Nenda kwa yaliyomo

Umaasumu wa Manabii

Kutoka wikishia
Makala hii inahusu umaasumu (Utoharifu) wa manabii. Ili kuielewa dhana ya umaasumu na umaasumu wa Maimamu, tazama kipengele kuhusu umaasumu na umaasumu wa Maimamu.

Umaasumu wa Manabii (Kiarabu: عصمة الأنبياء) ni usafi wa Mitume wa kuto kufanya aina yoyote ile ya dhambi, ubaya au uovu. Umaasumu wa manabii uanahisabiwa kuwa ni kanuni msingi mojawapo unaozihusisha dini zote kwa jumla; Lakini kuna tofauti ya maoni kuhusu suala la ni nini hasa maana ya umaasumu, pamoja na viwango vyake. Wanachuoni wa Kiislamu wanawafikiana juu ya kulinda au kutakaswa mitume kutokana na ushirikina na ukafiri pamoja na umaasumu katika kupokea na kuwasilisha wahyi (ujumbe wa Mungu au ufunuo); Lakini wamehitilafiana kuhusu kuto kosea kwao na kuto tenda madhambi mengine katika maisha yao ya kila siku. Wengi wanaamini ya kwamba, mitume wametakasika na yote hayo yalitajwa hapo juu.

Msingi uliozingatiwa katika kuthibitisha umaasumu huo, unatokana na rehema na elimu thabiti ya Mwenye Ezi Mungu walionayo kuhusiana na uchamungu na uhakika wa dhambi ulivyo. Elimu ambayo ni asili itokayo moja kwa moja kwa Mwenye Ezi Mungu. Elimu ambayo ni tunuko ya Mwenye Ezi Mungu mwenyewe, na si elimu ya kufunzwa au kujifunza. Pia elemu hiyo haiwezi kupinduliwa na matamanio ya nafsi.

Qur'an haikuzungumzia wazi suala la umaasumu wa mitume, ila wafasiri wamejaribu kudadisi na kuzungumzia suala la chini ya Aya kadhaa. Miongoni mwa Aya hizo ni Aya ya 36 ya Surat Al-Baqarah inayozungumzia kisa cha kuondoshwa au kuhamishwa Adam na Hawa kutoka mbinguni. Wanatheolojia wa Kiislamu wametoa hoja za kimantiki tofauti katika kuthibitisha umaasumu wa manabii, kama vile sababu iloegemea hoja ya uaminifu wa mitume. Katika muktadha huu, wanaothibitisha uwepo wa umaasumu wanategemea Aya za Qur'an, moja wapo ikiwa ni Aya ya saba ya Surat Al-Hashr.

Wapinzani wa umaasumu wa mitume pia nao wanategemea Aya za Qur'an zinazohoji au kutengua umaasumu wa mitume wote au baadhi yao. Katika jawabu, imesemwa kwamba Aya hizo zinazotumiwa na wapinzani hao, ni Aya tata (Mutashabihat) na zinapaswa kufasiriwa kwa kurejelea Aya msingi amabazo si Aya tata (Muhkamaat). Pia, Aya zisizounga mkono umaasumu wa manabii zimefanyiwa taawili na kufasiriwa kwa kusema ya kwamba; Kufanya kosa hakumaanishi kufanya dhambi, bali kunamaanisha kutotenda na kuachana na lililo bora na kutenda lenye daraja ya chini (tarku al-aulaa) maana ambayo ni tofauti na maana ya kawaida ya makosa na dhambi.

Welewa wa Dhana

Makala Asili: Umaasumu

Umaasumu wa Mitume maana yake ni usafi na utakatifu wa Mitume kutokana na kufanya aina yoyote ile ya ubaya, uchafu na uovu.[1] Umaasumu wa Mitume unatambuliwa kama ni sifa ya ndani ya nafsi inayowafanya wao wawe na uwezo wa kutofautisha matendo mabaya na matendo mema kwa njia iliyo wazi kabisa.[2]

Katika kuuchambua na kuufafanuwa welewa wa neno (العصمة) umaasumu kamusi za Kiislamu, kumetumika maneno kama vile; Tanziih (التنزیه), Tawfiq (التوفیق) , Sidiqun (الصدق) na Amanah (الامانة). Haya ndiyo maneno yanayotumika katika kueleza dhana ya Umaasumu wa Mitume.[3]

Hadhi na Umuhimu

Umaasumu wa Mitume (عصمة الأنبیاء) katika uwanja wa wahyi unachukuliwa kuwa ni msingi unaofungamanisha dini zote za Mwenyezi Mungu.[4] ingawa kuna tofauti ya maoni kati ya wanatheolojia wa kiislamu, wakiwemo wanatheolojia wa Kiislamu, kuhusu maana halisi ya isma (العصمة) au utoharifu na viwango vyake.[5]

Baadhi wanaamini kwamba; Itikadi kuhusiana na umaasumu wa mitume (عصمة الأنبیاء), ilianza tokea mwanzoni mwa Uislamu. Kwa mfano, kuna nukuu isemayo kwamba; Khalifa wa kwanza katika kumtukuza Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) alimhisabu kuwa ni maasum (aliyetoharika).[6] Pia imeripotiwa ya kwamba; Imam Ali (a.s) alitumia neno umaasumu alipokuwa akifafanua daraja za mitume.[7] Hata hivyo, baadhi ya wanafikra wana maoni kwamba, matumizi ya kistilahi ya neno 'maasumu' au 'umaasumu', kama maneno mengine ya kitheolojia yalivyo, ihusiana na kuibuka kwa nadhaia na makundi ya kitheolojia yalioibuka katika zama za Uimamu wa Imam Swadiq (a.s)[8] Quran haikufafanua wazi kuhusiana na umaasumu wa mitume.[9] Lakini wafasiri wa Qur'an wamelizungumzia suala hili katika tafsiri za Aya kadhaa za Qur'an. Miongoni mwazo ni: Aya ya 36 ya Sura Al-Baqarah,[10] Aya ya 23 Sura A’raf na Aya ya 121 ya Sura Taha kuhusiana na kisa cha Adam na Hawa na kukutana kwao na Shetani, Aya ya 33 ya Sura Aal Imran kuhusu kuteuliwa kwa baadhi ya mitume na pia Aya ya 3 hadi ya 5 ya Suratu Al-Najm inayoeleza ya kwamba; Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) Anazungumza kwa kuegemea kwenye wahyi, si kwa matakwa na matamanio yake mwenyewe. Hizo ni miongoni mwa Aya ambazo wafasiri wa Qur'ani wamezitumia kuhusiana na suala la umaasumu wa mitume.[11]

