kilicho ambatana na picha ndani yake. Kitabu hichi kiliandikwa na kuhaririwa na Kituo cha Afarinesh-haye Adabi na kuchapishwa na Surah Mehr.
  • Kitabu cha Miqadad bin Aswad al-Kindi, Mpamanaji wa Kwanza katika Uislamu (المقداد ابن الأسود الکندی أوّل فارس فی الإسلام) kilicho andikwa na Mohammed Jawad al-Faqih na kuchapishwa na Taasisi ya Al-A’alami ya Lebanon.
  • Kitabu cha Msururu wa Nguzo Nne (سلسلة الارکان الاربعة) vitabu hichi kimeandikwa katika nne, ambapo juzu ya tatu ya kitabu hichi, naangazia maisha ya Miqadad, nacho ni kitabu kilicho andikwa kwa lugha ya Kiarabu na Mohammed Jawad al-Faqih na kuchapishwa nchini Lebanon.
  • Kitabu cha Pamoja na Maswahaba na Taabiina (کتاب مع الصحابة و التابعین ). Kitabu hichi kimeandikwa na Kamal Sayyid katika juzu kumi nne, na juzu ya sita ya kitabu hichi inahusiana na Miqadad. Kitabu hichi kimeandikwa kwa Kiarabu na kuchapishwa na Kitengo cha Uchapishaji cha Ansariyan kilichoko Qom nchini Iran.

Maelezo

  1. Bila shaka, ikiwa kikosi cha askari waitwao Shurtatu al-Khamis (شرطة الخمیس) kiliundwa wakati wa utawala wa Imamu Ali (a.s), hatutawezi kumchukulia Miqdad kama ni mmoja wa wanachama wake, kwani mwaka wa kifo chake umeorodheshwa kama ni mwaka wa 33 Hijiria, na kuanza kwa utawala wa Imamu Ali ilikuwa ni mwaka wa 35 Hijiria.

Vyanzo

  • Amīn, Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan al-Amīn. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Ḥamīd Allāh. Egypt: Maʿhad al-Makhṭūṭāt bi-Jāmiʿat al-Duwal al-ʿArabīyya, 1959.
  • Ibn Abī l-Ḥadīd, ʿIzz al-Dīn b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-Balāgha. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Karīm al-Namrī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1418 AH.
  • Ibn al-Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba. Edited by Muḥammad Ibrāhīm al-Banā. Beirut: Dār al-Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1970 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd & Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Ḥazm al-Andulusī, ʿAlī b. Aḥmad. Jamhart ansāb al-ʿarab. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Salām Hārūn. Cairo: Dār al-Maʿārif, n.d.
  • Ibn Saʿd. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿImīyya, 1410 AH.
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl. Edited by Sayyid Mahdī Rajāʾī. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1404 AH.
  • Khoei, Abū l-Qāsim. Muʿjam rijāl al-ḥadīth. Qom: Markaz-i Nashr-i Āthār-i Shīʿa, 1410 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Third edition. Beirut: Dār al-Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Māmaqānī, ʿAbd Allāh. Qāmūs al-Rijāl. n.p. n.d.
  • Mazzī, Yūsuf b. ʿAbd al-Raḥmān al-. Tahdhīb al-kamāl fī asmāʾ al-rijāl. Edited by Bashshār ʿIwād Maʿrūf. Beirut: *Muʾassisat al-Risāla, 1400 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-.Al-Ikhtiṣāṣ. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, n.d.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād. Translated by Ḥasan Mūsawī Mujāb. Qom: Intishārāt-i Surūr, 1388 Sh.
  • Nawbakhtī, Ḥasan b. Mūsā. Firaq al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1404 AH.
  • Qummī, Shakh ʿAbbās. Muntahī l-āmāl. Qom: Intishārāt-i Hijrat, 1413 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1403 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Beirut: n.p. , n.d.
  • Yaʿqūbī.Tārīkh al-Yaʿqūbī. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1373 Sh.
  • Ziriklī, Khayr al-Dīn al-. Al-Aʿlām. Beirut: Dār al-ʿIlm li-l-