Ushirikina

Kutoka wikishia
Hakuna anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja

Ushirikina (Kiarabu: الشرك) ni miongoni mwa dhambi zilizoko katika orodha ya dhambi kubwa (kuu), maana ya ushirikina ni kumshirikisha Mungu na mtu au kitu kingine. Ushirikina unapingana na Umoja wa Mungu, na wanazuoni wa Kiislamu wameugawa ushirikina katika viwango tofauti: ushirikina katika asili ya Dhati, Sifa, na vitendo, na ushirikina katika ibada. Ushirikina umegawanywa katika aina mbili: ushirikina dhahiri na ushirikina ulio jificha. Ushirikina dhahiri hujadiliwa katika tafiti za masuala yanayo husiana na imani, na ushirikina ulio jificha unajadiliwa katika tafiti za maadili.

Kuabudu nafsi (kuitii nafsi bila ya mipaka), kuelemea kwenye ulimwengu wa hisia (kimaada), wingi wa shaka, na ujinga, ni miongoni mwa mambo yanayo hisabiwa kuwa ndio sababu za ushirikina. Mambo kama vile; kubatilika au kutokomea kwa natija ya amali, kunyimwa msamaha wa Mungu, kunyimwa Pepo, na kuingia Motoni, yametajwa kuwa ni matokeo ya ushirikina.

Ibn Taymiyyah na wafuasi wake ambao ni Mawahabi, wanawapa sifa za ushirikina Waislamu wote wanaomuomba msaada na kuomba msaada kupitia jaha ya wakubwa wa kidini. Kwa upande wa pili; Waislamu, hasa Mashia, wanalichukulia suala kumwomba msaada (kutawasali) kwa wakubwa wa kidini kama aina ya kuheshimu nembo za kidini. Mashia wanaamini kwamba kuomba msaada wa wafu si ushirikina, bali ushirikina utatimia iwapo suala hilo litaambatana na nia ya kuabudu na kuamini uungu wa wafu hao. Pia, kwa mujibu wa Aya za Qur’ani, msamaha wa wakubwa wa kidini haufanyiki bila ya kuwepo kwa idhini ya Mungu.

Welewa wa dhana

Dhana ya ushirikina ina maana ya kitendo cha kumshirikisha Mungu na mtu au kitu kingine katika mambo yanayomhusu Mungu peke yake, kama vile uwepo wake wa kiungu, uungu wake, ibada yake, na uendeshaji wa mambo ya viumbe. [1] Ushirikina ni kinyume cha tawhidi, au imani juu ya umoja wa Mungu. [2] Hata hivyo, Ayatullah Jawadi ameufasiri ushirikina kuwa ni kinyume cha Imani, na anaamini kwamba sio kila wakati ushirikina husababisha mtu kutoka katika tawhidi na kumweka nje ya kundi la Waumini. Katika Qur'an, neno mshirikina limetumika kwa wapagani (wanao abudu masanamu), [3] Ahlul-Kitab (Mayahudi na Wakiristo), [4] na hata kwa Waumini, [5] katika baadhi ya matukio. [6]

Mshirikina kitaalamu ni mtu anayemshirikisha Mungu na mtu au kitu chengine. Kwa maana hiyo ushirikina ni kuwa na imani kwamba mtu au kitu chengine kina sifa za Mungu, au kwamba sekta ya uumbaji imekabidhiwa mtu au kitu chengine, au kwamba mtu au kitu chengine kina mamlaka ya kuamrisha na kukataza kitu, [7] au kuamaini mtu au kitu chengine kuwa kina hadhi ya kuabudiwa. [8]

Ngazi za ushirikina

Ushirikina kama ilivyo tawhidi nao pia una ngazi mbali mbali, miongozi mwazo ni:

