Shufaa

Kutoka wikishia

Shufaa au Uombezi‏ (شفاعة) ni mojawapo ya imani za pamoja kati ya Waislamu. Maana ya shufaa ni kuomba msamaha kwa niaba ya watu wengine mbele ya Mwenye Ezi Mungu, yaani kwa lugha nyengine ni kuwaombea wengine msahaha mbele ya Allah. Hata hivyo, kuna tofauti za maoni miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na maana halisi ya dhana ya shufaa na mipaka yake. Madhehebu ya Imamiyyah, Murji'ah na Ash'ari yanaamini kuwa; Shufaa pia inajumuisha watu waliotenda maovu makubwa, yaani wapo watapata maombezi kupitia watu wema mbele ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, kwa mujibu wa Imamiyyah, shufaa ni kwa wale tu ambao Mwenyezi Mungu ameridhika na dini yao. Kwa upande mwingine, makundi kama vile Mu'utazilah na Zaydiyyah wanaamini kwamba; Shufaa hunamaanisha kuongezeka kwa thawabu na kupata manufaa, na ni makhususi kwa wanao tubu na watiifu peke yao.

Wanazuoni wa Kiislamu wanakubaliana ya kwamba bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni miongoni mwa watu wenye uwezo wa kuombea wengine msamaha (Shufaa) mbele ya Mwenyezi Mungu. Waumini wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa Maimamu watoharifu (a.s) pia wana uwezo wa kuwaombea wengine msamaha mbele ya Mola wao. Kwa kuongezea, wanazuoni wa Kiislamu, wakitegemea Hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya Shia na Sunni, wanawahisabu; manabii, wanazuoni wa dini, mashahidi, waumini, na walio hifadhi Qur'ani kuwa ni watu wenye uwezo wa kuwaombea wengine msamaha. Hata hivyo, baadhi ya Mawahabi wanadai kwamba; Uwezo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) wa kuwaombea wengine msamaha unahusiana na zama za uhai wake tu. Mtazamo huu unapingwa na wanazuoni wengine wa Kiislamu.

Wanazuoni wa Kiislamu kiujumla wanakubaliana ya kwamba; watu wasio na imani, kama vile makafiri na washirikina, hawawezi kufaidika na Shufaa (kuombewa msamaha) kutoka kwa watu wenye uwezo wa kuwaombea wengine msamaha mbele ya Mola wao. Pia, kuna baadhi ya Hadithi kutoka kwa Maimamu wa Shia, zinazoonyesha kuwa watu ambao hawajali swala, wenye tabia za kuwafanya wengine kama Miungu (Maghulati), na watawala madhalimu hawawezi kufaidika na Shufaa.

Neno «Shufaa» (kuombea msamaha) limetumika takriban mara 30 katika Qur'ani. Baadhi ya Aya zinaonyesha kuwa Shufaa ni ya Mwenye Ezi Mungu peke yake, wakati Aya nyingine zikionyesha kuwa Mwenye Ezi Mungu pia amempa uwezo huo Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) pamoja na watu wengine. Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusiana na Shufaa, vikiwemo: «Al-Shafaa Fi Al-Kitab Wa Al-Sunnah» cha Jaafar Subhani, na «Al-Shafaa» kilicho andikwa na Sayyid Kamal Haidari.

Imani za Waislamu Kuhusiana na Dhana ya Shufaa

Waislamu wote wanakubaliana juu ya kuwepo kwa uthibitisho juu ya uwpo wa suala la shufaa.[1] Allamah Majlisi katika kitabu chake kiitwacho Haq al-Iqin, aliichukulia imani ya shufaa kuwa ni miongoni mwa imani msingi za kidini zisizo epukika.[2] Ibn Taymiyyah aliichukulia suala hili la uombezi (shufaa), kuwa ni miongoni mwa imani zilikubaliwa na Waislamu wote, na yeye ana maoni ya kwamba; Riwaya zinazohusiana suala ni Riwaya mutawatir ( zilizo nukuliwa kupitia njia na matabaka mbali mbali ya wapokezi wa Hadithi), na Riwaya hizo zenukuliwa na kurikodiwa katika vitabu sahhihi, vinavyo aminika na vinavyo tegemewa.[3] Kwa kuzingatia riwaya aliyoipokea Sheikh Saduq kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), ni kwamba; iwapo mtu atakataa na kuikanusha dhana ya shufaa, basi huyo yeye si miongoni mwa Shia.[4]

Bila shaka kuna tofauti ya nadharia katika maana na athari za shufaa baina ya madhehebu na wanazuoni mbali mbali wa Kiislamu.[5] Kwa mujibu wa maoni ya Imamiyyah, Ash’airah na Marjie’ah ni kwamba; uombezi una maana ya kuepusha madhara na adhabu kutoka kwa wale walio tenda dhambi.[6] Baaadhi ya wengine wakiwemo Mu'utazila, wameifasiri shufaa kwa maana ya mtu kupata ongezeko la thawabu linalo pelekea kupata manufaa kwa wale wamchao Allah na warejeao kwa Mola wao na kuomba msamaha kutokana na makosa yao.[7]

Inasemekana kwamba neno «shufaa» pamoja na minyambuko yake, limetumika takribani mara 30 ndani ya Qur'ani.[8] Pia kuna Riwaya katika vyanzo vya Shia[9] na Sunni[10] kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Shia (a.s) zizumgumziazo juu ya masuala ya uombezi. Pia, suala hili limejadiliwa na wanatheolojia na wafasiri mbali mbali wa Kiislamu[11] Imani ya uombezi ni miongoni mwa imani zinazo patikana katika imani za Uyahudi na Ukristo.[12]

