Maghulati

Kutoka wikishia

Maghulati “غُلات” ni watu wanaompa Imamu Ali (a.s) na wanawe sifa za kiungu au za kinabii na kuzidisha au kutia chumvi katika wasifu wao. Vitabu vinavyochunguza madhehebu mbalimbali vinatafautiana katika kuorodhesha idadi ya madhehebu ya Maghulat; idadi ndogo kabisa iliorikodiwa kuhusiana nao tisa na idadi kubwa ikiwa ni mia moja. Baadhi ya madhehebu maarufu ya Maghulat yaliyotajwa katika vitabu hivyo ambayo yamenasibishwa na Shia ni pamoja na: Sabaa-iyyah (wafuasi wa Abdullah ibnu Saba), Kiisaniyyah, Bayaniyyah, Khitaabiyyah, Bashiiriyah, na Mufawwidah. Kuamini katika Uungu wa Maimamu wa Shia (a.s) na unabii wao, pamoja na kudai imamu au unabii kwa waasisi wa madhehebu haya ni miongoni mwa imani zinazoshirikiwa na madhehebu haya. Katika kipindi cha Ghaibat al-Sughra (kughibu kwa Imamu Mahdi (a.s) kipindi cha mpito), baadhi ya Masahaba wa Imamu Mahdi (a.s) walidai uwakilishi kutoka kwa Imamu Mahdi (a.s), wakatoa madai yaliyoongezeka chumvi na kupindukia mipaka, na hatimae kupata wafuasi walio shikanama nao. Kulingana na wanahistoria, watu kama Ahsan Shurai’i, Muhammad bin Ali Shalmaghani, Ahmad bin Hilal Abartai, na Muhammad bin Nusair Numairi ambao walikuwa Masahaba wa Imamu Hasan al-Askari walikuwa sehemu ya kundi hili la watu wazushi. Kwa mujibu wa imani za watafiti, Maghulati kwa kuzishulisha fikra za Mimamu wa Shia na kuzifanya ziaminiane nao, waliweza kuwavutia waumini dhaifu wa Shia na kuwaleta karibu yao, na hatimae kusababisha mgawanyiko miongoni mwa Shia, jambo ambalo lilisababisha kupoteza nguvu za Shia na kuleta madhara yasiyoweza kurekebishika kirahisi kwenye madhebu ya Shia. Utambulisho na Nafasi ya Maguhulati Neno Maghulati linatokana na neno la Kiarabu “غُلات” ambalo ni wingi wa neno Ghali غالی. Kiuhalisia Maghulati ni watu wanaompa Imamu Ali (a.s) pamoja na watoto wake (Maimamu wa Shia), sifa za kiungu au unabii, ambapo katika kuelezea hadhi na sifa zao kidini na kidunia, huwa wanatia chumvi na kufuata njia ya kupindukia mipaka. [1] Katika maandiko yanayohusiana na utambuzi wa madhehebu mbali mbali, kumekuwa na majadiliano makubwa kuhusiana na historia ya kuibuka kwa madhehebu ya Maghulat na imani zao. [2] Katika baadhi ya vyanzo vya riwaya za Shia, ndani yake kumetajwa majina ya baadhi ya Maghulati ambao wamekemewa na Maimamu wa Shia. [3] Inasemekana kuwa sehemu ya imani za Maghulat zinahusiana na sifa na hadhi za Maimamu 12 (a.s), na sehemu nyingine zinahusiana na dhati ya Maimamu hao, ambapo Maghulati wamezipamba dhati hizo hadi kuzifikisha kwenye daraja Uungu. Hii ndio sababu iliopelekea kuwepo kuwepo kwa uchambuzi mpana katika elimu ya kalamu (itikadi), kuhusiana na imani za Maghulati. [4] Wataalam wa fani ya elimu ya rijal (fani ya chunguzi wa maisha ya wapokezi wa Hadithi), pia wamewatuhumu baadhi wapokezi wa Hadithi kwa sifa za ughulati. [5] Kulingana nao, kule mpokeze wa Hadithi kusifika kwa sifa ya Ughulati ni ishara ya udhaifu na ukosefu wa uaminifu wa mpokezi huyo. [6] Elimu ya fiqh pia imetaja hukumu maalumu kuhusiana na Maghulat zimetajwa. [7] Ughuluti au Ughulati Uguhuluwwu katika istilahi humaanisha tendo la mcha Mungu fulani, la