Nasibi

Kutoka wikishia

Nasibi au Mchukivu (Kiarabu: الناصِبي) ni mtu mwenye chuki na uadui juu ya Imam Ali (a.s) au mmoja wa Ahlul-Bayt (a.s), na anadhihirisha na kuonyesha wazi chuki na uadui wake huo. Kukana fadhila za Ahlul-Bayt (a.s), kuwalaani na kuwatusi Maimamu (a.s) na vilevile kuwafanyia uadui Waislamu wa madhehebu ya Shia ni mambo ambayo yametambuliwa kuwa mifano na vielelezo vya unasibi (chuki na uadui dhidi ya Imam Ali au mmoja wa Ahlul-Bayt).

Kwa mtazamo wa mafakihi wa Kishia manasibi ni najisi na wako katika hukumu ya makafiri; kwa msingi huo haijuzu kula mnyama aliyechinjwa na wao, kama ambavyo haijuzu kuwapatia sadaka wala kuoana nao. Kadhalika manasibi hawawarithi Waislamu.

Kwa mujibu wa wahakiki wa zama hizi, unasibi ulianza sambamba na kuuawa Othman na ulichukua sura rasmi katika zama za utawala wa Bani Umayyah. Kuzuia kuenea fadhila za Ahlul-Bayt, kuwaua Mashia na kumtusi Imam Ali (a.s) katika mimbari, ni katika matokeo ya unasibi ambayo yametajwa kuwa yalifanyika katika zama hizo. Muawiyah bin Abi Sufiyan, makhawarij, Othmaniyah na Hariz bin Othman wametambuliwa kuwa ni manasibi. Wanazuoni na wasomi wa Kishia wameandika athari na vitabu mbalimbali kuhusiana na manasibi na unasibi.

Utambuzi wa maana

Nasb ina maana ya kufanya uadui kwa dhahiri na uwazi dhidi ya Ahlul-Bayt au wafuasi na watu wanaowapenda wao. [1] Ni kwa msingi huo ndio maana kuwafanyia uadui wapenzi wa Ahlu-Bayt (a.s) na Mashia wao [3] kutambuliwa kuwa ni unasibi pale tu uadui huo utakapokuwa ni kwa sababu ya wao kuwapenda [4] na kuwafuata Ahlul-Bayt (a.s). [5]

Maulamaa mashuhuri wa Kiislamu, wanamtambua Nasibi kwamba, ni mtu ambaye ana uadui na Ahlul-Bayt na uadui wake anaufanya kwa wazi na dhahiri [6] na baadhi wamelifanya suala la kumchukia Imam Ali (a.s) kuwa ni sehemu ya dini yao. [7] Wao wanaamini kwamba Imam Ali ni muovu au kafiri, [8] wengine ni wabora kuliko yeye, [9] kutusi na kuwalaani Ahlu-Bayt, [10] kukana fadhila zao, [11] na kuchukia kutajwa na kuenezwa sifa zao [12] kwamba, ni vielelezo na mifano ya wazi ya mtu kuwa nasibi.

Hassan bin Farhan Maliki, mmoja wa Maulamaa wa Ahlul-Bayt (a.s) anasema kuwa, aina yoyote ili ya kwenda kinyume na Ali na Ahl-Bayt ni mfano wa mtu kuwa Nasibi. [13] Aidha ameongeza kuwa, kudhoofisha hadithi sahihi zinazomsifu Imam Ali, kuamini kufanya kwake makosa katika zama za ukhalifa wake, kuchupa mipaka katika kuwasifia maadui zake, kutilia shaka katika ukhalifa wake na kukataa kumpa baia na kiapo cha utii ni mifano na vielelezo vya unasibi. [14] Muhadith Bahrani ambaye ni mpokezi wa hadithi na mmoja wa mafakihi wa Kishia anasema, kuwatanguliza watu wengine mbele ya Ali katika Uimamu (kuukubali Uimamu wao) na chuki dhidi ya Ali ni huo ni mfano na kielelezo cha chuki na uadui dhidi yake. [15]


