Nenda kwa yaliyomo

Imamu Hadi (a.s)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Abu Hassan Thalith)
Imamu Hadi (a.s)
Imamu wa Kumi wa Mashia
Haram ya Askariyein
JinaAli bin Muhammad (a.s)
KuniaAbu Hassan Thalith
Siku ya Kuzaliwa15 Dhul-hijjah, Mwaka 212 H
Mahali AlipozaliwaSarya - Madina
Kipindi cha UimamuMiaka 34 (220 - 254)
Kifo3 Rajab 254 Hijria
AlipozikwaSamarrah - Iraq
AlipoishiMadina - Samarrah
LakabuHadi - Naqii
BabaImamu Jawad (a.s)
MamaSamunah Magharibiyah
WakeHudith
WatotoHassan, Muhammad, Hassan, Ja'afar
UmriMiaka 42
Maimamu wa Kishia
Imamu Ali • Imamu Hassan MujtabaImamu Hussein • Imamu Sajjad • Imamu Baqir • Imamu SwadiqImamu Kadhim • Imamu Ridha • Imamu JawadImamu Hadi • Imamu Mahdi


Ali bin Muhammad (Kiarabu: الإمام علي الهادي عليه السلام), anaye tambulikana kama Imamu Hadi au Imamu Ali al-Naqi (a.s) (aliyezaliwa mwaka 212 na kufariki 254 Hijiria), ni Imamu wa kumi wa Mashia na ni mwana wa Imamu Jawad (a.s). Yeye alishika nafasi ya Imamu kwa muda wa miaka 34, kuanzia mwaka 220 hadi 254. Kipindi cha Uiamu wa uimamu wa Imamu Hadi, kiliwafikiana na utawala wa Makhalifa kadhaa wa Banu Abbasi waliokuwa wakiongoza wakati huo, ikiwa ni pamoja na Mutawakkil. Kipindi chake kikubwa cha Uimamu wake kilikuwa chini ya udhibiti wa utawala wa Babu Abbasi akiwa huko mjini Samarra.

Imam Hadi (a.s) ameandika Hadithi nyingi juu ya masuala ya imani na akida, tafsiri ya Qur'ani, fiqhi, pamoja na maadili. Pia kuna mada muhimu za kielemu zilizojadiliwa katika sehemu ya Hadithi hizo, ikiwa ni pamoja na; tashbihu (kumfananisha Mungu na vitu vyengine), tanzih (utakaso wa Mungu), jabru (shinikizo la Mungu katika matendo ya binadamu) pamoja na ikhtiyar (hiyari na uhuru wa mwanadamu). Pia miongoni ya mambo yalionukuliwa kutoa kwake ni Ziyara Jami'a Kubra na Ziyara Ghadiriyyah.

Makhalifa wa Banu Abbasi waliweka vizuizi vizito dhidi ya Imamu Hadi (a.s) na kuzuia mawasiliano yake na Waislamu wa madhehebu ya Shia. Hilo lilipelekea yeye alikuwa na mawasiliano zaidi na Waislamu wa Shia kupitia mtandao maalumu ambao ulikuwa umetengenezwa na kikundi cha mawakili wa Imamu. Abd al-Adhim Hassani, Othman bin Said, Ayub bin Nuh, na Hassan bin Rashid walikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Imamu Hadi (a.s).

Kaburi la Imamu Hadi huko Samarra ni mahali pa ibada kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Umaarufu wa mahali hapo ni Haramu Askariyyaini. Eneo hilo limepewa jina hilo kwa sababu ya kule eneo hilo kuwa ndilo sehemu la kaburi lake yeye pamoja na mwanawe, Imamu Hasan al-Askari (a.s). Haram ya Askariain iliharibiwa wakati wa mashambulizi ya kigaidi mnamo mwaka 1384 na 1386 Shamsia. Wizara ya Mambo ya Kidini ya Iran ilijenga upya eneo hilo kati ya miaka 1389 na 1394 Shamsia.

Jina Nasaba na Lakabu

Makala Asili: Orodha ya Kuniya na Lakabu za Imamu Hadi (a.s)

Ali bin Muhammad, maarufu kama Imam Hadi na Ali al-Naqi, ni Imamu wa kumi wa Shia. Baba yake ni Imamu Jawadi (a.s), Imamu wa tisa wa Shia, na mama yake alikuwa ni mjakazi (1) aliyeitwa Samanah al-Maghribiyyah [2] au Sawsan. [3]

Miongoni mwa majina maarufu ya Imamu wa kumi wa Shia ni Hadi na Naqi. [4] Inasemekana sababu ya yeye kupewa jina la Hadi ni kwamba wakati wake, alikuwa ni mwongozo bora kwa watu kuelekea kheri. [5] Majina mengine yanayotajwa kwa ajili yake ni Murtadha, Aalim, Faqihi, Aminu, Naasih, Khalis, na Tayyib. [6]

Sheikh Saduqu (aliyefariki mwaka 381 Hijiria) amenukuu kutoka kwa waalimu wake ya kwamba; Imamu Hadi na mwanawe (Imamu Hassan Askari) (a.s) walipewa jina la Askari kwa sababu ya kule wao kuishi katika eneo lililoitwa Askar huko Samarra. [7] Ibn Jawzi (aliyefariki mwaka 654 Hijiria) pia anaelezea katika kitabu chake Tadhkiratu al-Khawas kwamba; sababu ya Imam Hadi kuwaita jina la Askari, ni hiyo hiyo iliyo tajwa na Sheikh Saduqu. [8]

Kuniya yake ni Abu al-Hassan, [9] na katika vyanzo vya Hadithi, anaitwa Abu al-Hassan wa Tatu, [10] ili kuepuka kuchanganywa na Abu al-Hassan wa Kwanza, yaani Imamu Kadhim, na Abu al-Hasan wa Pili, yaani Imamu Ridha. [11]

