Wilayat al-Faqih
- Makala hii imeandikwa ili kuzungumzia Wilaya al-Faqih (uongozi wa faqih au utawala wa mwanazuoni) ikiwa kama ni nadharia ya kisiasa. Ili kujua maana jumla ya Wilayat al-Faqih, angalia makala ya Faqih Jami’ al-Sharait (fakihi aliyetimiza masharti).
Wilayat al-Faqih (Kiarabu: ولاية الفقيه), uongozi wa faqih au uongozi wa mwanachuoni ni nadharia iliyopo katika elimu ya fiqh ya Kishia ambayo kwa mujibu wake, katika zama za ghaiba ya Imam Mahdi (a.t.f.s) ambaye ndiye Imam wa zama, utawala upo mikononi mwa fakihi aliyetimiza masharti. Mzizi wa kihistoria wa nadharia hii unarejea katika zama za Bwana Mtume (s.a.w.w). Wanazuoni na mafakihi kama Sheikh Mufid, Muhaqqiq Karaki walizungumzia kuhusiana na mamlaka ya utawala wa mafakihi, lakini Mulla Ahmad Naraqi anahesabiwa kuwa fakihi wa kwanza ambaye alikusanya na kutimiza mamlaka, masharti na majukumu ya fakihi chini ya anuani ya Wilayat al-Faqih (uongozi wa Fakihi Mtawala).
Kwa mujibu wa nadhari ya uongozi wa mwanachuoni au fakihi, mamlaka yote ya masuala ya jamii ya Kiislamu yako mikononi mwa Fakihi Mtawala. Miongoni mwa wanachuoni na wasomi wa Kiislamu wanaokubaliana na nadhari hii ni Kashif al-Ghitaa, Muhammad Hussein Najafi na Imam Khomeini. Kundi la wanazuoni linalopinga mtazamo huu miongoni mwao ni Sheikh Ansari, Akhund Khorasani na Ayatullah Khui.
Hadithi iliyonukuliwa na Maqbula Omar bin Handhala inatajwa kuwa moja ya hoja za kinakili zinazotumiwa na wafuasi wa nadhari ya Wilayat al-Faqih. Kumeandikwa vitabu na makala ambalimbali kuhusiana na maudhui ya Wilayat al-Faqih. Baadhi ya vitabu hivyo ni: Wilayat al-Faqih kilichoandikwa na Imam Khomeini, Velatay Faqih; Velayat Fuqahat va Adalat, kilichoandikwa na Ayatullah javad Amoli.
Utambuzi wa Maana
Kwa mujibu wa fasili na maana iliyotolewa na mafakihi ya Wilatay al-Faqih ni kwamba, maana yake ni usimamizi, kuwa na udhibiti Mujtahidi aliyetimisha masharti katika masuala ya watu wengine, [1] na kwa ibara na maneno mengine ni kuwa na usimamizi wa jamii ya Kiislamu kwa minajili ya kutekelezwa sheria za Kiislamu na kupatikana thamani za kidini katika jamii. Kwa maana kwamba, thamani za kidini zitawale katika jamii. [2] Wilayat al-Faqih, uongozi wa faqih au uongozi wa mwanachuoni ni nadharia iliyopo katika elimu ya fiq’h ya Kishia ambayo kwa mujibu wake, katika zama za ghaiba ya Imam Mahdi (a.t.f.s) ambaye ndiye Imam wa zama, utawala wa jamii ya Waislamu upo mikononi mwa fakihi aliyetimiza masharti. [3]
Historia Yake
Baadhi ya waaandishi wamemtambua Mulla Ahmad Naraqi (aliyeaga dunia 1245 Hijria) kwamba, ndiye fakihi wa kwanza ambaye aliibainisha Wilayat al-Faqih kama suala la kifikihi na akiwa na lengo la kuthibitisha hilo alitumia hoja za kinakili na kiakili; [4] na wakasema kwamba, na ndiye aliyekusanya kwa mara ya kwanza na kwa pamoja katika kitabu cha Awaid al-Ayyam majukumu na mamlaka yote ya mtawala wa Kiislamu na Wilayat al-Faqih. [5] Hata hivyo kabla ya Mulla Naraqi baadhi ya Maualamaa wa Kishia waliwahi kuzungumzia suala la kuchukua baadhi ya mafakihi baadhi ya majukumu na mamlaka ya Maimamu. Kwa mfano Sheikh Mufidu mmoja wa Maulamaa wa karne ya 4 na 5 Hijria ameandika katika kitabu chake cha al-Muqni’ah: Maimamu wa madhehebu ya shia wamelikabidhi suala la kutekeleza adhabu (adhabu isiyo ya kifedha ambayo ni maalumu kwa baadhi ya madhambi). [6] Kadhalika Rasul Ja’afariyan ambaye ni msomi na mwandishi wa historia anasema: Muhaqqiq Karaki, mmoja wa Maulamaa wa karne ya 10 Hijiria alikuwa akiamini kwamba, mafakihi wana majukumu na mamlaka ya kiutawala ya Maimamu Maasumina (a.s). [7]
