Imamu Jawadi (a.s)

Kutoka wikishia
Haramu ya Imam Kadhim (a.s)

Muhammad bin Ali bin Mussa anayejulikana kwa umaarufu wa Imamu Jawad na wakati mwingine Imamu Muhammad Taqi. Muhammad bin Ali alizaliwa mnamo mwaka 195 na kufariki 220 Hijiria), naye ni Imamu wa tisa wa Mashia wanao amini Maimamu Kumi na mbili. Kunia yake ni Abu Jaafar, ambaye alikupewa lakabu ya Jawad na Ibn al-Ridha. Alipewa lakabu ya Jawad kwa sababu ya hisani na ukarimu alionao.

Imamu Jawad alishika nafasi ya Uimamu kwa muda wa miaka kumi na saba, ambayo iliambatana na utawala wa Maamuni Abbasi na Muu'tasim Abbasi. Kwa mujibu wa nukuu kadhaa kutoka katika vyanzo mbali mbali, Imamu JaWad (a.s) aliuawa kishahidi mwishoni mwa Dhul-Qaidah mwaka 220 Hijiri akiwa na umri wa miaka 25. wakati kifo chake cha kishahidi Imamu Jawadi alikuwa ndiye Imamu mdogo zaidi miongoni mwa Maimamu wa Kishia. Baada ya kifo chake yeye alizikwa karibu na babu yake Mussa bin Jafar (a.s) kwenye mava ya Maquraish huko Kadhimeini.

Umri mdogo aliokuwa nao Imamu Jawad (a.s) wakati wa kushika nafasi ya Uimamu -ambao ni umri wa miaka minane- uliwatia shana na wasiwasi wafuasi kadhaa wa Imamu Ridha (a.s) juu Uimamu wake. Wasiwasi huo ulipelekea wafuasi hao kugawika makundi manne; Baadi yao walimtambua Abdullah bin Mussa kuwa ni Imamu wao, wengine wakamfuata Ahmed bin Mussa aitwaye Shahcheragh kama ni Imam wao, kundi moja likajiunga na Waaqifiyyah na kundi la jengine amabolo lilikuwa ni kundi la wengi wao lilibaki mrengo wa kulia na kuukubali Uimamu wa Muhammad bin Ali (a.s).

Mawasiliano baina ya Imamu Jawadi (a.s) na Mashia wake, yalifanyika zaidi kupitia mawakala kwa njia ya mawasilianao ya barua. Wakati wa Uimamu wake, kulikua na harakati kadhaa za kimadhehebu zilizochukua nafasi katika kipindi hicho, nazo ni harakati za; Ahlul-Hadith, Zaidiyyah, Waaqifiyya na Ghulati. Imam Jawadi (a.s) aliwafahamisha Mashia wake juu ya imani ya madhehebu hayo na akawakataza kusali nyuma yao, na pia aliakawalaani Maghulati.

Mijadala maarufu zaidi ya kielimu kati ya Imamu Jawad (a.s) na wanazuoni wa madhehebu mengine ya Kiislamu, ilikuwa ni mijadala juu ya masuala ya kitheolojia, kama vile nafasi ya Makhalifa wawili (Omar na Abu Bakar) na masuala ya kifiqhi kama vile hukumu ya kumkata mwizi mkono na sheria za Hijja, ambayo ni mijadala maarufu iliyojulikana mingoni mwa Maimamu wa Shia.

Kuna idadi ya Hadithi zipatazo 250 zimesimuliwa kutoka kwa Imamu Jawad, ambapo sababu ya uchache huu wa Hadithi unahusishwa na maisha yake mafupi pamoja na kuwa chini ya udhibiti wa dola na utawala wa zama hizo. Idadi ya masahaba wasimulizi wa Hadithi zake, imekadiriwa kuwa ni idadi ya watu 115 hadi 193. Miongoni mwa masahaba wa Imamu Jawadi ni; Ahmad bin Abi Nasri Bizanti, Safwan bin Yahya na Abdul 'Adhim Hasaniy.

Kuna idadi ya karama zilizoripotiwa kuhusuiana na Imamu Jawadi (a.s) Ripoti zinapatikana katika vyanzo vya Kishia kuhusiala hilo ni; kuzungumza wakati wa kuzaliwa, kusafiri kutoka ardhi moja kwenda nyingine bila ya kutumia kipando, kuponya wagonjwa na kutakabaliwa dua zake bila kuchelewa. Wanazuoni wa Kisunni pia ni wenye kumpa heshima maalumu na kumuadhimu Imamu Jawadi (a.s).

Kuna zaidi ya kazi 600 za kielimu zilizoandwa kuhusiana na Imamu huyu wa 9 wa Kishia zililo chapishwa katika lugha tofauti. Miongoni mwa kazi mbalimbali zilizo andikwa kuhusiana naye ni; Wafatu al- Imam al-Jawad وفاة الامام الجواد, Musnad al-Imam al-Jawad مُسند الامام الجواد, Ensaiklopidia ya Imamu al-Jawad موسوعة الامام الجواد علیه‌السلام, Al-Hayatu al-Siyasiyyah lil-Imami al-Jawad الحیاة السیاسیة للامامِ الجواد na Al-Hayatu a-Imami Muhammad al-Jawad حیاة‌ الامام محمد الجواد.


Nasaba, kunia na lakabu

Makala Asili: Orodha ya lakabu na kunia za Imamu Jawad (a.s)

Muhammad bin Ali bin Musa bin Jafar ni Imamu wa 9 wa madhehebu ya Shia wanaofuata Maimamu Kumi na mbili, ambaye ni maarufu kwa jina la Jawadu al-Aimma (Imamu mkarimu). Nasaba yake inamfikia Imamu Ali (a.s), kupitia mababu sita. Ambapo Imamu Ali (a.s) hutambuliwa kuwa ndiye Imamu wa kwanza wa Mashia. Baba yake ni Imamu Ridha (a.s), ambaye Imamu wa nane wa Mashia. [1] Mama yake alikuwa ni mjakazi aitwaye Sabika Nuubiyyah. [2]

Kuniya yake ni Abu Jaafar na Abu Ali [3] Katika vyanzo vya simulizi za Hadithi, ametajwa kwa jina la Abu Ja'afar Thani (Abu Ja'afar wa pili) [4] ili asichanganywe na Abu Jaafar wa kwanza ambaye nia Imamu Baqir (a.s). [5]

Miongoni mwa lakabu za Imamu huyu wa 9 ni; Jawad (Mkarimu) na Ibn al-Ridha (Mwana wa Imamu Ridha). [6] Pia Imamu anatambulikana kupitia lakabu kadhaa kama vile; Taqi (Mchamungu), Zaki (Mtoharifu), Qaaniun (Aliye kinai), Radhiyyun (Aliye Ridhika), Mukhtar (Aliye Chaguliwa), Mutawakkil (Mwenye Kutawakali), [7] Murtadha (Aliye Ridhiwa) na Muntajab (Mteule). [8]


Mukhtasari wa maisha yake

Imamu Jawad (a.s) alizaliwa Madina mnamo mwaka 195 Hijiria. [17] Kuna tofauti kuhusiana siku na mwezi wa kuzaliwa kwake. [18] Vyanzo vingi vinachukulia tukio la kuzaliwa kwake kuwa lilitokea mwezi wa Ramadhani. [19] Badhi ya waandishi wameripoti tukio hilo kutokea ndani ya mwezi 15 Ramadhani, [20] huku wengine wakidai tukio hilo kutokea ndani ya mwezi 19 Ramadhani[21]. Sheikh Tusi ameripoti tukio hilo kutokea ndani ya mwezi 10 Rajab, ripoti hii ameripoti ndani ya kitabu chake kiitwacho Misbahu al-Muttahajad. [22]

Kwa mujibu wa Hadithi iliyosimuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho al-Kafi ni kwamba; kabla ya kuzaliwa kwa Jawadu al-Aimmah, baadhi ya wafuasi wa gurupu la Waqiffiyyah walimshukia Imamu Reza (a.s) juu ya Uimamu wake, shaka hiyo ilitokana na kule yeye kutokuwa na mtoto. [23] Hilo ndilo lililo pelekea Imamu Ridha (a.s) kumsifu Jawadu al-Aimmah baada ya kuzaliwa kwake, na kusema kuwa mtoto huyo ni mwenye baraka nyingi kwa Mashia. [24] Hata hivyo, baada ya kuzaliwa Imamu Jawad, baadhi ya wafuasi wa Waqifiyyah walikanusha kuhusishwa kwake na Imam Ridha (a.s), yaani hawakukubali kuwa yeye ni mwana wa Imamu Ridha (a.s). Wao walidai kwamba; katu Jawadu al-Aimmah hafanani na baba yake. Dhana hiyo iliendelea mpaka walipoletwa watambuzi wa fani ya nasaba, ambao walithibitisha kuwa yeye ni mwana wa Imamu Ridha (a.s). [25]

Hakuna habari tosha katika vyanzo vya kihistoria kuhusiana na maisha ya Imam Jawad (a.s). [26] Hilo linatokana na vikwazo vya kisiasa vya serikali ya Abbas dhidi yake, taqiyyah (kuficha kwa kwa imani yake) pamoja na ufupi wa maisha yake.[27] Yeye aliishi katika mji wa Madina. Kwa mujibu wa ripoti ya Ibnu Baihaq, katika maisha yake yeye alisafiri mara mojakuelekea mji Khorasan -ulioko Iran- kwa ajili ya kumtembelea baba yake [28] Baada ya kushika nafasi ya Uimamu wake, mara kadhaa alisafiri kuelekea Baghdad kupitia wito aliopewa na makhalifa wa Abbas. [29]


