Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Imamu Ridha (a.s)

Kutoka wikishia
Imam Ridha (a.s)
Imamu wa Nane wa Mashia wa Ithna Ashari
Dharih ya Imam Ridha (a.s)
JinaAli bin Musa
NafasiImamu
KuniaAbu al-Hassan (wa Pili)
Siku ya Kuzaliwa11 Dhul-Qa'dah, Mwaka 148 Hijria
Kipindi cha UimamuMiaka 20 (183203)
KifoMwishoni mwa Safar, 203 Hijria
AlipozikwaMash'had
AlipoishiMadinaMarwu
LakabuAr-RidhaAalimu Aali MuhammadDhamine AhuuGharibu al-Ghurabaa
BabaImamu Musa al-Kadhim (a.s)
MamaNajmah Khatun
WakeSabikah
WatotoImamu Muhammad al-Jawad (a.s)
UmriMiaka 55
Maimamu wa Kishia
Imamu Ali • Imamu Hassan MujtabaImamu Hussein • Imamu Sajjad • Imamu Baqir • Imamu SwadiqImamu Kadhim • Imamu Ridha • Imamu JawadImamu Hadi • Imamu Mahdi


Ali bin Musa bin Jafar (a.s), anayejulikana na kufahamika kwa lakabu ya Imamu Ridha (148–203 Hijria), ndiye Imamu wa nane katika orodha ya mlolongo wa Maimamu Kumi na Mbili (Ithna-Asharia) wa madhehebu ya Shia. Mtukufu huyu alishika hatamu na kubeba dhamana nzito ya uongozi na Uimamu wa Shia kwa kipindi cha miongo miwili mfululizo (miaka 20), kilichoanza mwaka wa 183 Hijria; ambapo zama za Uimamu wake zilienda sambamba na tawala za makhalifa watatu wa Bani Abbas, kuanzia Harun al-Rashid, Muhammad al-Amin, hadi kufikia zama za Ma’mun al-Abbasi.

Katika miaka ya lala-salama ya umri wake duniani, Imamu Ridha (a.s) aliamriwa na kulazimishwa na Khalifa Ma’mun kuhama kutoka mji mtukufu wa Madina kwenda mji wa Marw uliopo mkoani Khorasan nchini Iran, mahali ambapo alilazimika kuvaa joho la urithi wa ufalme (utawala) wa Ma’mun. Wanahistoria pamoja na wanazuoni wa Kishia wanaitazama kadhia hii ya urithi wa ufalme, kama tukio zito na la kisiasa zaidi katika maisha ya Imamu huyo, huku wakisisitiza kwa kauli moja kuwa, Imamu aliridhia kutingika na kura hiyo kupitia shinikizo la kulazimishwa na Ma’mun, bila kuwa na hiyari yoyote juu ya maamuzi hayo.

Pamoja na mazingira hayo ya kulazimishwa, baadhi ya waandishi wa historia na matukio ya kale wanashikilia msimamo usemao kuwa, hatua ya Imamu Ridha (a.s) ya kukanyaga ardhi ya Iran ilichochea ari kubwa na kuwa na athari kubwa katika kuenea na kushamiri kwa Ushia katika ukanda huo. Sababu ya mafanikio hayo ni kwamba, pale Imamu huyu muadhamu alipokuwa akipita katika miji mbalimbali ya Iran, alikuwa akikutana ana kwa ana na wananchi na kujibu kiu za maswali yao kwa kuegemea na kunukuu za Hadithi thabiti za Maimamu waliomtangulia kabla yake. Hali kadhalika, kushiriki kwake katika majopo ya mijadala mizito ya kielimu mbele ya wanazuoni wakubwa wa dini na madhehebu mbalimbali, na kuwabwaga kielimu kwa hoja madhubuti, kulidhihirisha wazi mbele ya macho ya watu, kilele cha ukwasi wake wa elimu kama Imamu wa haki wa madhehebu ya Shia.

Hadi leo hii, katika miji na vitongoji mbalimbali nchini Iran, kuna majengo, misikiti, na maeneo ya kihistoria yanayojulikana kama Qadamgah (sehemu zilizobarikiwa kwa nyayo zake), ambayo yamepewa jina la Imamu Ridha (a.s) kama kumbukumbu ya sehemu alizoweka kambi wakati wa msafara wake kuelekea mji wa Marw. Maeneo haya yanatajwa na watafiti kama alama za wazi zinazothibitisha mchango mkubwa wa safari hiyo katika kusambaza mbegu ya Ushia nchini humo.

Miongoni mwa mambo makuu na Hadithi zinazosimuliwa katika safari hiyo ya kuelekea Iran, ni ile simulizi ya Hadithi mashuhuri iliyopewa jina la Silsilat al-Dhahab (Mnyororo wa Dhahabu); jina hili lilitokana na ukweli kwamba wasimulizi wote wa Hadithi hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho ni Maimamu maasumu waliotakaswa na madhambi. Imamu (a.s) alitoa Hadithi hii tukufu ya Qudsi mbele ya umati wa wanazuoni, pale alipokuwa katika mji wa Nishapur. Hadithi hii imeifananisha Tawhidi (upweke wa Mwenyezi Mungu) na ngome madhubuti ya Mwenyezi Mungu ambayo kila anayeingia ndani yake, husalimika na adhabu. Hata hivyo, mwishoni mwa Hadithi hiyo, Imamu aligonga msumari wa mwisho kwa kusema kuwa ngome hiyo ina masharti yake, na kwamba yeye mwenyewe (kuukubali Uimamu wake) ni miongoni mwa masharti hayo ya msingi.

Kwa mujibu wa mitazamo ya wengi wa wanazuoni wa kishia, Imamu Ridha (a.s) aliuawa kwa kupewa sumu kupitia amri ya Khalifa Ma’mun akiwa na umri wa miaka 55 huko Tus, na akafanikiwa kupata daraja ya ushahidi (kufa kishahidi) kupitia sumu hiyo, na hatimaye akazikwa katika mava ya Haruniyyah ililopo katika kijiji cha Sanabad. Yeye ndiye Imamu pekee miongoni mwa Maimamu kumi na mbili wa Shia aliyelazwa na kuzikwa katika ardhi ya Iran. Leo hii, haramu na kaburi lake takatifu lililopo mji wa Mashhad ni miongoni mwa vituo vikuu na vizito vya ziara kwa Waislamu wa Kishia duniani kote. Hali kadhalika, kaburi la dada yake mpendwa, Bibi Fatima al-Ma'sumah (a.s), nalo lipo nchini Iran na linatajwa kama haramu na eneo maarufu zaidi la ziara nchini humo, baada ya haramu ya Imamu Ridha (a.s).

Kutokana na adhama ya Imamu Ridha (a.s), kuna vitabu vingi mno, machapisho ya kitaaluma, pamoja na kazi kemkem za kifasihi kama vile mashairi, riwaya, na hata filamu zilizoasisiwa kwa ajili yake. Miongoni mwa kazi hizo mashuhuri ni pamoja na: Kitabu cha Al-Hayat al-Siyasiyyah lil-Imam al-Rida kilichoandikwa na Sayyid Jafar Murtadha Amili; kitabu cha Al-Imam al-Rida; Tarikhun wa Dirasah cha Sayyid Muhammad Jawad Fadhlullah; kitabu cha Hayat al-Imam Ali bin Musa al-Rida; Dirasatun wa Tahlil cha Baqir Sharif al-Qurashi; na Hikmat-Namehye Radhavi kilichochapishwa na Muhammad Muhammadi Rey-Shahri na jopo lake. Aidha kuna kazi kadhaa katika nyanja za ushairi na sanaa zilizotayarishwa kwa ajili yake. Miongoni mwa kazi hizo ni shairi la "Qit'atun min al-Jannah" (Kipande cha Peponi) la Habibullah Chaychian; shairi la "Ba Ale-Ali Har Ke Dar Oftad Var Oftad" (Kila Aliyepambana na Kizazi cha Ali Aliangamia) la mshairi Nasime-Shomal; pamoja na mchoro maarufu wa picha ya "Dhamin Ahuu" (Mdhamini wa Paa) uliochorwa na nguli Mahmoud Farshchian.

Salawati maalumu zilizochorwa kwenye dari la koridoo linalounganisha Ukumbi wa Dar al-Dhikr na Daru al-Zuhd.

Maisha Yake

Ali bin Musa, anayejulikana na kufahamika zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu kwa lakabu ya Imamu Ridha (a.s), ni Imamu wa nane katika mlolongo wa Maimamu Kumi na Mbili madhehebu ya Shia ya (Ithna-Ashariya).[1] Baba yake mzazi alikuwa ni Imamu Musa bin Jafar (a.s) (Imamu Kadhim), aliyeshika nafasi ya saba ya Imamu ndani ya madhehebu ya Shia, na mama yake mzazi alikuwa ni mjakazi aliyetambuliwa katika nyaraka za kihistoria kwa jina la Najmah au Tuktam.[2]

Katika dondoo na kumbukumbu za kale za wanahistoria, kuna migongano, mashaka makubwa na hitilafu za kimitazamo kuhusiana na majira na tarehe halisi ya kuzaliwa na kufariki duniani kwa Imamu Ridha (a.s).[3] Kwa hiyo kuna mapokezi na simulizi tofauti kuhusiana na suala hilo. Baadhi yake yameelezwa kuwa Imamu Ridha (a.s) alizaliwa mnamo tarehe 11 ya mwezi mtukufu wa Dhul-Hijjah, mengine yametaja mwezi wa Dhul-Qa'dah, au Rabi' al-Awwal mwaka wa 148 au 153 Hijria. Ama kuhusiana na kifo chake, kuna vyanzo vilivyodai kuwa, aliuawa shahidi katika siku za mwisho za mwezi wa Safar, huku vyanzo vyengine vikitaja tarehe tofauti, ikiwemo; tarehe 17 au 21 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, tarehe 18 ya mwezi wa Jumada al-Awwal, au tarehe 23. Na vyanzo vyengine vinasema aliuawa mnamo siku ya mwisho kabisa ya mwezi wa Dhul-Qa'dah mwaka wa 202, au 203, au 206 Hijria.[4] Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti thabiti za mwanahistoria mahiri na mtafiti wa matukio mbalimbali, Sayyid Jafar Murtadha Amili, ni kwamba; wanazuoni wengi wakiwemo magwiji wa elimu na waandishi wa matukio ya kale wanashikilia msimamo thabiti na madhubuti usemao kuwa, Imamu Ridha (a.s) alizaliwa katika mji mtukufu wa Madina mnamo mwaka wa 148 Hijria, na akauawa mnamo mwaka wa 203 Hijria.[5]

Imamu Ridha (a.s) alibeba dhamana nzito ya Uimamu, baada tu ya kufariki dunia kwa baba yake mzazi (a.s). Kipindi na muda wa uimamu wake ulikudumu kwa muda wa miongo miwili kamili, yaani miaka ishirini (183–203 Hijria); zama ambazo zilienda sambamba na tawala na makhalifa watatu wa ukoo wa Bani Abbasi, ambao ni Harun al-Rashid, Muhammad al-Amin, pamoja na Ma’mun al-Abbasi.[6]

