Haram za Maimamu wawili Hadi na Askary (a.s)

Kutoka wikishia
Haram ya Maimamu wawili, Imam Hadi(a.s) na Imam Hassan Askary(a.s)

Haram ya Askariyein au haram ya Imamein Askariyein (Kiarabu: حرم الإمامين العسكريين (ع)) (haram Mbili za Maimamu wawili) yaani Imam Hadi na Askary (a.s) ni sehemu ambayo wamezikwa hapo Imam Hadi (a.s) (aliyeuawa shahidi 254 Hijiria) na mwanawe Imam Hassan Askary (a.s) (aliyeuawa shahidi 260 Hijiria). Haram hiyo inapatikana katika mji wa Samarra na inahesabiwa kuwa moja ya haramu na maeneo ya maziara ya Mashia katika nchi ya Iraq.Katika eneo hilo tukufu wamezikwa pia Nargis Khatun mke wa Imamu Hassan Askary (a.s) na mama wa Imamu Mahdi (a.t.f.s), Hakimah binti wa Imamu Jawad (a.s) na masharifu (watu wanaotokana na kizazi cha Mtume) wengine kadhaa pamoja na Maulamaa wa Kishia.

Imamu Hadi (a.s) alizikwa mwaka 254 Hijiria na Imamu Hassan Askary (a.s) mwaka 260 Hijiria katika nyumba yao. Ilikuwa mwaka 328 Hijiria ambapo kuba la kwanza lilijengwa katika makaburi ya watukufu hawa wawili na baada ya hapo eneo hilo lilijengwa, likaboreshwa, kukarabatiwa na kukamilishwa katika duru na zama tofauti. Katika miaka ya 2006 na 2007, sehemu ya haramu hiyo ilibomolewa kufutia mlipuko na shambulio la kigaidi. Baada ya mashambulio hayo kamati ya ukarabati wa maeneo matakatifu na ofisi ya Ayatullah Ali Sistani zilijenga haramu hiyo na eneo lake la ndani la haram ya Maimamu hawa wawili.

Mahali ilipo na umuhimu Wake

Haram ya Askariyein au Haram ya Maimamu wawili yaani Imam Hadi na Askary (a.s) ni sehemu ambayo wamezikwa hapo Maimamu wawili wa Kishia na eneo hilo linahesabiwa kuwa moja ya maziara ya Mashia katika nchi ya Iraq. Haram hii kijiografia ipo katika mji wa Samarra (kilomita 120 kaskazini mwa Baghdad). [1] Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebuu ya Kishia, imeusiwa kwenda kuwazuru Maimamu hawa wawili. [2] Kila mwaka Mashia wengi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia huenda katika mji wa Samarra kwa ajili ya kwenda kufanya ziara katika Haram ya Maimamu Wawili Hadi na Askry (a.s).

Historia fupi

Mchoro wa ramani ya Haram ya Maimamu wawili (a.s)

Imam Ali ibn Muhammad al-Hadi (a.s) ni Imamu wa 10 na Imamu Hassan Askary ni Imamu wa 11 katika mlolongo wa Maimamu 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka katika kizazi cha Bwana Mtume (s.a.w.w). Baada ya kufa shahidi walizikwa katika nyumba yao huko Samarra. [3] Imam Hadi alikuwa amenunua kutoka kwa Dalil ibn Ya'qub Nasarani. [4] Dhabihullah Mahallati anasema: Nyumba ambayo, Maimamu Hadi na Askary walizikwa ndani yake, mpaka mwaka 328 Hijiria ilikuwa katika hali yake ya awali ingawa ilikuwa na dirisha ambapo kupitia kwalo baadhi ya watu walikuwa wakiyazuru makaburi ya Maimamu hao na kuonyesha heshima na taadhima kwa watukufu hao wawili. [5]

Mahallati akitumia ushahidi wa kaswida na mashairi ya Muhammad Samawi (1292-1370 Hijria) anasema kuwa, Nasser al-Dawla Hamadani (aliyetawala 323-356 Hijria) mmoja wa watawala wa ukoo wa Aal Hamadani alikuwa mtu wa kwanza ambaye aliifanyia marekebisho nyumba hiyo na mwaka 328 akajengea kuba makaburi ya Maimamu hao wawili. [6] Baada ya hapo kulifanyika marekebisho na ukarabati tofauti katika haramu hizo mbili. Muizz al-Dawla Deylami [7] na Azud al-Dawla Deylami [8] watawala kutoka ukoo wa Aal Buya (uliotawala 322-448 Hijria), Arslan Basasiri (aliaga dunia 451 H) [9], Rukn al-Din Abu'l-Muzaffar Berkyaruq (aliaga dunia 776 H) mmoja wa watawala na wafalme wa ukoo wa Seljuk (Seljuk Empire), [10] Ahmad al-Nasser li-Din Allah, al-Mustansir Billah mtawala wa ukoo wa Bani Abbas (575-622), [11] Sultan Hassan Jalayeri (aliaga dunia 776), [12] Sultan Hussein Safavi (alitawala 1105-1135 H) [13] mmoja wa wafalme wa ukoo wa Safaviyah, Ahmad Khan Donboli, [14] Hassanqali Khan Donboli (aliaga dunia 1297 Hijria Shamsia), [15] Nasser al-Din Shah Qajar (alitawala 1264-1313) na Mirza Shirazi (1230-1312 H) [16] ni miongoni mwa watu ambao kwa amri na maagizo yao haramu yya Maimamu Hadi na Askray (a.s) ilifanyiwa marekebisho na ukarabati.