Hoja ya Waungaji Mkono
Wafuasi wa nadharia ya Wilaya al-Faqih, wakiwa na lengo la kuthibitisha mtazamo wao huo, wametumia hoja za kiakili na kinakili. [8] Hadithi ya Maqbula Omar ibn Handhala na tawqi’ (barua na maandiko ya Imam Mahdi) ni katika hoja zao za kinakili. Imepokewa kutoka kwa Omar bin Handhala ya kwamba amesema: Nilimuuliza Abu Abdillah (Imam Ja'afar Swadiq a.s): Watu wawili katika watu wetu wamezozana kuhusiana na deni au mirathi na wanaenda kutatuliwa mzozo na kesi yao kwa mtawala na makadhi wa zama hizi, je, kitendo hiki kinajuzu? Imam Swadiq (a.s) akasema: Mtu ambaye atawarejea watawala hao kwa ajili ya kutafuta utatuzi katika jambo la haki au batili, kwa hakika wamehukumiwa kwa taghuti, analitolea hukumu mtawala huyo hata kama litakuwa ni haki isiyo na shaka kwa mmoja wao, atakuwa amechukua mali ya haramu, kwa sababu amechukua kwa hukumu ya taghuti ilihali Mwenyezi Mungu ameamrisha walikatae hilo. Mwenyezi Mungu anasema:
Nikamwambia Imam: Basi wafanye nini? Akasema: Waangalie mtu miongoni mwenu ambaye amepokea hadithi kutoka kwetu na akaangalia katika haramu zetu na halali zetu na akafahamu hukumu zetu, waridhie hukumu yake. Kwa hakika mimi nimemjaalia kuwa hakimu kwenu nyinyi. Endapo atatoa uamuzi kwa mujibu wa hukumu zetu na mmoja kati ya wawili hao asiikubali hukumu na uamuzi huo, kwa hakika atakuwa amepuuza hukumu ya Mwenyezi Mungu na ametukataa sisi, na mwenye kutukataa sisi amemkataa Mwenyezi Mungu na huyo atakuwa katika kiwango cha shirki kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa mtazamo wa Imam Sadiq (a.s) ni kwamba, utawala unapaswa kuwa mikononi mwa faqih ili aweze kuhukumu na kutekeleza hukumu. [9] Katika Tawqi’ (barua na maandiko) ya Imam Mahdi kumezungumziwa na kubainishwa suala la matukio yatakayotokea kwamba, kuna ulazima wa kurejea kwa wapokezi wa hadithi za Ahlul-Bayt (a.s). [10] Imam Khomeini akitumia tawqi’ (barua au maandiko ya Imam Mahdi) kama nyaraka na hoja, amefikia natija hii kwamba, mambo na masuala yote ya jamii ya Kiislamu yanapaswa kukabidhiwa kwa mafakihi. [11]
Miongoni mwa hoja za kiakili ni kwamba, maisha ya kijamii ya mwanadamu na ukamilifu wa mtu binafsi na wa kimaanawi mbali na kuhitajia sheria za Mwenyezi Mungu na kulindwa na makosa na mapungufu, yanahitajia pia mtawala wa kidini na msomi muadilifu. Bila ya nguzo mbili hizi, maisha ya kijamii yatakumbwa na hali ya shaghalabaghala katika jamii na kujitokeza ufisadi wa kijamii, kiitikadi na kimaadili (kiakhlaqi). Hivyo basi, ili kuzuia kujitokeza shaghalabaghala na hali ya mparaganyiko na kutokuweko nidhamu na kuifanya jamii isikumbwe na ufisadi, hakuna chaguo bighairi ya kuundwa dola na utawala na kuwekwa nidhamu katika masuala yote ya nchi. Lengo hili lilitekelezwa na Mitume na Maimamu katika zama zao na katika zama za ghaiba, na hii leo litafikiwa na kupatika kupitia Waliyul Faqih (Fakihi Mtawala).
