Eidul-Fitr (Kiarabu: عيد الفطر) huadhimishwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal (Mfunguo Mosi), na hii ni moja ya sikukuu muhimu sana za Waislamu. Siku hii inatambulishwa katika hadithi kwamba, ni siku ya sikukuu na siku ya malipo kwa watu ambao Swaumu zao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani zimetakabaliwa na Mola. Kwa hakika Eidul-Fitri ni miongoni mwa sikukuu kubwa katika dini tukufu ya Kiislamu. Baada ya kukamilisha ibada ya funga, kuomba na kujipinda kwa ajili ya ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu hufanya sherehe katika siku hii kubwa wakimshukuru Mola Manani kwa kuwawezesha kukamilisha ibada hiyo. Kwa hakika Eidul-Fitr ni kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni mwezi wa ibada na kujitaka. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, ni haramu kufunga Swaumu katika siku hii. Ni wajibu kwa Waislamu kutoa Zakatul-Fitr katika siku hii. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu kuna adabu, hukumu na matendo maalumu yanayopaswa kufanywa katika usiku wake na katika mchana wa siku ya Eidul-Fitr. Miongoni mwayo ni: Kuhuisha usiku huu (usiku wa kuamkia siku ya Eidul-Fitr), kuswali na kusoma dua, kusoma Qur'an, kuoga (kufanya ghusli), Ziyara ya Imam Hussein(as), na kutamka takbira maalumu. Katika siku hii ni mapumziko rasmi katika mataifa mbalimbali hususan ya Kiislamu. Katika siku hii, Waislamu huswali Swala ya Eidul-Fitr kwa sura ya jamaa na huadhimisha na kusherehekea siku hii kwa mujibu wa ada na utamaduni wao.

Umuhimu wa Eidul-Fitr

Eidul Eidul-Fitr ni siku ya kwanza ya mwezi Shawwal (Mfunguo Mosi). Katika hadithi siku ya Eidul-Fitr imetajwa kuwa ni siku ya Mwenyezi Mungu kutoa zawadi ya funga,[1] siku ya kupewa ujira watenda mema,[2] na siku ya kusamehewa madhambi.[3] Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Ali(a.s) inasema: Eidul-Fitr ni sikukuu ya mtu ambaye Mwenyezi Mungu ameikubali funga, na ambaye ibada zake zimetakabaliwa.[4]

Siku ya Fitr imefanywa kuwa sikukuu ili Waislamu wakusanyike katika siku hii na watoke kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wamshukuru kutokana na neema alizowaruzuku, na siku ya eid ni siku ya kukusanyika, siku ya kula (ya kutokufunga Saumu), siku ya Zaka, siku ya shauku na hamasa na siku ya kuomba dua; kwa kuwa ni siku ya kwanza ya mwaka ambayo ndani yake ni halali kula na kunywa; hii ni kwa sababu mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwa watu wa haki (Shia Ithna'asharia). Hivyo basi Mwenyezi Mungu alipenda katika siku kama hii, Waislamu wawe na kongamano ambalo ndani yake watamhmidi na kumsifu Mwenyezi Mungu na katika siku hii takbira katika Swala ni nyingi kuliko siku nyingine, kwa sababu takbira ni kuonyesha taadhima, kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu kwa baraka za uongofu.[5]

Kupewa Jina

Neno Fitr linatokana na Fatara kwa maana ya kuanzisha, kuumba au kuvumbua.[6] Imeelezwa kuwa, Eidul-Fitr chimbuko lake ni hili; kwani katika siku ya Eidul-Fitr mfungaji Saumu hufungua mdomo na kinywa chake kwa ajili ya vyakula na vinywaji.[7]

Hukumu

 
Sala ya Eidul Fitr katika viwanja vya Tehran, ikiongozwa na Imamu wa jamaa Ayatullah Khamenei (mwaka 1437 H)
  • Zakat al-Fitr: Kwa mujibu wa kauli mashuhuri baina ya mafakihi (Maulamaa wa Fikihi) ni kwamba, wakati wa kuwa wajibu kutoa Zakat al-Fitr ni mwanzo wa usiku wa kumkia Eidul-Fitr. Hata hivyo, Sayyid Abul-Qassim Khui yeye anasema, kutoa Zakat al-Fitr huwa wajibu wakati wa kuchomoza alfajiri ya siku ya idi.[8] Vilevile kwa mujibu wa fat'wa za Marajii Taqlidi, wakati wa kutoa Zakatul Fitr katika siku ya Eidul-Fitr ni mpaka wakati wa adhuhuri [9]. Hata hivyo, mtazamo wa Sayyid Moussa Shubairi Zanjani ni kuwa, siku nzima ya siku ya Eidul-Fitr ni muda wa kutoa Zakatul-Fitr.[10] Hata hivyo kama mtu anakwenda kuswali Swala ya Idi basi anapaswa kutoa Zakatul Fitr yake kabla ya Swala ya Eid au kwa mujibu wa fatuwa ya baadhi ya wanazuoni, anapaswa kutenga kando Zakatul-Fitr na kuwa si yenye kuchanganyika na mali zake nyingine.[11]
  • Swala ya Eid: Kuswali Swala ya Idi katika zama za ghaiba ya Imam Mahdi(a.t.f.s) ni mustahabu; lakini katika zama za uwepo wa mamlaka na utawala wa Imam Maasumu(a.s), Swala hii inakuwa wajibu.[12]
  • Ni haramu kufunga Swaumu siku ya Eidul-Fitr.[13]
  • Abu Swalah Halabi anasema, kusafiri katika siku ya Eid baada ya jua kuchomoza ni haramu na kabla ya kuswali Swala ya Idi (kama itakuwa ni wajibu) na kinyume na hivyo, ni makuruhu [14] kusafiri katika mazingira yaliyotajwa.