Wasifu wa Maisha Yake

Kulingana na maoni ya Kulayni,[12] Sheikh Tusi, [13] Sheikh Mufid, [14] na Ibnu Shahriashub [15] ni kwamba; Imamu Hadi alizaliwa tarehe 15 Dhul-Hijjah mwaka 212 Hijria katika eneo la Sariya (karibu na Madina). Hata hivyo, pia miongoni mwa rikodi kuhusiana na tarehe ya kuzaliwa kwake ni tarehe 2 au 5 Rajabu ya mwaka huo huo wa 214 Hijiria, na pia wenge wamesema kuwa ni Jumada al-Thani mwaka 215 Hijria. Kwa mujibu wa maelezo ya Mas'udi, mwanahistoria wa karne ya nne, ni kwamba; katika mwaka ambao Imamu Jawad pamoja na mkewe (Ummul-Fadhli) walikwenda kufanya ibada ya Hija, Imamu Hadi akiwa bado mdogo pale walipokuja naye mjini Madina. [18] Naye akaishi katika mji huo wa Madina hadi mwaka 233 Hijiria. Ya'qubi, mwanahistoria wa karne ya tatu ya Kiislamu, aliandika kuwa katika mwaka huo, Mutawakkil Abbasi alimpa wito Imamu Hadi na kumtaka kwenda Samarra. [19] Alipofika Samarra alimpa makazi katika eneo lililoitwa Askar na nayeb alikaa huko hadi mwisho wa maisha yake. [20]

Hakuna habari nyingi zinazopatikana kuhusu maisha ya Imamu Hadi, Imamu Jawad, na Imamu Askari, ikilinganishwa na Maimamu wengine wa Shia. Muhammad Hussein Rajabi Duwani, mwanahistoria (aliyezaliwa 1339 Hijiria), ameelezea sababu ya suala hili kuwa ni umri mfupi wa Maimamu hao, kuweko kwao kifungoni na kuto kuwepo kwa waandishi wa historia wa Kishia katika wakati huo. [21]

Kisa cha Junaidiy Kuingia Katika Ushia

Kulingana na ripoti iliyosimuliwa katika kitabu cha Ithbatu al-Wasiyyah, baada ya kifo cha kishujaa cha Imamu Jawad, serikali ya Banu Abbasi ilituma mtu mmoja anayeitwa Abu Abdullah Junaidiy, ambaye alikuwa mwenye chuki kubwa na familia ya bwana Mtume (s.a.w.w) ambaye alikuwa adui yao mkubwa, serikali hiyo ilimpa yeye la kumfundisha Imamu Hadi na kumchunguza nyenendo zake, na kuzuia wafuasi wa Shia kuwasiliana naye. Hata hivyo, baada ya muda fulani, mtu huyu alikuja kupozwa na kutahayari chini ya elimu pamoja na utu wa Imamu, na hatomae akageuka na akawa ni miongoni mwa Mwislamu wa madhehebu ya Shia. [22]

Watoto Wake

Katika vyanzo vya Shia, inasemekana kwamba Imamu Hadi alikuwa na watoto wanne wa kiume wanaoitwa Hassan, Muhammad, Hussein, na Ja'afar. [23] Pia imeelezwa ya kuwa pia yeye alikuwa na binti ambaye Sheikh Mufid alimtaja kwa jina la Aisha [24] na Ibn Shahrashub amemtambua kwa jina la ‘Illiyyah (Au Aliyyah). Katika kitabu cha Dalail al-Imamah, inatajwa kuwa yeye alikuwa na mabinti wawili wanaoitwa Aisha na Dalalah. [26] Ibn Hajar al-Haythami, mmoja wa wanazuoni wa Sunni, pia katika kitabu chake Al-Sawa'iqu al-Muhriqah ameeleza kuwa Imamu wa Kumi wa Shia alikuwa na watoto wanne wa kiume na binti mmoja. [27]

Kifo Chake cha Kishujaa na Kaburi Lake

Kulingana na ripoti ya Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 Hijria) ni kwamba; Imamu Hadi alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 41 katika mwezi wa Rajabu mwaka wa 254 Hijiria baada ya kuishi Samarra kwa miaka 20 na miezi 9. [28] Pia, katika kitabu cha Dalailu al-Imamah na Kashfu al-Ghummah, imetajwa kuwa Imamu wa Kumi aliuawa kwa sumu wakati wa utawala wa al-Mu'tazzu Abbasi (aliye tawala kuanzia mwaka 252 hadi 255 Hijiria), na hiyo ikawa ndio sababu ya kifo chake cha kishujaa (kishahidi). [29] Ibnu Shahrashub (aliye fariki mwaka 588 Hijria) anaamini kuwa Imamu Hadi aliuawa shahidi mnamo mwisho wa utawala wa al-Mu'tamid (aliye tawala mwaka 256 hadi 278 Hijiria), naye akinukuu kutoka kwa Ibn Babawayh amesema kwamba; Mu'tamid alimuuwa Imamu Hadi kupitia sumu. [30]

Baadhi ya vyanzo vimeelezea siku ya kifo chake cha kishujaa, kuwa ni tarehe 3 Rajabu, [31] na wengine wameitaja kuwa tarehe 25 au 26 Jumada al-Thani. [32] Katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tarehe 3 Rajabu imesajiliwa kama ndio siku ya shahada ya Imamu Hadi (a.s).