Wapinzani
Miongoni mwa waliotajwa kuwa wapinzani wa Wilayat al-Faqih ni Sheikh Ansari, Akhund Khorasani, [12] Mirza Naini na Ayatullah Khui, [13]. Kwa mujibu wa fatwa ya Sheikh Ansari katika zama za ghaiba, masuala kama kutoa fat’wa na kutoa hukumu yapo mikononi mwa mafakihi, [14] lakini Wilaya na usimamizi wa mali na roho ni makhsusi kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watoharifu (a.s). [15]
Wilayat al-Faqih katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopatika mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini, Wilayat al-Faqih ilitiwa na kuongezwa katika katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Imekuja katika kipingee cha 57 cha kartiba hiyo kwamba: “Mihimili ya utawala katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni: Bunge, serikali na mahakama ambavyo vyote hivyo viko chini ya uangalizi Wilayat Mutlaki wa amri na Uimamu wa umma….” [16]
Katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini ndiye aliyekuwa Waliyul-Faqih na baada yake ni Ayatullah Sayyied Ali Khamenei. [17]
Utambuzi wa Kitabu
Kazem Ostadi ameorodhesha katika kitabu chake cha “Kitab Shenasi hukumat va velayat faqih” zaidi ya majina 700 ya vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na utawala wa Kiislamu na Wilayat al-Faqih. Akthari ya vitabu hivi vimeandikwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu. [18] Baadhi ya vitabu muhimu vilivyoandikwa kuhusiana na Wilaty al-Faqih ni:
- Wilayat Faqih: Majimui ya hotuba 13 za Imam Khomeini alizotoa katika Hawza ya Najaf kuhusiana na “Wilaya al-Faqih”. Kitabu hiki kilichapishwa kwa mara ya kwanza Beirut, Lebanon.
- Dirasat fil Wilayat al-Faqih wa Fiq’h al-Dawlah al-Islamiyah: Masomo na uhakiki wa Hussein Ali Montazeri.
- Velatay Faqih, va velayat Faqahat va adalat: Mwandishi, Ayatullah Javad Amoli.
- Velayat Faqih va hukumat Salihan, mwandishi: Neematullah Salihi Najafabadi.
- Al-Wilayat al-Ilahiyah al-Islamiyah au al-Hukumat al-Islamiya zaman hudhur al-Maasum a zaman al-Ghaibah, mwandishi Muhammad Mu’umin Qomi.
- Velayat Faqih dar hukumat eslam, majimui ya masomo ya Allama Tehrani ambayo yalipangwa na kukusanywa na baadhi ya wanafunzi wake na kuchapishwa katika mijalada minne.
Vyanzo
- Firhi, Daud, Fiqh va siyasat dar Iran Muashir, Teheran: Nashr Ney. 1393 S.
- Firhi, Daud, Nezame Siyasi va Daulate dar Eslam, Teheran: Penerbit Samt, 1386 S.
- Firhi, Daud, Qudrate Danesh Mashruiyat dar Eslam, Teheran: Nashr Ney. 1396 S.
- Firhi, Daud, Shieh va Demokrasi Mashverati dar Iran. Majalah Fakultas Hukum dan Ilmu Politik Universitas Teheran, No.67. 1384 S.
- Ghulpaighani, Sayyied Muhammad Ridha. Al-Hidayah ila man Lahu al-Wilayah. Atas tulisan: Ahmad Shabiri Hamadani, Qom: Daftar Nasyre Nuwide Islam, 1377 S.