Uchambuzi wa Dhana

Hadithi ya Sufaa iliyoandikwa katika kuta za Masjid al-Nabii

Maana ya Uombezi ni kumwombea mtu fulani ili aepushiwe adhabu na kumtete mtu fulani ambaye kiuhalisia ni mwenye kustahiki adhabu kutokana makosa fulani aliyoyatenda.[13], au kwa maneno mengine, ni kule mtu fulani kuingilia kati katika kutafuta suluhu ya amani baina mtenda makosa na hakimu, kwa nia ya kumpatia usamehevu mtu huyo mbele ya hakimu kutokana na makosa yake.[14]

Tofauti Kati ya Maana ya Kidini na ya Kimila ya Shufaa

Naser Makarim Shirazi, mfasiri wa kutoka madhehebu ya Shia, ametofautisha baina ya maana ya kidini ya uombezi (shufaa) na kimila inayo fahamika katika jamii za watu wa kawaida. Maoni ya mwanazuoni huyu ni kwamba; katika ya kawaida ya kimila: dhana ya muombezi ina maana ya kule mtu fulani kutumia nafasi yake aliyo nayo, utu wake na ushawishi wake katika jitihada za kubadilisha maoni ya mtu mwenye nguvu (kama vile kadhi), ili kumwepushia adhabu yule ambaye alikuwa akikabiliwa na adhabu ya ule amabye amemzidi kwa nguvu za kiuwezo au kimadaraka. Katika maana hiyo ya kimila, jambo hilo hutimia bila ya kupatikana mabadiliko yoyote yle katika roho ya wale wanaoombewa. lakini aina ya uombezi uliotajwa ndani ya Qur'an na Hadithi unazunguka kwenye mhimili wa kupatika kwa mabadiliko na kupatikana kwa maendeleo kwa yule mtu anayeombewa; Yaani, huwa kuna mabadiliko fulani yanayotokea ndani ya mtu huyo mwenye kuombea. Hii ina maana ya kwamba; kuna matokeo maalumu yanayo tokea ndani ya nasfi ya mtu huyo, ambayo hupelekea kuhama na kutoka katika hali mbaya na zinazostahiki adhabu, kuelekea katika hali mpa ya kustahiki rehema na msamaha kupitia fungamano lililopatikana baina na mwombezi huyo.[15]

Maombezi kwa Maana ya Mwongozo na Uongozi

Wengine pia wameichukulia shufaa kwa maana uwongofu na mwongozo, wao wanaamini kuwa akisiko la waombezi katika ulimwengu huu ni uwongofu unao akisika kutoka kwao, kwa hivyo mtu yeyote yulu ambaye atakosa uwongofu katika ulimwengu huu, huyo hatakuwa na hadhi ya kupata shufa huko Akhera.[16] Wasomi kama vile; Murtadha Mutahhari na Ja'afar Subhani wamesema kuwa shufaa na maombea ya Mtume (s.a.w.w) na manabii wengine katika kuwa tetea wafwasi wao, shufaa ya Qur'an na shufaa ya wasomi kwa waliofundishwa, inamaanisha hidaya na uongofu unaopatikana kupitia kwao.[17]

Uhusiano Kati ya Maombezi (Shufaa) na (Tawassul) Kutawasali

Kwa mujibu wa maelezo ya Ja'afar Subhani, Tawassul ina ngazi tofauti, mojawapo ikiwa ni kuomba shufaa (kumwomba Mungu uokovu) kupitia wale ambao Mungu amewapa idhini ya kuwaombea wengine. Kwa hiyo, shufaa ni moja ya aina za tawassul, ambapo mtenda makosa hutafuta hifadhi mbele ya mtu ambaye ana hadhi ya juu mbele ya Mungu, na humwomba Mwenye Ezi usamehevu na uokovu kupitia mtu huyo. Kwa maana hii, tendo la hili shufaa ni kazi ya yule mtu anaye mwombea mfanya makossa fulani mbele ya Mungu wake ilia pate msamaha kutokana na makossa yake.[18] Maneno yote mawili; «Shufa’a» (شفاعة‏) na «Tawassul» (توسل) yametumika sambamba katika dua ya Tawassul, ambayo ni moja ya dua maarufu, na yote kwa pamoja yametumika katika kutawasali kwa watukufu kumi na nne (Maasumina), ambapo kila mmoja kati yao huombwa shufaa kupitia dua.[19]

Kulingana na maelezo ya Murtadha Mutahhari; kiuhalisia maombezi (shufaa), ni ule ule msamaha wa Mungu, ambapo unapo husishwa na Mungu, ambaye ndiye chanzo asilia cha mema na rehema hunaoitwa «Maghufira», na anapohusishwa na waombezi wa kuwaombea wengine rehema zake, huchukua jina la «Shufa’a».[20]

Waombezi

Wanachuoni wa Kiislamu wote kwa jumla wanakubali ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni mmoja wa waombezi.[21] Maoni yao juu hilo ni kwamba, maana ya na makusudio ya cheo cha Mahmud kilicho tajwa katika Aya isemayo: «وَمِنَ اللَّیْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَکَ عَسَیٰ أَنْ یَبْعَثَکَ رَبُّکَ مَقَامًا مَحْمُودًا» (Na tumia sehemu ya usiku kwa ajili ya kumwabudu Mungu (kusali) hii ni makhususi kwa ajili yako wewe, huenda Mola wako akakuteuwa kwa kukupa cheo cha Mahmud (cheo cha uombezi)).[22] Wanazuoni hao wamesema kwamba, cheo cha maombezi ndio kile cheo cha «Mahmud» ambacho Mwenye Ezi Mungu alimuahidi bwana Mtume (s.a.w.w) katika Qur’ani.[23] Sheikh Mufidu katika kitabu chake Awaili al-Maqaalat amesema kwamba; Wanazuoni wa mashehebu ya Imamiyyah wote kwa jumla wanakubaliana ya kwamba; mbali na shufaa ya bwana Mtume (s.a.w.w), pia Imamu Ali (a.s) na Maimamu 12 (a.s) watasimama siku ya Kiama na kuwaombea shufaa wafwasi wao (Mashia).[24] Mashia wametaja Hadithi kadhaa zinazoashiria ya kwamba Imam Ali na Maimamu wengine wa Shia ni waombezi watako watetea Mashia wao siku ya Kiama.[25]