kuzidisha na kupindukia mipaka iliyowekwa na dini kuhusiana na jambo fulani. [8] Baadhi ya mifano ya ughuluu ni: Kumhisabu mmoja wa manabii au Imamu kama ni Mungu, kuwashirikisha manabii au Maimamu hao na Mwenyezi Mungu katika mambo ya kidunia, kuamini kwamba mtu fulani ni mwana wa Mungu, kuamini kwamba mtu fulani ana aina ya ushirika fulani na nabii Muhammad (s.a.w.w) katika suala la unabii, kuamini unabii wa Imamu Ali (a.s) au mmoja wa Maimamu wa Shia na kuamini mtu fulani kuwa ndiye Mahdi mwahidiwa tofauti na Mahdi asili aliyetabiriwa katika vyanzo vya Kiislamu. [9] Kwa mujibu wa ijmaa ya wanazuoni wa Shia (mawafikiano ya kiujumla jamala), kuamini kwamba Imam Ali au yeyote kati ya Mimamu 12 kuwa ni Mungu, kwa kuwa jambo hili linapelekea kukataa uwepo wa Mungu, hivyo basi kuamini hivyo ni ukafiri, na wanaoamini katika imani hiyo wanahesabiwa kuwa ni makafiri. Kulingana na baadhi ya nadharia za wanazuoni ni kwamba; ikiwa imani za ughulati zitapelekea kukataa mojawapo ya msingi mikuu ya dini, basi mwenye aina hiyo ya imani hukumiwa kama kafiri. [12] Madhehebu ya Maghulati Kuna tofauti ya maoni katika vitabu vya kimapokeo kuhusu idadi ya madhehebu ya kupindukia mipaka. [13] Mtafiti wa historia, Ne’ematullah Safawi Furushani, baada ya kuchunguza vitabu kadhaa vya kuhusiana na makundi mbali mbali ya Waislamu, amebaini kuwa idadi ndogo zaidi iliyo rikodiwa kuhusiana na madhehebu haya ni tisa, na idadi kubwa zaidi ni mia moja. [14] Baadhi ya madhehebu mashuhuri ya kupindukia mipaka ya Kishia ni: 1. Sabaa'iyyah (Sabaiyyah) Sabaa'iyyah kiasili walikuwa ni wafuasi wa Abdullah ibn Saba. [15] Baadhi ya watafiti na waandishi walio andika kuhusiana na madhehebu mbali mbali, wanasema kwamba; Sabaa'iyyah ni ndio madhehebbu ya ya Maghulati wanao nasibishwa na madhehebu ya Shia. Kulingana na maoni ya Ali bin Ismail Is-haka Ash'ari, mtaalamu wa theolojia wa karne ya tatu na nne Hijria, katika kitabu chake "Maqalat al-Islamiyyinni kwamba; Sabaa'iyyah waliamini kuwa Imamu Ali (a.s) hajafariki na atarudi tena kabla ya Siku ya Kiyama na kuijaza dunia haki na usawa badala ya dhuluma na uovu. Katika kitabu cha "Rijal al-Kashshi", kuna Riwaya kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) inayoelezea kwamba Abdullah bin Saba, mwanzilishi wa madhehebu ya Sabaa'iyyah, alidai kuwa ni nabii na kumwona Imamu Ali (a.s) kama ni Mungu. [18] 2. Kisaaniyya Vitabu vinaeleza ya kwamba, tokea hapo mwanzo katika zama za Muhammad bin Hanafiyya, kulikuwa na kikundi cha Washia ambao waliamini katika Uimamu wa Muhammad bin Hanafiyya. [19] Shahrestani katika kitabu chake Al-Milal wa al-Nihal amesema kwamba; baada ya Muhammad bin Hanafiya, tofauti zilizuka miongoni mwa wafuasi wake. [20] Baadhi yao waliamini kwamba Muhammad bin Hanafiya hajafariki na atarudi tena kuleta haki na usawa duniani. [21] Wengine miongoni mwa wafuasi wake walikubali kwamba yeye amefariki, na Uimamu umehamishiwa kwa mtoto wake aitwaye Abu Hashim. [22] Kulingana na maelezo ya Mohammad Jawad Mashkur (aliyefariki: mwaka 1374 Shamsia), ambaye ni mwanahistoria na profesa wa Chuo Kikuu cha Tehran, ameripotiwa katika kitabu “Farhange Firaqe Islami”, akisema