Nenda kwa yaliyomo

Muhammad bin Othman bin Said Amri

Kutoka wikishia
Alipozikwa Muhammad bin Othman bin Said Amri

Muhammad bin Othman bin Said Amri (aliyeaga dunia 305 Hijiria) ni Naibu wa Pili kati ya Manaibu Wanne wa Imam wa 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Alichukua jukumu hilo la Unaibu baada ya baba yake Othman ibn Said. Awali alikuwa wakili wa Imam wa zama na mmoja wa wasaidizi wa baba yake na baada ya kuaga dunia baba yake alichukua jukumu la Unaibu wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) kwa takribani miaka 40 (265-305 Hijiria) katika kipindi cha Ghaiba Ndogo. Alipofariki Naibu wa Kwanza, Imamu wa Zama (a.t.f.s) alimuandikia barua mwana wa Muhammad bin Othman baada kumfariji kwa kifo cha baba yake, alimteua kuwa mrithi wa nafasi ya Unaibu iliyokuwa ikishikiliwa na baba yake wakati wa uhai wake.

Licha ya kuwa ilibainishwa wazi katika hadithi ya Imam Askary (a.s) na barua ya Imamu wa Zama kuhusiana na Unaibu wa Muhammad bin Othman, lakini baadhi ya mawakili wa mtandao wa mawakala wa Maimamu walitilia shaka Unaibu wake na baadhi walidai Unaibu. Muhammad bin Othman alikuwa na wasaidizi ambao walikuwa na ushirikiano na mtandao wa uwakala. Muhammad Othman Amri ameandika vitabu katika uga wa Fiqhi na kumenukuliwa kutoka kwake hadithi kuhusiana na Imamu Mahdi (a.t.f.s). Dua maarufu kama vile Simaat, Iftitah na Ziyarat Aal-Yasin pia zimenukuliwa kutoka kwake.

Historia ya Maisha Yake

Hakujatajwa na kuzungumziwa kuhusu tarehe ya kuzaliwa kwa Muhammad bin Othman Amri. Jina lake limetajwa katika vyanzo vya kidini kama ni Muhammad, mtoto wa Othman bin Said (Naibu wa Kwanza wa Imam Mahdi (a.t.f.s) na kuniya yake ni "Abu Jaafar". Yeye anatokana na kabila la Bani Asad. [1] Hakuna kuniya nyingine yoyote iliyotajwa kama ni yake katika vitabu vya hadithi na vitabu vya wasifu wa wapokezi wa hadithi [2].

Kuna lakabu kadhaa zimetajwa kumhusu: Wakati mwingine aliitwa kwa lakabu ya "Amri" [3], ambayo imetajwa katika vitabu vingi vya hadithi na vya kueleza wasifu wa wapokezi wa hadithi. Kuna wakati mwingine aliitwa kwa lakabu ya "Asadi" [4] na wakati mwingine aliitwa "Kufi" [5]. "Samman" [6] na "Askary" [7] pia zimetajwa miongoni mwa lakabu zake. Yeye anajulikana kama "Khallani" nchini Iraq. [8]

Kuaga Dunia

Kwa mujibu wa hadithi, Muhammad bin Uthman alitabiri wakati wa kifo chake na akatangaza miezi miwili kabla habari ya kifo chake. Msimulizi alipokutana naye alimuuliza Muhammad bin Othman, kwa nini ulijichimbia kaburi? Akasema nina jukumu la kukamilisha kazi zangu na nitaondoka duniani baada ya miezi miwili. [9] [10]

Kifo cha Naibu wa Pili kilitokea siku ya mwisho ya Jumadi al-Awwal katika mwaka wa 305 Hijiria. [11] Mwili wake ulisindikizwa na kuagwa huko Baghdad na kisha kuzikwa karibu na kaburi la baba yake. [12] Kwa mujibu wa wasia wa Muhammad bin Othman na kwa mujibu wa agizo na amri ya Imamu Mahdi (a.t.f.s), Hussein ibnu Ruh al-Nawbakhti alihudhuria Dar al-Niyabah Baghdad na amkamrithi Muhammad Othman. [13]

Uwakala na Kuwa Naibu wa Imamu wa Zama

Imamu Hassan Askary (a.s) aliweka wazi jukumu la Muhammad bin Othman kwamba, ni Naibu wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). Wakati kundi la Mashia wa Yemen lilipomuendea Imamu Askary katika mji wa Samarra, Imam (a.s.) alimuita Othman bin Said, baba yake Muhammad bin Othman, na kutoa ushahidi juu ya uwakala na uaminifu wa Muhammad, na akamuita kuwa ni wakili wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). [14]

