Nenda kwa yaliyomo

Nguzo za Hija

Kutoka wikishia
Waislamu wakiwa katika ibada ya hija

Nguzo za Hija (Arabic: أركان الحج) ni mambo ya kiibada au mambo ya msingi na ya asili ya ibada ya hija, mambo ambayo kuachwa na kutoyatenda kwa makusudi hupelekea kubatilika na kuharibika kwa ibada ya Hija. Kwa mtizamo wa wanazuwoni wa kishia ni kwamba ihram, tawaf (kuzunguka Kaaba tukufu), kusimama katika jangwa na viwanja vya Arafa, kusimama katika viwanja vya Mash'aril-Haraam (muzdalifa) na kufanya sa'ayi kati ya swafa na mar'wa ni miongoi mwa nguzo za asili za ibada ya Hija. Baadhi ya wanazuwoni wa Imamiyah wanaamini kwamba nia, talbiyah (kiitikio cha kusema Labbaika Allahumma Labbaika) na mpangilio katika matendo ya Hija pia ni katika nguzo za asili za ibada ya Hija.

Imesemwa kwamba kuachwa na kutotekelezwa kwa mambo ya wajibu ambayo ni nguzo kwa makusudi au kwa sababu ya ujinga na kutojua hukumu ya kufanya hivyo, hupelekea kubatilika na kuharibika kwa ibada ya Hija, Lakini kuacha na kutotekeleza mambo ya wajibu yasiyo kuwa nguzo na ambayo si nguzo za asili katika ibada ya Hija hata kama itakuwa ni kwa makusudi, jambo hilo halipelekei kubatilika na kuharibika kwa ibada ya Hija na kwamba Mukallaf anaweza kumuweka naibu wa kuyatekeleza mambo hayo kwa niaba yake ikiwa ni njia ya (kufidia mambo yaliyo achwa).

Nguzo za Hija

Neno nguzo za Hija hutumika kuelezea mambo ya wajibu katika ibada ya hija, kwa ibara nyingine ni mambo ya asili na ya msingi katika ibada ya Hija nguzo ambazo kutozitekeleza kwa makusudi hupelekea kubatilika kwa ibada ya Hija.[1] Nguzo katika istilahi ya kifiqhi ni jambo au tendo ambalo kutolifanyika kwake kwa makusudi au kwa kusahau hupelekea kubatilika na kuharibika kwa ibada na miongoni mwake ikiwa ni swala.[2]

Kwa mtazamo wa wanazuoni wa fiqhi na sharia wa kishia ni kuwa ihram (nguo za ihram), tawafu, kusimam kwenye viwanja vya Arafa, kusimama kwenye viwanja vya Mash'aril-haraam na kufanya sa'ayi kati ya swaafa na mar'wah huzingatiwa kuwa ni miongoni mwa nguzo za Hija.[3] Ama kuhusiana na kwamba nia na talbiya (kusema Labaika Allahumma Labaika) ni katika nguzo za Hija au laa, na utaratibu kati ya matendo ya Hija ni jambo ambalo ndani yake kuna tofauti na nadharia nyingi. Shahidi wa kwanza[4], Swaimariy,[5] Kashiful-ghitwaa[6] na Muhaqqiq Karakiy[7] ni miongoni mwa wanazuoni na wanasheria wakifikihi wa kishia ambao wanaitakidi ya kwamba mambo hayo pia ni nguzo za Hija.

Mafakihihi na wanazuoni wa madhehebu za kisunni wametofautiana kuhuisiana na idadi ya nguzo za Hija na wanatofauti kubwa kuhusu jambo hilo, kwa mujibu wa mtazamo na itikadi ya mafakihi na wanazuoani wa kisheria wa madhehbu ya Shafi'i ni kuwa, Hija ina nguzo sita,[8] na kwa mujibu wa mtazamo wa mafakihi wa madhehebu ya Maalik na maulamaa wa madhehebu ya Maaliki ni kuwa ina nguzo nne[9] na kwa mujibu wa itikadi na mtazamo wa mashuhuri kati ya wanazuoni wa Hanafi ni kuwa ina nguzo mbili[10]. Mashaafi'i wanaitakidi kwamba pamoja na nguzo zingine, kunyoa na kupunguza nywele pia wanazitambua kuwa ni nguzo za Hija.[11] wanazuwoni wa madhehebu ya Maaliki hawakukubaliana kwamba kisimamo katika viwanja vya Mash'ari ni miongoni mwa nguzo za Hija[12] na wanazuwoni wa madhehebu ya Hanbali walitaraddadi na kutia shaka kuhusiana na kwamba saa'yi kati ya swafa na mar'wah ni miongoni mkwa nguzo za Hija.[13] wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi pia hawakukubali kuwa ihram, kisimamo cha kwenye viwanja vya Mash'ari na sa'ayi kati ya swafa na Mar'wah ni miongoni mwa nguzo za Hija[14]

