Nenda kwa yaliyomo

Halali

Kutoka wikishia

Halali (Kiarabu: الحلال) ni kinyume cha haramu, na ina maana ya kile ambacho kinaruhusiwa matumizi yake kupitia mtazamo wa sheria na kuto pingana na misingi ya akili salama. Katika baadhi ya vyanzo vya kisheria, neno "halal" limezingatiwa kuwa sawa na neno mubah (kilichokuwa hakikuwekewa hukumu maalumu)", lakini imeelezwa kwamba halali ni mojawapo ya hukumu ambazo hazihusiani moja kwa moja na vitendo vya wale waliopewa jukumu tu, na ni neno halali ni pana zaidi kimaana kuliko neno “mubah”, kwani kila mubah ni halali, lakini si halali zote ni mubah kufanywa na kila mtu.

Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni, ikiwa kuna shaka kuhusu halali au haramu ya kitu, katika hali kama hiyo, sheria hushikilia hukumu ya uhalali, ambayo ndiyo hukumu asili ya kila kitu kabla ya sheria kuingilia kati na kutoa hukumu maalumu juu ya vitu hivyo. Katika vyanzo hadithi, kuna wito na sisitizo juu ya kujifunza sheria za halali na haramu ili kupata riziki ya halali.

Mnamo mwaka 2007, Taasisi ya Kimataifa ya Halal ilianzishwa ili kueneza utamaduni wa halali. Pia, siku ya 17 ya Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Halal duniani.

Semantiki (utafiti wa kilugha)

Halal ni kinyume cha haramu, na ina maana ya kile ambacho kimepewa idhini na kinaruhusiwa kupitia sheria ya dini (Uislamu) na hakipingani na akili salama. [1] Kwa lugha nyingine ni kwamba, kitu halali kile ambacho haikikuhukumiwa na kupewa hukumu ya haramu, hivyo basi kufanya au kuacha huwa haimpelekei mja kuadhibiwa. [2]

Halal kilugha ina maana ya "kufungua fundo". [3] Kulingana na ufafanuzi wa Ali Akbar Qurashi, neno "halla حل" linamaana ya kungua fundo, hapa limetumika kama ni sitiari, kwa sababu halali ni kitu ambacho kimefungulia kutoka kifungu cha umarufuku. [4]

Kulingana na maoni ya watafiti wengine; matumizi ya neno “inajuzu یجوز” au "inasihi یصح" na wakati mwengine “inahalalika یحل” ambayo hutumiwa na mafaqihi katika ibara zao mbali mbali, humaanisha uhalali kwa kitu fulani, na hutumiwa katika mambo ambayo hayana umarufuku wa kisheria ndani yake. [5]

Katika Hadithi iliyosimuliwa na Imam Swadiq (a.s), kujifunza hadithi moja kuhusu halali na haramu kutoka kwa mtu mwaminifu, ni bora kuliko dunia na dhahabu na fedha yake zilizomo ndani yake. [6]

Tofauti ya halali na mubahu

Makala Asili: Mubah

Baadhi ya watafiti wamelihisabu neno "halali" kuwa ni sawa na neno "mubah". [7] Wengine wametofautisha kati ya maneno haya mawili [8] na wametaja tofauti kadhaa zilizopo kati ya maneno mawili hayo. Baadhi ya tofauti hizo ni:

  • Halal katika fiqhi hutumiwa kinyume na haramu na inajumuisha mambo yote yasiyo haramu kama vile: wajibu, suna, makruh na mubahu. [9] Kwa hivyo halali ni pana zaidi kuliko mubahu; yaani, kila mubahu ni halali, lakini si kila halali ni mubahu. Kwa mfano, makruh ni halali lakini si mubahu. [10]
  • Mubahu ni mojawapo ya hukumu za kiwadhifa (zinazo ainisha wadhifa wa mtu mbele ya jambo au suala fulani), hukumu hii huambatana moja kwa moja na matendo ya mja aliopewa jukumu ya kisheria (walioko chini ya kivuli cha sheria ya Uislamu); [11] lakini halali, ni mojawapo ya hukumu zinazovielekea vitu au mambo yalioko nje ya mja. [12] [Maelezo 1]
  • Halal humaanisha kufungua fundo la umarufuku na kuondoa umarufuku unaodhaniwa juu ya kitu fulani; wakati mubahu ina maana ya kupanua uwanja wa juu ya kitendo fulani, kwenye mwanga wa kufanya na kuacha kitendo fulani. [13]

