Ubora wa Imamu

Kutoka wikishia

Ubora wa Imamu (Kiarabu: أفضلية الإمام); Katika nafasi ya Uimamu, suala la ubora ni mojawapo ya masharti ya kustahiki nafasi ya Uimamu. Hii inamaanisha kwamba; Mtu anaye stahiki kuwa Imamu ni yule mtu mwenye ubora katika sifa tofauti pamoja na ubora wa maadili ya kibinadamu ukilinganisha na wengine. Kulingana na maoni ya wanatheolojia wa madhehebu ya Shia Ithanaashariyyah, Imamu anapaswa kuwa mbora kuliko wengine; kielimu, kidini, kiuchamungu, kiukarimu na kiujasiri. Imamu pia anatakiwa awe ni mtu wa mbele kabisa kuliko wengine katika njia ya kutafuta ujira na manufaa ya Akhera ... Suala la sharti ya ubora wa mshika nafasi ya Uimamu, imethibitishwa kupitia hoja ya kiakili za ni: tarjihu bilaa Murajjih "kuto kuingia akilini tendo kuchagua kitu fulani na kuachana na chengini bila sababu maalumu" na Kubhu taqdiimu al-mafdhuli ‘ala al-fadhil "kuto kubalika chaguo la kuchagua kilicho duni na kuachana na kilicho bora" na pia Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: "Kiongozi yeyote anayeongoza watu, kisha miongoni mwao kukawa kuna mtu aliye na elimu Zaidi kuliko yeye, mambo ya watu hao yataendelea kuwa mbaya hadi siku ya Kiyama". Pia ukachana na hoja hizi, kuna baadhi ya aya za Qur'an zilizo tumika katika kusisitiza suala hilo.

Wengi wa Waislamu wa madhehebu ya Sunni hawaoni suala la ubora wa Imamu kuwa suala la lazima au wajibu, bali kwa mtazamo wao hata mtu wa daraja ya chini pia anaweza kuwa Imamu katika hali ya kuwepo kwa kikwazo au manufaa maalumu. Kulingana na maelezo ya Saad al-Din al-Taftazani, mwanatheolojia wa Kisunni wa karne ya nane ya Hijiria, ni kwamba; Kwa mujibu wa maoni ya Sunni na madhehebu mengi ya Kiislamu, katika zama na nyakati zote, Uimamu ni haki ya yule aliye mbora zaidi miongoni mwa wanajamii, isipokuwa kama uteuzi wake utapelekea machafuko na fitna katika jamii. Hoja na vielelezo juu ya maoni ya Kisunni; ni mawafikiano ya wanazuoni juu ya kukubalika uteuzi wa Imamu kupitia makubaliano na maridhiano ya wanajamii katika kumchagua imamu mwenye daraja ya chini baada zama za Khulafau al-Rashidina na tendo la khalifa wa pili la kuteuwa kamati ya watu sita ili wamchague mmoja kati yao awe khalifa.

Kulingana na wanazuoni wa Shia ni kwamba, Maimamu wa Shia (a.s), baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), ni bora zaidi kuliko viumbe wote Mwenyezi Mungu. Allama Majlisi anaamini kwamba ni mjinga mpeke yake ndiye anaye kataa ubora wa Maimu wa Kishia. Hoja ya ubora wa mtu anayetaka kushika nafasi ya Uimamu, ndiyo hoja iliyo tumika kuthibitisha Uimamu wa Imam Ali (a.s), ambayo huitwa hoja ya ubora.