Ahlu-Sunna sio manasibi

Mafakihi mashuhuri wa Kishia wanasema kuwa, nasibi ni mtu ambaye anawafanyia uadui Ahlul-Bayt na anadhihirisha bayana uadui wake, kwa msingi huo kwa itikadi yao ni kwamba, Ahlu-Sunna ambao wamedhihirisha mapenzi na huba yao kwa Ahlu-Bayt sio manasibi. [16] Hata hivyo Muhadith Bahrani yeye anaamini kwamba, nasibi ni mtu ambaye anawatanguliza na kuwaona bora watu wengine kuliko Imam Ali (a.s) na akawa ni mwenye kuamini Uimamu wao. [17] Hoja yake ni hadithi ambayo inaeleza kwamba, kuamini Uimamu wa wasiokuwa Ahlu-Bayt ni unasibi. [18] Swahib al-Jawahir anasema kuwa, kauli hiyo ni kinyume na sira na utendaji wa Mashia, [19] na ametilia shaka juu ya kuwa sahihi wa maana na mapokezi ya hadithi hii. [20] Kitabu chenye anuani ya “Maal al-Nasib Wa anahu Lais Kull Mukhalif Nasiba” kinachonasibishwa na Sayyied Abdallah Jazairi msomi na mwanazuoni wa Kishia, kinaonyesha kupinga kwake Masuni kuwa Manasibi. [21]

Hukumu za nasibi

Kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa Kishia ni kwamba, manasibi ni najisi [22] na wako katika hukumu ya makafiri [23]. Katika vitabu vya fikihi katika mlango wa kuwa najisi makafiri, kumejadiliwa pia unasib na nasibi. [24]

Baadhi ya hukumu za manasibi ni:

  • Haijuzu kula walichokichinja wao. [25]
  • Haijuzu kuoana nao. [26]
  • Haijuzu kuwaswalia Sala ya maiti. [27]
  • Haijuzu kumfuata nasibi (kumfanya Imam) katika Swala. [28
  • Haijuzu kumfanyia hijja kwa niaba nasibi. [29]
  • Manasibi hawawarithi Waislamu. [30]
  • Haijuzu kuwapa sadaka manasibi. [31]
  • Haijuzu kuwapatia kafara manasibi. [32]

Kuibuka muelekeo wa Unasibi

Baadhi ya wahakiki wa zama hizi wanaamini kwamba, muelekeo wa unasibi na chuki dhidi ya Imam Ali na Ahlul-Bayt (a.s) ulianza baada ya kuuawa Othman bin Affan na hilo likawa rasmi katika zama za utawala wa Bani Umayyah. [33] Kwa mujibu wa ripoti za vyanzo vya kihistoria ni kwamba, Muawiyah bin Abi Sufiyan wakati mwaka 41 Hijiria alipomteua Mughira bin Shu’ba kuwa mtawala wa Kufa alimuamrisha amtaje kwa ubaya Imam Ali na kuwasema vibaya pia wafuasi na masahaba zake. [34] Baada yake, makhalifa wa Bani Umayyah mpaka katika zama za Omar bin Abdul Aziz [35] walikuwa wakimtusi na kumaali Ali katika mimbari. [36].

Hakim al-Nishaburi, msomi na mwanazuoni wa Kisuni ameitaja karne ya 4 Hijiria kuwa kipindi cha maadui wa Imam Ali (a.s) na kueleza kwamba, sababu iliyomfanya aandike kitabu cha: Fadhail Fatma al-Zahraa” ni kukabiliana na hali hii. Ameandika kuhusiana na anga na mazingira yaliyokuwa yakitawala katika karne ya 4 Hijria ya kwamba: Zama zetu zimetufanya tuwe na viongozi ambao ili watu wawakurubie basi lazima wafanye uadui dhidi ya aali-Rasul na wawadogoshe. [37]


Matokeo

Baadhi ya matokeo ya kuweko chuki za wazi dhidi ya Ali na Ahlul-Bayt (a.s) katika zama za utawala wa Bani Umayya ni:

  • Kuingizwa hadithi bandia katika vitabu vya Ahlu-Sunna zikiwa na madhumuni ya kuwadhoofisha Ahlul-Bayt na kukana fadhila zao kupitia wapokezi wa hadithi ambao ni manasibi. [38]
  • Marufuku ya kuitwa watoto kwa jina la Ali na kuuawa watoto waliokuwa na jina la Ali. [39]
  • Kuadhibiwa na kuuawa watu ambao walikuwa wakibainisha na kuelezea sifa na fadhila za Imam Ali (as), walikuwa wakikataa kumtaja kwa ubaya au hawakuwa wakitaja na kunukuu fadhila za Muawiyah, kupigwa mijeledi Atiyah bin Saad mmoja wa Mashia wa Imam Ali (as) kwa amri ya Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi [40] na kuuawa Ahmad bin Ali al-Nisai mmoja wa waandishi wa Sihah al-Sittah (sahihi sita) za Ahlu-Sunna, [41] ni miongoni mwa matukio hayo. [42]

Manasibi mashuhuri

Katika vyanzo kuna baadhi ya watu na makundi ambayo yametajwa kuwa ni manasibi:

  • Muawiya bin Abi Sufiyan, alikuwa mtawala wa kwanza wa Bani Umayyah ambaye alitawala Damascus kwa muda wa miaka 20. [43] Ibn Abil-Hadid Mu’tazila, aliyefafanua na kutoa sherh ya Nahaj al-Balagha amenukuu kutoka kwa Jahidh kwamba, mwishoni mwa hotuba za Swala ya Ijumaa, Muawiyah alikuwa akimlaani Ali (a.s) na alikuwa akisema, jambo hili linapaswa kuenezwa kwa namna ambayo mtu asinukuu fadhila yoyote kutoka kwa Ali. [44]
  • Othmaniyah: Ni watu ambao walikuwa wakiamini kwamba, Imam Ali alimuua Othman bin Affan au alisaidia jambo hili. [45] Na ni kwa msingi huo walikataa kumpa baia na kiapo cha utii. [46] Ibn Hajar al-Asqalani, mtambuzi wa wapokezi wa hadithi ambaye ni Msuni aliyeishi katika karne ya 9 Hijria, amewatambulisha manasibi kwamba, ni kundi ambalo linaamini kwamba, Imam Ali alimuua Othman au alisaidia kuuawa kwake. [47] Kundi hili kutokana na kuchupa mipaka katika kumpenda Othman liliamua kumdhoofisha na kumdogosha Imam Ali (a.s). [48]
  • Makhawariji: Hili lilikuwa ni kundi miongoni mwa jeshi la Imam Ali (a.s) katika vita vya Siffin ambalo lilimtuhumu Imam Ali kuwa amekufuru na hivyo likaanzisha uasi dhidi yake. Kutokana na uadui wao dhidi ya Imam Ali, hawa pia wanafahamika kwa jina la Manasibi au Nasiba. [49]
  • Hajjaj bin Yusuf al-Thaqafi (aliaga dunia 95 Hijria): Kwa mujibu wa Ibn Masu’d mwandishi wa historia wa karne ya 4 Hijiria ni kwamba, Hajjaj alikuwa na uadui na Ahlul-Bayt. [50] Hajjaj alikuwa akiwaua watu ambao hawakuwa wakitangaza kujibari na kujitenga na Imam Ali (a.s) na wafuasi wake. [51] Alikuwa akiwaua Mashia na alikuwa akiwatia mbaroni kwa dhana na tuhuma ndogo kabisa. [52] Katika zama za utawala wa Abdul-Malik awali Hajjaj alikuwa mtawala wa Hijaz na kisha baadaye akawa mtawala wa Iraq. [53]
  • Hariz bin Othman alikuwa akimtusi Imam Ali (a.s) katika mimbari. [54] Alikuwa akiipotosha hadithi isemayo: Wewe kwangu ni mithili ya Haruna kwa Mussa” iliyokuwa ikibainisha fadhila za Ali na kuwa: "Wewe kwangu ni mithili ya Qarun kwa Mussa”. [55] Ibn Habban mmoja wa watalamu wa elimu ya Rijaal anasema: Hariz alikuwa akimlaani mara 70 Imam Ali (a.s) kila siku asubuhi na usiku. [56]
  • Mughira bin Shu’ba, Wakati alipokuwa mtawala wa Kufa katika zama za utawala wa Muawiyah, alikuwa akimtusi na kumsema kwa ubaya katika mimbari Imam Ali pamoja na Mashia wake na alikuwa akimlaani. [57] Yeye alikuwa mmoja wa masahaba wa Mtume ambaye amezungumziwa nafasi na mchango wake katika kuhujumiwa na kushambuliwa nyumba ya Bibi Fatma Zahra (a.s). [58]
  • Mutawakkil Abbasi: Huyu alikuwa na chuki na Imam Ali na alikuwa akikaa pamoja na manasibi. [59] Alikuwa akipora mali za Mashia na kuwaua. [60] Chuki ya Mutawakkil kwa Ahlul-Bayt ilikuwa kubwa kiasi kwamba, mwaka 236 Hijiria alitoa amri ya kubomolewa kaburi la Hussein bin Ali (a.s); na kwa msingi huo kaburi la Imam Hussein na nyumba zote pamoja na athari zilizokuwa zikilizunguka eneo hilo zikabomolewa. Eneo hilo likafunguliwa maji, ardhi ikalimwa na kufanywa shamba. [61]
  • Ibn Taymiyyah: Huyu ni mmoja wa viongozi wa kifikra wa Usalafi. Baadhi ya wahakiki wa Kishia wakiwa na lengo la kuthibitisha kwamba, alikuwa Nasibi wanaashiria hatua yake ya kukana hadithi ya Radd al-Shams, [62] kudhoofisha hadithi ya Ghadir, [63] na vilevile uadui wake kwa Mashia. [64] Kadhalika Ibn Hajar al-Asqalani amesema, baadhi wamemnasibisha Ibn Taymiyah na nifaq kutokana na maneno yake kuhusu Imam Ali (a.s). [65]