 • Ushirikina katika ngazi ya Dhati ya Mungu; Ushirikina katika ngazi hii una maana mbili: Ya kwanza ni kuamini ya kwamba, Dhati ya Mungu ni mchanganyiko au imejengeka kupitia nyenzo au mambo tofauti. [9] Ya pili ni kuamini uwepo zaidi ya Mungu Mmoja. [10]
 • Ushirikina katika ngazi ya Sifa; Ushirikina katika ngazi hii ni kuamini kuwa Sifa za Mungu ni kitu cha ziada juu ya Dhati yake, na kwamba uwepo wa Sifa zake ni uwepo mwenza, yaani uwepo wa Dhati yake ni uwepo binafsi na uwepo wa Sifa zake ni uwepo mwengine kabisa. [11] 
 • Ushirikina katika ngazi ya vitendo; Ushirikina katika ngazi ya vitendo, ni kinyume cha upweke wa vitendo. Ushirikina katika ngazi hii umegawika katika vifungu tofauti, kama vile; ushirikina katika vitendo vya uumbaji na katika vitendo vya uhimili, ufadhili na malezi.
 1. Ushirikina katika ngazi ya uumbaji; Ushirikina katika ngazi hii, humaanisha imani ya kuwepo muumba zaidi ya mmoja, yaani ni kuamini uwepo wa chanzo asili zaidi ya kimoja cha uumbaji bila ya kimoja kuwa chini ya mamalaka ya chengine. Mfano wa ushirikina huu, kuamini miungu wawili, mmoja wa kuumba shari na mwengine wa kuumba kheri, kwa mujibu wa itikadi hii, mungu wa shari huumba viumbe au vitu vyenye shari tu, na mungu wa kheri huumba viumbe au mambo ya kheri tu. [12]
 2. Shirki katika ngazi ya malezi na uangalizi, nayo imegawika sehemu mbili:
 1. Ushirikina katika ngazi ya malezi, ukuzi na uangalizi wa ulimwengu wa kimaada; Ushirikina huu ni kuamani kwamba, Mwenye Ezi Mungu ameumba ulimwengu tu, ama suala la mipangilio ukuwaji uendeshali uhimili wake unashughulikiwa na au ameukabidhi miungu wengine.
 2. Ushirikina katika ngazi ya uendeshaji wa kisheria na upangaji wa kanuni; Katika ngazi hii shirki huwa kule kuamini ya kwamba, kuna ulazima wa kutekeleza sheria za asiye kuwa Mwenye Ezi Mungu, na kuhisi wajibu juu ya jambo hilo. [13]
 • Shirki katika ngazi ya ibada; Ni ibada, unyenyekevu, khofu juu ya  mtu au kitu chengine mbali na Mwenye Ezi Mungu. [14] Kwa ujumla, shirki inaweza kugawanywa katika aina mbili; shirki ya kinadharia na shirki ya kivitendo.

Mfano wa shirki ya kinadharia; Ni baadhi ya imani ambazo tunazo kuhusiana na Sifa za Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, kumpa Mwenyezi Mungu sifa na tabia za viumbe wengine, hii ni shirki ya kinadharia. Zaidi ya hayo, ikiwa tutafikiria kuwa kuna mwingine anaweza kuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu badala ya Mwenyezi Mungu, hii pia ni shirki ya nadharia.

Shirki ya vitendo; Kwa kiasi kikubwa aina hii ya shirki inahusiana na upande wa vitendo vya ibada. Kwa mfano, ikiwa tunasujudu mbele ya watu au vitu vingine badala ya Mwenye Ezi Mungu na kuonyesha unyenyekevu mbele yake, hapo tunakuwa katika hali ya shirki ya vitendo. [15]

Tathini ya ushirikina

Kuna Aya nyingi na makhususi Qur'an zinazungumzia na kukataza suala la ushirikina. Katika baadhi ya aya za Qur'an, inasemeezwa ya kwamba; washirikina hawana ushahidi wala hoja juu ya madai yao ya ushirikina; [Maelezo 1] [16] bali wanategemea dhana au matamanio yao binafsi. [17][Maelezo 2]