Uchambuzi

Umaasumu wa mitume umesawiriwa katika sura na hatua kadhaa, ambazo ni kama ifuatavyo: Umaasumu (kutakasika) kutokana na ushirikina na ukafiri, umaasumu katika kupokea na kuwasilisha wahyi, umaasumu dhidi ya dhambi kubwa na ndogo, na umaasamu dhidi ya makosa katika nyenendo za kila siku. Kwa mujibu wa ufafanuzi wa mwanazuoni Jafar Sobhani; Wanatheolojia wa Kiislamu wanawafikiana juu ya sura ya kwanza na ya pili ya umaasumu.[12] Wanatheolojia wote wanaamini kwamba; mitume kabla na baada ya utume wao hawakufanya ushirikina wala hawakuwa na ukafiri.[13] Pia, wanatheolojia wa Shia na Sunni, wote wanaamini kwamba; manabii katika kupokea, kuhifadhi na kuwasilisha wahyi (ufunuo), wamekingwa dhidi ya usaliti wa kimakusudi,[14] wa kimakosa maoja na makosa yatokanayo na kusahau.[15] Ingawaje Qadhi Abd Al-Jabbar, kiongozi wa madhehebu ya kitheolojia ya Mu'utazila aliyeishi katika karne ya tano ya mwandamo, imeitakidi uwezekano wa mitume kusema uwongo usiokuwa wa makusudi katika kufikisha.[16]

Wanatheolojia wote wa Kishia wamewafikiana kuhusiana na sura ya tatu ya umaasumu,[17] yaani, kwa mujibu wa nadharia zao, Mitume wametakasika kutokana na aina zote za dhambi, kubwa au ndogo.[18] Isipokuwa Sheikh Mufid, yeye anaitakidi ya kwamba; Mitume wanaweza kufanya makosa madogo ya kusahau katika maisha yao ya kabla ya kuteuliwa kwao kuwa mitume, makosa ambayo hayatokuwa na dosari kovu mbaya maishani mwao.[19]

Pia sura ya nne, yaani kujiepusha (kutoharika) na makosa katika nyenendo za kila siku, imewafikiwa na wanazuoni wengi wa Kishia. Wao wametoa ufafnuzi ya kwamba; Maneno na matendo ya Mitume katika nyenendo za kila siku aa kibinafsi na ya kijamii yote yamelindwa dhidi ya upotofu.[20] Ila Sheikh Saduq akitegemea Hadithi ya Dhu Al-Shimalain,[21] anamini ya kwamba; Mitume wanaweza kusahau. Yeye ameihisabu imani ya kuamini ya kwamba Mitume hawafanyi makosa katika nyenendo zao za maisha ya kila siku, kuwa ni Ughulati (kutia chumvi kwenye sifa za utume) na Taf-widh.[22] Pia riwaya katika kitabu Usul Al-Kafi zilizosimuliwa kuhusu kosa la kusahau kwa Mtume (s.a.w.w).[23] Kwa upande mwingine, Allama Sha'arani, katika ukosoaji wake wa madai ya Sheikh Saduq, anaamini ya kwamba matendo yote ya Mtume (s.a.w.w), zinazingatiwa kuwa ni mafunzo ya dini, na iwapo kutaaminiwa kutendeka makosa katika nyenendo za maisha ya Mtume ya kila siku, basi pia hakutakuwa na kizuizi cha kuto tokea makosa katika ufikishaji wa dini. Jambo ambalo linakwenda kinyume na malengo ya umaasumu. Pia, kulingana na maoni yake, Waislamu wanashikilia kila alichokifanya Mtume wao (hata kama atakuwa amekifanya mara moja tu).[24] Allamah Tabatabai, akimvua Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) kutokana na nafasi na daraja yake maalum mbele ya Mwenye Ezi Mungu, anaamini kwamba; mambo yote ambayo hayahusiani na wahyi na mwongozo wa watu, yako nje ya suala la umaasumu. Yaani yeye anaamini ya kwamba; Mtume wet (s.a.w.w) amekamilika kiisma (kiutakatifu na utoharifu), kasi ya kwamba katika nyenendo zake zote hawezi kuonekana na aina ya mitelezo. Ila manabii wengi hawakosei katika kuongoza na kufikisha ujumbe waliopewa, ila katika maisha yao ya kawaida, wanaweza kukosea. Yeye anasema; Kwa mujibu wa Aya za Qur’an Tukufu, manabii wamefanya makosa na kusahau katika nyenendo zao za kila siku. Moja ya mitelezo yao ni: Kusahau kwa Nabii Adamu kuhusu ahadi yake, ombi la Nuhu la kumwokoa mwanawe mwenye dhambi kutokana na dhoruba, kuondoka kihasira kwa Yunus kutoka katika qaumu yake, na dhana ya Nabii Mussa kuhusu Nabii Harun baada ya Bani Isra-il (Wana wa Israili) kuabudu ndama.[25]

Kutokukosea kwa Manabii Hakupingani na Uhuru wa Mwanadamu

Kuna waoamini ya kwamba; Umaasumu (kutokosea) kunaendana kinyume na la uhuru wa mwanadamu katika kutenda matendo yake. Kwa kuzingatia msingi huu, wengine wamekanusha umaasumu wa manabii, na wengine wamehitimisha kwa natija ya kwamba, umaasumu wa manabii hautokani na chaguo lao wenyewe, bali ni wa kulazimishwa (wakimaumbile).[26] Moja ya hoja za kundi la mwisho ni kwamba mwanadamu amefungwa au amezungukwa na makosa na dhambi, na haidhuru yeye anajaribu sana kujizuia asitende dhambi, ila wakati mwengine hutumbukia ndani yake. Hivyo basi kama mtu atakuwa amedikia daraja au nafasi ya kutokosea au kutotenda dhambi, daraja hiyo itakuwa inatoka yake yeye, yaasi si kitu kitokacho ndani yake yeye mwenyewe bali ni shinikizo la lazima litokalo nje yake. Ili kuthibitisha shinikizo hilo linalopelekea umaasumu wa manabii, pia wameegemea Aya za Qur'an.[27]