Lakabu na Kunia

Makala Asili: Faharasa ya Lakabu na Kunia za Imamu Ridha (a.s)

Imamu Ali bin Musa (a.s) anajulikana kwa lakabu mbalimbali kama vile al-Ridha, al-Sabir, al-Radhiy, al-Wafiy, na al-Zakiy.[7] Vilevile, kulingana na mapokezi yaliyomo kwenye kitabu kiitwacho I’lam al-Wara, kilichoandikwa na Fadhlu bin Hassan Tabrasi, lakabu nyengine iliyotumiwa na Imamu Kadhim kuhusiana na Imamu huyu muadhamu ni lakabu ya Alim Aali Muhammad.[8] Lakabu nyingine zinazotumika kwa ajili yake ni pamoja na; Dhamin al-Ahu,[9] Imam al-Rauf,[10] Gharib al-Ghuraba,[11] Thamin al-Hujaj,[12] na Thamin al-Aimmah.[13]

Lakabu maarufu zaidi ya Imamu Ridha (a.s.) ni "Ar-Ridha".[14] As-Suyuti, mmoja wa wanazuoni wa Ahlu Sunna, ameeleza kwamba lakabu hii alipewa na Al-Maamun, khalifa wa Bani Abbas.[15]

Hata hivyo, kwa mujibu wa hadithi iliyopokewa na Sheikh Saduq, mwanahadithi wa Kishia wa karne ya nne Hijria, kauli hiyo si sahihi. Hadithi hiyo inasema kwamba, Imamu Jawad (a.s.) alikataa akisema kwamba jina hilo halitokani na Maamun, na akasisitiza kwamba, baba yake aliitwa "Ar-Ridha" kwa sababu alikuwa ameridhika na Uungu wa Mwenyezi Mungu, Utume wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Uimamu wa Maimamu hapa duniani.

Katika hadithi hiyo, Imam Jawad (a.s.) aliulizwa: "Je, Maimamu wengine hawakuwa na sifa hiyo hiyo? Kwa nini basi baba yako pekee ndiye aliyepewa lakabu ya 'Ar-Ridha'?" Imamu akajibu: "Kwa sababu baba yangu aliridhiwa na marafiki zake pamoja na maadui zake, na sifa hii haikupatikana kwa yeyote miongoni mwa Maimamu wengine."[16]

Kunia maarufu ya Imamu Ridha (a.s) ni Abul Hasan,[17] nayo ni kunia aliyopewa na babake, Imam Kadhim (a.s), ambaye pia alikuwa akijulikana kwa kunia hiyo hiyo.[18] Hivyo wakati mwingine Imamu Ridha (a.s) alikuwa akijulikana kama Abul Hasan wa Pili (al-Thani) ili kumtofautisha na Imamu Kadhim (a.s) mwenye kunia kama hiyo.[19] Kunia nyingine za Imamu Ridha (a.s) ni pamoja na Abu Ali na Abu Muhammad.[20]

Mke na Watoto

Mke wa Imamu Ridha (a.s) alikuwa akijulikana kwa jina la Sabika wa Kinubia (سَبیکه النوبیّه)[21] au Khaizuran (خَیزُران),[22] ambaye ndiye mama halisi wa Imamu Jawad (a.s).[23] Katika vyanzo vya kihistoria na vya Hadithi, pia ametajwa mke mwingine wa Imamu Ridha (a.s) ambaye inasemekana kuwa alikuwa ni binti wa Maamun.[24] Kwa mujibu wa ripoti ya Sheikh Saduq, ni kwamba; baada ya Maamun kumteua Imamu Ridha (a.s) kuwa mrithi wa kiti cha enzi (waliyyu-l-ahd), alimwoza binti yake, ajulikanaye kwa jina la Ummu Habib.[25]

Sheikh Saduq, Sheikh Mufid, Ibn Shahrashub, na Tabarsi wameandika wakisema kuwa; Imamu Ridha (a.s) alikuwa na mtoto mmoja tu peke yake, naye si mwengine bali ni Imamu Jawad (a.s).[26] Hata hivyo, kwa mujibu wa maandiko ya Sayyid Muhsin Amin, mwandishi wa kitabu cha A'ayan al-Shia, kuna baadhi ya vyanzo vilivyomtaja watoto wengine na kumnasibisha na Imamu Jawad (a.s).[27]

Katika mji wa Qazwin, kuna kaburi linalojulikana kwa jina la Imamu-Zadeh Hussein, ambaye Mustawfi, mwanahistoria wa karne ya nane Hijiria, amemtaja mwenye kaburi hilo kuwa ni mtoto wa Imamu Ridha (a.s).[28] Kiya Gilani, ambaye ni mtaalamu wa nasaba, amemnasibisha mwenye kaburi hilo na nasaba ya Ja'afar al-Tayyar (جعفر طیار).[29] Kadhalika, katika baadhi ya vyanzo vya kihistoria, vimemtaja mtu huyo kuwa ni kaka au mdogo wa Imamu Ridha (a.s).[30]

Kaka na Dada zake

Ibrahim, Shahcheragh, Hamza, na Ishaq ni miongoni mwa kaka wa Imamu Ridha (a.s), huku Fatima al-Ma'sumah na Hakima wakiwa ni miongoni mwa dada zake.[31] Kati ya kaka na dada zake wote hao wa Imamu Ridha (a.s), Fatima al-Ma'sumah ndiye mwenye umaarufu zaidi ulimwenguni, bibi ambaye wanachuoni wa kishia wamempa daraja na nafasi ya juu mno. Aidha kuna Hadithi nyingi zinazoelezea utukufu wake pamoja na umuhimu wa kuzuru kaburi lake.[32] Bibi huyu muadhamu amezikwa huko Qom nchini Iran, na kaburi lake takatifu linasifika kuwa ndilo lenye fahari kubwa na mashuhuri zaidi nchini Iran baada ya lile la Imamu Ridha (a.s).[33]

Nass (Tamko la Wazi) Kuhusu Uimamu

Kwa mujibu wa mtazamo na itikadi za Kishia, Imamu huteuliwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu mwenyewe, na njia mojawapo ya kumtambua kiongozi huyo ni kupitia Nass; yaani tamko la wazi linalotolewa na Mtume (s.a.w.w) au tamko la Imamu aliyepita kuhusiana na Uimamu wa mtu atakayefuata baada yake.[34] Kuna mapokezi mengi kutoka kwa Imamu Kadhim (a.s), yanayopatikana katika vitabu vya Hadithi vya Kishia, ambayo ndani yake Imamu Kadhim (a.s) amebainisha wazi kabisa kuhusiana na Uimamu wa Imamu Ridha (a.s). Kwa mfano, katika vitabu vya al-Kafi,[35] al-Irshad,[36] I'ilam al-Wara,[37] na Biharu al-Anwar,[38] kuna milango maalum iliyotengwa kwa ajili ya Nass zinazohusiana na Uimamu wa Imamu Ridha (a.s), ambapo Hadithi zote zinazofungamana na suala hilo zimekusanywa pamoja ndani ya mlango huo.

Kwa mfano, Al-Kulaini amesimulia Hadithi fulani ambayo ndani yake Dawud al-Raqqi alimuuliza Imamu Kadhim (a.s) kuhusu Imamu atakayeshika hatamu baada yake, naye (Imamu) akamnyoshea kidole Imamu Ridha (a.s) na kusema: "Huyu ndiye kiongozi wenu baada yangu."[39] Sheikh Mufid naye pia, amepokea Hadithi nyingine kutoka kwa Muhammad bin Ishaq aliyesema kuwa: "Nilimuuliza Imamu Kadhim (a.s) iwapo anaweza kuniambia ni nani ninayepaswa kuchukua misingi ya dini yangu kutoka kwake? Naye akanijibu akisema: Kutoka kwa mwanangu Ali (Imamu Ridha); kwani kuna siku baba yangu (Imamu Sadiq) alinishika mkono akanipeleka mbele ya kaburi la Mtume (s.a.w.w) kisha akaniambia: Mwanangu, Mwenyezi Mungu ametamka akisema kuwa, Mimi nitaweka kiongozi (khalifa) katika ardhi,[40] na hakika Mwenyezi Mungu anapotoa ahadi Yake, huitimiza."[41]

Kipindi cha Uimamu

Kipindi cha mwanzo cha Uimamu wa Imamu Ridha (a.s) kilisadifiana na ukhalifa wa Harun al-Rashid, ambaye ni muuaji aliyemuua Imamu Kadhim (a.s). Kwa mujibu wa watafiti, Harun al-Rashid, hakuwa akimfanyia bughudha wala kumghasi Imamu Ridha (a.s), hiyo kutokana na hofu ya kutokea madhara na athari kutokana na mauaji ya Imamu Kadhim (a.s). Kwa hiyo, Imamu Ridha (a.s) alikuwa na uhuru mkubwa zaidi, ambapo hakuwa akifanya Taqiya (kuficha itikadi), bali alikuwa akiwalingania watu waziwazi kuelekea kwenye Uimamu wake.[42]

Al-Kulaini amesimulia Hadithi fulani katika kitabu cha al-Kafi, ambayo ndani yake Muhammad bin Sinan anamwambia Imamu Ridha (a.s) kwamba: "Wewe, kwa ulinganifu wako wa wazi kabisa kuelekea kwenye Uimamu, umepelekea uwe unatajwa midomoni mwa watu na hivyo kujiweka katika hatari ya kuuawa." Imamu Ridha (a.s) naye akamjibu akisema: "Kama vile Mtume (s.a.w.w) alivyokuwa akisema kwamba; iwapo Abu Jahl atapunguza unywele mmoja tu kutoka katika kichwa changu, basi mshuhudie kuwa mimi si Mtume, na mimi pia nakuambieni kwamba; iwapo Harun atapunguza unywele mmoja tu kutoka katika kichwa changu, basi mshuhudie kuwa mimi si Imamu wa haki."[43]

Kuibuka kwa Kundi la Waqifia

Kwa mujibu wa maelezo ya Rasul Jafariyan, ambaye ni mtafiti wa masuala ya kihistoria, ni kwamba; baada ya kuuawa shahidi Imamu Kadhim (a.s), na kwa sababu ya mambo kadhaa kama vile; kuwepo kwa mazingira ya Taqiya, fursa zilizotumiwa na baadhi ya watu ambao walikuwa na mali za Imamu Kadhim (a.s) mikononi mwao, pamoja na kuwepo kwa baadhi ya mapokezi yasiyo sahihi, kuliibua mivutano na hitilafu kubwa miongoni mwa Waislamu wa Kishia kuhusiana na nani atakayeishika hatamu baada ya Imamu Kadhim (a.s).[44] Katika mivutano hiyo, kundi fulani liliibuka miongoni mwa Mashia likidai kwamba Imamu Kadhim (a.s) hajafa, na kwamba yeye ndiye Mahdi aliyeahidiwa. Kundi hili liliishia kupata umaarufu kwa jina la Waqifia.[45] Hata hivyo, Masahaba wengi wa Imamu Kadhim (a.s) walikubaliana na Uimamu wa Imamu Ridha (a.s), na wala hawakuwa na upinzani dhidi yake.[46]

Urithi wa Kiti cha Enzi (Waliyyu-l-ahd)

Makala Kuu: Urithi wa Kiti cha Enzi wa Imamu Ridha (a.s)

Urithi wa kiti cha enzi wa Imamu Ridha (a.s) unachukuliwa kuwa ndilo tukio muhimu zaidi katika kipindi cha maisha yake ya kisiasa.[47] Tukio hili ni miongoni mwa masuala yanayoibua mivutano na mijadala mikubwa katika historia ya Kiislamu, jambo ambalo lina changamoto kubwa katika upande wa kisiasa na hata kielimu na kiitikadi (kwani suala la yeye kukubali kuwa mrithi wa kiti cha enzi kunagongana au kunakinzana naye isma yake).[48][49]

Sarafu ya uteuzi wa Imamu Ridha (a.s) kama mrithi wa ukhalifa, iliyochapwa kwa amri ya Ma'amun. Kwenye sarafu hiyo kuliandikwa kwa hati za Kufi maneno yafuatayo: «Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Muhammad Mtume wa Mungu, Ma'mun Khalifa wa Mungu, Miongoni mwa aliyoamuru Amir ni kwamba Ridha ni mrithi wa ukhalifa wa Waislamu, Ali bin Musa bin Ali bin Abi Talib, na ni Dhu al-Riyasatain (mwenye hadhi mbili).»

