Hadithi ya Rayyan bin Shabib
Hadithi ya Rayyan bin Shabib ni hadithi iliyonukuliwa na Rayyan bin Shabib kutoka kwa Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s) kuhusiana na mwezi wa Muharram (Mfunguo Nne), kulia na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein bin Ali bin Abi Twalib (a.s). Katika hadithi hii kunaashiriwa amali za siku ya kwanza ya mwezi wa Muharram kuvunjia heshima na utukufu wa mwezi huu kwa kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s) ndani ya mwezi huu, maagizo ya kulia kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s), kumzuru Imamu Hussein (a.s), kuwalaani waliomuua, kuwa na furaha katika furaha za Ahlul-Bayt (a.s) na kuhuzunika katika ghamau na huzuni zao na kuukubali Wilayah (uongozi) yao.
Katika sehemu ya hadithi hii, Imamu Ridha (a.s) anamuagiza Rayyan kwamba: (يَا ابْنَ شَبِيبٍ إِنْ كُنْتَ بَاكِياً لِشَيْءٍ فَابْكِ لِلْحُسَيْنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ فَإِنَّهُ ذُبِحَ كَمَا يُذْبَحُ الْكَبْشُ ; Ewe mwana wa Shabib! kama unataka kulilia kitu, basi mlilie Hussein bin Ali (a.s) ambaye alichinjwa kama kondoo). Katika hadithi hii, kumetajwa msamaha wa dhambi, malipo ya kumlilia Imamu Hussein (a.s) na Ziyara ya mtukufu huyo.
Hadithi hii imenukuliwa katika vitabu kama Uyun Akhrbar al-Ridha, al-Amali vya Sheikh Saduq, na vitabu vingine kama al-Iqbal, Wasail al-Shiah na Bihar al-Anwar vimenukuu kutoka katika vitabu hivyo.
Wanazuoni wa Kishia kama Muhammad Taqi Majlisi, Sahib Hadaiq, Sayyid Muhammad Said Hakim na Hussein Wahid Khorasani wameitambua hadithi hii kuwa ni Hasanu (nzuri) na sahihi.
Nafasi ya Hadithi katika Fasihi ya Ashura
Hadithi ya Rayyan bin Shabib inajulikana kuwa ni moja ya hadithi mashuhuri zaidi kuhusu maombolezo. [1] Hadithi hii inahusu mwezi wa Muharram, tukio la Karbala na malipo ya kulia na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein bin Ali (a.s). Kikawaida makhatibu (watoa mihadhara) na wasomaji kaswida na mashairi ya kuwasifu Ahlul-Bayt (a.s) husoma hadithi hii au sehemu ya hadithi hii kwa ajili ya kubainisha umuhimu wa kumlilia Hussein (a.s). Pia, sehemu ya hadithi hii hutumika kuandika maandishi katika vitambaa kuhusiana na maombolezo ya Muharram. Hadithi hii imetumiwa pia katika mashairi yanayohusiana na Ashura. [2] [3] Hadithi ya Rayyan imechukuliwa kuwa ni chanzo cha matumaini kwa waumini wa Wilayah (uongozi) Ahlul-Bayt (a.s) na kuwa ni ishara ya neema ya Mwenyezi Mungu kwa Mashia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s) kutokana na zawadi ya thawabu kubwa na ujira mbadala wa amali na sehemu za ibada. [4]
Maudhui ya hadithi
Maudhui zilizobainishwa katika Hadithi ya Rayyan bin Shabib ni: [5]
- Amali za siku ya kwanza ya Muharram: Katika hadithi hii kumeashiriwa siku ya kwanza ya Muharram na kujibiwa dua kama kujibiwa dua ya Zakaria katika siku hii. [6] Sayyid Ibn Tawus akitegemea hadithi hii na hadithi zingine, amesema kuwa, kufunga Saumu ni katika amali za siku ya kwanza ya Muharram na ameitanbua siku hii kwamba, ni katika masiku ya kutakabaliwa dua. [7]
- Kuvunjiwa utukufu wa mwezi wa Muharram: Imekuja katika hadithi hii kwamba, hawakuhifadhi utukufu wa Mtume (s.a.w.w), waliwauwa watoto wake na kuwateka wake zao, katika hali ambayo katika zama za ujahilia walihifadhi utukufu wa mwezi wa Muharram na walikuwa wakiepuka dhulma na vita katika mwezi huu. [8]
- Maagizo ya kumlilia Imamu Hussein (a.s): Imetajwa katika sehemu ya hadithi ya Imamu Ridha akimhutubu Rayyan kwamba: Ukitaka kulilia kitu, mlilie Hussein bin Ali ambaye alichinjwa kama kondoo. Pia inasemekana kwamba mbingu na ardhi zililia kwa ajili ya kuuawa kwake kishahidi na mbingu ikanyesha damu na udongo ukabadilika rangi na kuwa mwekundu. [9]
- Fadhila za kumlilia Imamu Hussein (a.s): Katika hadithi hii, kumetajwa suala la dhambi zote kusamehewa, malipo ya kilio na machozi yanayotiririka mashavuni kwa kufanya maombolezo kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s). [10]
- Agizo la kumzuru Imamu Hussein: Imam Ridha (a.s) alimuamuru Rayyan kuzuru kaburi la Imamu Hussein kama anataka kukutana na Mwenyezi Mungu hali ya kuwa yu msafi na bila dhambi. [11]
- Kuwalaani wauaji wa Imamu Hussein (a.s): Imekuja katika hadithi kwamba: Ewe mwana wa Shabib, kama unataka uwe pamoja na Mtume katika nyumba za peponi, walaani wauaji wa Imamu Hussein (a.s).