Kubomolewa katika shambulio la kigaidi

Makala asili: Kubomolewa Haram ya Askriyein
Uharibifu wa kaburi la Maimamu wawili (a.s) kutokana na milipuko ya kigaidi

Haram ya Askariyein (Maimamu Wawili) zililipuliwa kufuatia mashambulio ya kigaidi ya makundi ya kitakfiri katika miaka ya 1384 na 1386 Hijria Shamsia na kupelekea kubomolewa. Hatua hiyo ya kigaidi ilikabiliwa na radiamali kali ya Marajii Taqlidi na Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika maeneo mbalimbali ya dunia. Katika shambuio hilo la bomu, sehemu ya kuba ya haram hiyo ambayo ilikuwa imejengwa kwa matofali na kurembeshwa kwa dhahabu ya kuchovya na kuta zake ziliporomoka na kubomoka, lakini nguzo za kuba na jengo lake la asili pamoja na kuta zake zilibakia salama.[14] Kamati ya Ukarakati ya Maeneo Matakatifu ya Iran iliikarabati haram hiyo baina ya mwaka 1389 mpaka 1394.[42] Katika ukarabati huu zaidi ya matofali 23,000 yalichovewa dhahabu.[43] Kadhalika ujenzi wa dharih (eneo la ndani linalozunguka kaburi) mpya ulifanyika chini ya usimamizi wa Jawad Shahristani, mwakilishi wa Ayatullah Ali Sistani nchini Iran.[44]

Usanifu majengo na majengo mengine

Picha ya Haram mpya ya Maimamu wawili (a.s)

Haram ya Maimamu Hadi na Askary (a.s) inaundwa na majengo mbalimbali ambapo baadhi yake ni:

  • Kuba: Haram ya Askariyein ina ukubwa wa mita mraba 1,200 na kuba lake ni kubwa zaidi miongoni mwa haram za Maimamu wa Mashia. [45].
  • Minara: Katika pande mbili za kuba kuna minara miwili ambayo maeneo ya juu ya minara hiyo yamechovewa dhahabu. [46]
  • Dharih: Katika kujenga dharih (eneo la ndani linalozunguka kaburi) kulitumika kilo 4,500 za fedha na kilo 70 za dhahabu. [47]
  • Eneo la Ndani: Haram ya Maimamu Hadi na Askary (a.s) ina sehemu moja ya ndani ambayo ni kubwa ikiwa imegawanywa katika maeneo kadhaa.[48]

Waliozikwa hapo

Makala asili: Orodha ya waliozikwa katika Haram ya Askariyein (a.s) Dhabihullah Mahallati anasema katika kitabu cha Ma'athir al-kubra fi tarikh Samarra kwamba, mahali hapo kuna makaburi na watu mbalimbali waliozikwa katika eneo hilo kama Nargis mama wa Imamu Mahdi (a.t.f.s), Hakimah binti wa Imam Jawad (a.s), mama yake Hassan Askary (a.s), Hussein ibn Ali al-Hadi, kaka wa Imamu Askary yaani Jafar Kadhab na Abu Hashim Jafari mmoja wa wajukuu wa Jafar Tayyar.[49] Samana al-Maghribiyyah, mama wa Imam Hadi (as),[50] Ahmad Khan Donboli (aliaga dunia 1200 H) na mwanawe Husseinqali Khan Donboli [51] na Agha Reza Hamadani (aliyeaga dunia 1322 H) ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa Mirza Shirazi.

Rejea


Vyanzo

  • Goldastehha-e Haram Imamain Askariyain az Takhrib to Thalakari, Mashreqnews, diakses tanggal 22 Agustus 2022
  • Khamehyar, Ahmad. Takhrib Zeyaratgahha-e Eslami dar Kesywarha-e Arabi, Qom: Dar al-A'lam li Madrasah Ahl al-Bayt as.
  • Khatib al-Baghdadi, Ahmad bin Ali. Tarikh Baghdadi, riset: Basyar 'Iwad Ma'ruf, Beirut:Dar al-Gharb al-Islami, cet. pertama.
  • Mahallati, Dzabihullah. Ma'tsar al-Kubra fi Tarikh Samarra', Qom: al-Maktabah al-Haydariyah.
  • Qaidan, Ashghar. 'Atabat 'Aliyat 'Iraq, Teheran: Masy'ar.
  • Qumi, Syekh Abbas. Al-Fawaid al-Radhawiyah fi Ahwal Ulama al-Madzahib al-Ja'fariyah, Qom: Bustan Ketab.
  • Sakht-e Dzarih Muthahhar Imamain Askariyain, Seda wa Sima Markaz-e Qom, diakses tanggal 22 Agustus 2022.
  • Shehhati Sardurudi, Muhammad. Guzideh Sima-e Samara Sina-e Musa, Teheran: Masy'ar.
  • Syekh Mufid, Muhammad bin Muhammad, al-Irsyad fi Ma'rifah Hujajillah 'ala al-'Ibad, koreksi: Muassasah Al al-Bayt as, Qom: Kongres Syekh Mufid, cet, pertama.
  • Takhrib wa Bazsazi Haram Imamain Askariyain, Farsnews, diakses tanggal 22 Agustus 2022.
  • Thusi, Muhammad bin Hasan, Tahdzib al-Ahkam, Riset: Hasan Musawi Khurasan, Teheran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, cet. ke-empat.

Kigezo:Akhir Kigezo:Tempat-tempat Suci