Vyovyote iwavyo, kwa amri ya Maamun, Imamu Ridha (a.s) alihamishwa kutoka mji wa Madina kwenda mji wa Marw uliopo mkoani Khorasan, mji ambao ulikuwa ni mji mkuu wa serikali ya Maamun. Kabla ya kumpa nafasi hiyo ya urithi wa kiti cha enzi, kwanza kabisa Maamun alimpa Imamu ofa ya kumkabidhi ukhalifa mzima; lakini Imamu Ridha (a.s) alikataa kuipokea ofa hiyo kwa nguvu zote. Baada ya hapo, Maamun alimtaka Imamu awe mrithi wa kiti chake cha enzi (waliyyu al-ahd), huku akimtishia kuwa iwapo hatakubali suala hilo, basi atamuua. Hapo ndipo Imamu Ridha (a.s) alipoamua kukubali kwa kulazimika kufanya hivyo bila ya hiari; hata hivyo, aliweka sharti thabiti la kutojihusisha wala kuingilia kati kwa namna yoyote ile masuala ya kiserikali na ya kiongozi.[50]

Wanazuoni wa Kishia wanasema kuwa, Maamun alikteua Imamu kuwa mrithi wa kiti cha enzi, kwa malengo ya kumweka Imamu huyo chini ya uangalizi na ulinzi wake mkali.[51] Hiyo ni kwa ajili ya kudhibiti na kuzima harakati na mapinduzi ya Maalawi (wafuasi wa kizazi cha Ali),[52] pamoja na kuipa uhalali serikali na ukhalifa wake haramu.[53] Maamun alifanya sherehe rasmi za kumtawaza Imamu kuwa mrithi wa kiti cha enzi mnamo tarehe 7 ya mwezi wa Ramadhani, mwaka wa 201 Hijiria, ambapo wananchi pamoja na viongozi na watendaji wa serikali walimlia kiapo cha utiifu (bai’a) Imamu.[54] Tangu wakati huo, kwa amri ya Maamun, khutba zilianza kusomwa kwa kutaja jina la Imamu, na sarafu zikaanza kuchapwa zikiwa na jina lake.[55] Inasemekana kuwa, Imamu Ridha (a.s) alitumia fursa hiyo adhimu iliyojitokeza kwa manufaa ya Ushia, na aliweza kubainisha na kueneza kwa umma wa kawaida maarifa mengi sana ya Ahlul Bait (a.s).[56]

Sarakhs
Quraitain
Hausajah
Nabaj
Behbahan
Abarkuh
Istakhr
Deh Shir
Kharanaq
Ribat Posht-e Badam
Damghan
Ahuwan
Simnan
Nayin
Dezful
Kermanshah
Njia ya safari inayojulikana
Njia ya safari isiyojulikana sana
Ripoti zisizo sahihi
Qadamgah
Njia ya safari ya Imam Ridha (a.s.)
kutoka Madina hadi Marw


Maelezo Juu ya Hadithi ya Silsilat al-Dhahabi

Makala Kuu: Hadithi ya Silsilat al-Dhahabi

Hadithi ya Silsilat al-Dhahabi, au "Mnyororo wa Dhahabu," ni mashuhuri iliyopokewa na wanazuoni kadhaa akiwemo Sheikh Tusi. Hadithi hii ni ile Hadithi ya Qudsi iliyosimuliwa na Imam Ridha (as) wakati wa safari yake kupitia Nishapur.[57] Hadithi hii iliyopata umashuhuri kupitia jina la “حدیث سلسلة الذهبی” (Hadithi ya Mnyororo au Mlolongo wa Dhahabu), ilisimuliwa na Imamu Ridha (a.s) baada ya wakazi wa mji huo kumtaka awasimulie Hadithi fulani watakayeweza kufaidika na mafunzo ya dini ndani yake.[58] Wanazuoni wameeleza kwamba; yawezekana Hadithi hii ilipewa jina la Silsilat adh-Dhahabi kutokana na ukweli wa kwamba, wapokezi wote wa Hadithi hii ni wasafi wasio na dosari, ambao ni kuanzia Imamu hadi na kuishia kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe. Wengine wamesema kuwa, iliitwa hivyo kwa sababu mmoja wa watawala wa ukoo wa Wasamani aliandika Hadithi hiyo kwa wino wa dhahabu na akausia izikwe pamoja naye baada ya kufariki kwake dunia.[59]

Kwa mujibu wa riwaya ya Shaykh Saduq, matini ya Hadithi ya Silsilat adh-Dhahab ni kama ifuatavyo:

Hadithi ya Silsilat adh-Dhahab

اللَّه َ عَزَّ وَ جَل‏ یقُولُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ حِصْنِی فَمَنْ دَخَلَ حِصْنِی أَمِنَ مِنْ عَذَابِی قَالَ فَلَمَّا مَرَّتِ الرَّاحِلَةُ نَادَانَا بِشُرُوطِهَا وَ أَنَا مِنْ شُرُوطِهَا


Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Mwenye Ezi, amesema:

"Laa ilaaha illa Allah ni ngome Yangu. Basi yeyote atakayeingia katika ngome Yangu atasalamika kutokana na adhabu Yangu."Na pale msafara ulipoanza kuondoka, Imam Ridha (a.s.) alitunadia (alitupazia sauti) akisema: "Lakini ni kwa masharti yake (yaani si Laa ilaaha illa Allah kavu kavu tu, bali ni kwa masharti yake maalumu); nami ni miongoni mwa masharti yake."


Sala ya Eid al-Fitri

Makala Kuu: Sala ya Eid al-Fitr ya Imam Ridha (a.s.)

Tukio la Sala ya Eid al-Fitr ya Imam Ridha (a.s.) limeripotiwa katika vitabu kadhaa vya Hadithi kikiwemo kitabu cha al-Kafi na Uyunu Akhbar al-Rida.[61] Kwa mujibu wa report ya Hadithi hii, baada ya Imam Ridha kupewa urithi wa kiti cha ufalme (Wilayat al-Ahd), Maamun alimtaka aongoze Sala ya Eid al-Fitr. Hata hivyo, Imam alimkumbusha Maamun sharti lake la msingi aliloliweka wakati wa kukubali urithi huo, nalo ni kutojihusisha kabisa na mambo ya ukhalifa, na hivyo akaikataa amri hiyo. Ila baada ya Ma'mun kushikilia matakwa hayo kwa msisitizo, Imam akamwambia: "Basi mimi nitaelekea kusali sala hii kama alivyokuwa akiisali Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Imam Ali (a.s.)," Maamun naye akakubali na kuridhika na maamuzi hayo.[62]

Asubuhi ya siku ya Eid, Imam Ridha (a.s.) alikoga, akajifunga kilemba cheupe kichwani mwake, kisha akatoka nje akiwa miguu tupu (bila ya viatu), huku akiwa amefuatana na Masahaba zake, na akaanza kuleta takbira. Baada ya hapo, alianza kushika njia huku watu mbalimbali wakiambatana naye. Kila baada ya hatua kumi, alikuwa akisimama na kuleta takbira mara tatu. Mji mzima ulikumbwa na mguso mkubwa kutokana na mwenendo huu wa Imamu, kiasi kwamba ukajawa na vilio na dhoruba za majonzi. Habari hizi zikamfikia Maamun masikioni mwake. Fadhlu bin Sahl, aliyekuwa waziri wa Maamun, alisimama na kumwambia khalifa wake akisema: "Ikiwa Ridha atafika mahali pa kusalia sala ya Idi hali akiwa katika hali hii, basi watu wa mji huu wataungana naye na watakuasi na kuuasi utawala wako. Jambo la usalama ni kumtuma mtu amwamrishe kurejea makazini mwake." Kwa muktadha huo, Maamun alituma mtu aende kwa Imamu na kumwomba arudi nyumbani. Imamu naye akavaa viatu vyake na kurejea nyumbani kwake.[63]

Rasul Jafarian, ambaye ni mtafiti na mwanahistoria mashuhuri, amelitaja tukio hili kuwa ni miongoni mwa sababu muhimu zilizochochea mfarakano na kuharibika kwa uhusiano kati ya Maamun na Imam Ridha (a.s.).[64]

Athari ya Imam Ridha nchini Iran

Makala Kuu: Safari ya Imam Ridha (a.s.) kuelekea Marw

Imam Ridha (a.s.) ndiye Imamu pekee miongoni mwa Maimamu wa Kishia aliyezikwa katika ardhi ya Iran.[65] Rasul Jafarian analitaja jambo la kuwasili kwa Imam Ridha nchini Iran kuwa ni miongoni mwa sababu kuu zilizochochea kusambaa kwa Ushia ndani ya nchi hiyo. Yeye anamnukuu Sheikh Saduq akieleza kwamba; Jambo muhimu lililodhihiri katika mtiririko wa safari ya Imam Ridha ya kutoka Madina kuelekea Marw, ni kwamba; katika kila mji wa Iran aliyoukifikia na kuweka makazi ndani yake, watu walikuwa wakimiminika na kumwendea ili kumwuliza maswali yao mbalimbali, naye Imamu Ridha (a.s.) alikuwa akiwapa majibu kulingana na Hadithi ambazo silsila ya wapokezi wake (yaani mnyororo wa mapokezi) ilikuwa inaishia na Maimamu wa nyuma yake, hadi kufikia kwa Imam Ali (a.s.) na hatimaye kuishia kwa bwana Mtume (s.a.w.w.). Suala la kuwarejesha huku watu kwa Maimamu, kulikuwa ni miongoni mwa sababu muhimu za kupanuka kwa fikra za Kishia ndani ya maeneo hayo.[66]

