Nenda kwa yaliyomo

wikishia:مقالات پیشنهادی/مقاله

Kutoka wikishia


  • Karbala « Ni moja ya miji ya Mashia ya kufanya ziara na kijiografia mji huu upo nchini Iraq.»
  • Jeshi la Omar bin Sa’d « Ni jeshi lililokuwa limekusanywa na Omar bin Sa’d kwa amri ya Ubaidullah ibn Ziyad na katika siku ya Ashura lilipigana na Imamu Hussein (a.s) na maswahaba zake katika jangwa la Karbala.»
  • Mukhtar ibnu Abi Ubaid al-Thaqafi «Ni miongoni mwa tabiina (waliokutana na masahaba wa Mtume) ambaye alianzisha harakati na mapinduzi kwa ajili ya kulipiza kisasi cha damu ya Imamu Hussein (a.s).»
  • Harakati za Imamu Hussein (a.s) «Ni harakati za Imamu Hussein (a.s) dhidi ya utawala wa Yazid bin Muawiya ili kuonesha upinzani wake dhidi ya utawala huo. »
  • Abbas bin Ali bin Abi Talib (a.s) «Ni mtoto wa tano wa Imamu Ali (a.s) na mtoto wa kwanza wa Ummul-Banina, ambaye alizaliwa mwaka wa 26 na kuuwawa kishahidi na jeshi la Yazid bin Muawiya mwaka wa 61 Hijiria.»
  • Akhera «Ni ulimwengu baada ya kifo na mauti na ni ulimwengu ujao baada ya maisha ya dunia.»
  • Ulul-amri «Ina maana ya wenye mamlaka, na hao wenye mamlaka ni watu ambao ni wajibu kuwatii kwa msingi wa Aya ya Ulul-Amr. Istilahi hii imekuja na kuelezwa ndani ya aya ya 59 ya surat al-Nisaa.»
  • Kafara ya swaumu «Ni adhabu ambayo huwekwa kutokana na kubatilisha na kuharibu funga ya mwezi wa Ramadhan, funga ya nadhiri ya muda maalumu na pia kadhwaa au malipo ya funga ya mwezi wa Ramadhani.»
  • Safari ya Kisheria «Ni safari ambayo ndani yake msafiri analazimika kusali sala zake kwa kupunguza (Sala za rakaa nne azisali rakaa mbili) na hapaswi kufunga Swaumu.»