Sayyid Ibrahim Raisi

Kutoka wikishia
Mheshimiwa Sayyid Ibrahim Raisi

Mheshimiwa Sayyid Ibrahim Raisi al-Sadati (aliyezaliwa: 1339 Shamsia), maarufu kama Sayyid Ibrahim Raisi, ni mwanazuoni wa madhehebu ya Kishia, mwanasiasa, na Rais wa nane wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Yeye ni mwanafunzi aliyesoma katika Chuo Kikuu cha Kidini (Hawza) cha Qom na Mashhad pamoja na Chuo Kikuu cha Shahidi Mutahhari.

Raisi ni miongoni mwa wajumbe wa Jumuiya ya Wanazuoni Wanamapambano. Mheshimiwa Sayyid Ibrahim Raisi ameshika nyadhifa mbalimbali katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Miongoni mwa majukumu na nyadhifa alizoshikilia maishani mwake ni: Nafasi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu,, Mwanasheria Mkuu wa Taifa, Mkuu wa Shirika la Ukaguzi wa Taifa, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama Maalum ya Wanazuoni, mjumbe wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mwakilishi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu. Pia kwa muda wa miaka mitatu, alikuwa msimamizi wa Haram tukufu ya Imam Ridha (a.s) katika mji wa Mash'had.

Wasifu na Elimu Yake

Ibrahim Raisi alizaliwa manmo tarehe 23 Azar mwaka 1339 Shamsia huko Mashhad katika eneo la Noghan. Nasaba yake kutokea pande zote mbili za baba na mama inamfikia Zaid bin Ali. Yeye alianza masomo yake ya kidini huko Mashhad katika chuo cha Kiislamu cha Nawwab na kuendelea na masomo yake hayo ya kidini huko Qom mnamo mwaka wa 1354 Shamsia. Raisi akiwa mjini Qom, alipata taaluma za akiwa ni miongoni wa mwanafunzi waliojifunza kutoka kutoka kwa wanazuoni mbali mbali. Miongoni mwa waalimu wake ni: Yaddullah Duzduzani, Sayyid Ali Muhaqqiq Daamad, Ali Akbar Mishkini, Ahmad Beheshti, Murtadha Mutahhari, na Hussein Nuri Hamadani.[1] Pia alishiriki masomo ya nyaja za juu ya kiijitihadi yaliokuwa yakisomeshwa na wanzuoni wa fani hiyo, akiwemo: Sayyid Muhammad Hassan Mar'ashi Shushtari, Sayyid Mahmoud Haashimi Shahrudi, Ayatullah Khamenei, na wengineo.[2]

Ibrahim Raisi ni mwanafunzi aliye hitimu masomo yake ya Juu katika fani ya Fiqh na Sheria kutoka katika Chuo Kikuu cha Shahid Motahhari.[3].Mnamo mwaka wa 1362 Shamsia, alifunga ndoa na Jamilah Alamu-Alhuda, binti ya Sayyid Ahmad Alamu-Alhuda.[4]

Historia ya Mapambano Kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu

Raisi, kama alivyojieleza mwenyewe: aliwahi kukamatwa na kikosi cha SAVAK (askari maamumu wa utawala wa Shaa wa Iran) miaka kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, kukamatwa kwake kulitokana na shughuli zake za mapambano dhidi ya serikali ya wakati huo.[5] Pia alikuwa akishirikiana na baadhi ya wanafunzi kwenda kukutana na viongozi wa kidini waliokuwa wamehamishwa kufukuzwa nchini na serikali ya Pahlavi. Miongoni mwa harakati zake hizo ni pamoja na kukutana na Ayatullah Khamenei ambaye alikuwa amehamishiwa mji wa Iran Shahr.[6] Baada ya kuchapishwa kwa makala ya kumkashifu Imam Khomeini katika gazeti la Ettela'at tarehe 17 Dey mwaka 1356 Shamsia, Raisi alishiriki katika mikusanyiko na maandamano yaliyoanzia kutoka madrasa ya Ayatullah Borujerdi (Madrasa ya Khan).[7] Pia, mnamo mwezi wa Bahman 1357 Shamsia, alihudhuria katika mkusanyiko wa wanazuoni waliokusanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran kwa ajili ya kupinga kufungwa kwa viwanja vya ndege kwa nia ya kumzuia Imamu Khomeini kurejea Iran. [8]

Mlezi wa Astan Quds Radhawi

Ibrahim Raisi akiwa na wapiganaji wa Iran katika vita vya Iran na Iraq[9]