Kwa mujibu wa maelezo ya Rasul Jafarian ni kwamba; uwepo wa Imamu katika ardhi ya Khorasan uliwafanya watu wapate kuitambua zaidi shakhsia yake kama Imamu wa Mashia, na jambo hili liliwafanya wapenzi wa Ushia kuongezeka siku hadi siku. Yeye anaitaja nafasi ya kielimu ya Imamu pamoja na kuwa kwake miongoni mwa Alawiyyin (wazawa watukufu wa Imam Ali), kuwa ndiyo nguzo na muhimu zaidi katika kupanuka kwa madhehebu ya Ushia nchini Iran.[67]

Hali kadhalika, kushiriki kwa Imamu (a.s) katika mijadala ambayo Maamun alikuwa akiichochea na kuiandaa kati ya Imamu na wapinzani wake katika masuala ya Uimamu na Utume, kulikopelekea ufaulu wa hali ya juu (pamoja na ushindi) wa Imamu katika mijadala hiyo, kulidhihirisha shakhsia kubwa ya kielimu ya Imamu mbele ya macho ya watu. Moja ya ushahidi katika uwanja huu ni Hadithi aliyoipokea Sheikh Saduq, ambapo kwa mujibu wa Hadithi hiyo, Maamun alifikishiwa habari isemayo kwamba, Imam Ridha anafanya vikao vya kielimu na vya fani ya Kalam (theolojia) na watu wanavutiwa naye sana (huku wakivutika kwake), jambo ambalo lililomfanya Maamun kutoa amri ya kuwafukuza na kuwatoa watu katika vikao hivyo vya Imamu.[68]

Kuna majengo kadhaa katika miji ya mbalimbali ya Iran yakiwemo; mabafu, misikiti, na maeneo yenye alama za mapito (Qadamgah—ambayo ni sehemu inayosadikiwa kukanyagwa na Imamu Ridha). Maeneo hayo ambayo yalikuwa ni vituo vya makazi yake katika mtiririko wa safari yake kuelekea Marw, yanatambulikana kama ni nembo maalumu ya Imam Ridha (a.s). Jafarian analitaja jambo hili kuwa ni miongoni mwa ushahidi wa wazi wa athari za kuwasili kwa Imamu Ridha (a.s) nchini Iran, zilizopelekea kupanuka kwa Ushia ndani ya nchi hiyo.[69] Miongoni mwa majengo hayo maarufu, ni Msikiti wa Imam Ridha (a.s) uliopo katika mji wa Ahwaz, na maeneo yenye alama za miguu (Qadamgah) zinazonasibishwa kwake (a.s). Maeneo yanayonasibishwa na Imamu Ridha (a.s) yanapatikana katika miji mbalimbali nchini Iran. Miongoni mwa maeneo hayo ni yale yaliyopo Shushtar, Dezful, Yazd, Damghan, Nishapur, pamoja na Bafu la Ridha (a.s) lililoko mjini Nishapur.[70] Jafarian ameandika akisema kwamba; ijapokuwa uhusiano wa baadhi ya maeneo haya na Imamu Ridha unaweza ukawa si sahihi (mbele ya uhakiki wa kihistoria), lakini unadhihirisha wazi mapenzi makubwa na mfungamano wa Kishia walionao watu wa Iran.[71]

Namna ya Kuuawa Shahidi

Sala na Salamu Maalumu

اللّهُمَّ صَلِّ عَلَی عَلِی بْنِ مُوسَی الرِّضَا الْمُرْتَضَی الْإِمامِ التَّقِی النَّقِی وَحُجَّتِک عَلَی مَنْ فَوْقَ الْأَرْضِ وَمَنْ تَحْتَ الثَّرَی الصِّدِیقِ الشَّهِیدِ صَلاةً کثِیرَةً تامَّةً زاکیةً مُتَواصِلَةً مُتَواتِرَةً مُتَرادِفَةً کأَفْضَلِ مَا صَلیتَ عَلَی أَحَدٍ مِنْ أَوْلِیائِک.


Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu na Mbariki Ali ibn Musa ar-Ridha, Imamu Mteule, mchamungu, msafi na asiye na dosari; hoja Yako juu ya wote walioko juu ya ardhi na walioko chini yake; mkweli na shahidi. Mpe rehema na baraka nyingi, kamilifu, safi, endelevu zisizokatika, zinazofuatana kwa mfululizo, kama ulivyomshushia rehema na baraka bora zaidi yeyote yule uliyewahi kumteremshia miongoni mwa mawalii Wako.

Kuna ripoti na simulizi tofauti zinazopatikana katika vyanzo vya historia kuhusiana na namna ya kuuawa shahidi kwa Imamu Ridha (a.s.). Sayyid Ja'afar Murtadha Amili, ambaye ni mtafiti mashuhuri wa masuala ya kihistoria, ameandika kwamba; wanazuoni wa Kishia, isipokuwa wachache mno miongoni mwao, wana mwafaka na makubaliano ya pamoja (itifaki) ya kwamba Imamu Ridha (a.s.) aliuawa shahidi kufuatia amri ya Maamun. Hali kadhalika, idadi kubwa ya wanazuoni pamoja na wanahistoria wa mrengo wa Ahlu Sunna nao pia wanaamini, au wanaona kuna uwezekano mkubwa zaidi, wa kwamba Imamu (a.s) hakufariki duniani kwa kifo cha kawaida.[72]

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa yaliyomo ndani ya kitabu cha Tarikh al-Ya'qubi (kilichotungwa katika karne ya 3 H), ni kwamba; Maamun aliondoka kutoka mji wa Marw kwa nia ya kuelekea Baghdad, na akamchukua Imamu Ridha (a.s) ambaye alikuwa ndiye mrithi wa kiti cha ufalme, ili awe pamoja naye katika safari hiyo.[73] Baada ya kuwasili kwao katika ardhi ya Tus, Imamu Ridha (a.s.) alishikwa na maradhi, na baada ya kupita siku tatu, alifariki dunia akiwa katika kijiji kimoja kinachojulikana kwa jina la Nuqan. Mwandishi huyo huyo anaendelea kuandika akieleza kuwa; inasemekana kwamba, Ali bin Hisham, aliyekuwa jemadari na kiongozi wa kijeshi wa Maamun, alimpa sumu Imamu kupitia tunda la komamanga.[74] Naye At-Tabari, ambaye ni mwanahistoria wa upande wa Ahlu Sunna, katika kitabu chake cha historia, hakutoa maelezo kamili kuhusiana na tukio hili, bali ameripoti tu akisema kwamba, Imamu alikuwa katika hali ya kula tunda la zabibu na ghafla akakata roho na kufariki dunia.[75]

Sheikh Mufid, ambaye ni mwanatheolojia na faqihi mkuu vya Kishia, katika kitabu chake cha Tashih al-I'tiqad, amezungumzia suala la kuuawa kwa Imamu Ridha (a.s.) kwa kuonesha aina fulani ya kusitasita (shaka); ila pamoja na hayo, ameongeza katika maelezo yake hayo akisema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kwamba Imamu huyo aliuawa kwa sumu.[76] Hata hivyo, katika kitabu chake chengine kiitwacho al-Irshad, amepokea riwaya inayoeleza wazi kwamba; Imam Ridha alipewa sumu kupitia kinywaji cha maji ya komamanga, kulikotendeka kufuatia amri thabiti ya Maamun.[77] Sheikh Saduq naye amepokea Riwaya kadhaa ambazo kwa mujibu wa msingi wa mapokezi hayo, Maamun alimpa sumu Imam Ridha (a.s.) kwa kutumia tunda la zabibu, au komamanga, au kwa kuyachanganya matunda mawili hayo kwa pamoja.[78] Ili kuthibitisha kuuawa kwake shahidi, pia hutumiwa Riwaya isemayo "Hakuna yeyote miongoni mwetu (Maimamu) isipokuwa huuawa shahidi," Hadithi ambayo inafungamana na kuuawa shahidi kwa Maimamu wote wa Kishia.[79]

Sheikh Mufid katika kitabu chake cha Masar al-Shi'ah, anaona kwamba tukio la kuuawa shahidi kwa Imam Ridha (a.s.) lilijiri katika siku ya tarehe 23 ya mwezi wa Dhul-Qa'dah mwaka 203 H.[80] Kwa kufuatia mnasaba huo, kuna kauli kadhaa za wanazuoni zinazosisitiza kumzuru Mtukufu huyo katika siku hii maalumu (tarehe 23 ya mwezi wa Dhul-Qa'dah).[81] Aidha, baadhi ya wasomi wameitaja siku ya Ijumaa, tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuwa ndiyo siku hasa aliyouawa shahidi Imamu huyu muadhamu.[82]

Haramu ya Imam Ridha

Makala Kuu: Haramu ya Imam Ridha (a.s.)

Baada ya kuuawa shahidi kwa Imamu Ridha (a.s), Maamun aliamuru huyo azikwe katika bustani au jumba la utawala (Dar al-Amarah) la Humaid bin Qahtabah al-Ta'i, aliyekuwa mmoja wa makomanda na majemadari wa mrengo wa Kiabbasi, karibu na kijiji cha Sanabad. Kabla ya tukio hili, Harun al-Rashid, aliyekuwa khalifa wa Kiabbasi na baba mzazi wa Maamun, alikuwa amezikwa mahali hapo, jambo lililolifanya eneo hili kupata umaarufu wa jina la Kuba la Haruniyyah (Baq'atu al-Haruniyyah).[83] Imamu Ridha (a.s.) ndiye Imamu pekee miongoni mwa Maimamu wote wa Kishia aliyezikwa katika ardhi ya Iran.[84]

Iran, Mash'had, Haram ya Imamu Ridha (a.s)

Watafiti wameandika wakieleza kwamba; katika kipindi chote cha karne nyingi zilizopita, kaburi la Imam Ridha (a.s.) lilikuwa likipendwa na kuheshimiwa sana na Waislamu wote wa maeneo ya Khorasan, na mbali na Mashia wenyewe, hata waumini wa upande wa Ahlu Sunna nao pia walikuwa wakienda kufanya ziara (kumzuru) katika kaburi la Imamu huyo muadhamu (a.s).[85]

Kaburi la Imamu Ridha (a.s.) lilibadilika hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa ni miongoni mwa maeneo makuu ya ziara (haramu takatifu) katika ulimwengu wa Kiislamu, na hasa kwa upande wa madhehebu ya Shia. Suala la kumzuru Imam Ridha (a.s) imekuwa ni miongoni mwa itikadi misingi na muhimu zaidi katika mzunguko wa maisha ya watu mbalimbali. Mahali hapo alipozikwa Imamu Ridha (a.s), palipata umaarufu mkubwa chini ya jina la Mash'had ar-Rida (sehemu aliyofia shahidi Imamu Ridha), eneo ambalo kwa hivi sasa linajulikana kwa jina la mji wa Mash'had. Inasemekana kwamba; kufuatia mwitikio mkubwa sana na mfululizo wa watu wanaomiminika kwenda kumzuru Imamu Ridha (a.s.), mji wa Mashhad umekuwa ni mji wa pili duniani miongoni mwa miji ya kihistoria unaopokea watu wengi zaidi kiidadi wanaomiminika kwa ajili ya amali hiyo ya ibada ya kumzuru Imamu Ridha (a.s) na kutafuta baraka zake mbalimbali maishani mwao.[86]