kwamba; baada ya Muhammad bin Hanafiya kufariki, kikundi cha Kisaaniyya kiligawanyika katika makundi kumi na mbili, [23] ambayo yote yalishiriki imani katika Uimamu wa Muhammad bin Hanafiya. [24] Baadhi ya madhehebu ya Kisaaniyya ni pamoja na: Hashimiyya, [25] Karubiyya, [26] Hamziyya, [27] Bayaniyya, [28] na Harbiyya. [29] 4. Khattaabiyya Khattabiyya ni kundi la wafwasi wa Abu al-Khattab Muhammad bin Abi Zainab. [30] Kulingana na maandishi ya Shahrestani ni kwamba, Abu al-Khattab kwanza kabisa aliwahisabu Maimamu kama ni manabii na kisha akaendelea zaidi na hatimae akawaita ni Waungu, na aliamini juu ya Uungu wa Imamu Sadiq (a.s) na mababa zake waliopita kabla yake. Yeye alikuwa akisema kwamba; Imamu Sadiq (a.s) ni Mungu wa zama zake, na kiuhalisia yeye (Imamu Sadiq) si yule ambaye watu wanamhisi au kunukuu hadithi kutoka kwake, ila yeye anaakisika katika umbile hizo la kibinaadamu kwa kuwa ameshuka na kuja katika ulimwengu huu wa kudunia. [31] Kumepokewa Hadithi kutoka katika kitabu “Rijalu al-Kashi”, ambazo zinaelezea ya kwamba; Imamu Sadiq (a.s) alimkataa Abu al-Khattab, alimuita mwongo na akajitenga naye, na kumlaani mtu huyu. [32] Kundi la Khattabiya lenyewe baadae lilikuja kugawanyika katika madhehebu mbalimbali yakiwemo: Mukhammasah, [33] Bazi’iyah, [34] Umairiyah, [35] na Mu’ammariyya. [36]

4. Mughairiyya Mughairiyya ni wafuasi wa Mugheerah bin Said. [37] Kulingana na ripoti ya Nobakhti katika kitabu cha Firaqu al-Shia, ni kwamba baadhi ya wafuasi wa Mugheerah bin Said walimhisabu yeye kama Imamu, na waliamini ya kwamba; Imamu Hussein (a.s), Imamu Sajjad (a.s), na Imamu Baqir (a.s) waliwacha wasia kuhusiana na Uimamu wake na kumchagua kama mrithi wao katika suala la uongozi. [38] Wao pia walikataa Uimamu wa Imamu Sadiq (a.s) na waliamini kwamba baada ya Imamu Baqir, hakuna Imamu mwengine aliyekuja kutoka katika kizazi cha watoto wa Imamu Ali (a.s), na Mugheerah bin Said ndiye Imam anaye stahiki kushika nafasi ya Uimamu hadi wakati wa kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s). [39] Mugheerah pia aliamini kwamba Muhammad bin Abdullah bin Hassan, maarufu kama Nafsu Zakiyyah, ndiye Mahdi aliyetabiriwa, na pale alipouawa walisema kwamba; yeye hajafa bali anaishi katika mlima fulani uitwao “’Alamiyya” huko Makka, na ataendelea kuishi huko hadi wakati wa kudhihiri kwake utakapofika. [40] Imepokewa katika moja ya Hadithi kwamba; Imamu Sadiq na Imamu Ridha (a.s) walimlaani Mugheerah bin Said kwa sababu ya kutoa madai ya uongo dhidi ya Imam Baqir (a.s). [41] 5. Mansuriyya Mansuriyya walikuwa wafuasi wa Abu Mansur ‘Ijli. [42] Kulingana na maelezo ya Shahristani ni kwamba; ‘Ijli ni mwanzoni aliye jaribu kujikurubisha kwa Imamu Baqir (a.s); lakini baada ya Imamu Baqir (a.s) kumkataa kwa sababu ya imani zake potovu, hapo ndipo ‘Ijli Abu Mansur alipodai kuwa yeye ni Imamu na kuwalingania watu wafungamane naye. [43] Kulingana na maelezo ya Nobakhti; Abu Mansur alidai kwamba Mungu alimchukua na kumpeleka mbinguni na kuzungumza naye, akampapasa kwa mkono wake kwa njia ya kumdekeza, na akatumia lugha Kiibrania akimtambua yeye kama ni mwanawe. [44] Pia Nobakhti alisema kwamba; baada