Kulingana na Aya isemayo: «لا یَمْلِکُونَ الشَّفاعَةَ إِلاَّ مَنِ اتَّخَذَ عِنْدَ الرَّحْمنِ عَهْداً»[26] (Hawana mamlaka ya shufaa (maombezi) isipokuwa wale waliochukua ahadi kutoka kwa Mungu).[27] Wafasiri wametoa maoni tofauti kuhusiana na maana ya neno “ahadi” lilipo katika Aya hii.[28] Wafasiri kama vile; Tabrasi na Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai wametoa maoni yasemayo kwamba; maana ya «ahadi» katika Aya hii ni imani ya kuwamini Mungu na kuwasadiki manabii wake.[29] Wengine pia wamesema maana yake ni kufanya amali njema[30] na wengine wamelifasiri neno hilo kwa maana ya kuamini Mungu mmoja na kuingia katika Uislamu.[31] Kundi la wafasiri wa Shia, wakinukuu baadhi ya riwaya, wamefasiri[32] wakisema kwamba; maana ya «ahadi» ni uongozi wa Imam Ali na Maimamu Maasumina (a.s) wanao fuatia baada yake.[33]

Wakirejelea Aya ya 26 ya Suratu al-Najmu, wengine wamewachukulia malaika kuwa ni miongoni mwa waombezi.[34] Kwa mujibu wa Riwaya ya Imam Ali (a.s) katika Nahj al-Balagha, Qur'an ni mmoja wa waombezi mbele ya Mwenye Ezi Mungu.[35] Katika baadhi ya Riwaya zinazosimuliwa katika vyanzo vya masimulizi vya Shia na Sunni, imeelezwa ya kwamba: Mitume, wanazuoni wa kidini, mashujaa (mashahidi),[36] waumini[37] na walio hifadhi Qur'an,[38] ni miongoni mwa waombezi. Pia, kwa kuzingatia baadhi ya Hadithi zinazosimuliwa katika vyanzo vya masimulizi ya Shia, jirani anaweza kumwombea jirani yake na jamaa kumwombea jamaa yake.[39] Pia katika Riwaya, toba anatambulishwa kama ni mmoja wa waombezi.[40]

Waombewao Shufaa

Kuna tofauti za maoni miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na suala la nani hasa anaingia katika kundi la watu wenye hadhi kuingia kwenye kivuli cha maombezi ya waombezi.[41] Imamiyyah, wakiegemea kwenye Aya ya 28 ya Suratu Anbiyaa,[42] na Riwaya kutoka kwa Maimamu watakatifu (a.s),[43] wanaamini kwamba; maombezi ni kwa ajili ya mtu ambaye dini yake ameridhiwa na Mwenye Ezi Mungu, bila kujali ikiwa yeye alitenda dhambi kubwa au dhambi ndogo.[44] Kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya zilizosimuliwa kutoka kwa maimamu watoharifu ni kwamba;[45] wale waliotubia huwa hawana haja ya kupata maombezi.[46] Ash'ari na Murja’a, wakiaambatana na Imamiyyah, wanaamini kwamba; Wale waliotenda dhambi kuu katika Umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) wanaweza pia nao kuwa chini ya kivuli cha maombezi ya waombezi hao siku ya Kiama.[47] Kwa upande mwingine, Mu'utazila, Khawarij na Zaidiyyah wana maoni yasemayo kwamba; shufaa na maombezi hujumuisha tu wale waumini ambao tayari walikwisha tubia kutokana na dhambi zao,[48] na kwa kushikamana na Aya za Qur'an kama vile Aya ya 48 ya Surat Al-Baqara na Aya ya 18 ya Surat Ghaafir, wamehukumu ya kwamba; mtenda dhambi kuu ambaye hajatubia, hawezi kuingia chini ya kivuli cha maombezi ya bwana Mtume (s.a.w.w).[49]

"Imaamiyyah na madhehebu mengine ya Kiislamu wakizingatia baadhi ya Aya kama vile; Aya ya 18 ya Surat Ghafir[50] na Riwaya zitokazo kwa bwana Mtume (s.a.w.w)[51] na Maimamu wa Kishia (a.s.)[52] wanaamini ya kwamba; washirikina na makafiri hawatakuwa na fursa ya kushufaiwa.[53]

Imam Sadiq (a.s) amenukuu Riwaya kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ambayo kwa mujibu wake ni kwamba; Yeyote yule apuzaye sala hatakuwa na fursa ya kupata shufaa kutoka kwao, yaani kutoka kwa bwana Mtume pamoja na Maimamu.[54] Vilevile kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya za upande wa Kishia, Mnasibi (mwenye chuki na Ahlu al-Bait), watawala dhalimu na Maghulati, hawatakuwa na hadhi ya kupata shufaa.[55]

Shufaa Kupitia Idhini ya Mwenye Ezi Mungu

Wanazuoni wote wa Kiislamu wanaafikiana ya kwamba; shufaa ya wafanyao shafa'a pamoja na kukubaliwa kwa shufaa hiyo, huwa kunategemea idhini itokayo kwa Mwenye Ezi Mungu. Fikra na dhana hii imeegemea kwenye fikra zitokazo kwenye vyanzo vya Kiislamu, kama vile; Aya ya 255 ya Suratu Al-Baqara,[56] Aya ya 3 ya Suratu Yunus,[57] Aya ya 109 ya Suratu Taha[58] na Aya ya 26 ya Suratu An-Najmu.[59] Aya hizi zimetoa matamko ya wazi, kwamba shufaa haiwezi kupatikana bila ya idhini ya Mwenye Ezi Mungu.