Ndoa

Ima mwaka wa 202 [30] au 215 Hijiria [31], Maa'mun Abbasi aliamua kumwoza Imamu Jawad (a.s) binti yake Ummu al-Fadhli. Wengine wanadhani ya kwamba; yawezezakana ndoa hiyo ilfanyaka pale Imamu Jawadi alipokuwa na babake huko Tus, baada ya kwenda mjini humo ka nia ya kumtembelea baba yake, ambapo Maamuni alipochukuwa hatua ya kumwoza binti yake huyo. [32] Kupitia maelezo ya Ibnu Kathiri ambaye ni mwandishi wa historia wa madhehebu ya Sunni, aliyezaliwa mwaka 701 na kufariki 774 Hijira ni kwamba; Khutba ya ndoa baina ya Imamu Jawadi na Binti ya Maa'mun ilisomwa wakati wa uhai wa Imamu Ridha (a.s). Hata hivyo, karamu ya ndoa yao ilifanyika mwaka wa 215 Hijiria katika mji wa Tikrit, Iraq. [34]

Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika vyanzo vya kihistoria, ndoa ya Jawadu al-Aimmah na Ummu al-Fadhli ilifanyika kwa ombi la Maamun. [35] Imedaiwa ya kwamba; lengo la Maa'mun katika ombi hilo, lilikuwa ni kupata nasaba ya kuwa babu wa mtoto kutoka katika kizazi cha bwana Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali (a.s). [36] Kwa mujibu wa riwaya ya Sheikh Mufid katika kitabu chake kiitwacho al-Irshadu; Maamuni alimwoza binti yake Muhammad bin Ali (a.s) kutokana na haiba ya kielimu, sharaf (staha), hekima, na ukamilifu wa akili aliouona kwa Imamu Jawadi, licha ya umri wake mdogo aliokuwa nao. [37] ] Lakini Rasul Jafarian (aliyezaliwa 1343), amabaye ni mtafiti wa historia, anaamini kwamba; ndoa hii ilifanyika kwa nia ya kisiasa. Na mojawapo ya misukumo katika suala hilo ni kwamba; Maamuni alitaka kumdhibiti Imamu Jawad pamoja na wafuasi wake kupitia mahusiano hayo ya ndoa. [38] Au pia yawezekana kuwa alikusudia kufanya hadaa ya kujionyesha kwamba yeye ni mwenye shauku na famili ya bwana Mtume (s.a.w.w), ili aweze kuzuia harakati zao dhidi yake.[39] Kwa mujibu wa ripoti ya Sheikh Mufidu ni kwamba; Ndoa hii ilisababisha malalamiko ya baadhi ya watu wa karibu na Maamuni. Sababu hasa ya lalama hizo zilitokana na kuukhofia ukhalifa usije ukatoka mikononi mwa Bani Abbas kwenda kwa Ma'alawi (Banu Hashim). [40] Imamu Jawad (a.s) katika ndoa yake na Ummu Fadhli, alianisha mahari yake sawa na mahari ya bibi Fatima (a.s), ambapo kiwango cha mahari hayo kilikuwa ni dirhamu 500. [41] Hata hivyo Imamu Jawadi hakupata hata mtoto mmoja kutoka kwa Ummu Fadhli. [42]

Mke mwingine wa Imamu Jawadi (a.s) alikuwa ni Samanah Maghribiyya, [43] ambaye alikuwa kijakazi aliyenunuliwa kwa amri yake. [44] Watoto wote wa Imamu Jawad walitoka kwa Samanah. [45]


Watoto

Kwa mujibu wa maelezo ya riwaya ya Sheikh Mufidu ni kwamba; Imamu Jawad (a.s) alikuwa na watoto wanne walioitwa; Ali, Mussa, Fatima na Imama. [46] Baadhi wanahistoria wamerikodi katika vyanzo vyao mabinti watatu kutoka kwa Imamu Jawadi (a.s), nao ni: Hakimah, Khadijah na Ummu Kulthum. [47] Katika baadhi ya vyanzo vinavyohusiana matukio ya karne ya 14 ya Hijiria, wamewaingiza Ummu Muhammad, Zainabu na Maimuna katika kundi la mabinti wa Imamu Jawadi (a.s). [48] Katika kitabu Muntaha al-Aamaali, kupitia nukuu ya Dhaamin bin Shudqam, imeelezwa ya kwamba; Imamu Jawad (a.s) alikuwa na watoto wanne wa kiume walioitwa: Abu al-Hasan ambaye ni Imamu Ali Naqi (a.s), Abu Ahmad Musa Mubarqa, Hussein, Imran. Na kwa upande wa wanawake alikuwa na mabinti wanne walioitwa: Fatima, Hakimah, Khadijah na Ummu Kulthumu. [49] Baadhi ya watafiti wengine wanakadiria idadi ya watoto wa kiume wa Imamu Jawad (a.s), kuwa ni watoto watatu ambao ni: Imamu Ali Naqi (a.s), Musa Mubarqa naYahya. Na kwa upande wa watoto wa kike, waliwahisabu mabinti watano kuwa ni mabinti wa Imamu Jawadi (a.s), ambao ni: Fatimah, Hakimah, Khadijah, Bahjat na Borayhah. [50]


Kufariki kwake

Imamu Muhammad Taqi (a.s) alitumiwa barua ya wito kutoka utawala wa Abbas mara mbili, ukimtaka awasili Baghdad -kupitia tuhuma mbali bamli-. Safari ya kwanza ilikuwa ni katika zama za utawala wa Maamuni, ambayo haikuchukua muda ndefu sana. [51] Mara ya pili, ilikuwani mwezi 28 Muharram 220 Hijiria, ambapo aliingia Baghdad kupitia wito wa amri ya Muu'tasimu Abbasi. Ulipongia mwezi wa Dhul-Qaidah [52] au kwa riwaya nyingine na Dhul-Hijjah mwaka huo huo, [53] aliuawa kishahidi huko Baghdad. Vyanzo vingi vya rikodo za kihistoria, zimetoa taarifa ya tukio hilo la kifo chake kishahidi, na kusema kuwa tukio lilitokea mwisho mwa mwezi wa Dhu al-Qaida [54]. Pia ni vyema kuewa ya kwamba; katika vyanzo vingine, tarehe ya kifo chake imetajwa kuwa ima ni mwezi 5 Dhul-Hijjah [55] au mwezi 6 Dhul-Hijjah [56] ]. Mwili wake ulizikwa karibu na kaburi la babu yake (Musa bin Jafar) (a.s), kwenye mava ya Maquraish ilioko huko Kadhimeini. [57] Imamu Jawadi, wakati wa kifo chake, alihisabiwa kuwa ndiye imamu aliyeisha maisha mafupi zaidi miongoni mwa Maimamu wa Shia. Yeye alipo uawa kishahidi, alikuwa na kiasi cha umri wa miaka 25 tu. [58]

Baadhi wamesema ya kwamba; sababu ya kifo chake cha kishahidi fitna za Ibn Abi Daud, ambaye alikuwa hakimu wa Baghdad wakati wa utawala wa Mu'utasim. Sababu ya hilo ilikuwa ni kukubaliwa kwa rai ya Imamu kuhusu hukumu ya kifiqhi kuhusiana na kukata mkono wa mwizi, jambo ambalo lilimuaibisha Ibn Abi Daud na idadi kadhaa ya mafaqihi na watumishi wa Mu'utasim. [59]

Kuna maoni tofauti kuhusiana na namna ya kuuawa shahidi kiongozi wa tisa wa Mashia. Katika baadhi ya vyanzo, inasemekana kwamba; Mu'utasim alimpa sumu kupitia katibu mmoja wa mawaziri wake na kummaliza kupitia kifo cha kishahidi. [60] Ila baadhi ya watafiti na wanazuoni, wanaamini ya kwamba; Mu'utasim alimtilia sumu kumtumilia Ummu al-fadhli. [61] Kwa mujibu wa ripoti ya mwanahistoria Masoudi wa karne ya tatu Hijiria, ni kwamba; Mu'utasim na Ja'far bin Maamuni walikuwa na dhamira ya kumuua Muhammad bin Ali (a.s) kwa sababu Jawadu al-Aimmah hakuwa na mtoto kutoka kwa Ummu al-fadhli. Baada ya kifo cha Maamun, Ja'far alimtia vijiti vya mashikio dada yake (Ummu al-fadhli) kwa ajili ya kumpa sumu Muhammad bin Ali. Wawili hao (Ja'afar na dada yake) -kupitia msaada wa Mu'utasim- walizichovya zabibu kwenye sumu na kumlisha Imamu Jawadi (a.s). Umm al-fadhli alijuta baada ya kumtilia sumu Imamu (a.s). Baada ya kitendo chake hicho cha Kishetani, Imamu Jawadi (a.s) akamjulisha ya kwamba Mungu atasibu kwa ugonjwa usiotibika. [62] Kuna riwaya kadhaa zilizoelezea tukio hilo la kuuawa kwa Imamu Jawadi (a.s) kupitia mkono wa Umm al-fadhli.

