Muhammad ibn Ali al-Hadi (a.s)

Kutoka wikishia
Haram ya Muhammad ibn Ali al-Hadi (a.s)

Muhammad ibn Ali al-Hadi (a.s) (aliaga dunia 252 Hijiria). Yeye ni mashuhuri kwa jina la Sayyid Muhammad na anajulikana pia kama Sab'u al-Dujayl (Simba wa Dujayl) ni mtoto wa Imam al-Hadi (a.s). Baadhi walikuwa wakidhani kwamba, atachukua jukumu la uongozi baada ya baba yake; hata hivyo kuaga kwake dunia katika zama za uhai wa baba yake, Imam Hassan al-Askary (a.s) akachukua jukumu la Uimamu. Kizazi cha Sayyid Muhammad kiliendelea kupitia kwa mjukuu wake Shams al-Din Muhammad mashuhuri kwa jina la Mirsultan Bukhari. Kadhalika Masayyid (masharifu) wa Aal Ba'aj wanaoishi katika maeneo ya Iraq na Iran wanatambuliwa kama wanatokana na kizazi chake.

Sayyid Muhammad ana nafasi maalumu miongoni mwa Wairaqi: Watu hawaapi kwa jina lake, karama zake ni mashuhuri na kawaida watu wanaokwenda kuzuru Haram za Maimamu wawili Hadi na Askary (a.s) huko Samarra huenda kumzuru. Sayyid Muhammad aliaga dunia mwaka 252 Hijiria katika eneo la Balad yapata kilomita 50 kusini mwa mji wa Samarra na kuzikwa katika eneo hilo. Kaburi lake kwa mara ya kwanza lilijengewa katika karne ya nne Hijiria na baada ya hapo lilikarabatiwa katika duru mbalimbalui za Maulamaa wa kidini, Marajii Taqlidi na wafalme tofauti. Adud al-Dawla al-Daylami mmoja wa watawala wa ukoo wa Buwaih, Shah Ismail Safavi miongoni mwa watawala wa Kisafavi, Mirza Shirazi, Marajii Taqlidi wa karne ya 14 Hijiria na Mirza Hussein Nouri mpokezi wa hadithi wa Kishia katika karne yua 14 walilifanyia ukarabati na kuliboresha kaburi la Sayyid Muhammad katika duru mbalimbali.

Kuna athari na vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na Sayyid Muhammad ambapo akthari yake vinahusiana na maisha yake na makarama yaliyokuliwa kutoka kwakke: Miongoni mwa vitabu hivyo, ni kitabu cha lugha ya Kiarabu cha “ Hayat Wakaramat Abu Ja’far Muhammad ibn al-Imam Ali al-Hadi (a.s)” kilichoandikwa na Muhammad Ali Urdubadi (kuzaliwa 1312 kuaga dunia 1380 Hijiria). Kitabu hiki kimetarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi kikiwa na anuani ya “Setareh Dujayl”.

Historia ya Maisha Yake

Sayyid Muhammad ni mtoto wa Imam Hadi (a.s). [1] Inasemekana kuwa, mama yake alifahamika kwa jina la Hudayth au Sulayl. [2] Alizaliwa katika eneo la Sarya jirani na Madina mwaka takribani 228 Hijria. [3]. Wakati mwaka 233 Hijria Imam Hadi (a.s) alipatiwa aende Samarra kwa amri ya mtawala mutawakkil Abbasi, Sayyid Muhammad alikuwa na umri wa miaka 5 wakati huo na alibakia huko Sarya. [4] Kuhusiana na kwamba, ni mwaka gani alielekea Samarra alipokuwa baba yake, hakuna taarifa kuhusu hilo. Hata hivyo inaelezwa kwamba, ilikuwa mwaka 252 wakati alipoondoka Samarra na kuelekea Madina. Wakati alipofika Balad aliaga dunia baada ya kuugua na kuzikwa katika eneo hilo. [6] Kuniya ya Sayyid Muhammad ilikuwa Abu Ja’far na Abu Ali. [7] Aidha alifahamika kwa lakabu za Sayyid Muhammad Ba’aj, [8] Sab’u al-Dujayl na Sab’u al-Jazirah. [9]