Kulingana na ripoti ya al-Mas'udi, mwanahistoria wa karne ya nne Hijiria, ni kwamba; Imam Hassan Askari alishiriki katika mazishi ya kumzika baba yake. Maiti ilihamishwa kupitia karibu na nyumba ya Mussa ibn Bugha, na haraka kabisa kabla ya Khalifa wa Banu Abbasi kushiriki katika mazishi hayo, Imam Askari alimsalia baba yake sala ya maiti. Al-Mas'udi ameiripoti msongamano mkubwa wa watu kwenye mazishi ya Imam Hadi (a.s). [33]

Haramu ya Askariyyaini

Makala Asili: Haram ya Askariyyein

Imamu Hadi (a.s) alizikwa nyumbani kwake huko Samarra. [34] Mahali alipozikwa Imamu Hadi (a.s) na mwanawe, (Imamu Hassan Askari (a.s)), hujulikana kama Haram ya Askariaini huko Samarra. Baada ya maziko ya Imamu Hadi (a.s) yaliofanyika nyumbani kwake, Imamu Askari (a.s) alimteua mtumishi maalumu wa kuhudumia kaburi lake. Katika mwaka wa 328 Hijiria, kuba la kwanza lilijengwa juu ya makaburi yao. [35] Haram ya Askariain imekarabatiwa, kukamilishwa, na kufanyiwa marekebisho katika nyakati tofauti. [36] Kila mwaka, Waislamu wa Kishia kutoka maeneo mbalimbali hufanya ziara ya kwenda kutembelea makaburi ya Imamu Hadi na Imamu Hassan Askari (a.s) huko Samarra.

Makala Asili: Kubomolewa Haram ya Askariyein

Katika miaka ya 1384 na 1386 Shamsia, baadhi ya sehemu za Haram ya Askariyyaini ziliharibiwa katika milipuko ya kigaidi. [37] Kitengo maalumu kinachoshughulikia ukarabati na ujenzi wa taasisi tukufu kilikamilisha ujenzi wa jingo hilo katika mwaka wa 1394. [38] Jengo lililozunguka makaburi yaliomo ndani ya Haram hiyo, limejengwa kupitia msaada wa Ayatullahi Sistani. [39]

Kipindi cha Uimamu

Ali bin Muhammad, alipata uimamu akiwa na umri wa miaka nane mnamo mwaka 220 Hijiria. [40] Kulingana na vyanzo mbali mbali, umri mdogo aliokuwa nao Imam Hadi (a.s) pale aliposhika nafasi ya Uimamu haukupelekea wafuasi wa madhehebu ya Shia kuwa na shaka juu ya Uimamu wake. Kwani hata baba yake (Imamu Jawad) (a.s) naye pia alishika nafasi ya Uimamu akiwa bado na umri mdogo. [41] Kulingana na maandishi ya Sheikh Mufid ni kwamba; Mashia wengi walikubaliana na Uimamu wa Imamu Hadi (a.s) baada ya kuondoka Imamu wa tisa wa Mashia, na ni wachache tu miongoni mwao walio onekana kupingana na Uimamu wake. [42]

Kauli Moja ya Wafuasi wa Shia kuhusu kuwafikiana na Uimamu wa Imam Hadi (a.s) na Kutokudai Uimamu na Mtu Mwingine isipokuwa yeye tu, imechukuliwa kama ni hoja imara ya kuthibitisha Uimamu wake. [47] Muhammad bin Ya'aqub al-Kulaini na Sheikh Mufidu wameorodhesha maandiko kadhaa katika kazi zao yanayohusiana na uthibitisho wa Uimamu wake (a.s). [48] Kulingana na maelezo ya Ibnu Shahriashub ni kwamba; Wafuasi wa Shia walifahamu kuhusiana na Uimamu wa Ali bin Muhammad kupitia maandiko yanayohusiana na Imamu wake kutoka kwa Imamu wa awali, ambayo yamenukuliwa na waandishi wa Hadithi kama vile; Ismail bin Mihran na Abu Ja'far al-Ash'ari. [49]

Makhalifa wa Zama Hizo

Imamu Hadi (a.s) alishika nafasi ya Uimamu kwa muda wa miaka 33 (kuanzia mwaka 220 hadi 254 Hijiria) [50]. Katika kipindi hichi, watawala kadhaa wa Banu Abbasi waliingia madarakani. Wakati wa mwanzo mwa Uimamu wake ulisadifiana na wakati wa utawala wa al-Mu'tasim, na ukamalizika wakati wa utawala wa al-Mu'utasim. [51] Hata hivyo, Ibn Shahriashub amesema kuwa; mwisho wa maisha ya Imamu Hadi (a.s) ilikuwa ni katika kipindi cha utawala wa al-Mu'tamidu Abbasi. [52]

Imamu wa Kumi wa Shia alitumikia miaka saba ya Uimamu wake wakati wa utawala wa al-Mu'utasim Abbasi. [53] Kulingana na Jassim Hussein, mwandishi wa kitabu Tarikhe Siyasi Ghaybate Imame Dawazdahom (Historia ya Kisiasa ya Kughibu kwa Imamu wa Kumi na Mbili), ni kwamba; al-Mu'utasim alikuwa na msimamo laini zaidi kwa Wafuasi wa mahdehebu ya Shia wakati wa Imamu Hadi (a.s), ikilinganishwa na kipindi cha Imamu Jawad (a.s), na alikuwa na imani nao zaidi kuliko viongozi waliopita kabla yake. Mabadiliko haya ya mtazamo wake yalitokana na kuboreshwa kwa hali ya kiuchumi na kupungua kwa uasi wa Alawiyyina (watu wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w)). [54] Pia, karibu miaka mitano ya kipindi cha Uimamu wa Imamu wa Kumi, ilikuwa ni wakati wa utawala wa al-Wathiqu, miaka kumi na nne na nusu Uimamu wake ulisadifiana na wakati wa utawala wa al-Mutawakkil, miezi sita ikasadifiana na wakati wa utawala wa al-Muntasir, miaka miwili na miezi tisa ilisadifiana na wakati wa utawala wa al-Mustain, na zaidi ya miaka nane ya Uimamu wake ikawa ndani ya wakati wa utawala wa al-Mu'atazz. [55]