Welewa wa Dhana na Upeo Wake

Kwa maoni ya wanatheolojia wa madhehebu ya Shia Imamiyah, ubora wa Imamu unamaanisha na kulenga zaidi kwenye ubora wake juu ya wengine katika sifa maalumu kama vile; elimu, uadilifu, ujasiri na uchamungu, sifa hizi ndizo zinazo zaingatiwa kuwa ndio masharti ya Uimamu. [1] Katika baadhi ya vyanzo vya kitheolojia, ubora huu unamaanisha pia ubora katika ibada na ubora katika jitihada za kutafuta thawabu na kujikirubisha kwa Mwenye Ezi Mungu. [2] Kwa hivyo, wanatheolojia wa madhehebu ya Shia Imamiyah wanaamini kwamba; Imamu ni bora kuliko watu wengine katika sifa zote za kiroho na kimwili kama vile elimu, dini, uchamungu, ukarimu, ujasiri, [3] na ubora katika kutafuta thawabu na mafanikio ya siku ya mwisho (mafanikio ya Akhera). [4] Manatheolojia hao wanaamini kwamba; ni Imamu lazima awe ni mtu mwenye elimu zaidi, mwenye ujasiri zaidi, mwenye ukarimu zaidi, mwenye subira zaidi, mwenye uchamungu zaidi, na kadhalika, kuliko watu wote manaoishi katika zama zake, [5] ili awe ni kigezo kwa watu na awe ni mwenye kustahiki kufuatwa na wengine. [6]

Imeelezwa ya kuwa; si lazima Imamu awe bora kuliko wengine katika mambo ya kidunia kama vile mali, hadhi na nguvu; kwa sababu lengo ni kumfuata Imamu kwa dhati na kumuamini kwa dhati, sio kufuata na kiju juu tu. [7]

Kwa Mtazamo wa Shia, Imamu Lazima awe Bora Zaidi Kuliko Wengine

Wanatheolojia wa Shia Imamia wanaamini kwamba ubora ni mojawapo ya masharti ya Uimamu [8] nao wanakubaliana na wanawafikiana kinadharia juu ya hili. [9] Ili kuthibitisha ubora wa Imamu, hoja za kimantiki na vielelezo vya maandiko vimewasilishwa ili kudhatiti dhana hiyo.

Hoja za Kimantiki

  1. Katika wasifu na ukamilifu, Imamu anaweza kuwa na hali tatu tofauti; ima atakuwa ni sawa na wengine au duni kuliko wao au anaweza kuwa ni mbora zaidi ya wao. Ikiwa yeye atakuwa ni sawa na wengine, kumchagua yeye kama ni Imamu chaguo hilo litakuwa na upendeleo lisilotegemea uzito wowote ule katika chaguo hilo. Kitaalamu chaguo la aina hii huitwa (kuchagua la moja ya vitu viwili vilivyo sawa, bila ya kuwepo sababu maalumu), ambapo kwa lugha ya Kiarabu huitwa “Tarjihu bilaa murajjihi”. Iwapo Imamu atakuwa duni kuliko wengine, katika hali hii, kwa mujibu wa hukumu ya akili, ni kwamba; kumpendelea mtu duni kuliko aliye bora, ni jambo la kuchukiza na lisilo ingia akili. Kwa hiyo Imamu ni lazima awe bora kuliko wengine. [10]
  2. Ni wajibu kwa Imamu kuwa ni mtu maasumu. Maasumu ni bora kuliko asiye maasumu. Hivyo Imamu ni bora kuliko wengine. [11]
  3. Imamu ni mtu anaye teuliwa na Mtume (s.a.w.w). Daima bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akizingatia suala la ubora katika kuchagua mrithi wake atakaye shika madaraka ya uongozi baada yake. [12]

Hoja na Vielelezo vya Maandiko

Kuna vielelezo kadhaa vya maandiko vilivyo tumika katika kuwasilisha na kuthibitisha hoja ya ulazima wa kuwepo kiwango cha ubora kilicho wapindukia wengine kwa mtu anaye taka kushika nafasi ya Uimamu. Miongoni mwa maandiko yalio tumika kuthibitisha hilo ni; Aya ya 35 ya Surat Yunus, [13] Aya ya Sadiiqina (Aya ya 119 ya Surat al-Towbah) [14] na Aya ya 9 ya Surat al-Zamar. [15] Aya hizi zimetajwa kama ni hoja katika kuthibitisha ubora wa Imamu. Katika aya hizi, imebainishwa kwamba; mwenye kuongoza kwenye haki anatangulizwa mbele kuliko yule anayehitaji kuongozwa, kutangulizwa “aliye mwaminifu” kuliko asiye kuwa mwaminifu, na kupewa kipau mbele mwanachuoni kuliko asiyekuwa mwanachuoni. yote haya yanaonyesha kipaumbele cha mtu mwenye uzito maalumu kuliko mtu asiye kuwa na uzito wowote ule naozingatiwa kuwa ni sifa njema zinazo mwezesha mtu kuiongoza jamii kwa mfumo salama. [16]

