Nenda kwa yaliyomo

Kaffaratul-Jam'

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Kafara ya kukusanya)

Kafara ya kukusanya (Kiarabu: كفارة الجمع) ni kafara inayotolewa kwa kumuachilia mtumwa huru, kufunga swaumu siku 60 na kuwalisha mafukara 60 kwa pamoja. Kufanya haya kwa pamoja ndio inajulikana kama kafara ya kukusanya. Kafara ya kukusanya kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu huwa wajibu kwa ambaye amefungua na kubatilisha swaumu kwa jambo la haramu au ameua kwa makusudi. Hata hivyo baadhi ya mafakihi wanasema kuwa, kutekeleza kafara zote hizo katika suala la kufungua swaumu kwa jambo la haramu ni kwa mujibu wa ihtitiyati.

Katika kafara ya kukusanya ni lazima kufunga swaumu siku 31 mfululizo, katika kulisha mafukara kwa uchache kila fukara mmoja apatiwe kibaba kimoja cha chakula (ambacho ni sawa na gramu 750 za ngano, shayiri na mfano wa hivyo). Kwa mujibu wa fat'wa za mafakihi kama mtu hana uwezo wa kutekeleza kafara zote tatu, basi anaweza kutekeleza moja kati ya hizo na kama hana uwezo wa kutekeleza kafara yoyote ile miongoni mwa kafara hizo basi anapaswa kufanya Istighfaru.

Utambuzi

kafara ya kukusanya (كفارة الجمع) ni kutekeleza kafara kadhaa kwa pamoja yaani zote kwa pamoja. Mtu huwajibika kufanya hivyo pale anapofanya baadhi ya mambo ya haramu. Kwa maneno mengine ni kuwa, mhusika anapaswa kutekeleza kwa pamoja kafara tatu za kumuachilia huru mtumwa, kufunga swaumu siku sitini na kuwalisha masikini sitini. [1] Kafara ni faini ya kifedha na kimwili ambayo chimbuko lake ni kufanya baadhi ya madhambi. [2]

Inapowajibika

kafara ya kukusanya (كفارة الجمع) inakuwa wajibu katika mambo kama kufungua na kubatilisha swaumu kwa jambo la haramu na kuua makusudi:

Kubatilisha Swaumu kwa Jambo la Haramu

Kwa mujibu wa fat’wa ya baadhi ya mafakihi kufungua na kubatilisha swaumu kwa jambo la haramu kama vile kula najisi, kuzini na kujichua ni mambo ambayo yanawajibisha kutekeleza kafara ya kukusanya (كفارة الجمع), yaani kutekeleza kafara zote; [3] bila kujali kile ambacho ni haramu katika asili yake au kimekuwa haramu kutokana na sababu kama unyang'anyi, kunajisika au kula chakula chenye madhara. [4] Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali bin Mussa al-Ridha (a.s) ni kuwa, kufungua swaumu kwa jambo la haramu ni kitendo ambacho kinawajibisha kafara ya kukusanya. [5] Baadhi wakitegemea kanuni za kifikihi na baadhi ya hadithi nyingine wametambua jambo moja tu kwamba, ndilo linalowajibisha kafara ya kukusanya nalo ni kufungua swaumu kwa kitu cha haramu [6]. Ayatullah Khamenei [7] na Ayatullah Sistani [8] wanaamini kwamba, kutekeleza kafara ya kukusanya ni Ihtiyati ya mustahabu. Baadhi wametoa hukumu kwamba, ni ihitiyati ya wajibu. [9]

Kwa mujibu wa fat’wa za baadhi ya Marajii Taqlidi, kafara ya kukusanya sio maalumu tu kwa funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, bali inajumuisha pia swaumu nyingine za wajibu. [10] Baadhi ya wengine pia wamejumuisha hukumu hii na kitendo cha kumeza makamasi na makohozi kwa makusudi. [11] Kadhalika kumeza mate yaliyochanganyika na damu kwa mujibu wa fat’wa ya baadhi ya mafuqaha kunawajibisha kafara ya kukusanya [12] au kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu mhusika atekeleze kafara zote tatu. [13]

Kwa mujibu wa fat’wa za baadhi ya Marajii, kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w) katika hali ya swaumu kunapelekea na kuwajibisha kafara ya kukusanya, licha ya kuwa kuna hitilafu na mitazamo tofauti kuhusiana na hili. [14]

