Kitabu cha Ali (a.s)

Kutoka wikishia

Kitabu cha Ali (a.s) au al-Jami’ah ni kitabu cha hadithi ambacho kiliandikwa na Imam Ali (a.s) kwa kusomewa na Mtume (s.a.w.w). Kwa maana kwamba, Mtume alikuwa akisoma na Ali alikuwa akiandika. Kitabu hiki ni katika vitu vya Uimamu vilivyoachwa na Mitume, Imam Ali na Bibi Fatma Zahra (a.s) kwa ajili ya Imam na vinahesabiwa kuwa ni vigezo na ishara au alama za kumtambua Imam. Kitabu hiki kinatoa hoja ya kuwa Imam kwa mwenye kuwa na kitabu hiki. Kwa mujibu wa hadithi, kitabu cha al-Jami’ah kimebainisha hukumu zote za kisheria hata mambo madogo madogo kabisa. Akhlaq (maadili), aqaid (itikadi), visa vya Manabii na kadhalika miongoni mwa maudhui ziingine zilizomo ndani ya kitabu hiki. Imekuja katika hadithi ya kwamba, kitabu hiki kilionwa pia na watu wasiokuwa Ahlul-Beiti; miongoni mwao ni Muhammad ibn Muslim, Zurarah ibn A’yun na Mansur Abbasi. Mahdi Mehrizi ameandika kitabu kwa jina la Kitab Ali kwa maudhi ya al-Jami’ah.

Utambulisho na Umuhimu

Kwa mujibu wa hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, Kitab al-Jami’ah ni kitabu ambacho kiliandikwa kwa hati ya Imam Ali (a.s) ambapo aliandika mambo aliayokuwa akisomewa na Mtume yaani Mtume alikuwa akimsomea imla Imam Ali. [1] Katika hadithi kitabu hiki kimeatjwa kwa anuani zingine tofauti kama: “Sahifa” [2] na “Kitab Ali” [3] ambapo baadhi ya watafiti wanaamini kwamba, anuani zote hizo zinahusiana na kitabu kimoja; kwani katika hadithi hizi, kumenukuliwa sifa ambazo ni za aina moja kwa ajili ya anuani hizi. [4] Mkabala na mtazamo huo, Agha Bozorg Tehrani (1293-1398 H) anaamini kuwa, Kitab Ali ni tofauti na al-Jamia’h. [5]

Al-Jami’ah, Ishara ya Imam

Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, al-Jami’ah ni miongoni mwa ni miongoni mwa  vitu aliavyoachiwa vya Uimamu na ambavyo vinahesabiwa kuwa ni vigezo na ishara au alama za kumtambua mwenye kuwa navyo kuwa ni Imam. [6] Agha Bozorg Tehran anaamini kuwa, Kitab Ali kama ilivyokuwa kwa vitu vingine vilivyoachiwa Uimamu, na Imam ajaye, nacho kilipokezwa kwa Maimamu wa Kishia mmoja baada ya mwingine na hivi sasa kipo mikoni mwa Imam wa mwisho Imam Mahdi (a.t.f.s). [7]
Yaliyomo Ndani ya Kitabu

Hadithi na riwaya mbalimbali zinaonyesha kuwa, ndani ya kitabu hiki cha al-Jami’ah kumetajwa hukumu zote zinazohusiana na halali na haramu hata mambo madogo madogo kabisa kama vile dia (fidia) ya mkwaruzo (kama mtu atamsababishia mwezake mkwaruzo mwilini. [8] Baadhi ya wasomi na wahakiki wamesema kuwa, kuna uwezekano kitabu hiki kimeitwa al-Jam’iah kutokana na kujumuisha na kukusanya humo hukumu zote. [9] Sayyid Hussein Modarresi Tabatabai, mmoja wa wahakiki wa Kishia wa karne ya 15, akitegemea hadithi mbalimbali, anasema kuwa, Kitab Ali kinajumuisha maudhui zifuatazo: Hukumu za Fur'u al-Din - Matawi ya Dini - (yanayojumuishwa Swala, Hija, jihadi, ndoa, talaka, utoaji hukumu, ushahidi, adhabu za makosa mbalimbali (kama kuzini, kuiba na kadhalika) na dia (fidia), akhlaqi (maadili), itikadi (aqaid), fadhila, visa vya Manabii na kadhalika. [10]

Sifa Maalumu

Katika hadithi kumebainisha namna hii kiwango na ukubwa wa Kitab Al (a.s) kwamba, urefu wake ni takribani mita 35, [11] na upande wake ni wa kiwango cha unene wa paja la ngamia, [12] ambapo hilo linaonyesha na kudhihirisha ni kwa namna gani kitabu hicho ni kikubwa; [13] hata hivyo imekuja katika baadhi ya hadithi ya kwamba, kitabu hiki kilikuwa kidogo na kilikuwa kikitosha katika sehemu ya kuhifadhia upanga (ngozi ya kuwekea upanga). [14]

Maripota

Kwa mujibu wa uhakiki na utafiti uliofanywa na Majid Maarif (aliyezaliwa 1332 Hijria Shamsia) ni kwamba, zaidi ya watu 40, wameripoti na kusimulia kuhusiana na uwepo wa kitabu cha al-Jami’ah. [15] Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, masahaba kadhaa wa Maimamu kama Muhammad ibn Muslim, [16], Zurarah ibn A’yun [17], Abu Basir Muradi, [18], Abdul-Malik ibn A’yun, [19] na Muattab, [20] na baadhi ya maadui wao kama Mansur Abbasi walikiona kitabu cha al-Jami’ah. [21] Kwa mujibu wa Sayyid Kadhim Tabatabati ni kuwa, katika kitabu cha Wasail al-Shia’h kumenukuliwa hadithi 80 kutoka kwa Kitab Ali (a.s). [22]

Mtazamo wa Ahlu Sunna

Kwa mujibu wa baadhi ya wahakiki ni kwamba, kinyume na ripoti na habari zilizonukuliwa na Mashia ambapo wao wametofautisha baina ya kitabu cha Jafr na Jami’ah pamoja na yaliyomo ndani yake, katika ripoti ya Waislamu wa madhehebu ya Kisuni, hakuna utofautishaji huo. Hata katika maeneo ambayo ripoti za Masuni zimetaja kwamba, hivi ni vitabu viwili, lakini muhtawa na yaliyomo ndani yake yametajwa kuwa ni kitu kimoja. [23] Sayyid Mir Sharif Jarjani, mmoja wa Maulamaa wa madhehebu ya Hanafi katika karne ya 8 Hijria anaamini kuwa, Kitab cha al-Jami’ah kimeandikwa kwa sura ya mafumbo na mbinu ya elimu ya herufi. [24]