Ili kuthibitisha kuwa ubora wa sifa maalumu, ni jambo la kwa mshika nafasi ya Uimamu, Wanazuoni wanukuu Hadith kadhaa kama ni vielelezo juu ya ulazima wa jambo hilo. [17] Kwa mfano, katika Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), yeye amesema kwamb: "Mwenye kuongoza umma na ndani yao kukawa na mtu mbora zaidi kielemu kuliko yeye, basi mambo yao yataendelea kuharibika mpaka Siku ya Kiyama". Pia kwa upande wa madhehebu ya Sunni, mepokewa Hadithi isemayo kwamba; Abu Darda alikuwa akitembea mbele ya Abu Bakr, Mtume (s.a.w.w) akamwambia: “Je, (huoni kwamba), unatembea mbele ya mtu ambaye ni mbora kuliko wewe duniani na Akhera?” [20] Imeelezwa kwamba; Riwaya hii inasisitiza ubaya wa kutembea na kumtangulia mbele mtu aliye zidi daraja kuliko wengine. Kwa hiyo, itakuwa ni vibaya zaidi kumtanguliza mtu wa chini kwenye nafasi ya Uimamu na kuachana na yule aliye juu zaidi yake. [21]

Kwa Mtazamo wa Ahlu al-Sunnah, Inajuzu Mtu wa Chini Kushika Nafasi ya Uimamu

Masunni wengi hawachukulii ubora wa Imamu kuwa ni sharti au faradhi na kwa mtazamo wao mtu wa daraja ya chini anaweza kumtangulia na kumpiku mwenye daraja ya juu katika kushika nafasi ya Uimamu.

Mtazamo wa wanazuoni wa Kiash'ariy: Wanatheolojia wa Ash'ari hawakubali ulazima na sharti ya ubora wa Imamu. Kwa sababu hii, wao wanaona kuwa inajuzu kumuweka au kumchagua Imamu wa daraja ya chini na kuachana na Imamu wa daraja la juu. [22] Hata hivyo, Qazi Abu Bakar Baghalani, mwanatheolojia wa Ash'ari wa karne ya tano Hijiria, ana maoni kwamba; ubora ni moja ya sifa za lazima za Imamu, isipokuwa kama kutajitokeza kizuizi juu ya kumteua Imamu bora, katika hali kama hiyo inajuzu mwenye daraja ya kuchaguliwa kama ni Imamu na kuachana na yule mwenye daraja kuliko yeye. [23] Yeye ametaja vielelezo kadhaa katika kuthibitisha ulazima huo wa ubora katika kushika nafasi ya uongozi, miongoni mwazo ikiwemo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (یَؤُمُّ القَومَ اَفْضَلُهُم) Mtu bora wa taifa ndiye anaye takiwa kuliongoza taifa (mbora wa kaumu ndiye anaye takiwa kuiongoza kaumu." [24] Baghelani anaamini kwamba; ikiwa kuna hofu ya machafuko, ufisadi, kuzorota au kutoweka kwa hukumu za kisheria, au kuhofiwa kwa uroho wa maadui wa Uislamu kuunyemelea Uislamu na kuuhujumu, hicho kitakuwa ni kisingizio tosha na halali cha kumwacha mtu bora na kumkabishi uongozi mtu mwenye daraja ya chini kuliko yeye. [25] Pia, kwa mujibu wa maelezo ya Saad al-Din Taftazani, mmoja wa wanatheolojia wa Ash'ari wa karne ya 8, ni kwamba; Makundi mengi ya Sunni na madhehebu kadhaa ya Kiislamu yanaamini kwamba, Uimamu ni haki ya mtu aliye mbora zaidi kuliko wengine. Nadharia inafanya kazi katika kila zama na nyakati, isipokuwa wakati ambao Uimamu wake utakuwa ndio chanzo cha machafuko na fitna, katika hali hiyo nadharia hii itabidi kuwekwa kando. [26]