Wajukuu

Kwa mujibu wa Sheikh Abbas Qomi mwandishi wa historia wa karne ya 14 ni kuwa, imenukuliwa kutoka kwa Sayyid Hassan Baraqi (aliaga dunia 1332 H) kwamba, kizazi cha Sayyid Muhammad kiliendelea kupitia kwa mmoja wa wajukuu zake aliyejulikana kwa jina la Shams al-Din Muhammad (aliaga dunia 832 au 833 Hijria). [10] Nasaba ya Shams al-Din inafika kwa Ali mtoto wa Sayyid Muhammad kwa pengo la watu wanne na kwa kuwa alizaliwa katika mji wa Bukhara na kukulia huko ameondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Mir Sultan Bukhari. Watoto wake ni mashuhuri kwa jina la Bukhariyun. [11] Baadaye alikwenda kuishi Bursa na aliaga dunia akiwa huko na kuzikwa katika mji huo. [12] Sheikh Abbas Qomi amenukuu pia kutoka kwa Sayyid Hassan Baraqi ya kwamba, amemtambua Sayyid Muhammad Ba’aj kwamba, ni katika wajuu wa Sayyid Muhammad. [13] Inasemekana kuwa, masharifu wa Aal Ba’aj wanaishi na kupatikana katika maeneo kama Maysan, Dhi Qar, Wasit, Qadisiyah, Baghdad na Najaf Iraq [14] na Khozestan Iran na wao wanatokana na kizazi cha Ali na Ahmad ambao ni watoto wa Sayyid Muhammad. [15]

Nafasi Yake

Baqir Sharif al-Qureshi mhakiki wa Kishia (aliyeaga dunia 1433 Hijiria) anasema kuwa, akhlaqi (maadili mema) na adabu njema za Sayyid Muhammad zilikuwa zikimtofautisha na watu wengine. [16] Ni kwa kuzingatia hali hiyo, ndio maana baadhi ya Mashia walikuwa wakidhani kwamba, atapokea jukumu la Uimamu baada ya baba yake yaani Imam Hadi (a.s). [17] Sayyid Muhammad daima alikuwa akifuatana na kaka yake Imam Hassan al-Askary (a.s). [18] Kwa mujibu wa Baqir Sharif al-Qureshi ni kwamba, Imam Hassan Askary (a.s) alikuwa na na jukumu la kumlea na kumfundisha Sayyid Muhammad. [19] Kwa mujibu wa kile kilichonukuliwa na Sheikh Abbas Qomi ni kwamba, baada ya kifo cha Sayyid Muhammad, Imam Hassan al-Askary (a.s) alijiumiza shingo yake na alipokosolewa kwa hatua hiyo, aliashiria kitendo kama hicho kilichofanywa na Nabii Mussa (a.s) baada ya kifo cha nduguye Harun (a.s). [20]

Kwa mujibu wa Sa’ad ibn Abdallah Ash’ari na Hassan Mussa Nawbakhti waandishi wa wa historia ya makundi mbalimbali katika Uislamu walioishi katika karne ya tatu na ya nne ni kuwa, kundi miongoni mwa makundi ya Kishia baada ya kufa shahidi Imam Hadi (a.s) lilikana kifo cha Sayyid Muhammad na kuamini Uimamu wake na wakamtambua Sayyid Muhammad kuwa ni mrithi wa baba yake na kiongozi baadaye yake na kwamba, huyu ndiye yule Mahdi aliyeahidiwa; hii ni kutokana na kuwa, Imam Hadi alimtambulisha Sayyid Muhammad kwa ajili ya Uimamu na kwa kuwa uwongo haufai kutoka kwa Imam na bad’a pia haijatokea, basi yeye kimsingi hajaaga dunia na baba yake amemficha kunako watu. [21] Hayo yote yalisemwa na kubainishwa katika kipindi ambacho Sayyid Muhammad alikuwa ameaga dunia katika zama za uhai wa Imam Hadi (a.s), [22] na siku ambayo watu walikwenda kwa Imam Hadi kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na rambirambi kutokana na kifo cha Sayyid Muhammad, aliashiria Uimamu wa Imam Hassan al-Askary (a.s) [23]. Kwa mujibu hadithi, wakati Imam Hadi (a.s) anaashiria hilo walikuweko takribani watu 150 kutoka katika ukoo wa Aal Abi Twalib, Bani Hashim, Kureshi na kadhalika. [24]

