Sala ya maiti (Kiarabu: صلاة الميت) ni sala iliyowajibishwa kwa Waislamu kuisalia maiti ya Muislamu mwenzao kabla ya kuizika maiti hiyo. Sala ya maiti ina takbira tano. Mfumo wa kumsalia maiti kama ifuatavyo: Baada ya takbira ya kwanza ya husomwa shahada mbili, baada ya takbira ya pili husaliwa Mume (s.a.w.w), baada ya takbira ya tatu huwaombewa msamaha waumini na Waislamu kwa jumla, na baada ya takbira ya nne humuombewa msamaha marehemu anayesaliwa Sala hiyo, kisha huhitimishwa Sala hiyo kwa kusomwa takbira ya tano, yaani haimalizwi kwa kutoa salamu, bali itolewapo takbira ya tano, huwa ndiyo hitimisho la Sala hiyo.

Sala ya maiti ni tofauti na Sala nyingine; Sala hii huwa haina Surat al-Fatiha ndani yake, haina rukuu, haina sijda, haina tashahhud (tahiyyatu) na wala haina salamu, yaani huwa haihitimishwi kwa kutoa salamu. Tohara (usafi wa mwili pamoja na udhu) huwa haizingatiwi ndani ya Sala ya maiti, hivyo mtu yuwaweza kusali Sala ya maiti bila ya kuwa na udhu au hata bila ya kukoga josho la wajibu, yaani hata kama mtu atakuwa na janaba basi hatolazimika kukoga, bali anaweza kusali Sala ya maiti akiwa na janaba. Bila shaka ni bora zaidi iwapo mtu atachunga masharti ya Sala nyingine za faradhi katika Sala hiyo.

Sala ya mazishi inaweza kusaliwa kwa jamaa na pia yaweza kusaliwa furada (ya kila mtu kusali peke yake bila ya kuunga jamaa). Katika Sala ya maiti, hata mtu akiisali Sala hiyo kwa mfumo wa jamaa, yeye atawajibika kukariri au kusoma kila kisomwacho ndani ya Sala hiyo. Yaani haitoshi imamu peke yake kusoma yasomwayo katika sala hiyo, watu wanaosali sala hiyo wanatakiwa nao kusoma kila kisomwacho ndani yake.

Sala ya maiti kwa mujibu wa madhehebu ya Sunni huwa ina takbira nne na humaliziwa kwa salamu.


Ufafanuzi

Sala ya maiti ni mkusanyiko wa dua pamoja na takbira ambazo ni wajibu kwa Waislamu kumsomea maiti wa Kiislamu baada ya kumuosha na kumkafini na kabla ya kumzika. Kwa mujibu wa vyanzo vya kifiqhi, baadhi ya sharti za sala ya faradhi kama vile usafi na tohara ya udhu pamoja na mwili, si sharti katika Sala ya maiti.


Sala ya maiti si miongoni mwa Sala

Kwa mujibu wa maneno ya Shahidi Thani ni kwamba; Kulingana na maoni ya mafaqihi mashuhuri, Sala ya maiti haizingatiwi kuwa ni miongoni mwa Sala, bali ni aina maalumu ya kumombea maiti. Kwa sababu hakuna Sala isiyo na rukuu wala sujudu, pia tohara nayo ni sharti ya kila sala, ila sala ya maiti haina lolote lile miongoni mwa mambo hayo. [3]

Katika kitabu cha Fiqh al-Ridha, imeelezwa katika Hadithi ya Imamu Ridha (a.s) ya kwamba; Sala ya maiti sio Sala bali ni takbira tu; Kwa sababu Sala halisi ni lazima ndani yake iwe na rukuu na sujudu. [4]

Jinsi ya kusali Sala ya maiti

Ili kusali sala ya maiti kuanze, kanza kabisa maiti huelekezwa upande wa Qibla, yaani kichwa cha maiti kiwe upande wa kulia na miguu iwe upande wa kushoto wa wenye kusali. [5] Msalia maiti natakiwa asimame akiwa ameelekea upande wa Qiblah, [6] wala asiwe mbali na maiti, [7] ] naye anatakiwa kusali sala hiyo hali akiwa wima. [8]

Baada ya wanaomsalia maiti kutia nia ya kusali sala ya maiti, hapo wasali sala hiyo kwa kutoa takbira tano, baada ya kila takbira katika nne za mwanzo, huwa kuna sua maalumu ndani yake, baaya ya kumaliza kusoma takbira nne za mwanzo pamoja na dua lizizomo ndani yake, mwishi watoa takbira ya tano, na hapo sala yao itakuwa imeshakamilika. [9]

Baada ya takbira ya kwanza hutolewa (husomwa) shahada mbili, baada ya takbira ya pili husaliwa Mtume (s.a.w.w), baada ya takbira ya tatu huwaombea msamaha waumini na Waislamu wote kwa jumla na baada ya takbira ya nne humuombewa msamaha yule anayesaliwa sala hiyo ya maiti. [10] Adhkari (nyiradi) na dua zisomwazo baada ya kila takbira miongoni mwa takbira nne za mwazo, kama vile:

Takbira Dua za Mustahabu Dua za Wajibu
Takbira ya kwanza →
اَشْهَدُ اَنْ لا الهَ الَّا اللَّهُ وَ اَنَّ مُحَمَّداً رَسوُلُ اللَّهِ
اَشْهَدُ اَنْ لا اِلهَ الا اللَّهُ وَحْدَهُ لاشَریک لَهُ وَ اَشْهَدُ اَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَ رَسُولُهُ اَرْسَلَهُ بِالْحَقِّ بَشیراً وَ نَذیراً بَینَ یدَی السّاعَةِ
Takbira ya pili →
اَللَّهُمَّ صَلِّ عَلی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ
اَللّهُمَّ صَلِّ عَلی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ وَ بارِک عَلی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ وَارْحَمْ مُحَمَّداً وَ آلَ مُحَمَّدٍ کاَفْضَلِ ما صَلَّیتَ وَ بارَکتَ وَ تَرَحَّمْتَ عَلی اِبْرهیمَ وَ آلِ اِبْرهیمَ اِنَّک حَمیدٌ مَجیدٌ وَ صَلِّ عَلی جَمیعِ الاَنْبِیآءِ وَالْمُرْسَلینَ
Takbira ya tatu →
اَللَّهُمَّ اْغفِرْ لِلْمُؤْمِنینَ وَ الْمُؤْمِناتِ
اَللّهُمَّ اغْفِرْ لِلْمُؤْمِنینَ وَالْمُؤْمِناتِ وَالْمُسْلِمینَ وَالْمُسْلِماتِ الاَحْیآءِ مِنْهُمْ وَالاَمْواتِ تابِعْ بَینَنا وَ بَینَهُمْ بِالْخَیراتِ اِنَّک مُجیبُ الدَّعَواتِ اِنَّک عَلی کلِّشَیئٍ قَدیرٌ
Takbira ya nne → Iwapo maiti atakuwa ni mwanamme:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِهذَا المَیت


Iwapo maiti ni mwanamke:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِهذِهِ المَیتَةِ
Iwapo maiti atakuwa ni mwanamme:
اَللّهُمَّ اِنَّ هذا عَبْدُک وَابْنُ عَبْدِک وَابْنُ اَمَتِک نَزَلَ بِک وَ اَنْتَ خَیرُ مَنْزُولٍ بِهِ اَللّهُمَّ اِنّا لا نَعْلَمُ مِنْهُ اِلاّ خَیراً وَ اَنْتَ اَعْلَمُ بِهِ مِنّا اَللّهُمَّ اِنْ کانَ مُحْسِناً فَزِدْ فی اِحْسانِهِ وَ اِنْ کانَ مُسیئاً فَتَجاوَزْ عَنْهُ وَاغْفِرِ لَهُ اَللّهُمَّ اجْعَلْهُ عِنْدَک فی اَعْلا عِلِّیینَ وَاخْلُفْ عَلی اَهْلِهِ فِی الْغابِرینَ وَارْحَمْهُ بِرَحْمَتِک یا اَرْحَمَ الرّاحِمینَ
Iwapo maiti ni mwanamke:
اَللّهُمَّ اِنَّ هذِهِ اَمَتُک وَابْنَةُ عَبْدِک و ابنَةُ اَمَتِکَ نَزَلَتْ بِک وَ اَنْتَ خَیرُ مَنْزوُلٍ بِهِ اَللّهُمَّ اِنّا لا نَعْلَمُ مِنْها اِلاّ خَیراً وَ اَنْتَ اَعْلَمُ بِهامِنّا اَللّهُمَّ اِنْ کانَتْ مُحْسِنَةً فَزِدْ فی اِحْسانِها وَ اِنْ کانَتْ مُسیئةً فَتَجاوَزْ عَنْها وَاغْفِرْ لَها اَللّهُمَّ اجْعَلْها عِنْدَک فی اَعْلا عِلِّیینَ وَاخْلُفْ عَلی اَهْلِها فِی الْغابِرینَ وَارْحَمْها بِرَحْمَتِک یا اَرْحَمَ الرّاحِمینَ
Takbira ya tano → Mwisho wa sala Mwisho wa sala

Maoni ya Mafaqihi wa Kisunni

Kwa mujibu wa madhehebu ya Sunni; Sala ya maiti ina takbira nne. Sala hufungulia (huanza) kwa takbira ya kwanza, baada ya hapo husomwa Suratul Al-Fatiha. Baada ya takbira ya pili, husaliwa Mtume (s.a.w.w), baada ya takbira ya tatu, huombewa dua huyo maiti anayesaliwa, kisha hosomwa takbira ya nne na papo hapo hutolewa salamu, na huo huwa ndio mwisho wa sala.