Vitabu

Maulamaa na wahakiki wa Kishia wameandika vitabu na athari kuhusiana na maana ya unasibi na hukumu zake. [66] Miongoni mwa vitabu hivyo ni:

  • Al-Nasb wal-Nawasib, kilichoandikwa na Mohsin Muallim kwa lugha ya Kiarabu. Ndani ya kitabu hiki kumebainishwa masuala mbalimbali kama maana ya unasibi, vielelezo vyake, [67], hukumu ya manasibi, [68] na taathira ya mtu kuwa na chuki dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s). [69] Mwandishi ametaja pia kwamba, uadui na chuki dhidi ya Imam Ali ni kigezo cha mtu kuwa Nasibi, [70] na kumetajwa majina ya zaidi ya watu 250 kwa anuani ya Manasibi. [71] Kadhalika katika kitabu hiki, kumetajwa maeneo ambayo Manasibi walikuwa wakiishi. [72] Kitabu hiki kilichapishwa mwaka 1418 Hijria Beirt, Lebanon. [73]

Al-Shahab al-Thaqib fi bayan ma'na al-nawasib, mwandishi: al-Muhaddith al-Bahran. [74]

Kadhalika katika anuani ya baadhi ya majibu yaliyoandikwa na Maulamaa wa Kishia wakikisoa vitabu vya wapinzani, neno manasibi, limetumika. [76]

Kitabu cha: Masa'ib al-nawasib fi l-radd ala l-nawaqid al-rawafidh kilichoandikwa na Qadhi Nur Allah ShushtarI [77] na Baadh Mathalib al-nawasib fi Naqdh Fadhaih al-Rawaafidh kilichoandikwa na: Abd al-Jalil al-Qazwini, [78] ni miongoni mwa athari hizo. Aidha kumetajwa athari 29 katika kitabu cha al-Nasb Wal-Nawasib kuhusiana na unasibi na Manasibi. [79]