ya kifo cha Imamu Baqir (a.s), Abu Mansur alidai kwamba Imamu Baqir (a.s) alimfanya kuwa ndiye mrithi wake wa kushika nafasi ya uongozi baada yake. [45] Pia inasemekana kwamba Abu Mansur ‘Ijli aliamini kwamba Maimamu watano wa kwanza wa Mashia walikuwa ni manabii, na kwamba yeye na vizazi vyake sita vya watoto wake watakaokuja baadaye hadi kudhhiri kwa Imamu Mahdi (a.s), wote ni mitume. [46] Katika moja ya Hadithi iliyonukuliwa kutoka katika kitabu “Rijal al-Kashi”, imeelezwa ya kwamba; Imam Sadiq (a.s) alimlaani Abu Mansur na kumtaja kama mjumbe wa Shetani. [47] Bashiiriyya Bashiiriyya ni wafuasi wa Muhammad ibnu Bashir al-Kufi. [48] Wao walikuwa wakiamini ya kwamba; Imamu Musa al-Kadhim (a.s) hakuwa kifungoni na wala hajafa, bale yeye ndiye Mahdi anayetarajiwa kuja kuleta uadilifu na kuondoa dhuma ambaye kwa hivi yuko mafichoni na kwamba yeye amemteua Muhammad ibn Bashir (mwanzilishi wa kundi hili) kushika nafasi yake katika wakati wa ghaiba yake, na kwamba yeye ndiye mwakilishi na mrithi wake katika masuala ya uongozi. Yeye alida kwamba Imamu Kadhim alimpa pete yake, akamkarithisha elimu yake, na akampa kila kitu kinacho hitajiwa na watu kuhusiana na masuala ya kidini na kidunia. [49] Wafwasi wa Muhammad ibn Bashir waliamini kwamba; baada ya kufariki kwa Muhammad bin Bashir, nafasi yake itahamia kwa mtoto wake aitwaye Sami’i, naye ndiye mwakilishi wa kushika nafasi ya Uimamu baada ya baba yake. Wao walisema kwamba; baada ya Sami’I, watu wanapaswa kumtii yeyote ambaye Sami’ ibn Muhammad atamteua kama ni mrithi wake, kisha mteuliwa huyo naye atamteua atakaye shika nafasi yake baada yake hadi Imam Musa al-Kadhim (a.s) atakapo dhihiri na kushika tena nafasi yake kama ni Imamu mtarajiwa atakaye kuja kuondoa dhulma. [50] Kuna riwaya kutoka kwa Imamu Musa al-Kazim (a.s) inayoonesha kuwa Imamu Kadhim (a.s) alimlaani Muhammad ibn Bashir mara tatu. [51] 6. Sariyya Kikundi cha Sariyya ni wafuasi wa mtu aliye julikana kwa jina la “Sariyya Aqsam. [52] Wao waliwa wakiamini ya kwamba Sariyys alikuwa ni nabii aliyetumwa na Imamu Sadiq (a.s), na kwamba yeye alikuwa ni mtu mwenye nguvu na mwaminifu kama alivyo kuwa nabii Musa (a.s), na kwamba roho yake ndiyo roho ile ile ilikuwamo ndani ya mwili wa nabii Musa (a.s). [53] Wafuasi hawa pia waliamini kwamba; Imam Sadiq (a.s) yeye wenyewe ndiye Uislamu halisi na Uislamu ni Salamu (amani), na Salamu ni Mwenye Ezi Mungu, hivyo basi Imamu Sadiq (a.s) ndiye Mungu, na sisi ni watoto wa Salamu (Mungu). [54] Wafuasi wa Sariyya walikuwa wakiwalingania watu kumfuata nabii huyu na amali zao za sala walikuwa wakizielekeza kwa Imam Sadiq (a.s) kama ndiye Mungu wao. [55] Pia Hija na Saumu walitekeleza kwa ajili yake. Katika moja ya Hadithi imeelezwa kwamba; Imamu Sadiq (a.s) alimtaja Sariyya kama mwongo na akamlaani kwa matendo yake maovu. [56] Makundi Maarufu Yaliyotambuliwa Kupitia Majina ya Imani Zao Katika vitabu vya Milalu wa Nihal (Vitabu vilivyo tafiti makundi na madhehebu), kuna majina ya makundi kadhaa ya Maghulati yalio tajwa na kutambuliwa kupitia imani zao kuu. [57] Baadhi ya makundi haya ni kama ifuatavyo: Ethnainiyyah: Kundi la Maghulati lililo amini ya kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali (a.s) kuwa ni Miungu. [58] Kuna kikundi kilichomtanguliza Mtume kama Mungu kiitwacho “Mimiyyah” na kikundi kingine kilichomtanguliza Imam Ali kama ndiye Mungu wa awali kiitwacho “Ainiyyah”. [59] Azdariyyah: Hili ni kundi linalo amini juu ya Uungu wa Imam Ali (a.s), likiamini kwamba Ali aliyekuwa ni baba wa Hasanain (Hassan na Hussein) (a.s) aliyeishi duniani, alikuwa ni mtu aitwaye “Ali Azdari” naye ni tofauti yule Ali ambaye ni Imam, kwa kuwa kiuhalisia yule Ali ambaye alikuwa Imamu alikuwa ndiye Muumba, na bila shaka yeye (Muumba) hana mtoto. [60] Mufawwidhah: Hili ni miongoni mwa kundi la Washia linaloamini iamani ya Tafwidh. [61] Tafwidh inamaanisha imani ya kwamba; Mwenyezi Mungu alimuumba bwana Mtume (s.a.w.w) na Imam Ali (a.s), kisha akawakabidhi wao yale mambo muhimu kama vile; kuumba, kifo, maisha, na riziki za viumbe. [62] Dhubaabiyya, Gharamiyya, na Dhimaamiyya: Ni makundi yanayohesabiwa miongoni mwa Maghulati ambao wana imani shirikisho ya kuamini kwamba; nafasi ya unabii ni haki ya Imam Ali (a.s). Wao walikuwa wakiamini kwamba; Jibrilu alifanya makosa katika kushusha Wahyi, kosa ambalo lilitokea kutokana kule Imamu Ali (a.s) kufanana mno na Mtume (s.a.w.w), hivyo basi badala ya yeye kumshushia wahyi Imamu Ali (a.s), alikwenda kuuteremsha wahyi huo kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [63] Sayyid Mohsen Amin amemadai kwamba; kuyanasibisha makundi haya na kuyahisabu kuwa ni miongoni mwa makundi ya Shia, ni madai potofu yasio na msingi. Yeye amedai kwamba; majina ya makundi kama haya hayapatikani ndani ya vyanzo vya Shia vinavyo husina na utambuzi wa madhehebu na makundi ya Waislamu. [64] Badala yake yeye anaamini kwamba; majina ya makundi haya yalibuniwa kwa nia ya kuleta motisha katika kujenga picha mbaya dhidi ya madhehebu ya Shia. [65] Shariikiyya: Hili ni kundi lililoamini kwamba kwa jinsi ya Harun alivyoshirikiana na Nabii Musa katika unabii latika nafsi ya unabii, ndivyo hivyo hivyo Imam Ali (a.s) alivyo shirikiana na bwana Mtume (s.a.w.w) katika suala hilo la unabii. [66] Waliodai Ukaimu wa Imamu Mahdi (a.s) Katika Kipindi cha Ghaiba Ndogo Inakisiwa kwamba wakati wa Ghaybatu al-Sughra (kipindi cha mpito cha kutoonekana kwa Imam Mahdi (a.s)), baadhi ya watu mashuhuri miongoni mwa Shia walifuata njia ya ughuluu (kuongeza chumvi au kuzidisha) na kudai mambo yasiyowezekana kuhusiana na wao wenyewe, na wakati mwingine kuhusiana na Maimamu (a.s). Walidai madai ya uongo ya kwamba wao ni manaibu maalum wa Imam Mahdi (a.s). [67] Waliweza pia kupata wafuasi na makundi kadhaa yalijengwa juu ya msingi wa madai yao. [68] Baadhi ya makundi haya ni kama ifuatavyo: Shari’iyya: Wafuasi wa Hassan Sharia ambaye ni miongoni mwa masahaba wa Imamu Hadi (a.s) na ambaye alikuwa ni masahaba wa Imamu Hassan Askari (a.s). [69] Yeye anamchukulia kama ndiye mtu wa kwanza baada ya kifo cha Imamu Hassan Askari (a.s) na katika kipindi cha Ghaibat Sughra, aliye dai madai ya uongo, akisema kwamba yeye ni naibu wa Imamu Mahdi (a.s). [70] Baada ya hapo, barua Imamu Mahdi (a.s) alaitoa hati ya maandishi ya kumkataa na kupinga madai hayo [71] amabapo Waumini wa Shia walimchukia na kuanza kumlaani kutokana na matendo yake hayo. [72] Numeiriyya: Kundi hili ni kundi la wafuasi wa Muhammad bin Nusair Numairi. Sheikh [73] Tusi katika kitabu chake “Al-Ghaybah” akitoa ripoti juu ya habari za mwanzilishi wa kundi hili alisema; huyu alikuwa ni mmoja wa masahaba wa Imamu Hasan Askari (a.s) ambaye, baada ya kifo chake cha Imamu Hassan Askari, yeye aliamua kulidai ya kwamba; yeye ni wakala na naibu maalumu kutoka kwa Imam Mahdi (a.s). [74] Kulingana na ripoti ya Sa’ad bin Abdullah Ash’ari katika kitabu “Al-Maqalat wal-Firaq”, yaonesha kuwa; Muhammad bin Nusair aliamini juu ya Uungu wa Imamu Hadi (a.s) na alijiona yeye mwenyewe kuwa ni nabii na mjumbe wake. [75] Pia, imesemekana kwamba; yeye alihalalisha matendo ya ushoga na pamoja mambo mengine ya haramu yalio katazwa na Mwenye Ezi Mungu. [76] Shalmaghaniya: Kundi hili ni kundi la wafuasi wa Muhammad bin Ali Shalmaghani, ambye ni miongoni mwa masahaba wa Imam Hasan Askari (a.s). [77] Inasemekana kwamba hapo awali yeye alikuwa ni miongoni mwa mafaqhi wa Shia, na baada ya kifo cha Imamu Hasan Askari (a.s), Shalmaghani alitaraji kupata nafasi ya uwakilishi kutoka kwa Imamu Mahdi (a.s), ila hakufanikiwa kupata nafasi hiyo, na badala yake nafasi hiyo alipewa Hussein bin Rouh. Hiyo ndiyo ikawa sababu ya kupanga njama dhidi ya Hussein bin Rouh na kumsingizia yeye pamoja na wawakilishi wengine maneno ya uongo. [78] Imedaiwa kwamba Shalmaghani aliamini juu ya itikadi ya “hululi” (kuingia kwa roho ya Mungu ndani ya miili ya viumbe) na aliamini itikadi ya tanasukh (reincarnation), akisema kwamba roho ya Mungu iliingia katika kwenye mwili wa Adam na baada yake ikaendelea kuingia katika miili ya manabii wengine na mawasii wao hadi kufikia Imamu Hasan Askari, na baada yake, roho hiyo ilihululi (iliingia) katika mwili wake yeye. [79] Katika moja ya barua kutoka kwa Imam Mahdi (a.s), imeripotiwa kwamba; Imamu Mahdi (a.s) amemlaani Shalmaghani na kujitenga naye, akimhukumu kwa kwa tendo la kuritadi (kurejea nyuma kutoka katika imani ya Uislamu). [80] Hilaliyah: Ni Wafuasi wa mtu anayeitwa Ahmad bin Hilal Al-Abarti, [81] naye ni miongoni mwa masahaba wa Imamu Hadi (a.s) ambaye pia alikuwa ni sahaba Imamu Hassan Askari (a.s). [82] Kulingana na ripoti ya Sheikh Tusi katika kitabu kiitwacho “Al-Ghaybah”; Baada ya kifo cha Imamu Hassan Askari (a.s), Ahmad bin Hilal, alikataa na kuukanusha uwakilishi wa Muhammad bin Othman (ambaye alikuwa ni mwakishi maalumu wa Imamu Mahdi (a.s)) na baada ya muda, alilaaniwa kupitia ujumbe ulio pokewa kutoka kwa Imamu Mahdi (AS). [83] Balaliyyah: Hili ni kundi lililohusishwa na Muhammad bin Ali bin Balali. [84] Inasemekana kwamba; yeye hapo mwanzoni alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Imamu Hasan Askari (a.s) [85] na ni wakili maalumu wa Imamu wa Mahdi (a.s) katika kupokea zaka, khumsi pamoja na michngo mengine; [86] hata hivyo, baada ya Muhammad bin Othman kuchaguliwa kama naibu kwa niaba ya Imamu wa Mahdi (a.s), yeye alidai mali zote zilizokuwa chini ya uangalizi wake, na hatimae kukataa uwakilishi wa Muhammad bin Othman, yeye alikataa katu kurejesha mali