Kuhamishwa Kwake Kutoka Madina Kwenda Samarra

Mnamo mwaka 233 Hijiria, al-Mu'tawakilu al-Abbasi alimwamuru Imamu Hadi (a.s) kuhama kutoka Madina kwenda Samarra. [56] Sheikh Mufidu ameandika akisema ya kwamba; hatua hii ilifanyika mwaka 243 Hijri [57], lakini kulingana na utafiti wa Ja'farian, mtafiti wa historia ya Kiislamu, tarehe hii si sahihi. [58] Inasemekana kwamba sababu ya hatua hii ya al-Mu'tawakil ilikuwa ni kutokana na ushawishi na tuhuma dhidi ya Imamu iliyotolewa na Abdullah bin Muhammad, afisa wa utawala wa Abbasid huko Madina [59], yakifuatana na uchochezi dhidi ya Imamu Hadi (a.s) uliofanya na Buraiha Abbasi Imamu wa sala za jamaa aliyeitwa na khalifa huko Makkah na Madina [60], pamoja na ripoti za watu kumuunga mkono Imamu wa Kumi wa Shia. [61]

Kulingana na maeelezo ya Mas'udi, ni kwamba; Buraiha aliandika barua kwa al-Mu'tawakkil akimwambia ya kwamba: "Ikiwa unaitaka Makkah na Madina, basi mtoa nje ya miji hiyo Ali bin Muhammad; kwani nafanya kazi ya kuwalingania watu, na tayari jopo kubwa la limeshaungana naye." [62] Kwa msingi huu, Yahya bin Harthama akaamriwa na al-Mu'tawakil kuhamisha Imamu Hadi (a.s) kwenda Samarra. [63] Imamu Hadi (a.s) alijibu katika barua yake kwa al-Mu'tawakil akikataa madai mabaya yalio elekezwa dhidi yake [64], lakini al-Mu'tawakil alimjibu kwa heshima akimwomba ahamie Samarra. [65] Nakala ya barua ya al-Mu'tawakil imenukuliwa katika kazi za Sheikh Mufid na Kulayni. [66]

Kulingana na maoni ya Ja'fariyyan; al-Mu'tawakil alipanga mpango wa kuhamisha Imamu Hadi (a.s) kwenda Samarra kwa njia ambayo asiweze kutonesha sana hisia za watu ili safari hiyo ya lazima ya Imamu isilete athari mbaya katika jamii. [67] Walakini, Subait bin Juzi, mmoja wa wanazuoni wa Sunni, alinukuu ripoti kutoka kwa Yahya bin Harthama ambayo kwa mujibu wake; watu wa Madina walikuwa wamekasirika na kuchafuka sana, na huzuni yao ilifikia kiwango cha kilio na ghasia, ambapo katu Madina haikuwahi kuona hali kama hiyo hapo awali. [68] Baada ya Imamu Hadi (a.s) kuondoka Madina, aliwasili Kadhimaini na kukaribishwa vizuri na watu wa mji huo. [69] Alipofika mji wa Kadhimaini, alienda nyumbani kwa Khazimah bin Hazam na baada ya hapo aliondoka na kuelekea Samarra. [70]

Kwa mujibu wa maoni ya Sheikh Mufid, Imamu Hadi (a.s) alionekana kuwa na heshima kwa al-Mu'tawakil, hata hivyo al-Mu'tawakil alikuwa akifanya njama dhidi yake. [71] Kulingana na maandishi ya Tabarsi, lengo la al-Mu'tawakil katika hatua hii lilikuwa ni kumnyima hadhi na heshima Imamu huyo machoni mwa watu. [72] Kulingana na maelezo ya Sheikh Mufid; siku ya kwanza Imamu alipowasili Samarra, kwa amri ya al-Mu'tawakil, kwa muda wa siku nzima alishikiliwa katika Nyumba ya Sa'aliq (mahali pa makazi na watu omba omba) na siku ya pili akapelekwa nyumbani ambapo alipangiwa kuishi ndani yake. [73] Kwa mujibu wa maoni ya Saleh bin Said, hatua hii ilifanywa kwa lengo la kumdharau Imamu Hadi (a.s). [74]

Watawala wa Banu Abbasi walimdhibiti na kumtesa sana Imamu Hadi (a.s) wakati wa kukaa kwake mjini humo. Kwa mfano, walichimba kaburi ndani ya chumba chake cha kuishi. Pia, bila ya kumpa habari ghafla usiku walimtaka kuhudhuria kwenye kasri la Khalifa, pia walizuia uhusiano baina yake na Shia wake. [75] Baadhi ya waandishi wametja sababu za uadui wa al-Mu'tawakil dhidi ya Imam Hadi kama ifuatavyo:

  1. Al-Mu'tawakil alikuwa na mwelekeo wa kijamaa kwa Ahlul-Hadith, ambao walikuwa wakipingana na Mu'tazilah na Shia, na Ahl al-Hadith walimchochea al-Mu'tawakil dhidi ya Shia.
  2. Al-Mu'tawakil alikuwa na wasiwasi juu ya hadhi yake kijamii na alikuwa na hofu juu ya kupatikana kwa uhusiano baina ya watu na Maimamu wa Shia. Kwa hiyo, alijaribu kuvunja uhusiano huo kadri iwezekanavyo. [76] Kwa nia hiyo hiyo Al-Mu'tawakil alichukua hatua ya kuharibu la kaburi ya Imamu Hussein (a.s) na akawa mkali dhidi wale waendao kuzuru kaburi la Imam Hussein (a.s). [77]

Baada ya kufariki kwa al-Mu'tawakil, mtoto wake (al-Muntasiru) alikaa madarakani. Katika kipindi hichi, shinikizo la serikali dhidi ya familia ya Alawi (Ahlul-Baiti) (a.s) lilipungua, na Mashia kwa ujumla ikiwa ni pamoja na Imam Hadi (a.s), wakapata nafasi ya kuvuta pumzi. [78]