Kuna baadhi ya walionukuu baadhi Aya ili kuthibitisha kwamba hakuna mwenye haki ya kuwaombea wengine mbele ya Mungu. Miongo mwa Aya walizo tumia katika madai hayo ni kama vile Aya isemayo: «قُلْ لِلَّهِ الشَّفَاعَةُ جَمِیعًا»[60] (Sema: Shufaa yote ni ya Mwenyezi Mungu),[61] na Aya isemayo: «مَا لَکُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَلِیٍّ وَلَا شَفِیعٍ» (Hamna mwengine kinyume Naye (Mungu) wa kushikamana naye, wala mwombezi (mbele yake) isipokuwa Yeye tu).[62] Aya hizi zimetumika katika kudai ya kwamba; shufaa ni ya Mwenye Ezi Mungu pekee.[63] Kuhusu hilo wamejibiwa ya kwamba; shufaa kiuhalisia ni ya Mwenye Ezi Mungu pekee; hata hivyo, wafasiri wa Qur'ani wanaafikiana kwamba; kwa mujibu wa Aya ya 79 ya Suratu Al-Israa na kwa kuzingatia Riwaya zinazohusiana nayo,[64] Mwenye Ezi Mungu amempa bwana Mtume (s.a.w.w) cheo hicho kilichotajwa kama kwa jina la “مقام محمود” "Cheo cha kuhimidiwa".[65] Wengine pia wakizingatia Aya zinazo onesha ya kwamba, kuna waja kadhaa ambao watakuwa na hadhi ya kushufaia wengine mbele ya Mola wao kwa idhini Yake, wamesema kwamba; ni kweli shufaa ni haki ya Mwenye Ezi Mungu pekee, lakini Mwenye Ezi Mungu amewatunukia fursa hiyo waja wake walio karibu Naye, jambo ambalo liko wazi katika Aya za Qur’ani.[66]

Upinzani wa Kiwahabi Dhidi ya Kuomba Shufaa Kutoka kwa Wafu

Ibn Taymiyyah na baadhi ya wafuasi wa madhebu ya Kiwahabi, kwa kufuata na kuiga mafundisho yake, wanachukulia kwamba; kuomba shufaa kutoka kwa asiye Mungu ni bid’a, na kuomba shufaa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na wengineo ambao wanao dhaniwa au kusadikiwa kuwa wana uwezo wa kushufaia wengine baada ya kufa kwao au hata katika katika za maisha ya kidunia ni miongoni mwa vitendo vya ushirikina.[67] Ibn Taymiyyah alisema kwamba; hakuna hata mmoja wa masahaba, baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w), aliye omba shufaa kutoka kwake, na hakuna hata mmoja wa wanazuoni wanne mashuhuri (Hanafi, Maliki, Ibnu Hanbal na Malik) aliyeona ni mustahab au wajib au kutoa fatwa juu ya kuruhusu jambo hilo, hivyo basi kitendo hicho ni kisicho na hati halali na kinakinzana na nyenendo za masahaba na wanazuoni.[68] Abdul Aziz bin Baz (Mufti wa Kiwahabi kutoka Saudi Arabia) akijibu moja ya maswali alisema kwamba; shufaa ni milki ya Mwenye Ezi Mungu pekee, na Mtume (s.a.w.w) pamoja na wengineo wanaoweza kuwashufai wengine katika zama za uhai wao, hawawezi kuwa na nafasi yoyote ile katika milki hiyo baada ya kufa kwao. Hivyo basi ni ushirikina na si halali kuomba shufaa kutoka kwa mtu aliyekufa na asiye na uwezo wa kutekeleza jambo lolote lile baada ya kifo chake.[69]

Sayyid Ali Milani, mchambuzi wa Kishia katika theolojia, ametumia rejeleo kutoka katika vyanzo vya Kisunni na kusema kwamba; Masahaba, katika hali fulani (za dhiki), walikuwa wakiomba maombezi (shufaa) kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), matendo yalitokea baada ya yeye kuaga dunia.[70] Kulingana na moja ya Riwaya; katika kipindi cha ukhalifa wa Omar bin Khattab, kulitokea ukame mkali na Bilal bin Harith, ambaye alikuwa ni mmoja wa Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), alikwenda kuzuru kaburi la Mtume (s.a.w.w) na kuomba mvua kutoka kwa Allah ili umma uweze kuokolewa kutokana na njaa ya ukame huo.[71]

Kama ilivyoelezwa na Ja’far Subhani katika kitabu chake “Aine Wahabiyyat”, kuomba maombezi (shufaa) kutoka kwa wale waliofariki dunia, hamaanishi kuiombo miili yao iliyozikwa makaburini; bali ni kupeleka maombi hayo na kuyawasilisha kwenye roho zao toharifu na zenye uhai kamili, ambazo zinaishi katika na miili ya ulimwengu barzakh, jambo limebaishwa wazi Qur’an tukufu.[72]

Ukanusha wa Shufaa na Jawabu Zake

Kuna baadhi ya watu miongoni wa wanazuoni wa mdehebu fulani waliokataa uhalali wa uombezi, na wakatoa hoja juu ya dhana yao hiyo, ambazo baadhi yake ni kama ifuatavyo:

  • Mafundisho ya uombezi (shufaa), yanapingana na kanuni asili za uadilifu, na yanawafikia zaidi na mfumo wa dhuluma na kijahili, na kwa msingi huu, kuamini katika hilo ni kumvunjia heshima Mwenye Ezi Mungu.[73] Hata hivyo, kulingana na maoni ya Ayatullahi Makarim Shirazi, ni kwamba; kuwaadhibu matenda dhambi ni haki inayo wastahikia waovu hao, ila kukubali uombezi yanayo watetea waovu hao ni aina ya fadhila na hisani juu yao, hisani ambayo kwa upande mmoja inatokana na mazingira saidizi aliyo nayo yule anayeombewa uombezi huo, na kwa upande mwingine hisani hiyo inatokana na heshima, hadhi na wingi wa amali njema alizonazo muombezi huyo wa shufaa.[74]
  • Kutoa ahadi ya shufaa kwa watu, kunaweza kuwa ni sababu ya watu kuendelea na dhambi zao na kuwafanya wasiwe na haya katika kutenda dhambi na hatimae kuvunja heshima za Kiungu.[75] Katika kujibu madai haya imesemwa kwamba; kama shaka hii ni madhubuti basi Mwenye Ezi Mungu asingeshusha Aya za ahidi maghurira. Hali ya kwamba Mwenye Ezi Mungu amewaahidi waja wake kuwapa maghufira katika Aya kadhaa za Qur’ani wala hakuna mtu anayetilia shaka kwamba Aya hizo zinazo ahidi msamaha hazisababishi watu kuto kuwa na haya katika kuvunja heshima mbele ya Mwenye Ezi Mungu.[76] Vilevile, Aya za shufaa zinategemea matakwa ya Kiungu, na hakuna mtu anayeweza kuwa na uhakika wa kwamba yeye atakuwa ni miongoni wale watakao pata shufaa hiyo, hivyo basi hilo si sababu itakayo sababishi ujasiri wa kutenda dhambi; badala yake, athari pekee ya ahadi ya shufaa ni kuwapa watu matumaini na kuwaokoa kutokana na kukata tamaa juu rehema ya Kiungu.[77]
  • Baadhi ya watu wanaamini kwamba shufaa inalazimiana na kupatikana kwa mabadiliko katika elimu na matakwa ya Mwenye Ezi Mungu. Hii inamaanisha kwamba yule mwombezi wa shufaa huwa anamshawishi au anamtaka Mungu kufanya jambo kinyume na matakwa yake ya awali na kutoa hukumu mpya kabisa. Hata hivyo jambo hilo haliishii hapo tu, bali linalazimiana na kupatikana mabadiliko katika dhati asili ya Mungu, kwani mabadiliko ya elimu na matakwa ya Mungu moja kwa moja yanahusiana kupatikana kwa mabadiliko katika asili ya dhati yake, jambo ambalo haliwezekani kukubalika kimantiki wala kiitikadi. Kwa hiyo, shufaa haiwezi kuthibiti.[78] Katika kujibu shaka na utata huu, baadhi wametoa jawabu wakisema kwamba; kukubali uwepo wa shufaa kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu, haimaanishi kutokea mabadiliko katika matakwa yake au elimu yake. Badala yake, Mwenye Ezi Mungu kiuhalisia tokea mapema alikuwa anajua hali na hatua zote tofauti za maisha ya binadamu. Maarifa haya ya Mungu katika kuelewa mabadiliko na hatua hizo hayamaanishi kupatikana mabadiliko katika elemu yake. Kwa hiyo, matakwa ya Mungu yanatembea juu ya hali tofauti za binadamu maisha mwake. Kiuhalisia binadamu huwa na hali maalum, kulingana na hali na sababu zilizopo, na Mwenye Ezi Mungu pia naye huwa na matakwa maalum kuhusiana naye kulingana na hali hizo alizo nazo katika nyakati tofauti. Matakwa haya tofauti ya Mungu yanahusiana na hali tofauti za binadamu na yanalingana na hali hizo, na hayamaanishi mabadiliko katika maarifa na matakwa ya Mungu.[79]

Ukanushaji wa Uombezi Siku ya Kiyama

Baadhi wananukuu Aya isemayo: (یَوْمٌ لَا بَیْعٌ فِیهِ وَ لَا خُلَّةٌ وَ لَا شَفَاعَةٌ...)[80] (Siku ambayo hakuna mauzo na manunuzi ndani yake, wala urafiki, wala maombezi...)[81] Pi Baadhi ya Aya nyingine za Qur'ani[82] zinazingatia uombezi katika ulimwengu huu tu na kuukataa kuwepo kwa uombezi Siku ya Kiyama.[83] Ila, kwa mujibu wa maelezo ya Ayatullahi Subhani ni kwamba; Aya hii haipingi moja kwamoja uwepo wa shufaa Siku ya Kiama, ila kulingana na sentensi isemayo «لَا خُلَّةٌ» (hakuna urafiki), ni kwamba Aya hii inakataa ule uombezi batili tu.[84] Katika uombezi batili, muombewaji hupata shufaa kiholela, bila ya kujali kwamba yeye alikuwa ni mtekeleza makini wa wajibu na nyadhifa zake za kidini, bali yeye hupata maombezi ya shufaa kwa sababu ya urafiki uliopo baina yake na mwombezi huyo, maombezi ambayo mara kwa mara huonekana kutokea katika ulimwengu huu tulio nao.[85] Baadhi ya wafasiri pia wanaamini kuwa Aya hii haikatai kiukamilifu aina zote za maombezi ya Siku ya Kiyama; Bali inakataa maombezi waiokuwa waumini, yaani shufaa ya kuwambea makafiri.[86] Pia kuna riwaya kuna baadhi ya Hadithi kutoka katika vyanzo vya Shia na Sunni, zinazoelezea uwepo wa uombezi wa wanaoombea wengene shufaa mbele ya Mwenye Ezi Mungu Siku ya Qiyaamah.[87]