Kulingana na Aya isemayo: ((إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ; Hakika Mwenyezi Mungu hatoi msamaha katika kushirikishwa kwake, na anasamehe yasiyokuwa hili kwa anayetaka.)) [18] Ukiachana na ushirikina, Mwenye Ezi Mungu anasamehe dhambi zote. Baadhi ya wafasiri katika katika kufasiri Aya hii wamesema kwamba; maana ya Aya hii ni kwamba; ushirikina ni dhambi kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa hiyo itasamehewa basi dhambi nyingine pia nazo zitasamehewa. [19] Na ikiwa mshirikina hatatubu na akakufa katika hali ya ushirikina wake, basi kamwe hatasamehewa. Wafasiri hao wanaamini kwamba; kitendo cha toba hakiko ndani ya madumuni ya Aya hiyo. Kwa hiyo Makusudio ya Aya hiyo ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu hasamehe kosa la ushirikina ambalo mtendaji wake hakufanya toba, na kinyume chake ni kwamba; ikiwa mshirikina atatubu kutokana na ushirikina wake anaweza kusamehewa. [20] Katika baadhi ya hadithi pia, imani ya kuamiuni kwamba Mweny Ezi Mungu ana washirika, kumehisabiwa kuwa ndio dhambi kubwa zaidi. Katika Hadithi kutoka kwa Abdullah bin Masoud kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) dhambi kubwa zaidi ni kumwekea Mwenye Ezi Mungu mwenza na kumfanafanisha na wengine. [21]

Imam Ali (a.s) ameligawa tendo la ushirikia kwa mujibu wa Qur’an, katika aina nne: ushirikina wa kimaneno, kimatendo, kiuzinzi, na ushirikina wa unafiki (kujionesha), na alithibitisha kila moja kwa Aya za Qur’an. Katika kuthibitisha ushirikina wa kimaneno ameitegemea Aya isemayo: ((لَقَدْ كَفَرَ الَّذِینَ قَآلُواْ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِیحُ ابْنُ مَرْیمَ ; Kwa hakika wamekufuru waliosema kuwa Mwenyezi Mungu ni Masihi bin Maryam)). [22] Akithibitisha ushirikina wa kimatendo ametumia Aya zifuatazo: ((وَمَا یؤْمِنُ أَكْثَرُهُمْ بِاللَّـهِ إِلا وَهُمْ مُشْرِكُونَ ; Na wengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa wanamshirikisha)). [23] Na Aya isemayo: ((اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّـهِ ; Na wakawafanya wanazuoni makuhani (watawa) wao kuwa ni waabudiwa wao badala ya Mwenye Ezi Mungu)). [24] Akithibitisha shirki ya zinaa ametegemea Aya isemayo: ((وَ شارِكْهُمْ فِی الأَمْوالِ وَالأَوْلادِ ; Na shirikiana nao katika mali na watoto)). "[25] Ili kuthibitisha ushirikina wa unafiki (kujionesha) ametumia Aya ifuatayo: ((فَمَن کانَ یرْجُوا لِقاءَ رَبِّهِ فَلْیعْمَلْ عَمَلاً صالِحاً وَ لایشْرِکْ بِعِبادةِ رَبِّهِ أَحَدا ; Basi mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi afanye mambo mema (yanayo stahiki), wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi)). [26] [27] Kwa mujibu wa Hadithi; tendo la jimai haramu, tonge ya haram, kutomkumbuka Mungu wakati wa kujamiiana na baadhi ya matendo mengine kadha, ni sababu inayo pelekea Shetani kushiriki katika tendo la kutunga mimba. Bila shaka popote Shetani alipo -kwa kadiri hudhurio lake lilivyo- tauhidi safi haitawezi kupatikana, na kwa sababu hiyo, aina hii ya ushiriki wa Shetani katika tendo la ndoa, inaweza kuchukuliwa kama mfano hai wa ushirikina wa kiuzinzi, hii ni kulingana na maelezo ya Hadithi yalivyo. [chanzo kinahitajika]