Katika Kitabu cha Al-Ghaibah, Sheikh Tusi amenukuu hadithi ambayo kwa mujibu wake Muhammad bin Othman na baba yake, Othman bin Said, walikuwa waaminifu na wanaoaminiwa na Imam Hassan Askary (a.s). Kwa mujibu wa hadithi, Imamu Hassan Askary (a.s) alisema: Chochote watakachokifikisha, basi wanakifikisha kwa niaba yangu na chochote wanachokisema kinatoka kwangu. Sikilizeni maneno yao na muwafuate, kwani hao ni waaminifu wangu. [15]

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa na Sheikh Tusi, alipofariki naibu wa kwanza, mtoto wake Muhammad alimuosha, akamkafini na kumzika [16]. Alipata barua ya mkono wa pole kutoka kwa Imam wa 12, ambayo ndani yake Imamu alimliwaza na kuonyesha kuwa pamoja naye katika msiba huo. Aidha ndani ya barua hiyo kuliashiriwa unaibu wake kwa Imamu Mahdi baada ya baba yake. [17]

Muda wa Unaibu Wake

Sheikh Tusi amebainisha wazi katika kitabu cha al-Ghaiba kwamba, muda wa unaibu wa Muhammad bin Othman ulikuwa karibu miaka hamsini [18]. Lakini Sayyid Muhammad Sadr aliyachukulia madai hayo kuwa yasiyo sahihi, kwa sababu kwa mujibu wake, kifo cha Muhammad bin Othman kilitokea mwaka 305 Hijiria, na kuna tofauti ya miaka 45 na kuuawa shahidi Imam Hassan Askary (a.s.) na kwa kuwa naibu wa kwanza (baba yake) alishikilia jukumu la unaibu kwa takribani miaka mitano, jukumu la unaibu wa Naibu wa Pili wa Imamu Mahdi muda wake utakuwa takribani miaka 40 na sio miaka 50. [19]

Wapinzani

Watu ambao baada ya kifo cha Otman bin Said (Naibu wa kwanza) walitilia shaka unaibu wa Muhammad bin Othman na wakadai wao kuwa ndio manaibu ni:

Hali ya Kipindi cha Unaibu

Miongoni mwa matukio muhimu katika kipindi cha unaibu wa Muhammad bin Othman, ni harakati ya Sahib al-Zanj na kuibuka kundi la Qaramitah.Kutokana na kuwa, Sahib al-Zanj nasaba yake inaishia kwa Zayd, mtoto wa Imamu Sajjad (a.s), kundi miongoni mwa Alawiyun (watu kutoka katika kizazi cha Imamu Ali a.s) walijiunga naye [22]. Watafiti wanaamini kwamba Sahib al- Zanj alijitambulisha kwa uwongo kwamba yeye ni Alawi na alikuwa mbali na Ahlul-Bayt kwa nasaba na kiutendaji. [23] Imamu Hassan al-Askary (a.s) pia alimtambua Sahib al-Zanj kwamba, yuko mbali na Ahlul-Bayt (a.s).

Kundi la Qaramitah likiwa tawi la madhehebu ya Ismailia, lilikuwa na uhusiano na Shia pia na huu uhusiano ungeweza kuleta matatizo kwa Shia Imamiyyah. Kwa mujibu wa nukuu ya Jassim Hussein, propaganda za Qaramitah kuhusiana na harakati ya Qaim (Imamu Mahdi) zilikuwa zikiichochea serikali ili itambue kwamba, harakati zao zina uhusiano na Ghaiba ya Imam Mahdi (a.t.f.s) na hivyo zizihesabu kuwa ni hatua ya maandalizi kwa ajili ya harakati ya Imamu Mahdi (a.t.f.s). Yeye anaamini kwamba Tawqi’ (barua na maandiko) ya Imamu wa Zama katika kumlaani Abu al-Khattab aliyomuandikia Muhammad bin Othman ilikuwa ikihusiana na hatari ya Qaramitah na ilikuwa ikiwakataza Mashia kuwa mawasiliano yoyote nao. [25]

Mbinu ya Harakati

Muhammad bin Othman ili aweze kutekeleza majukumu yake mbali na aina yoyote ile ya unyeti na kuangaliwa kwa jicgho na hatari na wapinzani, alikuwa akifanya Taqiyyah. Alikuwa akifanya mambo kwa namna iliyokuwa ikionyesha kuwa, dhana na fikra ya utawala wa Bani Abbas kwamba, Imamu Hassan Askary (a.s) hakuwa na mrithi; na alikuwa akiwaagiza mawakili wake wafanye mambo yao kwa kuchunga taqiya (kuficha itikadi kwa kuhofia uhai) ili lisije likajitokeza jina la Imamu wa Kumi na Mbili na ili kwa njia hiyo fikra za utawala zibakie hivyo hivyo. Msimamo huu wa Muhammad bin Othman ulikuwa kwa ajili ya kwamba, utawala uwe na hali ya utulivu kabisa kwamba, Mashia hawana kiongozi na hivyo hawataanzisha harakati. [26]

