Nenda kwa yaliyomo

Ibn al-Ridha

Kutoka wikishia

Ibn Ridha(Kiarabu: ابن الرضا ) ni lakabu ya watoto wa kizazi cha Imamu Ridha (a.s) ambapo maarufu zaidi miongoni mwao ni Imamu Jawad (a.s),[1] Imamu Hadi (a.s),[2] na Imamu Hassan Askary (a.s).[3] Mussa Mubarqa’ mtoto wa Imam Jawad (a.s) pia ni miongoni mwa watu ambao waliitwa kwa lakabu ya Ibn al-Ridha.[4] Lakabu hii ilikuwa ikitumiwa na wafuasi wa Maimamu (a.s) na watu wengine hususan Bani Abbas.[5]

Kuhusiana na sababu ya kutumia lakabu hii, baadhi wamesema kuwa, Bani Abbas waliwaita watoto wa Imamu Ridha (a.s) kwa lakabu ya Ibn al-Ridha ili kuonyesha kwamba, watu hawa wana nasaba na uhusiano na mtu ambaye alikubali cheo cha Walii Ahad (mrithi wa kiti cha utawala) na alikuwa na muelekeo wa kupenda dunia.[6] Sababu nyingine ambayo imebainishwa kuhusiana na umashuhuri wa lakabu hii ni kwamba, umashuhuri wa Imamu al-Ridha uliotokana na kufanya mijadala na midahalo ya kielimu na makundi mbalimbali ya kidini na kiteolojia ulipelekea watoto wake waondokee kuwa mashuhuri kwa jina la Ibn al-Ridha.[7]

Rejea

  1. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 281; Ṭabrisī, Iʿlām al-warā, juz. 2, uk. 101.
  2. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 301; Ṣaffār, Baṣāʾir al-darajāt, juz. 1, uk. 51, 374.
  3. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 321; Rāwandī, al-Kharāʾij wa l-jarāʾiḥ, juz. 1, uk. 422, 432.
  4. Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 50, uk. 3 (notes).
  5. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 281; Ṭabrisī, Iʿlām al-warā, juz. 2, uk. 101.
  6. Pasokh.org; quoting by Ayatullāh Shubayrī Zanjānī.
  7. Pasokh.org; quoting by Ayatullāh Ḥujjat

Vyanzo

  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. 2nd edition. Tehran: Islāmiya, 1363 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. 1st edition. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Rāwandī, Saʿīd b. Hibat Allāh al-. Al-Kharāʾij wa l-jarāʾiḥ. [n.p], 1409 AH.
  • Ṣaffār, Muḥammad b. Ḥasan. Baṣāʾir al-darajāt fī faḍāʾil-i Āl-i Muḥammad. [n.p], 1404 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Iʿlām al-warā bi-aʿlām al-hudā. [n.p], 1417 AH.