Kwa mujibu wa riwaya nyingine ni kwamba; Baada ya watu kumpa Mu'utasimu kiapo cha utiifu, aliamua kutuma barua kwa Abdul Malik Zayat, gavana wa Madina, na kumtaka amuamuru Muhammad bin Ali (a.s) kwenda Baghdad yeye pamoja na Umm al-fadhli. Pale Imamu Jawad (a.s) alipoingia Baghdad, Mu'utasim alijifanya kumheshimu na akampelekea zawadi yeye pamoja na Umm al-fadhli. Kulingana na simulizi hii, Mu'utasim alimtumia sharubati ya machungwa kupitia kwa mtumwa wake aliyeitwa Ashnas. Ashnas alipofika kwa Imamu alimwambia Imamu ya kwamba; kabla yako wewe, Khalifa amelinywesha kundi la waheshimiwa sharubati hii, naye anakuamuru nawe pia unywe sharubati hii. Imam akasema: "Nitakunywa usiku" Lakini Ashna alisisitiza kwamba inapaswa kunywa ikiwa bado ni baridi. Hapo Imamu akanywa sharubati hiyo, nayo ikawa ndio sababu ya kuuawa kishahidi. [64]

Sheikh Mufidu (aliyefariki 413 Hijiria) alitilia shaka suala la Imamu kuuawa kishahidi kupitia sumu. Akizungumzia suala hili amesema kwamba; Mimi siwezi kutoa ushahidi juu ya kuuliwa kwake kupitia sumu, kwani hakuna habari hata moja iliyothibiti ushuhuda wake mbele yangu. Mwanazuoni huyu (Sheikh Mufidu) katika kitabu chake kiitwacho Tashihu al-I'itiqad, amesema kibaga unaga ya kwamba; Hakuna njia ya uwezekano itakayowezesha kutupa uhakika juu ya vifo vya kishahidi vya baadhi ya Maimamu kama vile Imamu Jawadi. (a.s) [66] Ila Sayyid Muhammad Sadri (aliyekufa kishahidi mnamo mwaka1377 Shamsia) katika kitabu Tarikhu al-Ghaibah, akitegemea riwaya isemayo: "ما مِنّا إلّا مقتولٌ شهیدٌ" ; Hakuna hata mmoja kati yetu, isipokuwa atakuwa ameuawa kishahidi, [67] amekubaliana na nadharia ya kuuawa shahidi kwa Imamu huyo. [68] Mwanahistoria maarufu Rasul Jafarian, pia naye amekubaliana na thibitisho la kuuawa shahidi kwa Imamu Jawadi (a.s). [69] Sayyid Ja'afar Murtadha 'Aamili (aliyefariki mwaka 1414 Hijiria), ambaye ni mwanahistoria wa Kishia, ameyatabiri maneno ya Sheikh Mufidu kwamba ni maneno ya taqiyyah (yaliozungumzwa kutokana na khofu maalumu). Kwa mujibu wake, Sheikh Mufidu alikuwa ni mkaazi wa Baghdad, na kwa kuzingatia hali iliyokuwapo dhidi ya Mashia mjini humo, ilimfanya yeye asiweze kutaja kwa uwazi rai za Kishia kuhusu kuuawa kishahidi kwa Maimamu (a.s) kupitia mikono ya Bani Abbas. Pia moja ya hoja alizozitaja 'Aamili kuhusiana na maelezo ya Sheikh Mufidu, ni ukosefu wa vyanzo vya kutosha na ugumu wa kupata vyanzo asilia, kulikomfanya Sheikh Mufidu asiweze kufikiwa na ripoti halisi juu suala hilo. [70]

Kipindi cha Uimamu wake

Imam Jawad (]]) alishika nafsi ya Uimamu baada ya kifo cha kishahidi cha Imam Ridha (]]) kilichotokea mnamo mwaka 203 Hijiria. [71] Muda wa Uimamu wake ulikuwa ni miaka kumi na saba, [72] ambayo iliambatana na ukhalifa wa makhalifa wawili wa ukoo wa Bani Abbas, ambo ni Maamuni na Mu'utasim. Takriban miaka yake kumi na tano aliishi katika ukhalifa wa Maamun (kuanzia mwaka198 hadi 218 Hijiria) na miaka miwili alisshi katika ukhalifa wa Mu'utasim (kuanzia mwaka 218 hadi 227 Hijiria.) [73] Baaya ya kifo chake cha kishahidi kilichotokea mnamo mwaka 220 Hijiria, Uimamu ulihamia kwa mwanawe ambaye ni Imamu Hadi (a.s). [74]


Nyaraka kuhusiana na Uimamu wake

Mara kadhaa Imamu Ridhaa (a.s) alikuwa tayari ametangaza Uimamu wa Muhammad bin Ali kwa masahaba zake. Katika kila moja ya vitabu vya al-Kafi, [75] al-Irshadu, [76] A'alamu al-Wara [77] na Bihar al-Anwari, [78] kuna sura na milango makhususi kuhusiana na nukuu na nyaraka juu ya Uimamu wa Muhammad bin Ali (a.s), ambapo kuna masimulizi ya riwaya14 kutoka kitabu cha al-Kafi, 11 kiatia kitabu al-Irshadu, 9 katika kitabu A'alamu al-wara na 26 kutoka katika kitabu Biharu al-Anwari. Moja ya riwaya hizo, ni Hadithi ilionukuliwa na mmoja wa masahaba wa Imamu Ridha (a.s), aliye muuliza kuhusu mrithi atakaye fuatia baada yake. Imamu Ridha (a.s) akijibu swali lake, alimuashiria mwanawe ambaye ni Imamu Jawad (a.s) kwa mkono wake. [79] Pia katika moja ya riwaya zake alijibu kwa kusema “Ni huyu Abu Ja’far (ambaye ni Imamu Jawadi) ndiye mrithi wangu, na yeye ndiye nilie muachia nafasi yangu ya uongozi." [80] Kwa mtazamo wa Kishia, Imamu huteliwa tu kwa tangazo au ibara ya wazi kutoka kwa Imamu aliyetangulia. [81] Yaani, kila Imamu ni lazima amteue Imamu kwa atakaye fuata baada yake kwa njia ya wazi kabisa isio na utata.


Uimamu katika utoto wake na kutangatanga kwa Mashia

Imamu Jawad (a.s) alifikia cheo cha Uimamu tokea alipokuwa na umri wa miaka minane. [82] Kwa mujibu wa maelezo ya Hassan bin Nuubakhtiy ni kwamba; kutokana na umri wake mdogo, suala la uendelevu wa Uimamu lilileta mzozo miongoni mwa Mashia, watu walikuwa wakijiuliza ni nani atakaye shika nafasi ya Uimamu baada ya Imamu Ridha (a.s). Baadhi watu walimfuata Abdullah bin Mussa, ndugu wa Imamu Ridha, Lakini haikuchukua muda wakagundua kuwa yeye hastahiki Uimamu na hatimae wakampa kisogo. [83] Ktika kizaa zaa hicho, baadhi ya watu walikimbilia kwa Ahmad bin Mussa, ndugu mwengine wa Imamu Ridha (a.s) na wengine wakajiunga na kundi la Waaqifiyyah. [84] Hata hivyo, masahaba wengi wa Ali bin Mussa Al-Ridha (a.s) waliamini Uimamu wa mwanawe ambaye ni Imamu Jawad (a.s). [85]

Kulingana na maoni na maelezo ya Nuubakhtiy, sababu hasa ya kutokea kwa khitilafu hizo kulitokana na ile fikra yao ya kwamba; kubalehe ni moja ya sharti za Uimamu. [86] Bila shaka, suala hili pia lilijadiliwa wakati wa uhai wa Imamu Ridha (a.s). Imamu Ridha (a.s), akiwajibu wale waliodadisi na kuazisha utata kuhusiana na udogo wa Jawadi (a.s), aliashiria utume wa Nabi Issa akiwa katika hali ya mtoto na akasema: "Issa alipewa utume hali aikiwa ni mdogo zaidi ya mwanagu mimi." [87]

Imamu Ridha (a.s) akiendelea kujibu hoja juu ya kikwazo ch utoto wa Imamu Jawad (a.s), alitumia vielelezo vya Aya za Qur'an juu ya unabii wa Nabii Yahya aliopewa utume utoto mwake, [88] pia kutamka kwa Nabii Issa hali akiwa mbwelekoni. [89] Pia Imamu Jawad akijibu hoja za wale walizua utata juu suala la umri wake, alikumbusha nafasi ya Nabii Suleiman aliorithi badala ya Nabii Daudi hali akiwa bado ni mdogo. [90] ambapo pale Nabi Daudi alipomtawalisha na kumweka kuwa ni mrithi wa nafasi yake ya uongozi, Nabii Suleiman alikuwa ni mtoto mdogo aliye kuwa akichunga kondoo tu, ila wasomi wa Bani Israeli walikataa suala hilo. [91]


Udadisi wa Mashia na majibu ya Imamu Jawadi (a.s)

Licha ya kuwepo bayana na fafanuzi nyingi za wazi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) juu ya Uimamu wa Jawad al-Aimmah, [ 92] ila bado Mashia wengine walijaribu kumuuliza Imamu Jawadi (a.s) maswali. Lengo hasa la maswali hayo lilikuwa ni kumtahini kwa ajili ya kujiridhirisha na kuondoa wasiwasi waliokuwa nao. [93] Ingawaje hata mtindo huo haukuwa ni kwa ajili yake tu, bali hata Maimamu wengine pia walikabiliwa na aina kama hiyo ya kudadisiwa kimaswali, [94] ila muktadha wa hali yake yeye (udogo wake), ulichochea na kuchangia zaidi kaitika kukabiliwa na changa moto za maswali. [95] Kulingana na maelezo ya Rasuli Jafarian ambaye ni wanahistoria wa Kishia, aliyezaliwa mnamo mwaka 1343 Ahamsia, ni kwamba; Mashia hao walifanya hivyo kutokana na sababu kadhaa, likiwemo suala la taqiyyah yenye nia ya kuhifadhi roho ya Imamu, jambo ambalo Mashia kadhaa walisihiwa kulifanya. [96]