Makabiliano Dhidi ya Maghulat

Ghulat walikuwa na harakati kadhaa katika zama za Uimamu wa Imamu Hadi (a.s). Wao walijitambulisha kama ni wafuasi na Masahaba wa karibu wa Hadi (a.s), na walianasibisha maneno na mafunzo yao kwa Maimamu wa Kishia, ikiwa ni pamoja na Imamu Hadi (a.s), habari ambazo kiuhalisia zilikuwa zilichafua kila nyoyo za wale waliofikiwa na habari hizo, kama ilivyoelezwa katika barua ya Ahmad bin Muhammad bin Isa Ash'ari alioituma kwa Imam Hadi (a.s). Kwa kuwa habari hizo zilikuwa wanazihusisha na Maimamu, hivyo hapakuwa na mtu aliyetokea kuwa na ujasiri wa kukataa au kupinga habari hizo. Walifasiri Wajibat na Muharamat kwa njia yao wenyewe. Kwa mfano, wao katika kuifasiri sala na zaka iliokuja katika Aya isemayo: (وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ ; Na simamisheni sala na toeni zakat) [79], walisema kuwa; Aya hii haikuwa na maana ya sala na zaka, bali inaashiria watu maalumu kupitia lugha hiyo ya sala na zaka. Imam Hadi (a.s), alijibu kwa kuandika barua kwa Ahmad bin Muhammad kwamba; tafsiri kama hizo sio sehemu ya dini yetu. Jiepusheni na watu kama hao. [80] Fathu bin Yazid Jorjani aliamini kuwa kula na kunywa hailingani na hadhi ya Uimamu, na Maimamu hawana haja ya kula wala kunywa. Katika jibu lake, Imamu Hadi (a.s) alinukuu na kurejelea Aya za Qur’ani zinazo husiana na kula na kunywa kwa Mitume na kutembea kwao katika masoko na akisema: Kila mwili unahitajia kula na kunywa, isipokuwa Mungu tu ambaye ndiye aliye umba kiwiliwili. [81]

Imamu wa kumi wa Shia, katika jibu barua ya Sahlu bin Ziyad, iliyo kuja kumpa khabari za Ughulat wa Ali bin Hasakau, Imamu (a.s) akakanusha uhusiano wa mtu huyo na Ahlul-Bayt (a.s), na kuyatangaza maneno yake kuwa ni maneneo batili, kisha akawataka Mashia wajiepushe naye, na hata akatoa hukumu ya kifo juu yake. Kulingana na barua hiyo, Ali bin Huska aliamini kuwa Imamu Hadi ni Mungu na kwamba yeye ndiye mjumbe (Mtume) na msiri wa Imam Hadi (a.s). [82] Imam Hadi aliwalaani Maghulat kadha akiwemo Muhammad bin Nusayr, anayejulikana kama ndiye mwanzilishi wa madhehebu ya Nusaariyya, [83] Hassan bin Muhammad maarufu kama Ibnu Baba, na Faaris bin Hatam Qazwini. [84]

Ghulat mwingine aliye jitambulisha kama ni mfuasi wa Imamu Hadi (a.s), alikuwa ni Ahmad bin Muhammad Sayyari, ambaye wengi miongoni wa wataalamu wa nasaba za wapokezi wa Hadithi waliomchukulia kuwa ni miongoni mwa Maghulat, na mwenye madhehebu mabovu. [86] Kitabu chake kiitwacho Al-Qiraa-aatu ndio chanzo chake muhimu cha Hadithi, ambacho wengine wamekitumia kama kama ndio msingi wa ithibati na kielelezo cha kuthibitishia upotoshwaji wa Qur'an. [87] Imam Hadi (a.s), katika barua iliyo nukuliwa na Ibn Shu'bah Harani, alisisitiza ndani yake umuhimu wa ukweli wa Qur'an na kuitambulisha kuwa ndio kigezo cha kuchunguza Hadithi na kutambua yalio sahihi na yasiyo sahihi. [88] Kando na hayo, Imam Hadi (a.s) aliwatetea Mashia ambao kimakosa, walikuwa wakilaumiwa kuwa ni miongoni mwa Maghulati. Kwa mfano, pale wakaazi wa Qom walipo mfukuza Muhammad bin Urmah kwa madai ya Ughulati, Yeye (a.s) aliandika barua kwa watu wa Qom na kumtakasa kutokana na tuhuma hizo za Ughulati. [89]

Mawasiliano na Mashia

Ingawa wakati wa Imamu Hadi (a.s) kulikuwa na ukandamizaji mkali kutoka upande wa Makhalifah wa Banu Abbasi waliokuwa wakitawala katika zama hizo, ila kulikuwa na uhusiano mzuri kati ya Imamu Hadi (a.s) na Mashia nchini Iraq, Yemen, Misri, na maeneo mengine. [90] Yeye aliwasiliana na Mashia kupitia mtandao wake wa mawakala na kwa njia ya uandishi wa barua. Kulingana na Riwaya ya Ja'farian, ni kwamba; katika zama za Imamu Hadi (a.s), Qom ilikuwa ni kitovu kikuu cha kukusanyika Mashia wa Iran, na kulikuwa na uhusiano imara kati ya Mashia wa mji huu na Maimamu (a.s). [91] Muhammad bin Daudi Qommi na Muhammad Talhi kutoka Qom walifanya kazi ya kukusanya khumsi, zawadi pamoja na maswali ya watu wa kutoka miji ya jirani na kumfikishia Imam Hadi (a.s). [92] Kulingana na maelezo ya Ja'farian, mawakili, mbali na kukusanya mali za khumsi na kuwasilisha kwa Imamu (a.s), pia walikuwa na jukumu la kutatua masuala ya kiitikadi na kifiqhi, pamoja na jukumu la kusimamisha na kudhatiti dhana ya Uimamu wa Imamu wa baadaye katika eneo lao. [93] Muhammad Rida Jabbaari, mwandishi wa kitabu Saazimane Wikaalat Mtandao wa Mawakala, amemtaja Ali bin Ja'afar Hamani, Abu Ali bin Rashid, na Hassan bin Abdul Rabbi kama ni mawakala wa Imamu Hadi (a.s). [94]