Muutazila: Pia Muutazila hawaoni ubora wa imamu kuwa ni wajibu katika kumchagua bali wanaona kuwa inajuzu kumpa kipaumbele mtu mwengine ambaye kidaraja yuko chini zaidi. Pia baadhi ya wakati mteua na mtu wa daraja la chini huwa ni bra Zaidi kuliko kumpa nafasi hiyo aliye bora ambaye kisifa na wasifu ndiye anayestahili zaidi. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kupelekea kutopewa kipau mbele kwa mtu aliye bora ni pamoja na:

  • Ikiwa mtu bora hana baadhi ya sifa ambazo zinahitajika kwa Imamu, kama vile elimu na maarifa ya kisiasa.
  • Ikiwa mtu bora ni mtumwa, au ana ugonjwa maalum au matatizo ya kiakili, na hawezi kuhukumu kisheria na kusimamisha jihad.
  • Ikiwa mtu bora sio Mquraishi; lakini mtu mtu wa daraja ya chini ni Mquraishi. [28]

Hoja za Ahlu-Sunna

Hoja za Ahlu-Sunna katika kuruhusu ukhalifa wa mtu aliye chini kidaraja:

  • Wanazuoni wanakubaliana (kuna ijmaa ya wanazuoni) ya kwamba; uteuzi wa khalifa kwa mtu aliye chini ulifanyika miongoni mwa Quraish baada ya zama za Makhalifa waongofu (Khulafau al-Rashidun) licha ya kuwepo kwa mtu aliye bora zaidi.
  • Omar ibn al-Khattab aliutelekeza ukhalifa kwa baraza la watu sita, wakati miongoni mwao alikuwepo Ali (a.s) na Othman ambao kwa wakati huo walikuwa ni bora zaidi kuliko wengine.
  • Ubora wa sifa ni jambo la siri la kibatini na kuna utata na ugumu katika kuelewa jambo hilo. [29]

Ubora wa Imamu kupitia ubora wa malipo ya Akhera

Kuna hoja kadhaa kwa ajili ya kuthibitisha ubora wa Imam kupitia ubora wa malipo ya Akhera [30], miongoni mwazo ni:

  • Umaasumu: Ni lazima Imamu awe mtoharifu (Maasumu). Yeyote aliye takaswa ni bora kuliko wengine katika suala la thawabu za Akhera; [31] Kutokana na utoharifu alio nao, Imamu huwa sawa katika hali yake ya ndani pamoja hali yake ya nje. Kwa lugha nyingine, Imamu huwa hana mvutano na msuguano baina ya dhahiri na batini yake, kwa hiyo Imamu huwa ana uchamungu wa hali ya juu kabisa kuliko wengine, na hilo ndilo linalo pelekea yeye kupata ujira mkubwa zaidi kuliko wengine. [32]
  • Majukumu mazito zaidi huwa na thawabu zaidi: Imamu, kwa sababu ya kubeba mzigo wa uimamu, huwa ana majukumu makubwa na zaidi kuliko wengine. Kwa hivyo thawabu na ujira wake huwa ni zaidi kuliko wengine. [33]
  • Imamu kuwa dalili (kigezo na hoja): Imamu ni dalili hoja ya Mungu kama vile alivyo Mtume (s.a.w.w). Hivyo basi na kama vile Mtume (s.a.w.w) alivyo kuwa bora kuliko wengine katika suala la thawabu na malipo ya Mwenye Ezi Mungu, pia Imamu naye ana ujira mkubwa zaidi na thawabu bora zaidi kuliko wengine. [34]