Bibliografia (Seti ya Vitabu Kuhusiana na Mada ya Shufaa)

Baadhi ya kazi kuhusiana na mada ya shufaa ni kama ifuatavyo:

  • Al-Shafa’atu fi al-Qur'an wa al-Sunnah: cha Ja'afar Subhani, kitabu hiki kina sura nane:
  1. Sura ya kwanza inajadili mitazamo ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusu Shufaa.
  2. Sura ya pili inahusu mada ya Shufaa katika Qur'an.
  3. Sura ya tatu inafafanua Shufaa na aina zake.
  4. Sura ya nne inajadili hoja za Shufaa.
  5. Sura ya tano inahusu athari za Shufaa.
  6. Sura ya sita inahusu kuomba Shafaa kutoka kwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa ruhusa.
  7. Sura ya saba inahusiana na masuala yanayohusiana na kuomba Shufaa.
  8. Sura ya nane imekusanya ndani yake Hadithi zilizosimuliwa kuhusu Shufaa kutoka katika vyanzo vya Shia na Sunni.[88]
  • Al-Shafa’ah: Kitabu kilicho andikwa na Sayyid Kamal Haidari, kitabu hiki kina utangulizi na sura sita ndani yake:
  1. Sura ya kwanza inafafanua Shufaa kwa dhana ya kilugha, kiistilahi pamo na aina za shufaa.
  2. Sura ya pili inahusiana na athari za Shufaa.
  3. Sura ya tatu inachunguza pingamizi na mashaka au tata kuhusiana uwepo wa Shufaa.
  4. Sura ya nne inajadili masharti ya wale wanaostahili Shufaa.
  5. Sura ya tano inahusu wale wanaoweza kutoa Shufaa.
  6. Sura ya sita inachunguza ruhusa ya kuomba Shufaa kutoka kwa wale wanaoweza kutoa Shufaa.[89]
  • Al-Shafa’atu al-Udhma fi Yaumi al-Qiama: Kitabu hichi kimeandikwa na Fakhru al-Razi:
  1. Baada ya kufafanua Shufaa na mipaka yake, kitabu hiki kimeanza kuchunguza na kukosoa mitazamo ya Khawarij, Mu'tazila, na Ahlul-Kitab kuhusiana na Shufaa.[90]
  • Ithbatu al-Shafa’ah: cha Shams al-Din al-Dhahabi: Mwandishi wa kitabu hiki, ni mwanahistoria na mtaalamu wa Hadith wa upande wa madhehebu ya Sunni wa karne ya nane Hijiria. Shams al-Din al-Dhahabi kitabini mwake, amekusanya baadhi ya Hadithi zilizosimuliwa na Maswahaba.[91]