Mjadala juu ya Uumbwaji wa Qur'an

Imamu Hadi (a.s) katika barua yake kwa mmoja wa Mashia zake, alimwomba katu asitoa maoni juu ya suala la uumbwaji wa Qur'an na asijisimame na upande wowote wa nadharia; si upande wa nadharia ya utangu na umilele kwa Qur'an, wala si upande wa nadharia kuumbwa kwa Qur’ani. Katika barua hiyo, Imamu (a.s), alitaja suala la uumbwaji wa Qur'an kuwa ni mzozo, na aliona kuingia katika mjadala kama huo ni kuhiliki. Pia alisisitiza kuwa Qur'an ni maneno ya Mweny Ezi Mungu na mazungumzo juu ya hilo ni bid'ah (uzushi) ambapo wanaouliza maswali na wanaojibu wote wanashiriki katika dhambi ya uzushi huo. [95] Wakati huo, mjadala juu ya uumbwaji na utangu wa milele wa Qur'an, ulisababisha kuzuka kwa madhehebu na makundi mbali mbali kati ya Waislamu wa Kisunni. Ma'muni na Mu'tasimu walisimama upande wa nadharia ya uumbwaji wa Qur'an na waliwafinya na kuwakandamiza wapinzani wa nadharia hiyo, hivyo kipindi hicho kinasemekana kuwa kilikuwa ni kipindi cha mateso. Walakini, al-Mutawakkil alisaidia hoja ya kuwa Qur'an ni kitabu kilichokuwepo tangu na tangu, na akawasifu wapinzani wa nadharia hiyo, wakiwemo Mashia, kuwa ni waanzishaji wa bid'ah. [96]

Hadithi

Kuna Hadithi kadhaa katika vyanzo vya Kishia, zilizonukuliwa kutoa kwa Imamu Hadi (a.s). Hadithi hizo zinapatikana katika vyanzo mbali mbali maarufu vya Kishia, kama vile Kutubu al-Arba'ah, Tuhafu al-'Uqul, Misbahu al-Mutahajjid, al-Ihtijaaju na Tafsiri 'Ayyashi. Ni idadi chache ya Hadithi zilizonakuluwa kutoka kwa Imamu Hadi (a.s) ikilinganishwa na Maimamu wengine waliotangulia kabla yake. Ataaridi anachukulia sababu ya suala hili kuwa linatokana na kukaa kwake huko Samarra kwa kulazimishwa akiwa chini ya utawala wa Banu Abbasi, ambao haukumpa yeye fursa ya kusambaza elimu na maarifa yake. [97] Imamu Hadi (a.s) alitajwa na kutambuliwa kwa majina mbali mbali, katika riwaya zilizonakiliwa kutoka kwake (a.s). Miongoni mwa majina hayo ni; Abu al-Hassan al-Hadi, Abu al-Hassan al-Thaalith, Abu al-Hassan al-Akhiir, Abu al-Hassan al-Askari, al-Faqih al-Askari, al-Rajul, al-Tayyib, al-Akhir, al-Sadiq bin al-Sadiq, na al-Faqih. Imesemekana kuwa matumizi ya majina hayo mbalimbali ilikuwa ni mbinu ya taqiyyah (kuficha siri). [98]

Riwaya zilizonakuluwa kutoka kwa Imamu Hadi (a.s) zinahusiana na masuala ya Tawhidi (upwekeshaji wa Mungu), Imamah (uongozi wa kiimamu), ziara (sala na salamu takatifu), tafsiri ya Qur'an, na masuala mbalimbali ya fiqhi kamakama vile; tohara (usafi), sala, saumu, khumsi (seheme maalumu ya kipato), zakaat (zaka), ndoa, na maadili. Zaidi ya riwaya 21 kutoka kwa Imamu Hadi (a.s) zimenukuliwa kuhusiana na Tawhid na kujiepusha na shirki (ushirikina). [99]

Kuna barua iliyoka kwa Imamu Hadi (a.s) kuhusu suala la jabru (shinikizo la mungu katika matendo ya wanadamu) na ikhtiyaru (uhuru). Katika barua hiyo, ile Hadithi maarufu isemayo: Hakuna shinikizo la lazima wala ihtiyari huria, bali ni kati ya mambo mawili hayo (لا جبر و لا تفویض بل امر بین الاَمرین), imefafanuliwa kulingana na Qur'an, na misingi ya elimu ya tawhidi ya Kishia, katika ufafanuzi huo wa masuala ya jabr na ikhtiyaru.[100] Miongoni mwa Hadithi zilizonukuliwa kuhusiana na mijadala mbali mbali ya Imamu Hadi (a.s), ni Hadithi zinazo husiana na ithibati juu ya masuala ya jabru na ikhtiyaru. [101]

Ziara (Sala na Salamu)

Makala Asili: Ziara ya Jamia Kubra

Kuna Ziara mbili zilizonukuliwa kutoka kwa Imam Hadi, nazo ni; Ziaratu Jami’a al-Kabira [102] na Ziaratu al-Ghadiriyyah. [103] Ziaratu Jami’a al-Kabira, inatambulika kama ni moja wapo ya maandiko yanayotoa elimu juu ya dhana ya Uimamu. [104] Dhana kuu ya Ziaratu al-Ghadiriyyah ni juu ya suala na kufungamana na Maimamu na Kutengana na maadui zao, na maudhui yake ni kuelezea wasifu wa Imam Ali (a.s). [105]

Mashairi ya Imamu Hadi (a.s) Mbele ya Mutawakkil

Katika ripoti ya Masudi, mwanahistoria wa karne ya nne Hijiria, emeelezwa ya kwamba; kuna watu waliomwambia Mutawakkil kwamba nyumbani kwa Imamu Hadi (a.s) kulikuwa na silaha za kivita pamoja na barua kutoka kwa wafuasi wa madhehebu ya Shia. Hilo lilipelekea Mutawakkil kutuma maafisa wake kadhaa kuivamia nyumba ya Imam Hadi (a.s) bila ya taarifa za awali. [106] Pale walipompeleka Imamu kwenye kikao cha Mutawakkil, Khalifa alikuwa na kikombe cha divai (pombe) mkononi mwake na akamkaribisha Imamu kinywaji hicho. [107] Imam alikataa ombi la Mutawakkil akisema kuwa katu mwili na damu yake haijawahi kuchafuliwa na divai. [108] Kisha Mutawakkil akamwomba Imam amsomee shairi ambalo lingemfurahisha. [109] Mwanzo Imamu alikataa ombi lake, ila baada ya Mutawkkil kusisitiza zaidi na zaidi, Imamu Hadi (a.s) akasoma shairi lifuatalo:


باتوا علی قُلَلِ الأجبال تحرسهم * غُلْبُ الرجال فما أغنتهمُ القُللُ
واستنزلوا بعد عزّ عن معاقلهم * فأودعوا حُفَراً، یا بئس ما نزلوا
ناداهُم صارخ من بعد ما قبروا * أین الأسرة والتیجان والحلل؟
أین الوجوه التی کانت منعمة * من دونها تضرب الأستار والکللُ
فأفصح القبر عنهم حین ساء لهم * تلک الوجوه علیها الدود یقتتل (تنتقل)
قد طالما أکلوا دهراً وما شربوا * فأصبحوا بعد طول الأکل قد أُکلوا
قد طالما أکلوا دهراً وما شربوا * فأصبحوا بعد طول الأکل قد أُکلوا
وطالما کنزوا الأموال وادخروا * فخلفوها علی الأعداء وارتحلوا
أضحت مَنازِلُهم قفْراً مُعَطلة * وساکنوها إلی الأجداث قد رحلوا

[110]

Maana ya Shairi hili ni kwamba: Walikuwa juu ya vilele vya milima wakilindwa na wanaume wenye nguvu. Lakini milima hiyo haukuwa na faida kwao. Waliondoka kutoka kwenye makazi yao ya heshima na hatimae kuingizwa mashimoni, wameporomoka mporomoka baya ulioje. Baada ya kuingizwa kaburini, sauti ililingana juu yao: "Vile Viti vya enzi na mataji ya kifalme yameenda wapi? Nyuso zilizofurahia neema na kufunikwa na pazia zimefikia wapi?" Na kaburi likajibu: "Wadudu wanakula kwa kuwaniana nyuso hizi. Walivaa na kula kwa muda mrefu na leo ni yao kuliwa. Walijenga nyumba kwa muda mrefu ili kujilinda na kisha wakawaachana nyumba hizo na kutengana na watu na wao wenyewe wakatokomea. Walikusanya mali kwa muda mrefu na kuzihifadhi na mwishowe wakawaachia maadui zao na wakaenda waliokwenda. Nyumba zao zilibaki tupu na wenyeji wao wakasafiri kuelekea kaburini. [111]

Masudi ameeleza akisema ya kwamba; Mashairi ya Imamu Hadi (a.s), yalimwathiri Mutawakkil na wenzake kikaoni humo, kiasi ya kwamba uso wa Mutawakkil ulionekana kuroa machozi, na akaamuru meza ya divai iondolewe na kumrudisha Imamu nyumbani kwake kwa heshima. [112]

Wafuasi na Wapokezi wa Hadithi

Makala Asili: Orodha ya Masahaba wa Imamu Hadi (a.s)

Katika kitabu cha Al-Imam Al-Hadi Min al-Mahdi ila Al-Lahdi, cha Sayyid Muhammad Kadhim Qazwini (aliyefariki: 1415 Hijiria), kuna idadi ya watu watu 346 waliotajwa kama ni Masahaba wa Imam Hadi (a.s) kitabuni humo. [113] Kulingana na Ripoti ya Rasuli Jaafarian ni kwamba; idadi ya wapokezi wa Hadithi waliosadikika kuwa ni wafwasi wa Imamu Hadi (a.s) ni kiasi cha watu 190, ambao wamepokea kiasi cha Hadithi 180. [114] Kulingana na kitabu kiitwacho Rijal Sheikh Tusi, ni kwamba; kuna idadi ya wapokezi 185 waliopokea Hadithi kutoka kwake (a.s). [115] Al-Ataridi katika kitabu Musnad al-Imam Al-Hadi ametaja watu 179 kama wapokezi wa Hadithi za Imam Hadi (a.s), na anasema kwamba; miongoni mwao kuna watu wenye sifa za thiqa (waaminifu), madhaifu, hasan (wanaokubalika kiasi), matruuk (waliotelekezwa bila ya kupewa umuhimu), na pia ndani yao kuna watu majhuul (wasiojulikana). [116] Kulingana na maelezo ya Al-Atariidi, ni kwamba; miongoni mwa baadhi ya wapokezi aliyowataja yeyeye, hawapo katika kitabu cha Rijal cha Sheikh Tusi, na pia baadhi ya wapokezi aliowataja Sheikh Tusi katika kitabu chake cha Rijali hawaonekani katika kitabu cha Musnad al-Ataridi. [117]

Abdul Adhaimu Hassani, Othman bin Said, [118] Ayub bin Nuh, [119] Hassan bin Rashid, na Hassan bin Ali Nassir [120] ni miongoni mwa Masahaba wa Imamu Hadi (a.s). Ibn Shahriashub anamtaja Ja'afar bin Suhail al-Saiqal kama mmoja wa mawakala wa Imamu Hadi (a.s), na anamtaja Muhammad bin Othman kama mlango mkuu wa Imamu Hadi (a.s), yaani ndiye kiungo baina yake na wafwasi wake. [121]