Mnamo mwaka wa 1394 Shamsia, kufuatia kifo cha Abbas Waidh-Tabasi kwa amri ya Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Raisi aliteuliwa kuwa ni kiongozi wa Tuwliat Astane Qudsi Radhawi (Kiongozi Mkuu wa Haram ya Imamu Ridha (a.s)).[10] Bwana Raisi alishika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitatu hadi mwezi wa Farwardini mwaka 1398.[11] Katika kipindi cha utawala wa wake, huduma nyingi zilifanyika ndani ya Astane Qodsi Radhawi. Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na ujenzi wa mji wa wageni wenye uwezo wa kupokea idadi ya wageni elfu tatu kwa siku. Pia alisimamia ujenzi wa vituo vingi vya wageni karibu na Haram ya Imam Ridha (a.s).12. [12] Aidha, alisimamia mipango ya kuwapeleka wanyonge kiuchumi kwenda Mashhad kwa ajili ya kufanya ziara kwenye kaburi la Imamu Ridha (a.s), alisimamia ujenzi wa vituo vya kupumzikia kwa ajili ya wageni kwenye njia za kuelekea mjini Mash’had, pia alisimamia mpango wa Huduma wa kuteuwa vijana wa kutoa huduma kwa wageni wafanyao ziara mjini Mash’had.[13]

Shughuli za Kisiasa

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ibrahim Raisi alianza shughuli zake za ukadhi akiwa na umri wa miaka 20 akiwa kama jaji msaidizi katika mahakama ilioko mkoani Karaj. Pia kwa muda fulani alihudumu kama mwendesha mashtaka mkoani Hamadan.[14] Kati ya majukumu yake mengine ni pamoja na:

  • Mwendesha mashtaka mkuu wa Tehran kuanzia mwaka 1368 hadi 1373 Shamsia15. [15]
  • Mkuu wa Shirika la Ukaguzi la Kitaifa kuanzia mwaka 1373 hadi 1383 Shamsia[16]
  • Naibu wa kwanza wa Mamlaka ya Mahakama kutoka mwaka 1383 hadi 1393 Shamsia[17]
  • Mwakilishi wa watu wa mji Khorasan ya Kusini katika Baraza la Wajumbe wa Kiongozi Mkuu (Bunge la Walinzi wa Sheria la Majlis Khubregan.), tangu mwaka wa 1385 Shamsia[18]
  • Mwendesha mashtaka wa Mahakama Maalum ya Kidini kutoka mwaka 1391 hadi 1400 Shamsia[19]
  • Mwendesha mashtaka Mkuu wa nchi kutoka 1393 SH hadi 1394 Shamsia[20]
  • Mwanachama wa Baraza la Kutathmini Maslahi ya Serikali tangu mwaka 1396 Shamsia[21]
  • Kiongozi wa Mahakama kuu ya Iran tangu mwaka 1397 hadi 1400 Shamsia[22]
  • Rais wa Iran tangu mwaka wa 1400 Shamsia.[23]
  • Mwanachama wa Baraza Kuu la Jamii ya Wanazuni Wapambanao tangu mwaka wa 1376 Shamsia. [24]

Kuongeza Msaada kwa Kikosi cha Harakati cha Palestina

Sayyid Ibrahim Raisi akiwa ameshika Qur'ani na kusoma baadhi ya Aya katika kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa[25]

Sayyid Ibrahim Raisi ni mmoja wa wale wanaotambuliwa kama wanaounga mkono wa dhati kwa Kikosia cha Harakati cha Palestina. Katika awamu za awali za urais wake, alisafiri kwenda Syria pamoja na baadhi ya mawaziri wake na kufanya mikutano kadhaa na viongozi wa makundi ya Kipalestina na Hizbullah huko Damascus. Ibrahim Raisi alikuwa rais wa kwanza wa Iran kusafiri kwenda Damascus baada ya vita vya ndani vya Syria na baada ya miaka 15.

Kulingana na shirika la habari la IRNA, bwana Raisi, katika kipindi cha siku 165 baada ya Operesheni ya Tufani dhidi ya Wazayuni ya Jerusalem na shambulio la Israel dhidi ya Gaza, alichukua zaidi ya hatua 100 kwa ajili ya kuisaidia Gaza na vikundi vya upinzani vya Kipalestina.[26] Pia, sehemu ya hotuba yake aliyoitoa katika Mkutano wa 78 wa Umoja wa Mataifa, ilizingatia zaidi suala la uvamizi wa ardhi ya Palestina na maeneo mengine ya Lebanon na Syria kupitia utawala wa Kizayuni, ambapo alielezea akisema:

Je, huu si wakati wa kumaliza miaka 75 ya uvamizi wa ardhi ya Palestina na dhulma dhidi ya watu wanyonge na mauaji ya wanawake na watoto, na kutambua haki za watu wa Palestina?[27]

Rejea

  1. Najafi, Riwayat Intikhabat Davozdahom, uk. 186-188 Be Naqil Az «Riwayat Hujatul-Islam Raisi Az Dauran Mubarize Aleih Razhim Puhlawi/Shakligiri Hastehai Mubarezat Tulab Dar Qom / Majraa Didor Ba Ayatullah Khamenei Dar Iran Shahr», Markaz Isnad Inqilab Islami.
  2. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabargozari Hamshahri.
  3. Sawabiq wa Zindeginame Hujatul al-Islam wal-muslimin Raisi, Khabarigozari Seda wa Sima.
  4. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabargozari Hamshahri.
  5. Najafi, Riwayat Intikhabat Davozdahom, uk. 186-188 Be Naqil Az «Riwayat Hujatul-Islam Raisi Az Dauran Mubarize Aleih Razhim Puhlawi/Shakligiri Hastehai Mubarezat Tulab Dar Qom / Majraa Didor Ba Ayatullah Khamenei Dar Iran Shahr», Markaz Isnad Inqilab Islami.
  6. Najafi, Riwayat Intikhabat Davozdahom, uk. 186-188 Be Naqil Az «Riwayat Hujatul-Islam Raisi Az Dauran Mubarize Aleih Razhim Puhlawi/Shakligiri Hastehai Mubarezat Tulab Dar Qom / Majraa Didor Ba Ayatullah Khamenei Dar Iran Shahr», Markaz Isnad Inqilab Islami.
  7. «Sherh Zindegi Sayyid Ibrahim Raisi», Paygah Itilai‌ Resani Sayyid Ibrahim Raisi.
  8. Najafi, Riwayat Intikhabat Davozdahom, uk. 186-188 Be Naqil Az «Riwayat Hujatul-Islam Raisi Az Dauran Mubarize Aleih Razhim Puhlawi/Shakligiri Hastehai Mubarezat Tulab Dar Qom / Majraa Didor Ba Ayatullah Khamenei Dar Iran Shahr», Markaz Isnad Inqilab Islami.
  9. « Riwayat Hujatul-Islam Raisi Az Dauran Mubarize Aleih Razhim Puhlawi/Shakligiri Hastehai Mubarezat Tulab Dar Qom/Majraa Didor Ba Ayatullah Khamenei Dar Iran Shahr», Markaz Isnad Inqilab Islami.
  10. «Intikhab Hujatu al-Islam Raisi Be Tauliyat Ustan Quds Radhawi», Daftar Hifdhi wa Nashr Athar Hadharat Ayatullah al-Udhma Khamenei.
  11. Tazama: « Intikhab Hujatu al-Islam Raisi Be Tauliyat Astan Quds Radhawi»,Daftar Hifdhi wa Nashr Athar Hadharat Ayatullah al-Udhma Khamenei.
  12. «Negah Be Amalikard Se Sale Hujatul al-Ismam Raisi Dar Astan Quds Radhawi», Khabarigozari Iran.
  13. Tazama:«Negah Be Amalikard Se Sale Hujatul al-Ismam Raisi Dar Astan Quds Radhawi», Khabarigozari Iran.
  14. «Sherh Zindegi Sayyid Ibrahim Raisi»، Paygah Itilai ‌Resani Sayyid Ibrahim raisi.
  15. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  16. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  17. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  18. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  19. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  20. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  21. «Intikhab Hujatu al-Islam wal-Muslimin Sayyid Ibrahim Raisi Be Riyasat Quwat Qadhaiye», Daftar Hifdhi wa Nashr Athar Hadhrat Ayatullah al-Udhma Khamenei.
  22. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  23. «Zindeginame: Sayyid Ibrahim Raisi», Khabarigozari Hamshahri.
  24. «Sherh Zindegi Sayyid Ibrahim Raisi»، Paygah Itilai ‌Resani Sayyid Ibrahim raisi.
  25. «Matni ka’mil Sukhun-ranii Raisi Dar Sazman Milal »، Insafnews‌.
  26. «Pish Az 100 Maudhui-giri Dar Himayat Az Ghaze / Raisi Chegune Dast Mad-iyan Huququ Bashar Ra Rukard »، Khabargozari Iran.
  27. «Matni ka’mil Sukhun-ranii Raisi Dar Sazman Milal »، Insafnews‌.