Ubora wa Maimamu wa Kishia

Makala Asili: Ubora wa Ahlul-Bayt (a.s)

Wanazuoni wa Shia wanaamini kwamba baada ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w), Maimamu wa Shia (a.s) ni bora na wana daraja ya juu kuliko wengine wote, (ikiwa ni pamoja na manabii, malaika na watu wengine). [35] Imeelezwa ya kwamba; Hadithi zinazo onesha ubora wa Imamu (a.s) juu ya viumbe wengine wote, ni Hadithi “mustafidha”. Yaani ni Hadithi zilizo karibia daraja ya “Hadithu mutawatiru”. [36] Allama Majlisi anaamini kwamba; mtu yeyote atakaye tafiti Hadithi, bila shaka yeye mwenye atathibitisha ubora wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na Imamu (a.s) na kwamba ni mtu mjinga peke yake ambaye hata taaluma ya Hadithi ndiye anaye jaribu kukanusha uhakika huu. Kwa maoni yake, kuna ripoti na Hadithi nyingi mno kuhusiana na suala hili. [37]

Katika Hadithi ya Imamu Ridha (a.s) aliyo inukuu kupitia baba na babu zake kutoka kwa Imam Ali (a.s) amabaye ameinukuu kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), ni kwamba Mtume (s.a.w.w) amesema:

...Ewe Ali! Hakika Mwenye Ezi Mungu amewatakasa manabii juu ya malaika walio karibu na Mungu, naye amenifanya mimi kuwa bora kuliko manabii wote. Ewe Ali! Ubora baada yangu mimi ni kwa ajili yako na Imamu baada yako. Hakika malaika ni watumishi wetu na wapenzi wetu!... [38]

Kuna Aya na Riwaya kadhaa zilizo tajwa kwa ajili ya kuthibitisha ubora wa Imamu Ali (a.s) kuliko watu wengine wakiwemo masahaba. [39] Allama Hilli katika Kashf al-Murad [40] ametoa hoja na vielelezo 25 na Ibn Maitham Bahrani katika kitabu al-Najaatu fi al-Qiyaama [41] ametoa hoja 22 juu ya ubora wa Imam Ali (a.s.). Baadhi ya hoja hizi ni; Aya ya Mubahala, Aya ya Mawaddah, Hadithi ya Tairu, Hadithi ya Manzila na Hadithi ya Rayah. [42] Imeelezwa kuwa wafuasi wote Mu'utazila wa Baghdad, ikiwa ni pamoja na Ibn Abi al-Hadid, ambaye ni mfasiri wa Nahju al-Balagha, na baadhi ya wafuasi wa Mu'utazila wa Basra pia wamemzingatia Imamu Ali (a.s) kuwa ni mtu bora kuliko Makhalifa watatu pamoja na masahaba wengine wote. [43]

Thibitisho la Hoja ya Ubora

Ubora wa Imamu umetumiwa kama ni hoja juu ya kuthibitisha Uimamu wa Imam Ali (a.s). Uthibitisho huu, unaojulikana kama Uthibitisho wa Ubora, ni kama ifuatavyo:

  • Msingi wa kwaza: Kulingana na hoja za Qur'an na Hadithi, Imam Ali (a.s) alikuwa ni mtu bora kuliko masahaba na Waislamu wengine wote.
  • Msingi wa pili: Ni sharti kwa Imamu kuwa bora kuliko wengine katika sifa na ukamilifu wa kibinadamu.
  • Natija: Kwa hivyo, Imam Ali (a.s.), ndiye alikuwa Imamu na mrithi wa Mtume (s.a.w.w). [44]

Pingamizi

Kuna kundi kati ya wafuasi wa madhehebu ya Sunni waliozua pingamizi dhidi ya wajibu Imamu kuwa na sifa bora, 45 miongoni mwa pigamizi hizo ni kama ifuatavyo:

  • Ubora haufungamani wala haulazimiani na sula la kipaumbele katika uongozi: kwa sababu mwenye daraja ya chini anaweza kupata kipau mble katika hali fulani na kutangulizwa mbele kuliko mbora wao. Kwa mfano; Iwapo mtu mwenye ubora wa wa chini atakuwa na uwezo kuwa na ujuzi zaidi katika uongozi wa jamii na kisiasa kuliko mtu aliye bora zaidi yake, jamii itampendelea yeye zaidi katika kushika nafasi ya Uimamu na uongozi wa jamii. [46] Jawabu juu pingamizi hii ni kwamba; Utangulizi ulio tumika katika pingamizi hii, ni utangulizi dhaifu, kwa sababu makadirio ya utangulizi huu yamezungumzia ubora katika nyanja za matendo ya ibada na uchamungu, na msingi huo sio sahihi kwa sababu ubora wa Imamu unahusisha sifa ambazo ni muhimu kwa Imamu, zikiwemo sifa zinazo wezesha usimamizi wa kisiasa na uongozi wa jamii. Pia, katika pingamizi hii, ubora wa Imamu umezingatiwa kwenye kiwago cha malinganisho kinachoweza kupatikana kwa kiwango fulani na kutofautiana na wengine kwa viwango walivyo navyo, wakati linapozungumzwa suala la ubora wa Imamu, hukusudiwa ubora kamili na ubora katika sifa zote na ukamilifu ambao ni muhimu kwa ajili ya uwepo wa Uimamu. [47] Kwa hiyo madai ya Shia yanalenga ubora kamili sio kiwango fulani ambacho kinaweza kulinganishwa na kupikuliwa na mtu mwingine.
  • Mifano isiyo afikiana na ubora: Imedaiwa kwamba nadharia ya ubora haiwiani na mifano ya uteuzi wa viongozi ulio fanyika katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w) na makhalifa. Uteuzi wa maimamu au makamanda wa jeshi haukuonekana kufuata kanuni hiyo. [48] Miongoni mwao, ni uteuzi wa amri ya Zaidu bin Harith katika vita vya Mauta, licha ya kuwepo kwa Jafar bin Abi Talib, uteuzi wa Usama bin Zaid, katika siku za mwisho za uhai wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na kuwepo kwa Imam Ali (a.s) [49]. Mifano mengine ni kuuwakilisha uteuzi wa ukhalifa mikononi mwa baraza la watu sita, ambapo Omar bin Khattab pamoja na kuwepo kwa Ali (a.s) na Othman, aliwakabidhi hatu hao sita wenyewe kwa wenyewe wamchague mmoja miongoni mwao kuwa khalifa. Waliojibu pingamizi hii wamesema ya kwamba; Uteuzi wa kamanda hauzingatii wala hauhitaja ukamilifu na ubora wa mtu katika nyanja zote, wala kamda hahitaji kuwa na ukamilifu timamu na kuwa mbora kuliko wote, bali inatosha yeye kuwa ni mbora katika mambo yanayohusiana na vita tu. Kwa vile Zaid na Osama walikuwa na wabora katika seta hizo, hilo lilitosha kuwa ni ndio sababu ya kuteuliwa kwao. Kuhusu uteuzi wa Usama, inasemekana kwamba; Imam Ali (a.s) alikuwa karibu na kitanda cha Mtume (s.a.w.w) siku hiyo, na wala Mtume (s.a.w.w) hakumtaka Imam Ali (a.s) kujiunga na jeshi la Usama. Kwa hiyo, Ali (a.s.) hakulazimika kuwa katika jeshi la Usama. [51] Kwa upande wa pili unao husiana na maamuzi ya Omar ni kwamba; Usahihi wa matendo ya Omar bin Khattab umeegemea juu uhalali wa matendo ya Masahaba, ambapo Mashia hawayakubali na nadharia hiyo. [52] Yaani Mashia hawayahisabu matendo ya Masahaba kuwa ni hoja na kielelezo kinachoweza cha kutegemewa katika kusimamisha hoja.

Monografia (Vitabu Maalumu Juu ya Mada hii)

Masuala Yanayo Fungamana