Kinamaanishwa na Rasuli Jafarian ni kwamba: Mashia hao walijariju kuleta utata juu ya Uimamu wa Imamu Jawadi, ili kupoteza dira ya maadui wenye ni ya kuwasaka vuingozi wa Ahlul-Bayt na kuwadhibiti au kuwaua. Vyanzo mbalimbali vya simulizi za Hadithi vimeripoti Maswali ya Mashia pamoja na Majibu yaliyotolewa kutoka kwa Imam Jawad (a.s). [97] Jawabu zake zilipelekea kupata jaha na kukubalika mbele ya Mashia. [98] Katika moja ya riwaya imeelezwa ya kwamba; Moja kati ya makundi ya Mashia kutoka Baghdad pamoja na miji mingine lilitoka mijini mwao kwa ajili ya kuhiji, lilikwenda Madina kumtembelea Imamu Jawadi (a.s) huko Madina. Walipofika Madina walikutana na mjomba wa Imam Jawad, ambaye ni Abdullah Bin Mussa na kumuuliza maswali. Yeye akawa anajibu mswali yao sivyo ndivyo, kundi hilo likashangaa kutokana na jawabu zake, mara Imamu Jawad (a.s) akafika nao wakaibua tena maswali yao na hatimae kuridhika na kutosheka na jawabu za Imam Jawad (a.s). [99]


Mawasiliano yake na Mashia

Imam Jawad (a.s) alikuwa akiwasiliana na Mashia wake kupitia mtandao wa mawakala. Yeye alikuwa na wawakilishi katika ardhi kadhaa za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na: Baghdad, Kufa, Ahwazi, Basra, Hamadani, Qom, Rey, Sistani na Busti (Busti ni mji ndani ya Mkoa wa Sistani). [100] Idadi ya mawakala wake inasemekana kuwa kumi na tatu [102] ambao ni: Ibrahim bin Muhammad Hamadaniy katika mji wa Hamadani [103] na Abu Amru Huza katika maeneo jirani na Basra, [104] Saleh bin Muhammad bin Sahil katika mji wa Qom, yeye alikuwa ni wakala wake katika kushughulikia mali za waqfu. [115] Zakaria bi Adam Qummiy, [106] Abul Azizi bin Muhtadi Ash-'ari Qummiy, [107] Safwani bin Yahya, [108] Ali bin Mahziyar [109] na Yahya bin Abi Imrani [110]. Hao ni miongoni mwa mawakala wa Imamu Jawadi (a.s). Mwandishi wa kitabu Sazemane Wikalat, akinukuu kupitia baadhi ya vilelezo, amewataja Muhammad bin Faraj Rokhaji na Abu Hashim Jafari kama ni miongoni mwa mawakala wake wa Imamu (a.s). [111] Ahmad bin Muhammad Siyari pia naye alidai kuwa alikuwa na wakala, Lakini licha ya Imamu kupinga madai yake, pia aliwataka Mashia wasipeleke dhamana (zaka na khumsi) za Wailamu mikononi mwake. [112] Ayatullah Khamenei, katika uchambuzi wake, anazingatia uundwaji wa asasi zilizoshikamana na maandalizi ya kuelekea katika mfumo wa Imam Mahdi (a.s) kuingia mafichoni, aliashiria kuwa; mipango hiyo iliandaliwa na Imam Jawad (a.s). Ayatullahi Khamenei anasema kwamba; mipango hiyo Ilikuwa ni kitu kinacho watia khofu sana makahlifa na viongozi wa wakati huo.[113]

Inasemekana kwamba; Imam Jawad (a.s) alitumia shirika la mawakala kuwasiliana na Mashia wake kwa sababu mbili:

  1. Kuotokana na kwamba yeye alikuwa chini ya udhibiti wa chombo tawala.
  2. Kutokana na dhamira na madhumuni ya kuweka misingi madhubuti kwa ajili ya kipindi kijacho cha kughibu kwa Imamu Mahdi (a.s) na kuingia mafichoni. [114]

Bila shaka kuna tofauti kubwa baina ya kipindi ambacho wanajamii itakuwa na uwezo wa kuonana na kiongozi wao, na kipindi cha kughibu (kuingia mafichoni) kwa kiongozi huyo. Hivyo basi kulihitajika maandalizi maalumu kwa ajili ya kuilinda jamii katika kipindi cha kughibu kwa Imamu Mahdi (a.s). Kiongozi wa tisa wa Mashia pia alikuwa na kawaida ya kukutana na kuzungumza na Mashia wakati wa Hajj. Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba; safari ya Imam Ridha (a.s) ya kuelekea Khurasani ilipelekea kupanuka kwa mahusiano baina ya Mashia na Maimamu wao. [115] Kwahiyo, Mashia kutoka Khorasan, Rey, Busti na Sajistani walikuja kumtembelea Imamu Jawadi wakati wa msimu wa Hija. [116]

Mashia pia walikuwa wakiwasiliana na Jawadi al-Aimma kupitia barua. Mara nyingi katika barua zao, waliuliza maswali yalihusiana na masuala ya kifiqhi, na Imam alikuwa akiwajibu maswali yao kulingana na kuktadha wa maswali hayo. [117] Katika ensaiklopidia ya al-Imam al-Jawad, kuna orodha kubwa kuhusiana na barua baina ya Imau na wafuasi wake. Ukiachana na barua walizokuwa wakiandikiana baina ya baba (Imamu Jawadi) na mwana (mtoto wa Imamu Jawadi), ensaiklopidia imeorodhesha majina ya watu 63 ambao Imamu alikuwa na mawasiliano nao kwa njia ya barua. [118] Baadhi ya barua hizo ziliandikwa kwa ajili ya kujibu kundi fulani la Mashia. [119]


Mgongano na madhehebu mengine

Kulingana na maswali ya Mashia na majibu ya Imamu Jawad (a.s.) yaliyonukuliwa katika vyanzo vya Shia, imebainika ya kwamba; wakati wa Uimamu wa Imamu Jawadi (a.s), kulikuwa na kadhaa yalikuwa na harakati za kidini ndani ya zake. Miongoni mwa madhehebu yalio jishughulisha na harakati hizo za kini ni; madhehebu ya Ahlul-Hadith, Waaqifiyyah, Zaidiyyah na Ghulat. [120] Kwa mujibu wa nukuu za Hadithi kuhusiana na hali iliyopo wakati wa Imamu Jawadi (a.s), ianonesha ya kwamba; mijadala yenye kutia shaka na masuala tata iliyoibuliwa na miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Ahlul-Hadithi, ilipelekea baadhi ya Mashia kupata shaka juu ya tauhudi ya Mwenyezi Mungu kuokana na dhana ya Mungu kuwa na kiwiliwili. Ukiachana na jitihada za Imamu Jawadi (a.s) za kujibu kwa kutoa bayana dhidi ya nadharia ya Mungu kuwa na mwili, pia aliwakataza Mashia kusali nyuma ya wale wanaoamini kwa Mungu ana mwili. Kwa upande mwingine, pia Imamu Jawadi (a.s) alikataza kuwapa zaka watu hao. [121] Yeye akimjibu Abu Hashim Ja'afariy aliuliza, kuhudu tafsiri ya Aya isemayo: "لا تُدْرِکهُ الْأَبْصارُ وَ هُوَ یدْرِک الْأَبْصار" ; "Macho hayamfikii (hayamwoni), ila yeye (Mungu) ni mwenye kuyaona macho hayo" [122] Kupia Aya hii Imamu Jawadi (a.s) aliirudi na kuibatilisha dhana ya imani juu ya uwepo wa Mungu mwenye mwili na madai ya uwezekano wa kumuona Mungu. Akijibu hoja ya dhana hizo alisema: Uoni wa kiakili ni wenye nguvu zaidi ukilinganisha na uoni wa macho haya mawili, kwa sababu uoni wa kiakili unaweza kujenga taswira ya vitu ambavo macho bado hayajaviona. Ila licha ya nguvu hizo zilizopo kwenye macho ya kiakili, katu akili haina uwezo wa kumuona Mungu au kujenga taswira yake. Basi yawezaje macho yako mawili dhaifu kumwona Mungu? [123]

Kuna riwaya iliyoripitiwa kutoka kwa Jawad (a.s) akishutumu kundi la Waaqifiyyah. [124] Yeye katika riwaya hiyo, makundi ya Zaidiyyah na Waaqifiyyah aliyaweka daraja moja na kundi Manawasib (Wanaowachukia Alhlu al-Bait). [125] Imamu jawadi kuhusiana na Aya isemayo: "وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ" ; "Siku hiyo nyuso za waovu zitatahayari na kuwa na khushuu hali zikiwa zimepata tabu katika kutenda matendo yake duniani." Alisema: Aya hii iliteremshwa juu yao, kutoka na juhudi zao za kutenda mema, [26] hali ya kwamba jitihada zao ni bure tu, na hazitawaa kitu. [127] Vile vile akawakataza masahaba zake kusali nyuma ya Waaqifiyyah.[128]