Aina za ushirikina

Makala asili: Ushirikina ulio kifichoni

Ushirikina unaweza kugawanywa katika aina mbili kulingana na uwazi au kuto kuwa wazi kwake. Mfano wa ushirikina wa wazi, ni kufanya taratibu na matendo fulani ya ibada kama vile kurukuu, kusujudu na kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu, [28] pamoja na kuwa na imani juu ya uungu wa anayetendewa matendo hayo. Ushirikina uliofichika nao unajumuisha aina yoyote ya kuabudu mambo ya kilimwengu, kutii matamanio ya nafsi (kuiabudu nafsi) na unafiki (kutenda amali kwa ajili ya kujionesha) n.k. [29] Imam Swadiq (a.s) katika maelezo yake juu ya Aya ya 106 ya Surat Yusuf [Maelezo 3] ameiorodhesha baadhi ya misemo kama vile; asingekuwa fulani basi ningeangamia, lau asingelikuwako fulani, ningeingia katika matatizo fulani, na kuihisabu kuwa ni shirki katika mamlaka ya utawala wa Mwenyezi Mungu. [30] Mtume wa uislamu Muhammad (s.a.w.w) akitoa sifa za ushirikina ulio kifichoni, amesema kwamba; ushirikina umefichika zaidi kuliko sisimizi anayetembea juu ya jiwe tambarare katika usiku wa giza [31] Ushirikina uliojifichwa unajadiliwa zaidi katika elimu ya maadili au elimu ya akhlaqi.

Sababu na mizizi ya ushirikina

Kuna vishawishi na sababu zilizotajwa kuhusiana na ushirikina, miongoni mwazo ni:

 • Kufuata dhana potofu na shaka zisizo na mashiko: Katika surat Yunus Mwenye Ezi Mungu akizungumza na washirikina amewaambia: “Kutokana na kule nyinyi kufuata dhana na makadirio, hilo limekupelekeeni kuingia katika shirki” [32]
 • Kuamini tu ulimwengu wa kimaada: Kutokana na kuamini tu ulimwengu wa kimaada, kumepelekea misingi ya elimu za baadhi ya watu kujikita katika mambo yanayohisiwa na viungo vya hisia peke yake, na kushindwa panda daraja ya juu zaidi, hilo ndilo lililo pelekea wao kuyashusha daraja ya chini mambo na masuala yanayo husiana na dhana za utambuzi wa Mwenye Ezi Mungu, na kuyaweka katika mizani ya ulimwengu wa hisia. [33]
 • Ujinga: Qur’ani imelihisabu suala la kumpachika Mungu sifa ya kuwa na watoto, na kumshirikisha Mwenye Ezi Mungu, kuwa ni suala linalotokana na ujinga. [34]

Pia kuipenda dunia, kuabudu matamanio ya nafsi, kutomkumbuka Allah, kuwapa vyeo na sifa zilizopindukia mipaka wanazuoni au watumishi wa kidini, usugu wa kutokubali haki pamoja na uwepo wa serikali zisizostahiki kutawala, ni miongoni mwa mambo yaliyo hisabiwa na Qur’ani kuwa ni sababu na vishawishi vinavyo chochea uwepo wa ushirikina. [35]

Matokeo ya hatima ya shirki

Kwa mujibu wa maelezo ya Qur'ani, tendo la shirki hufwatiwa na matokeo kadhaa, miongoni mwayo:

 • Kuharamikiwa na Pepo; Kwa mujibu wa maelezo ya Aya ya 72 ya Surat al-Maida ni kwamba, ni haramu kwawashirikinakuingia Peponi.[36][Maelezo 4]
 • Kuharamikiwa na kupata radhi za Allah; kwa maelezo ya Aya ya 4 na Aya ya 116 za Surat al-Nisaa, washirikina wameharamishiwa kupata radhi za Mwenye Ezi Mungu, ila dhambi nyengine ni zenye kusamehewa. [37][Maelezo 5][38]
 • Kuingia Motoni; kwa maelezo ya Aya ya 72 ya Surat al-Maida ni kwamba, hatima ya washirikina ni motoni. [39]
 • Kubatilika kwa matendo; Shirki hupelekea kubatilika kwa amali njema za mwanadamu.[Maelezo 6][41]