Hukumu za Hija

  • Tofauti kati ya nguzo za Hija na mambo ya wajibu ya Hija ambayo sio nguzo na wala hayahesabiki katika nguzo za Hija ni kuhusiana na suala la kubatilika na kuharibika kwa Hija kwa kuyaacha na kutoyafanya kwa makusudi. Katika sura ambayo iwapo moja wapo kati ya nguzo za Hija zitachwa na kutofanya kwa makusudi na sio kwa kusahau, basi ibada ya Hija inabatilika na kuharibika,[15] lakini ikiwa mambo ya wajibu ambayo sio nguzo (kama vile kunyoa na kupunguza nywele, kurusha vijiwe na kuchinja) ikiwa mambo haya pia yataachwa kwa makusudi haitapelekea kubatilika kwa Hija.[16] kuacha kutekeleza nguzo kwa sababu ya kutofahamu na kwa sababu ya ujinga na kutofahamu hukumu yake pia kwa mtizamo wa baadhi ya wanazuoni wa fiqhi ni sawa na kuacha kwa makusudi nguzo ya Hija hivyo hupelekea kubatilika kwa ibada ya Hija.[17]
  • Kuacha visimamo viwili (kisimamo cha Arafa na Mash'ari) sawa iwe kwa makusudi au kwa kusahau hupelekea kubatilika kwa ibada ya Hija.[18]
  • Kwa Mujibu wa fat'wa za wanazuoni na mafakihi wa Kishia ni kwamba ikiwa moja wapo kati ya nguzo za Hija itasahaulika au iwapo nguzo yoyote ya Hija itasahaulika, katika sura pekee ambayo haitawezekana kurudi na kurejea au ikawa vigumu na taabu kurudi makkah na kumuweka au kumtafuta naibu au uwezekano wa kumuweka naibu ukawa haupo, lakini katika sura ambayo kusahaulika kwa mambo ya wajibu ambayo sio nguzo katika sura yoyote ile ambayo kuna uwezekano wa kumuweka naibu basi awekwe naibu katika kila sura ambayo uwezekano wa kumuweka naibu upo.[19]
  • Kwa mujibu wa fat'wa za wanazuoni mashuhuri wa Imamiyah, mustabswir (ni Muislamu ambae amejiunga na kuingia kwenye madhehebu ya Kishia) sio lazima ibada ya Hija ambayo ameitekeleza kwa mujibu wa madhehebu yake ya mwanzo Hija ambayo aliitekeleza kwa njia sahihi sio lazima kuirudia ibada au Hija hiyo, kwa sharti kwamba nguzo za Hija awe amezitekeleza sawa sawa zikiwa sahihi, (20) ama kuhusiana na suala kwamba je, kigezo ni kwamba ni nguzo na rukni katika madhehebu ya mwanzo au nguzo na rukni katika madhehebu ya kishia, kuhusu suala hilo kuna tofauti kati ya wanazuoni.[20]

Rejea

  1. Shahidul-awwal, Ad-duruusus-shar'iyah, 1417 H, juz. 1, uk. 328; Swaimariy, Ghaayatulmaraam, 1420 H, juz. 1, uku. 456; Najafiy, Jawaahirul-kalaam, 1404 H, juz. 18, uk. 136; Golpaiganiy, Kitaabul-hajji, 1403 H, juz. 1, uk. 17
  2. Mishkiiniy, Mustwalahaatul-fiq'hi, 1428 H, uk. 274-275.
  3. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, 1404 H, juz. 18, uk. 136.
  4. Shahidul-awwal, Ad-duruusus-shar'iyah, 1417 H, jUZ. 1, uk. 328-329.
  5. Swaimariy, Ghaayatulmaraam, 1420 H, juz. 1, uk. 456
  6. Kashiful-ghitwaa, Kashufl-ghitwaa, 1422 H, juz. 4, uk. 470-471.
  7. Muhaqqiq Karakiy, Jaamiul-maqaaswid, 1414 H, juz. 3, uk. 110.
  8. Sharbiiniy, Mughnil-muhtaaj, 1418 H, juz. 1, uk. 745-746.
  9. 9. Karamiy, Dalilut-twaalib, 1425 H, juz1, uk. 107-108.
  10. Samarqandiy, Tuhfatul-fuqahaa, 1405 H, juz. 1,uk. 381.
  11. Sharbiiniy, Mughnil-muhtaaj, 1418 H, juz. 1, uk. 745-746.
  12. Ibnu Qudaamah, Al-mughniy, 1388 H, juz. 3, uk. 351-352.
  13. Samarqandiy, Tuhfatul-fuqahaa, 1405 H, juz. 1, uk. 381.
  14. Shahidul-awwal, Ad-duruusus-shar'iyah, 1417 H, juz. 1, uk. 328.
  15. Ibnu Fahdi Al-hilliy, Al-muhadhabul-baariu, 1407 H, juz. 2, uk. 206; Swaimariy, Ghaayatulmaraam, 1420 H, juz. 1, uk. 456, Najafiy, Jawaahirul-kalaam, 1404 H, juz. 18, uk. 136; Golpaiganiy, Kitaabul-hajji, 1403 H, juz. 1, uk. 17.
  16. Muhaqqiq Karakiy, Jaamiul-maqaaswid, 1411 H, juz. 3, uk. 201; Shahidut-thaniy, Masaalikul-afhaam, 1413 H, juz. 2, uk. 275; Muusawiy Aamuliy, Madaarikul-ahkaam, 1410 H, juz. 8, uk. 174.
  17. Shahidul-awwal, Ad-duruusus-shar'iyah, 1417 H, juz. 1, uk. 328. Shahidut-thaniy, Masaalikul-afhaam, cha mwaka 1413q, j2, ukurasa 275, Hilliy, Al-jaamiu lis-sharaaiyi, 1405 H, uk. 180-181.
  18. Ibnu Fahdi Al-hilli, Al-muhadhabul-baariu, 1407 H, juz. 2, uk.206; Swaimariy, Ghaayatulmaraam, 1420 H, juz. 1, uk. 456.
  19. Ibnu Hamzah, Al-wasiilah, 1408 H, uk. 157; Ibnu Idris, As-saraair, 1411 H, juz. 1, uk. 518-519.
  20. Najafiy, Jawaahirul-kalaam, 1404 H, juz. 17, uk. 304.