Mirza Hussein Nouri msomi na mtaalamu wa hadithi (aliaga dunia 1320 H) anasema kuwa, karama za Sayyid Muhammad na simulizi zake zimepokewa kwa wingi na ni mashuhuri pia hata kwa Waislamu wa madhehebu ya Suni; na ni kutokana na sababu hiyo ndio maana watu wa Iraq walikuwa wakiogopa kuapa kwa jina lake, kama mtu akituhumiwa kwamba, ameiba na kuchukua mali fulani, basi alikuwa yuko tayari kurejesha mali hiyo (ambayo kimsingi haikuchukua) lakini hakuwa tayari kuapa kwa jina la Sayyid Muhammad. [25] Katika baadhi ya karama za Sayyid Muhammad yaliyonukuliwa ni yale yanayonukuliwa na Muhammad Ali Urdubadi (1312-1380 H) katika kitabu cha “Hayat Wakaramat Abu Ja’far Muhammad ibn al-Imam Ali al-Hadi (a.s)” ambapo ndani yake kumetajwa takribani karama 60. [26]

Haram ya Sayyid Muhammad

Uharibifu wa jengo la Haram ya Sayyid Muhammad katika shambulio la ISIS (mwaka 2016)

Kaburi la Sayyid Muhammad linapatikana katika mji wa Balad, kilomita 85 kaskazini mwa Kadhmein na kilomita 50 kusini mwa Samarra na linahesabiwa kuwa, moja ya maeneo ya Mashia nchini Iraq ya kufanya ziara. Ni kawaida watu wanaokwenda kuzuru Haram za Maimamu wawili (Imam Hadi na Askary a.s) huko Samarra huenda kumzuru pia Sayyid Muhammad. [27]

Hakuna taarifa makini na za kuaminika kuhusiana na kujengwa Haram ya mwanzo ya Sayyid Muhammad; pamoja na hayo inaelezwa kwamba, kwa kuzingatia marekebisho na ukarabati uliofanyika katika miaka ya 1379 mpaka 1384 Hijria katika jengo lilipo kaburi lake inafahamika kuwa, jengo la awali historia yake inarejea katika karne ya nne Hijiria ambapo lilijengwa kwa amri ya Adud al-Dawla al-Daylami mmoja wa watawala wa ukoo wa Buwaih. [28] Jengo la pili historia yake inarejea katika karne ya sita Hijiria ambapo lilijengwa kwa amri ya Shah Ismail Safavi baada ya kuukomboa mji wa Baghdad. [29] Kumeelezwa pia kuhusiana na kujadidishwa jengo lilipo kaburi la Sayyid Muhammad katika mwaka 1189 Hijiria. [30]

Kadhalika Zaynul Abidin ibn Muhammad Salmasi (aliaga dunia 1266 H) ambaye ni mmoja wa wanafuzni wa Sayyid Muhammad Mahdi Bahr al-Ulum akitekeleza amri ya Amir Khan Sardar mwaka 1208 Hijria alijenga jengo katika kaburi la Sayyid Muhammad akitumia matofali na chokaa na kuandaa eneo hilo kwa ajili ya kuwapa makazi wafanyaziara. [31] Mwaka 1244 Mullah Muhammad Saleh Qazwini Hairi aliyabomoa majengo ya kale yaliyokuweko hapo na kuanza kujenga jengo jipya ambapo ukabarati na ujenzi huu ulifikia tamati mwaka 1250. [32] Kadhalika Mirza Shirazi 91230-1312 H) mmoja wa wanazuoni na Marjaa Taqlidi, baada ya kuanza kukaa Samarra na vilevile Mirza Muhammad Tehran Askary (1281-1371 H) walifanya ukarabati katika haramu ya Sayyid Muhammad na kuongeza vyumba vya jengo lake. [33]. Agha Bozorg Tehrani anasema, Mirza Hussein Nouri (1254- 1320 H) alifanya ukarabati wa Haram ya Sayyid Muhammad mwaka 1317. [34]

Sayyid Muhammad Tabatabai, mtoto wa Agha Hussein Qomi Marjaa mkubwa wa Kishia alitumia mali zilizokuwa zimekusanywa katika kipindi cha Umarjaa wa baba yake kwa ajili ya jengo jipya la Haram ya Sayyid Muhammad. Hiyo ilikuwa ni baina ya miaka ya 1379-1384 Hijiria, ambapo ujenzi huu ulihusisha ukubwa wa mita mraba takribani 150. Katika ujenzi huo kuliwekwa pia mnara na kuba pamoja na kujengwa eneo la ndani la kaburi lake. [35] Kamati ya Ukarabati wa Maeneo Matakatifu mwaka 1392 Hijria Shamsia ilianza ukarabati wa kaburi la Sayyid Muhammad. [36] Hata hivyo tarehe 7 Julai 2016, kaburi la Sayyid Muhammad lilishambuliwa na kundi la kigaidi la Daesh na sehemu ya Haram hiyo ikaharibiwa, [37] hata hivyo ukarabati wake uliendelea hadi mwaka 2020. [38]