Masuala Yanayo Fungamana

Rejea

  1. Allamah Hali, Kashf al-Murad, 1413 AH, uk. 416; Jurjani, Sharh al-Mawaqif, 1325 AH, juz. 8, uk. 312.
  2. Allamah Majlisi, Haqu al-Yaqin, Intisharat Islamiyyah, juz. 2, uk. 445.
  3. Ibn Taymiyyah, Majm al-Fatawi, 1416 AH, juz. 1, uk. 313-314.
  4. Sheikh Saduq, al-Amali, 1417 AH, uk. 370.
  5. Tazama Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 29.
  6. Tazama Sayyid Murtaza, Sharh Jamal al-Ilim wal-Amal, 1419 AH, uk. 157; Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 29; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 3, uk. 496.
  7. Tazama: Qazi Abd al-Jabbar, Sharh al-Asul al-Khumsa, 1422 AH, uk. 463.
  8. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, Dar al-Kitab al-Islamiyyah, juz. 1, uk. 273.
  9. Tazama: Kuleni, al-Kafi, 1407 AH, juz. 8, uk. 101; Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 AH, juz. 3, uk. 574.
  10. Tazama Bukhari, Sahih al-Bukhari, 1422 AH, juz. 9, uk. 139; Nasa'i, Sunan al-Nasa'i, 1406 AH, juz. 2, uk. 229.
  11. Fani Asl, «Shafaa Az Didegahe Sadr al-Mutaalihiin», uk.
  12. Fakhr Razi, Al-Shifa'a al-Udhma Fi Yami al-Qiyama, 1988, uk. 7-10.
  13. Sayyid Murteza, Rasail al-Sharif al-Radhi, 1405 AH, juz. 1, uk. Sheikh Tusi, al-Tibyan, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 1, uk. 213.
  14. Mutahari, Majmuat Athar, 1389, juz. 1, uk. 254.
  15. Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, Dar al-Kitab al-Islamiyyah, juz. 1, uk. 271-272.
  16. Khomeini, Sharh Chehel Hadith, 1380 S, uk. 150; Mutahari, Adl Ilahi, 1391, uku. 226-230; Subhani, Al-Shifa'a fi al-Kitab wa Sunnah, Qom, ukurasa wa 29-30.
  17. Mutahari, Adl Ilahi, 1391 S, uku. 226-230; Subhani, Al-Shifa'a fi al-Kitab wa Sunnah, Qom, uku. 29-30.
  18. Subhani, Istiftaat, 1389 S, juz. 2, uk. 15.
  19. Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 102, uk. 247-249.
  20. Mutahari, Adl Ilahi, 1391 s, uk. 235.
  21. Tazama Sheikh Mufid, AwaIl al-Maqalat, 1413 AH, uk. 79; Sayyid Murtaza, Sharh Jamal al-Ilm wal-Amal, 1419 AH, uk. 156; Jurjani, Sharh al-Maqasid, 1325 AH, juz. 8, uk.312.
  22. Surat al-Israa, Aya ya 79.
  23. Tazama: Tabarsi, Majmau al-Bayan, 1415 AH, juz. 6, uk. 284; Tabari, Jamiu al-Bayan, 1412 AH, juz. 15, uk. 97; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 21, uk. 387.
  24. Sheikh Mufid, Awail al-Maqalat, 1413 AH, uk. 79-80.
  25. Tazama: Sheikh Mufid, Awail al-Maqalat, 1413 AH, uk. 79-80; Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 41-42.
  26. Surat Maryam, Aya ya 87.
  27. Sheikh Tusi, al-Tibyan, juz. 7, uk. 150.
  28. Tazama: Sheikh Tusi, al-Tibiyan, juzi 7, uk. 150; Tabrasi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juz. 6, uk. Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyyah, juz.a 14, uk. 111.
  29. Tabrasi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juz. 6, uk. 452; Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyyah, juz. 14, uk. 111
  30. Sheikh Tusi, al-Tibiyan, juz. 7, uk. 150.
  31. Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 3, uk. 499.
  32. Qomi, Tafsir Qomi, 1404 AH, juz. 2, uk. 57.
  33. Tazama: Hawizi, Nur al-Saqalein, 1415 AH, juz. 3, uk. 361.
  34. Tazama: Tabrasi, Majmau al-Bayan, 1413 AH, juz. 9, uk. Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 19, uk.40; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 28, uk. 256.
  35. Nahj al-Balagha, Iliyohaririwa na Subhi Saleh, Khutba nambari 176, uk. 252.
  36. Sheikh Saduq, Al-Khisal, 1362, juz. 1, uk. 156; Ahmad bin Hanbal, Musnad Ahmad, 1421 AH, juz. 34, uk. 90.
  37. Kuleini, Al-Kafi, 1407 AH, juz. 8, uk. 101.
  38. Hurru Amili, Wasal al-Shia, 1416 AH, juz. 6, uk. 171. Tirmidhi, Sunan al-Tirmidhi, 1395 AH, juzuu ya 5, uk.
  39. Tazama: Kuleini, Al-Kafi, 1407 AH, juz. 8, uk. 101.
  40. Tazama: Nahj al-Balagh, Iliyohaririwa na Subhi Saleh, Hekima ya 371, uk. 540.
  41. Bahbahani, Shafaat, 1392 S, uk. 33.
  42. Tazama: Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 14, uk. 277.
  43. Tazama Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 34.
  44. Tazama: Sheikh Saduq, Al-Itiqadat, 1414 AH, uk. 66.
  45. Tazama: Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 AH, juz. 3, uk. 574.
  46. Tazama: Sheikh Saduq, Man La Yahdhuruhu al-Faqih, 1413 AH, juz. 3, uk. 574; Sheikh Saduq, Al-Itiqadat, 1414 AH, uk. 66.
  47. Sayyid Murtaza, Sharh Jamal al-Ilm wa Al-Amal, 1419 AH, uk. 157; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 3, uk. 496-497.
  48. Tazama: Qazi Abdul-Jabbar, Sharh al-Usul al-Khamsa, 1422 AH, uk. 463; Sayyid Murtaza, Sharh Jamal al-Ilm wa Al-Amal, 1419 AH, uk. 156; Subhani, Buhuthi Fi Millal wa An-Nihal, juz. 3, uk. 206.
  49. Tazama: Qazi Abdul-Jabbar, Sharh al-Usul al-Khamsa, 1422 AH, 464; Jurjani, Sharh al-Maqasid, 1325 AH, juz. 8, uk. 313.
  50. Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 3, uk. 496.
  51. Tazama: Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, Dar Ihya Al-Kitab al-Arabiyyah, juz. 2, uk. 1440.
  52. Tazama: Sheikh Saduq, al-Khisal, 1362 S, juz. 2, uk. 355.
  53. Sheikh Saduq, Al-Itiqadat, 1414 AH, uk. 66; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 3, uk. 496.
  54. Kuleini, al-Kafi, 1407 AH, juz. 6, uk. 400.
  55. Barqi, Al-Mahasin, 1371 AH, juz. 1, uk. 186; Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 25, uk. 268-269.
  56. Tabrasi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juz. 4, uk. 60; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 7, uk. 11.
  57. Tabrasi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juz. 5, uk. 56; Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, Dar al-Kitab al-Islamiyyah, juz. 17, uk. 127.
  58. Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 22, uk. 101.
  59. Sheikh Tusi, Al-Tibyan, Dar Ihya Al-Turath al-Arabi, juz. 9, uk. 429-430.
  60. Surat Zumar, Aya ya 44.
  61. Ilahi Qomshei, Tarjume Qur'an karim, Nashr Fatima Al-Zahra (s.a),uk. 207.
  62. Surat Sajdah, Aya ya 4.
  63. Subhani, Al-Shifa'a fi al-Kitab wa Sunnah, Qom, uk. 19 na 58.
  64. Tazama AllamAh Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 48; Bukhari, Sahih al-Bukhari, 1422 AH, juz. 6, uk. 86; Suyuti, Dar al-Manthur, Dar al-Fikr, juz. 5, uk. 377.
  65. Tazama Tabari, Jamiu al-Bayan, 1412 AH, juz. 15, uk. Tabrasi, Majma al-Bayan, 1415 AH, juzuu ya 6, uk. Qurtubi, Tafsir Qurtubi, 1384 A.H., juz. 10, uk. 309.
  66. Tazama: Tabatabai, Al-mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 1, uk. 156 na juz. 17, uk. 270.
  67. Tazama: Ibn Taymiyyah, Majmau al-Fatawa, 1416 AH, juz. 1, uk. 159; Ibn Abdul-Wahhab, Al-Rasail al-shakhasia, Jamiat al-Imam Muhammad bin Saud, uk. 154; Munjid, Mauqiu al-Islami Suali wa Jawab, 1430 AH, juz. 1, uk. 938.
  68. Ibn Taymiyyah, Majmau al-Fatawa, 1416 AH, juz. 1, uk. 161-162.
  69. Munjid, Mauqiu al-Islami Suali wa Jawab, 1430 AH, juz. 1, uk. 938.
  70. Husseini Milani, Ar-rad Ala Ibn Taymiyyah fi al-Shifa'a wa al-Ziyarah wa al-Istighatha, 1435 AH, uk. 65-66.
  71. Tazama: Asklani, Fat-hu al-Bari, 1379 AH, juz. 2, uk. 495.
  72. Subhani, Ainu wahabi, Jamie Mudarisin Hauze Qom, uk. 283-284.
  73. Kasrawi, Khuda Ba Maast; Bikhond wa Dovari Koniid, 1323 S, uk. 32-33.
  74. Makarim Shirazi, Payam Qur'an, 2006, juz. 6, uk. 533.
  75. Tazama: Qalmadaran, Rahe Najat Az Shar Ghulat, uk. 286.
  76. Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 1, uk. 165; Mutahari, Adl Ilahi, 1391 S, uk. 241.
  77. Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 1, uk. 165; Mutahari, Adl Ilahi, 1391 S, uk. 241.
  78. Tazama: Rashid Ridha, Tafsir al-Manar, 1990, juz. 1, uk. 255; Qalmadaran, Rahe Najat Az Shar Ghulat, uk. 362.
  79. Tabatabai, Al-Mizan, Intisharat Ismailiyan, juz. 1, uk. 164-165; Haydari, Al-Shafa'a, 1425 AH, uk. 161-162.
  80. Surat al-Baqarah, Aya ya 254.
  81. Makarim Shirazi, Tarjume Qur'an, 1380 S, uk. 42.
  82. Surat Dukhan, Aya ya 41.
  83. Tazama: Qalmadaran, Rahe Najat Az shar Ghulat, uk. 294-295; Rashid Ridha, Tafsir al-Manar, 1990, juz. 1, uk. 255.
  84. Subhani, Manshur Jawid, 1388 S, juz. 8, uk. 210.
  85. Mudarisi, Tafsir Hidayat, 1377 S, juz. 7, uk. 91.
  86. Tazama: Sheikh Tusi, al-Tibyan, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 2, uk. 306; Tabrasi, Majmau al-Bayan, 1415 AH, juz. 2, uk. 156.
  87. Tazama: Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, 1983, juz. 8, uk. 34-37; Muslim, Sahih Muslim, Dar Ihya Al-Turath al-Arabi, juz. 1, uk. 188-191.
  88. Subhani, Al-Shifa'a fi al-Kitab wa Sunnah, Qom, uk. 93.
  89. Haydari, Al-Shafa'a, 1425 AH, uk. 433-439.
  90. Fakhr Razi, Al-Shifa'a al-Adhim Fi Yawmi al-Qiyamah, 1988, uk. 4-5 na 7-10.
  91. Dhahabi, Ithbat al-Ashafaa, 1420 AH, uk. 69-70.