Rasuli Jaafarian katika jitihada za kuthibitisha Uirani wa baadhi ya Masahaba wa Imamu Hadi (a.s), amezingatia majina yao ya Kiirani kama ndio hoja na ithibati ya Uirani wao. Yeye amewazingatia watu kadhaa kuwa ni miongoni mwa Mashaaba wenye asili ya Kiirani, miongoni mwao ni kama vile; Bashar bin Bishaar Nishaburi, Fathu bin Yazid Jorjani, Hussein bin Said Ahwazi, Hamdan bin Ishaq Khurasani, Ali bin Ibrahim Taliqani, Muhammad bin Ali Kashani, [122] Ibrahim bin Shaibah Isfahani, na Abu Muqatil Dailami. [123] Yeye amewataja watu hawa na kusema kuwa; wao walikuwa ni miongoni mwa Masahaba wa Imamu Hadi (a.s) waliokuwa wakiishi nchini Iran. [124] Jaafarian, kwa kurejea kwenye barua ambayo Imam Hadi (a.s) alio iandika kwa wakala wake huko Hamadani ambapo kwa mujibu wake alimwambia kwa kusema "Nimekuarifisha kwa marafiki zangu (waungaji mkono wangu) huko Hamadan," [125] anasema kwamba; baadhi ya Masahaba wa Imamu walikuwepo huko Hamadan na pia kulingana na ushahidi, baadhi ya Masahaba wa Imamu walikuwa wakiishi Qazwini. [126]

Bibliografia (Seti ya Orodha ya Vitabu)

Kuna vitabu vilivyoandikwa kuhusu Imamu Hadi (a.s) katika lugha za Kiarabu na Kifarsi. Katika bibliografia ya Imam Hadi, vitabu thelathini katika uga huu vinaelezewa katika lugha za Kifarsi na Kiarabu. Baadhi ya kazi hizi ni pamoja na:

  1. Musnad al-Imam al-Hadi: Hichi ni kitabu kilicho andikwa na Azizullah Attaridi (aliyefariki: mwaka 1393 Shamsia): Kitabu hichi kina kiasi cha Hadithi 350 kutoka kwa Imamu Hadi (a.s).
  2. Hayat al-Imam Ali al-Hadi: Kazi ya Baqir Sharif Qarshi (aliyefariki: 1433 AH): Kitabu hichi kinajadili maisha ya Imamu Hadi (a.s).
  3. Al-Nur al-Hadi ila Ashab al-Imam al-Hadi: Kazi ya Abdulhussein Shabistari (aliyefariki: mwaka 1395 Shamsia): Kitabu hichi kinawatambulisha Masahaba 193 wa Imamu Hadi (a.s).
  4. Mausu’atu Imam al-Hadi (Encyclopedia ya Imamu Hadi): Nacho ni kitabu kilicho chapishwa katika juzuu nne kurasa nne chenye kurasa 2019.

Aidha, kuna kitabu kiitwacho (Shokuh-e Samarra) kinacho jumuisha mkusanyiko wa makala kuhusu Imamu Hadi na Imamu Askari (a.s), kilichapishwa na Chuo Kikuu cha Imamu Sadiq (a.s) mnamo mwaka 1390 Shamsia, che

Rejea

Vyanzo

  • Isfahani, Abu l-Faraj al-. Maqatil al-talibiyyin. Beirut: Mu'assisa al-A'lami li l-Matbu'at, 1987
  • 'Atarudi, 'Aziz Allah al-. Musnad al-Imam al-Hadi (a). Qom : Al-Mu'tamar al-'Alami li l-Imam al-Rida (a), 1410 AH.
  • Ash'ari al-Qumi, Sa'd b. 'Abd Allah al-. Al-Maqalat wa l-Firaq. Tehran: Intisharat 'Ilmi wa Farhangi, 1361 SH.
  • Dakhil, 'Ali al-. A'immatuna, Sirat al-a'imma al-ithna 'ashar. Qom: Sattar, 1429 AH.
  • Ibn al-Jawzi, Yusuf. Tadhkirat al-khawass. Qom: Leyli, 1426 AH.
  • Ibn Hajar al-Haytami, Ahmad b. Muhammad. Al-Sawa'iq al-muhriqa 'ala ahl al-rafd wa al-dalal wa al-zandaqa. Cairo: Maktabat al-Cairo.
  • Ibn Shahrashub, Abu Ja'far Muhammad b. 'Ali. Manaqib al-i Abi Talib. Beirut: Dar al-Adwa', 1421 AH.
  • Irbili, Abu l-Hasan 'Ali b. 'Isa al-. Kashf al-ghumma fi ma'rifat al-a'imma. Qom: Ahl al-Bayt World Assembly, 1426 AH.
  • Khasibi, Husayn b. Hamdan al-. Al-Hidayat al-kubra. Beirut: Mu'assisa al-Balagh, 1991.
  • Kulayni, Muhammad b. Ya'qub al-. Usul Al-Kafi. Beirut : Dar al-Ma'arif li l-Matbu'at, 1998.
  • Majlisi, Muhammad Baqir al-. Bihar al-anwar'. Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-'Arabi, 1403 AH.
  • Mufid, Muhammad b. Muhammad b. Nu'man al-. Al-Irshad trans. by Sa'idi Khurasani. Tehran: Intisharat Islamiyya, 1380 sh.
  • Nawbakhti, al-Hasan b. Musa al-. Firaq al-Shi'a Trans. by Muhammad Jawad Mashkur. Tehran: Intisharat 'Ilmi wa Farhangi, 1361 SH.
  • Nuri, Mirza Husayn. Mustadrak al-wasa'il wa mustanbat al-masa'il. Beorut: Al al-Bayt, 1408 AH.
  • Saduq, Muhammad b. 'Ali al-. Al-Tawhid. Qom: Jami'a Mudarrisin, 1389 AH.
  • Saduq, Muhammad b. 'Ali al-. 'Uyun akhbar al-Rida. Tehran: Nashr Jahan, 1378 SH.
  • Sayyid al-Murtada, 'Ali b. Husayn Al-. Masa'il al-nasiriyya. Tehran: Mu'assisa al-Huda, 1417 AH.
  • Tabrisi, al-Fadl b. al-Hasan al-. I'lam al-wara bi a'lam al-huda. Qom: Sitarih, 1417 AH.
  • Tusi, Muhammad b. al-Hasan al-. Al-Ghiba. Dar al-Ma'arif al-Islamiyya, 1411 AH.
  • Tusi, Muhammad b. al-Hasan al-. Ikhtiyar ma'rifat al-rijal al-ma'ruf bi rijal al-kashshi. Mashhad: Mashhad University, 1348 SH.