Imamu Jawad pia alikabiliana na imani za Maghaliyan za kipindi hicho na alijitahidi kuwaweka mbali Mashia wake na imani za Maghulati [129] Yeye alionekana kuwalaani baadhi ya wakuu wa Maghulati, kama vile Abu al-Khattab na wafuasi wake. Vile vile aliwalaani wanao acha au kusitasita katika kumlaani Abul Khattab. [130] Aliwatambulisha baadhi ya watu kama; Abu al- Ghamar, Jafar bin Waqidi na Hashim bin Abi Hashim kuwa ni wafuasi wa Abu al-Khattab, na akasema kwamba watu hawa wanawanyonya watu kupitia jina letu (Ahlul-Bayt). [131] Kwa mujibu wa riwaya iliopo katika kitabu kiitwacho Rijalu al-Kashi ni kwamba; Kwa maoni Imamu ilikuwa inajuzu kuwaua Maghulati walili maarufu, ambao ni: Abu al-Samhari na Ibnu Abi Zarqaa, na alisema sababu ya hukumu hiyo kosa lao la kuwapotosha Waislamu wa madhehebu ya Shia. [132]

Akizungumza na Muhammad bin Sinan, alikanusha madai ya Mufawwidha, yasemayo kwamba; uumbaji na mipango ya uendeshaji wa dunia imekabidhiwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Maimamu (a.s). Yeye moja kwa moja suala la Maimamu kupewa uwakala juu ya juu ya fatwa za kisheria aliliegemeza kwenye matakwa ya Mungu, na kaseme yeyote yule atakayevuka zaidi ya hapo, atakuwa ametoka nje ya Uislamu. Aliendelea kusema; pia yeyote atakaye kanusha uwakala huo basi itabomokadini yake, na atakaye kubaliana na uwakala wao, huyo atakuwa amefungamana na haki. [133]


Riwaya na mijadala

Kwa mujibu wa maelezo ya Azizullah Ataaridiy, takriban kuna Hadithi 250 zilizo simuliwa kutoka kwa Imamu Jawadi (a.s) kuhusisna na masuala ya fiqhi, tafsiri na imani. [135] Imeelezwa ya kwamba; Uchache wa riwaya zilizonukuliwa kutoka kwake ukilinganisha na maimamu wengine kutokana na kule yeye kuwa chini ya udhibiti wa chombo tawala na ufupi wa umri wake. [136]

Siyyid Ibnu Taawus katika kitabu chake Mohaj al-Da'awaat, amenukuu kielelezo cha hirizi kutoka kwake ambayo ni kinga kwa ajili ya kuepukana na shari za Maamuni Abbasi. [137] Hirizi hiyo ilikuwa na ibara ifuatayo: "يَا نُورُ يَا بُرْهَانُ يَا مُبِينُ يَا مُنِيرُ يَا رَبِّ اكْفِنِي الشُّرُورَ وَ آفَاتِ الدُّهُورِ وَ أَسْأَلُكَ النَّجَاةَ يَوْمَ يُنْفَخُ فِي الصُّورِ" ; "Ewe Nuru, ewe hoja na Kielelezo, ewe Bayana, ewe mwongozaji (ewe MMurikaji), ewe Mola wangu Mlezi niepushe na shari na madhara ya dahari na ninakuomba uokovo." [138] Ni jambo la kawaida na maarufu miongoni mwa Mashia kutembea na hirizi ya Imamu Jawadi (a.s), ambapo ni sitiari itayotumika katika kuashira kutobandukana na kiti au mtu fulani. Kwa mfano kusemwa "fulani yuko na fulani kila wakati, kama vile hirizi ya Imamu Jawadi". [139]

Imamu Muhammad Taqi (Imamu Jawadi) (a.s) wakati wa Uimamu wake, mara kadhaa alijadili na baadhi ya mafaqihi wa kasir ya utawala wa Abbas. Ripoti za kihistoria zinaonyesha kuwa; baadhi ya midahalo hiyo ilifanywa kwa ombi la wapambe wa Maamuni na Mu'utasim kwa lengo la kumjaribu na kumtahini kiongozi wa tisa wa Mashia. Matokeo ya mijadala hiyo yalisababisha mshangao na kuvutika kwa watu waliohudhuria. [140] Vyazo vya kidini vimeripoti midahalo tisa kutoka kwa Imamu Jawadi (a.s). Monni miongoni mwa mijadala hiyo ilikuwa na baina yake na Yahya bin Aktham na mmoja ni baina yake na Ahmed bin Abi Daudi, ambaye ni mkuu wa makadhi wa Baghdad. Pia, kuna majadiliano yalionukuliwa baina yake na watu wengine kama vile; Abdullah bin Mussa, Abu Hashim Jafari, Abdul Adhim Hassaniy na Mu'uatasim. Mada ya mijadala hiyo ilikuwa ni masuala ya kifiqhi yanayohusiana na; Hija, talaka, hukumu ya wizi na masuala mengine kama vile sifa za masahaba wa Imamu wa kumi na mbili, fadhila zinazonasibishwa kwa Abu Bakar na Omar, na majina na sifa za Mwenyezi Mungu. [141]


Mjadala kuhusu fiqhi

Moja ya mijadala muhimu sana ya Imamu Muhammad Taqi (a.s) ambayo ilifanyika wakati wa Maamuni Abbasi huko Baghdad ulikuwa ni mjadala baina yake na Yahya Ibn Aktham, faqihi kutoka kasri ya Abbas. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya Kishia, sababu ya mjadala huu ilikuwa ni pingamizi ya baadhi viongozi kutoka serikali ya Bani Abbas katika kupinga pendekezo la Maamuni la kumtaka Imamu Jawadi kumuoa Ummu al-Fadhli. Ili kuthibitisha usahihi wa uamuzi wake, Maamuni alipendekeza maafisa hao wa serikali yake waijaribu Jawadu al-Aimmah (a.s). Viongozi hao walikubaliana na wazo hilo na wakapanga kikao cha mjadala ili kumjaribu Imamu huyo. Katika mjadala huo, Yahya kwanza aliibua suala la kifiqhi kuhusu hujaji ambaye aliwinda mnyama hali ya kuwa amevaa ihramu. Imamu Jawadi (a.s) aliibua vipengele tata mbalimbali kupitia swali hilo, baada ya hapo akamuuliza Yahya bin Aktham ni kipengele gani alichomaanisha. Yahya bin Aktham akawa hoi na hajui la kusema katika kujibu swali la Imamu. Kisha Imamu Jawadi (a.s) akajibu tata zote kupitia sura tofauti kuhusiana na swali lake. Baada ya kusikia jibu la Imamu, watumishi na wanazuoni wa Abbas waliukubali utaalamu wake katika elimu ya sheria. Inasemekana kwamba; baada ya mjadala huo, Maamun alisema: "Namshukuru Mungu kwa baraka hii kwamba kile nilichokipanga kimetia kama nilivyo kitarajia. [142] Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, baada ya majibu ya Imamu Jawad (a.s) katika mjadala huo na Yahya bin Aktham, Maamuni aliwashutumu watu waliomzunguka na waliokuwepo katika mkusanyiko huo. Akasema na kubainisha akisema ya kwamba: jaha ya familia hii ni dhahiri kwa kila mtu na umri wake haupuguzi kitu katika ukamilifu na jaha yake. Ameongeza kwa kusema; "Mtume (s.a.w.w) alianza malinganio yake kwa kumlingania Imamu Ali (a.s) hali akiwa bado hajafikisha umri wa miaka kumi na akaukubaliana Uislamu wake. [143] Kulingana na moja ya riwaya kutoka katika kitabu Biharu al-Anwari ni kwamba; Kambala ya mjadala huu, Maamuni aliwambia watu walio karibu naye kwamba: familia hii inatofautiana na familia nyingine, ila kwa kuwa wao waliendelea kubishana naye, basi pakatoka uamuzi wa kumtahini. [144]


Mjadala kuhusu makhalifa

Kwa mujibu wa vyanzo vya Hadithi vya Shia, Imamu Muhammad Taqi (a.s) alijadiliana na Yahya Ibn Aktham kuhusu nafasi na ubora wa Abu Bakar na Omar katika moja ya mikutano uliohudhuriwa na Maamun na idadi kadhaa ya mafaqihi na maafisa wa serikali. Yahya akamwelekezea maneno Imamu Jawadi akisema: Jibril alikuja na ujumbe kotoka kwa Mola wake na akamtaka Mtume wa Mungu kwa niaba ya Mungu, amuulize Abu Bakar, je, ameridhika na mimi (Mungu)? Naye akajibu: "mimi nimeridhika naye". Imamu akajibu: mimi sikanushi daraja ya Abu Bakar; Lakini mwenye kuisimulia riwaya hii azingatie Hadithi nyingine zilitokazo kwa Mtume (s.a.w.w), na imepokewa ya kwamba, Mtume (s.a.w.w) alisema itapokujieni Hadithi kutoka kwangu, iwasilisheni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah zangu, Ikiwa anakubaliana nayo, basi ikubalini na ikiwa sio hivyo, msiikubali; Kwa sababu kutakuwa na waongo na wazushi wengi wa Hadithi. Kisha Imamu akasema kwamba: Hadithi hii haikubaliani na Qur’an; Kwa sababu Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema: "وَنَحْنُ أَقْرَ‌بُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِ‌يدِ" ; "Na sisi tuko karibu naye zaidi kuliko mshipa wa uhai ulioko shingoni mwake. [145] Je, Mwenyezi Mungu hakujua kama Abu Bakar ameridhika au hakutosheka kiasi ya kwamba awe na haja ya kuuliza? [146]

Baada ya hapo, Yahya akauliza kuhusu riwaya isemayo: "Mfano wa Abu Bakar na Omar duniani ni kama Jibril na Mikaili mbinguni." Jawadu al-Aimma akajibu kuwa; maudhui ya simulizi ya riwaya hii si sahihi; Kwa sababu Jibril na Mikaili wamemtumikia Mungu siku zote na hawakuwahi kutenda dhambi; Wakati Abu Bakar na Omar walikuwa ni washirikina kwa miaka mingi kabla ya kusilimu kwao. [147]