Vitabu Kuhusu Sayyid Muhammad

Kuna vitabu vilivyoandikwa kuhusiana na Sayyid Muhammad. [3] Katika makala hii tutaashiria baadhi tu ya athari na vitabu hivyo:

  • “Hayat Wakaramat Abu Ja’far Muhammad ibn al-Imam Ali al-Hadi (a.s)” kilichoandikwa na Muhammad Ali Urdubadi (1312-1380 Hijiria). Kitabu hicho cha lugha ya Kiarabu kimetarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi na Ali Akbar Mahdipoor kikiwa na anuani ya “Setareh Dujayl” yaani Nyota ya Dujayl. Kitabu hiki kina sehemu mbili ambapo katika faslu yake ya kwanza kinatoa utambulisho wa Sayyid Muhammad na Haram yake [40], huku faslu ya pia ikiwa maalumu kwa nukuu za karama zake.
  • Risaleh Dar Karamaat Sayyid Muhammad ibn Ali al-Hadi: Mwandishi Jabir Al Abdul-Ghaffar Kashmiri. [41]
  • Risalat fi Karamaat al-Sayyid Muhammad ibn al-Imam Ali al-Hadi, kimeandikwa na Hashim Muhammad Ali Baldawi. [42]

Vyanzo

  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Taʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Ashʿarī, Saʿd b. ʿAbd Allāh al-. Kitāb al-maqālāt wa al-firaq. Edited by Muḥammad Jawād Mashkūr. Tehran: Markaz-i Intishārāt-i ʿIlmī wa Farhangī, 1360 Sh.
  • Āgā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-shīʿa. Qom and Tehran: ʿIsmāʿiliyān and Islāmiya, 1408 AH.
  • Badāwī, ʿAbd Allāh ʿAlī Ḥasan. Sabʿ al-jazīra. Iraq: Sabʿ al-Dujayl l-Tabligh wa al-Irshād, [n.d].
  • Ḥirz al-Dīn, Muḥammad. Marāqid al-maʿārif. Edited by Muḥammad Ḥusayn Ḥirz al-Dīn. Qom: Manshūrāt Saʿīd b. Jubayr, 1371 Sh.
  • Ḥusaynī Madanī, Ḍāmin b. Shadqam. Tuḥfat al-azhār wa zulāl al-anhār fī nasab al-aʾimmat al-aṭhār (a). [n.p]. Al-Turāth al-Maktūb, [n.d].
  • Iṣfahānī, ʿAbd Allāh. Sitāra-yi dirakhshān-i manṭaqa-yi Dujayl Iraq. Farhang-i Ziyārat. No 24-25. Winter 1393 Sh.
  • Ibn Ṣūfī, Nasāba. Al-Majdī fī ansāb al-ṭālibīn. Qom: Maktabat Ayatullāh al-Marʿashī al-Najafī, 1422 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1388 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. Tehran: Islāmiyya, 1363 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Nawbakhtī, Ḥasan b. Mūsā al-. Firaq al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1404 AH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Najm al-thaqib fī aḥwāl al-Imām al-ghāʾib'. Qom: Intishārāt-i Masjid-i Jamkarān, 1384 AH.
  • Qarashī, Bāqir Sharīf al-. Mawsūʿat sīra-yi Ahl al-Bayt; al-Imām al-Ḥasan al-ʿAskarī (a). Edited by Mahdī Bāqir Qarashī. Najaf: Muʾssisa al-Imām al-Ḥasan, 1433 AH.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Safīnat al-biḥār wa madīnat al-ḥikam wa l-āthār. Qom: Dār al-Uswa, 1414 AH.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahā l-āmāl fī tawārīkh al-Nabī wa al-Āl. Qom: Dalil-i Mā, 1379 Sh.
  • Sayyid Muḥammad b. al-Imām ʿAlī al-Hādī (a). Imām Riḍā Network. visited: 2021/4/19.
  • Urdūbādī, Muḥammad ʿAlī. Ḥayāt wa kirāmāt Abū Jaʿfar Muḥammad b. al-Imām ʿAli al-Hādī. [n.p]. Dār al-Maḥajjat al-Bayḍā, 1427 AH.