Miongoni mwa Aya hizo ni Aya ya 46 ya Surat Saad, ambamo ndani yake mna maneno kadhaa yanayothibitisha maoni yao, kama vile: neno tumewatakasa (اخلصناهم) lililotumika kuwahusiana na Mitume. Pia Aya ya utakaso (آیه تطهیر), ambayo kulingana nayo Mungu amewatakasa baadhi ya watu kutokana na dhambi.[28]

Kinyume na rai hii, Allamah Tabatabai naye ametoa nadhari maalumu isemayo kwamba; Mungu amewapa mitume elimu ili kuelewa uhakika na kiini cha dhambi. Kwa hiyo wao hawafanyi dhambi, na kutofanya kwao dhambi kunatokana na welewe wao juu ya ubaya wa dhambi, na si kwa sababu yao Jabr ((kulindwa wasifanye dhambi)). Alilinganisha ujuzi wa manabii kuhusiana na dhambi na ujuzi wa mwanadamu kuhusiana na chakula kilichotiwa sumu, ujuzi ambao humpelekea manadamu kukiepuka chakula chenye sumu.[29]

Ja'afar Subhani naye akifafanu suala la umaasumu, ameandika akisema ya kwamba; nafasi ya umaasumu tunuko inayotolewa na Mwenye Ezi Mungu na kupewa mtu maasum (nabii au imamu) kwa mapenzi yake Mungu, na pia kuna baadhi ya Aya zinasisitiza kuwa umaasumu ni zawadi. Lakini sharti za kufikia hadhi ya umaasumu hupatikana kwa kujitahidi na kupigana dhidi ya matamanio ya nafsi. Kwa hivyo, daraja hiyo inaweza kufikiwa kupia hiari na uhuru wa mtu mwenyewe.[30]

Ithibati

Ithibati (hoja) za umaasumu wa Mitume zimegawanywa katika makundi mawili: Ithibati (hoja) za kimantiki (kiakili) na za maandiko:

Ithibati (Hoja) za Kiakili (Kimantiki)

Moja ya ithibati na hoja ya kiakili muhimu zaidi ya kutofanya makosa kwa Mitume, ni kuaminika mbele za wanowaamini.[31] Kwa kuzingatia hoja hii, iliyopewa jina la "Ithibati ya kuaminiwa",[32] ni kwamba; Iwapo matendo ya manabii hayalingani na maneno yao, watu hawatakubaliana uongozi wao.[33]

Hoja na ithibati nyingine ya kimantiki, ni ukiukaji wa nia ya ujumbe. Watetezi wa suala la umaasumu wamesema ya kwamba; Kwa mujibu lengo Mungu kuwatuma manabii lilivyo, nalo ni kuwataka watu wawatii manabii hao, Hivyo basi iwapo manabii au mitume watafanya dhambi, hapo patakuja swali, nalo ni je, tuwafuate au tusiwafuate? Ikiwa tutatii na kuwafuata, kutakuwa na ukiukaji wa dhumuni la kutumwa kwa mitume na manabii; Kwa sababu manabii walikuja kuongoza watu. Pia kutowafuata kutasababisha kudharau hadhi ya manabii na umbe waliokuja nao.[34]

Ithibati za Maandiko

Ithibati za maandko ni mjumuiko wa Aya za Qur'an pamoja na Hadith. Kwa mujibu wa wafasiri, kuna Aya kadhaa za Qur'an zinaashiria umaasumu wa mitume. Allameh Tabatabai ametaja miongoni mwa Aya hizo kuwa ni: Aya ya 64, 69 na Aya ya165 za Surat Nisaa, Aya ya 90 ya Surat Al-An'aam na Aya ya 17 ya Surat Al-Kahf.[35]

Katika Aya ya 17 ya Surat Al-Kahf, imeelezwa kwamba: Mwenye kuongozwa na Mwenyezi Mungu basi ameongoka. Kwa mujibu wa maoni ya Allamah Tabatabai, Aya hii inakanusha na kukataa uwepo wa aina yoyote ile ya upotofu kutoka kwa walioongoka, na kwa vile kila dhambi ni aina ya upotofu, hivyo basi Aya hii itakuwa inaashiria kwamba Mitume hawatendi aina yoyote ile ya dhambi.[36]

Suala la Umaasumu wa Mitume ni suala lililosisitizwa katika Hadith kadhaa.[37] Miongoni mwazo ni hadithi ya Imam Baqir (a.s) ambapo katika Hadihi hiyo imeelezwa ya kwamba: “Mitume hawatendi dhambi; Kwa sababu wote ni maasumu na ni wasafi, kwa hiyo wao hawafanyi aina yoyote ile ya dhambi, si ndogo wala kubwa.”[38]

Dosari (Ukosoaji) na Majibu

Wapingao umaasumu wa mitume wakizingatia baadhi ya Aya za Qur'an na Hadithi, wamekanusha kabisa umaasumu wa mitume. Mingoni mwa hoja na ithibati za madai yao ni Aya kadhaa za Qur'ani, kama itakavyofafanuli baadae.

Kukata Tamaa na Shaka Juu ya Ahadi ya Mungu

Wale wanaokanusha umaasumu wa Mitume wametumia Aya ifuatayo kama ni moja ya ithibati za madai yao;

(...حَتَّی إِذَا اسْتَیأَسَ الرُّ‌سُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ کُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُ‌نَا فَنُجِّی مَن نَّشَاءُ)
(Hata ufikapo wakati wa Mitume kukata tamaa na (watu) wakadhania kuwa wamedanganywa (na mitume wao) hapo basi nusura yetu ikawafikia).

