Al-Mustabsir

Kutoka wikishia


Al-Mustabsir (Kiarabu: المُستَبصِر) ni mtu ambaye ametoka katika madhehebu au dini nyingine na kuingia katika madhehebu ya Shia Ithnaasharia. Katika vitabu vya hadithi na sehemu mbalimbali za vitabu vya fiqhi, suala la mustabsir limezungumzwa sana na hukumu zimetajwa kwa ajili yake; miongoni mwazo ni kuwa, kwa mujibu wa Fat’wa ya mafaqihi wa Kishia, si lazima kurudia matendo ya ibada ambayo Mustabasr aliyafanya kwa mujibu wa madhehebu yake ya awali baada ya kuwa Shia; isipokuwa Zaka ya mali na Zakat al-Fitr kama alimpatia asiyekuwa Shia ni lazima alipe tena.

Baadhi ya waliobadilisha madhehebu na kuuingia katika Ushia ambao ni mashuhuri ni: Ali bin Mahziyar Ahvazi, Muhammad bin Mas'oud Ayyashi (mwandishi wa Tafsiri Ayyash), Muhammad Khodabandeh mtawala wa Ilkhani, Sayyid Muhammad Tijani na Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Mashia nchini Nigeria.

Maana ya mustabsir na matumizi yake katika vitabu vya fikihi na hadithi

Mustabasr, katika utamaduni wa Shia, huitwa mtu ambaye baada ya kufanya utafiti na uhakiki ameamua kubadilisha dini au madhehebu yake kutoka mojawapo ya madhehebu ya Kiislamu [1] au dini za Mwenyezi Mungu [2] na kuingia katika madhehebu ya Shia Ith’naasharia. Fadhl bin Hassan Tabarsi, mmoja wa wafasiri wa Kishia, anasema katika kitabu chake cha Maj’maa al-Bayan kwamba, mustabsir ni mtu mwenye akili na mwenye uwezo wa kupambanua haki na batili kwa hoja na fikra. [3] Istabsar maana yake ni kuwa na hali ya ufahamu na weledi katika dini. [4]

Hukumu za mustabsir hujadiliwa katika milango mbalimbali ya fikihi kama Sala, [5] Saumu, [6] Zaka, [7] Hija, [8] mirathi, [9] na kisasi. [10] Mjadala wa hukumu za Mustabsir umetajwa katika Fat’wa ya Ibn Abi Aqeel Omani (aliyefariki: 329 AH), ambaye alidiriki na kuishi katika zama za Ghaiba ndogo, [11] na Ibn Junayd, mmoja wa mafaqihi wa karne ya nne Hijiria. [12] Katika vitabu vinne vya hadithi (Kutub al-Ar’ba’a), kuna hadithi zinazohusiana na Mustabsir, katika milango kama vile ya Zaka na Hija. [13] Kadhalika kwa mujibu wa vyanzo vingi vya kifiqhi, kumejadiliwa kutokuweko haja ya kulipa kadha ibada ambazo hakuzifanya mustabsir kabla ya kubadilisha madhehebu yake na kuingia katika madhehebu ya Shia Ith’naasharia. [14]

Kwa mujibu wa fat’wa ya Sahib Jawahir, hukumu za Istibsar zinajumuisha madhehebu zote za Kiislamu, hata madhehebu na makundi ya Kiislamu ambayo yanahukumiwa kwa ukafiri, kama vile Manasibi (watu wenye chuki na uadui dhidi ya Imam Ali (a.s) au mmoja wa Ahlul-Bayt (a.s), na wanadhihirisha na kuonyesha wazi chuki na uadui wao huo) na maghulati (watu ambao wanamhesabu Imamu Ali na watoto wake kuwa ni waungu au ni Mitume na ambao wamechupa mipaka katika kuwasifu); [15] lakini Sayyid Muhammad Kadhim Tabatabai Yazdi haoni kama hukumu za Istibsar zinajumuisha maghulati. [16]

Hukumu za ibada za kabla za mustabsir

Baadhi ya fat’wa za mafakihi wa Kishia kuhusiana na ibada za kabla (kabla ya kuingia katika Ushia) za mustabsir ni kama ifuatavyo:

  • Sala na Saumu kabla ya kuingia katika Uishia: Kwa mujibu wa fat’wa za mafakihi wa Kishia ni kwamba, sio lazima kurejea kufanya ibada alizofanya kabla ya kuingia katika Ushia isipokuwa Zaka; kwa sharti kwamba, ibada alizofanya kabla ya istibsar ziwe sahihi kwa mujibu wa madhehebu hayo. [17]
  • Sala za Saumu ambazo hakufunga: Kwa mujibu wa fat'wa ya akthari ya mafakihi wa Kishia, ni wajibu kwa mustabsir (mtu ambaye ameingia katika Uishia) hasali Sala ambazo hakuzisali na kufunga Saumu ambazo hakuzifunga kabla ya kubadilisha madhehebu yake na kuingia katika Ushia kama alifanya hayo kinyume na madhehebu yake. [18] Hussein Aal-Usfur (aliaga dunia) 1216 Hijiria) fakihi na mtaalamu wa elimu ya hadithi yeye anasema kuwa, hakuna wajibu katika hilo. [19]
  • Hija: Mustabasr hana haja ya kurudia Hija ambayo ameitekeleza kwa mujibu wa madhehebu yake. [20] Hata hivyo, baadhi ya mafakihi kama Sahib Jawahir, [21] Sheikh Tusi, [22] na Allama Hilli [23] wameshurutisha kwamba, katika Hija yake kusiwe kuna dosari katika nguzo miongoni mwa nguzo za Hija kwa mujibu wa madhehebu ya Shia. [24]
  • Zaka ya Mali na Zakat al-Fitr: Kama mustabsir kaba ya kubadilisha madhehebu yake alitoa Zaka ya mali na kumpatia mmoja wa watu wa madhehebu yake, ni wajibu kurejea kutoa; [25] lakini kama atakuwa alimpatia mmoja wa Mashia hakuna haja ya kurejea kutoa. [26] Hata hivyo Muhammad Taqi Amoli anasema kuwa, hata katika hali hii kuna ulazima wa kurejea kutoa Zaka hiyo. [27] Kwa mujibu wa fat’wa ya Shahid al-Awwal katika kitabu cha al-Bayan ni kuwa, kama alitoa na kumpatia Zaka yake asiyekuwa Shia kisha baadaye akabadilisha madhehebu na kuingia katika madhehebu ya Shia Ith’anaasharia na Zaka aliyotoa ikawa bado ipo kama ilivyo, anaweza kuichukua. [28] Hukumu ya Zakat al-Fitr ni mithili ya Zaka ya Mali. [29]

Hukumu ya matendo yasiyo ya kiibada ya mustabsir

Hukumu ya kisheria ya matendo yasiyo ya kiibada ya mustabsir, kwa mujibu wa mitazamo ya mafakihi wa Kishia ni kama ifuatavyo:

  • Ndoa mpya ya mustabsir baada ya kubadilisha madhehebu (kwa kuzingatia kutofanya tawafu Nisaa) hakuna tatizo na ni sahihi. [30]
  • Hukumu ya talaka ya mustabsir: Ikiwa Mustabsir atamtaliki mke wake kwa mujibu wa madhehebu yake kabla ya Istibsar, ikiwa talaka hii si sahihi kwa mtazamo wa Shia, kwa mujibu wa fat’wa ya Sayyid Mohsen Hakim (aliaga dunia 1390 AH), talaka yake si sahihi na anaweza kurejea. kwa mwanamke huyo baada ya Istbasar, bila ya kufunga tena ndoa; [31] lakini kulingana na Sheikh Tusi, talaka yake ni halali na kutengana kumepatikana na kumetimia. [32]
  • Hukumu ya nadhiri, ahadi, kiapo na waqfu: Ikiwa mustabsir atakuwa aliweka nadhiri, alikula kiapo au alitoa wakfu kitu kabla ya istibsar, kwa mujibu wa madhehebu ya Imamiya yakawa sio sahihi, hakuna ulazima wa kuyafanyia kazi hayo; lakini kama kwa mujibu wa madhehebu ya Imamiya ni sahihi ni lazima kuyatekeleza hata kama kwa mujibu wa madhehebu yake ya kabla yalikuwa batili. [33]
  • Taathira ya istibsar kwa tohara au najisi: Kwa mujibu wa fat’wa ya Sahib Jawahir, kama mustabsir kabla ya istibsar aliosha na kukitoharisha kitu kilichokuwa najisi kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, baada ya kubadilisha madhehebu na kuingia katika Usahia, hakuna ulazima wa kukiosha tena; lakini kama aliosha na kusafisha kwa mujibu wa madhehebu yake na jambo hilo likawa linapingana na madhehebu ya Shia, kwa mujibu wa kauli yenye nguvu ni wajibu kuosha tena. [34]

Watu mashuhuri waliongia katika Ushia

Monografia

Kitabu cha “Mausuah min Hayat al-Mustabsirin” kimeandikwa na kuchapishwa na taasisi ya “Markaz al-Ab’hath al-Aaqaidiya” ambacho kina mijalada 14 na ndani yake kinatambulisha watu waliongia katika Ushia kutoka mataifa mbalimbali. [57]