Hukumu ya shirki kwa mujibu wa fiqhi

Kwa mtazamo wa dini ya Kiislamu, shirki ni haramu na inachukuliwa kuwa ni miongoni mwa dhambi kubwa (dhambi kuu). [42] Wanafiki wamewahukumu washirikina kwa hukumu ya najisi na kupiga marufuku wasiingie Msikiti Mtukufu (Msikiti wa Makka). Hukumu hiyo ni kulingana na Aya isemayo: “إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلاَ يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ”.

Ila tukirejea katika mitabu cha Sheikh Tusi kiitwacho “al-Nihayah” tutaona kuwa hakujuzisha kwa wanaume wa Kiislamu kuwaoa wanawake washirikina, lakini amejuzisha  kuwaoa wanawake wa Kiyahudi na Wakristo kwa ndoa ya muda, si kwa ndoa ya daima. [45]

Tuhuma za Mawahabi kwa Mashia

Mawahabi wanaichukulia imani ya Waislamu ya kuwaomba mambo yao kupitia jaha za wafu, kuwaomba shufaa manabii na mawalii wa Mungu, kutafuta baraka kwenye makaburi na kuwaomba msaada walioko katika ulimwengu wa Barzakh, kuwa ni miongoni mwa mifano ya ushirikina katika ibada. Ibn Taymiyyah anaamini kuwa; kuuomba dua kupitia jaha ya Mtume (s.a.w.w) au watu wema si shirki wakati wa uhai wao. Yaani ikiwa mtu atakwenda kwa watu hao na kuwataka wamwombee dua, hiyo haitakuwa shirki, bali kuwakimbilia wao baada ya kufa kwao ni shirki. [46] Kwa mtazamo wa Ibnu Taymiyyah; yeyote yule atakaye kwenda na kuomba msaada kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w) au kwa walii yeyote yule, basi huyo atahisabiwa kuwa ni mshirikina. Na ni lazima mtu huyo kulazimishwa kutubu, na asipotubia basi ni lazima auwawe. [47] Abd al-Aziz bin Baaz, Mufti wa Kiwahabi pia katika kazi zake za uwandishi, ameorodhesha masuala kadhaa na kuyahisabu kuwa na masuala ya kishirikina. Kwa mtazamo wake; kuomba dua au kuomba msaada kwa walio ndani ya makaburi, kuomba ponyo la maradhi na kuomba ushindi dhidi ya maadui, ni miongoni mwa mifano hai ya ushirikina mkuu (Shirku Akbar). [48] Mawahabi Wanalinganisha vitendo hivi vya Waislamu na vitendo vya washirikina wa mwanzoni mwa zama za Uislamu katika kuabudu masanamu. [49]

Kwa kujibu tuhuma hizo, wanazuoni wa Kiislamu wamewaambia kwa kusema: Vitendo vya washirikina vilifanywa kwa kuamini kwamba masanamu ni miungu walezi na wamiliki; Lakini matendo ya Waislamu kuhusu mawalii wa Mungu hayahusiani na imani hiyo. Bali kuyajengea makaburi na kuomba shufaa kutoka kwao, ni miongoni mwa kuzitukuza nembo za kidini. [50] Pia, Waislamu wanaofanya vitendo hivi hawakusudii kamwe kuwaabudu manabii na mawalii hao wa Mungu na wala hawana imani ya uungu juu yao. Bali nia yao ni kuwaheshimu tu manabii na mawalii hao, na kutafuta ukaribu wa Mungu kupitia kwao. [51]