- Imam Khomaini, Sayyied Ruhullah, Kitab al-Bai'. Qom: Penerbit Ismailiyan, 1363 S.
- Imam Khomaini, Sayyied Ruhullah, Welayat-e Faqih. Teheran: Muasseseh Tanzhim va Nashre Atsare Imam Khomaini, 1373 S.
- Ja'fariyan, Rasul, Din va Siyasat dar Daure Safavi. Qom: Penerbit Anshariyan, 1370 S.
- Jahan Bozorgi, Ahmad, Pishine Tarikhi Nazariye Velayate faqih. Majalah Qabasat. No 5 dan 6. 1376 S.
- Jawadi Amuli, Abdullah, Velayate Faqih, Velayate Faqahat va Edalat, Qom: Markaz Nashre Esra. 1378 S.
- Kadivar, Muhsen, Hukumate Velai, Teheran: Nasyre Ney, 1378 S.
- Kadivar, Muhsen, Nazariyehhaye Daulat dar Fiqh Shieh, Teheran: Nashre Ney, 1387 HS.
- Kasyif al-Ghita, Ja'far bin Khidhr, Kashf al-Ghita an Mubhamat al-Shariah al-Gharra, Qom: Penerbit Islami, 1422 H.
- Kulaini, Muhammad bin Yakub. Al-Kafi. Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1407 H.
- Mukmin Qummi, Muhammad, Jaigahe Ahkam Hukumati va Ekhtiyarate Wali Faqih. Qom: Nashre Ma'arif, 1393 HS.
- Muntazeri, Hussein Ali, Badru al-Zhahir fi Shalati al-Jumah wa al-Musafir, tulisan: Sayyied Muhammad Hussein Burujerdi. Qom: Kantor Ayatullah al-Uzma Muntazeri. 1416 H.
- Muntazeri, Hussein Ali. Dirasat fi Wilayat al-Faqih wa Fiqh al-Daulah al-Islamiyah. Qom: Maktab al-A'lam al-Islami, 1408 H.
- Muntazeri, Hussein Ali. Mabani Fiqh Hukumate Eslami. Penerjemah: Mahmud Shalawati, Abulfadhl Shakuri. Teheran: Kaihan, 1367 S.
- Muntazeri, Hussein Ali. Nizhamu al-Hukmi fi al-Islam. Teheran: Nashre Sarai. 1375 S.
- Mutahhari, Murtadha, Piramune Jumhurie Eslami, Teheran: Penerbit Sadra, 1368 S.
- Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam. Beirut: Dar al-Ihya al-Turath al-Arabi, 1404 H.
- Naraqi, Ahmad bin Muhammad Mahdi, Awaid al-Ayyam, Qom: Penerbit Islami, 1417 H.
- Salehi Najaf Abadi, Nikmatullah, Wilayat-e Faqih Hukumat-e Salehan. Teheran: Intisyarate Umid Farda, 1382 S.
- Swaduq, Muhammad bin Ali, Kamal al-Din wa Tamamu al-Ni'mah. Editor: Ali Akbar Ghaffari, Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1395 H.
- Shahid Awal, Muhammad bin Makki, Al-Qawaid wa al-Fawaid, Qom: Toko buku Mufid, 1400 H.
- Sheikh Anshari, Murtadha, Al-Makasib al-Muharramah, Qom: Kongres Sheikh A'zham Anshari, 1415 H.
- Sheikh Mufid, Al-Muqni'ah, Qom: Muasseseh Intisyarat-e Islami, Cet. Kedua. 1413 H.
- Undang-Undang dasar Republik Islam Iran, website Pusat Penelitian Majelis Permusyawaratan Islam, dikunjungi pada 3 September 2009.
- Ustadh, Kazhem, Kitab Shenasi Hukumat va welayat-e Faqih, Qom: Perpustakaan Ayatullah Mar'ashi Najafi, 1390 S.
- Velayati, Ali Akbar, Khamenei, Ayatullah Sayid Ali. Dairat al-Ma'arif Buzorge Islami, juz. 21. Teheran: Markaz Dairat al-Ma'arif Buzorge Islami. Cet. Pertama, 1392