Kuua kwa Makusudi

Kumuua muislamu kwa makusudi kunawajibisha Kaffaratul-Jam' (kafara ya kukusanya). [15] Hukumu hii imekuja katika hadithi mbalimbali. [16] Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi ni kwamba, miongoni mwa masharti ya kukubaliwa toba ya muuaji ni kutoa Kaffaratul-Jam' (kafara ya kukusanya). Baadhi ya mafakihi wanaamini kwamba, kafara ya kukusanya inakuwa wajibu kwa ambaye amefanya mauaji yeye mwenyewe [17, lakini ikiwa mauaji hayo yamefanyika kwa kitu na sababu au ameamrisha, basi kwake yeye siyo wajibu kutoa kafara ya kukusanya. [18]

Kafara ya kuua inakuwa wajibu kwa kumuua mwanamke, mtu huru, mwenye akili, mtumwa, kichaa, mtu aliyebaleghe na mtoto Mwislamu. [19] Hukumu hii ni wajibu hata kwa mimba ambayo imepuliziwa roho. [20] Kuna tofauti za kimitazamo kuhusiana na kuwa wajibu kafara ya kukusanya kwa kichaa na mtoto ambaye ameua; baadhi wameandika kwamba, wengi wanaamini kwamba, ni lazima kutolewa katika mali zao gharama za kulisha masikini, kumuachilia huru mtumwa na yeye mwenye aje kufunga swaumu baada ya kupona (kwa kichaa) na baada ya kubaleghe (kwa mtoto huyo). [21]

mafakihi wengi wanaamini kwamba, baada ya kutekelezwa kisasi, gharama za kulisha mafukara na kufunga swaumu zinatolewa katika mali za muuaji; [22] kadhalika kama muuaji atauliwa kabla ya kutoa kafara, gharama za kafara zitatolewa katika mali yake; [23] kama muuaji hatojumuishwa katika hukumu ya kisasi, kama vile baba kumuua mtoto, huwa wajibu kwake Kaffaratul-Jam' (kafara ya kukusanya). [24]

Kama watu kadhaa watamuua mtu mmoja kwa pamoja, kila mmoja wao inamuwajibikia kafara ya kukusanya. [25] Katika baadhi ya hadithi imenukuliwa kwamba, kama mtu atafanya mauaji katika miezi mitukufu (Dhul-Qaadah, Dhul-Hija, Muharram na Rajab) katika kutekeleza kafara anapaswa kufunga swaumu katika miezi hiyo. [26]

Hukumu

Baadhi ya hukumu za kafara ya kukusanya ni:

  • Katika kipengee cha kufunga swaumu miezi miwili mfululizo (siku sitini), kwa akali anapaswa kufunga siku 31 mfululizo (na baada ya hapo anaweza kufunga kwa kutenganisha sio lazima afunge mfululizo. [27]
  • Katika kulisha masikini anapaswa kumpatia kila fukara kwa uchache kibaba kimoja (gramu 750 za ngano, shayiri na mfano wa hivyo). [28] Hata hivyo Allama Majlisi anasema, kuna hitilafu za kimitazamo baina ya Maulamaa baina ya kibaba kimoja au viwili. [29]
  • Kama haiwezekani kutekeleza Kaffaratul-Jam' (kafara ya kukusanya) kwa pamoja, (kutokana na kutokuwa na uwezo)abasi afanye kafara yoyote kati ya hizo na kama hana uwezo wa kutekeleza kafara yoyote ile miongoni mwazo, basi na afanye Istighfaru na kuomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu. [30]