Vyanzo

  • Ibnu Idris, Muhammad bin Ahmad, As-saraairul-haawiy litahriiril-fataawa, Qom, Intishaarat islaami, mwaka 1410 H.
  • Ibnu Hamzah Tousiy, Muhammad bin Aliy, Al-wasiilah ilaa nailil-fadhiilah, Qom, Intishaaraat kitaab khooneh Mar'ashi Najafiy, mwaka 1407 H.
  • Ibnu Fahd Hilliy, Al-muhadhabul-baariu, Qom,. Intishaarat islaamiy, mwaka 1407 H.
  • Ibnu Qudaamah, Abdallah bin Ahmad, Al-mughniy, Kairo, Maktabatul-qaahirah, mwaka 1388 S.
  • As-sharbiiniy, Muhammad bin Khatwiib, Mughnil-muhtaaj, Bairut, Daarul-ma'aarifah, mwaka 1418 H.
  • Al-karamiy, Mar'aa bin Yusuf, Dalilut-twaalib linailil-matwaalib, Riyaadh, Darut-twayyibah linnashri wat-tawzi'i, mwaka 1425 H.
  • Bahraaniy, Yusuf bin Ahmad, Al-hadaaiqun-naadhirah fii Ahkaamil-itratit-twaahirah, kwa juhudi za Aliy Aakhondiy, Qom, Nashru Islaamiy mwaka 1363sh.
  • Hilliy, Yahya bin Saiid, Al-jaamiu lils-sharaai'i, Biija, Muassasatu Sayyidis-shuihadaa (a.s) Al-ilmiyah, mwaka 1405 H.
  • Samarqandiy. Alaaud-din Muhammad, Tuhfatul-fuqahaa, Bairut, Darul-kutubil-ilmiyah, mwaka 1405q.
  • Shahiidul-awwal, Muhammd bin Makkiyh, Ad-duruusus-shariyah fi Fiqhil-imamiyah, Qom, Intishaaraat Islaamiy, mwaka 1417 H.
  • Shahiidut-thaniy, Zainud-din bin Aliy, Masaalikul-af'haam, Qom, Muassasatul-ma'aarifil-islaamiyah, mwaka 1413 H.
  • Swaimariy, Muflihu bin Hasan, Ghaayatul-maraam fii sharhi sharaai'il-islaam, Bairut, Darul-hudaa, mwaka 1420 H.
  • Golpaiganiy, Muhammad ridhaa, Kitabul-hajj, Qom, Darul-qur'anil-kariim, mwaka 1403 H.
  • Muhaqqiq Karakiy, Aliy bin Husein, Jaamiul-maqaaswid fii sharhil-qawaaidi, Qom, Aalul-baiti, mwaka 1414 H.
  • Mishkiiniy, Miirzaa Aliy, Mustwalahaatul-fiqhi, Qom, Al-hadiy, mwaka 1428 H.
  • Muusawiy Aamuliy, Muhammad bin Aliy, Madaarikul-ahkaam, Qom, Muassasatu Aalul-baiti, mwaka 1410 H.
  • Najafiy, Muhammad HaSsan, Jawaahirul-kalaam fii sharhi sharaa'iul-islaam, Bairut, Daru Ihyaait-turaathil-arabiy, mwaka 1404 H.

{[End}}