Vyanzo

  • Qur'an
  • Ibn Manzur, Muhammad bin Mukram. Lisan al-'Arab. Beirut: Dar Sadir, 1388
  • Al-Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-anwar li durar akhbar al-a'imma al-athar. Tehran: Al-Islamiyya, 1363
  • Al-Razi, Fakhr al-Din. Al-Tafsir al-kabir.
  • Hanbal, Ahmad. Musnad Ahmad.
  • Al-Nasa'i, Ahamd bin 'Ali. Sunan al-kubra
  • Mutahhari, Murtada. 'Adl-i ilahi.
  • New Catholic Encyclopedia. Washington DC: Gale,2002
  • Jawadi Amuli, 'Abd Allah, Tasnim.
  • Al-Ash'ari, Abu l-Hassan. Maqalat al-islamiyyin.
  • Zamakhshari, Mahmud al-. Al-Kashshaf. Beirut: Dar al-Kitab al-'Arabi, 1407
  • Jawadi Amuli, 'Abd Allah. Ma'ad dar Qur'an.
  • Himyari, 'Abd Allah b. Ja'far al-. Qurb al-isnad.
  • Qazwini, Ibn Maja al-. Sunan Ibn Maja.
  • Al-Fayd al-Kashani, Muhsin. 'Ilm al-yaqin fi usul al-din.
  • Bukhari, Muhammad bin Isma'il al-. Sahih.
  • Ridwani, 'Ali Asghar. Salafigari wa pasukh bi shubahat. Qom: Masjid Jamkaran
  • Ibn Taymiyya. Majmu' al-fatawa. Medina: Majma' al-Malik Fahad, 1416
  • Muhammad bin 'Abd al-Wahhab. Kitab al-tawhid.
  • Scholars of Najd. Al-Durar al-sunniyya fi l-ajwabat al-Najdiyya. 1417
  • Al-Tirmidhi, Abu 'Isa. Sunan al-Tirmidhi. Egypt: Maktaba wa Matba'a Mustafa al-Babi al-Halabi, 1395
  • Al-Sharif al-Radi. Nahj al-balagha
  • Abu Dawud, Suleiman bin Ash'ath. Sunan Abi Dawud. Beirut: Al-Maktaba al-'Athriyya
  • Muhammad bin 'Abd al-Wahhab. Kashf al-shubahat. KSA: 1411