Masahaba wa Imamu Ridha

Makala Kuu: Orodha ya Masahaba wa Imamu Ridha (a.s)

Sheikh at-Tusi ametaja majina ya takriban watu 320 katika kitabu chake cha fani au elimu ya Rijal (elimu ya uhakiki wa wapokezi wa Hadithi), akiwahisabu kuwa ni miongoni mwa Masahaba wa Imamu Ridha (a.s).[87] Ni vyema tukaelewa kwamba, kuna idadi tofauti zilizotajwa katika vyanzo na marejeo mengineyo kuhusiana na idadi ya Masahaba hao.[88] Muhammad Mahdi Najafi amekusanya jumla ya majina ya watu 831 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Kishia wakiwemo wapokezi wa Hadithi pamoja na masahaba wa Imam Ridha (a.s.). Orodha hii inapatikana katika kitabu chake kiitwacho al-Jami' li-Ruwat Ashab al-Imam ar-Rida.[89] Wafuatao ni Baadhi ya Masahaba wa Imamu (a.s), kwa mujibu wa mapokezi na nakala ya Sheikh at-Tusi:

Muhammad bin Omar al-Kashshi amewataja watu sita miongoni mwa Masahaba wa Imam Ridha (a.s.) kuwa ni kundi maalumu la "As’hab al-Ijma'" (yaani kundi la Masahaba waliokubaliwa kwa kauli moja kuhusu ukweli wao). Kundi la watu hao ni: Yunus bin Abdul-Rahman, Safwan bin Yahya, Ibn Abi 'Umair, Abdullah bin Mughirah, Hasan bin Mahbub, pamoja na Ahmad bin Abi Nasr al-Bazanti.[91]

Vitabu Vinavyonasibishwa Naye

Mbali na Hadithi mbalimbali zilizopokewa kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) zinazopatikana ndani ya vitabu mbalimbali vya Hadithi, pia kuna kazi kadhaa andishi na baadhi ya vitabu vinavyonanasibishwa na Imamu Ridha (a.s). Jambo muhimu lililodhihiri katika uwanja huo ni kwamba; wanazuoni wengi wa Kishia wana aina fulani ya kusitasita (shaka) na mashaka makubwa kuhusiana na usahihi wa kunasibishwa kwa kazi mbalimbali andishi na Imamu Ridha (a.s). Vifuatavyo ni vitabu vinavyonasibishwa naye (a.s):

Risala ya Dhahabu (al-Risalatu al-Dhahabiyyah), inayojulikana pia kama Tiba ya al-Ridha, ni miongoni mwa kazi andishi zinazonasibishwa na Imam Ridha (a.s).
  1. Tibbu ar-Ridha au Risala adh-Dhahabiyyah (Ujumbe wa Dhahabu): Kitabu hicho ni kitabu kinachohusiana na fani ya tiba. Watafiti wameandika wakieleza kwamba; Tibbu ar-Ridha kililipata umaarufu mkubwa miongoni mwa wanazuoni wa Kishia na wengi wao walikipokea na kukikubali na kukitambua kama ni kazi yake (a.s).[92]

2. Sahifat ar-Ridha: Kitabu hichi kimeandikwa kuhusiana na fani ya Fiqhi (sheria za Kiislamu). Idadi kubwa ya wanazuoni wa Kishia hawajathibitisha wala kuridhika na suala la kunasibishwa kwa kitabu hiki kwa Imam Ridha (a.s).[93]

3. Al-Fiqhu ar-Radhawiy: Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Muhammad Jawad Fadhlullah, wanazuoni wengi wa Kishia wamekataa na hawajakubali kabisa kunasibishwa kwa kitabu hiki na Imamu Ridha (a.s). Ila pamoja na hayo, katika mtiririko wa maoni hayo, kuna kundi la wasomi akiwemo; Muhammad Baqir al-Majlisi, Muhammad Taqi al-Majlisi, Bahr al-Ulum, Yusuf al-Bahrani (anayejulikana zaidi kama Sahib al-Hada'iq), pamoja na Muhaddith al-Nuri ambao wanaamini kuwa kitabu hiki ni kazi andishi ya Imamu Ridha (a.s).[94]

4. Mahdhu al-Islam wa Sharas'iu ad-Din: Taarifa ya kitabu hiki kimepokewa na Sheikh Saduq kutoka kwa Fadhlu bin Shadhan; lakini kutokana na kutothibitika kwa uaminifu wa baadhi ya wapokezi waliopo kwenye silsila (mlolongo) wa mapokezi wake, hali kadhalika kuwepo kwa mambo na maudhui yanayopingana wazi na hukumu thabiti za kifikhi, imepelekea watafiti kutokuwa na uhakika wala utulivu wa moyo juu kuwepo kwa uhusiano kati ya kitabu hicho na Imam Ridha (a.s).[95]

Mijadala (Midahalo) ya Imamu Ridha

Kwa mujibu wa maelezo ya Rasul Jafariyan ni kwamba; katika zama za Imam Ridha (a.s), mijadala na makongamano ya elimu ya kiitikadi (Ilmul-Kalam) ilikuwa imeenea kwa kiwango kikubwa mno miongoni mwa Waislamu wa zama hizo. Pia kulikuwa na mivutano pamoja na tofauti kubwa za kifikra kati ya makundi ya Waislamu mbalimbali. Makhalifa wa Bani Abbas, hususan Maamun, nao pia walikuwa wakiingia na kushiriki katika mijadala hiyo. Kwa sababu hiyo, idadi kubwa ya Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) zinahusiana na uwanja wa elimu ya kiitikadi (Ilmul-Kalam), ambazo zimekuja kwa mtindo wa maswali na majibu au mijadala ya ana kwa ana. Miongoni mwa maelezo yaliyomo kwenye mijadala hiyo, ni maudhui zinayohusiana na Uimamu, Tawhidi (Umoja wa Mwenyezi Mungu), Sifa za Mwenyezi Mungu, pamoja na suala la Jabri na Ikhtiyari (kulazimishwa au kuwa na hiyari kwa mwanadamu).[96]

Mchoro wa picha ya Imamu Ridha (a.s), anayejulikana kwa lakabu ya "Mwanazuoni wa Familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.)".

Baada tu ya kuwasili kwa Imamu Ridha (a.s) katika mji wa Marw, Maamun alianza kuandaa vikao na makongamano kadhaa ya kielimu yaliyohudhuriwa na wanazuoni pamoja na wasomi wa fani mbalimbali, na siku zote alikuwa akimuomba Imamu Ridha (a.s) kushiriki katika vikao hivyo.[97] Katika vikao hivyo, Imam Ridha (a.s) alifanya mijadala mingi na wanazuoni wa dini na madhehebu mbalimbali, na matini za mijadala hiyo zimenakiliwa ndani ya vitabu vya Hadithi vya Kishia. Miongoni mwa vitabu maarufu vilivyonukuu mijadala hiyo ni pamoja na; kitabu cha Al-Kafi kilichoandikwa na Kulaini, kitabu cha At-Tawhid na Uyunu Akhbar ar-Rida vilivyotungwa na Sheikh Saduq, pamoja na kitabu cha Al-Ihtijaj cha Ahmad bin Ali Tabarsi. Baadhi ya mijadala iliyoripotiwa vitabuni humo ni kama ifuatavyo:

Imepokewa kutoka kwa Sheikh Saduq kwamba lengo la Maamun katika kuandaa vikao hivi vya mijadala, ni kumfanya Imamu Ridha (a.s) ashindwe mbele ya wakuu wa madhehebu na makundi mbalimbali, ili kuidhoofisha hadhi yake ya kielimu na kijamii mbele ya jamii yake; hata hivyo, kila mtu aliyejaribu kufanya mjadala na Imamu Ridha (a.s), hatimaye alikiri juu ya ukubwa wa hadhi yake ya kielimu pamoja na kukubaliana na hoja zake thabiti.[105]

Nafasi Yake Mbele ya Ahlu Sunna

Ibn Hajar al-Asqalani, ambaye ni mwanahadithi na mwanahistoria mkubwa wa mrengo wa Ahlu Sunna, amesifu na kutukuza nasaba, elimu, na fadhila za Imamu Ridha (a.s).[106] Miongoni mwa report za mwanazuoni huyu, ni ile isemayo kwamba; wakati Imamu Ridha (a.s) akiwa na umri wa miaka ishirini na ushei tu, alikuwa tayari ameshaanza kutoa fatwa ndani ya Msikiti wa bwana Mtume (Msikiti wa Madina) (s.a.w.w).[107] Hali kadhalika, Al-Yafi'i, ambaye pia ni miongoni mwa wanazuoni wa Ahlu Sunna wa karne ya nane Hijriya, amemtaja Imamu Ridha (a.s) kwa kutumia lakabu za kiongozi "Mtukufu" (Jalil) na "Mwenye Kuheshimiwa Sana" (Mu'adhdham), na akamtambua kama mmoja wa Maimamu Kumi na Mbili wa madhehebu ya Imamiyyah; huku akiongeza kwa kusema kuwa, Maamun hakuona mtu yeyote bora na mwenye haki zaidi ya kupewa ukhalifa katika ukoo mzima wa Bani Hashim isipokuwa yeye (Imamu Ridha), ndio maana akaamua kumpa kiapo chake utiifu (Bai'ah).[108]

Baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Ahlu Sunna wa Turkmenistan wakiwa katika ziara ya kutembelea Nyumba ya Imamu Ridha (a.s) huko Marw.

