Sheikh Ibrahim Zakzaky

Kutoka wikishia
Sheikh Ibrahim Zakzaky

Sheikh Ibrahim Zakzaky (Kiarabu: إبراهيم بن يعقوب الزكزكي) (alizaliwa 1953), ni mwanazuoni wa Kishia na Kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Nigeria. Zakzaky aliingia katika Ushia na kushikamana na madhehebu hayo akiathirika na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Imamu Khomeini. Ibrahim Zakzaky aliasisi Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kuanzisha shule 300 za Kiislamu ndani ya Nigeria na katika mataifa jirani. Kadhalika alianzisha vituo na taasisi za masuala ya kheri kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha, kitiba na kielimu kwa Mashia.

Kama Zakzaky alivyosema, sambamba na mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (1979), alianza kuhubiri nchini Nigeria kwa kuvutia makumi ya watu, na idadi ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) nchini Nigeria, katika miaka ya 2010 ilifikia mamilioni kutokana na juhudi zake.

Watoto watatu wa Zakzaky waliuawa katika shambulio la vikosi vya jeshi la Nigeria katika maandamano ya Siku ya Quds ya 2015. Pia, Zakzaky alikamatwa na kufungwa jela wakati wa shambulio la vikosi vya jeshi la Nigeria dhidi ya Husseiniyeh ya Baqiyallah katika mji wa Zaria mnamo 2015 huku akiwa amejeruhiwa vibaya hasa jicho. Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hussein Wahid Khorasani Marjaa Taqlid na Sheikh Issa Qasim, Kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain walipaza sauti kulalamikia na kulaani mauaji ya Mashia nchini Nigeria. Kulifanyika pia mikusanyiko na maombolezo katika mataifa ya Iran, Marekani, Australia, Sweden na Uturuki, kupinga utendaji wa serikali ya Nigeria.

Yeye na mkewe baada ya kushikiliwa kwa miaka 6 katika mzingiro wa nyumbani na gerezani, mwaka 2021 waliachiliwa huru na baada ya kufutiwa tuhuma zote walizokuwa wakikabiliwa nazo.

Masomo na maisha yake

Ibrahim Yaqub Zakzaky alizaliwa mwaka 1953 kaskazini mwa Nigeria. [1] Sambamba na masomo yake alijiendeleza na usomaji wa masomo ya dini hadi mwaka 1976 katika mji wa Kano. [2]. Alipata shahada yake ya kwanza katika uchumi kutoka katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello huko Zaria na baada ya muda, alichukua jukumu la kuwa Uimamu wa Sala ya Jamaa katika msikiti wa mojawapo ya shule za kidini. [3] Awali Zakzaky alikuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wanachuo Waislamu na baadaye akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo. [4]

Ibrahim Zakzaky, wakati wa safari yake ya Paris mwaka 1979, alikutana na Imamu Khomeini na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, akiwa na lengo la kujiendeleza zaidi kielimu alijiunga na Hawza ya Qom [5] (Chuo kikuu cha dini) kwa ajili ya kusoma elimu ya juu ya kidini. [6] Zakzaky amezungumzia jinsi alivyaothirika na Imamu Khomeini na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [6] Awali Zakzaky alikuwa Sunni Maliki, na baada ya kukutana na Imamu Khomeini, akawa Shia. [7]

Harakati

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Zakzaky alisafiri hadi Iran na baada ya kurejea alianzisha Harakati ya Kiislamu ya Nigeria katika nchi yake. [8] Alianzisha takribani shule za Kiislamu zipatazo 300 nchini Nigeria na nchi jirani [9] na pia ni mmoja wa wajumbe Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s). [10] Kuanzisha kwa Taasisi ya Al-Shuhadaa kwa lengo la kuwalea na kuwahudumia watoto wa mashahidi na mayatima, kuanzisha kwa Taasisi ya Hisani ya Al-Zahra kwa lengo la kutoa huduma za kijamii na kiraia, na kuanzisha kituo cha tiba kwa lengo la kutoa huduma za matibabu na elimu, ni miongoni mwa hatua na mambo mengine yaliyofanywa na Ibrahim Zakzaky. [11]

Kulingana na Nasiba Zakzaky, mwana wa Ibrahim Zakzaky, kwa juhudi zake, watu milioni 12 wamekuwa Mashia nchini Nigeria. [12] Kama Zakzaky alivyosema, kazi yake ya tablighi mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980 (sambamba na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran) ilivutiwa na makumi ya watu, na baada ya miaka kumi, idadi hiyo ikafikia mamia ya maelfu ya watu, na katika miaka ya 2110 ikafikia mamilioni ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s).[13]

Kukamatwa na kutiwa jela

Wakati wa kumbukumbu ya maadhimisho ya Arubaini mwaka 2015 iliyoandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, vikosi vya usalama vya Nigeria vilifanya hujuma na mashambulio dhidi ya mkusanyiko huo wa kidini wa Mashia na kusababisha vifo vya makumi ya watu. [14] Zakzaky na mkewe pia awali walikamatwa na kutiwa gerezani 2015 wakati wa shambulio la jeshi la Nigeria dhidi ya Husseiniyeh ya Baqiyallah katika mji wa Zaria, ambalo lilisababisha kuuawa na kujeruhiwa kwa idadi kubwa ya Waislamu wa Kishia. [15]

