Ukweli kama ulivyo (kitabu)

Kutoka wikishia
Al-Haqiqah Kama Hiya

Al-Haqiqah Kama Hiya (Kiarabu: الحقيقة كما هي) ni kitabu ambacho ni mukhtasari na kinachobainisha fikra za Shia Imamiyah. Kitabu hiki kimeandikwa na Ja’afar al-Hadi (aliaga dunia: 2020), msomi na mwanazuoni wa Kishia. Katika kitabu hiki mwandishi akitumia Aya za Qur’an na hadithi akiachana na ujengeaji hoja anayatambulisha madhehebu ya Shia. Kitabu cha Al-Haqiqah Kama Hiya (ukweli kama ulivyo), kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) mwaka 2005 ilichapisha kitabu hiki na hadi mwaka 2023 kilikuwa kimetarjumiwa kwa lugha 33 za dunia ikiwemo lugha ya Kiswahili ambapo kimepewa anuani ya Ukweli Kama Ulivyo.

Nakala ya sauti ya kitabu hiki pia inapatikana kwa lugha za Kihispania, Kifaransa na Kiindonesia.

Utambulisho

Al-Haqiqah Kama Hiya (Ukweli Kama Ulivyo) ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na kinatambulisha itikadi za Waislamu wa madhehebu ya Shia Imamiyah kwa kutumia Aya na hadithi. [1] Mwandishi wa kitabu hiki ni Sheikh Ja’afar al-Hadi (aliaga dunia 2020), alimu na mwanazuoni wa Iraq ambaye alikuwa pia muumbe wa baraza la Kitabu la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s).

Katika kitabu hiki, kumefanyika juhudi za kutoa ufafanuzi na maelezo mafupi ya mfumo wa fikra za Shia, bila ya kujali hoja yoyote na marejeleo na kutoa majibu ya shaka, shutuma na tofauti zilizopo kati ya madhehebu za Kiislamu. [2] Katika maudhui 40 katika kitabu hiki, mwandishi amefanya hima ya kubainisha ili kuashiria mambo ambayo yanatofautisha itikadi za Mashia na itikadi za makundi mengine ya Kiislamu. [3] Kitabu hiki kimetarjumiwa na kuchapishwa katika lugha 33. [4]

Muundo na maudhui

Al-Haqiqah Kama Hiya ni kitabu mukhtasari (kidogo) ambacho kinajumuisha utangulizi wa mwandishi, matini ya kitabu na hakina faharasa na ugawaji wa milango. [5] Maudhui ya kitabu hiki imo katika mambo 40 ambayo yamewekewa namba na na maudhui hizi zinatambulisha Mashia na kueleza itikadi zao. [6] Kwa muktasari maudhui ya kitabu hiki ni:

Kutarjumiwa na kuchapishwa

Kitabu Ukweli kama ulivyo Tafsiri ya Kiajemi "Al-Haqiqah Kama Hiya"

Kitabu cha al-Haqiqah Kama Hiya kimetarjumiwa na kuchapishwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kifarsi. Mbali na Kifarsi kitabu hiki kimetarjumiwa kwa lugha nyingine 32 ambazo ni:

  1. Kialbania.
  2. Kijerumani.
  3. Kiurdu.
  4. Kihispania.
  5. Kiindonesia.
  6. Kiingereza.
  7. Kitaliano.
  8. Kibarma.
  9. Kibulgaria.
  10. Kibangali.
  11. Kibosnia.
  12. Kireno.
  13. Kipashtu.
  14. Kitagalog (Kifilipino).
  15. Kithailand.
  16. Kituruki (Istanbul).
  17. Kichewa.
  18. Kidenmark.
  19. Kinyarwanda.
  20. Kirusi.
  21. Kiromania.
  22. Kijapani.
  23. Kisindhi.
  24. Kiswahili.
  25. Kifaransa.
  26. Kifulani.
  27. Kikyrgyz.
  28. Kikhmer (Cambodia).
  29. Kikurdi (Kurmanji).
  30. Kilezgia.
  31. Kipoland.
  32. Kihausa. [9]

Aidha idara ya elimu na masuala ya kiutamaduni ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) imetoa nakala ya kitabu cha sauti ya kitabu hiki ambayo inapatikana kwa lugha za Kihispania, Kifaransa na Kiindonesia.