Amali na Adabu

Usiku wa Kuamkia Siku ya Eid

Baadhi ya Hukumu na mambo ya kufanya usiku wa kumkia siku ya Eidul-Fitr ni:

یَا ذَا الْمَنِّ وَالطَّوْلِ، یَا ذَا الْجُودِ، یَا مُصْطَفِیَ مُحَمَّدٍ وَ ناصِرَهُ صَلِّ عَلَیٰ مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّددٍ وَاغْفِرْ لِی کُلَّ ذَنْبٍ أَحْصَیْتَهُ وَ هُوَ عِنْدَکَ فِی کِتابٍ مُبِینٍ
Ewe Mwenye neema na ukarimu, Ewe uliyemteua Muhammad, na mwenye kumnusuru, mswalie Muhammad na Aali za Muhammad, na unisamehe kila dhambi uliyoihesabu na ambayo iko dhahiri na wazi katika kitabu.

Baada ya hapo sujudu na ukiwa katika hali ya kusujudu tamka mara 100, "Atubu ilallah" yaani "Natubia kwa Mwenyezi Mungu" na kisha omba haja yoyote kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[20]

  • Takbira maalumu; ni mustahabu baada ya Swala ya Magharibi na Isha katika usiku wa kumkia siku ya Eidul-Fitr kusoma takbira hizi: (الله اکبر الله اکبر، لا اله الا الله و الله اکبر، و لله الحمد، الحمدلله علی ما هدانا، و له الشکر علی ما اولانا)[21]

Inaelezwa kuwa makusidio ya maneno (na mumtukuze Mwenyezi Mungu) yanayopatikana katika Aya isemayo: Na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru, ni hizi takbira ambazo zimeelezwa zisomwe katika usiku wa kumkia Eidul-fitr.[22]

Siku ya Eid

  • Kuoga: Miongoni mwa mambo ya mustahabu kufanya siku ya Eidul Fitr ni kuoga. Mwanzo wa muda wa kuoga ni kuanzia kuchomoza alfajiri; lakini kuhusiana na mwisho wa wakati wa kuoga, kabla ya kutoka na kuelekea kuswali au ni wakati wa Swala ya Adhuhuri au kuzama jua, kuna rai na mitazamo tofauti.[23]
  • Kufuturu: Ni mustahabu kula kitu kabla ya Swala ya Eid hususan tende.[24]
  • Takbira maalumu baada ya Swala ya Alfajiri na Swala ya Eid [25] na vilevile Swala ya Adhuhuri na Alasiri [26], ni mustahabu kusoma takbira hizo maalumu siku ya Eid.
  • Kuswali Swala ya Eidul-Fitr.
  • Ni mustahabu kusoma dua ya Nudba.[27]

Ada na Tamaduni

Eidul-Fitr ni katika sikukuu muhimu za Waislamu ambayo huadhimishwa na kusherehekewa kwa ada na utamaduni maalumu kulingana na eneo husika. Katika mataifa mengi hasa ya Kiislamu, siku hii huwa likizo rasmi kuanzia siku moja hadi siku 23.[28]

NCHI Saudi Arabia Qatar Syria Emirates Oman Kuwait Malysia Jordan Sudan Endonesia Bahrain Afghanistan Pakistan Uturuki Iraq Iran
Mapumziko Siku 23 Siku 11 Siku 9 Siku 9 Siku 9 Siku 9 Siku 7 Siku 6 Siku 5 Siku 5 Siku 5 Siku 3 Siku 3 Siku 3 Siku 3 Siku 2[29]