Vyanzo

  • Āqā Buzurg Tihrānī. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-shīʿa. Tehran: Ismāʿīlīyān, 1408 AH.
  • Bahjat, Muḥammad Taqī. jamiʿ al-masāʾil. Qom: Office of that late Ayatollah Bahjat, 1426 AH.
  • Baḥrani, Yūsuf b. Aḥmad al-. Al-Ḥadāʾiq al-nādira fī aḥkām al- ʿitrat al-ṭāhira. Daftar-i Nashr-i Islami, 1405 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Beirut: Jam'iyat al-Mustashriqin al-Almaniya, 1400 AH.
  • Fāḍil al-Miqdād, Miqdad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Tanqīh al-rāʾiʿ lī mukhtaṣar al-shariʿa'. Qom: Ayatollah Mar'ashi Najafi Library Publications, 1404 AH.
  • Ḥakim al-Nayshābūrī, Muḥammad b. ʿAbd Allāh. Faḍaʾil Fāṭima al-Zahrā. Cairo, Dar al-Furqan, 1429 AH.
  • Ibn Abi l-Ḥadīd, ʿAbd al-Ḥamīd b. Hibat Allāh. Sharḥ Nahj al-Balāgha. Qom: Ayatollah Mar'ashi Najafi Library, 1404 AH.
  • Ibn al-Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fi l-tārīkh. Beirut: Dar Sadir, 1965.
  • Ibn Barraj al-Ṭarābulusī, ʿAbd al- ʿAzīz. Al-Muhadhdhab. Qom: Daftar-i Intisharat-i Islami, 1406 AH.
  • Ibn Ḥajar al- ʿAsqalānī, Ahmad b. Ali. Al-Durar al-kamina fi a'yan al-mi'a al-thamina. Beirut: Dar Sadir.
  • Ibn Ḥajar al- ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Fatḥ al-bārī bi sharḥ Saḥiḥ al-Bukhāri. Beirut: Ihya' al-Turath al-Arabi, 1408 AH.
  • Ibn Idrīs al-Ḥillī, Muḥammad b. Manṣūr. Ujūbat masāʾil wa rasāʾil fī mukhtalaf funūn al-maʿrifa. Qom: Dalil-i Ma, 1429 AH.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa al-nihāya. Beirut: Dar al-Fikr, 1407 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad b. Saʿd. Al-Ṭabaqʿt al-kubrā. Beirut: Dar al-Kutub al-Ilmiya, 1410 AH.
  • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Majmu'at al-fatawa.
  • Ibn Taymiyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Halīm. Minhāj al-sunna al-nabawiyya fī naqd al-kalām al-shīʿa al-qadarīyya. Saudi Arabia: Imam Muhammad ibn Saud Islamic University, 1406 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istiʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Beirut: Dar al-Jalil, 1412 AH.
  • Imām Khomeinī. Risāla-yi najāt al-ʿibād. Tehran: The Institute for Compilation and Publication of Imam Khomeini's Works.
  • Mālikī, Ḥasan b. Farḥān al-. Inqādh al-tārīkh al-īslāmī. Jordan: al-Yamama al-Hafiya Inistitute, 1418 AH.
  • Maqrizī, Aḥmad b. Ali. Al-mawaʿiz wa l-iʿtibār fī dhikr al-khiṭaṭ wa l-āthār. London: 2002.
  • Masʿud‭i, ʿAl‭ b. Husayn. Muruj al-Dhahab wa ma'adin al-jawhar. Qom: Dar al-Hijra, 1409 AH.
  • Mizzī, Yūsuf b. ʿAbd al-Raḥmān. Tahdhīb al-kamāl fī asma' al-rijal. Beirut: al-Risala Inistitute, 1413 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad. Al-Jamal wa al-nuṣra li sayyid al-ʿitra fī ḥarb al-Baṣra. Qom: the World Conference of the Millennium of al-Shaykh al-Mufid, 1413 AH.
  • Mughnīa, Muḥammad Jawād al-. Al-shīʿa wa l-ḥākimūn. Beirut: Dar al-Jawad, 2000.
  • Muḥaqqi al-Ḥillī, Jaʿfar b. Ḥusayn al-. Al-Muʿtabar fī sharḥ al-mukhtaṣar. Qom: Sayyid al-Shuhada Inistitute, 1407 AH.
  • Muḥaqqiq al-Karakī, ʿAlī b. Ḥusayn al-. Jamiʿ al-maqāṣid fī sharḥ al-qawāʿid. Qom: Al al-Bayt Inistitute, 1414 AH.
  • Muḥsin al-Muʿallim. Al-Naṣb wa al-nawāṣib. Beirut: Dar al-Hadi, 1418 AH.
  • Najafī, Muḥammad Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ Sharaʾiʿ al-islām. Beirut: Dar Ihya' al-Turath al-Arabi, 1404 AH.
  • Ṣadr, Sayyid Muḥammad al-. Ma warāʾ al-fiqh. Beirut: Dar al-Adwa' li l-Tiba'a wa al-Nashr wa al-Tawzi', 1420 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAli al-. Man lā yahḍuruh al-faqīh. Qom: Daftar-i Intisharat-i Islami, 1413 AH.
  • Samʿānī, ʿAbd al-Karīm b. Muḥammad al-. Al-Ansāb. Heydar Abad: Majlis Da'irat al-Ma'arif al-Uthmaniyya, 1382 AH.
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Din b. ʿAli. Rawḍ al-jinān fī sharḥ irshād al-adhān. Qom: Daftar-i Nashr-Islami, 1402 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Al-Khums fi l-shariʿa al-islāmīya al-gharra'. Qom: Imam Sadiq (a) Inistitute, 1420 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīri al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Dar al-Turath, 1387 AH.
  • Ṭurayhī, Fakhr al-Dīn al-. Majmaʿ al-Baḥrayn. Tehran Murtadawi, 1416 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. Ḥasan al-. Al-Nihāya fī mujarrad li fiqh wa l-fatawa. Beirut: Dar al-Kutub al-Arabi, 1400 AH.
  • Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿ Umar. Rabīʿ al-abrār wa nuṣuṣ al-akhbār. Beirut: al-A'lami li l-Matbu'at Inistitute, 1412 AH.
  • Kawtharī, Aḥmad. Barrasī rīshiha-yi tārīkhi-yi naṣibīgarī. No. 16, winter of 1393 Sh.
  • Al-Majd Sayyid Hasan. Nishānihāyī az nāṣibīgarī-yi Ibn Taymīyya. Sirat Quarterly, no. 12, 1393 Sh
  • Tawallāyi, Raḥmat, Naqībī, Sayyid Abu l-Qāsim. Milāk-i naṣib ingārī, aḥkām wa āthār-i murtabiṭ bar naṣb dar fiqh-i imāmiya. Fiqh wa Usul Journal, Spring of 1396 Sh.