Mawakili na Wasaidizi

Katika kipindi cha unaibu wa Muhammad bin Othamn, kuna watu waliokuwa wakishirikiana naye. Baadhi ya wawakilishi wake katika baadhi ya maeneo walikuwa wanafunzi wake na walikuwa wakinukuu hadithi kutoka kwake. Inaelezwa kuwa katika mji wa Baghdad walikuweko watu 10 ambao walikuwa wakiendesha na kufanya mambo kwa usimamizi na miongozo yake ambapo mmoja wao alikuwa Hussein bin Ruh ambaye baadaye alikuja kuwa naibu wa Imamu Mahdi (a.t.f.s). [27] Baadhi ya majina yao ni:

Daraja ya Kielimu na Kihadithi

Sheikh Tusi amewatambua Muhammad na baba yake katika vitabu vya Rijaal na al-Ghaibah kwamba, ni mawakili wa Imamu Mahdi ambao walikuwa na daraja kubwa na maneno yao ni ya kuaminika na ya uhakika. [29] Allama Hilli pia katika kitabu chake cha Rijaal, amekutambua kuteuliwa Muhammad bin Othman kuwa naibu wa Imamu Mahdi kwamba, maana yake ni kuwa kwake na daraja ya juu. [30] Mamaqani katika kitabu chake cha Tanqih al-Maqal, ameitambua daraja ya Muhammad bin Othman kwamba, ni ya juu na mashuhuri kiasi kwamba, haina haja ya kutolea maelezo au kutoa hoja za kuthibitisha hilo. [31] Sayyid Abul-Qassim Khui pia katika kitabu chake cha Mu’jam Rijaal al-Hadithi, amezitambua kuwa za kutosheleza hadithi ambazo zimekuja kuelezea na kubainisha hadhi na adhama ya naibu huyu wa pili wa Imamu Mahdi. [32]

Hadithi na Athari

Kumenukuliwa hadithi kutoka kwa Muhammad bin Othman kuhusiana na Imamu wa zama (a.t.f.s); miongoni mwazo ni kuhusiana na Imamu Mahdi (a.t.f.s) [33], ni haramu kutaja jina lake katika zama za Ghaiba ndogo [34] na kukutana na kuonana kwake na Imam Mahdi, [35] dua za Simaat, Iftitah, Ziyarat Aal Yasin ni dua ambazo zimenukuliwa kutoka kwa Muhammad bin Othman. [36] Yeye pia amenukuu hadithi kutoka kwa baba yake Othman bin Said.

Muhammad bin Othman aliandika vitabu pia katika uga wa Fiqhi ambavyo ndani yake vina hadithi kutoka kwa Imamu Hassan Askary (a.s) na Imamu Mahdi (a.t.f.s). Miongoni mwa vitabu hivyo ni: Kitabu al-Ashribah”. [37]

Rejea

Vyanzo

  • Ghaffārzāda, ʿAlī. Zindigānī-yi nuwwāb-i khāṣ-i imām zamān. Third edition. Qom: Intishārāt-i Nubūgh, 1379 Sh.
  • Ibn Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1399 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma. Qom, Islāmīyya, 1421 AH.
  • Jāsim Ḥusayn. Tārīkh-i sīyāsī-yi Imam dawāzdahum. Translated to Farsi by Muḥammad Taqī Āyatollāhī. Tehran: Amīr Kabīr, 1385 Sh.
  • Māmaqānī, ʿAbd Allāh al-. Tanqīḥ al-maqāl. Najaf: [n.p], 1352 AH.
  • Najāshī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Rijāl al-Najāshī. Edited by Sayyid Mūsā Shubiyrī Zajānī. Qom: Markaz al-Nashr al-Islāmī, 1416 AH.
  • Nawbakhtī, Ḥasan b. Mūsā al-. Firaq al-Shīʿa. Edited by Muḥammad Ṣādiq Āl Baḥr al-ʿUlūm. Najaf: al-Maktaba al-Murtaḍawīyya, 1355 AH.
  • Ṣadr, Sayyid Muḥammad. Tārīkh al-ghayba. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1412 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Kamāl al-dīn wa tamām al-niʿma. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī, Qom: [n.p], 1363 Sh.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, [n.d].
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Ghayba. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1411 AH.