Rejea

  1. Kuleini, Al-Kafi, 1429 Qamaria, juzuu ya 7, kurasa ya 650
  2. Saduq, Man la yahdhuruhu al-faqih, 1413 Qamaria
  3. Nurii, Mustadrak al-wasail, 1408 Qamaria, juzuu ya 6, kurasa ya 154
  4. Nahjul-balagha, hekima ya 428
  5. Saduq, Man la yahdhuruhu al-faqih, 1413 Qamaria, juzuu ya 1, kurasa ya 522
  6. Ibnu Mandhur, Lisanul-arab, mada "Fitr"
  7. Ibnu Mandhur, Lisanul-arab, mada "Fitr"
  8. Tazama: Tabatabai Yazdi, Uruwatul-uthiqa, 1419 Qamaria, juzuu ya 4, kurasa ya 222
  9. Banu-hashim Khomeini, Taudhihul-masail marajiu, 1381, juzuu ya 2, kurasa ya 180
  10. Shibri Zanjani, Risalatu Taudhihul-masail, 1388 Shamsii, kurasa ya 418
  11. Banu-hashim Khomeini, Taudhihul-masail marajiu, 1381, juzuu ya 2, kurasa ya 180
  12. Najafii, Jawahirul-kalam, 1404 Qamarii, juzuu ya 11, kurasa ya 332
  13. Najafii, Jawahirul-kalam, 1404 Qamarii, juzuu ya 16, kurasa ya 324
  14. Halabii, Al-kafii fil-fiqh, 1404 Qamarii, kurasa ya 155
  15. Tusii, Misbahul-mutahajud, 1417 Qamarii, kurasa ya 589-590
  16. Mufiid, Masaru-shia, 1413 Qamarii, kurasa ya 29
  17. Sayyied Ibnu Tausi, Iqbalul-amal, 1376 Shamsii, juzuu ya 1, kurasa ya 464
  18. Banu-hashim Khomeinii, Taudhihul-masail(marajiu), Maktaba ya Intisharat islamii, juzuu ya 1, kurasa ya 359
  19. Sayyied Ibnu Tausi, Iqbalul-amal, 1376 Shamsii, juzuu ya 1, kurasa ya 457
  20. Qumii, Mafatihul-jinan, Amal shab eid fitr
  21. Qumii, Mafatihul-jinan, Amal shab eid fitr
  22. Sayyid Ibnu Tausi, Iqbalul-amal, 1376 Shamsii, juzuu ya 1, kurasa ya 461
  23. Sayyid Ibnu Tausi, Iqbal bil-amali al-hassanah, 1376 Shamsii,juzuu ya 1, kurasa ya 459; Babu-hashimii Khomeinii, Taudhihul-masail(marajiu), maktaba ya Intisharat islamii, juzuu ya 1, kurasa ya 827
  24. Surat al-baqara, Aya ya 185
  25. Qumii, Mafatihul-jinan, Amali shab eid fitr
  26. Humairii, Qurbul-isnad, 1413 Qamarii, kurasa ya 54
  27. Tusii, Misbahul-mutahajud, 1418 Qamarii, kurasa ya 589; Sayyid Ibnu Tausi, Iqbal bil-amal al-hasanah, 1376 Shamsii, juzuu ya 2, kurasa ya 189
  28. Sayyid Ibnu Tausi, Iqbalul-amal, 1376 Shamsii, juzuu ya 1, kurasa ya 465
  29. «آداب و رسوم عید فطر در کشورهای مختلف»، Shirika la habari Tasnim.

Vyanzo

  • Qurʾān.
  • Abū l-Ṣalāḥ al-Ḥalabī, Taqī al-Dīn b. Najm al-Dīn. Al-Kāfī fī l-fiqh. Edited by Riḍā Ustādī. Isfahan: Kitābkhānih ʿUmūmī-yi Amīr al-Muʾminīn, 1403 AH.
  • Āmulī, Muḥammad Taqī. Miṣbāḥ al-hudā fī sharḥ ʿurwat al-wuthqā. Tehran: n.p. , 1310 AH.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. ʿUmar. Al-Tafsīr al-kabīr. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1425 AH.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukrim. Lisān al-ʿArab. Third edition. Beirut: Dār Ṣādir, 1414 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1429 AH.
  • Mufīd, Mūammad b. Muḥammad al-. Masār al-Shīʿa. Qom: Kungirh-yi Shaykh-i Mufīd, 1413 AH.
  • Nahj al-balāgha. Edited by Ṣubḥī Ṣāliḥ. Qom: Hijrat, 1414 AH.
  • Najafī, Muḥammad Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām. Beirut: Dār al-Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
  • Nūrī, Ḥusayn b. Muḥammad Taqī al-. Mustadrak al-wasāʾil. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt (a), 1408 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1413 AH.
  • Sayyid b. Ṭāwūs, ʿAlī b. Musā. Al-Iqbāl bi-l-aʿmāl al-ḥasana. Edited by Jawād Qayyūmī. Qom: Markaz al-Nashr al-Tābiʿ li-Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1376 Sh.
  • Ṭabāṭabāʾī, Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, n.d.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Miṣbāḥ al-mutihajjid wa silāḥ al-mutiʿbbid. Beirut: Muʾssisat al-Aʿlamī, 1418 AH.
  • Yazdī, Sayyid Kāẓim. Al-ʿUrwa al-wuthqā. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1419 AH.