Wakanusha wa umaasumu, wamekanusha umaasumu wa mitume wakitegemea maelezo ya Aya hii katika suala la mitume kukata tamaa na kuwa na dhana mbaya dhidi ya Mola wao, ambapo walidhani kwamba Mola wao kawadanganya.[39] Wamethibitisha madai yao wakisema ya kwamba; Muktadha ibara isemayo ((وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ کُذِبُوا ; Wakadhani ya kwamba wamedanganywa)), ni kwamba Mitume walidhani kwamba Mungu amewadanganya kuhusu nusura yake.[40]

Allamah Tabatabai akijibu ukosoaji na dosari hiyo amefafanua kwa kusema kwamba; Maana ya kiwakilishi kilichoko katika ibaya ya wakadhani (ظنّوا), ni kwamba, sio mitume walidhani bali ni watu. Kwa hiyo basi, maana ya Aya ni kama ifuatavyo: Ukaidi wa watu wa kutoitikia wito wa manabii uliwafanya Mitume kukata tamaa na watu wakadhani kuwa ahadi ya adhabu ni uwongo[41] [Maelezo 1] Ayatullah Subhani amevihisabu viwakilishi vyote katika aya hiyo vinawawakilisha Mitume, na anaamini ya kwamba; Mitume hawakufikiri kwamba Mwenyezi Mungu amewadanganya, bali hali yao ilipelekea wengine wakawadhania kuwa Mola wao kawadanganya kuhusiana na ahadi yake ya kuwanusuru.[42]

Wasiwasi wa Shetani Kupenya Nyoyoni mwa Manabii

Muonekano dhahiri wa maana Aya isemayo:

(...وَمَا أَرْ‌سَلْنَا مِن قَبْلِک مِن رَّ‌سُولٍ وَلَا نَبِی إِلَّا إِذَا تَمَنَّیٰ أَلْقَی الشَّیطَانُ فِی أُمْنِیتِهِ فَینسَخُ الله مَا یلْقِی الشَّیطَانُ)
(Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila kila anapo soma (Aya mingoni mwa Aya), Shet'ani hutia (ushawishi wake) katika usomaji wake. Basi Mwenyezi Mungu hufuta yale aliyoyatia shetani...)[43]

Umepelekea Aya hii kutumika katika kukanusha umaasumu na uaminifu wa Mitume. [44] Kutokana na muktadha wa dhahiri ya Aya ulivyo, ni kwamba Shetani anaingilia kweye mawazo, matakwa pamoja na fafanuzi za mitume; Ila Mwenye Ezi Mungu hufuta na kuutokomeza ushawishi wa Shetani.[45] Hadithi ya Gharaniq imechukuliwa kuwa ni moja ya uthibitisho wa nadharia hii.[46]

Ufafanuzi na tafsiri ilitajwa hapo juu, inakwenda kinyume na Aya nyengine za Qur'an.[47] Aya ambazo zinathibitisha ya kwamba; Shetani haingilii matakwa na maamuzi ya waja wa Mwenye Ezi Mungu, na mfano wa wazi wa waja wa Mwenyezi Mungu ni mitume na manabii.[48] Baadhi katika kuifasiri Aya hiyo, wamesema ya kwamba; Kinachokusudia hapo, ni kwamba Shetani huwashawishi watu wasiyashike ayafikishayo mtume, na wasimame dhidi ya mitume. Ambapo kutoka na Shetani kuingiza ushawishi wake ndani ya nyoyo za watu, jambo hilo hupelekea mitume kutofaulu kisawasawa katika kazi yao za kufukisha ujumbe Mwenye Ezi Mungu .[49] Pia kule kufuta kwa Mwenye Ezi Mungu yale ayaingizayo Shetani, ndiyo nusura ya Mwenye Ezi Mungu kwa Mitume wake.[50]

Watu Wote Wana Dhambi Hata Manabii

Mwenye Ezi Mungu katika moja ya Aya zake za Qur'ani anasema:

(...وَلَوْ یؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَ‌ک عَلَیهَا مِن دَابَّةٍ)
(Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa mujibu wa dhulma zao, basi asingeli mwacha hapa hata mnyama mmoja...)[51]

Dhulma na ukandamizaji, ni ilinasibishwa na watu wote, nadhula maana yake ni dhambi; Kwa hiyo Aya hii inathibitisha kwamba watu wote ni watenda dhambi wakiwemo manabii.[52]

Katika kujibu dosari na ukosoaji huu, Fakhrazi akinukuu baadhi ya Aya, kama vile Aya ya 32 ya Surat Faatir amesema: Aya hiyo haimaanishi kuwa watu wote ni madhalimu na wakandamizaji; Bali madhumuni ya neno watu katika Aya hiyo, ni madhalimu wote wanaostahiki adhabu au washirikina waliotajwa katika Aya zilizotangulia kabla yake.[53] Kwa mujibu wa maoni ya Allamah Tabatabai, maana ya dhulma katika Aya iliyotajwa hapo juu, ni aina zote za dhambi na makosa, na haihusishi tu makosa ya kushikamana na jambo duni na kuachana na lililobora. Kwa hiyo inawezekana Mitume, kutenda kosa na kukamata lililo duni na kuachana na lililo bora.[54]

Aya Zisizo endana na Umaasumu wa Baadhi ya Manabii

Muonekano dhahiri wa baadhi ya Aya za Qur'an unaashiria kuto thibiti umaasumu wa baadhi ya mitume, kama vile Nabi Adam (a.s),[55] Nuhu (a.s),[56] Ibrahim (a.s),[57] Mussa (a.s),[58]Yusufu (a.s),[59] Yunus (a.s) na[60] Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) [61] wameanzisha.[61]

Ayatullah Ja’afar Subhani amezihisabu Aya hizi kuwa ndizo Aya muhimu na kuu zinazotumiwa na wapinzani wa nadharia ya umaasumu wa mitume, kama ni ithibati katika kusimamisha hija zao.[62] Ahmad Amin Masri, akiegema kwenye Aya hizi hizi,[63] amesema kuwa; Umaasumu wa mitume kutokana na madhambi makubwa na madogo kabla na baada ya utume ni ughulat (imani ni utiaji chumvi), na imani hiyo inapingana moja kwa moja na Aya za Qur'an.[64]

Majibu ya Jumla Jamala

Wafasiri wamezichunguza Aya zote zisizowafikiana na umaasumu wa mitume moja baada ya nyengine kisha wakatafiti dhana juu ya dosari na mashaka kuhusiana nazo.[65] Pia kuna majibu ya kijumla jamala yametolewa kuhusiana nazo yakiwemo majibu yafuatayo:

  • Aya zinazohusu umaasumu wa manabii, ni Aya za Muhkamati (Aya zinazofasirika bila ya utata) na Aya zinazopingana na umaasumu wa Mitume ni Aya za Mutashabihati (zenye maana tata), ambazo zinapaswa kufasiriwa na kueleweka kwa kurejeshwa kwenye Aya za Muhkamat.[66]
  • Ikiwa Aya hizo zinathibitisha kinyume na ithibati za wazi kabisa katika suala la umaasumu wa manabii, ima itabidi ziachwe kando bila ya kufasiriwa au zifasiriwe kulingana na muqtadha uwendao sawa na umaasumu wa manabii; Kwa hiyo, Aya ambazo zinaonekana kutopatana na umaasumu wa manabii, lazima zifasiriwe kulingana na muqtadha uwendao sambamba na uwepo wa umaasumu wa manabii.[67]
  • Tukikubaliana na nadharia inayojuzisha mitume kushikamana na lililo duni na kuachana na lililo bora, au kushikamana na lililo bora na kuachana na lililo bora zaidi, basi Aya zote ambazo haziendani na umaasumu wa Mitume zitabidi zifasiriwa kulingana na nadharia hii. Lakini kama hatukubalianai na nadharia hii, ya kujuzu kwa mitume kushikamana na lililo duni na kuachana na lililo bora au makini zaidi, itabidi isemwe kwamba; Kesi za Aya hizo zilikuwa na maslahi maalumu ambayo sisi hatuyaelewi undani wake, kama vile siri na hekima za kisa cha Nabii Mussa na Khidhri (a.s), ambapo hata Nabii Mussa mwenyewe alipigwa na butwaa.[68]

Vile vile katika baadhi ya hadithi, Aya ambazo kidhahiri zinapingana na umaasumu wa Mitume zimeshiriwa na kujibiwa;[69] kwa mfano, katika riwaya ya Imam Ridha (a.s) imepokewa ya kwamba: "katika kikao kimoja miongoni mwa vikao vya Ma'amun, kilichohudhuriwa na wanachuoni mbali mbali wa dini na madhehebu tofauti, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ali Ibn Jahm alimuuliza Imamu Ridha (a.s), je wewe unaamini umaasumu wa Mitume? Imamu Ridha (a.s) akamjibu kwa kusema: Ndiyo. Kisha Ali bin Jaham akauliza kuhusu tafsiri ya Aya kama vile Aya ya 121 ya Surat Taha, Aya ya 87 ya Surat Al-Anbiyaa na Aya ya 24 ya Surat Yusuf, Ambapo Imamu Redha (a.s) kabla ya kumjibu, kwanza alimkataza kuyanasibisha matendo maovu na ubaya kwa Mitume wa Mwenye Ezi Mungu, pia alimkataza kufasiri Qur'an kwa mujibu wa rai yake. Baada ya hapo Imamu Redha (a.s), akampa tafsiri sahihi kuhusiana na ya Aya alizoziuliza.[70]

Mauwaji ya Nabii Mussa

Mussa (a.s) alikutana na watu wawili (mmoja ni miongoni mwa wafuasi wake na wa pili ni miongoni mwa adui zak) waliokuwa wakipigana wao kwa wao. Yule ambaye ni miongoni mwa wafuasi wake kamwomba msaada, Musa akiwa katika juhudi za kumtenganua, alimpiga kwa ngumi yule ambaye ni miongoni mwa maadui zake, jambo ambalo lilipelekea kifo chake.[71] Baada ya hapo, Mussa (a.s) akasema: “Hili ni miongoni mwa matende ya Shetani”.[72]na akamwomba Mungu kwa kusema: “Ewe Mola wangu, nimejidhulumu nafsi yangu, basi nakuomba unisamehe”.[73]

Baadhi wanaamini kwamba; hadithi hii ni ithibati ya Mussa kutokuwa na umaasumu; Kwa sababu ikiwa yule aliyemuuwa hakustahili kuuawa, basi bila shaka Mussa (a.s) alifanya dhambi,[74] na ikiwa mtu yule alistahili kuuawa, basi kwa nini Mussa (a.s) alijihisabu kuwa ni mfanya dhambi na akamwomba Mungu wake msamaha kwa kama ilivyokuja kaitka Aya.[75] Kwa upande mwingine, wafasiri wa Qur'an wanaamini kwamba mtu yule aliyeuliwa na Mussa, alistahili kuuawa na Mussa (a.s) hakufanya kosa katika kumuuwa kwake, ingawaje ilikuwa ni bora zaidi kama Nabi Mussa (a.s) angelichelewesha suala la kumuua kwake; Kwa sababu kitendo cha kuuwa mtu huyo, kilimtia Musa mashakani, na hatimae akalazimika kuhama kutoka Misri na kueleke mji mwingine. Kwa hiyo kosa la Mussa ni kushikamana na kitendo chenye thamani ya chini (cha kumuuwa papo hapo) na akaachana na kitendo chenye thamani ya juu (cha kumuuwa katika wakati muwafaka zaidi). Hiyo basi ndiyo dhambi ya Mussa ambayo alimwomba Mola wake amsamehe.[76] Baadhi ya wafasiri wa Kisunni wanaamini kuwa; Mauwaji ya Mussa hakuwa ni mauwaji ya makusudi, na mauwaji yasiyokuwa ya makusudi, hayahisabiwi kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, bali ni miongoni mwa dhambi ndogo. Kwa hiyo Mussa alimuomba Mola wake toba kutokana na dhambi hiyo ndogo aliyoitenda.[77]

Orodha ya Vitabu

Umaasumu wa manabii umejadiliwa katika vitabu vingi vya kitheolojia[78] Pamoja na hayo, pia kuna vikitabu kadhaa vilivyojikita katika mada ya umaasumu peke yake, miongoni mwavyo ni:

  • Tanziyyah Al-Anbiya, cha Sayyid Murtadha (Aliyezaliwa mwaka 436 na kufariki mwaka 355 Hijiria), ambaye ni faqihi na mwanatheolojia wa Kishia wa karne ya nne na tano. Yeye katika kitabu chake hicho, ametafiti umaasumu wa Mitume na Maimamu (a.s) na kujibu ukosoaji na dosari juu ya Aya na Hadithi zinazoonekana kupingana Umaasumu wa Mitume.[79] Kitabu hichi kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiajemi kwa jina la "Pazuheshiy Qur'aniy Dar Baariye Ismate Peyanbarane wa Imaaman.
  • 'Ismatu Al-Anbiya, kilichoandikwa na faqihi, mwanatheolojia na mfasiri waKisunni, bwana Fakhru Al-Din Razi (aliyefariki mwaka 606 Hijiria). Azimio la Kitabu hichi, ni kutetea nafsi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu dhidi ya shaka na kashfa,[80] baada ya kuelezea na kufafanua mitazamo mbalimbali kuhusu umaasumu wa Mitume na uthibitisho wa umaasumu wao,[81] kinachunguza na kukosoa dosari na tuhuma mbali mbali dhidi ya umaasumu wa mitume.[82] Na katika milango yake tofauti, kitabu hichi kimejibu na kukosoa dosari juu ya manabii kama Adam, Nuh, Ibrahim, Mussa, Daudi, Suleiman na Mtume Muhammad (s.a.w.w).[83]
  • Tanzihu Al-Anbiyaa 'An Maa Nasiba Ilaihim Huthalatu Al-Aghbiyaa, kilichoandikwa na Ali Ibn Ahmad anayejulikana kwa jina la Ibn Khumair (Aliyefariki mwaka 640 Hijiria), ambaye ni mmoja wa wanazuoni wa karne ya 6 na 7 ya Mwandamo. Kitabu hichi pia kiliandikwa kwa ajili ya kujibu mashaka na dosari juu ya umaasumu wa Mitume.[84] Nacho kimetafiti shaka mbali mbali juu ya baadhi ya Mitume (a.s) kama vile Adam, Daud, Sulaiman, Musa, Yunus na Mtume Muhammad (s.a.w.w).[85]

Vitabu vingine makhususi kuhusu umaasumu wa Mitume vinaweza kuashiriwa hapa ni: Ismatu Al-Anbiyaa Fil Qur'ani Al-Karim kilichoandikwa na Ja'afar Subhani, Ismatu Al-Anbiyaa wa Al-Rusul, cha Sayyid Mortadha Askari, Ismatu Al-Anbiyaa Fil Qur'an Madkhalun Ila Nubuwwati Al-'Aammah cha Sayyid Kamal Al-Heydariy, Ismatu Al-Anbiyaa cha Zain Al-Abidin Abdul Ali Tahir Al-Kaabiy, Ismatu Al-Anbiyaa Baina Al-Yahuudiyyati Wal Masiihiyyati Wal Islam cha Mahmud Maadhiy, Al-Muraajiatu Fil 'Ismati Al-Anbiyaa-i Min Mandhuri Qur'aniy cha Abdul Salam Zain Al-Abidin, Nure Ismat Bar Simaaye Nubuwwat, ni kitabu kinachojibu hoja dhidi ya umaasumu, zilizosimamishwa kupitia Aya za Qur'an, kilichoandikwa na Jafar Anwari.

Maelezo

  1. Wafasiri wametaja uwezekano mbalimbali katika kufasiri aya hii. (Tazama: Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 53-55).