hizo na kujiona kuwa yeye mwenyewe ndiye naibu halali. [87] Taahira za Maghulati Katika Madhehebu ya Shia Kulingana na maoni ya watafiti mbali mbali; Maimamu (a.s) na wanazuoni wa Kishia, walijitahidi kadri ya uwezo wao kupambana na Maghulati, jitihada zao zote zilijikita kwenye lengo la kuzokomeza fikra za Kighuluu kwa nia kuepusha mchanganyiko kati ya Shia na Maghulati, pamoja na kuzuia kuenea kwa fikra zao potofu; hata hivyo, Maghulati walikuwa na athari mbaya mno kwenye madhehebu ya Shia. [88] Kusema kwao uongo na kuuhusisha uongo huo kwa Maimamu wa Shia, kujinasibisha kwao kwa Maimamu, na kuziegemeza imani zao potofu kwa Maimamu, mbali na kuharibu sifa za Maimamu, pia wao walikuwa ndio chanzo cha chuki na uadui wa watu dhidi ya Maimamu na Mahia kwa jumla. Wao walikuwa ndio sababu ya kutengwa kwa Mashia katika jamii ya Kiislamu. [89] Pia kule Maghulati kutengeneza na kughushi baadhi ya imani, au kuunda imani za ushirikina na potofu na kuzinasibisha imani hizo na masahaba wa karibu wa Maimamu wa Shia, walikuwa ndio chimbuko la kuharibu sifa za masahaba, na matokeo yake, kuharibu sifa na hadhi za Maimamu wa Shia. [90] Maghulati walikuwa na mchango mkubwa katika kuharibu jina la Mashia na kuchafua fikra za kimapinduzi za upande wa madhehebu ya Shia. [91] Kulingana na Ne’ematollahi Safiriy Furushani, mtafiti wa historia, ni kwamba; Maghulati hawakuwa na nafasi ya moja kwa moja katika miamko ya fikra za kimapinduzi za Mashia dhidi ya wapinzani wao; lakini maadui wa Shia walikuwa wakitumia sifa ya Ughulu katika kuchafua majina ya viongozi wa upinzani, na kuunda madhehebu kwa jina la Maghulati. [92] Pia baadhi ya Maghulati, kwa kujinasibisha na viongozi wa upinzani, walichangia katika kuchafua majina ya viongozi hao wa upinzani na kupotosha mwelekeo na fikra za upinzani huo. Kwa mfano, kikundi cha Maghulati kutoka madhehebu ya Maghayriya, kwa kudai kuungwa mkono kwao naMuhammad bin Abdullah bin Hassan, walitekeleza mauaji dhidi ya wapinzani wao; ambapo Mansur ambaye ni Khalifa wa Bani Abbasi, aliyahusisha matendo haya na Muhammad bin Abdullah. [93] Kwa ujumla, Maghulati na imani zao za kupindukia mipaka ilikuwa ndio nyenzo na kisingizio kilichotumiwa na maadui wa Shia. Maadui wa walizitangaza imani za Maghulati na kuzihusisha na Mashia, walifanya hivyo ili waonyeshe sura mbaya ya Mashia katika kupindukia kwao mipaka na kushikamana kwao na imani potofu. Pia jambo hili bado linaonekana kutendwa baadhi ya Mawahabi au hata baadhi ya watafiti wa Uislamu wa Kimagharibi. Kuna wengi ambao wanajaribu kuhusisha baadhi ya imani za kupindukia mipaka za makundi ya Maghulati, ahali ya kwamba Maimamu na wanazuoni wa Shia wameyakataa makundi hayo na kukataa imani zao potofu. [94] Kwa mtazamo wa Safari Furushani, ni kwamba; Kule Maghulati kutumia mbinu za kuzishughulisha akili za Maimamu ili waweze kuvutika nao, wao liweza kuzichota baadhi ya akili za Mashia wenye nyoyo na akili dhifu, na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa safu za Mashia, wao pia walichangia kupoteza na kupunguza nguvu za Mashia na hatimae kusababisha madhara yasiyoweza kukarabatika kirahisi katika madhehebu ya Shia. [95]