Rejea

Vyanzo

  • Abi, Hasan bin Abi Thalib. Kasyf ar-Rumūz Fī Syarh Mukhtashar an-Nāfi'. Riset: Ali Panah Esytehardi & Hasan Yazdi. Qom: Daftar-e Entesyarat-e Eslami, 1417 H.
  • Allamah Hilli, Hasan bin Yusuf. Irshād al-Adzhān Ilā Ahkām al-Īmān. Qom: Daftar-e Entesyarat-e Eslami, 1410 H.
  • Allamah Hilli, Hassan bin Yusuf. Tahrīr al-Ahkām al-Shar'iyyah 'Alā Madzhab al-Imāmiyyah. Riset: Ibrahim Bahadri. Qom: Muassese-e Emam Shadeq, 1420 H.
  • Allamah Majlisi, Muhammad Baqir. Hudūd Wa Qishāsh Wa Diyāt. Riset: Ali Fadhil. Teheran: Muassese-e Nasyr-e Āsar-e Eslami.
  • Baha'i, Baha'uddin. Jame-e Abbasi Wa Takmil-e Ān Muhassyā. Qom: Datar-e Entesharat-e Eslami, 1429 H.
  • Bahrani, Husain bin Muhammad. 'Uyūn al-Haqā'iq an-Nādzhirah Fī Tatmīm al-Hadā'iq. Qom: Daftar-e Entesyarat-e Eslami, 1410 H.
  • Bahrani, Husain bin Muhammad. Sidād al-'Ibād Wa Rasyād al-'Ibād. Riset: Muhsin Āl Ushfur. Qom: Kitab Furushi-e Mahallati, 1421 H.
  • Fadhil Miqdad, Miqdad bin Abdullah. Kanz al-'Irfān Fī Fiqh al-Qurān. Qom: Entesyarat-e Murtezawi, 1425 H.
  • Fakhrul Muhaqqiqin, Muhammad bin Hasan. Īdhāh al-Fawā'id Fī Syarh Musykilāt al-Qawā'id. Riset: Sayid Husain Musawi Kermani. Qom: Muassese-e Esma'iliyan, 1378 H.
  • Faq'ani, Ali bin Ali. Ad-Durr al-Mandhūdh Fī Ma'rifah Shiyagh an-Niyyāt Wa al-Īqā'āt Wa al-'Uqūd. Riset: Muhammad Barekat. Qom: Maktabah Imam al-'Ashr af al-Ilmiyyah, 1418 H.
  • Faq'ani, Ali bin Ali. Masā'il Ibn Thayy - Al-Masā'il al-Fiqhiyyah. Estensakh Az Selsele-e Yanābī' al-Mawaddah.
  • Ha'iri, Sayyid Ali. Al-Sharh Fī Mukhtashar al-Nāfi' - Hadīqah al-Mu'minīn. Riset: Sayyied Mahdi Raja'i. Qom: Entesyarat-e Ketabkhane-e Ayatullah Mar'asyi Najafi, 1409 H.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hasan. Hidāyah al-Ummah Ilā Ahkām al-A'immah - Muntakhab al-Masā'il. Mashhad: Majma' al-Buhuts al-Islamiyyah, 1412 H.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hasan. Wasā'il Shī'ah. Qom: Muassese-e Āl al-Bait (as), 1409 H.
  • Ibn Idris Hilli, Muhammad bin Manshur. Al-Sarā'ir al-Hāwī Li Tahrīr al-Fatāwā. Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami, 1410 H.
  • Kermansyahi, Muhammad Ali. Maqāmi' al-Fadhl. Qom: Muassese-e Allame-e Mujadded Wahid Bahbahani, 1421 H.
  • Khamene'i, Sayyied Ali. Ajwibah al-Istiftā'āt. Beirut: Dar al-Islamiyyah. Cet. 3, 1420 H.
  • Khomeini, Sayyied Ruhullah. Tahrīr al-Wasīlah. Qom: Muassese-e Mathbu'at-e Dar al-'Ilm, 1409 H.
  • Khomeini, Sayyied Ruhullah. Taudhīh al-Masā'il (Muhassyā). Riset Sayyid Muhammad Husein Bani Hashimi. Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami, 1424 H.
  • Khomeini, Sayyied Ruhullah. Taudhīh al-Masā'il. Riset Muslim Qali Pur Gilani. 1426 H.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. Al-Kāfī. Riset Ali Akbar Ghaffar. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah. Cet. 4, 1407 H.
  • Majlisi, Muhammad Taqi. Lawāmi' Shāhidqarānī. Qom: Muassese-e Esma'iliyan, 1414 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Taudhīh al-Masā'il. Qom: Entesharat-e Madrese-e Emam Ali bin Abi Talib (a.s). Cet. 52, 1429 H.
  • Shaduq, Muhammad bin Ali. Man Lā Yahdhuruh al-Faqīh. Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami, 1413 H.
  • Sistani, Sayyied Ali. Taudhīh al-Masā'il. Mashhad: Daftar-e Hazrat-e Ayatullah al-'Udzhma Sistani, 1393 H.
  • Shahid Awal, Muhammad bin Makki. Al-Lum'ah al-Damishqiyyah Fī Fiqh al-Imāmiyyah. Riset: Muhammad Taqi Murwarid & Ali Asghar Murwarid. Beirut: Dar at-Turats, 1410 H.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Hāshiyah al-Irshād. Riset Ridha Mukhtari. Qom: Daftar-e Tablighat-e Eslami, 1414 H.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali. Hāshiyah al-Mukhtashar an-Nāfi'. Qom: Daftar-e Tablighat-e Eslami, 1422 H.