Hukumu ya kukatwa mwizi mkono

Katika zama ambazo Imamu (a.s) alikuwa akiishi mjini Baghdadi, kulitokea khitilafu miongoni mwa wanazoni wa madhehebu ya Sinni kuhusiana na kiwango cha mkono wa mwizi kinachostahiki kukatwa kisheria. Baadhi yao walisema akatwe kuanzia kiganjani, huku wengine wakidai kukatwa kwenye vifundo viwili vya mkono. Katika hali hiyo, Muutasim akamtaka Imamu Jawadi a.s) atoe maoni yake kuhusiana na suala hilo. Imamu Jawadi (a.s) akamtaka udhuru na ruhusa ya ili asimuingize kwenye utata wao juu ya suala hilo. Muutasim alisisitia msimamo wake, Imamu naye akamjibu kwa kusema: “Ni vidole tu ndivyo vinavyotakiwa kukatwa, na sehemu nyengine za mkono zinatakiwa kubaki kama zilivyo. Hoja ya Imamu kuhusu hukumu hiyo, ilikuwa ni kielelezo cha Aya ya Qur’an kisemacho: “وَ أَنَّ الْمَساجِدَ لِله فَلا تَدْعُوا مَعَ اللهِ أَحَداً” ; “Kwa hakika misiskiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimwabudu mwenza yeyote yule pamoja na Mwenyezi Mungu” [148] Muutasim akaridhika na jawabu hiyo, kisha akaamuru mwizi akatwe vidole vyake. [49] Yasemekana ya kwamba; suala hilo lilipelewa shani ya Imamu kukuwa miongoni mwa jamii. [150]


Shani (sifa) na karama

Kuna karama tofauti zilizonasibishwa na Imamu Jawadi (a.s) kutoka katika vyanzo vya Kishia. Moja ya karama zilizosajiliwa na vyanzo hivyo ni; kuzungumza akiwa mchanga, kusafiri bila ya usafiri, ambapo alisafiri kimiujiza kutoka Madina hadi Khorasani nchini Iran. Karama nyingine ni kutakabaliwa dua zake bila kuchelewa na kutoa habari kuhusiana na siri za watu pamoja na mambo yajayo. [155]

Muhaddithu Qommiy alisimulia kutoka kwa Qutubu Rawandi na Muhammad bin Maimon ya kwamba: “Wakati Imamu Rdha (a.s) alikuwa bado hajahamia Khorasan, alifunga safari kwenda Makka nami nikiwa pamoja naye. Nilipotaka kurudi, nilimwambia Imamu ya kwamba: Nataka kwenda Madina, Naomba uniandikie barua kwa ajili ya Mohammad Taqi (Iamu Jawadi) ili nimpelekee. Imamu Ridha akaniandikia barua hiyo name nkaenda nayo Madina. Wakati huo macho yangu yalikuwa yamepofuka, baada ya kufaka nyumbani kwao huko Madina, Mufaq ambaye ni mtumishi wa Imamu Ridha, alikuwa nyumabani hapo kwa ajili ya kutoa kumhuduma akamleta Imam Jawad (a.s), hali akiwa mbwelekoni (yaani alikuwa ni mtoto mchanga) nami nikampa barua ile -huyo mtoto mchanga-naye akamwamuru Mawafaq, aifungue naye akaifungua. Kisha akasema: Ewe Muhammad, hali ya macho yako ikoje? Nikasema, Ewe Ibnu Rasulullah, macho yangu yamepoteza uwezo wa kuona. Baada kumwambia hivyo, aliyapangusa macho yangu, na kwa mkono wake wenye baraka, macho yangu yakapona, na nikaendelea kuona kama kawaida.” [156]

Pia imesimuliwa ya kwamba: wakati wa safari ya Imamu Jawadi (a.s) ya kurejea kutoka Baghdad kwenda Madinah, kundi la watu fulani lilimshindikiza hadi nje ya mji. Jua lilipotua, Imamu Jawadi (a.s) alitawadha na kusali katika ua wa msikiti karibu na mkunazi ambao haukuzaa matunda hadi wakati huo. Baada ya kumaliza sala yake, watu waliuona mti huo tayari umushazaa matunda. Watu hao alishangaa na walipokula matunda ya mti huo, waliyakuta kuwa ni matamu yasio na mbegu ndani yake. Pia imepokewa kutoka kwa Sheikh Mufidu kwamba; Baada ya kupita miaka kadhaa, Sheikh Mufidu aliuona mti huo na akala matunda yake. [157]

Masahaba

Makala Asili: Orodha ya Masahaba wa Imamu Jawad (a.s)

Sheikh Tusi amewataja watu wapatao 115 kuwa ni miongoni mwa Masahaba wa Jawadu al-Aimma. [158] Qurashiy katika kitabu Hayatu al-Imam Muhammad al-Jawad (a.s), ameorodhesha idadi ya masahaba 132 [159] na Abdul Hussein Shabistariy katika kitabu "Subulu al- Rashad Ilaa Ashabi al-Imami al-Jawad", amerikodi idadi ya watu 193[160] alio watambulisha kama ni masahaba wa kiongozi wa tisa wa Mashia. Attardiy katika kitabu chake "Musnad al-Imamu Al-Jawad", amezingatia idadi ya wapokezi wake (masahaba zake) kuwa 121. [161] Baadhi ya Masahaba wa Imamu al-Jawad pia walikuwa ni masahaba wa Imamu Ridha (a.s) [162] pamoja na Imamu Hadi (a.s) na kupokea Hadithi kutoka kwao. [163] Pia walikuwepo wapokeza wa Miongoni mwa wapokezi wa Muhammad Taqi (Imamu Jawadi) (a.s) walikuwepo wapokezi ambao walikuwa ni wafuasi wa madhehebu nyinginezo wakiwemo Masunni. [164] Imeelezwa ya kwamba; Idadi ya wapokezi hao wasiokuwa Mashia, ni watu 10. [165]

Ahmad bin Abi Nasri Bizanti na Safwan bin Yahya, Abdul Azim Hosaaniy, Hassan bin Saeed Ahwazi, Zakaria bin Adam, Ahmad bin Muhammad bin Isa Ash'ari, Ahmad bin Muhammad Barqi na Abu Hashim Jafari wote kwa jumla walikuwa ni miongoni mwa masahaba wa kiongozi wa tisa wa Mashia. [166]


Jaha na hadhi ya Imamu Jawadi mbele ya Masunni

Wanazuoni wa Kisunni wanamheshimu sana kiongozi wa tisa wa Mashia na wanamtambua kama ni mwanachuoni wa kidini. [167] Baadhi yao wamemsifu na kumuhisabu kuwa ni mmwanazuoni mahiri zaidi kielimu. [178] Baadhi yao wameuadhimu uwezo wake wa kielimu aliokuwa nao, na wamesema ya kwamba; kule kuvutiwa naye Maamuni Abbasi kunatokana na wasifu wake wa kielimu na kiroho aliokuwa nao tokea zama za utoto wake. [169] ] Pia wamezungumzia sifa nyingine kadhaa za ubora wa Muhammad bin Ali (a.s), nazo ni kama vile; uchamungu, kutosheka na ukarimu. [170] Kwa mfano Shamsu al-Ddini Dhahabi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni maarufu wa Kisunni wa fani ya Hadithi wa karne ya nane Hijiria, [171] yeye pamoja na Ibnu Taimiyyah, [172] wamesema ya kwamba; Kule yeye kupewa lakabu ya Jawadi, kunatokana na umashuhuri wa sifa ya ukarimu aliyosifika nayo. Jahidh Othman, mwanatheolojia wa Mu'tazili na mwandishi wa karne ya pili na ya tatu Hijirria, pia alimtambulisha Muhammad bin Ali (a.s) kama ni mwanazuoni, mtawa (aliye kinai), mchamungu, shujaa, mwenye kusamehe na msafi. [173] Muhammad bin Talha Shafi'i, mmoja wa wanazuoni wa madhdhebu ya Shafi'i wa karne ya saba Hijiria, ameandika kuhusu Imamu Jawadi (a.s) akisema: "Hata kama alikuwa ni mdogo kiumri, ila alikuwa na kijaha, kihadhi na kidaraja, jina lake na sifa zilikuwa ni za juu kabisa." [174]


Maombi kwa jaha ya Imamu Jawadi (a.s)

Kupitia mapendekezo ya baadhi ya wanachuoni wa Kishia, baadhi ya Mashia wanamwelekea Imamu Jawad (a.s) katika maombi yao ili kupanua riziki na kutafuta afueni maishani mwao, wao wamempa jina la Bab al-Hawaij (mlango ufumbuzi wa haja). Miongozi mwa mapendekezo juu ya suala hilo, ni riwaya iliyo nukuliwa kutoka kwa Majlisi wa pili ambaye ni Muhammad Baqir bin Muhammad Taqi Majlisi, yeye amenukuu riwaya hiyo kutoka kwa Abu al-wafaa Shirazi, aliye dai ya kwamba alimona Mtume (s.a.w.w) ndotoni mwake, na alimshauri katika ndoto yake hiyo amwelekee Imamu Jawad (a.s) katika mahitaji yake ya kidunia. [175]