Kwa mujibu wa aya za Qur’an Tukufu, uombaji wa shufaa huhisabiwa kuwa ni shirki iwapo mwombwa ataombwa kwa kutegemewa yeye mwenyewe binafsi, na kwamba yeye mtekelezaji wa kujibu maombi hayo bila ya kuhitaji idhini ya Mwenyezi Mungu. [52] Kwa sababu uombaji kama huo utakua ni kumshirikisha Mungu katika Umola wake Malezi na mamlaka yake ya uendeshaji. Wanazuoni wa Kiislamu wakiendelea kujibu hoja za Mawahabi, wameeleza kwamba; hoja za Kiwahabi zinategemea Aya za Qur'an Tukufu ambamo ndani mmekatazwa kuyaomba masanamu. Wanazuoni hao pia wanabainisha tofauti za kimsingi kati ya kuomba shufaa kutoka kwa Mtume na mfumo wa kuomba shufaa ulikuwa ukitumiwa na waabudio masanamu kutoka kwa masanamu hayo, na wanaamini kwamba Waislamu, ni tofauti na waabudio masanamu, kamwe hawamchukulii Mtume kuwa ni Mungu, Bwana au mtawala wa ulimwengu. [54]

Mutahri, ambaye ni mwanatheolojia wa Kishia, kwa kuzingatia mtazamo wa Qur’an katika Aya ya 86 ya Surat Zukhruf isemayo: (( وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنْ شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ )). Anaamini kwamba Hakuna hata mmoja asiye kuwa Mungu katika wale wanao waomba (shufaa), mwenye kumiliki shufaa, isipokuwa wale walioshuhudia haki (ndio wanao weza kuwa na shufaa) nao wakiwa na elimu juu ya haki hiyo (tawhidi). Na sio kukiri kwa ulimi tu juu ya haki hiyo bali elimu yao pia inafahamu ukweli huo. Na hapo hapazungumziwi elimu ya kinadharia tu, bali ni elimu yanye nuru ya kuona na kuifikia haki hiyo. Wenye uwezo huo wa kielimu wa kuiona haki kwa nuru ya elimu, ni wenye kujielewa na wanjuwa ni nani anaye stahiki kuombewa shufaa na nani hastahiki kupata shufaa hiyo. Kwa imani Mutahari ni kwamba; shufaa ni jambo jambo linalowahusu wapwekeshaji Mungu, na halihusiani na wasio kuwa na hisia wa akili ya kitauhidi (masanamu), kwa hiyo masananu hayawezi kuwa ni waombezi wa kuwaombea watu shufaa. [55] Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai, mfasiri wa Kishia, akiamini kwamba; Mwenyezi Mungu ni chanzo cha neema kwa viumbe vyote. Amaamini pia mambo yote yanayo husiana na viumbe kama vile; kifo, riziki, baraka, na mengineyo yaliyopo katika mfumo wa sababu na visababishaji ni yenye kuhusiana na mamlaka ya Mungu [hii ni kwamba kila moja kati ya haya, yanahusiana na Mwenyezi Mungu kupitia fungamano maalumu linalo yafungamanisha na Mola Mweza.] Naye analichukulia suala la uombezi kuwa ni sehemu ya mfumo wa sababu na visababu zinazotawala katika ulimwengu wa uwepo. Kwa hiyo mfumo wa sababu na visababishaji vya matokeo mbali mbali haumaanishi kuwa upo njia ya Mwenye Ezi Mungu, au ni wenye kuvunja mamlaka ya sheria na desturi za kiungu zinazotawala ulimwengu na kukengeuka kila moja miongoni mwa visababishaji, kuwa ni njia ya moja mpya isio kuwa ya Mwenye Ezi Mungu Mweza. [56]