- Kuja kusaidia Malaika 4,000: Kwa mujibu wa hadithi, Malaika 4,000 waliteremka ardhini kwa ajili ya kuja kumsaidia Imamu Hussein, lakini hawakupatiwa idhini, hivyo wapo kando ya kaburi la Imamu Hussein wakiwa na vumbi na hali ya kutatizika mpaka atapoadhihiri Imamu Mahdi na kuanzisha harakati na watakuwa miongoni mwa wafuasi wake wenye nara na kaulimbiu ya Ya litharaat al-Hussein yenye maana ya kutaka kulipiza kisasi damu ya Imamu Hussein (a.s). [13]
- Agizo la kufurahi katika furaha za Ahlul-Baty na kuhuzunika katika huzuni zao: Katika sehemu ya mwisho ya hadithi hii imenukuliwa kwamba: Ewe mwana wa Shabib, kama unapenda uwe katika daraja za juu peponi pamoja na Ahlu-Bayt (a.s), basi huzununika katika ghamu na huzuni zetu sisi Ahlul-Bayt na kuwa na furaha katika furaha zetu na kubali Wilayah (uongozi) yetu; kwani siku ya Kiyama mtu atafufuliwa (hata) na jiwe ambalo alilipenda. [14]
Vyanzo na Ithibari
Sheikh Saduq ameinukuu kadithi hii katika kitabu cha Uyun Akhbar al-Ridha (15] na katika kitabu chake cha al-Amali [16], kutoka kwa Muhammad bin Ali Majilaweih kutoka kwa Ali bin Ibrahim Qumi kutoka kwa baba yake Ibrahim Hashim kutoka kwa Rayyan bin Shabib kutoka kwa Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s). Vitabu kama al-Iqbal cha Sayyid Ibn Tawus, [17] Wasail al-Shiah Sheikh Hurr Amili, [18] Bihar al-Anwar cha Allam Majlisi, [19] na Awalim al-Ulum Wal-Maarif cha Abdalla bin Bahrani Isfahani (aliaga dunia 1148 Hijria), [20] vimenukuu hadithi hii kutoka katika vitabu vya Uyun Akhbar na Aamali vya Sheikh Saduq.
Muhammad Taqi Majlisi ameitaja hadithi hii kuwa ni hasan (nzuri) na wanazuoni kama Sahib Hadaiq na Sayyid Muhammad Said Hakim wameitambua kuwa ni sahihi. [22] Sanadi na mapokezi ya hadithi hii katika kitabu cha Mausu’ah Ahadith Ahlul Bayt pia imetambuliwa kuwa na itibari. [23] Hussein Wahid Khorasani, [24] na baadhi ya wahakiki, [25] wamewatambua wapokezi wa hadithi hii kuwa ni watu thiqah (wa kuaminika) na Shia Imamiyyah na kwa muktadha huo wameitambua hadithi hii kuwa ina itibari na ya kuaminika. Miongoni mwa hoja zingine za kuwa na itibari hadithi hii imetajwa kuwa ni kuweko kwake ndani ya kitabu cha al-Nawadir, cha Ibrahim bin Hashim. [26]
Monografia
- Kitabu cha “Fabki Lil-Hussein: Mwandishi Sayyid Muhammad Baqir Hashimi Shahroudi, kinatoa tathmini mukhtasari kuhusiana na maagizo ya Imamu Ridha (a.s) kwa Rayyan bin Shabib.
- Kitabu “Parishan Moye va Khaq Alud”, kilichoandikwa na Muhammad Ali Fattahzadeh kinatoa ufafanuzi kuhusiana na hadithi ya Rayyan bin Shabib.