Kwa mujibu wa riwaya iliyo simuliwa na Dawood Sirafi kutoka kwa Imamu Hadi (a.s), ni kwamba; kuzuru kaburi la Jawadu al-Aimmah ni amali yenye thawabu nyingi mno. (a.s) Pia Ibrahimu bin 'Uqba katika moja ya zake kwa Hadi (a.s) aliyo mwandikia akimuuliza kuhusiana na suala la ziara (tungo makhususi zenye ibara maalumu za sala na salamu) za Maimamu watatu, ambao ni Imamu Hussein, Imamu Kadhim na Imam Jawad (a.s). Imamu Hadi (a.s) akijibu barua yake hiyo, kwanza aliitanguliza ziara ya Imamu Hussein (a.s), na akasema kuwa hiyo ndiyo ziara bora na yenye kipaumbele zaidi, pia aliengeza kwa kusema ya kwamba; ziara hiyo ni kamilifu zaidi na ina thawabu nyingi zaidi kulinganisha na ziara za Maimamu wengine wote. [177] Makaburi mawili ya Imamu Jawad na Imamu Kadhim (a.s) yaliopo mjini Baghdad, ni moja ya sehemu tukufu mbele ya Waislamu, hasa Mashia. Mashi wana kawaida ya kutembelea kaburi la Imamu Jawadi (a.s) lililoko Kadhimeini. Wao huomba haja zao kupitia jaha yake na husoma ziara (tungo za sala na salamu) katika kaburi la mtukufu huyo. Katika kumbukumbu ya maombolezo ya kuuawa kishahidi kwa Jawad al-Aimma, Mashia hujiunga mikusanyiko ya maombolezo, kusoma mashairi ya huzuni na kupiga vifua vyao, pia humwomba Mola wao kupitia jaha ya Imamu wao huyo. [178]

Kisomo maalum pindi unapomzuru Imam Jawadi (a.s)

السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا أَبَا جَعْفَرٍ مُحَمَّدَ بْنَ عَلِيٍّ الْبِرَّ التَّقِيَّ الْإِمَامَ الْوَفِيَّ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الرَّضِيُّ الزَّكِيُّ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا وَلِيَّ اللهِ‏ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا نَجِيَّ اللهِ‏ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا سَفِيرَ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا سِرَّ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا ضِيَاءَ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا سَنَاءَ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا كَلِمَةَ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا رَحْمَةَ اللهِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النُّورُ السَّاطِعُ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْبَدْرُ الطَّالِعُ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الطَّيِّبُ ابْنُ الطَّيِّبِينَ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الطَّاهِرُ ابْنُ الطَّاهِرِينَ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْآيَةُ الْعُظْمَى السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْحُجَّةُ الْكُبْرَى السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْمُطَهَّرُ مِنَ الزَّلَّاتِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْمُنَزَّهُ عَنِ الْمُعْضِلَاتِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الْعَلِيُّ عَنْ نَقْصِ الْأَوْصَافِ السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا الرَّضِيُّ عِنْدَ الْأَشْرَافِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا عَمُودَ الدِّينِ السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا ابْنَ الْأَئِمَّةِ الْمَعْصُومِينَ أَشْهَدُ أَنَّكَ وَلِيُّ اللهِ وَ حُجَّتُهُ فِي أَرْضِهِ وَ أَنَّكَ جَنْبُ اللهِ وَ خِيَرَةُ اللهِ‏ وَ مُسْتَوْدَعُ عِلْمِ اللهِ وَ عِلْمِ الْأَنْبِيَاءِ وَ رُكْنُ الْإِيمَانِ وَ تَرْجُمَانُ الْقُرْآنِ وَ أَشْهَدُ أَنَّ مَنِ اتَّبَعَكَ عَلَى الْحَقِّ وَ الْهُدَى وَ أَنَّ مَنْ أَنْكَرَكَ وَ نَصَبَ لَكَ الْعَدَاوَةَ عَلَى الضَّلَالَةِ وَ الرَّدَى أَبْرَأُ إِلَى اللهِ وَ إِلَيْكَ مِنْهُمْ فِي الدُّنْيَا وَ الْآخِرَةِ وَ السَّلَامُ عَلَيْكَ مَا بَقِيتُ وَ بَقِيَ اللَّيْلُ وَ النَّهَارُ وَ رَحْمَةُ اللهِ وَ بَرَكَاتُهُ



Amani iwe juu yako, ewe Abu Ja`afar Muhammad bin Ali, Imamu mwema na mchamungu, mshikamanifu, amani iwe juu yako ewe mtakatifu uliyemridhia Mungu, amani iwe juu yako ewe juu yako ewe walii (khalifa) wa Mungu, amani iwe juu yako ewe msiri wa Mungu, amani iwe juu yako ewe mwakilishi wa Mungu, amani iwe juu yako ewe siri ya Mungu, amani iwe juu yako ewe nuru ya Mungu, amani iwe juu yako ewe mwanga wa Mungu (mwenye hadhi ya juu mbele ya Mungu) amani iwe juu yako ewe neno la Mungu, amani iwe juu yako ewe rehema ya Mungu, amani iwe juu yako ewe nuru ing’aayo, amani iwe juu yako ewe mwezi ulio timia, amani iwe juu yako ewe mwana na mwema wa watu wema, amani iwe juu yako ewe mwana wa wasafi (kizazi cha Mtume (s.a.w.w)), amani iwe juu yako ewe ishara kuu, amani iwe juu yako ewe hoja kuu (kielelezo kikuu), amani iwe juu yako ewe uliye takaswa na mitelezo, amani iwe juu yako ewe uliye wekwa kando na miyumboyumbo, amani iwe juu yako ewe uliye juu zaidi ya upungufu wa sifa (uliye kiuka mapungufu ya sifa na maelezo), amani iwe juu yako ewe unayependeza (uliyekubalika) mbele ya watukufu, amani iwe juu yako ewe nguzo ya dini amani iwe juu yako ewe mwana wa Maimamu Watakatifu. Ninashuhudia ya kwamba wewe ni walii (kahlifa) wa Mwenyezi Mungu na hoja yake (mwakilishi na kielelezo chake kamili) katika ardhi yake. Ninashuhudia kwamba wewe uko karibu na Mwenyezi Mungu, na ni mbora wa (mbele ya) Mwenyezi Mungu. Ninashuhudia kwamba wewe ni hazina ya elimu ya Mwenyezi Mungu na manabii. Ninashuhudia kwamba wewe ni nguzo ya imani na mfasiri wa Qur'an. Ninashuhudia ya kwamba mwenye kukufuata wewe atakuwa kwenye haki na uongofu, na kwamba atakaye kukanusha na kukufanyia uadui atakuwa kwenye upotofu na udhalili. Mbele ya Mungu na mbele yako mimi ninajitenga na watu hao dunia na Akhera, na naomba amani iwe juu yenu katika kipindi chote cha maisha yangu, na kwa kipindi chote cha dawamu ya usiku na mchana, na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu.. [26]


Kisha busu kaburi na sema:

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ أَهْلِ بَيْتِهِ وَ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدِ بْنِ عَلِيٍّ الزَّكِيِّ التَّقِيِّ وَ الْبَرِّ الْوَفِيِّ وَ الْمُهَذَّبِ النَّقِيِّ هَادِي الْأُمَّةِ وَ وَارِثِ الْأَئِمَّةِ وَ خَازِنِ الرَّحْمَةِ وَ يَنْبُوعِ الْحِكْمَةِ وَ قَائِدِ الْبَرَكَةِ وَ صَاحِبِ الِاجْتِهَادِ وَ الطَّاعَةِ وَ وَاحِدِ الْأَوْصِيَاءِ فِي الْإِخْلَاصِ وَ الْعِبَادَةِ وَ حُجَّتِكَ الْعُلْيَا وَ مَثَلِكَ الْأَعْلَى وَ كَلِمَتِكَ الْحُسْنَى الدَّاعِي إِلَيْكَ وَ الدَّالِّ عَلَيْكَ الَّذِي نَصَبْتَهُ عَلَماً لِعِبَادِكَ وَ مُتَرْجِماً لِكِتَابِكَ وَ صَادِعاً بِأَمْرِكَ وَ نَاصِراً لِدِينِكَ وَ حُجَّةً عَلَى خَلْقِكَ وَ نُوراً تُخْرَقُ بِهِ الظُّلَمُ وَ قُدْوَةً تُدْرَكُ بِهِ الْهِدَايَةُ وَ شَفِيعاً تُنَالُ بِهِ الْجَنَّةُ اللَّهُمَّ وَ كَمَا أَخَذَ فِي خُشُوعِهِ لَكَ حَظَّهُ وَ اسْتَوْفَى مِنْ خَشْيَتِكَ نَصِيبَهُ فَصَلِّ عَلَيْهِ أَضْعَافَ مَا صَلَّيْتَ عَلَى وَلِيٍّ ارْتَضَيْتَ طَاعَتَهُ وَ قَبِلْتَ خِدْمَتَهُ وَ بَلِّغْهُ مِنَّا تَحِيَّةً وَ سَلَاماً وَ آتِنَا فِي مُوَالاتِهِ مِنْ لَدُنْكَ فَضْلًا وَ إِحْسَاناً وَ مَغْفِرَةً وَ رِضْوَاناً إِنَّكَ ذُو الْمَنِّ الْقَدِيمِ وَ الصَّفْحِ الْجَمِيلِ الْجَسِيمِ بِرَحْمَتِكَ يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.(مجلسی، زاد المعاد، ۱۴۲۳ق، ص۵۳۶-۵۳۷)



Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu Mtume Muhammad na Aali zake, na usalie Muhammad bin Ali alie msafi na mchamungu, na mwema mshikamanifu, na mstaarabu nadhifu, mwongozaji wa umma, mrithi wa Maimamu, hazina (ghala) ya rehema, chemchemi ya hekima, kiongozi wa baraka, mwenye bidii (katika uchamungu) na utiifu (mwenye taa), mrithi pekee katika ikhlasi (upwekeshaji) na kuabudu (mrithi pekee aliyerithi nafasi ya upwekesha halisi kutoka kwa wapwekeshaji na kuabudu (ukoo wa Mtume)), na Uthibitisho wako mkuu na mafno wako wa juu kabisa, na neno lako zuri (jema), mlinganiaji kwako na ishara inayokuashia wewe, uliye mweka kuwa bendera kwa waja wako, na mfasiri wa kitabu chako, na msimamisha amri zako kwa amri yako (mkemea maovu), na mtetezi wa dini yako, na hoja (bayana na kielelezo wazi) juu ya watu wako, na nuru itumikayo kuchania giza, na kigezo cha kuufikia uwongofu, na mwombezi mbele ya Mwenyezi Mungu ambaye Peponi hupatikana kupitia kwake. Ewe Mola kama vile yeye alivyochukua sehemu ya muda wake kukuabudu na akatimiza fungu lake katika kukutii wewe, basi nawe msalie mara kadhaa ya unavyo msalia mmoja ya mawalii uliye iridhia taa yake na ukaukubali utumishi wake, na umfikishie sala na salamu zitokazo kwetu, na utufadhili kutoka na taa yetu kwake (kumtii na kumfuata) na utufanyie hisani, utupe msamaha na radhi zako kwa yakini wewe ni mwenye upendo wa dahari na msamaha mwema na adhimu, ewe Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu. (Majlisi, Zaadu al-Ma’ad, chapa ya mwaka 1423 Hijiria, ukurasa wa 536 hadi 537) [26]

Vitabu

Makala Asili: Orodha ya vitabu kuhusu Imamu Jawadi (a.s)

Kuna kazi kadhaa za kiuandishi zilizuandikwa kwa lugha tofauti kuhusiana na Imamu Jawadi (a.s), hasa kwa lugha ya Kiajemi na Kiarabu. Katika Makala yenye jina la: “Kitabshenasi Imamu Jawadi (a.s), kumeorodheshwa idadi ya kazi 605, vikiwemo vitabu 324 na makala 248 na tasnifu 33.

Kati ya kazi hizo, kuna idadi ya vitabu 474 vilivyo andikwa kwa lugha ya Kiajemi, 122 kwa lugha ya Kiarabu, na 9 kwa lugha nyinginezo. [180]

Miongoni mwa vitabu ambavyo vimechapishwa kwa lugha ya Kiarabu kuhusu Imam al-Jawad ni; Wafatu Imam al-Jawad, Musnad al-Imami al-Jawad, Mausuu'atu aI-Imami al-Jawad Alaihi al-Sala, al-Hayatu al-Siyasiyyah lil-Imami al-Jawad, Hayatu al-Imami Muhammad al-Jawad na Subalu al-Rashad.

Mnamo mwaka wa 2016, lilifanyika kongamano maalumu katika Taasisi ya Utafiti ya Sayansi na Tamaduni za Kiislamu huko Qom, lililopewa jina la "Maisha na Nyakati za Imam Jawadi (a.s)" na matokeo yake yalikuwa ni kitabu kilichoitwa "Mkusanyo wa Makala ya Kongamano la Maisha na Nyakati za Imamu Jawadi (a.s)" kilichochapwa katika juzu tatu. [181]


Vyanzo

  • Qurān al-Karīm.
  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Al-Ḥayāt al-sīyāsīyya li-l-Imām al-Jawād. Third edition. Beirut: al-Markaz al-Islāmī li-l-Dirāsāt, 1425 AH.
  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Al-Ṣaḥīḥ min sīrat al-nabīyy al-aʿẓam. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1426 AH.
  • Ashʿarī, Saʿd b. ʿAbd Allāh al-. Kitāb al-maqālāt wa al-firaq. Tehran: Markaz-i Intishārāt-i ʿIlmī wa Farhangī, 1361 Sh.
  • ʿAṭārudī, ʿAzīz Allāh. Musnad al-Imām al-Jawād. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamī li-l-Imām al-Riḍā, 1410 AH.
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Kitāb al-tafsīr. Edited by Hāshim Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmīyya al-Islāmīyya, 1380 AH.
  • Bayhaqī, ʿAlī b. Zayd. Tārīkh-i Bayhaq. Edited by Aḥmad Bahmanyār. Tehran: Intishārāt-i Furūghī, 1361 Sh.
  • Fattāl al-Nayshābūrī, Muḥammad b. Aḥmad al-. Rawḍat al-wāʿiẓīn. Qom: Manshūrāt al-Sharīf al-Raḍī, 1375 Sh.
  • Haythamī, Aḥmad b. Ḥajar al-. Al-Ṣawāʿiq al-muḥriqa. Istanbul: Maktabat al-Ḥaqīqa, 1424 AH.
  • Ḥājīzāda, Yadullāh. Ghāliyān dar dura-yi Imām al-Jawād wa nuʿ barkhurd-i haḍrat bā ānān. Tārīkh-i Islām No 65. Spring 1395 Sh.
  • Ḥassūn, Muḥammad. Aʿlām al-nisāʾ al-muʾmināt. Tehran: Dār al-Uswa, 1421 AH.
  • Ibn Abī l-Thalj. Tārīkh al-Aʾimma. Qom: Kitābkhānih Āyat Allāh al-Marʿashī, 1406 AH.
  • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Minhāj al-sunna al-nabawīyya. Edited by Muḥammad Rashād Sālim. [n.p]. [n.d].
  • Ibn Kathīr. Al-Bidāya wa l-nihāya. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1408 AH.
  • Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Edited by Ḥāshim Rasūlī. Qom: Nashr-i ʿAllāma, [n.d].
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Qom: Raḍī, 1421 AH.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Ḥayāt-i fikrī wa sīyāsī-yi Imāmān-i Shīʿa. Third edition. Tehran: Nashr-i ʿIlm, 1393 Sh.
  • Jāsim, Ḥusayn. Tārīkh-i sīyāsī-yi ghaybat-i Imām Dawāzdahum. Translated Muḥammad Taqī Āyat Allhī. Tehran: Muʾassisi-yi Intishārāt-i Amīr Kabīr, 1386 Sh.
  • Jabbārī, Muḥammad Riḍā. Sāzmān-i wikālat wa naqsh-i ān dar ʿaṣr-i Aʾimmah. Qom: Muʾassisa-yi Imām Khomeini, 1382 Sh.
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl. Edited by Muḥammad Rajāʾī. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1404 AH.
  • Khazʿalī, Abu l-Qāsim. Mawsūʿa al-Imām al-Jawād (a). Qom: Muʾassisa al-ʿAṣr (a) l-Dirāsāt al-Islāmiya, 1419 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Translated by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Masʿūdī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Ithbāt al-waṣīyya. Third edition. Qom: Muʾassisat Anṣārīyān, 1426 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād. Translated by Hāshim Rasūlī. Second edition. Qom: Intishārāt-i ʿIlmī-yi Islāmī, 1413 AH.
  • Najāshī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Rijāl al-Najāshī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn, 1365 Sh.
  • Nawbakhtī, Ḥasan b. Mūsā al-. Firaq al-Shīʿa. Edited by Muḥammad Ṣādiq Baḥr al-ʿUlūm. Najaf: Maktabat al-Murtaḍawīyya, 1355 AH.
  • Pīshwāyī, Mahdī. Sīrah-yi pīshwāyān. Qom: Miʾassisah-yi Imām-i Ṣādiq, 1379 Sh.
  • Qarashī, Bāqir Sharīf al-. Ḥayāt al-Imām Muḥammad al-Jawād. Second edition. N.p: Amīr, 1418 AH.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahā l-āmāl. Seventeenth edtion. Qom: Muʾassisat Intishārāt-i Hijrat, 1386 Sh.
  • Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh al-. Al-Kharāʾij wa l-jarāʾiḥ. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Mahdī, 1409 AH.
  • Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh. Daʿwāt al-Rāwandī. Qom: Manshūrāt Madrisat al-Imām al-Mahdī, 1407 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Translated by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Tehran: Nashr-i Ṣadūq, 1373 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Tawḥīd. Edited by Hāshim Ḥusaynī Tehrānī. Qom: Jāmiʿa Mudarrisīn, 1398 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Ṣadr, Sayyid Muḥammad. Tārīkh al-ghayba. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1412 AH.
  • Sayyid b. Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā al-. Al-Durūʿ al-wāqīya. Beirut: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1415 AH.
  • Sayyid b. Ṭāwūs, ʿAlī b. Mūsā al-. Muhaj al-daʿwāt wa manhaj al-ʿibādāt. Edited by Ābū Ṭālib Kirmānī and Muḥammad Ḥasan Muḥraz. Qom: Dār al-Dhakhāʾir, 1411 AH.
  • Sibṭ b. al-Jawzī, Yūsuf b. Qazāwughlī. Tadhkirat al-khawāṣ. Qom: al-Sharīf al-Raḍī, 1418 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Dalāʾil al-imāma. Qom: Dār al-Dhakhāʾir, 1383 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-Ṭabarī. Fourth edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Ṭabrisī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Al-Iḥtijāj. Mashhad: Nashr al-Murtaḍā, 1403 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1417 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Ghayba. Edited by ʿIbād Allāh Tihrānī & ʿAlī Aḥmad Nāṣiḥ. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1425 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Edited by Sayyid Ḥasan al-Khirsān. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiya, 1407 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan. Misbāḥ al-mutahajjid. Qom: Maktaba al-Islamīyya.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār Ṣādir, [n.p].