Mada zinazohusiana

Maelezo

 1. Kwa mfano Aya isemayo: (وَ مَنْ یدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلهاً آخَرَ لابُرْهانَ لَهُ بِهِ ; Na anaye mwomba mungu mwengine akimjumuisha pamoja na Mwenyezi Mungu, katu hatakuwa na hoja juu ya hilo). Rejea Surat al-Muuminun, Aya ya 117.
 2. وَ ما یتَّبِعُ الَّذینَ یدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّـهِ شُرَكاءَ إِنْ یتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَ إِنْ هُمْ إِلاَّ یخْرُصُون ; Na wale wanaomlingania asiyekuwa Mwenyezi Mungu wanafuata dhana isiyo na msingi na wanasema uwongo tu." Rejea Surat Yunus, Aya ya 66.
 3. (( وَمَا یؤْمِنُ أَكْثَرُهُمْ بِاللَّـهِ إِلا وَهُمْ مُشْرِكُون ; Na wengi katika wanaodai kumuamini Mwenyezi Mungu ni washirikina )). Rejea Surat Yusuf, Aya ya 106.
 4. إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ (Surat al-Maida, Aya ya 72).
 5. إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا (Surat al-Nisaa, Aya ya 48).
 6. وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ (Surat Zumar, Aya ya 65).

Vyanzo

 • Āmulī, Sayyid Ḥaydar. Tafsīr al-muḥīṭ al-aʿzam wa l-baḥr al-khaṣm fī taʾwīl kitāb Allāh al-ʿazīz al-muḥkam. Edited by Muḥsin Mūsawī Tabrīzī. Qom: Muʾassisa Farhangī wa Nashr Nūr ʿala Nūr, 1422 AH.
 • Fāḍil Lankarānī, Muḥammad. Tafṣīl al-sharīʿa fī sharḥ Taḥrīr al-waṣīla. Qom: 1409 AH.
 • Ḥusaynī Shīrāzī, Sayyid Muḥammad. Taqrib al-Qurʾān ila l-adhhān. Beirut: Dār al-ʿUlūm, 1424 AH.
 • Ibn Manẓūr, Muḥammad b. Mukarram. Lisān al-ʿArab. Qom: Adab al-Ḥawza, 1405 AH.
 • Ibn Shuʿba al-Ḥarrānī, Ḥasan b. ʿAlī. Ṭuḥaf al-ʿuqūl. Edited by Ali Akbar Ghaffāri. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmiyya, 1404 AH.
 • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Majmūʿa al-fatāwā. Edited by Shaykh ʿAbd al-Raḥmān b. Qāsim. Medina: Majmaʿ al-Malik Fahd li-Ṭibāʿa al-Muṣḥaf al-Sharīf, 1416 AH.
 • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Ziyārat al-qubūr wa l-istinjād bi-l-maqbūr. Tanta: Dūr al-Ṣaḥāba li-l-turūth, 1412 AH.
 • Jawādī Āmulī, ʿAbd Allāh. Tawhīd dar Qurʾān. Qom: Markaz-i Nashr-i Isrāʾ, 1395 Sh.
 • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. 2nd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
 • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Payām-i Imām Amīr al-Muʾminīn (a). Qom: Intishārāt-i Maṭbūʿātī-yi Hadaf, 1374 Sh.
 • Muṣṭafawī, Ḥasan. Al-Tahqīq fī kalimāt al-Qurʾān al-karīm. Tehran: Bungāh tarjuma wa nashr-i kitāb, 1360 SH.
 • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Mustadrak al-wasāʾil wa musṭanbit al-wasāʾil. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1408 AH.
 • Qafārī, Naṣir b. Abd Allāh. Usūl madhhab al-shīʿa al-imāmīyya al-ithnā ʿasharīyya.
 • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Edited by Ṭayyib Mūsawī Jazāʾrī. Qom: Dār al-Kitāb, 1367 Sh.
 • Subḥānī, Jaʿfar. Marzha-yi tawhīd wa shirk dar Qurʾān. Tehran: Mashʿar, 1380 Sh.
 • Subḥānī, Jaʿfar. Āʾyīn-i Wahhābiyyat. [n.p]. [n.d].
 • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Intishārāt-i Islāmī (Jāmiʿat al-Mudarrisīn), 1417 AH.
 • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Nihāya fī mujarrad al-fiqh wa l-fatāwā. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1400 AH.
 • Ustādī, Riḍā. Shīʿa wa pāsukh bi chand pursish. Tehran: Mashʿar, 1385 Sh.