Kabla ya hapo, mnamo 2014, watoto watatu wa Ibrahim Zakzaky waliuawa pamoja na Mashia 33 wakati wa shambulio la wanajeshi wa Nigeria katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds. [16]

Mahakama Kuu ya Nigeria mnamo Septemba 2016, ilipinga kuachiliwa kwa Sheikh Zakzaky [17], lakini mnamo Desemba 2016, iliamuru kuachiliwa kwa Zakzaky na mkewe. [18] Pamoja na hayo hakuachiliwa huru, na Desemba 2017 baada ya kuenea tetesi za kuaga kwake duniani gerezani, alijitokeza mbele ya waandishi wa habari. [19] Mei 2018 alizungumza kwa njia ya simu na mwanawe, ambapo alisema kwamba mauaji ya Mashia katika mji wa Zaria, Nigeria, yalitokana na msaada wa kifedha wa serikali ya Saudi Arabia kwa jeshi la Nigeria. [20]. Zakzaky alifungwa mara tatu na serikali ya Nigeria kuanzia mwaka 1981-1989) yaani jumla ya miaka saba. [21]

Radiamali

Shambulio dhidi ya Waislamu wa Kishia na kuwaua kwao sambamba na kumkamata Zakzaky na mkewe nchini Nigeria lilichochea maandamano na malalamiko mengi nchini Nigeria [22] na sehemu nyingine za dunia ikiwa ni pamoja na Iran, [23] Marekani, Australia, Sweden na Uturuki. [24]

Ayatullah Hussein Wahid Khorasani, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia, mwaka 2014 na katika radimali yake kwa mauaji yaliyofanyika katika maandamano ya Siku ya kimataifa ya Quds nchini Nigeria na vilevile mauaji ya watoto watatu wa Ibrahim Zakzaky na vikosi vya serikali ya Nigeria, alitoa mkono wa pole katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Zakzaky, kutokana na kuuawa shahidi kwa Mashia na watoto wake watatu. [25] Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtaja Ibrahim Zakzaky kuwa ni miongoni mwa shakhsia wanaodhulumiwa duniani [26] na katika mkusanyiko wa viongozi wa Iran na wageni wa Kongamano la Umoja wa Kiislamu akiashiria matukio ya Nigeria alimchukulia Zakzaky kuwa "mfanya mageuzi mkurubishaji na muumini" ambaye watoto wake sita waliuawa shahidi ndani ya miaka miwili. [27] Ayatullah Khamenei pia aliita shambulio dhidi ya Mashia nchini Nigeria kuwa ni maafa. [28] Sheikh Issa Qasim, kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain, aliita shambulio dhidi ya Mashia na mauaji dhidi yao kuwa ni jinai na kwamba, serikali ya Nigeria inawajibika kwa hilo. [29]

Kwa mujibu wa tangazo la serikali ya Nigeria, Hassan Rouhani, Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya shambulio la maajenti wa serikali ya Nigeria dhidi ya Hussainieh ya Mashia katika mji wa Zaria, alifanya mazungumzo kwa njia ya ya simu na Rais wa Nigeria wakati huo, Muhamadu Buhari ambapo, alimwomba aunde kamati ya kutafuta ukweli ili kuchunguza vitendo vya ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya Mashia. [30] Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika radiamali yake dhidi ya mashambulizi dhidi ya Mashia, ilimwita balozi wa Nigeria mjini Tehran na kutoa wito wa kulindwa (maisha ya) Mashia nchini Nigeria. [31]

Kutotekelezwa hukumu ya kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky nchini Nigeria nako kulikabiliwa na radimalia mbalimbali. Katika marasimu na kumbukumbu ya Arubaini, kundi la Mashia nchini Nigeria liandamana katika mji wa Abuja likilalamikia kushikiwa gerezani Sheikh Zakzaky na kutotekelezwa hukumu ya kuachiliwa kwake huru. Waandamanaji hao walitoa wito wa kuachiliwa huru Sheikh zakzaky. Jeshi la Nigeria liliwashambulia waandamanaji hao na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za vyombo vya habari, zaidi ya Waislamu wa Kishia 40 waliuawa shahidi katika shambulio hilo. [32] Kadhalika mwishoni mwa mwaka 2019 kufuatia kuwa mbaya afya ya Zakzaky, kundi kubwa la Mashia liliandamana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja na kutoa mwito wa kuachiliwa huru kiongozi huyo wa Kiislamu. Polisi na vyombo vya usalama vya Nigeria viliwashambulia waandamanaji hao na kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Mashia 11 waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa. [33]

Kuachiliwa huru

Hatimaye 29 Julai, 2021, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe waliachiliwa huru kutoka katika kifungo cha nyumbani na gerezani baada ya kushikiliwa kwa muda wa miaka 6. Waliachiliwa huru baada ya kufutiwa tuhuma zote walizokuwa wakikabiliwa nazo. [34]

Kwa maelezo zaidi

  • Ili kujua zaidi kuhusiana na mauudhui hii unapendekezewa kusoma kitabu cha "Sheikh Ya’qub Zakzaky na mchango wake wa kimsingi katika kujitokeza na kuenea Ushia nchini Nigeria", mwandishi Amirbahram arabahmadi.