Msingi wa asili ya uhalali

Makala Asili: Msingi wa asili ya uhalali

Msingi wa asili ya uhalali: ni msingi kisheria inayo halalisha vitu vyote unavyo vitilia shaka juu ya uhalali wake. Kwa hiyo hukumu hii inaidhinisha kuamiliana na vitu hivyo kama ni vitu halali kabisa. [14] Kulingana na msingi huu, wakati utakapo kuwa na shaka juu ya uhalali au uharamu wa kitu fulani, inachukuliwa kuwa halali. [15] Uthibitisho wa kanuni hii unaweza kupatikana katika aya ya 29 ya sura ya pili ya Qur’an isemayo: ((...هُوَ الَّذي خَلَقَ لَكُمْ ما فِي الْأَرْضِ جَميعاً ; Yeye ndiye aliye kuumbieni kila kitu kilichopo ardhini….)) [16] na Hadithi isemayo: "Kila kitu ni halali kwako ila utakapopata ushahidi wa haramu wake." [17]

Rizki halali

Rizki halali ni mapato yaliyopatikana ndani ya pembe nne za fremu ya mfumo wa kanuni za kisheria na haki za Mungu kama vile: ushuru wa khumsi na zaka zikawa zimezingatiwa ndani yake, na hakuna haki ya mtu ndani yake (hakuna mali ya haramu ndani yake). [18] Umuhimu wa kupata riziki halali umesisitizwa katika Hadithi kadhaa. [19] Kwa mfano, katika Hadithi kutoka kwa Imam Swadiq (a.s), mtu anayejitahidi kupata riziki halali amefananishwa na mtu anayepigana Jihad katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. [20] Pia katika Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), ilipokewa kwamba ibada ina sehemu 70, na sehemu ya juu zaidi ni kupata riziki ya halali. [21]

Taasisi ya Halali Duniani

Nembo ya Taasisi ya Halal Ulimwenguni, ambayo imeandikwa kwenye upau wake, "Shirika la Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa ya Halal".[22]

Taasisi ya Kimataifa ya Halal ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kukuza utamaduni wa kutumia vitu halali. Taasisi hiyo inafanya kazi katika sekta za viwanda, vyakula, dawa na vipodozi, mikahawa na hoteli, utalii, michezo na biashara za halali. [23] Pia, siku ya mwezi 17 ya Ramadhani imeteuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Halali Duniani. [24] Kulingana na ripoti ya kituo cha habari cha IKNA; uteuzi huo ni kwa sababu Aya ya 168 ya Suratu al-Baqara isemayo: "Enyi watu, kuleni katika vilivyomo ardhini ambavyo ni halali na kizuri…" [25] ambayo ilishuka mwezi 17 wa Ramadhani, na kufwatia Aya hii, siku hiyo ilipewa jina la Siku ya Kimataifa ya Halali Duniani. [26] Kila mwaka ifikapo siku hii, hufanyika kongamano la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Halali Duniani na matukio muhimu zaidi yanayo tafitiwa ndani yake, ni masuala na matatizo ya tasnia ya halali duniani. [27] Mzunguko wa kwanza wa kongamano hili ulifanyika Iran mnamo Julai 15 ya mwaka 2014 katika Kituo cha Mikutano cha Mnara wa Miladi mjini Tehran. [28]

Masuala yanayo fungamana nayo

Maelezo

  1. Mfano wa mubahu ni kama vile; tendo la kulala, kula na kunywa, matendo haya ni mubahu na yameambatana mja mwenyewe. Kwa upande wa pili, halali ni kama vile haji, chakula na mahala pa kulala; vitu ambo haya yapo nje ya mja. Kwa hiyo pale isemwapo: “Maji ni halali”, huwa panaashiriwa kitu likichoko nje ya mja. Huu ndio mpambanuko wa aina mbili hizi za hukumu.

Rejea

Vyanzo