Rejea

  1. Maʿrifat, Iṣmat-i payāmbarān, uk. 7.
  2. Tamimy Āmidī, Ghurar al-ḥikam, uk. 6; Maʿrifat, Iṣmat-i payāmbarān, uk. 6.
  3. Yūsufīyān wa Sharifi, Pazhūhishī dar ʿiṣmat-i maʿṣumān, 1388 S, uk. 27-30.
  4. Anwārī, Nūr-i ʿiṣmat bar simā-yi nubuwwat, uk. 52.
  5. Ṣādiqī Ardakānī, Iṣmat, uk. 19.
  6. Yūsufīyān wa Sharifi, Pazhūhishī dar ʿiṣmat-i maʿṣumān, 1388 S, uk. 26.
  7. Majlisī, Biḥār al-anwār, uk. 164 na 200.
  8. Subḥānī, Buhuth fi al-milal wa al-nihal, juz. 2, uk. 113-167; Mudhafar, Dalailu al-sidq, juz. 1, uk. 432-552 nakala kutoka kwa Yūsufīyān na Sharifi, Pazhūhishī dar ʿiṣmat-i maʿṣumān, 1388 S, uk. 26
  9. Yūsufīyān na Sharifi, Pazhūhishī dar ʿiṣmat-i maʿṣumān, 1388 S, uk. 41
  10. Mughniyah, Tafsiri al-kashif, 1424 H, juz. 1, uk. 98.
  11. Naqii-Pur, Pazhūhishī Payaramuni Tadabur Dar Qur'an, 1381 S, uk. 339-345.
  12. Subḥānī, Manshūr-i jāwīd, juz. 5, uk. 31.
  13. Ṭabāṭabāʾī, al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān, juz. 16, uk. 313; Taftāzānī, Sharḥ al-Maqāṣid, juz. 5, uk. 50.
  14. Ījī, Sharḥ al-mawāqif, juz. 8, uk. 263.
  15. Taftazan, Sharh al-maqasid, 1412 H, juz. 5, uk. 50.
  16. Subḥānī, Manshūr-i jāwīd, juz. 5, uk. 31.
  17. Mufid, al-Nukat al-I'tiqadiah, 1413 H, uk. 37; Hilli, Kashf al-Murad, 1382 S, uk. 155; Subḥānī, Manshūr-i jāwīd, juz. 5, uk. 31.
  18. Tazama: >Mufid, al-Nukat al-I'tiqadiah, 1413 H, uk. 37; Hilli, Kashf al-Murad, 1382 S, uk. 155.
  19. Mufid, Awail al-Maqalat, uk. 62
  20. Mufid, Adam Sahw al-Nabi, uk. 29 na 30; Hilli, Kashf al-Murad, uk. 155-157
  21. Saduq, Man Laa Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 1, uk. 358-359
  22. Saduq, Man Laa Yahdhuruhu al-Faqih, juz. 1, uk. 359
  23. Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 164 na juz. 3, uk. 294, 355-356
  24. Saduq, Man Laa Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 H, Pavarqi juz. 1, uk. 359
  25. Faryab, 'Ishmat-e Payambaran dar Mandhumeh Fikri Allamah Tabatabai, uk. 24-28
  26. Yusufiyan na Sharifi, Pezuheshi-e dar 'Ishmat-e Ma'suman (a.s), 1388 S, uk. 39.
  27. Yusufiyan na Sharifi, Pezuheshi-e dar 'Ishmat-e Ma'suman (a.s), 1388 S, uk. 39-41.
  28. Yusufiyan na Sharifi, Pezuheshi-e dar 'Ishmat-e Ma'suman (a.s), 1388 S, uk. 39-41.
  29. Tabatabai, al-Mizan, juz. 5, uk. 354
  30. Subhani, 'Ismah al-Anbiya' fi Al-Quran al-Karim, uk. 29; Mishbah Yazdi, Amuzesh 'Aqaid, juz. 2, uk. 161
  31. Tazama: Hilli, Kashf al-Murad, uk. 155.
  32. Ashrafi na Redhai, 'Ismat-e Payambaran dar Qu'ran wa 'Ahdain, uk. 86.
  33. Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 37; Sayyid Murtadha, Tanzih al-Anbiya', uk. 5.
  34. Ma'rifat, Amuzesh 'Ulum-e Qur'an, uk. 602.
  35. Tazama: Tabatabai, al-Mizan, juz. 2, uk. 135-138.
  36. Tazama: Tabatabai, al-Mizan, juz. 2, uk. 135.
  37. Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 202-203; Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 14, uk. 103; juz.12, uk. 348; juz. 4, uk. 45; Saduq, 'Uyun Akhbar al-Ridha, juz. 1, uk. 192-204.
  38. Saduq, al-Khiswal, uk. 399.
  39. Qur'an:Surat Yusuf: 110.
  40. Zamakhshari, al-Kashaf, juz. 2, uk. 52; Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 52.
  41. Tabatabai, al-Mizan, juz. 11, uk. 279.
  42. Subhani, Manshur Jawid, 1383 S, juz. 5, uk. 55-59; Kwa mtazamo wa majibu mengine, tazama: Anwari, Nur-e 'Ismat bar Simai Nubuwat, uk. 109-115.
  43. Qur'an: Surat al-Hajj: 52.
  44. Fakhrurazi, Ismah al-Anbiya, uk. 122
  45. Fakhrurazi, 'Ismah al-Anbiya, uk. 122; Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 60
  46. Fakhrurazi, Ismah al-Anbiya, uk. 122
  47. Tazama: Qur'an: Surat al-Hijr: 42; Surat al-Isra: 65; Surat Swad: 82 na 83.
  48. Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 60-62.
  49. Tabatabai, al-Mizan, juz. 14, uk. 391; Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 62.
  50. Subhani, Manshur Jawid, juz. 5, uk. 63.
  51. Qur'an: Surat Nahl: 61.
  52. Fakhrurazi, al-Tafsir al-Kabir, juz. 20, uk. 227
  53. Fakhrurazi, al-Tafsir al-Kabir, juz. 20, uk. 227
  54. Tabatabai, al-Mizan, juz. 12, uk. 281.
  55. Qur'an: Surat al-Baqarah: 35-37; Surat Taha: 115 na 121.
  56. Qur'an: Surat Hud: 45-47.
  57. Qur'an: Surat Swafat: 88-89; Surat al-Shu'ara: 82.
  58. Qur'an: Surat al-A'raf: 150; Surat al-Qasas: 15-16; Surat Taha: 94.
  59. Quran: Surat Yusuf: 24.
  60. Qur'an: Surat al-Anbiya: 87; Surat al-Swafat: 139-148
  61. Qur'an: Surat al-Baqarah: 120; Surat An-Nisa: 105-106; Surat Tauba: 43; Surat Muhammad: 19; Surat al-Fat-h: 1-3; Surat 'Abasa: 1-10.
  62. Subhani, Ismah al-Anbiya fi Al-Qur'an al-Karim, uk. 91-229; Jawadi Amuli, Wahy wa Nubuwat dar Qur'an, uk. 246-286; Makarim Shirazi, Payam-e Quran, juz. 7, uk. 101-160.
  63. Ahmad Amin, Dhuha al-Islam, juz. 3, uk. 228.
  64. Ahmad Amin, Dhuha al-Islam, juz. 3, uk. 235.
  65. Tazama: Sayyid Murtadha, Tanzih al-Anbiya, UK. 9-131; Subhani, Ismah al-Anbiya fi Al-Qur'an al-Karim, uk. 91-229; Jawadi Amuli, Wahy wa Nubuwat dar Qur'an, uk. 246-286; Makarim Shirazi, Payam-e Qur'an, juz. 7, uk. 101-160.
  66. Milani, 'Ismat-e az Mandhur Fariqein, 1394 S, uk. 102-103.
  67. Milani, 'Ismat-e az Mandhur Fariqein, 1394 S, uk. 100.
  68. Milani, 'Ismat-e az Mandhur Fariqein, 1394 S, uk. 100-102.
  69. Tazama: Sheikh Saduq, 'Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), juz. 1, uk. 192-204.
  70. Saduq, 'Uyun Akhbar al-Ridha (a.s), juz. 1, uk. 192-204.
  71. Qur'an: Surat al-Qasas: 15.
  72. Qur'an: Surat al-Qasas: 15.
  73. Qur'an: Surat al-Qasas: 16.
  74. Sayyid Murtadha, Tanzih al-Anbiya, Sharif Ridha, uk. 67.
  75. Fadhil Miqdad, Lawamiu Ilahiyah, 1380 S, uk. 259.
  76. Sheikh Tusi, Tibiyan, Dar Ihiyau Turath al-Arabi, juz. 8, uk. 137.
  77. Zamakhshari, al-Kashaf, juz. 3, uk. 398.
  78. Ḥillī, Kashf al-murād, uk. 155-157; Taftāzānī, Sharḥ al-Maqāṣid, juz. 4, uk. 49-60; Ījī, Sharḥ al-mawāqif, uk. 263-280.
  79. Haidari Fitrat, Kitabshenasi-yi tawṣīfī-yi tanzīh al-anbiyā' wa l-aʾimma, uk. 103-104.
  80. Fakhr al-Rāzī, ʿIṣmat al-anbīyāʾ, uk. 25.
  81. Fakhr al-Rāzī, ʿIṣmat al-anbīyāʾ, uk. 26-34.
  82. Fakhr al-Rāzī, ʿIṣmat al-anbīyāʾ, uk. 35.
  83. Fakhr al-Rāzī, ʿIṣmat al-anbīyāʾ, uk. 3.
  84. Ibn Khumayr, Tanzīh al-anbīyāʾ ʿan mā nasab-a ilayhim ḥuthālāt al-aghbiyāʾ, uk. 18-19.
  85. Ibn Khumayr, Tanzīh al-anbīyāʾ, uk. 5-6.