Zaidi ya hayo, Al-Hakim al-Nishaburi, ambaye ni mwanahadithi na mwanasheria (Faqihi) wa madhehebu ya Shafi'i wa karne ya nne Hijriya, aliandika kitabu maalumu chenye jina la "Mafakhirur-Ridha" kinachohusiana na fadhila za Imamu Ridha (a.s). Kitabu hicho kwa bahati mbaya kimepotea na ni sehemu ndogo tu ndiyo iliyobaki, ambayo inapatikana ndani ya kitabu cha Al-Thaaqib fil-Manaaqib, kilichotungwa na Ibnu Hamzah al-Tusi.[109]

Jafarian amewatambulisha wanazuoni kadhaa wa Ahlu Sunna ambao hadi kufikia karne ya sita walikuwa na tabia ya kuenda kuzuru kaburi la Imamu huyu wa Nane (a.s). Miongoni mwa wanazuoni walioorodheshwa ndani ya orodha hiyo ya Jafarian ni; Abu Bakr Muhammad bin Khuzaimah (mwanahadithi wa Kisunni wa karne ya tatu na ya nne Hijriya), Abu Ali al-Thaqafi (miongoni mwa wanazuoni wa Nishabur), Abu Hatim Muhammad bin Hibban al-Basti ambaye ni mwanahadithi na mtaalamu wa sayansi ya wapokezi wa Hadithi (Ilmul-Rijal), Al-Hakim al-Nishaburi mwanahadithi mashuhuri, Abu al-Fadhl al-Baihaqi mwanahistoria mashuhuri wa Kiirani, pamoja na Imamu Muhammad al-Ghazali, mwanazuoni na mwanafalsafa mkubwa wa karne ya tano Hijriya.[110]

Pia kuna ripoti na masimulizi mbalimbali kutoka kwa wanazuoni wa upande wa Ahlu Sunna zinazohusiana na suala la kuzuru kaburi la Imamu Ridha (a.s). Kwa mfano; Ibn Hibban ameeleza akisema kwamba: "Nilikuwa nikienda mara kwa mara kulizuru kaburi la Ali bin Musa huko Mash'had, na kila nilipokuwa nikikabiliwa na matatizo, nilikuwa nikitawasali kupitia kwake, na Mungu naye alikuwa akiniondolea shida zangu."[111] Ibnu Hajar al-Asqalani naye ameripoti kuwa; Abu Bakar Muhammad bin Khuzaimah, pamoja na Abu Ali al-Thaqafi, wakiwa pamoja na kundi jengine la wanazuoni wa Ahlu Sunna, walikwenda kuzuru kaburi la Imamu Ridha (a.s). Mpokezi wa kisa hiki amemwambia Ibn Hajar kwamba: "Abu Bakar bin Khuzaimah alionesha utukuzaji mkubwa, unyenyekevu, na kulia kwa unyonge mbele ya lile kaburi (Buq'ah) kiasi ya kwamba alitufanya sote kubaki na mshangao."[112]

Kazi za Kisanaa na Kiutamaduni

Kuhusiana na Imamu Ridha (a.s), kuna athari (kazi) mbalimbali za kisanaa ambazo zimetengenezwa katika muundo wa mashairi, riwaya (riwaya andishi), filamu, picha za uchoraji, na kazi nyinginezo:

Kazi Andishi za Fasihi ya Kiushairi

Kuna idadi kubwa ya mashairi maalumu yaliyotungwa kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Imamu Ridha (a.s).[113] Kwa mujibu wa maelezo ya waandishi wa kitabu cha Madaihu al-Radhawiy dar Shi'ri Farsi (Sifa za Kiridha katika Mashairi ya Kiajemi) ni kwamba; inadhihirika wazi kuwa Sanai al-Ghaznawi, ambaye ni miongoni mwa washairi wa karne ya tano Hijriya, ndiye mshairi wa kwanza kabisa kutunga mashairi ya sifa (Madaihu) kwa ajili ya Imamu Ridha (a.s); na kama kulikuwa na mashairi mengine yaliyotungwa kabla yake kuhusiana na jambo hilo, basi aidha yamepotea au hayapatikani kwa hivi sasa.[114]

Kwa mujibu wa maoni ya waandishi wa kitabu hicho ni kwamba; hadi zama za Waseljuk na mwanzoni mwa Wasafawi, kulikuwa na mashairi machache mno kuhusiana na Imamu Ridha (a.s). Ila kuanzia zama za utawala wa Wasafawi, idadi hiyo iliongezeka kwa kiwango kikubwa mno.[115] Ndini ya kitabu cha Madaihu al-Radhawiy Dar-Shiri Farisi, kuna qasida mbalimbali kutoka kwa washairi 72 wanaozungumza lugha ya Kiajemi,[116] zilizotungwa kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Imamu Ridha (a.s). Kasida hizo zinahusiana na kuanzia zama za Sanai al-Ghaznawi hadi kufikia zama hizi za sasa.[117] Shairi la "Qit’eye az Behesht" (Kipande kutoka Peponi) ambalo ni kazi ya Habibullah Chaichiyan mwey lakabu ya kisanii ya Hassan,[118] pamoja na shairi la "Ba Ali Har ke Dar Oftad War Oftad" lililotungwa na Nasim Shimal, ambaye ni mwanachuoni na mshairi wa zama za vuguvugu la kikatiba (Mashrutiyat), ni miongoni mwa mashairi mashuhuri yanayomhusu Imamu huyu wa Nane (a.s).[119]

Kazi za Riwaya

Pia kuna kazi mbalimbali za riwaya andishi zilizoandikwa maalumu kwa ajili ya Imamu Ridha (a.s). Miongoni mwa riwaya hizo ni pamoja na; "Be Bolandiye An Radaa" (Kwenye Kilele cha Lile Joho) kazi ya Sayyid Ali Shojaei, "Oqyanoose Mashreq" (Bahari Kuu ya Mashariki) kazi ya Majid Pourwali Keleshteri, pamoja na riwaya ya "Raaze An Boye Shegeft" (Siri ya Ule Mvuto wa Harufu ya Kushangaza) kazi ya Fariba Kalhor.[120]

Kazi za Sanaa ya Uchoraji

Kuna kazi kadhaa za sanaa ya uchoraji zilizofanywa na wataalamu mbalimbali wa sanaa hiyo. Na picha mashuhuri ya uchoraji iliyozagaa ulimwenguni, ni ile ya "Dhamine Ahoo" (Mdhamini wa Paa), ambayo ni kazi ya sanaa iliyochorwa na Mahmoud Farshchian, inayosawiri na kuonesha kisa cha Imamu Ridha (a.s) cha kudhamini paa (kulungu). Kwa mujibu wa ripoti za baadhi ya mashirika ya habari ni kwamba; picha hii ya uchoraji ilitengenezwa katika matoleo mawili tofauti: toleo la kwanza lilichorwa mnamo mwaka 1358 Sh (sawa na mwaka wa 1979 Miladia), na toleo la pili lilichorwa mnamo mwaka 1389 Sh (sawa na mwaka 2010 Miladia), picha iliyochorwa na kutolewa kama zawadi iliyowasilishwa rasmi kwenye taasisi ya Astan Quds Razavi mjini Mash’had.[121]

Mchoro wa "Dhamin Aahuu" (Mdhamini wa Paa), kazi ya Mahmoud Farshchian.

Kongamano la Kimataifa

Kongamano la Kimataifa la Imamu Ridha (a.s) ni mjumuiko wa mfululizo wa makongamano na semina mbalimbali ambazo huandaliwa na kufanyika maalumu kwa ajili ya kujadili na kuangazia fadhila za Imamu Ridha (a.s).[122] Kongamano la kwanza kabisa miongoni mwa mfululizo wa makongamano hayo lilifanyika mnamo mwaka 1363 Sh (sawa na mwaka wa 1984 Miladia).[123] Imeelezwa kuwa; lengo kuu la kuanzishwa na kuundwa kwa kongamano hili, ni kuanzisha harakati thabiti za kielimu, kitamaduni, na kiutafiti katika uwanja wa kuwatambua na kuwatambulisha Maimamu Maasumu (a.s), hususan katika kueneza maarifa yanayomhusu Imamu Ridha (a.s).[124]

Tamasha la Kimataifa

Kwa mujibu wa report ya Taasisi ya Kimataifa ya Utamaduni na Sanaa zinazohusiana na Imamu Ridha (a.s) ni kwamba; Tamasha la Kimataifa la Imamu Ridha (a.s) huandaliwa na kufanyika mara moja kila mwaka. Tamasha hili huanza sambamba na kuanza kwa masiku ya "Dahe Karamat" (Muongo wa Ukarimu), chini ya Wizara ya Utamaduni nchini Iran. Tamasha hili hufanyika katika mikoa mbalimbali nchini Iran pamoja na baadhi ya nchi nyingine za kigeni. Tamasha hili lenye mwelekeo na mtazamo wa kielimu, kiutafiti, kitamaduni, pamoja na kisanaa; ambalo hutoa mwito wa kuwasilishwa kwa kazi mbalimbali katika nyanja hizo na kisha kuwatangaza washindi walioteuliwa.[125]

Mipango na programu za kimataifa za tamasha hili nje ya nchi, husimamiwa na kuendeshwa chini ya uratibu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu, kwa ushirikiano wa karibu na taasisi za kitamaduni zinazohusika na masuala ya nje ya nchi; hususan Taasisi ya Mikutano ya Kimataifa ya Ahlu-Bait (a.s), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (Al-Mustafa International University), pamoja na Kituo cha Shule za Nje ya Nchi.[126]