Hukumu za Sala ya maiti

Baadhi ya hukumu za kifiqhi za Sala ya maiti ni:

  • Sala ya maiti ni faradhi inayojitosheleza (faradhi kifaya); Kwa hiyo, iwapo mtu mmoja ajitokeza na kuchukuwa jukumu la kumsalia maiti huyo, wajibu huo wa kumsalia maiti utawaepeka Waislamu wengine waliobaki. [14]
  • Kwa mujibu wa maelezo ya Sahib Jawahar ni kwamba; Maoni ya mafaqihi walio maarufu yanesema kuwa, ni makuruhu (haikupendekezawa) kusalia maiti sala kadhaa. [15] Kwa mujibu wa fatwa za Ayatullah Sistani ni kwamba; Hakuna ithibati juu umakruhu (kutopendekezwa) kwa suala hilo, hasa kama maiti hiyo itakuwa ni maiti ya mwanazuoni na uchamungu, katu hakutakuwa na umakruhu juu ya kussalia yeye sala zaidi ya moja. [16]
  • Sala ya maiti inaweza kusaliwa kwa jamaa, na pia inaweza kusaliwa kwa mfumo wa furada (kila kusali bila ya kumfuata imamu). Lakini hata kama mtu asali sala hiyo kwa jamaa, ni lazima yeye asome takbira zote tano pamoja na kinachotakiwa kusomwa ndani ya sala hiyo, yaani kisomo cha imamu hakishelezi katika kuikamailisha sala ya maamuma wake (anayesali kwa kumfuata yeye). [17]
  • Sala ya maiti ni wajibu kwa kila Muislamu ambaye amefikisha umri wa miaka sita. [18]
  • Maiti aliye kafiri au nasibi (mwenye uadui na na kizazi cha Mtume (s.a.w.w)) huwa hasaliwi sala ya maiti. [19]
  • Si lazima katika sala ya maiti, mtu kutoharika kutokana na josho la wajibu, kama vile janaba, hedhi au nifasi, na wala si lazima mtu kuwa na udhu katika kumsalia maiti. [20] Bila shaka, ni bora zaidi iwapo mtu azingatia masharti yote ya sala nyingine za faradhi katika sala hiyo ya maiti. [21]
  • Ni lazima maiti asaliwe kabla ya kuzikwa kwake [22] na iwe ni baada ya kukoshwa na kuvikwa sanda (kukafiniwa). [23]
  • Ikawa Mwislamu atazikwa bila ya kusaliwa, basi ni lazima Waislamu waende kusalia kaburini kwake. [24]
  • Inawezekana kusaliwa sala moja ya maiti kwa ajili ya maiti kadhaa.[25]
  • Inachukiza (makuruhu au hauikupendekezwa) kuwasalia maiti misikitini. [26] Baadhi ya mafaqihi wameuvua Msikiti wa Makka kuhusiana na hukumu hii, [27] ila wanazuoni wengine hawajakubaliana na nadharia ya manazuoni hao katika suala hilo. [28]
  • Pia mtu anaweza kusala bila ya kuvua viatu, ingawaje ni mustahabu(inapendekezwa) na ni bora zaidi kusali bila viatu. [29]

Sala za maiti za kihistoria

Sala ya maiti ya bibi Fatima Zahraa (a.s) na sala ya maiti ya maiti ya Imam Khomeini ni miongoni mwa sala za maiti, ambazo kila moja kati yake zina sura maalumu yenye mazingatio kwa walimwengu: kwa mujibu wa maandishi ya wanahistoria; Ali bin abi Talib (a.s) aliikosha maiti ya mkewe (bibi Fatima) (a.s) katika wakati wa usiku [30] kisha akamsalia wakati katika wakati huo huo wa usiku. [31] Kwa mujibu wa maelezo ya Tabarsi; Miongoni mwa watu wailoshiriki katika sala ya kumsalia bibi Fatima (a.s), ni: Imam Hasan, Imam Hussein, Miqdad, Salman Farsi, Abu Dharr Al-Ghafari, Ammar bin Yasir, Aqiil bin Abi Talib, Zubeir bin Awam, Boraidah bin Husaib Aslami pamoja na baadhi ya watu wa okoo wa Bani Hashim. [32]

Sababu hasa ya bibi Fatima kuoshwa, kusaliwa na pia kuzikwa wakati wa usiku, inatokana na kwamba; Fatima alimuusia Ali bin Abi Talib (a.s) kumzika usiku, ili watu waliomdhulumu wasihudhurie mazishi yake na wala wasipate nafasi ya kuusalia mwili wake. [33]

Swala ya maiti ya Imam Khomeini ilikuwa ni moja ya sala zenye zlizohudhuriwa na watu wengi zaidi. Sala hiyo ilifanyika mnamo mwezi wa Khordad 1368 Shamsia, sawa na tarehe 5 June 1989 chini ya uongozi wa Ayatollah Gulpaygani. Mazishi ya Imam Khomeini yanachukuliwa kuwa ndio mazishi yaliohudhuriwa na watu wengi zaidi katika historia. [34]


Masuala yanayofungamana