Vyanzo

  • Haydari Fitrat, Jamal al-Din. Kitabshinasi-yi tawṣīfī-yi tanzīh al-anbiyā' wa l-aʾimma. Hadith-i Hawza magazine. no. 1, 1389 Sh.
  • Aḥmad Amīn. Ḍuha l-Islām. Cairo: Maktaba al-Usra, 2003.
  • Akramī, Ayyūb. Nubuwwa, pajūhishī dar nubuwwat-i ʿamma wa khāṣṣa. Tehran: Teacher Training University, 1383 Sh.
  • Āmidī, Abū l-Fatḥ ʿAbd al-Wāḥid b. Muḥammad al-. Ghurar al-ḥikam wa durar al-kalim. Edited by Sayyid Mahdi Raja'i. Qom: Dār al-Kitāb al-Islāmī, 1410 AH.
  • Anwārī, Jaʿfar. Nūr-i ʿiṣmat bar simā-yi nubuwwat: pāsukh bi shubahāt-i Qurʾānī. First edition. Qom: Imam Khomeini Education and Research Institute, 1397 Sh.
  • Āqā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1403 AH.
  • Ashrafī, ʿAbbās, Riḍāyī, Umm al-Banīn. ʿIsmat-i Payāmbarān dar Qurʾān wa ʿAhdayn. Published in Pazhuhishnama-yi Maʾarif-i Qurʿani Quarterly, no. 12, 1392 Sh.
  • Baḥrānī, Ibn Maytham al-. Al-Najāt fi l-qiyāma fī taḥqīq amr al-imāma. Qom: Majmaʿ al-Fikr al-Islāmī, 1417 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. ʿIṣmat al-anbīyāʾ. Second edition. Beirut: Dār al-Kutub al-Islāmīya, 1409 AH.
  • Fāryāb, Muḥammad Ḥusayn. 'Iṣmat-i payāmbarān dar manzūma-yi fikrī-yi ʿAllāma Ṭabātabāʾī. Published in Maʿrifat journal, no. 214, 1394 Sh.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Kashf al-murād fī sharḥ tajrīd al-iʿtiqād. Edited by Ja'far Subḥānī. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Ṣādiq (a), 1382 Sh.
  • Ibn Khumayr, ʿAlī b. Aḥmad. Tanzīh al-anbīyāʾ ʿan mā nasab-a ilayhim ḥuthālāt al-aghbiyāʾ. Second edition. Damascus: Dar al-Fikr, 1420.
  • Ījī, Mīr Sayyid Sharīf. Sharḥ al-mawāqif. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1325 Sh.
  • Jawādī Āmulī, ʿAbd Allāh. Waḥy wa nubuwwat dar Qurʾān. Qom: Nashr-i Asrāʾ, 1392 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Payām-i Qurʾān. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1386 Sh.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 Sh.
  • Maʿrifat, Muḥammad Hādī. Āmūzish-i ʿulūm-i Qurʾān. Markaz-i Chāp wa Nashr-i Sāzmān-i Tablīghāt, 1374 Sh.
  • Milānī, Sayyid ʿAli. ʿIṣmat az manzar-i farīqayn. Qom: Markaz al-ḥaqāʾiq al-islāmīyya, 1394 Sh.
  • Misbāḥ Yazdī, Muḥammad Taqī. Āmuzish-i ʿaqāʾid. Qom: Sāzmān-i Tablīghāt, 1367 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Taṣḥīḥ al-iʿtiqād. Edited by Ḥusayn Dargāhī. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamīyya li-alfīya al-Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. ʿAdam sahw al-Nabī (s). Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamīyya li-alfīya al-Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Al-Tafsīr al-Kāshif, Qom: Dār al-Kitab al-Islāmi, 1424 AH.
  • Mullā Ṣadra, Muḥammad b. Ibrāhīm. Tafsīr al-Qurʾān al-karīm. Edited by Muhammad Khajawi. Qom: Intishārat-i Bīdār, 1361 Sh.
  • Naqīpūr far, Walī Allāh. Pajūhishī pīrāmun-i tadabbur dar Qurʾān. Tehran: Uswa, 1381 Sh.
  • Ṣādiqī Ardakānī, Muḥammad Amīn. Iṣmat. Qom: Intishārāt-i Ḥawza ʿIlmīyya, 1388 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1362 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Sharīf al-Murtaḍa al-. Al-Dhakhīra fī ʿilm al-kalām. Qom: Muʾassisa Nashr-i Islāmī, 1411 aH.
  • Sharīf al-Murtada al-. Tanzīh al-anbīyāʾ. Tehran: 1380 Sh.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Manshūr-i jāwīd. Qom: Muʾassisa al-Imām al-Ṣādiq (a), 1383 Sh.
  • Ṭabāṭabāyī, Mūhammad Ḥusayn. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: al-Aʿlamī inistitute, 1390 AH.
  • Taftāzānī, Saʿd al-Din al-. Sharḥ al-Maqāṣid. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1412 AH.
  • Ṭūsī, Naṣīr al-Dīn al-. Taḥṣīl al-muḥaṣṣal. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1405 AH.
  • Yūsufīyān, Ḥasan, Sharīfī , Aḥmad Ḥusayn. Pajūhishī dar ʿiṣmat-i maʿṣumān. Qom: Pajūhishgāh-i Farhang wa Andīsha-yi Islāmī, 1388 Sh.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Third edition. Al-Kashshāf ʿan ḥaqā'iq ghawāmiḍ al-tanzīl wa ʿuyūn al-aqāwīl fī wujūh al-taʾwīl. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿArabī, 1407 AH.