Rejea

  1. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 12-13.
  2. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 14, 16; Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 40.
  3. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 12-13.
  4. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 12.
  5. Amili, Al-Hayat al-Siyasiyyah li-al-Imam al-Radha, uk. 139-140.
  6. Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 41-42.
  7. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 13.
  8. Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 64-65.
  9. Angalia: Mir-Aqa'i, Zamen-e Ahoo wa Tajalli-ye an dar She'r-e Farsi, uk. 11-13.
  10. Majlisi, Bihar al-Anwar, Juz. 99, uk. 55.
  11. "Limadha-shtahara al-Imam al-Radha (a.s) bi-Gharib al-Ghuraba", Tovuti ya Khabargozari-ye Buratha (Shirika la Habari la Buratha).
  12. Amini, Al-Ghadir, Juz. 4, uk. 100.
  13. Dehkhoda, Loghatname-ye Dehkhoda, chini ya neno "Thamin al-A'immah".
  14. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 13.
  15. Suyuti, Tarikh al-Khulafa, uk. 363.
  16. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 13.
  17. Majlisi, Bihar al-Anwar, Juz. 49, uk. 3.
  18. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 21.
  19. Qurashi, Hayat al-Imam al-Radha, Juz. 1, uk. 25.
  20. Ibn Shahrashub, Manaqib, Juz. 4, uk. 366.
  21. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 492; Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 273.
  22. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 492.
  23. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 492; Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 273.
  24. Suyuti, Tarikh al-Khulafa, uk. 363; Ibn Shahrashub, Manaqib, Juz. 4, uk. 367; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 147.
  25. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 147.
  26. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 250; Sheikh al-Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 271; Ibn Shahrashub, Manaqib, Juz. 4, uk. 367; Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 86.
  27. Amin, A'yan al-Shiah, Juz. 2, uk. 13.
  28. Mostowfi, Nozhat al-Qolub, uk. 100.
  29. Kia Gilani, Siraj al-Ansab, uk. 179.
  30. Modarresi Tabataba'i, Bargi az Tarikh-e Qazvin, uk. 12.
  31. Sheikh al-Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 244.
  32. Shushtari, Tawarikh al-Nabi wa al-Aal, uk. 65.
  33. Sajjadi, Astane-ye Hazrat-e Ma'sumeh, uk. 358.
  34. Fazil Miqdad, Irshad al-Talibin, uk. 337.
  35. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 311-319.
  36. Sheikh al-Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 247-253.
  37. Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 43-52.
  38. Majlisi, Bihar al-Anwar, Juz. 49, uk. 11-28.
  39. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 312.
  40. Sura al-Baqarah, aya ya 30.
  41. Sheikh al-Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 249.
  42. Naji, Al-Radha, Imam.
  43. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 8, uk. 257-258.
  44. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 427-428.
  45. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 429.
  46. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 427.
  47. Eftekhari, Imam Reza (a.s), Ma'mun wa Mowdhu-e Velayat'ahdi, uk. 104; Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 430.
  48. Sayyid al-Murtadha, Tanzih al-Anbiya, uk. 179; Tusi, Talkhis al-Shafi, Juz. 4, uk. 206.
  49. Baghestani, Al-Radha, Imam (Velayat'ahdi), uk. 83.
  50. Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 259-260; Sheikh al-Saduq, Al-Amali, uk. 69-70.
  51. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 170.
  52. Amili, Al-Hayat al-Siyasiyyah li-al-Imam al-Radha, uk. 226.
  53. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 170.
  54. Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, Dar Sader, Juz. 2, uk. 448.
  55. Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, Dar Sader, Juz. 2, uk. 448.
  56. Rafiei, Zendegani-ye Imam Reza (a.s), Pazhouheshkade-ye Tahqiqat-e Islami, uk. 198-199.
  57. Saduq, Al-Tawhid, uk. 25; Saduq, Ma'ani al-Akhbar, uk. 371; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 135; Tusi, Al-Amali, uk. 589.
  58. Amoli, Misbah al-Huda, Juz. 6, uk. 221.
  59. Amoli, Misbah al-Huda, Juz. 6, uk. 221.
  60. Saduq, Ma'ani al-Akhbar, uk. 371; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 135.
  61. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 489-490; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 150-151.
  62. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 489; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 150.
  63. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 489-490; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 2, uk. 150-151.
  64. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 443.
  65. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 459.
  66. Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 219.
  67. Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 219.
  68. Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 219-220.
  69. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 463.
  70. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 463-467.
  71. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 463.
  72. Amili, Al-Hayat al-Siyasiyyah li-al-Imam al-Radha, uk. 422.
  73. Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, Dar Sader, Juz. 2, uk. 451.
  74. Ya'qubi, Tarikh al-Ya'qubi, Dar Sader, Juz. 2, uk. 453.
  75. Tabari, Tarikh al-Tabari, Juz. 7, uk. 610.
  76. Mufid, Tashih I'tiqadat al-Imamiyyah, uk. 132.
  77. Mufid, Al-Irshad, Juz. 2, uk. 270.
  78. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, uk. 246.
  79. Amili, Al-Sahih min Sirat al-Nabi al-A'dham, Juz. 33, uk. 182.
  80. Sheikh al-Mufid, Masar al-Shiah, uk. 34.
  81. Qummi, Muntaha al-Amal, Juz. 2, uk. 312; "Waqayi' al-Ayyam", uk. 97.
  82. Tabrisi, I'lam al-Wara, Juz. 2, uk. 41.
  83. Jafarian, Atlas-e Shiah, uk. 93.
  84. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 459.
  85. Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 228.
  86. Yahaghi, Radha (a.s) Imam.
  87. Sheikh al-Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 351-370.
  88. Kwa mfano angalia: Atardi, Musnad al-Imam al-Radha, uk. 509; Qurashi, Hayat al-Imam Ali bin Musa al-Radha, Juz. 2, uk. 86-180.
  89. Najaf, Al-Jami' li-Ruwat Ashab al-Imam al-Radha, uk. 571.
  90. Angalia: Tusi, Rijal al-Tusi, uk. 351-370.
  91. Kashshi, Rijal al-Kashshi, uk. 556.
  92. Fadlallah, Tahlili az Zendegani-ye Imam Reza (a.s), uk. 191.
  93. Fadlallah, Tahlili az Zendegani-ye Imam Reza (a.s), uk. 196-197.
  94. Fadlallah, Tahlili az Zendegani-ye Imam Reza (a.s), uk. 187.
  95. Fadlallah, Tahlili az Zendegani-ye Imam Reza (a.s), uk. 197-198.
  96. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 450.
  97. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 442.
  98. Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 131-133; Saduq, Al-Tawhid, uk. 250-252; Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 78-79; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 396-397.
  99. Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 401-404; Saduq, Al-Tawhid, uk. 441-454; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 179-191.
  100. Kulayni, Al-Kafi, Juz. 1, uk. 130-131; Saduq, Al-Tawhid, uk. 110-111; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 405-408.
  101. Saduq, Al-Tawhid, uk. 417-441; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 154-175; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 415-425.
  102. Saduq, Al-Tawhid, uk. 417-441; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 154-175; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 415-425.
  103. Saduq, Al-Tawhid, uk. 419; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 167-168; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 424.
  104. Saduq, Al-Tawhid, uk. 417-441; Saduq, Uyun Akhbar al-Radha, Juz. 1, uk. 154-175; Tabrisi, Al-Ihtijaj, Juz. 2, uk. 415-425.
  105. Jafarian, Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah, uk. 442.
  106. Angalia: Asqalani, Tahdhib al-Tahdhib, Dar Sader, Juz. 7, uk. 389.
  107. Angalia: Asqalani, Tahdhib al-Tahdhib, Dar Sader, Juz. 7, uk. 387.
  108. Yafi'i, Mir'at al-Jinan, Juz. 2, uk. 10.
  109. Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 230.
  110. Angalia: Jafarian, Tarikh-e Tashayyu' dar Iran, uk. 228-232.
  111. Ibn Hibban, Al-Thiqat, Juz. 8, uk. 457.
  112. Asqalani, Tahdhib al-Tahdhib, Dar Sader, Juz. 7, uk. 388.
  113. 1. "She're Zibaye Akhavan-e Sales dar Vasf-e Ali bin Musa al-Radha (a.s)", Khabargozari-ye Jomhuri-ye Islami (IRNA).
  114. Ahmadi Birjandi na Naqavizadeh, Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi, uk. 16 na 28.
  115. Ahmadi Birjandi na Naqavizadeh, Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi, Utangulizi wa Chapa ya Pili, uk. 27.
  116. Ahmadi Birjandi na Naqavizadeh, Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi, Utangulizi, uk. 16.
  117. Ahmadi Birjandi na Naqavizadeh, Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi, Utangulizi, uk. 16 na 19.
  118. Hassan: She'r-e 'Amadam Ey Shah Panaham Bede' Zabane Hale Madaram ast, Tovuti ya Khabargozari-ye Fars (Shirika la Habari la Fars).
  119. Mousavi-Abadi na wengineo, Jelvehaye Tamsil wa Ersal-e Masal dar She'r-e Sayyid Ashrafuddin Gilani, uk. 140.
  120. Zeinali, Imam Reza (a.s) be Revayat-e Ketabha, Khabargozari-ye Jomhuri-ye Islami (IRNA).
  121. 2. Ahmadi Birjandi na Naqavizadeh, "Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi", Utangulizi, uk. 16.
  122. Majmue-ye Athar-e Nokhostin Kongere-ye Jahani-ye Hazrat-e Reza (a.s), uk. 5.
  123. Majmue-ye Athar-e Nokhostin Kongere-ye Jahani-ye Hazrat-e Reza (a.s), uk. 5-11.
  124. Majmue-ye Athar-e Nokhostin Kongere-ye Jahani-ye Hazrat-e Reza (a.s), uk. 5.
  125. Ashnai-ye Mokhtasar ba Jashnware-ye Bainul-Milali-ye Farhangi wa Honari-ye Imam Reza (a.s), Tovuti ya Bonyad-e Bainul-Milali-ye Farhangi Honari-ye Imam Reza (Taasisi ya Kimataifa ya Utamaduni na Sanaa ya Imam Reza).
  126. Ashnai-ye Mokhtasar ba Jashnware-ye Bainul-Milali-ye Farhangi wa Honari-ye Imam Reza (a.s), Tovuti ya Bonyad-e Bainul-Milali-ye Farhangi Honari-ye Imam Reza (Taasisi ya Kimataifa ya Utamaduni na Sanaa ya Imam Reza).

Vyanzo

  • Ahmadi Birjandi, Ahmad na Ali Naqavizadeh. Madayih-e Radhavi dar She'r-e Farsi. Mash'had: Bonyad-e Pazhouheshha-ye Islami ya Astan-e Quds-e Radhavi, Chapa ya tatu, 1998 M.
  • Amili, Sayyid Ja'far Murtadha. Al-Hayat al-Siyasiyyah li-al-Imam al-Radha (a.s). Qom: Uchapishaji wa Jame'eh-ye Modarresin-e Howzeh-ye Ilmiyyeh-ye Qom, 1403 H.
  • Amin, Sayyid Muhsin. A'yan al-Shiah. Beirut: Dar al-Ta'aruf li al-Matbu'at, 1403 H.
  • Amini, Abdul Husayn. Al-Ghadir fi al-Kitab wa al-Sunnah. Qom: Kituo cha Al-Ghadir li al-Dirasat al-Islamiyyah, 1416 H.
  • Amoli, Muhammad Taqi. Misbah al-Huda fi Sharh al-Urwat al-Wuthqa. Bila mji, 1384 H.
  • Asqalani, Ibn Hajar. Tahdhib al-Tahdhib. Beirut: Dar Sader, Bila tarehe.
  • Atardi Quchani, Azizullah. Musnad al-Imam al-Radha (a.s). Beirut: Dar al-Safwah, 1413 H.
  • Baghestani, Esmail. «الرضا، امام (ولایتعهدی)» (Imamu al-Radha (Urithi wa Kiti cha Enzi)). Ndani ya Daneshname-ye Jahan-e Islam (Ensaiklopidia ya Ulimwengu wa Kiislamu). Tehran: Bonyad-e Da'irat al-Ma'arif al-Islami, 2015 M.
  • «آشنایی مختصر با جشنواره بین‌المللی فرهنگی و هنری امام رضا(علیه‌السلام)» (Fahamu kwa Muhtasari kuhusu Tamasha la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa la Imamu Reza), Bonyad-e Bainul-Milali-ye Farhangi Honari-ye Imam Reza. Tarehe ya kutembelewa: 16 Juni 2024 M.
  • Dehkhoda, Ali Akbar. Kamusi ya Loghatname-ye Dehkhoda.
  • Eftekhari, Sayyid Ghani. Imam Reza (a.s), Ma'mun wa Mowdhu-e Velayat'ahdi. Mashhad: Beh-Nashr, 2019 M.
  • Fadlallah, Muhammad Jawad. Tahlili az Zendegani-ye Imam Reza (a.s). Mtafsiri: Muhammad Sadiq Aref. Mashhad: Astan-e Quds-e Radhavi, 2003 M.
  • «قصیدهٔ شمارهٔ ۱۳۹ - در نعت امام هشتم (ع)» (Kasida Na. 139 - Katika Sifa za Imam wa Nane).
  • Habibi, Salman. Ketabshenasi-ye Imam Reza (a.s). Mashhad: Astan-e Quds-e Radhavi, Chapa ya kwanza, 2013 M.
  • Ibn Hibban, Muhammad. Al-Thiqat. Hyderabad: Matba'at Majlis Dairat al-Ma'arif al-Othmaniyyah, 1402 H.
  • Ibn Qulawayh, Ja'far bin Muhammad. Kamil al-Ziyarat. Uhakiki: Abdul Hussein Amini. Najaf: Dar al-Murtadhawiyyah, Chapa ya kwanza, 1356 H.
  • Ibn Shahrashub al-Mazandarani, Muhammad bin Ali. Manaqib Al Abi Talib (a.s). Qom: Allameh, Chapa ya kwanza, 1379 H.
  • Jafarian, Rasul. Atlas-e Shiah. Tehran: Sazman-e Joghrafiya-ye Nirouha-ye Mosallah, 2008 M.
  • Jafarian, Rasul. Tarikh-e Tashayyu' dar Iran az Aghaz ta Tolou'-e Dowre-ye Safavi. Tehran: Nashr-e Elm, Chapa ya pili, 2008 M.
  • Jafarian, Rasul. Hayat-e Fekri wa Siyasi-ye Imamane Shiah. Qom: Ansariyan, 2002 M.
  • Kashshi, Muhammad bin Umar. Rijal al-Kashshi. Mashhad: Nashr-e Daneshgah-e Mashhad, Chapa ya kwanza, 1409 H.
  • «حسان: شعر «آمدم ای شاه پناهم بده» زبان حال مادرم است» (Hassan: Shairi la "Nimekuja Ee Mfalme Nipe Hifadhi" Ndiyo Hali ya Mama Yangu), Shirika la Habari la Fars. Tarehe ya kuwekwa: 2 Januari 2014 M. Tarehe ya kutembelewa: 17 Juni 2021 M.
  • «فرهنگ رضوی در آینهٔ سینما/ شوق زیارت از یا ضامن آهو تا بدون قرار قبلی» (Utamaduni wa Kiradhavi kwenye Kioo cha Sinema), Tovuti ya IRNA. Tarehe ya kuwekwa: 11 Juni 2022 M. Tarehe ya kutembelewa: 26 Juni 2023 M.
  • «مجید مجیدی: یا ضامن آهو شاهکاری مستند دربارهٔ امام رضاست» (Majid Majidi: Ya Zamen-e Ahoo ni Filamu ya Hati ya Kisanaa Kuhusu Imam Reza), Tovuti ya IRNA. Tarehe ya kuwekwa: 26 Mei 2023 M. Tarehe ya kutembelewa: 26 Juni 2023 M.
  • «استاد فرشچیان: چهرهٔ امام رضا(ع) را دیدم و نقاشی کردم» (Ostad Farshchian: Niliona Sura ya Imamu Ridha na Nikaichora), Shirika la Habari la Javan Online. Tarehe ya kuwekwa: 22 Oktoba 2020 M. Tarehe ya kutembelewa: 17 Juni 2021 M.
  • "She're Zibaye Akhavan-e Sales dar Vasf-e Ali bin Musa al-Radha (a.s)", Khabargozari-ye Jomhuri-ye Islami (IRNA).
  • «دانشنامهٔ امام رضا(ع)» (Ensaiklopidia ya Imam Reza), Shirika la Habari la Radhawi. Tarehe ya kuwekwa: 7 Januari 2019 M. Tarehe ya kutembelewa: 14 Juni 2021 M.
  • «سروده‌هایی در مدح امام رضا(ع)» (Mashairi katika Sifa za Imam Reza), Shirika la Habari la Tasnim. Tarehe ya kuwekwa: 14 Julai 2019 M. Tarehe ya kutembelewa: 17 Juni 2021 M.
  • «ترجمهٔ کتاب محمدرضا حکیمی دربارهٔ زندگی امام رضا به ۴ زبان» (Tafsiri ya Kitabu cha Mohammad Reza Hakimi Kuhusu Maisha ya Imam Reza katika Lugha 4), Shirika la Habari la Tasnim. Tarehe ya kuwekwa: 3 Agosti 2016 M. Tarehe ya kutembelewa: 14 Juni 2021 M.
  • Kia Gilani, Ahmad bin Muhammad. Siraju al-Ansab. Uhakiki: Mehdi Rajai. Qom: Maktaba ya Ayatullah Mar'ashi Najafi, Chapa ya kwanza, 1409 H.
  • Majmue-ye Athar-e Nokhostin Kongere-ye Jahani-ye Hazrat-e Reza (a.s). Mashhad: Kongamano la Kimataifa la Imam Reza, 1986 M.
  • Kulayni, Muhammad bin Ya'qub. Al-Kafi. Uhakiki: Ali Akbar Ghaffari na Muhammad Akhundi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, Chapa ya nne, 1407 H.
  • Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar al-Jami'ah li-Durar Akhbar al-A'immah al-Athar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, Chapa ya pili, 1403 H.
  • Modarresi Tabataba'i, Hossein. Bargi az Tarikh-e Qazvin. Qom: Maktaba ya Ayatullah Mar'ashi Najafi, 1982 M.
  • Mostowfi, Hamdullah bin Abi Bakr. Nozhat al-Qolub. Uhakiki: Muhammad Dabirsiaqi. Qazvin: Hadis-e Emrouz, Chapa ya kwanza, 2002 M.
  • Mousavi-Abadi, Reza na wengineo. «جلوه‌های تمثیل و ارسال مَثَل در شعر سید اشرف‌الدین گیلانی» (Udhihirisho wa Mifano katika Mashairi ya Sayyid Ashrafuddin Gilani). Ndani ya *Tahqiqat-e Tamsili dar Zaban wa Adab-e Farsi*, Toleo la 9, Na. 34. 2017 M.
  • Mir-Aqa'i, Sayyid Hadi. «ضامن آهو و تجلی آن در شعر فارسی» (Zamen-e Ahoo na Udhihirisho wake katika Mashairi ya Kiajemi). Ndani ya *Farhang-e Mardom*, Toleo la 43 na 44. 2012 M.
  • «لماذا اشتهر الامام الرضا(ع) بغریب الغرباء» (Kwa nini Imam Reza Alifahamika kama Gharib al-Ghuraba), Khabargozari-ye Buratha. Tarehe ya kuwekwa: 27 Juni 2022 M. Tarehe ya kutembelewa: 30 Mei 2023 M.
  • Naji, Mohammad Reza. «الرضا، امام» (Imam al-Radha). Ndani ya Daneshname-ye Jahan-e Islam (Ensaiklopidia ya Ulimwengu wa Kiislamu). Tehran: Bonyad-e Da'irat al-Ma'arif al-Islami, 2015 M.
  • Najaf, Muhammad Mehdi. Al-Jami' li-Ruwat wa Ashab al-Imam al-Radha (a.s). Mashhad: Al-Mu'tamar al-Alami li-al-Imam al-Radha, Chapa ya kwanza, 1407 H.
  • «در هر دو اثر عنایاتی از سوی امام رضا(ع) داشته‌ام» (Nilipokea Neema kutoka kwa Imam Reza katika Kazi Zote Mbili), Qods Online. Tarehe ya kuwekwa: 6 Julai 2019 M. Tarehe ya kutembelewa: 18 Juni 2021 M.
  • Qummi, Hasan bin Muhammad. Tarikh-e Qom. Uhakiki: Jalaluddin Tehrani. Tehran: Toos, Bila tarehe.
  • Qurashi, Baqir Sharif. Hayat al-Imam Ali bin Musa al-Radha (a.s); Dirasah wa Tahlil. Qom: Bila mchapishaji, 2001 M.
  • Rafiei, Ali. Zendegani-ye Imam Reza (a.s). Tehran: Pazhouheshkade-ye Tahqiqat-e Islami, Bila tarehe.
  • Sajjadi, Seyyed Jafar. «آستانهٔ حضرت معصومه» (Haramu ya Hazrat Ma'sumah). Ndani ya Dairat al-Ma'arif al-Bozorg al-Islami (Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu). Tehran: Kituo cha Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu, 1988 M.
  • Sayyid al-Murtadha, Ali bin Husayn. Tanzih al-Anbiya (a.s). Qom: Dar al-Sharif al-Radhi, 1998 M.
  • Shafaei, Amanullah na Ghulam Reza Behrouzlak. «هنر هفتم و فرهنگ رضوی؛ همسویی‌ها و تعاملات» (Sanaa ya Saba na Utamaduni wa Kiradhawi). Ndani ya *Rasaneh*, Na. 81, 2010 M.
  • Sheikh al-Saduq, Muhammad bin Ali. Al-Tawhid. Uhakiki: Hashem Hoseini. Qom: Daftare Entisharat-e Islami, Chapa ya kwanza, 1398 H.
  • Sheikh al-Saduq, Muhammad bin Ali. Ma'ani al-Akhbar. Uhakiki: Ali Akbar Ghaffari. Qom: Daftare Entisharat-e Islami, Chapa ya kwanza, 1403 H.
  • Sheikh al-Saduq, Muhammad bin Ali. Uyun Akhbar al-Radha. Uhakiki: Mehdi Lajevardi. Tehran: Nashr-e Jahan, Chapa ya kwanza, 1999 M.
  • Sheikh al-Mufid, Muhammad bin Muhammad. Al-Irshad fi Ma'refat Hujaj Allah 'ala al-Ibad. Uhakiki: Muassasat Aalul Bait. Qom: Kongamano la Sheikh Mufid, Chapa ya kwanza, 1413 H.
  • Sheikh al-Mufid, Muhammad bin Muhammad. Tashih I'tiqadat al-Imamiyyah. Uhakiki: Hosein Dargahi. Qom: Kongamano la Sheikh Mufid, Chapa ya pili, 1414 H.
  • Shushtari, Muhammad Taqi. Tawarikh al-Nabi wa al-Aal. Tehran: Bila mchapishaji, 1391 H.
  • Suyuti, Jalaluddin Abdul Rahman bin Abi Bakr. Tarikh al-Khulafa. Uhakiki: Ibrahim Salih. Beirut: Dar Sader, Chapa ya kwanza, 1417 H.
  • Tabari, Muhammad bin Jarir. Dala'il al-Imamah. Qom: Uchapishaji wa al-Bi'ithah, Chapa ya kwanza, 1413 H.
  • Tabari, Muhammad bin Jarir. Tarikh al-Tabari. Beirut: Muassasat Izzuddin, 1413 H.
  • Tabrisi, Ahmad bin Ali. Al-Ihtijaj 'ala Ahl al-Lijaj. Uhakiki: Muhammad Baqir Khurasan. Mashhad: Nashr-e Mortadha, Chapa ya kwanza, 1403 H.
  • Tabrisi, Fadhl bin al-Hasan. I'lam al-Wara bi-A'lam al-Huda. Qom: Muassasat Al al-Bayt li-Ihya al-Turath, 1417 H.
  • Tusi, Muhammad bin Hasan. Rijal al-Tusi. Qom: Muassasat al-Nashr al-Islami, Chapa ya kwanza, 1415 H.
  • Tusi, Muhammad bin Hasan. Talkhis al-Shafi. Qom: Mohebbin, 2003 M.
  • Yahaghi, Muhammad Ja'far. «رضا(ع) imam» (Imam al-Radha). Ndani ya Dairat al-Ma'arif al-Bozorg al-Islami (Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu), Juzuu. 4. Tehran: Kituo cha Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu.
  • Yafi'i, Abdullah bin As'ad. Mir'at al-Jinan wa Ibrat al-Yaqdhan. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiyyah, 1417 H.
  • Ya'qubi, Ahmad bin Abi Ya'qub. Tarikh al-Ya'qubi. Beirut: Dar Sader, Bila tarehe.
  • «امام رضا(ع)، به روایت کتاب‌ها» (Imam Reza kulingana na Masimulizi ya Vitabu), Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu (IRNA). Tarehe ya kuwekwa: 2 Julai 2020 M. Tarehe ya kutembelewa: 28 Khordad 18 Juni 2021 M.